Nay wa mitego ;-Natamani kumuona Diamond Msibani.

Msanii Nay wa Mitego ambae pia alikuwa moja ya watu waliofika katika msiba wa Ruge amefunguka na kusema kuwa amekuwa akitamani sana kumuona Diamond Platinmz katika msiba wa bwana Ruge mutahaba lakini anashangaa kwanini msanii huyo hatokei.

Akiongea na waandishi wa habari, Nay wa mitego  anasem “Duniani Tunapita tu, leo hatunaye Bosi Ruge , kiukweli natamani sana kumuona Diamond hapa msibani, muda bado lakini tusubiri labda tutamuona”

Diamond amekuwa moja ya wasanii walioshangaza watu wengi hasa kutokana na ukweli kuwa hakuna alieyetegemea kutokumuona msibani ukizingatia kuwa hata yeye alipita mikononi mwa Ruge hata kama wawili hao wanasemwa kuwa na mfarakano hapo nyuma.

 

Dada Wa Daimond aliekuwa Akiishi Nje awasili Dar, Amuombea Msahama Baba yake

Dada wa msanii diamond platinumz kutoka nje ya nchi amewasili nchini tanzania huku lengo kubwa likiwa ni kwa ajili ya kuwakutansiah Diamond na baba yake kwa ajili ya mazungumzo na kuweka mambo sawa.

Haba huyo ambae kwa muda mwingi amekuwa akilalamika kuwa hapatani kabisa na mtoto wake na kwamba mtoto wake hamjali kutokana na hasira ya kumtelekeza mama yake akiwa mdogo  ameamua kuongea na dada yake huyo ili kuja tanzania na kufanya maswala ya usuluhishi.

Hata hivyo mwanadada huyo kutoka marekeni ameomba msamaha mbele ya waandishi wa habari akiwa uwanja wa ndege na kutaka familia ya Diamond kukubali mwitiko wake pale anapotaka kuongea nao ili kufanikisha lililomleta tanzania.

Mc Pilipili Asubiri Diamond Aoe

Mchekeshaji na mc maarufu katika shughuli mbalimbali mc pilipili ambae alweza kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake hivi karibuni amefunguka na kusema kuwa anakaa anasubiri msanii diamond platnumz aoe na ndipo yeye pia ataamua kufunga ndoa.

Ndoa ya Diamond ambayo ilitangazwa kuwa ingefanyika February 14, imeshindwa kufanyika tena kwa sababu mwanamuziki huyo amesogeza mbele bila kusema itakuwa lini.

Mc pilipili amba alitrend sana katika mitandao baada ya kumvsiha mke wake huyo mtarajiwa pete anasema kuwa foleni yake inategemea foleni ya diamond platinumz.

Mc pilipili anasema kuwa amsikia Diamond atafunga ndo pale uwanja wa Taifa hivyo na yeye anasubiri Diamond akishafanya mambo yake basi na yeye atakamilisha ya kwake.

 

Diamond Awaonya Wasanii Watoa Rushwa

Msanii Diamond Platnumz ambae ni bos wa televiesheni ya wasafi ambae pia ni meneja wa ebo ya WCB amefunguka na kuwaonya wasanii ambao wamekuwa wakitoa pesa kwa ajili ya kutaka kupata nafasi za nyimbo zao kupigwa kati atv yake.

Diamond anasema kuwa kwa uande wake alishasema kabisa kuwa kila anaeleta nyimbo yake katika Tv hiyo basi itapigwa lakini kama kuna mtu anakuwa akitaka kutoa pesa ili aweze kupewa muda mwingi wakati kazi yake sio nzuri kuliko wengine basi huyo hana nafasi katika Tv hiyo.

Akiongea katika mkusanyiko mkubwa wa wasanii uliofanyika jana, baada ya mkuu wa mkoa kukutana na wasanii kuzungumzia changamoto za wasanii wa bongo movie , Diamond anasema kuwa tv yake ni bure kabisa na hakuna haja ya kutoa pesa.

 

 

Baba Diamond Aomba Kuhalikwa Harusini

Baba wa msanii Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa kuna tetesi zinazosambaa kuhusu mtoto wake wa kuje Diamond Platinum kufunga ndoa ingawa hajazipata kutoka kwa mhusika lakini anachosikia ni kutoka katika mitandao tu.

Hata hivyo baba huyo anasema kuwa hana kinyongo na swala hili ingawa anatamani sana kuhudhuria katika harusi hiyo lakini hawezi kwa sababu hajaalikwa lakini anaomba sana kualikwa katika harusi hiyo kwa sababu yule ni mtoto wake wa kiume.

Baba huyo na Diamond pamoja nakwamba wamekuwa na uadui lakini yeye hana kinyongo na mtoto wake kila mara amekuwa akiongea na kumtakia mema Diamond ingawa kwa upande wake hataki kabisa kuongelea chochote kuhusu baba yake.

Diamond Ampaka Mafuta Tanasha , Asema Anajua Mapishi

Msanii Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa moja ya kitu anachokilingia sana kwa mwanamke wake huyo mpya ambae anatarajia kumuoa hivi karibuni ni kwamba  mwanamke huo anajua sana kupika na amekuwa akimuweka sawa karibia kwa kila kitu.

Diamond anasema kuwa watu wasishangae sana kunenenpa kwake ni kutoaka na mapishi na vyakula vya mwanadada huyo ambae amekuwa akimpikia kila siku na pia hata style zake za nywele kwa sasa zimekuwa zikitengenezwa na mke wake huyo.

Mapishi shemeji yenu anajua sana, matunzo moyo umetulia sana, nadekezwa , natengenezwa styke za nywele, yeye ndio anasema baby nyoa hivi , baby tengeneza hivi , mwanamke anatakiwa awe kama christian ronaldo anapiga mpita kwa miguu  yote.

Kwa kuongezea swala hilo,  Diamond anaongezea na kusema kuwa amekuwa akimpenda mwanamke huyo kwa sababu hataki makuu na mtu na hapendi kulinga wala mambo ya kishari na kujibizana na watu  au kusema watu vibaya.

 

Shiloleh amuomba Diamond Amuoe Zari

Mwanadada Shiloleh ambae ndoa yake imedumu mpaka sasa tangu walipofunga ndoa na mume wake, amemshauri msanii mwenzake Diamond platinumz kuamua kumuoa zari ambae alikuwa mpenzi wake lakini pia ni mzazi mwenzake wa watoto wawili.

Shiloleh anasema kuwa hakuna mwanamke anaeona anamfaa diamond zaidi ya zari kwa sababu wanawake wengine hawawezi kuendana hata siku moja.

nitafurahi sana kama Diamond ataoa, lakini katika kumbukumbu zake lazima arudi nyuma, akumbuke kumuoa zari kwa sababu hata akioa mwanamke mwingine sijui ni nani atakaemfaa.

Ni zaidi ya mwaka sasa tangu msanii huyo aliachana na mwanamama huyo kutoka Uganda na kila mtu kuendelea na maisha yake huku msanii huyo akiwa anabadilisha idadi ya wanawake kila siku.

 

 

Tatoo Mpya ya Diamond Yachanganya Mashabiki.

Msanii Diamond platinumz amechora tatoo mpya mkononi mwake tatoo ambayo imeacha maneno mengi kwa mashabiki na kuhoji kwanini kujiongezea tatoo wakati tayari anazo nyingi za kujaza mwili.

Tatoo hiyo ambayo ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii siku ya jana , iliacha gumzo zaidi kutokana na muonekano wake na herufi zilizokuwepo katika tatoo hizo ambayo watu wanahisi kuwa ni herufu a mwanzo za majini ya watoto wake.

Tatoo iyo ina herufi N, D,T, N in asemekana kuwa ni majina ya watoto wake watatu Nillan, Dylan , Tifaah na jina lake yeye mwenyewe.

 

 

Wakenya Wamlilia Diamond Kuhusu Wasafi Festival.

Mashabiki wa msanii diamond kutoka kenya, wamefunguka na kumsemam maneno mengi huku wengine wakilalamika na kujuta sana kuhusu show ya wasafi festival iliyofanyika jijini Nairobi huku wakisema kuwa kile walichokitaka na kukitegemea sio kile walichokiona katika show hiyo.

Katika mtandao wa twitter kulichafuka sana baada ya mashabiki ho kulalamika  huku wakisema kama inavyoonyesha .

 

 

Maulid Kitenge Amshauri Diamond Ajipange.

Mtangazaji maarufu wa media moja hapa nchini  Maulid  Kitenge amefunguka na kumshauri  msanii damond platinumz kuacha kub weteka anapokuwa jukwaani na kufanya kama wanavyofanta wasanii wengine na kuacha kufatiliza kuimba kwa nyuma katika CD.

Maulid amemshauri iamond baada ya show yake ya wiki iliyopita , show ambayo ililalamiki wa na baadhi ya mashabiki kuwa badala ya kwenda huko ni bora hata wangelala na sio kile walichokiona ambavho hawakukitegemea kabisa.

Maulid anamwambia Diamond kuwa ‘ Wakenya hawataki kabisa  hayo, wakenya wanataka uimbe na sio kuwiambisha wao playback” 

Hii inakuja baada ya wasaii wengi bongo kshindwa kufanya muziki wa live band wanapokuwa jukwaani wakitengea DJ na CD za kugandamizia.

Alichondika Wakazi Kuhusu Kufungiwa kwa Diamond.

Baada ya kufungiwa na Basata hata kukaidi  amri hiyo na kuamua kufanya vile wanavyotaka wao BASATA  waliwaongezea adhabu msanii Diamond Platinumz pamoja na ravyanny kwa kutokufanya kazi za sanaa kabisa kwa muda usiojulikana .

Wasanii  walizua gumzo sana katika mitandao ya kijamii  hasa kwa sababu wao ni moja ya wasanii wanaochngamsha sana indusrty ya sanaa kwa sasa kutokana na nyimbo zao, lakini pia wamefungiwa muda mabao mashabiki wengi walitegemea kupata burudani kutoka kwao.

Baadhi ya wasanii waliongea kila mtu alisema hisia zake, Moja ya walioongea hivi karibuni ni msanii WAKAZI ambapo yeye anasema kuwa swala la diamond kufungiwa na BASATA itakuwa ni kwa sababu  amekuwa akihitenga sana na wasanii wenzake na hata vikundi mbalimbali vya sana nchini.

WAKAZI anasema kuwa kuna mambo ambayo wasanii waaweza kuyafanya kwa pamoja kuepuka hayo yote lakii kwa sababu yeye tayari anaingiza pesa za kumtosha anaona hata hakuna haja ya kumjuika na wenzake.

anasema “Maybe ungekuwa unakuja kushiriki nasi tungekuwa tumei vunja BASATA na kuanzisha BASATA mpya inayoelewa kuwa the society is different, kuzingatia biashara, etc. Kuwa to mkaidi (Kwa Waziri Shonza, Basata) sio solution. Kwa nguvu uliyonayo ungeweza kusaidia sana ila inaonyesha we uliridhika as long as you were making money. Well “Karma is a B”. Kuna Chama chetu cha TUMA (Tanzania Urban Music Association) hebu kuwa karibu, changia mawazo, onekana kwenye vikao. Utafanya kazi zako huru kabisa kama tutaibadilisha system, ila haitobadilika bila kujihusisha na kuungana na wenzako.”

Dkt.Kikwete Aliniambia Nioe, Umri Umefika :-Diamond

Msanii mkubwa Tanzania na Duniani kwa ujumla amefunguka na kuelezea kwa undani juu ya mkutano wake aliokutana na mheshimiwa Jakaya Kikwete wiki iliyopita mabapo picha nyingi sana zilisambaa katika mitandao ya kijamii zikiwaonyesha akiwa na kiongozi huyo.

Hata hivyo Diamond anasema kuwa kabla ya kwenda kumuona , aliongea nae kwenye simu na kumtaka wakutana ili kumpa pole kutokana na ajali aliyokuwa ameipata akiwa sumbawanga.

nilipokuwa Mwanza , niliambiwa kuwa amekuwa akinitafuta hivyo niliamua kumpiga na kuongea nae, aliniliuza kama kweli nimedondoka na nikamuelezea jinis situation ilivyokuwa na kwa sababu hakutukuwa tumeonana siku nyingi sana nikamwambia kuwa nikirudi dar ntakuja kukuona baba.

nilivyorudi nikaenda kuonana nae na aliniambia mambo mengi lakini alisema nioe muda wa kuoa umefika sasa, kuna clip moja  aliona tulikuwa tunahesabu ela na tanasha akaniambia kuwa sio vizuri kuna watu hawana hata riziki kwaio wakiona wanakuwa wanajisikia vibaya.

Afande Sele Amkingia Kifua Diamond Baada ya Kufungiwa na BASATA.

Msanii Afande Sele amefunguka na kuongelea swala la msanii Diamond Platinumz kufungiwa kufanya show ndani na nje ya nchi kutokana na kosa lake la kuimba wimbo ambao uliwahi kukatazwa na BASATA Tangu hapo awali.

Mwanamuziki huyo ambae kila siku amekuwa aijonyesha kuwa yeye ni team-diamond anasema kuwa kufanya hivyo kwa BASATA ni adhabu kubwa sana kwa wasanii hao walitakiwa kupewa adhabu ya kujifunza na wala sio ya kuwakomoa kabisa.

Katika ukurasa wake , afande sele aliandika ” Haijawahi kutokea….unacheza faulo kwenye ligi ya ndani lkn unapewa adhabu ya kutoshiriki hadi mechi za kimataifa…Basata ni mfano wa mtu aliyesifiwa kwa mbio hadi amepitiliza kwao…lkn wao kama wazazi wametimiza wajibu kwani bakora moja haimuui mtoto bali humnyoosha ktk njia sahihi ingawa ktk hili la sasa Baraza limetumia panga au rungu kumuadhibu mtoto kitu ambacho kiasi fulani kinaleta ukakasi hata kama mtoto ameonyesha ujeuri kiasi gani…ila ukweli utabakia palepale kwamba Basata ni Jiwe na wasanii ni Nazi hivyo busara ni wasanii nao kutimiza wajibu wao kwa kuomba Radhi…huo ndio uungwana…Sabalkheriiiii…”

 

 

 

Diamond Atishia Kuhama Nchi.

Msanii Diamond Platinumz aliwahi kusikika kuwa katika maisha yake ya muziki amekuwa akiona kila mara anatishiwa kufanya uchaguzi wa kazi zake kitu ambacho kimekuwa kikimbana sana kufanya kazi kwa uhuru.

Msanii huyo aliwahi kusikika siku moja katika video ambayo kwa sasa imessmbaa sana katika mitandao ya kjamii kuwa kama wataendelea kumfungia hivi basi atafanya uamuzi wa kuhama nchi na kuhamia nchi ambayo anaona kuwa atakuwa huru zaidi na kufanya show kama anavyotaka.

Ikumbukwe kuwa siku zilizopita , Diamond na msani mwenzake rayvanny wote kutoa lebo ya WCB , walipokea taarifa za kufungiwa kazi za muziki kwa muda usiojulikana kwa sababu ya kuimba wimbo wa mwanza  ambao ulishakatazwa na BASATA.

MAONI YA MASHABIKI : Inaonekana kuwa diamond amekuwa akitumia nafasi yake kubwa aliyonayo katika jamii kuvunja maadili kwa sababu tu anamchango mkubwa katika jamii yake, lakini ukweli utabaki kuwa hakuna aliye nje ya sheria ya tanzania hivyo inampasa kufuata tu sheria.

Ukiachana na kazi zake kukosa maadili, lakini pia ilitokea majibizano na viongozi hata na watu wakubwa huku msanii huyo akionekana kutojali hata hisia za mashabiki zake.

Diamond ni Mtu wa Kigoma, Sifa Kubwa ya wa Kigoma ni Ma**ya :-Mwijaku

Moja ya wadau wa sanaa nchii na pia muigizaji mwijaku amefunguka na kusema kuwa kwa anavyojua yeye na kwa sifa za watu wa Kigoma ni igumu sana kusema kuwa Diamond anaweza kuoa kwa sababu watu wa kigoma ni malaya..

Akiulizwa ni mwanamke gani kati ya wale aliyowahi kuwa nao Diamond mpaka sasa anaweza kuwa mke wake mwijanku anasema kuwa hawezi kusema itakuwa ni kama anamchagulia mke lakini ukweli ni kuwa ni vigumu sana Diamond kuoa.

siwezi kumchagulia mke diamond, lakinikwa ninavyojua mimi dimaond ni mtu wa kigoma na sifa kubwa ya watu wa kigoma ni malaya,piga ua garagaza hii ni sifa yao kubwa kwaio mimi dimaond siwezi kumshangaa, na ninakuapia kuwa hata huyu wa sasa hatoolewa na diamond kwa sababu chjaracter za kuoa hazipo vile.

Mwijaku anasema kwa pamoja na kwamba Diamond ametangaza kumuoa mwanamke huyo mwezi february lakini ukweli ni kuwa haweiz kumuoa mwanamke huyo.

Mume wa Mama Diamond Akubali kuwa Mshenga wa Diamond Nchini Kenya.

Mume wa mwanamama Bi Sandra amefunguka nia yake ya kutaka kumuozesha mtoto wa mke wake ambae ni mtoto wake wa kambo Diamond Platinumz kwa mwanadada Tanasha kutoka nchini Kenya huku akionekana kuji-commit kabisa kuwa yeye atakuwa mshenga,

Katika maongezi yao huko instagram,  uncle huyo anejulikana kwa jina la Rally Jones au Shamte, amesema kuwa haoni shida kwake kwenda mpaka nchin Kenya kwa ajili ya kuoa mwanmke anaependwa na mtoto wake.

Diamond alishatangaza tangu awali kuwa mwaka 201 ndio mwaka wake wa kuoa huku akitaja mpaka tarehe rasmi ya kufungwa kwa ndoa hiyo kuwa itakuwa siku ya valentine.