Nedy music Atamani Mtoto

Baada ya kushinda Tuzo Kutoka nchini Ghana msanii Nedy Music sasa ametangaza kilio chake kuwa mwaka huu anahitaji kupata mtoto ingawa wa kuzaa nae hajamjua.

Akiwa kwenye mahojiano Nedy Music maarufu kwa sasa kama mpemba mmoja amesema “Natamani kupata mtoto mwaka huu na kabla ya mwezi wa 12 ila bado sijapata mama wa huyo mtoto natamani nimpate kipindi hichi”

Aidha Nedy amekuwa mtu ambaye hapendi kuweka mahusiano yake hadharani japo huko nyuma alishakuwa na tetesi za kutoka na binti mmoja mwenye pesa zake ni mtazania ambaye anaishi Dubai.

Nedy Music Afungukia Mipango Ya Kolabo na Vanessa Mdee

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nedy Music amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kufanya kolabo na msanii mwenzake wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

Nedy Music ambaye amekamata headlines kwa siku kadhaa sasa Baada ya kujishindia tuzo za Afrimma zilizofanyika nchini Ghana ameweka wazi Kama ana mpango wa kufanya kolabo na Vanessa Mdee.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Nedy Music amesema si kweli kwamba walifanya kolabo nchini Ghana walipokutana Kama tetesi zinavyosambaa kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa.

Hapana sijafanya kolabo na Vanessa Mdee nchini Ghana na kama kutakuwa na kolabo itafanyika nchini Tanzania”.

Nedy Music na Vanessa Mdee walikutana na nchini Ghana ambako wote wawili walikuwa wamechaguliw kushiriki tuzo hizo lakini Vanessa hakuweza kupata tuzo hizo na Nedy alifanikiwa kijinyakulia tuzo moja.

Nedy Music Anyakua Tuzo za Afrimma Nchini Ghana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya ‘Pozi kwa Pozi Entertainment Nedy Music ametangaza rasmi kupokea tuzo ya Afrimma siku ya jana.

Nedy Music,  alishinda  tuzo ya All Africa Music Awards 2018 (AFRIMA) usiku wa kuamkia leo Novemba 25, 2018 nchini Ghana kipengele cha African Fans Favourite.

Asante Kwa Wote Mnaonipa pongezi Natamani kujibu hata mmoja mmoja kwa furaha??Hii Ni Tuzo Yetu Wote?Thanks once again kwa upendo na Sapoti yenu?? Kubwa Mnoooo #MPEMBAMMOJATU”.

Haya ni baadhi  ya Majina ya wasani mbali mbali walionyakua tuzo hizo za Afrimma 2018:

Album of the Year
Betty G – Wegegta (Ethiopia)

 

Best Artiste, Duo or Group in African Contemporary
Kidi (Ghana) – ‘Odo’ remix ft Mayorkun, Davido

 

Best Artiste, Duo or Group in African Hip Hop
M.anifest (Ghana) – Me Ne Woa ft King Promise

 

Best Artiste, Duo or Group in African Pop
2baba (Nigeria) – ‘Amaka’ ft Peruzzi

 

Best Artiste, Duo or Group in African Dance or Choreography
Mr P (Nigeria) – Ebeano

 

Best Artiste, Duo or Group in African Ragga, Reggae or Dancehall
Stonebwoy (Ghana)

Nedy Music Adai Ataoa Wanawake Wanne

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na wimbo wake wa ‘Homa Ya Jiji’ Nedy Music amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuoa wanawake wanne katika siku za mbeleni.

Lakini pia Nedy amedai kwa yeye kama Muislamu anaruhusiwa kuoa idadi hiyo ya Wanawake Lakini pia amedai anataka kuzaa watoto wengi kadri atakavyoweza hata ishirini.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Nedy Music amefunguka haya:

Mimi Baba yangu alioa wanawake wanne hata kwangu kama nitajaliwa riziki ya kutosha basi nitaoa wanawake wanne panapo majaaliwa na hata watoto nataka kuwa na hata timu inshallah na hata wakifika ishirini mimi ninao uwezo wa kuwaandaa”.

Lakini pia Nedy Music amemkingia kifua Ommy Dimpoz na kumtetea dhidi ya tuhuma kuwa ametafuta kiki kwa kusambaza taarifa kuwa yupo ICU na kusema Ommy hawezi kufanya kitu kama hiko maana sio mtu wa kiki.

Nedy Music Afungukia Hali Ya Kiafya Ya Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri katika Tasnia hii ya Bongo fleva amefunguka hali yake ilivyo kwa sasa kutokana na kuumwa kwa Msanii mwenzake Ommy Dimpoz.

Wiki chache zilizopita Ommy Dimpoz alitangaza kwa mara ya kwanza kuwa alikuwa hoi hospitalini akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa operesheni Kwenye shingo.

Ommy Dimpoz aliweka wazi kuwa tangia kipindi kile hali yake ilikuwa imeanza kuimarika kwa kiasi kikubwa.

Nedy Music ni mmoja kati ya wasanii waliopo chini ya label ya Ommy Dimpoz inayoitwa PKP Entertainment na amefunguka hali ilivyo tangu Ommy Dimpoz aanze kuugua.

Kwenye mahojiano na Clouds FM, Nedy Music amekiri kuwa  kipindi hiki ambacho Dimpoz anaumwa kuna vingi anavikosa kutoka kwake.

Kuna vitu vingi ambavyo navimisi kutoka kwa Ommy Dimpoz haswa kipindi hiki anachoumwa. Ni mtu ambaye ananishauri mambo mengi, na mara nyingi huwa tunakaa na kusikiliza kazi zetu”.

Ommy Dimpoz bado yuko nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Nedy Muziki Awaumbua Washkaji Wanaomsumbua Mpenzi Wake.

Msanii anaetamba na kibao chake cha one and aonly alichomshirikisha Ruby amefunguka na kuwarushia madongo baadhi ya washkaji zake ambao wamekuwa wakimsumbua mwanamke wake kwa kumtongoza na kusema kuwa anaawajua kwa sababu anaona meseji zote ambazo zinakuwa zinaingia katika simu ya mpenzi wake huyo.

Akiandika hayo katika ukurasa wake wa instagram akiwa ameweka  picha yake na mpenzi wake huyo Nedy muziki anasema kuwa  anawajua watu wote alionao karibu ambao wamekuwa wakimfanyia majungu kwa mpenzi wake huyo na hata wale ambao wamekuwa wakimtongoza shemeji yao na screen shots anazo hivyo anawasubiri kuwaumbua na wala haogopi kufanya hivyo.

Kama nawaona washkaji zangu wanafiki wanavyohaha muda huu kujiuliza files zao na amdishi yao ya kishamba yoote nnayo, screenshots, txt za majungu na kujitongozesha zaidi kweli washkaji zangu ku…..nyoko #mpemba haachimpakakufa #jiandaekufichasurayakokwaaibu.

Imekuwa ni kama tabia kwa wasanii kuwa wanatafuta kiki ywa kutangaza kuwa wasanii na washkaji zao wamekuwa wakiingilia mahusiano yao au kuwatongoza wanawake zao , na baada ya hapo kiki hiyo inaweza kuja kuzimwa kwa kuachia wimbo mpya, haijajulikana kwa Nedy amekuwa akimlenga nani.

 

Nedy Music Adaiwa Kumtosa Ommy Dimpoz

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nedy music amefungukia tuhuma na maneno yanayondelea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amemtosa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz.

Nedy Music alianza sanaa yake ya muziki akiwa kama msanii anayejitegemea kutokana na kipaji chake alichukuliwa na Ommy Dimpoz na kusainiwa chini ya label ya Pozi kwa Pozi (PKP).

Lakini baadae Ommy Dimpoz na yeye alienda akasainiwa chini ya label ya Alikiba Rock star 4000 na tangia hapo kukawa na tetesi kuwa Nedy Music amejitoa PKP.

Lakini pia tetesi hizo zilizidi kushika kasi Siku mbili hizi baada ya Nedy Music kutoa wimbo wake mpya aliomshirikisha Ruby na kwenye video hiyo hapakuonekana logo ya PKP hivyo kusemekana amejitoa PKP.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews Nedy Music amefunguka na kukataa tuhuma hizo na kuweka wazi kuwa bado yuko PKP:

Mimi najibu kuwa nipo PKP bado sijatoka na CEO ni Ommy dimpoz na PKP bado tupo kama kawaida.

Naomba Mashabiki waendelee kusapoti kazi zangu maana nafanya kwa ajili yao kwaiyo wasiniangushe wanipe tu sapoti ya kutosha”.

Nedy Music Atamani Kufanya Kazi na Alikiba na WCB

Msanii wa Bongo fleva Nedy Music anayefanya vizuri hivi sasa na wimbo wake wa One and only amefungukia mipango yake ya kufanya Kolabo na staa wa Bongo fleva Alikiba Lakini pia kusainiwa WCB.

Nedy Music anayefanya muziki wake chini ya label ya PKP ya msanii Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo itatokea nafasi ya yeye kusainiwa WCB basi ataichukua kwani ni uamuzi wa kibiashara:

Nedy Music amefungukia  kusaini katika label ya WCB amesema ikitokea nafasi hiyo atasaini kwa sababu ni biashara, pia amekanusha taaarifa za kuachana na label yake ya PKP mara baada ya wimbo wake mpya kutoka bila kuwa na logo ya label hiyo.

Kwenye Interview aliyofanya na The Playlist ya Times Fm, Nedy Music aliweka wazi kuwa yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba lakini anataka afanye naye kazi huku watu waone amestahili kufanya naye kazi kwa ajili ya kipaji chake alichonacho na sio sababu anamfahamu tu Kiba basi ndio afanye naye Kolabo:

Unajua usifanye kitu kimazoea, usifanye kitu kwakuwa unajuana na mtu nilitamani watu wajue uwezo wangu, nikiwa na maana hata pale ninapoenda na kazi nataka afanye na mimi basi pawe na urahisi na si kinyonge atafanya kwa kuwa tunajuana, kwa hiyo ni wazo bado lipo na panapo majaliwa litatokea”

.