Diamond Aomba Radhi Mashabiki Wake Kwa Kutokutokea Katika Shoo

Diamond Platinumz ,Akiwa kama Msanii mkubwa nchini  ameomba radhi mashabiki wake ambao walikuwa wamekaa wakimsubiri kwa hamu katika shoo iliyoandaliwa na Mh. Paul Makonda huku ikihusisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoa vyuo vyote Dar Es Salaam , show hiyo ambayo ilikuwa ikifanywa na kushiriki kwa wasanii wengi wakubwa na wakongwe ilitegemewa kuwa Diamond atakuwa ni mmoja ya wasanii watao kwenda ku-perfom katika jukwaa hilo lakini haikuwezekana.

Siku iliyofuata Diamond Platinumz alitumia ukurasa wake wa instagram kuwaomba radhi mashabiki wake wote ambao hata yeye mwenyewe alitumia njia kubwa kuwahasisha waweze kutokea alafu yeye akashindwa kutokea.

Najua wengi mlikuwa ma shaulu ya kuona uwepo wangu   pale mlimani city jana.. ila amini kabisa kuwa hata mimi nilikuwa nina shauku zaidi ya ile ya kwenu, ya kuimba na kufurahi pamoja nanyi, na shauku iyo ilikuwa kubwa kuliko yenu na ndio maana nilitumia jitihada sana  kuwahamasisha ili muwepo kwa wingi katika tamasha hilo ili tufike kwa wingi pale , lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu nilishindwa kufika pale,hivyo tusisononeke wala kuchukukia , naomba radhi  na kuwapa pole wale wote waliokwazika jana ,Inshallah Mwenyezi Mungu siku akiniandikia kuwa na nyie ntawaarifu-Alifunguka Diamond

Show iyo ilikwenda vizuri na kufana sana kutokana na uwepo wa wasanii wengi wakubwa na wakongwe akiwepo AY,Mwana FA, Fid Q, Lady jay dee, rich mavoko.Lakini katika tamasha hilo wasanii lady jay dee na mwana Fa walionekana kwa mara ya kwanza wakiwa wote jukwaani tangu walipokorofishana miaka mingi iliyopita na kupata mwaka huu.

Kushoto ni mwanadada Lady Jay Dee akiwa na Ay, kulia ni Mwana Fa na Lady Jay Dee katika show ya freshersparty

Ukumbi wa Mlimani City ulikuwa umefurika wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali

Hawa Ndio Wanawake Waliomtesa Diamond Kwenye Mapenzi.

Diamond ni moja wa wasanii wanaosemekana kuimba nyimbo nzuri na kupendwa na mashabiki kutokana na kuimba nyimbo zinazotoa historia ya maisha yake kila siku.Hivi juzi Diamond alitoa audio mbili mfululizo ya Sikomi na Niache, nyimbo ambazo zimepokelewa vizuri sana na mashabiki kwa sababu zimeelezea kwa undani kabisa maisha yake ya mapenzi na kuwataja wanawake wake wote ambao aliwahi kuwa nao katika mahusiano na vitendo vya kikatili walivyomfanyia katika mapenzi.

Hawa ndio wanawake haliowataja diamond katika nyimbo zake hizo.

WEMA SEPETU.

Aliwahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2016, baadae alikuja na kujiingiza katika tasnia ya bongo movies.Ni moja kati ya wasanii wa kike maarufu na wanaopendwa na kuongoza katika mitandao kuwa na mashabiki wengi sana.Alishawahi kuwa na mahusiano na watu wengi maarufu na kila siku amekuwa ni mwanadada mwenye drama nyingi sana katika mapenzi.Alishatoka na Mr. Blue, Idris Sultan, na Steven Kanumba.

Ukiachana na urembo lakini pia Wema anajihusisha na ujasiriamali wa vipodozi.Amekuwa ni moja ya wanadada wanaojisifu kuwa na application inayoelezea maisha yake inayopatikana Playstore.

VJ PENNY

Kwa sasa ni mtangazaji wa kipindi kimoja cha harusi katika television moja nchini, jina lake lilipata umaarufu sana alipokuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond, huyu ndie diamond aliemlilia baada ya kupata mimba na kuitoa ilhali diamond alikuwa akitamanai mtoto

HAMISA MOBETO

Ni mwanamitindo ambae kwa sasa amaeona fursa nyingine kupitia uigizaji, alikuwa na mahusiano na Diamond kwa muda mrefu lakini yalikuwa ni siri yao, alikuja akapata mimba na Diamond aliikataa ktika mitandao na vyombo vya habari.Baada ya kutoa ushaidi wa mahusiano yao Diamond alikubali  majukumu ya mtoto wa mrembo huyo.Ameingia katika vichwa vya habari kutokana na mahusiano yake na Diamond kwenda mrama mpaka kufikia hatua ya kupelekana polisi.Amezaa na Diamond mtoto mmoja.

ZARINA HASSAN

Ni mama wa watoto watano lakini wawili kazaa na Diamond, ni mwanamke inaesemekana kuwa amesaidia kwa kiasi kikubwa sana mafanikio ya msanii huo.ni mwanamama kutoka Uganda, mwenye utajiri mkubwa alioachiwa na baba mzazi wa watoto wake watatu wa kwanza.aAmepitia misukosuko mingi ya kimahusiano  na msanii Diamond lakini  bado wapo pamoja.

 

 

Gigy Money Bado Anamuwinda Diamond Platinumz

Mwanamuziki kutoka Tanzania asiyeishiwa na matukio kila kukicha Gigy Money  ameibuka na kuongelea jinsi gani anavyotamani kila siku kutoka kimapenzi na msanii mkubwa kutoka bongo Diamond Platinumz.Msanii huyo ambae kwa sasa anatamba na kibao chake cha papa ambacho kinafanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari amefunguka bila kuwa na wasiwasi kuhusu hisia zake kwa msaanii huyo mkubwa kutoka Tanzania.

Akihojiwa na moja ya waandishi wa habari , aliulizwa kuhusu ndoto aliokuwa nayo muda mrefu ya kutaka kutoka kimapenzi na Diamond Platinumz, Gigy Money alisema kuwa yeye na Diamond wamekuwa wakiwindana kwa muda mrefu sana lakini yeye hana wasiwasi anaamini muda ukifika tu kila kitu kitakuwa sawa maana hajui kitu gani mwanamke mwenzie atakosea na yeye akapatia ili kuwa na Diamond lakini anaamini kabisa ipi siku hataweza kutoka na Diamond

iyo ndoto kama chemchem inachemka tu sijui lini mwenzangu,mimi na Diamond tunawindana, tukipishana baadhi ya sehemu tunaambiana tu wewe..wewe , lakini ninachoamini muda ukifika tu kila kitu kitakuwa sawa mambo mazuri hayataki haraka, na inawezekana hata tukadate, you never know wenzie watakosea wapi na wewe utapatia wapi, kila kitu kinawezekana” alifunguka Gigy Money

Gigy Money alishawahi kutangaza katika vyombo vya habari kuwa alikuwa na mahusiano na alikiba na kusema kuwa endapo wameacha lakini huwa wanakutana na kukumbushia mapenzi yake, hata hivyo alipoulizwa tena kuhusu hisia zake kwa msanii alikiba gigy money alisema kuwa kwa alikiba alishapita wala hana ya kurudi tena huko yeye saivi na diaond tu“kwa alikiba tulishapitaga huko, unajua ukipita sehemu kuja kurudi inakuwa  sijui unaonaje ..haaaa unarudiaa, saivi tunaenda mbele kwa mbele  kama ccm

Gigy Money ni moja wa wasichana wanaokwa wazi sana anapokuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasanii, hivi karibuni amekuwa akiongelea sana kutamani kuwa na mahusiano na Diamond Platinumz huku akikana kurudiana na Rich Mavoko. Hata hivyo Gigy Money alikuwa katika mahusiamo na mtangazaji mwenzake wa radio moja wapo hapa nchini  na haijafahamika kama wameshaachana au la.

 

“Mimi Na Diamond Ni ndugu”–Tahiya

Moja ya video queen alietumika katika wimbo wa Harmonize ‘sheri’ Tahiya ambae hivi karibuni pia alikuwa katika scandal ya kutembea na boss wa wasafi Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa yeye na Diamond hawana mahusiano yoyote zaidi ya kazi.mwanadada huyo ambae amekuwa akionekana kuwa karibu na wasanii kutoka Wcb anasema kwa yeye kuonekana karibu na wasanii hao ni kitu kusichokwepeka kwa sababu kazi zake zinamfanya awe nao karibu kila muda.Hata hivyo dada huyo alisema kuwa yeye na Diamondi ni ndugu.

Mimi na diamond ni ndugu, sio ndugu wa karibu sana ila kupitia Esma, so ikitokea shughuli shughuli zake,party zake na events mimi ninakuwa ni mmoja kati ya watu wanaosapoti kazi hizo, so mimi kuwa karibu  nae recently ni kwa sababu ya yeye na  birthday zake kufululiza,birthday tano alifanya na zote nilikuwepo kuanzia ya kwanza hadi ya mwisho.” aliongea Tahiyo

Hata hivyo aliendelea kuelezea pia ni kwa sababu gani,watu walianza kumzushia kuwa anatembea nae,”katika birthday tulikuwa tunasnap na vitu kama hivyo, waking up nakutana na post kuwa katika birthday yake ya mwisho niliondoka nae nikaenda kulala nae nyumbani kwake,na kwamba ile snap ya Diamond karanga pale kitandani ni kitandani kwake na ule mkono wa mamangu ni mkono wake,…lakini nobody knows the truth zaidi ya sisi hapa” aliongezea

Imekuwa ni gumzo mitandaoni kuwa karibia kila msichana ambae anaonekana kuwa karibu na msanii huyo kwa sasa basi anakuwa nae katika uhusiano wa kimapenzi labda kutokana na kile kilichotokea kwa video queen Hamisa Mobeto hivyo mashabiki wa Diamond wamepoteza uaminifu kwa msanii wao.

Hata hivyo baadhi ya mambo yanakuwa yanakuzwa sana katika  mitandao ya kijamii, mwanadada Tahiya anasema kuwa kitendo cha yeye   kupost snap ile wakati maneno ya yeye kutembea na msanii huyo yanendelea kumeafanya katika mitandao kuzidi kuchafuka kuwa anatembea nae lakini ukweli wanaujua wao wawili kuwa hakuna kitu chochote kinachoendelea zaidi ya kuwa katika kazi pamoja

 

Diamond Na Rick Ross Kufanya Ngoma Ya Pamoja

Msanii mkubwa kutoka Tanzania Diamond Platinumz anatarajia kufanya kazi pamoja na msanii mkubwa duniani na anaejulikana kama msanii mkubwa na tajiri Duniani  Rick Ross.Kwa muda sasa wasanii hao wamekuwa wakionekana kuwa na mahusiano ya karibu kwa sababu ya wote kuwa mabalozi wa kinywaji cha Belaire ambacho kinatengeneza nchi za Ulaya.Rick Ross amekuwa akimpost Diamond katika kurasa zake za mitandao ya kijamii zaidi ya mara moja huku akimpongeza kwa sikukuuu ya kuzaliwa na kumkaribisha katika ubalozi wa kutangaza kinywaji hicho.

Akiandika na kupost kipande cha video kinachoonyesha wasanii hao wapo pamoja wakiimba  katika ukurasa wake wa Instagram, meneja wa Diamond Platinumz, Sallam K alirusha video iyo na kuthibitisha kuwa wawili hao  wapo katika maandalizi  na wanatarajia kutoa  kazi yao  wakiwa pamoja.Kipande hicho kinaonyesha wapo  katika moja ya location .

Sallam K aliandika “Diamond Platinumz x Rick Ross on set now  somewhere in Miami  #BlackBottleBoys and we never stop!!!” alituma meneja wa diamond,

Diamond Platinumz kutoka Tanzania  akiwa katika picha ya pamoja na Rick Ross wa Marekani  na msanii mwenzie kutoka Tanzania Rayvanny.

Diamond ambae kwa sasa yuko nje ya nchi alikoenda katika tuzio za AFRIMA na kushindwa tuzo mbili katika vinyanganyio tofauti amekuwa ni mmoja wa wasanii wakubwa bongo wanaofungua mipaka na kufanya kazi na wasanii wakubwa kutoka nje,hivi karibuni Diamond Platinumz alitoa wimbo mpya unajulikana kwa jina la Hallellujah aliowashirikisha kundi kubwa la muziki  Duniani linalojulikana kama Morgan Heritage na wimbo huo umekuwa ukifanya vizuri katika vituo vya  radio na televisheni.

Akiwa balozi mkubwa wa muziki kutoka nchini Tanzania Diamond amekuwa akijitaidi kufanya vizuri katika muziki na kusaidia hata wengine wanaotaka kuendelea katika muziki kwa kuanzisha lebel yake ya Wcb inayoibua wasanii wakubwa na  kujulikana Afrika na duaniani kwa ujumla.Diamond amekuwa ni msanii anaeweza kuthubutu kufanya kitu chochote ili kukuza muziki wake na Tanzania kwa ujumla.Yeye ni msanii wa kuigwa na wasanii wengine

 

Birthday Ya Diamond Yafunika (Matukio Katika Picha)

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platinumz jana usiku alifanya private party akijumuika na baadhi ya wanafamilia wake, wafanyakazi wenzake, ndugu , jamaa na marafiki katika ukumbi wa Hyatt Regency uliopo jijini Dar Es Salaam.

Na hizi ni baadhi ya picha zilionyesha jinsi alivyosherekea sherehe hiyo,

Diamond akimlisha mama yake mzazi cake

B-Dozen nae alikuwepo kama mtu wa karibu katika kujuika pamoja na wanandugu katika shughuli iyo.

Vinywaji pia viliweza kupendezesha meza ukumbini hapo

Diamond akiwa na bodyguard wake muda wa maakuli.

Queen Darling akiwa pamaoja na  Beka Flavour.

Meneja wa Diamond sallam k akifurahia jambo aakiwa pamoja na Diamond

Hata hivyo kabla Diamond ajaaanza party hiyo ya usiku alikwenda kutembelea katika hospitali  ya Amana aliyozaliwa iliyopo Ilala jijini hapo na kutoa msaada kwa wagonjwa wenye thamani ya million 4 ili kuweza kusaidia wagonjwa.

Maneno Ya Rick Ross Kwenye Birthday Ya Diamond

Msanii mkubwa Duniani Rick Ross amepost picha  katika ukurasa wake wa Facebook kumpongeza msanii wa muziki wa Tanzania anaefanya vizuri Duniani kote Diamond Platinumz ambapo jana ilikuwa ni sikukuu yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa.Diamond ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha “Hallelujah” alichowashirikisha MorganHeritage

Hivi karibuni msanii Diamond alionekana katika baadhi ya post za Rick Ross akiwa kama mwakilishi mpya wa pombe ya Belaire kutoka Tanzania, kampuni ambayo Rick Ross pia anafanya kazi.Hivyo akiwa kama mwanafamilia wa Balaire Rick Ross aliamua kumpongeza msanii Diamond  kwa kazi nzuri anayoifanya  ya kutangaza kinywaji icho vizuri nchini Tanzania.Lakini pia amemkaribisha kwa mara nyingine tena katika familia ya wana Belaire.

Katika ukurasa wake wa Facebok Rick Ross aliandika ‘Happy Birthday to my brother Diamond Platinumz ,love how you have been reppin#belaire so with that said, Welcom  to the Belaire Family….#BlackBottleBoy”  aliandiak Rick Ross akiwa ameweka picha ya msanii Diamond katika ukurasa huo.

Ni kwa muda sasa kidogo tangu Diamond awe Ambassor wa kampuni ya kutengeneza vinywaji hivyo na amekuwa akijitaidi kwa kiasi kikubwa katika kufanya matangazo ya kinywaji hicho katika account zake mitandaoni.

Diamond ambae jana alishereka siku yake ya kuzaliwa, alianza kwa kutoa sadaka na misaada yenye thamani ya zaidi ya milioni  4 na kutoa zawadi mbalimbali kwa baadhi ya wagonjwa  katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar Es Salam . Diamond  akiwa kama mmoja wa watu waliozaliwa katika hopitali hiyo miaka kadhaa iliyopita aliamua kufanya hivyo kwa sababau anaamini kwamba wapo watu wengi maeneo  kama hayo wanaoitaji misaada, lakini pia msanii huyo anaamini kuwa hata waliopo hospitali pia ni mashabiki wa nyimbo zake , na hali hii ilijidhiirisha baada ya Diamond kufika hospitalini hapo baadhi ya kushughuli zilisimama kutokana na mashabiki kuwa wengi wakitaka kumwangalia msanii wao.

Bada ya shughuli hizo za mchana Diamond  alijumuika pamoja   na ndugu, rafiki  na jamaa zake wa karibu  katika kusherekea    sikukuu yake ya kuzaliwa.

 

Diamond Asherekea Siku Yake Ya Kuzaliwa Hospitali

Ikiwa jana ni siku yake ya kuzaliwa msanii mkubwa nchini Tanzania  Diamond Platinumz amesherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar Es Salaam, msanii huyo ambae anajulikana kitaifa na kimataifa ameamua kujumuika pamoja na wagonjwa ikiwa kama moja ya kutoa sadaka na shukrani kwa kutimiza miaka kadhaa.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wasanii kufanya sherehe kubwa zinazotawala vinywaji na vyakula mbalimbali katika kumbi za starehe lakini Diamond aliamua kuwa ni lazima kuwakumbuka watu wenye shida pia, ambapo anaamini hata hao waliopo hospitali pia ni mashabiki zake.

Diamond pia aliamua kutoa vifaa vya hospitali vyenye thamani zaidi ya mil.4 ili kusaidia shughuli za kimatibabu ziendelee katika hospitali hiyo.Hata hivyo Diamond ni mmoja wa watu waliozaliwa katika hopitali ya Amana Ilala jijini Dar Es Salaam miaka kadhaa nyuma , ivyo kitendo cha yeye kutoa misaada hiyo ni kama kurudisha shukrani hospitalini hapo.

Akiongea na mwandishi wa gazeti la Mwananchi msanii Diamond Platinumz alisema kuwa aliamua kuja hospitali na kuleta baadhi ya vifaa maana anajua kuwa hata huku wapo watu wengi wenye shida na wanahitaji misaada pia”najua hospitali kuna mahitaji mengi , nikaona kwa uwezo wangu mdogo  nami nishiriki  kusaidia mahali nilipozaliwa, ili nipate fursa ya  kuwaona pia watoto waliozaliwa siku kama yangu” alisema Diamond

Kwa kipindi kifupi ambacho msanii Diamond alichokuwepo hospitalini hapo, baadhi ya shughuli zilishindwa kuendelea kutokana na hamu ya mashabiki walikuwa hospitalini hapo tukata kuwa karibu na msanii wao.Hata hivyo baada ya shughuli ya kutembela wagonjwa Diamond alipata nafasi ya kufanya sherehe  kwa ajili ya kujumuika na baadhi ya ndugu, jamam na marafiki wa karibu kwa ajili ya kusherekea siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Imekuwa ni kama desturi kwa Diamond kutoa misaada au sadaka hizo kwa jamii kimyakimya bila kushirikisha vyombo vya habari, tofauti na baadhi ya wasanii ambao mara nyingi hujikuta wakitaka kutangaza uwepo wao mahali fulani na kusema wanakwenda kufanya nini.Pongezi kwa Diamond na tunamtakia mafanikio zaidi na aendelee na moyo wa kutoa.

Maneno Ya Diamond Baada Ya Kutoa Ngoma Mpya

Diamond Platinumz ni moja kati ya wasanii wakubwa ambao wamekuwa na roho ya kuthubutu kufanya kitu chochote ili mradi tu aweze kufanikiwa kimuziki, Diamond ambae tangu ameingia katika soko la muziki amekuwa ni mtu wa kufanya vizuri kwa kila ngoma anayoimba haijalishi ameshirikisha, ameshirikishwa au ameimba peke yake. Diamond ambae pia amekuwa mfano bora kwa baadhi ya wasanii na kujitolea kusaidia wasanii chipukizi wadogo na kuwakuza mpaka kujulikana Duniani kote anastaili kupewa pongezi kwa juhudi anazozionesha kila siku katika muziki na jinsi anavyoiwa vizuri Tanzania.

Ikiwa ni kama siku tatu tu zimepita tangu Diamond atoe wimbo wake mpya na kundi kubwa la muziki  Duniani MorganHeritage unajulikana kama Hallelujah , msanii Diamond aliwakaribisha mashabiki wake kuangalia wimbo huo lakini aliwaambia pia mashabiki kile alichojifuunza baada ya kufanikiwa kutoa collabo hiyo.

Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram Diamond aliandika'”#Hallelijah ft@morganheritage LINK IN MY BIO !(nyimbo hii ya #Hallelujah Imenifunza kwamba  uwoga wetu na kutokujiamini unaotucheleweshea muziki wetu  kuwa mkubwa Duniani,…pia umenifunza kuwa  ukithubutu kila kitu kinawezekana ….Lakini pia imenifunza pia  kuwa wana afrika mashariki  tuna nafasi nzuri ya kuweza kuvuma duniani. Imenifunza pia kuwa  hata ukiimba Kiingereza  ila nyimbo ikiwa nzuri  itapendwa na kuvuma kote hadi Uswahilini… Imenifunza pia mwenyezi mungu hana upendeleo ukijituma,ukawa na nia nzuri  na ukimuomba atakuoa…..je wewe umejifunza nini)” haya ni maneno aliyoandika diamod huku pia akiwauliza mashabiki wake waweze kutoa maoni yao katika wimbo huo.

Wimbo wa Diamond na Morgan unaweza kuwa kithibitisho tosha kwa wasanii wengine kuwa kumbe kama una nia na unaweza kuthubutu basi unaweza kufanya vizuri, lakini pia Diamond amekuwa ni msanii anaejituma na kupambana sana ili kupata collabo kutoka nje ya nchi na akiaamini kuwa ili muziki wake ukue basi anawahitaji watu hao.diamond ametoa wimbo  na wasanii wengi wakubwa duniani kama Ne-yo , P-square,.

Kama alivysema kutokuogopa kumemfanya aweze kusonga katika katika muziki, Diamond amekuwa kweli ni msanii mwenye kujaribu bila kuwa na uoga, nathanisasa ni muda wa wasanii wengi kuiga kile anachokifanya msanii Diamond.

 

Diamond Aandamwa Tena ,Tetesi Mpya Zaibuka.

Ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu msanii  mkubwa wa Bongo Fleva nchini kuamua kufunguka katika vyombo vya habari na kusema na kukiri ukweli juu ya tuhuma nzito zilizokuwa zikimuandama juu yake kuhusu yeye kutelekeza mtoto aliyezaa na video queen maarufu nchini,Hamisa Mobeto .Msanii huyo alisema ukweli kuwa mtoto huyo ni kweli wa kwake na sio kweli alikuwa haihudumii ila tu aliamua kufanya siri kwa sabbu kuna vitu alitaka kuviweka sawa ilhali msanii huyo tayari anafamilia yenye  watoto wawili.

Jana Septemba 21, katika mitandao tena kumeibuka kwa tetesi nyingine mpya ambazo hazizathibitishwa na pande zote mbili kuwa Diamond alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Miss Burundi mwaka 2012, hata hivyi taarifa hizo zinadai kuwa mlimbwende huyo ana watato wawili mapacha  aliozaa na msanii huyo mkubwa nchini na aliamua kuitelekeza mimba ya watoto hao mara tu alipojua habari hizo.Hata hivyo katika ukurasa huohuo wa instagram   huyo anaelezea jinsi yeye na Diamond walivyokutana Burundi alipokuwa kwenye show, na kipindi icho Diamond alikuwa bado hajakutana na Zari ambae ndio mama wa watoto wake wawili.

Kwa mujibu wa mwandishi wa ukurasa huo wa Instagram , anaeleza kuwa hata mama wa watoto wa Diamond anamjua yeye na anajua kuwa ana watoto wawili mapacha ambao amezaa na msanii huyo, akionekana kuandika kwa shida lugha ya kiswahili aliandika kuwa watoto hao mapacha ni wa msanii Diamond na msanii huyo amewakataa.

Ingawa imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wasanii kukutwa na tetesi za kutelekezwa  watoto lakini inakuwa kama tofauti kwa  Diamond kwa sasa kutokana na swala la kifamilia ambalo limetokea hivi karibuni.Tangu tetesi hizo zitokee msanii huyo hajaamua kusema chochote ukizingatia ni taarifa zilizozuka tu katika mtandao wa Instagram.katika  interview yake Diamond alikaririwa  akisema kuwa mtu yeyote anaejiamini kuwa mtoto aliyenae amezaa na yeye basi amlete na yeye atakubali.

Hata hivyo kama kawaida ya watu wa  mitandao , maneno uwa hayakosekani, wameendelea kumtuhumu na kumtupia maneno msanii huyo bila kuwepo na uhakika wa taarifa hizo huku wakifananisha watoto hao na mtoto wa kike wa kwanza wa msanii huyo.Nadhani ni wakati wa kusubiri ili msanii huyo aweze kufunguka kuhusu taarifa hizo.

Mamia Wampongeza Diamond na Zari

Jana  Septemba 19 katika kurasa nyingi za mtandao ya Instagram kulikuwa kulikuwa kukipostiwa picha za Diamond huku wakimpongeza kwa hatua nzuri aliyoichukua ya kukubali kuwa yeye ndie  baba kwa mtoto wa Hamisa.

Diamond ambae siku ya jana alikuwa akiongea na waandishi wa Leo tena katika Television ya Clouds, aliamua kufunguka na kusema ukweli kuwa alikuwa na mahusiano na mwanadada mrembo Hamisa Mobeto na amepata nae mtoto ,tetesi ambazo zilikuwepo kwa muda mrefu na Diamond  Alikuwa akipinga tetesi hizo kwa mara ya kwanza.

Baada ya Diamond kukubadi kuwa Abdul Naseeb ni mtoto wake baadhi ya viongozi walimpongeza Diamond kwa hatua hiyo.Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Saalm Paul Makonda “Thamani yako kwangu bado ni kubwa sana , kwani uwezo wako wa kupita kwenye dhoruba na ukabaki imara na familia yako unaendelea kukupa heshima”.aliandika hivi kwa Zari

Pia mbunge wa Mikumi mh. Joseph Haule aliandika hivi “Ukweli humuweka Mtu huru kweli kweli, Big up mdogo wangu @diamondplatnumz Umekuwa Mfano bora sana,”

Ukiachana na viongozi kuna wasanii kama Bactuli Actreess , Faiza ally, Tanzanian Sweetheart Wema Sepetu , ukiachana na kuwa alikwishaachna na Diamond lakini pia alimpongeaza na kuandika”he is such a brave soul”  pia hakuacha kumpa heshima yake Zari The Bosylady ambae ndio mama halali wa watoto wawili  na anaejulikana kwa diamond ,ukiachana na kwamba kiindi cha nyuma wawili hao wawikuwa katika migogoro pia.

Diamond alichukua uamuzi wa kukubali mtoto wa hamisa baada ya kuzongwa kwa muda mrefu na maneno ya mitandaoni,lakini pia picha zilizovuja zikiwaonyesha yeye na hamisa wakiwa chumbani.Hata hivyo Diamond amekubali kosa ilo na kuiomba msamaha familia yake kwa kudhalilika katika mitandao kwa sababu ya ujinga wake.Lakini pia Diamond amemtaka hamIsa kufikiria biashara ya kufanya ili kumsaidia yeye na mtoto huyo, pia Diamond amehakisha kuwa yeyey na Zari hawataachana yuko radhi kupiga magoti Tanzania mpaka Afrika ya Kusini kuomba msamha kwa Zari.

Zari amjia juu mzazi mwenzie

Ikiwa hata interview haijaisha kati ya Diamond na kituo cha habari cha Clouds Media Zari amjibu mzazi mwenzie kuhusu yale aliyokuwa anayasema leo katika interview iyo.Diamond ambae leo ameamua kusema ukweli kuhusu tetesi zilizokuwa zinasambaa mitandaoni juu ya mtoto wa video quen Hamisa Mobeto .

Diamond amekiri kuwa alitembea na Hamisa na amepata mtoto nae  na kusema kuwa alishaongea na mzazi mwenzie (Zari) na kwamba mama wa watoto wake yuko sawa na walishayamaliza lakini Zari ameonekana kupinga maneno hayo .

Katika ukurasa wake wa Snapchat Zari aliandika “haha… u playing yourself ..the lies telling about me knowing about your side chic..try and fix your mess and stop  with lies .Me being quite doesnt mean am stupid .Be very careful with your words’ aliandika zari akikanusha kuwa kitendo cha Daimond kusema kwa yeye alikuwa anajua juu ya yeye kuwa na mahusiano na Hamisa ni uongo.

Hata hivyo Zari anaongezea na kusema kuwa  kitendo cha yeye kukaa kimya ni kwa sababu yeye ni mama wa watoto wake ” i may be the mother of your kids  and that’s the reason am keeping silence &respect. You might want to Google about ‘Defarmation of character law suit’ Dont try me” aliandika Zari

Majibu haya yamekuja baada ya Diamond kukubali na kuomba msamaha kuhusu ukweli kuwa mtoto alizaliwa kwa Hamisa Mobeto ni wakwake lakini alikaa kimya ili kuweka kwanza mambo sawa ndipo atangaze.

Akiwa bado katika  mahujiano Diamond aliulizwa kuhusu maneno hayo aliyopost mama wa watoto wake , na alijibu hivi “Anavyosema hivyo namuelewa  anachokizungumza,najua hawezi kuwa sawa kwa muda huu, lakini pia yapo baadhi ya mambo nimeyazungumza hapa  ,  hakuwahi kuyasikia.” alipoulizwa ni mambo gani alijibu vitu kama ela za matumizi , kumnunulia gari Hamisa ni vitu ambavyo hakuwahi kumwambia Zari ivyo ana haki ya kuijsikia vibaya.

Zari na Diamond  wamekuwa katika mahusiano kwa miaka zaidi ya mitatu na wamefanikiwa kupata watoto wawili wakike moja na kiume mmoja.

Diamond akiri kuzaa na Hamisa Mobeto

Hatimaye  msanii mkubwa wa Bongo Fleva nchini Diamond Platinumz ameamua  kusema ukweli kuhusu tetesi zilikuwa kuwa zikisambaa mitandaoni  kuhusu ujauzito wa mwanadada video queen maarufu nchini Hamisa Mobeto.Diamond amesema ukweli baada ya kuenea kwa picha na video clips nyingi mitandaoni zikimuonyesha akiwa kitandani na mwanadada .

akiongea katika kipindi cha leo tena Cha clouds tv, Diamond amekiri kuwepo na mahusiano kati yake na Hamisa kipindi cha nyuma na hapo katikati walirudiana ilhali mrembo huyo akijua  kuwa Diamond ana familia .

“Mimi na Hamisa tulikutana tangu mwaka 2010, tukawa na mahusiano lakini mahusiano yetu hayakudumu, kipindi icho nilikuwa sijakutana na Wema wala Zari.” akiri diamond “kipindi nipo na zari alianza kunirequest turudiane  lakini nilimwambia mimi nina familia tayari,tukaendelea..baada kama ya siku tatu habari zikaanza kusambaa mitandaoni Diamond anatembea na hamisa” amesimulia.

‘Baada kama ya miezi alinipigia simu kuwa  ana ujauzito wangu, basi nikamuuliza yeye ameamuaje, nikamwambia sawa ila mimi nina familia yangu , nilikubali na nikaanza kulea ujauzito wangu” amekiri diamond

“Mpaka mimba inakuwa , kila siku alikuwa anapokea si chini ya elfu sabini kwa siku,na hata mimba ilikuwa kubwa nilimnunulia Rav4, na tushakubaliana tukae kimya ,sikuwa tayari kuzungumzia swala ilo kwenye media”

Baada ya kuona maneno yanazidi katika mitandao Diamond aliamua kumwambia ukweli mzazi mwenzie zari na kukiri kosa lakini alimwambia hamisa hana haja aya kumtukana zari na watoto wake maana watoto watachukiana wakati wote ni wake.

Diamond anasema kuwa alikuwa akimuhudumia hamisa, na hata alipoenda kujifungua aliacha zaidi ya mil7 kwa ajili ya shopping ya mtoto na bado akampa ela kwa ajili ya kujifungua, anakiri kuwa ni ujinga wake ndo ulifanya yote yakatokea  “familia yangu imetukanwa kwa sababu ya ujinga wangu.. nilitoka uingereza usiku nikaenda kulala na mtoto wangu ”

Diamond anakiri kuwa alikuwa karibu na Hamisa kwa sababu alikuwa anaamini kuwa mtu anapokuwa na tumbo(ujauzito) hapaswi kujisikia vibaya.hata hivyo Diamond ameomba radhi kwa familia yake, watoto wake na mama mzazi wa watoto wake Zari.

 

 

Picha za Hamisa na Diamond zavuja

Ni zaidi ya mwaka sasa  upite tangu kuwepo na tetesi za kuwepo kwa mahusiano kati ya msanii wa Bongo Fleva Diamond Platinumz na video queen maarufu wa Bongo Hamisa Mobeto.Hamisa ambae amekuwa akitishia uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na mzazi mwenzie  na msanii  huyo Zari The Bosylady,hata hivyo  miezi michache iliyopita  Hamisa alijifungua mtoto wa kiume aliempa jina la Prince Adbul Nasib  au’ Tanzania baby’, mtoto ambae inasemekana  kuwa ni mtoto wa Diamond Platinumz huku akiongeza idadi ya watoto wa msanii huyo mkubwa kuwa watatu .Tangu kuwepo kwa tetesi hizo Diamond mwenyewe amekuwa akikanusha tetesi hizo na kusema  kuwa hana uhusiano wowote na video queen huyo ,zaidi ya mahusiano ya kikazi tena hasa walipokutana katika kushoot video ya wimbo wa ‘salome’ , wimbo  ambao uliozua mambo mengi na ndipo tetesi za wawili hao kutoka ulipoanza kusambaa.

Zari , mama mzazi wa watoto wawili aliozaa na Diamond amekuwa akijikuta katika vita ya kimtandao na mashabiki na hata Hamisa mwenyewe huku  sababu kubwa ikiwa ni kuwepo kwa   tetesi hizo. Pamoja na hayo yote nata   Hamisa mwenyewe  amekuwa akirusha madongo  hewani bila kudhibitisha  moja kwa moja ukweli wa tetesi hizo.

Wapo mashabiki wanaosema kuwa wawili hao (Hamisa na Diamond ) wamekuwa wakionekana pamoja baadhi ya maeneo, lakini  pia ukiachana na hayo, kipindi ambacho Hamisa Mobeto amejifungua wanafamilia wa Diamond walikuwa ni moja ya watu wa karibu walikwenda kumtembelea Hamisa  hospitali ambapo alilazwa mrembo huyo.

Baada ya tetesi hizo kuwepo kwa muda sasa, zimevuja picha  zinazosadikika kuwa ni picha za Diamond na Hamisa Mobeto wakiwa chumbani , huku mkono wa diamond wenye kuonyesha tatoo yake, hata hivyo picha zingine zinazoendelea kusambaa ni zile zinazimuonyesha Hamisa yupo kwenye chumba ambacho ni chumba cha kulala cha Diamond na mama watoto wake huku eneo ilo likionekana kufafanana kabisa na lile ambalo Zari amekuwa akipost picha katika ukurasa wake wa instagram kama sehemu yake ya kulala pia.

Diamond ,Vannessa,Alikiba kuwakilisha Tanzania tuzo za MEAMA

Wasanii Diamond, Vannessa pamoja na Alikiba wamechaguliwa kuwania  katika tuzo za Middle East Africa Music Award (MEAMA) ,tuzo hizo ambazo zinapangwa kufanyika tarhe 5 Oktoba mwaka hu zina lengo la kuibua vipaji na kuonyesha amasa kwa wasanii wa africa kwa ujumla.Akiongea katika uzinduzi wa tuzo hizo kwa awamu ya pili CEO  wa FAJ GLOBAL ENT.L.T.D ,MAJESTICAL ROYAL CLUB (MRC)  na pia ni mwenyekiti wa FAJ ONLINE-RADIO Mr. Fajuyi Adeniyi Oluwaseun amesema kwamba wanaahidi kuwa kwa mwaka huu tuzo izo zitakuwa zenye ubunifu zaidi na zina kuwa na lengo la kuibua vipaji vingi zaidi ili kuendelea kuipa sifa na kuitangaza Africa.

Tuzo hizo ambazo zimejumuisha  washiriki wengi  ambao wametoka nchi mbalimbali za Africa kama Kenya,Uganda, Nigeria, South Sudan,Tanzania, Egypt na zinginezo jana tarehe 13 Septemba imeelekezwa kuwa majina ya washiriki kutoka nchi zote yanapatikana katika website ya tuzo hizo hivyo mashabiki  waweze kuwapigia kura wasanii wao wanaowapenda ili waweze kujinyakulia tuzo izo.

Kwa upande wa Tanzania msanii wa kike Vannesa Mdee ndiye   msanii pekee wa kike kutoka nchini hapa aliyewekwa katika kategoria ya msanii bora wa kike wa mwaka huku akichuana na  Victoria Kimani,Yemi Arade na Seyi Shayi, kwa upande wa wanaume yupo alikiba  katika kategoria ya msanii bora wa kium wa mwaka,pamoja na Diamond Platinumz katika kategoria ya wimbo bora ya mwaka na wimbo wa Eneka .

Wasanii wengine wanaoshiriki kuwania tuzo izo kutaka nchi tofauti na Tanzania  ni pamoja na Davido,Wizkid,Mr.Eazi katika kategoria tofauti tofauti.

Mashabiki wanahamasishwa kupigia kura msanii anaependa kushinda katika tuzo izo,na jinsi ya kupiga kula ni kuingia moja kwa moja katika website ya tuzo izo (MEAMA) ambapo upigaji wa kula umeanza mara baada ya kutangazwa kwa washiriki huku mwisho wa kupiga kula ikiwa ni tarehe 30 septemba mwaka huu na tuzo kufanyika oktoba 5 nchi Egypt.Tunawatakia mema wasanii wote waliopo katika kategoria mbalimbali , muziki wa Africa unafika mbali kwa sasa.

Faiza Ally: Tanzania nzima na East Africa tunatakiwa tumpenda Diamond sana

Faiza Ally amedai kuwa ni sharti Tanzania na Afrika Mashariki nzima kumpenda Diamond. Mrembo huyo aliandika ujumbe wake kwenye mtandao wa Instagram.

Ally alimpigia kifua Diamond kwa kusema kuwa muziki wa Tanzania haukua na ushindani kabla ya Diamond kuingia kwenye game.

“Hivi hamjawaji kujiuliza kwamba toka zamani kabla ya Diamond kulikua na mziki mzuri lkn hakujawahi kuwa na ushindani kama changamoto alio leta Diamond kwenye game. Hivi mnajua kwamba Tanzania nzima na East Africa tunatakiwa tumpenda Diamond sana ???? Hivi hamjawaji kujiuliza kwamba toka zamani kabla ya Diamond kulikua na mziki mzuri lkn hakujawahi kuwa na ushindani kama changamoto alio leta Diamond kwenye game , sasa nasema hivi mziki mzuri peke yake hautoshi na akili kubwa inahusika , unapo kuwa huna akili ktk unalo lifanya ni sawa na mwanamke mzuri hlf hajielewi…. Leo hii kwa u star wenye akili alio uleta Naseeb wazazi wengi wanaona fursa ya mziki kupitia Diamond tofauti na miaka ya zamani, mziki ulikua unaonekana kama sio kazi lkn Leo mziki unaendesha familia nyingi, hata mm ningependa mwanangu awe mwanamziki mwenye mafanikio kama Diamond , sasa nasema hivi ku mpenda Diamond ni amri sio ombi,” aliandika Faiza Ally.

Aliandelea kwa kusema kuwa Diamond ni kama Obama:

” Diamond ni kama Obama marekani kwa watu weusi , yeye alionyesha kuwa mtu mweusi ana uwezo kwenye siasa na Diamond tanzania kaonyesha mziki unalipa na msisahau katoa vijana wengi na bado wengine wamepata ajira kupitia yeye na naona watapata wengi zaidi ! Sasa nakuomba D ufungue music school basi tuwalete watoto wetu na wenyewe wapate mkwanja kama wako maana shule sio maisha pekee mention town na vipaji navyo ni sehemu ya mafanikio ktk maisha a special kwa maisha tunayo elekea , mm nakupendaga sana na zaidi ni jitihada zako kwenye kazi ! Keep it up dogo ? #ZILIPENDWA”