Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu Afya Yake Kwa Sasa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amevunja ukimya kwa mara ya kwanza na kuongea kuhusu hali yake kiafya kwa sasa.

Siku chache zilizopita taarifa za ugonjwa zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kudai a kuzidiwa gari kulazwa hodi ya wagonjwa mahututi (ICU) taarifa ambazo zilikanwa na uongozi wake wa Rockstar 4000.

Hatimaye amevunja ukimya kuhusu afya na kufunguka kwa kuweka wazi kuwa anaendelea vizuri kwa sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Ommy Dimpoz aliandika:

?? Asanteni sana sana kwa Msg zenu Alhamdulilah naendelea vyema sana Inshallah kwa uwezo wakeboard Allah nitavuka katika kipindi hiki kigumu shukran ❤️❤️❤️❤️ “.

Ommy Dimpoz aliweka wazi hali yake kiafya mapema mwaka huu baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo nchini Afrika ya Kusini.

Rockstar 4000 Wakanusha Taarifa Za Ommy Dimpoz Kuzidiwa

Uongozi wa Msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz Rockstar 4000 umekanusha tetesi za Msanii huyo kuzidiwa.

Siku ya Jumamosi taarifa za Ommy Dimpoz kuumwa mpaka kuzidiwa ICU zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha taharuki juu ya afya ya Msanii huyo.

Kwenye mazungumzo na Mwananchi Communication Limited,  siku Jumamosi Agosti 25, 2018, meneja wa msanii huyo Seven Mosha amesema hali ya msanii huyo kwa sasa inaendelea vizuri na kudai Ommy Dimpoz alifanyiwa upasuaji wa koo miezi minne iliyopita na tangu hapo hali yake imekuwa ikiendelea vizuri hadi sasa.

Juzi alikwenda hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kwa kuwa kila baada ya miezi mitatu anatakiwa kurudi hospitali ili kuangalia maendeleo yake kama tulivyoelekezwa na madaktari.

Dimpoz ni mzima wa afya na hajalazwa, yupo nyumbani baada ya uchunguzi,” amesema na kusisitiza kuwa madaktari kutoka Hospitali ya Milpark iliyopo nchini Afrika Kusini wanamhudumia vyema”.

Baada ya taarifa za Ommy Dimpoz kusambaa siku chache zilizopita wasanii wenzake mbali mbali walijitokeza kumpa pole na kumuombea akiwemo Diamond Platnumz ambaye walikuwa hawana maelewano mazuri hapo nyuma.

BASATA Wafungukia Afya Ya Ommy Dimpoz

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limefunguka kuhusu hali ya kiafya ya Msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz.

Baada ya kuwepo kwa taarifa mbali mbali kuhusu hali ya kiafya ya Msanii huyo huku kukiwa na taarifa mbali mbali za afya yake kuterereka mpaka kuzsidiwa na kulazwa hodi ya wagonjwa mahututi (ICU).

BASATA ambao pia ni walezi wa sanaa hapa nchini wameguswa na hali ya ugonjwa wa Ommy Dimpoz’ ambaye yupo nchini Afrika Kusini akipatiwa matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji wa koo mapema mwezi uliopita.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, BASATA wanefunguka na  wameandika;

Wema Sepetu Athibitisha Kuwa Hali Ya Ommy Dimpoz ni Njema

Msanii wa filamu za Bongo Movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa hali ya Msanii wa Bongo fleva Ommy Dimpoz imeendelea kuwa vizuri tangu taarifa zake za kuzidiwa kuvuma.

Siku ya Jumamosi taarifa za Ommy Dimpoz kuzidiwa na kulazwa ICU zilisambaa kama moto wa kifuu na kusababisha taharuki kubwa miongoni wa mashabiki zake.

Wema ambaye ana Ukaribu mkubwa na Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi baada ya kuwasiliana na Ommy anaamini anaendelea vizuri na hakuna kibaya kitakachotokea:

https://www.instagram.com/p/Bm9N1eJH2vo/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=sov38uq6c8e3

Taarifa za Ommy kupelekwa ICU zilipingwa na uongozi wake wa label ya Rockstar 4000 ambao waliweka wazi kuwa Msanii huyo anaendelea vizuri tu na matibabu.

Seven Mosha Ataja Ugonjwa Unaomsumbua Ommy Dimpoz

Meneja wa msanii wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz, Seven Mosha amefunguka kuhsuu ugonjwa ambao umekuwa ukimsumbua Msanii huyo.

Ommy Dimpoz aliweka wazi ugonjwa wake kwa mara ya kwanza Miezi miwili iliyopita ambapo alitangaza kuwa alifanyiwa operesheni.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Seven Mosha amefunguka na kusema Ommy bado yupo nje ya nchi ambapo anaendelea na matibabu:

Ugonjwa uliokuwa unamsumbua ni koo yaani Esophagus ambayo ilikuwa inampa shida kupitisha chakula halafu baadae hata kupitisha kinywaji chochote kwaiyo ilibidi atengenezewe mfumo mpya”.

Lakini pia Seven amesema hivi sasa Ommy anaendelea vizuri ingawa bado yupo nje ya nchi ambapo anaendelea na matibabu:

Bado yupo nje ya nchi hospitali ambapo anaendelea na check-up kwa sababu ilikuwa ni operesheni kubwa sana lakini tu nashukuru Mungu anaendelea vizuri na bila Shaka mwisho wa wiki hii ataweza kurudi kufanya kazi kama kawaida”.

Seven ameweka wazi pia operesheni aliyofanyiwa haitaathiri uimbaji wake hata kidogo tofauti na maneno ambayo yamekuwa yakisemwa Kwenye vyombo vya habari.

Mubenga Afungukia Hali Ya Ommy Dimpoz

Kama utakuwa ni shabiki wa Ommy Dimpoz basi utakuwa uliwahi kusikia kwenye intro ya nyimbo za zake akitaja jina ‘Mubenga’ basi huyo alikuwa Meneja wake siku za nyuma.

Mubenga amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kwamba hamsimamii Tena Ommy kikazi lakini hana bifu naye ameshampigia kumjulia hali siku nyingi.

Ommy Dimpoz alitangaza siku ya Eid kuwa alikuwa anaumwa sana mpaka kufanyiwa operesheni ya koo na kusema alikuwa hoi kitandani nchini Afrika ya Kusini.

Mubenga alifunguka haya kuhusu afya ya Ommy Dimpoz na uhusiano wao kwa sasa mara baada ya kuacha kufanya kazi pamoja:

Unajua watu wamekuwa wakirushiana Kimitandao sana sio kila kitu lazima tuweke kwenye mitandao.

Nimewasiliana na OMMy na nimempa pole na watu wajue kuwa sisi hatuna ugomvi na hata tatizo lake lilimuanza muda kidogo maana alikuwa hawezi Kula mpaka awe na maji pembeni maana koo lake lilikuwa halipitishi chakula vizuri.

Lakini sasa tunashukuru Mungu tunamuombea apone kabisa na kurejea kazini “.

Ommy Dimpoz hivi sasa yupo chini ya uongozi mpya wa Rockstar 4000 ambao upo chini ya staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba.

Ali Kiba Amtaja Ommy Dimpoz Kama Sababu Ya ‘Mo Faya’ Kutoingia Sokoni

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguk na kuweka wazi sababu iliyosababisha kuchelewa kuingia sokoni kwa kinywaji chake cha Mo Faya.

Ali Kiba alizindua rasmi kinywaji chake Miezi Michache iliuopita kwenye hatusi yake lakini tangu hapo kinywaji hicho hakijaonekana Tena kikiwa kinauzwa sokoni.

Kwenye mahojiano na Shilawadu ya Clouds Tv, Ali Kiba ameweka wazi kuwa sababu pekee iliyofanya mpaka kinywaji hivho kuchelewa kuongia sokoni ni maradhi ya msanii Ommy Dimpoz ambaye amemtaja kama balozi wa kinywaji hicho.

Mo Faya zilitakiwa ziingia mtaani toka Idd lakini tumepata mtihani kidogo, mtihani tulioupata ni kwamba balozi wetu (Ommy Dimpoz) anaumwa sana, nasikitika kusema hivyo kwa sababu hali yake si nzuri lakini kila siku kunakuwa na uhafadhali, ndio ninachosubiriwa.

Hali yake ikiwa sawa wakati tunazitambulisha anatakiwa awepo. Tunahitaji hali yake iwe sawa, tunatamani awepo”.

Ommy Dimpoz yupo nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya kufanyiwa matibabu baada ya kufanyiwa operesheni mwezi uliopita.

Lakini pia Ali Kiba amekana tetesi zilizokuwa zimesambaa kuwa vinywaji hivyo vimepigwa stop na Serikali kutokana na kukosa ubora.

Nedy Music Afungukia Hali Ya Kiafya Ya Ommy Dimpoz

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri katika Tasnia hii ya Bongo fleva amefunguka hali yake ilivyo kwa sasa kutokana na kuumwa kwa Msanii mwenzake Ommy Dimpoz.

Wiki chache zilizopita Ommy Dimpoz alitangaza kwa mara ya kwanza kuwa alikuwa hoi hospitalini akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa operesheni Kwenye shingo.

Ommy Dimpoz aliweka wazi kuwa tangia kipindi kile hali yake ilikuwa imeanza kuimarika kwa kiasi kikubwa.

Nedy Music ni mmoja kati ya wasanii waliopo chini ya label ya Ommy Dimpoz inayoitwa PKP Entertainment na amefunguka hali ilivyo tangu Ommy Dimpoz aanze kuugua.

Kwenye mahojiano na Clouds FM, Nedy Music amekiri kuwa  kipindi hiki ambacho Dimpoz anaumwa kuna vingi anavikosa kutoka kwake.

Kuna vitu vingi ambavyo navimisi kutoka kwa Ommy Dimpoz haswa kipindi hiki anachoumwa. Ni mtu ambaye ananishauri mambo mengi, na mara nyingi huwa tunakaa na kusikiliza kazi zetu”.

Ommy Dimpoz bado yuko nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Baba Diamond na Baba Ommy Dimpoz Warushiana Maneno

Baba mzazi wa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz,  Mzee Faraji Nyembo amemtolea povu Baba wa staa Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma kutokana na tabia yake ya kumsema mwanaye vibaya.

Gazeti la Risasi Mchanganyiko  linaripoti kuwa Kwenye mahojiano waliyofanya na Baba Ommy Dimpoz alitoa taarifa ya mtoto wake kuendelea vizuri na kusisitiza hata kama mtoto wake hamsaidii kwa lolote maishani lakini hawezi kumsema vibaya kama Baba Diamond anavyofanyaga kwa mwanaye.

Unajua mimi ni mzazi wa tofauti sana, siwezi kumlalamikia au kumsemea mabaya mwanangu kwenye vyombo vya habari kama anavyofanya baba Diamond, ninachofanya huwa namuombea mwanangu awe na maisha mazuri maana nikimuombea mabaya anaweza kupoteza dira ya maisha yake nitakuwa nimefaidika na nini.

Namshauri baba Diamond awe anamuombea mwanaye mafanikio, aungane naye wawe kitu kimoja, afurahie mafanikio yake ipo siku Mungu atamrudisha kwake amsaidie na siyo kumzungumzia maneno ya kumlaani na kumlalamikia kila siku.

Aige mfano wangu maana mimi huwa simlazimishi mtoto anisaidie bali huwa napambana na hali yangu kwa kufanya kazi kwa bidii na ninampenda sana mwanangu Dimpoz na siwezi kumlaani au kumlaumu maana jina nililompa la Omary ni la baba yangu inakuwaje sasa nimlaani ni sawa na kumlaani baba yangu”.

Baada ya povu hilo gazeti hilo lilimsaka Baba Diamond na kumuhoji kuhusu kile alichosema Baba Dimpoz na alimwaga povu hili:

Sitaki shobo, huyo baba Dimpoz simfahamu kama hana la kuongea anyamaze, amzungumzie mwanaye hata kama niliongea kuhusu Diamond si mtoto wangu yeye inamuhusu nini?”.

Kuhusu huyo Diamond sihitaji kuzungumza chochote kuhusu yeye wala watoto wangu maana hawana faida yoyote kwangu kwa sasa”.

 

Ommy Afunguka Nyimbo Anazozipenda WCB.

Msanii wa muziki kutoka rockstar nation anaefanya kazi na alikiba amefunguka na kusema kuwa kuna nyimbo anazipenda sana kutoka katika lebel ya wcb ambayo bosi wao ni Diamond Platinumz.Ommy anasema kuwa  wasanii anaowakubali ni pamoja na harmonize na rayvanny na nyimbo zao mpya za sasa hivi.

moja ya nyimbo ninazozipenda ni pamoja na hiyo ya kwangaru ya harmonize inayofanya vizuri, kuna mwingine niesikia wa rayvanny wa pochi nene , kwaio kwa currently nyimbo ninazowz kusema ninazikubali ni hizo mbili.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu ugomvi alionao na Diamond , Ommy alisema kuwa kila kitu kina muda wake hivyo muda wa kumaliza bifu ukifika tu tutamaliza tu”kila jambo lina wakati wake  muda ukifika litakaa sawa.”

 

Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu Bifu Lake na Diamond

Staa wa muziki anayefanya vizuri kwa hivi sasa na kibao chake cha ‘Yanje’ Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu bifu lake na msanii mwenzake Diamond Platnumz.

Ommy Dimpoz na Diamond walikuwa marafiki kwa muda mrefu na hata kutoa pamoja nyimbo kali kama Prokoto na nyinginezo.

Lakini wasanii hao waliingia katika bifu zito miaka michache iliyopita hadi kupelekea wawili hao kupelekana polisi baada ya Ommy Dimpoz kumuongelea mama Diamond Mtandaoni.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Citizen Radio hivi karibuni Kwenye Media your nchini Kenya Ommy Dimpoz alipoulizwa kama bifu lake na Diamond litaishia alifunguka:

Kila jambo lina wakati wake kwa hiyo time itakapofika mambo yote yatakaa sawa, tuombe Mungu”.

Lakini pia Kutokana na mgawanyiko uliopo kati ya WCB na Team Kiba, Ommy Dimpoz aliulizwa endapo kuna nyimbo zozote anazozipenda kutoka kwa WCB:

Moja wapo ni hiyo kama unavyosema Kwa Ngwaru ni wimbo ambao unafanya vizuri, yeah!, kuna mwingine nimesikia wa Rayvanny Pochi Nene, kwa hiyo kwa currently ni nyimbo ambazo naweza kusema zinafanya vizuri“.

 

Ommy Dimpoz- Sijawahi Ku-date na Wema ile Ilikuwa ni Kiki Tu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Omari Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi hata siku moja kutoka kimapenzi na Wema Sepetu.

Kipindi cha nyuma ilishawahi kusemekana Kuwa Ommy Dimpoz na Wema Sepetu walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi hasa baada ya picha zao kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Tetesi za Ommy dimpoz na Wema kuwa kwenye mahusiano zilizidi pale ambapo alionekana na Wema Kwenye chumba wakiwa wamelala ambapo baadae ilikuwa kujulikana walikuwa location kwa ajili ya kushoot wimbo wa Wanjera ambao Wema alikuwa ni video queen.

Lakini Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Ommy Dimpoz amethibitisha kuwa zile zilikuwa ni kiki tu kwa ajili ya project zao.

No, Sijawahi ku-date na msichana yeyote maarufu hapa Bongo, sijawahi.“

Lakini pia Ommy Dimpoz amesisitiza kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na msichana yoyote ambaye ni staa kwa Bongo.

Hivi sasa Ommy Dimpoz anafanya vizuri sana na wimbo wake wa Yanje aliomshirikisha Msanii Seyi Shay kutoka Nigeria, wimbo inaoshikilia nafasi ya kwanza Kwenye mtandao wa Youtube.

 

Nedy Music Adaiwa Kumtosa Ommy Dimpoz

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nedy music amefungukia tuhuma na maneno yanayondelea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amemtosa Staa wa Bongo fleva Ommy Dimpoz.

Nedy Music alianza sanaa yake ya muziki akiwa kama msanii anayejitegemea kutokana na kipaji chake alichukuliwa na Ommy Dimpoz na kusainiwa chini ya label ya Pozi kwa Pozi (PKP).

Lakini baadae Ommy Dimpoz na yeye alienda akasainiwa chini ya label ya Alikiba Rock star 4000 na tangia hapo kukawa na tetesi kuwa Nedy Music amejitoa PKP.

Lakini pia tetesi hizo zilizidi kushika kasi Siku mbili hizi baada ya Nedy Music kutoa wimbo wake mpya aliomshirikisha Ruby na kwenye video hiyo hapakuonekana logo ya PKP hivyo kusemekana amejitoa PKP.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews Nedy Music amefunguka na kukataa tuhuma hizo na kuweka wazi kuwa bado yuko PKP:

Mimi najibu kuwa nipo PKP bado sijatoka na CEO ni Ommy dimpoz na PKP bado tupo kama kawaida.

Naomba Mashabiki waendelee kusapoti kazi zangu maana nafanya kwa ajili yao kwaiyo wasiniangushe wanipe tu sapoti ya kutosha”.

Ommy Dimpoz Amfungukia Amber Lulu Baada Ya Kumwambia Hana Mvuto

Mwanamuziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amemjibu msanii mwenzake Amber Lulu ambaye wiki iliyopita alisema Ommy hana muonekano wa kiume.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Jonijoo wiki iliyopita Amber aliulizwa kati ya Jux na Ommy Dimpoz ni mwanaume yupi ambaye anaweza akawa naye kimapenzi na moja kwa moja Amber Lulu alisema Jux kwa sababu Ommy hana muonekano wa kiume

Jux sawa, Dimpoz hajakaa kama mwanaume, Ommy Dimpoz hawezi kukaa au kushindana na Jux ni zero, hana mvuto wowote , hamna chochote kinachonivutia kutoka kwake”.

Baada ya video clip hiyo kutrend sana ambayo ilikuwa inamuonyesha Amber akiongea hayo Ommy Dimpoz alijibu tuhuma hizo za Amber Lulu kuwa hana mvuto na hana muonekano wa kiume ambapo ameweka nyeusi kwa kusema hataki kumuongelea mtu huyo (Amber Lulu).

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka maneno haya:

Mimi sijui chochote na sijui hizo stori zimetoka wapi na zimeanzia wapi lakini kikubwa sisi kama wasanii unajua kila siku vitu ambavyo vinatuzunguka ni mambo ya mitandao, kwa hiyo in short no comment”.

 

Ommy Dimpoz Afunguka Kuhusu Safari Zake za Nje Ya Nchi

Mwanamuziki wa Bongo fleva Omary Nyimbo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuongelea undani wake wa kupenda kusafiri nje ya nchi.

Moja kati ya mastaa wa Bongo  ambao wanaonekana kula bata sana nje ya nchi basi mmoja wapo ni Ommy Dimpoz kwani kila uchao utamuona nchi za nje akiwa anakula bata.

Miezi michache iliyopita tu Ommy Dimpoz alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa nchini Uingereza alipoenda kwa ajili ya kuangalia mechi ya Manchester United Lakini pia ndani ya miezi michache tu ameonekana akiwa katika nchi kama vile Marekani, South Africa, Italy na kwingineko.

Lakini Ommy amefunguka na kusema kuwa watu wanavyomuona anasafiri sio kwamba anakula bata tu bali anakuwa anasafiri kikazi.

Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Bongo 5, Ommy Dimpoz amesisitiza anaenda nje ya nchi Kwa ajili ya Kushoot video za nyimbo zake ambazo anatarajia kutoa:

Safari zangu nyingine za nje watu wasifikirie naenda kufanya starehe, ni moja ya kazi kwa hiyo nimerekodi, nika-shoot video kama nne natakiwa ni-shoot nyingine Mwanza next week”.

Lakini pia Ommy Ameongeza kuwa kuanzia October mwaka jana alikuwa anarekodi nyimbo kwa ajili ya albamu yake ambapo amerekodi na producer wa hapa Bongo na wengine ndio amekuwa akiwafuata nje ya nchini.

Baba Mzazi Wa Ommy Dimpoz Amtaka Mwanaye Asimzike Akifa

Baba mzazi wa Mwanamuziki wa Bongo fleva Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ anayejulikana kama Mzee Faraji Nyembo ametoa dukuduku lake la moyoni na kusema hata akifa leo mwanaye huyo asimzike.

Kwa taarifa iliyotolewa na gazeti la Risasi Mchanganyiko zimedai kuwa mzee huyo alifikia hatua ya kuongea maneno huku akidai kuwa mwanaye huyo hajawahi kumjali kwa lolote kabla na hata baada ya kuwa staa.

Ommy Dimpoz ni moja kati ya wasanii wa Bongo wanaojulikana kwa kula bata refu ndani na nje ya nchi ni wiki iliyopita tu Ommy alikuwa anarusha picha mtandaoni akiwa nchini Uingereza huku akihudhuria mechi ya Man United Vs Tottenham iliyofanyika katika uwanja wa Wembley stadium.

 

Kwa taarifa iliyotolewa na gazeti hilo imedai kuwa Baba mzazi wa Ommy Dimpoz anaishi mkoani Tabora katika lindi la umaskini huku maisha yake yakitegemea kuendesha bajaji:

Hivi mna habari kuwa baba mzazi wa Ommy Dimpoz ana maisha magumu sana huku Tabora? Kwa taarifa yenu huyu mzee anaishi kwa kubangaiza Kwenye bajaji tofauti kabisa na jina alilonalo mwanaye ambaye ana uwezo kabisa wa kumsaidia baba yake akaishi maisha mazuri”.

Baba mzazi wa Ommy Dimpoz akipata mihogo kwa Mama ntilie

Baada ya taarifa hizo gazeti hilo lilifanya jitihada za kumsaka Baba Ommy na kuongea naye ambaye alifunguka mazito juu ya mtoto wake huyo;

Hakuna kitu kikubwa duniani kama kuletwa duniani…Hayo mengine ya kuwa alilelewa na upande tu wa mama ni madogo tu hivyo sina kosa kwa sababu nilishamleta duniani na ninamshukuru Mungu kwa kunipa nguvu ya kufanya kazi kwani nina bajaji niliyonunua mwenyewe nina miaka 64 lakini bado napambana”.

Lakini pia Baba Ommy aliendelea kufunguka na  kusema:

Kwa mfano nikifa leo ni bora huyu Ommy asinizike au kuja Tabora maana kwanza watu watampiga na kwanza atasema ni nani wake amefariki maana  hivi niko hai hana ushirikiano”.

Baada ya maongezi hayo gazeti hilo lilimtafuta Ommy kwa njia ya simu ambapo simu iliita bila ya kupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya WhatsApp alijibu “Nipo Hospitalini”.