Esma Afungukia Maisha Baada Ya Kuachwa

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kuongelea maisha yake Baada ya kuachwa na aliyekuwa mume Wake Petit Man.

Esma amefunguka na kusema kuachika kwake kwenye ndoa hakujamfanya akate  tamaa ya kuendelea na maisha mengine ya kawaida.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Esma ambaye ni mama wa watoto wawili alisema kuna wanawawake wengine wakiachwa huwa wanakuwa kama wamepatwa na ugonjwa wa kuwafanya washindwe kufanya chochote maishani wakiwaza tu mapenzi, jambo ambalo halipaswi kufanywa na mwanamke anayejitambua.

Ukweli ni kwamba kuachika kwangu hakujanifanya nishindwe kuendelea na maisha yangu ya kujitafutia riziki. Kwanza nilipoachwa ndiyo maisha yakaninyookea“.

Esma alikuwa amefunga ndoa na Petit kwa miaka kadhaa kabla ya kuachana mapema mwaka jana Baada tetesi kusikika kuwa Petit alikuwa amempa mimba mwanamke mwingine.

Esma Platnumz Amuweka Wazi Mpenzi Wake Mpya (picha)

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amemuanika mpenzi wake  Mpya kwa Mara kwanza kwenye mitandao ya kijamii tangu Atangaze mahusiano mapya.

Miezi michache iliyopita Esma aliachana rasmi na aliyekuwa mume Wake ndoa Petit Man Wakuache Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka kadhaa.

Esma aliweka wazi kuwa sababu ya kuvunja ndoa yao ni pale alipogundua kuwa baba watoto wake huyo amechepuka na mwanamke mwingine na ameishia kumpa mimba.

Esma ametumia social media kumuanika Mpenzi Wake Mpya ambapo ameweka picha zake na kusindika na maneno matamu ya kimahaba akiwa ameandika:

Roho yangu furaha yangu kipenzi changu umeniambukiza ugonjwa wa mapenzi naona Kama dunia nzima tuko wawili tu”.

Ukaribu Wa Petit Man na Lynn Wazua Gumzo Ukumbini

Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva na ambaye pia ni meneja wa wasanii wengi Hamad Manungwa ‘Petit Man’ na mrembo Irene Hillary maarufu kama Lynn wamezua gumzo kutokana na ukaribu wao.

Global Publishers wanaripoti kuwa  wawili hao waluonekana pamoja ndani ya Klabu ya Next Door Arena iliyopo Masaki jijini Dar ambapo mwanamuziki, Faustina Charles ‘Nandy’ alikuwa akisheherekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ samba mba na kuzindua albamu yake iitwayo African Princes.

Wawili hao wakiwa ukumbini hapo walionekana kuwa na kikao kizito na pozi lao kuzua mino ng’ono ndipo walipofuatwa na GPL, ili kujua walicho kuwa wakijadiliana ambapo Petit Man alisema wako kwenye mikakati ya kikazi.

Usione tuko kwenye pozi hili na tunano ng’onezana ni kwamba kuna kitu tunaandaa na Lynn na muda si mrefu tunataka kufanya bonge la sapraiz kwa mashabiki wa burudani hivyo watu wasitufikirie vibaya“.

Ukaribu wao ukimya gumzo kutokana na kwamba Petit alikuwa mume wa Esma Dada yake na Diamond na Lynn alikuwa Mpenzi wa Diamond Platnumz.

Karen Afungukia Mahusiano Ya Petit na Baba Yake Gadner

Msanii wa muziki kutoka THT anayefanya vizuri hivi sasa kwenye tasnia ya Bongo fleva na ngoma yake ya ‘Washa’ amesema Baba yake ambaye ni mtangazaji wa Clouds fm Gadner G Habash Hana tatizo na Petit Man.

Kwa wiki kadhaa kulikuwa na tetesi Kuwa Petit Man Ana mahusiano ya kiampenzi na Karen na hata kusemekana kuwa wamefunga ndoa Baada ya picha zilizowaonyesha wakiwa kwenye video shoot ya wimbo wake kusambaa mtandaoni.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Karen amesema ingawa mitandao mingi ilikuwa ikiandika ndivyo sivyo kuwa yeye ana uhusiano wa kimapenzi na Petit Man, jambo ambalo si kweli Alisema familia yake inajua vizuri ishu hiyo kuwa ukaribu uliokuwepo kati yake na Petit na hata baba yake hakuwa na tatizo naye.

Watu wengi ninaojuana nao na baba anajuana nao vizuri kwa hiyo hata hiyo habari ilivyoanza kuvuma haikuleta shida kwa sababu familia yangu inafahamu kila kitu kuhusu Petit Man”.

 

Esma Platnumz Athibitisha Mahusiano Ya Petit Man na Karen

Dada wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ ameanika mahusiano ya mumewe wa zamani Petit Man na msanii wa Bongo fleva Karen Gadner.

Miezi michache iliyopita Esma na aliyekuwa mume wake na mzazi mwenzake Petit Man walitangaza kuachana baada ya miaka michache ya ndoa lakini muda mfupi baadae tetesi za Petit kuwa Kwenye Mahusiano na Karen zilianza kusambaa.

Lakini Kwenye mahojiano na Global Publishers, Esma amefanya kama kuweka wazi Mahusiano hayo ambapo aliulizwa endapo Mtoto wake na Petit anamkumbuka baba yake ambaye kwa sasa hawaishi pamoja ndipo alipojibu:

Anamkumbuka tena sana tu sasa atafanyaje na baba yake ndio kashanogewa na penzi jipya la mtoto wake Gadner jamani mbona mnajifanya hamjui wakati mnajua kila kitu kwani hamjui mbona hata wanaishi pamoja jamani sio siri tena”.

Lakini pia Esma ameweka wazi kuwa hana mpango wa Kuolewa Tena kwa sasa lakini ametaja vigezi anavyovitaka kwa mwanaume ili Awe naye Kwenye Mahusiano:

Napenda mtu mzima ambaye kashamaliza ujana halafu ‘Gentleman’ nitulie naye utoto utoto hapana kwa sasa maana kinyago ukichonge mwen-yewe mwisho wa siku kinakutisha mwenyewe sitaki mimi nimejifunza”.

Karen Gadner Afungukia Ndoa Yake na Petit Man

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Karen Gadner amefungukia tetesi zilizomzunguka hivi sasa kwa kuwa amefunga ndoa na mdau wa muziki wa Bongo fleva Petit Man.

Tetesi za Petit kuwa na Mahusiano na Karen zilianza kupamba moto Wiki chache zilizopita baada ya kuonekana kama wanavaliana nguo lakini sakata hilo limechukua Sura mpya baada ya Tetesi za ndoa.

Picha zinazoonekana Kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kama wawili hao wamefunga ndoa lakini kuna taarifa kuwa inawezekana ikawa sio ndoa bali ni video ya wimbo mpya wa Karen wanashoot.

Baada ya sintofahamu Hizi mtandao wa Bongo 5, ulimtafuta Karen na kutaka kumuhoji kuhusiana na tetesi hizo za ndoa na Petit.

Picha nilizoweka zinajielezea tayari kwa kile kilichotokea, kwa sasa siwezi kusema kitu kingine nimechoka Jamani”.

Karen alikataa kufunguka kwa undani zaidi kuhusu kilichotokea na kuwataka watu waendelee kisubiri kwani watajionea mwishoni.

Petit Man Afungukia Tetesi Za Kufulia Mpaka Kuweka Bondi Passport

Mdau mkubwa wa muziki wa Bongo fleva Petit Man Wakuache amefunguka na kukana tetesi zinaendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefulia.

Petit Man ambaye ni mume wa Esma Platnumz dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekana taarifa za yeye kufulia mpaka kuweka passport yake ya kusafiria rehani.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Petit amesema taarifa hizo ni za uongo na zinasambazwa na mtu ambaye ni mbaya wake ambaye anapenda tu kumchafua;

Sijawahi kufanya kitu hicho ndio maana hata sikuwahi kukizungumzia kwa sababu hates wako wengi sana, kuna watu wengi wanachuki na maisha yangu lakini sio habari za kweli na sijawahi hata kuitwa na Migration kwaajili ya hiyo ishu”.

Tetesi za Petit Man kufulia zilipamba moto hasa pale alipodaiwa kuweka ndani polisi baada ya kushindwa kulipa deni shilingi milioni 10.

Petit Man Hajahusika Kufuta Video Yangu Youtube- Billnas

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap Billnas ameibuka na kumkingia kifua Petit Man Wakauache na kusema hajahusika katika kufuta video yake Youtube.

Kwa muda mrefu Petit Man alikuwa anasimamia kazi za Billnas mpaka pale alipohiondoa Kwenye Label hiyo mwaka jana mwishoni hivyo kuacha kumsimamia Billnas.

Siku ya juzi Billnas alilalamika kufutwa kwa video yake mpya ya wimbo wake ‘LAbda’ na watu wasio julikana na mara moja tetesi zilianza kutembea na Petit alinyoshewa vidole na kudaiwa kuhusika.

Lakini Kwenye Interview na kituo kimoja cha habari Billnas amemkingia kifua Petit Man na kudai sio yeye Lakini pia amesema sio mara ya kwanza anafanyiwa mchezo huo mchafu:

Sio mara ya kwanza watu kutoa video Yangu Youtube na sielewi kwanini wananifanyia hvyo maana mimi aio mtu wa kupiga views milioni 10, sijajua ni nani anafanya hivyo lakini sio Petit Man kama watu wanavyodai.

Naamini mtu anayenifanyia hivyo anataka kunikwamisha maana hakuna kingine anachofaidi akishanifanyia mimi hivyo”.

 

 

Petit Man Ayatetea Mapishi Ya Mke Wake Esma

Hamad Manungwa maarufu kama Petit Man ameibuka na kumkingia kifua mke wake Asmah Khan ‘Esma Platnumz’ baada ya kutuhumiwa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa hajui kupika.

Siku chache zilizopita Esma aliposti picha ya chakula alichomuandalia mume wake kama futari lakini mambo yaligeuka kwani mashabiki walimjia juu na kumsema hajui kupika.

Lakini Petit ameibuka na kusema wote wanaotokwa na maneno kuwa mke wake hajui kupika hawajui wanachokiongea kwani yeye ndio anajua anapikiwa nini kila siku.

Petit alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo alizidi kufunguka:

Unajua mimi sibishani hata siku moja na watu wa mitandaoni kwa sababu najua wazi sio mke wangu aliyepika ile futari. Akipika yeye chakula kinakuwa cha uhakika, nikila nasikia raha hadi najivunia kumuoa, hao wanaosema Esma hajui kupika, wana lao jambo”.

Baada ya Tuhuma hizo kuzidi Esma aliposti chakula kingine huku akisisitiza kuwa chakula watu walichokiona hakupika yeye.

 

Mirror- Sipo Chini Ya Wema Lakini Nampenda Sana

Staa wa Bongo fleva Mirror aliyetamba na nyimbo zake kali kama Baby na One and Only ametangaza rasmi kurudi kwenye gemu.

Mirror alijizolea umaarufu baada ya kusainiwa chini ya Endless Fame ya mwanadada wa Bongo movie Wema Sepetu.

Baada ya kimya kirefu Mirror ameifungukia Millard ayo Tv na kuweka wazi kuwa alikuwa amepata ajali kubwa ya gari lakini hivi sasa anaendelea vizuri na yupo tayari kurudi kwenye gemu.

Mirror ameweka wazi kuwa kwa hivi sasa amefanikiwa kupata management mpya ambayo ndiyo itakayohusika na kusimamia kazi zake na mara tu mwezi mtukufu utakapoisha basi staa chia Rasmi wimbo wake mpya.

Lakini pia Mirror amekana tetesi zote zilizosambaa kuwa amegombana na Wema Sepetu na Petit Man na kusema hana ugomvi na Wema na anampenda kama Mama yake na hata hivisasa akitaka ushauri kuhusu kazi zake basi anamtafuta Wema na Petit.

Mirror- Sipo Chini Ya Wema Lakini Nampenda Sana

Staa wa Bongo fleva Mirror aliyetamba na nyimbo zake kali kama Baby na One and Only ametangaza rasmi kurudi kwenye gemu.

Mirror alijizolea umaarufu baada ya kusainiwa chini ya Endless Fame ya mwanadada wa Bongo movie Wema Sepetu.

Baada ya kimya kirefu Mirror ameifungukia Millard ayo Tv na kuweka wazi kuwa alikuwa amepata ajali kubwa ya gari lakini hivi sasa anaendelea vizuri na yupo tayari kurudi kwenye gemu.

Mirror ameweka wazi kuwa kwa hivi sasa amefanikiwa kupata management mpya ambayo ndiyo itakayohusika na kusimamia kazi zake na mara tu mwezi mtukufu utakapoisha basi staa chia Rasmi wimbo wake mpya.

Lakini pia Mirror amekana tetesi zote zilizosambaa kuwa amegombana na Wema Sepetu na Petit Man na kusema hana ugomvi na Wema na anampenda kama Mama yake na hata hivisasa akitaka ushauri kuhusu kazi zake basi anamtafuta Wema na Petit.

Billnas: Sijashuka Kwenye Muziki

Mwanamuziki wa Bongo fleva Billnas ambaye ametamba sana na kibao chake cha ‘Sina jambo’ amefunguka na kusema taarifa zinazodai kuwa yeye amefulia sio za kweli kabisa kwani hajatoa nyimbo yeyote tangu alipotoa ‘Sina jambo’.

Baada ya kukaaa kimya kwa muda mrefu  fununu zimeanzq kuzagaa kuwa mziki wa Billnas umeanza kushuka huku wengine wakidai Petit Man Wakuache kuondoka LFMG ndio kumesababisha hayo yote.

Billnas yupo chini ya uongozi unaoitwa LIve Fast LIve good (LGLF) na kwa muda mrefu Petit alikuwa manager wake lakini baada ya mikwaruzano na manager mwingine mwishoni mwa mwaka jana Petit aliondoka kwenye label hiyo na kusababisha Billnas kuwa chini ya uongozi mwingine kitu kilichowaaminisha wengi kuwa ndio Chanzo cha Billnas kushuka kimuziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Billnas amekana tuhuma hizo na kufunguka yafauatayo:

Huwezi kusema nimepanda au nimeshuka kimuziki kwa sababu so far kwa sababu sijatoa ngoma yoyote at least wangesema hayo kama ningekuwa natoa nyimbo zinakataa bado naaamini niko juu na material ambayo niko nayo ni nyingi lakini anayeitwa hayo ni mawazo ya watu wengine siwezi kuwakataza kusema “.

Lakini pia Billnas amesema ukimya aliokuwa nao kwenye kutoa nyimbo ni kawaida yake sio kwa sababu hayuko na Petit Man lakini pia amesema ukimya huo kwenye game unatokana na majukumu mengine aliyokuwa nayo ambapo anajishighulisha na biashara zake nyingine sio muziki tu.

Petit Man: Bill Nas Sipo Naye Tena

Petit Man Wakuache anayejulikana kwa ukaribu na kufanya kazi na mwanadada Wema Sepetu amefunguka kuhusu kuacha kumsimamia mwanamuziki wa Bongo fleva Bill Nas anayefanya vizuri na ngoma yake ya Sina jambo.

Petit Man alikuwa anawasimamia Bill Nas na Country Boy kupitia kampuni yake ya usimamizi/ management company inayoitwa ‘Living Fast Living Good’ (LFLG).

Petit Mama amevunja ukimya na kudai kuwa ameamua kujitoa LFLG na sababu ya kujitoa kwenye kundi hilo ni kuwa amedai anataka kuanzisha kundi/ label yake binafsi licha ya watu kudai kuwa Petit man na Bill Nas walichana kwa uhasama Mkubwa.

Inasemekana kuwa Petit ameondoka LFLG kwa sababu ya ugomvi uliotokea na kutokana na kwamba LFLG kulikuwa na mameneja wawili yeye Petit na Mchafu hivyo alivyoondoka aliosepa na Country boy na Mchafu akabaki na Bill Nas.

Kwenye interview aliyofanya na Enews ya East Africa TV Petit amefunguka haya kuhusu sababu za kutengana na msanii wake Bill Nas:

Mimi nimejiengua LFLG sipo tena LFLG panini sio kwamba nimejitoa kwa matatizo au kwa ubaya na ugomvi hapana ile itabaki kuwa ni familia yangu na mchafu ni braza wangu na pia Bill Nas bado mshikaji wangu kiroho safi kabisa maskani kama kawaida panini sahivi niko na Rooftop ambao nimeingia nao share ambapo nawasimamia baadhi ya wasanii akiwemo Country Boy”.

Lakini pia Petit amekiri kuwa pamoja na kwamba Bill Nas ni msanii mzuri na amefanya naye kazi kwa zaidi ya miaka mine lqkini anaamini ulifika wakati wa kila mtu kwenda upande wake ingawa hawana ugomvi na bado anamsapoti kwenye kazi zake.

 

Tunda Anapenda Sana Kufatilia Maisha Yangu Binafsi: Petit Man

Petit Man Wakuache ambaye ni mume wa dada wa Diamond, Esma Platnumz amefunguka kuhusu skendo iliyomwandama wiki chache zilizopita pale alipomtolea matusi ya nguoni mrembo Tunda.

Petit Man alipata umaarufu kwa mara ya kwanza alipokuwa na ukaribu na mrembo Wema Sepetu. Baada ya kumuoa Esma na kuwa shemeji wa Diamond ndipo pale umaarufu ulipozidi. Lakini muda wote Petit aliweka ukaribu wake zaidi na Wema kuliko na familia ya Esma, lakini hata baada ya kupatana na Wema siku za hivi karibuni Petit ameonekana kuweka ukaribu zaidi na familia ya Diamond.

Tunda ambaye amekuwa na urafiki wa siku nyingi na Petit Man alirushiwa matusi hayo na Petit baada ya kumuita Petit chawa wa Diamond baada ya Petit kusafiri na timu nzima ya Diamond kuelekea Zanzibar kwaajili ya shoo ya Diamond. Kitendo kile cha kuitwa chawa na Tunda kilimuumiza Petit na kumtukana Tunda.

Alipohojiwa na clouds tv Petit alifunguka yafuatayo kuhusiana na Tunda:

Yaani yule msichana Tunda anapenda sana kuingilia vitu vyangu binafsi yaani anachimba vitu vyangu vya ndani sana anapenda kuviingilia na kuviongelea sasa sielewi kwa nini anapenda kunizungumzia wakati mimi simzungumzii hata siku moja kwaiyo kitu kama hicho kinatokea kea binadamu yoyote unaposikia unazungumziwa kitu kibaya kupaniki kitu cha kawaida sana”.

Pia Petit alifunguka kuwa kwa sasa anasimamia wasanii wawili ambao ni Country Boy na Bill Nass ambao wanategemea kutoa kazi zao mpya hivi karibuni.