Lulu Diva Ajitabira Ndoa na Mtoto 2019

Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye mwaka huu alifanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Diva amefunguka na kusema mwakani ana ndoto ya kuzaa na kuolewa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Lulu Diva amefunguka kuwa kwa kazi yake ya muziki anayoifanya hivi sasa,  kufanya kitu ambacho huko mbeleni hakitampa kikwazo kama kupata mtoto mapema ili akiwa anaendelea kumtafutia maisha, yeye anaendelea kukua.

Ni vizuri sana kujipangia malengo ya kimaisha na mimi ndiyo hivyo nimeshapanga ninachokitaka mwakani kwa sababu maisha yenyewe ni mafupi. 2019 nikifanikiwa kupata ndoa ni heri, lakini hata kama nitapata mtoto nitashukuru pia”.

Mwaka huu ulianza kwa tetesi za Lulu Diva kuolewa lakini taarifa hizo ziliyeyuka Baada ya Lulu Diva kuachwa na mchumba Wake Baada ya kuenea kwa tetesi za mahusiano na Rich Mavoko.

Rich Mavoko Afungukia Mahusiano Yake na Lulu Diva na Mipango Ya Ndoa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Richard Martin maarufu kwa Jina la usanii kama ‘Rich Mavoko’ amefunguka na kuweka wazi kuhusiana na tetesi za Mahusiano Yake na Lulu Diva.

Kunekuwa na tetesi za muda mrefu kuwa Rich Mavoko na Msanii mwenzake Lulu Diva wapo Kwenye Mahusiano ingawa wamekuwa wakikataa mara kwa mara lakini bado tetesi hizo zimekuwa zikiwaandama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Rich Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa hana uhusiano na Lulu Diva zaidi ya kikazi na kirafiki:

Hivi unajua sijawahi kusema au kukiri sehemu nina uhusiano na Lulu Diva! Nafikiri hayo ni mambo ya kazi na yameshapita”.

Lakini pia Mavoko amefungukia mipango ya kufunga ndoa hapo baadae na tofauti na wasanii wengi yeye anaamini kufunga ndoa hakuwezi kuharibu Taratibu za mtu kimuziki:

Sijaoa bado ila nina watoto wawili, lakini kuoa ni jambo la kheri sana wanaosema wakioa watashuka kimuziki kwa hiyo wataoa lini sasa, uzeeni? Kwangu mimi muda ukifika nitafanya hivyo“.

 

 

Lulu Diva- Kolabo na Rich Mavoko Imebadilisha Maisha Yangu

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Ona’ Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa wimbo wa Ona umempa mafanikio makubwa.

Lulu Diva aliachia Kolabo hiyo miezi miwili iliyopita aliyomshirikisha msanii anayesemekana kuwa mpenzi wake Rich Mavoko na amepata mafanikio makubwa baada ya utumbo hiyo kufanya vyema.

Kwenye Interview aliyofanya na Global Publishers, Lulu Diva alieleza kwamba nyimbo zake za nyuma zilikuwa ni nzuri na zilifanya vizuri lakini baada ya Wimbo wa Ona, umemfanya atambulike kwenye gemu la Bongo Fleva kama msanii mkubwa na kumpatia shoo za kila mara.

Wimbo wa Ona umenipeleka kwenye levo nyingine kabisa kiukweli. Kwa sasa na mimi ni miongoni mwa wasanii wakubwa, shoo zimeongezeka na hata hadhi pia”.

Kutokana na kufanya vizuri na  wimbo huo Lulu Diva ameonekana kwenye shoo mbali mbali akitumbuiza kama vile In Love and Money Tour ya Vanessa Mdee na Jux hivi karibuni.

Lulu Diva Kuchezea Kipigo Kizito Kisa Rich Mavoko

Msanii wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Fiva anayefanya vizuri na kibao chake cha Ona alichomshirikisha Rich Mavoko amedaiwa yuko mbioni kuchezea kipigo kizito.

Global Publishers wanaripoti kuwa Muigizaji wa kitambo kidogo kwenye filamu ambaye hivi sasa ni mtangazaji wa Redio Times, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ambaye ni dada wa Rich Mavoko amehaidi kumpa kichapo Lulu Diva kama ataendelea kutembea na kaka yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Amani, Dokii alisema hajawahi kumpenda mwanamuziki huyo hata kidogo na wala hafikirii kama anaweza kuwa mke bora (Wife Material) kwa kaka yake.

Acha watu waseme mimi mkorofi. Mimi ninayemjua ni wifi yangu ambaye amezaa na Mavoko na si vinginevyo, kiukweli ataniona mimi mtata kwa sababu simuelewi hata kidogo Lulu Diva.

Safari hii nikimkuta kwa kaka yangu Mavoko siwezi kumuacha lazima achezee kichapo changu kama alivyofanya mama Diamond kwa Mobeto maana kiukweli simpendi kabisa Lulu Diva”.

Baada ya povu hilo kwa Dada mtu Gazeti hilo lilimsaka Lulu Diva lilipompa ujumbe huo alimwaga povu hili:

Siwezi kumzungumzia Dokii. Kama yeye kinamuuma basi amkataze Mavoko, kwani mimi nina kosa gani? Mwambie aongee na kaka yake.

Lulu Diva alipoulizwa kama anatumia ndumba kumtengeneza Mavoko hadi kumsahau msichana aliyezaa naye, alisema si kweli kwani mwanamke anayejiamini hawezi kutumia ushirikina katika kumdhibiti mwanaume.

Mimi ni mwanamke ninayejiamini na katika maisha yangu yote sijawahi kutumia kabisa hayo mambo (ya kishirikina), sioni umuhimu wake, mtu akinipenda mimi basi ujue kanipenda jinsi nilivyo na mambo yangu“.

Povu hili la Lulu Diva limekuja baada ya kukataa kata kata kuwa hana Mahusiano ya kimapenzi na RIch mavoko siku chache tu zilizopita.

Rich Mavoko: Mimi na Lulu Diva ni Washkaji Tu

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Rich mavoko ameibuka na kudai kuwa yeye na msanii mwenzake Lulu Diva ni washkaji tu.

Siku chache zilizopita Mavoko na Lulu Diva waliamsha Tetesi za kuwa Kwenye Mahusiano baada ya video iliyowaonyesha wakibusiana kuenea Mtandaoni na baadae Mavoko kumposti Lulu Diva na kumpa maneno matamu.

Lakini baadae ilikuja kujulikana kuwa yalikuwa ni maneno yanayopatikana Kwenye wimbo wao mpya unaojulikana kama Ona ambao kwa hivi sasa inafanya sana pia Kwenye Sehemu mbali mbali.

Siku ya jana Mavoko alihudhuria hafla ya Iftari iliyoandaliwa na Wasafi Tv na alipoulizwa na Dizzim Online kuhusu Lulu Diva ambaye walikuwa wameongozana alidai hawana mahusiano bali marafiki wazuri tu.

Mimi Lulu Diva ni kama washkaji tu kwaiyo kwa ajili ya urafiki wetu tuliamua kufanya kazi pamoja na ndio ile mnayoiona nyimbo inaitwa Ona, na alivyokuja kwangu alikuja kibiashara na alipitia Kwenye management kila kitu kwaiyo unaweza ukaona kabisa siyo  demu wangu na wala sina mahusiano naye zaidi ya urafiki”.

Kuna tetesi zinazodai kuwa Lulu Diva alimuacha mpenzi wake aliyekuwa amemchumbia na aliyekuwa tayari kumuoa kwa ajili ya penzi la Mavoko.

Lulu DIva na Rich Mavoko Waendelea Kuficha Penzi Lao

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rich Mavoko na msanii mwenzake Lulu Diva wamedaiwa kuendelea kuficha penzi lao.

Kwa muda mrefu imekuwa ikisemekana kuwa Lulu DIva na Rich Mavoko ni wapenzi na hata tetesi hizo zimesapotiwa na picha zao mbali mbali ambazo zimekuwa zikionekana wakiwa pamoja.

Tetesi za wawili hawa kuwa pamoja zilianza tangu mwaka jana baada ya kudaiwa Lulu Diva ametoswa na mpenzi wake na hata mahari yake aliyotolewa kirudishwa baada ya kudaiwa kuchepuka na Mavoko.

Baada ya kutoa wimbo wao unaoitwa Ona unaofanya vizuri kwa hivi sasa wawili hao wamedai kuwa ukaribu wao ulikuwa kwa ajili ya kazi tu lakini hawana mahusiano yoyote zaidi ya urafiki wa kawaida.

Kwenye mahojiano na Mikito Nusunusu, Lulu Diva alisema kwamba, tetesi hizo si za kweli na zilitokana na watu kuunga baadhi ya video na picha na kuonesha kwamba wapo kwenye mahaba lakini si kweli, yupo karibu na jamaa huyo kwa sababu za kikazi.

Mimi na Rich hatujawahi kuwa na uhusiano wowote, ni mtu wangu, tunasaidiana kwenye kazi, maana ndiye kanitungia hata wimbo wangu mpya wa Ona, kuhusu mapenzi hapana kiukweli”.

 

Rich Mavoko Ashindwa Kujizuia Aanika Penzi Lake na Lulu Diva Hadharani

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka WCB, Rich Mavoko ameshindwa kuzuia hisia zake na kuanika hadharani penzi lake kwa msanii mwenzake Lulu Diva.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Rich Mavoko anafaidi penzi la Mrembo Lulu Diva ingawa wenyewe wamekataa tetesi hizo mara kwa mara huku wakidai sio wapenzi.

Siku za nyuma Lulu Diva alitakiwa Kuolewa na mwanaume ambaye alikuwa ameshamtolea mahari lakini mahari Ile iliishia kurudishwa huku ikidaiwa sababu kubwa ni Rich Mavoko.

Kama waswahili wanavyosema mapenzi kikohozi basi ndio mahaba yamemzidi Rich Mavoko kwani siku moja baada ya video yao wakibusiana kusambaa Mtandaoni Rich Mavoko kakiri mapenzi yake kwa Lulu Diva.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rich Mavoko kaandika ujumbe mzito wa kimahaba kwa mpenzi wake Lulu Diva:

Sioni maneno ya watu kwangu kama Choo. Mtoto kama chumvi nilipokuonja nikaomba poo”.

 

 

Baada ya Mavoko kufunguka hayo mazito, Lulu Diva aliachia makopa kibao yakisindikizwa na ujumbe uliosema:

Aaaawwww My Love”.

 

Lulu Diva- Sina Mpango Wa Kuzaa Kwa Sasa

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Huba’ Lulu Diva amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuzaa mtoto kwa hivi sasa labda baada ya miaka mitano.

Kama utakumbuka siku mwezi uliopita wakati Lulu Diva anasheherekea siku yake ya kuzaliwa (birthday) CEO wa WCB Diamond Platnumz alianika wazi uhusiano wake na Rich Mavoko na kumtaka Lulu Diva Azae naye mtoto.

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi za Lulu Diva kuwa na Mahusiano ya kimapenzi na Rich Mavoko ingawa wawili hao wamekuwa wakikataa na hata kuficha lakini wamebambwa pamoja mara kadhaa.

Kwenye mahojiano ambayo Lulu Diva alifanya na Sam Misago Tv, ameweka wazi licha ya kuwa Diamond alimtaka azae mtoto hivi karibuni na yeye akakubali hjamaanisha atazaa siku za hivi karibuni kwani hana mpango wa kuzaa mpaka miaka mitano ipite.

Mbona mimi kila siku ninasemaga siwezi kupata mtoto sahivi labda miaka mitano sita huko na kuendelea sio sasa hivi kabisaaa”.

Lakini pia Lulu Diva aliendelea kukataa kuongelea Mahusiano Yake na Rich mavoko huku akidai hayo ni maisha yake binafsi na asingependa kuyaani

Diamond Aliweka Hadharani Penzi la Mavoko na Lulu Diva

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameliweka hadharani penzi la msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Rich Mavoko na Lulu Diva.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa msanii wa muziki Lulu Diva na Rich Mavoko ni wapenzi ingawa wenyewe wamekataa mara kwa mara kuwa hawana uhusiano wowote.

Lakini Diamond ametoa siri hiyo ya muda mrefu na kulianika penzi hilo Hadharani baada ya kumposti Lulu kwenye ukurasa wake wa Instagram Ikiwa ilikuwa ni birthday ya Lulu  Diva.

Kwenye posti hiyo Diamond aliwataka Rich Mavoko na Lulu Diva waache kujificha na badala yake wakae na wazae mtoto wao:

Pamoja na wawili hao kukataa kuwa walikuwa hawana uhusiano wa kimapenzi lakini mara kwa mara picha zao zilisambaa mitandaoni zilizowaonyesha katika mapozi ya kimahaba.

Baada ya kupewa dongo hilo Lulu Diva alimjibu Diamond kuwa wanataka wajenge kwanza nyumba kabla ya kuanza kuzaa kuwa na familia.

Rich Mavoko Amkana Lulu Diva Hadharani

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka kundi kubwa kabisa la WCB, Rich Mavoko amemkana hadharani msanii mwenzake Lulu Diva anayedaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Rich Mavoko ana uhusiano wa kimapenzi na Lulu Diva ingawa wote wawili wamekuwa wakikataa tuhuma hizo na mara kwa mara Rich Mavoko amekuwa akigoma kuongelea suala hilo.

Wiki chache zilizopita habari zilienea kuwa Lulu Diva ametemwa na mwanaume anayejulikana kama Richard ambaye alikuwa mpenzi wake kwa kile kilichodaiwa kuwa aligundua kuwa Lulu Diva ana mchepuko ambaye ni Rich Mavoko jambo lilipopelekea kuvunjika kwa Mahusiano yao.

Lakini pia ilidaiwa Lulu Diva alinyang’anywa kila kitu alichopewa na mpenzi wake huyo baada ya habari hizi kusambaa kwa kipindi kirefu Rich Mavoko hatimaye amefunguka kwenye interview na Lemutuz Online na kumkana hadharani mchana kweupe Lulu Diva:

Lulu Diva kwangu ni mtu wa kawaida tu kama watu wengine yaani ni rafiki yangu kama marafiki wengine wa kawaida sina uhusiano naye mwingine zaidi ya huo”.

Rich Mavoko pia amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kwani anapika nyimbo zake mpya jokoni kwa hivi sasa na angependa wasikilize muda ukifika.