Baba Dimpoz Aibuka na Kumchagulia Mwanaye Mke Wa Kuoa

Baba wa Msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz, Faraji Nyembo ‘Baba Dimpoz’ ameibuka na kumchagulia mwanaye mke wa kuoa kuangalia sifa na tabia.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Baba Dimpoz alisema vijana wengi siku hizi wamekuwa wakiwachagua wanawake wa kuoa kwa kuangalia maumbile ya nje, jambo ambalo siyo sawa kwani watajikuta wanajuta baadaye wakishaingia kwenye ndoa.

Lakini pia aliendelea kusema kwa upande wa mwanaye Dimpoz anamshauri akifikia muda wa kuoa aangalie mwanamke mwenye hofu ya Mungu, yaani mcha Mungu, mwenye akili ya maisha, busara na familia anayotokea na asiangalie shepu na sura kwani atakuja kujilaumu baadaye.

Unajua Dimpoz kwa mama yake yuko peke yake na mama yake alishafariki dunia hivyo anatakiwa akitaka kuoa amtafute mwanamke mwenye hofu ya Mungu ambaye atakuwa faraja kwake, atakuwa mke bora pia kwa upande mwingine awe kama mama kwake na asiangalie shepu, sura au ustaa.

Tatizo la vijana wa siku hizi wanapenda sana kuangalia sura na shepu hata wakishauriwa vipi wanaona ni ujinga, lakini cha muhimu wanachotakiwa kuangalia wanapochagua wake waangalie wacha Mungu na wenye tabia njema”.

 

Mama Diamond Afungukia Uhusiano Wa Ommy Dimpoz na Zari

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra Kassim maarufu kama Mama Diamond amefunguka na kuongelea uhusiano na kinachoendelea kati ya Zari na Ommy Dimpoz.

Siku chache zilizopita msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ na mzazi mwenzake na Diamond Zari the Bosslady walitengeneza headlines baada ya picha zao wakiwa pamoja nchini South Africa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi, Mama Diamond amesema kuwa ukaribu wa Zari na Dimpoz ni wa kawaida kama watu wengine na kuwataka watu waache maneno maneno yasiyo na msingi.

Kwani kuna ubaya gani? Hivyo ni vitu vya kawaida kwa mtu kukumbatiana na mtu aliyekutana naye Mimi sijaona hiyo picha ambayo kamshika pajani lakini bado nasema hayo ni mambo ya kawaida tu. Ina maana Zari asiongee na watu? Watu wanasema Nasibu na Ommy wana ugomvi, mimi sijaona wakipigana, najua wanaongea na wala mimi sina ugomvi na mtu”.

Siku za nyuma Diamond aliwahi kuingia kwenye ugomvi mzito na Ommy Dimpoz uliopelekea kutukanana matusi ya nguoni hadi Ommy kumkashifu Mama Dimoand lakini tangu alipougua kuna tetesi kuwa bifu hilo limeisha na wasanii hao wamesahameana.

 

Ommy Dimpoz Uso kwa Uso na Zari

Mwanamama Zari the bossy amekutana uso kwa uso na msanii Ommy dimpoz ambae hapo awali iliwahi kuripotiwa lkuwa alikuwa na bifu na mwanaume aliyezaa  watoto na mwanamama huyo.

Hata hivyo Zmmy na zari wamekutana nchini afrika ya kusini ambapo ndipo kuna makazi maarum ya zari na familia yake na pia ndio kumekuwa makazi ya ommy dimpoz kwa sasa na uongozi wao.

Hata hivyo haijafahamika sana kuwa wawili hao walikutana kwa sababu ya tukio gani lakini imekuwa ikionekana kuwa mkutana wao umekaa kikazi zaidi.

Ikumbukwe kuwa pindi cha mahusiano ya Zari na Diamond  hakukuwa na ukaribu kati ya Ommy na zari na picha hiyo imezua gumzo kwa sababu ya mahusiano yaliyopo kati ya diamond na Ommy.

Picha Za Irene Uwoya na Ommy Dimpoz Zazua Mazito

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali Irene Uwoya amekuwa  anatrend sana Kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kuvunjika kwa ndoa yake na staa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku ya jana Uwoya amerudi Kwenye headlines kwa ajili ya picha zake alizopiga na msanii mwingine wa Bongo fleva Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz ambaye alikuwa mgonjwa kwa Miezi kadhaa baada ya kufunyiwa upasuaji wa koo nchini Afrika ya kusini.

Siku ya jana wawil hao wamezua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana wakiwa pamoja baada ya kila mmoja kiposti picha hizo Kwenye kurasa zao za Instagram.

Mashabiki wengi wa Uwoya walimtaka aanzishe Mahusiano na Ommy na kudai ndio anaendana naye kuliko hata Dogo Janja.

Wawili hao hawajaweka wazi sababu ya kuonekna pamoja kama ni wako ktika harakati za kuleta project ya pamoja au ni Mahusiano.

Ommy Hatoimba Tena , Hilo Najua :-Steve nyerere.

Msanii wa vichekesho nchini, Steve Nyerere amefunguka na kusema kuwa anavyojua kuhusu hali ya ommy dimpoz mwanamuziki huyo hawezi kuimba tena kwa sababu hana sauti kama aliyokuwa nayo hapo mwanzo.

steve anasema kuwa tangu hapo awali yeye alikuwa mtu wa kwanza kujua hali ya Ommy lakini hata aliposema hadharani wapo waliomuona kama anataka kiki hivyo waliamua kumbeza lakini yeye alikuwa akijua ukweli.

Ommy ni mwanamuziki na mungu amembariki namimi ndio mtu wa kwanza kumposti na kusema ommy pole sana kwa maradhi hayo, wengune wakanibeza lakini nilikuwa najua nini kinaendelea.tunachotakiwa kufanya, najua ommy hatoimba tena kwa sababu ili uimbe inabidi uwe na vocal 

Ikumbukwe kuwa Ommy dimpoz alifanyiwa uapasuaji wa koo kutokana na atahari alizopata baada ya kuonekana kuwa alikunywa kinywaji chenye sumu kilichoharibu mfumo wake wa koo na kusababisha kushindwa kumeza vitu.

 

“Mwenyezi Mungu Ndio Muumbaji Wa Wanyonge na Wajanja”- Ujumbe Wa Ali Kiba Kwa Ommy Dimpoz

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amemtumia salamu za Birthday njema Msanii mwenzake na rafiki yake Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz.

Siku ya leo ni siku ya kuzaliwa ya Ommy Dimpoz na rafiki yake na mtu wake wa karibu kabisa Ali Kiba kamuwish Birthday njema na ujumbe mzito.

Ali Kiba amemtaka asijali sana wala asiyawaze yale magumu aliyopitia Miezi michache iliyopita baada ya kulazwa hospitali kwa Miezi karibia mitano badala yake amshukuru tu Mwenyezi Mungu.

https://www.instagram.com/p/Bnp-7T9ll_E/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1azp61dlmsurf

Kwenye posti yake ya leo ya birthday Ommy Dimpoz amemshukuru sana Ali Kiba kwa kuwa naye kipindi chote cha ugonjwa na hata kuweka wazi kuwa amemuuguza.

Ali Kiba alisimamisha kuachia kinywaji chake  cha Mofaya Miezi michache iliyopita baada ya kukizindua kutokana na maradhi ya Ommy Dimpoz.

Alichokiandika Ommy Dimpoz Katika Siku Yake ya Kuzaliwa.

Ikiwa leo ni 13 septemba , ni siku ya kumbukumbu ya watu wengi lakini pia ni kumbukumbu ya kuzaliwa ya msanii Ommy Dimpoz na aliamua kuweka picha yake aliyowahi kupigwa kipinid akiwa mgonjwa sana na akiwa katika chumba cha wagonjwa mahutiuti siku za nyuma.

Ommy dimpoz amweka picha hiyo na kuandika maneno yenye hisia sana huku akijaribu kumshukuru Mungu na watu wote kwa ujumla ambao wamekuwa nae kwa kipindi chote cha ugonjwa wake na maobi waliokuwa wakituma kwa mwenyezi mungu kwa ajili ya afya yake.

Ommy anasema kuwa haikuwa rahisi yeye kuwa katika hali ile lakini leo yuko mzima na  anaweza kurudi katika hali yake kama kawaida , lakini pia anwakumbusha watu kuwa ugonjwa ni ibada ambayo mungu anaamua kukupitisha ili kukukumbusha kuwa yeye yupo.

Ommy anasema kuwa kuna kipindi alikuwa tayari ameshakata tamaa kabisa ya kuishi , lakini alipokuja mgonjwa mwingine ambae alikuwa ameshambuliwa na majambazi na madaktari wakamtibu na kuokoa maisha yake ndipo alipoamini kuwa hata yeye mungu atampigania kwa sababu mungu ndie mwenye nguvu pekee yeye  haja haja ya kukata tamaa.

“Tusiishi Kwa Chuki na Uadui Maana Hatujui Kesho Yetu Itakuwaje”- Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo Maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuongelea hali yake ya kiafya baada ya kuumwa kwa zaidi ya Miezi mitano.

Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya Ommy Dimpoz ambaye alikuwa hoi mahututi kwa Miezi michache iliyopita baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo nchini South Africa.

Akiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa Ommy Dimpoz ameweka ujumbe mzito ambapo pia ameweka picha yake alipokuwa hoi taabani ICU.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ommy Dimpoz ameandika umuhimu wa kutokuwa na vinyongo wala chuki na watu maana hakuna anayejua sana wala siku ya kufa.

https://www.instagram.com/p/Bno_S2-gBcU/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=8ubavf33rhok

Ommy Dimpoz Atoka Afrika ya Kusini na Kutua Kenya.

Hii inaweza kuwa habari njema kuliko zote kwa mashabiki wa msanii Ommy Dimpoz ambae alikuwa mgonjwa sana hapo siku za nyuma na kuonekana kudhoofika sana kutokana na ugonjwa wa koo alikuwa ameupata huku sababu kubwa ikisemwa kuwa ni kutokana na sumu aliyowahi kunywa katika kinywaji.

Msanii Ommy Dimpoz sasa ameshatoka kule alipokuwa ambapo inawezekana kulikuwa kukiwapa watu wengi wasiwasi kutokana na ukaribu wa sehemu hiyo, Ommy Dimpoz ssasa yuko nchini Kenya na ameshatoka Afrika ya Kusini ambapo ndipo alipokuwa akipatiwa matibabu hayo.

Hata hivyo kwa picha mpya ilisambaa sana katika mitandao, msanii huyo amebadilisha muonekana huku muonekano wake ukionekana kuimarika na wa kupendeza zaidi na umekuwa ukitia moyo kulingana na hali aliyokuwa nayo hapo awali.

Muonekano wa Ommy Dimpoz kwa sasa.

Pamoja na kwamba haijajulikana  dhumuni la safari yake ya Kenya lakini mashabiki wamefarijika na kusema labda sasa ni wakati wa msanii huyo kurejea nyumbani na kuungana nae.

Viongozi wa Dini Wamfanyia Dua Ommy Dimpoz.

Viongozi wa dimi ya kiislamu kutoa katika mkowa Tabora ambapo ndipo baba yake mzazi na Ommy Dimpoz anapoishi kwa sasa wamejitokeza nyumbani kwa baba mzazi huyo na kufanya dua kwa ajili ya kuombea hali ya mtoto wake ambae mpaka sasa bado yuko Afrika ya Kusini akipatiwa matibabu.

Baba mzazi wa Ommy Dimpoz aliwahi kusikika baada ya kutangazwa sana kuwa mtoto wake amekuwa mgonjwa kwa takribani miezi mitatu sasa na kusema kuwa amekuwa akitamani ana kumuona mtoto wake huyo ambae anasikia tu kwamba ni mgonjwa.

Ommy Dimpoz aliripotiwa kuwa amefanyiwa upasuaji ya koo na yeye mwenyewe kuthibitisha hilo huku sababu kubwa ya ugonjwa wake ikisemwa kuwa ni sumu aliwahi kunywa katika kinywaji bila yeye kujua swala hilo.

Hata hivyo Ommy alithibitihsa kuwa kwa sasa anaendelea vizuri na afya yake ingawa bado anahitaji kuwa akiripoti hospitali mara kwa mara kwa ajili ya uchunguzi wa hali yake.

Baada ya kupata ubuyu huo waandishi wa habari wa GPL waliamua kumtafuta baba mzazi wa Ommy ili kuthibitisha hilo na ndipo aliwajibu”namuombea sana mwanangu na wale waliompa sumu mwaka huu usiishe kabla Mungu hajafanya kitu kwao, naumia sana na hali ya mwanangu na ninatamani huo ugonjwa uwarudie wenyewe”

Baba Dimpoz-Natamani Kwenda Kumuona Mwanangu Sauzi

Baba mzazi wa Msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz, Faraji Nyembo amefunguka na kudai anatamani sana kuenda nchini Africa ya kusini  kwenda kumuona mtoto wake.

Ommy Dimpoz amekuwa nchini Afrika ya Kusini kwa Miezi kadhaa kwa ajili ya matibabu anayopata baada ya kufanyiwa opersheni Miezi michache iliyopita.

Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Baba Dimpoz amesema anatamani sana kwenda kumuona mwanaye Afrika Kusini alipo kwa matibabu lakini anashindwa kutokana na kwamba hana nauli ya kufika huko.

Namuombea mwanangu usiku na mchana ili Mungu amponye arudi kwenye muziki kama kawaida na kwa uwezo wake atapona, pia natamani sana kwenda kumuona lakini sina uwezo na naamini angeshangaa na angefurahi sana kuniona.

Ommy Dimpoz na Baba yake hawana uhusiano mzuri kwani siku za nyuma Mzee Nyembo ambaye anaendesha bajaji aliwahi kumtuhumu Dimpoz kwa kumtelekeza Kwenye maisha magumu na yeye Kula bata nje ya nchi.

Daktari Aeleza Ugonjwa wa Ommy, Asema Uliwahi Kuwapata Watu Maarufu kama Maria Carey

Daktari wa maagonjwa ya koo, pua na masikio kutoka katika chuo kikuu cha muhimbili dokta godlove mfuko ameelezea matatizo yanayomkabili msanii wa muziki wa bongo fleva  ommy dimpoz kwa sasa na kusababisha afya yake kudhoofika sana.

Ommy dimpoz ambae mpaka sasa yupo nchini afrika ya kusini akiptaiwa matibabu ya ugonjwa wa koo ulisababisha kushindwa kumeza chakula na vimiminika hivyo kufanyiwa upasuaji inaripotiwa kuwa hali yake inadhidi kuimarika siku hadi siku.

Hata hivyo dakatari huyoa anaeleza kuwa ugonjwa huo umekuwa ukiwapata baadhi ya wasanii ikiwemo watu maarufi kama Marai Carey, Lauryn hills miaka ya hapo nyuma na kushindwa kuendelea na kazi zao za muziki kwa kipindi kirefu.

Daktari huyo anasema ugonjwa huo kitaalamu unaitwa dysphagia,  unaosababisha kupata maumivu sana kwenye koo wakati wa kula na kunywa  anasema ” matatizo yanayoweza kumpata mtu katika kushindwa kumeza chakula au vimiminika yapo mengi ikiwepo matatizo ya  kuziba kwa mfumo wa kupitisha chakula,uvimbe au saratani.”

“mwanzoni tunaangalia aina gani ya uvimbe kwa kipimo cha endoscopy lakini kama tutashindwa kuona vizuri basi tunapima kwa CT Scan , ambayo inaweza kutuonyesha vizuri uvimbe umeenda mpaka wapi.”

Kinyama kidogo utolewa katika koo na kupimwa kama ni saratani basi unatolewa kwa kufanyiwa upasuaji lakini kama ni uvimbe mdogo kweny umio tunaweza kukata  ili aendelee kumeza chakula vizuri.

Hata hivyo dakatai mfuko alipoulizwa kuhusu takwimu ya ugonjwa huo alisema kuwa tangu amekuwa mtaalamu wa magonjwa hayo hajawahi kupata mgonjwa mwenye tatizo hilo chini ya miaka 50, hivyo wengi wao sio watoto na vijana.

Ommy Dimpoz Afunguka Jinsi Ugonjwa Wake Ulivyomuunganisha na Diamond

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kueleza jinsi ugonjwa wake ulivyomrudisha na watu ambao aligombana nao.

Ommy Dimpoz amedai pamoja na kuumwa na Kupitia kipindi kigumu lakini anaamini ugonjwa wake umekuwa kama ibada kwani amejikuta akipata maombi ya watu wengi.

Sio siri kuwa Ommy Dimpoz na msanii mwenzake Diamond Platnumz walikuwa maadui kwa muda mrefu lakini siku chache zilizopita tulishuhudia jinsi Diamond alivyoweka tofauti zao pembeni na kumuombea kheri katika maradhi yake.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Ommy Dimpoz amefunguka

Kuumwa kwangu naweza kusema imekuwa kama ibada unaweza ukajikuta hata watu ambao ulikuwa huongei nao wamekutumia meseji ya pole labda kutokana na kuguswa kwaiyo nimefarijika sana sana kwaiyo Nana huku tu Mungu kwa hapa nilipofikia”.

Lakini pia Ommy Dimpoz alifunguka kuhusu salamu za rambi rambi alizotumiwa na Diamond:

Kusema kweli sijawasiliana na Diamond mpaka hivi sasa lakini pamoja na kuwa wote Watanzania sisi pia ni ndugu kwaiyo amefanya jambo jema kunipa pole kwa sababu mimi ni mgonjwa na ndio ubinadamu zaidi”.

Lakini pamoja na kuonekana Diamond kuweka tofauti zake na Ommy na kumtumia salamu za pole Lakini pia aliyekuwa Meneja wake Mobenga ambaye pia hakuwa katika maelewano ameonekana kuweka tofauti zao pembeni na kwenda kumtembelea Ommy hospitali South Africa mara mbili tangu ameanza kuumwa.

Ommy Dimpoz Aweka wazi Chanzo cha Ugonjwa Wake ni Sumu.

kwa muda sasa msanii wa muziki wa bongo fleva amekuwa akiumwa na hata hivi karibuni kulizuka kwa maneno katika mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo amepelekwa chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi zaidi yaani ICU .lakini baada ya kufatilia sana na watu wake wa karibu walikanusha msanii huyo kuwa ICU lakini walisema kuwa bado ni mgonjwa.

Baada ya kusambaa kwa taarifa hizo baadhi ya waandishi wakubwa nchi, Milladr ayo aliamua kumtafuta na kumjulia hali Ommy dimpoz na kutaka kujua hali yake na chanzo cha ugonjwa wake na ndipo alipifunguka na kusema :-

ugonjwa huu kwenye mfumo wangu wa chakula ulianza muda mrefu kidogo,nilikuwa nikiangaika katika hospitali tofauti Tanzania na kila nilipoenda walikuwa wakinipa majibu tofauti pia.wengi waliniambia kuwa koo langu linauvimbe na kwamba hii inasababisha kutoweza kupitisha chakula vizuri, wengine waliniambia nina kansa ya koo.

nakumbuka katika harusi ya alikiba nilikutana na Gavana Joh wa mombasa na akanisaidia kunikutanisha na madaktari nchini kenya, madakatari nchini kenya waliniambia kuwa ugonjwa wangu ulisababishwa na kunywa kitu chenye sumu na wakasema kwa ukubwa wa tatizo nililokuwa nalo inabidi kutibiwa nje ya nchi.

Hata hivyo Ommy anasema kuwa anaendelea vizuri na bado yupo huko kwa matibabu lakini hali yake inazidi kuimarika sio kama siku za nyuma.

Nedy Music Adai Ataoa Wanawake Wanne

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na wimbo wake wa ‘Homa Ya Jiji’ Nedy Music amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kuoa wanawake wanne katika siku za mbeleni.

Lakini pia Nedy amedai kwa yeye kama Muislamu anaruhusiwa kuoa idadi hiyo ya Wanawake Lakini pia amedai anataka kuzaa watoto wengi kadri atakavyoweza hata ishirini.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Nedy Music amefunguka haya:

Mimi Baba yangu alioa wanawake wanne hata kwangu kama nitajaliwa riziki ya kutosha basi nitaoa wanawake wanne panapo majaaliwa na hata watoto nataka kuwa na hata timu inshallah na hata wakifika ishirini mimi ninao uwezo wa kuwaandaa”.

Lakini pia Nedy Music amemkingia kifua Ommy Dimpoz na kumtetea dhidi ya tuhuma kuwa ametafuta kiki kwa kusambaza taarifa kuwa yupo ICU na kusema Ommy hawezi kufanya kitu kama hiko maana sio mtu wa kiki.

Ommy Dimpoz Adai Chanzo Cha Ugonjwa Wake ni Sumu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Yanje’ Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amedai sumu ndio chanzo cha ugonjwa wake.

Miezi michache iliyopita Ommy Dimpoz aliuambia uma wa Watanzania kuwa alikuwa mgonjwa na kufanyiwa upasuaji ambapo chanzo kilikuwa ni ugonjwa Kwenye koo.

Baada ya taarifa za Ommy Dimpoz kuzidiwa ICU kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii siku chache zilizopita hatimaye mwenyewe amefunguka na kuweka wazi kuwa anaendelea vyema.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo huko Johannesburg South Africa ambako anaendelea na matibabu, Ommy ameweka wazi kuwa alienda Kwenye hospitali nchini Kenya na nchini South Africa na kote madaktari walimwambia kuwa aliwekewa sumu.

Ommy Dimpoz amedai alishangazwa sana alipoulizwa kama ameshawahi kunywa sumu kwani hajawahi kufanya hivyo kwa hiari yake Lakini pia amekataa kusema kama inawezekana aliwekewa sumu hiyo bila kujitambua.

Ommy ambaye anaonekana kupungua sana mwili amedai baada ya kuonekana na matatizo Kwenye koo yaliyokuwa yanamzuia Kula wala kunywa alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kutengeneza njia mpya ya kupitisha chakula.

Ommy amesema anaendelea na matibabu nchini humo lakini ameweka wazi kuwa anashukuru Mungu kwani anaendelea vizuri sana kwa sasa tofauti na siku za nyuma.