Zari Atoa Ruhusa ya Hamisa Kuzaa Hata Watoto Kumi.

Mwanamama Zari the Bossy amemwaga povu lake huko katika ukurasa wake wa instagram baaada ya moja ya mashabiki zake kumwambia kuwa pamoja na kwamba yeye anataka kurudiana na Diamond lakii akae akijua kuwa mwanamke mwenzie ambae ni Hamisa kwa sasa ana mimba nyingine.

Kwa kuonyesha kuwa hata yeye hajali kwa hilo, Zari aliandika na kumnibu shabiki huyo kuwa huyo hamisa hata kama anataka kuzaa watoto kumi azae.

Zari kuwa makini maana kuna tetesi huko mtaani kwetu kuwa Hamisa ameshanasa mimba nyingine, Lisemwali lipo kama halipo laja.

Lakini kitu cha  kushangaza zari alijibu tu kwa kifupi na kusema ‘azae tu hata watoto kumi’ 

Wikiendi iliyopita Diamond alioneka akiwa Afrika ya Kusini akiwa na watoto wake aliozaa na zari ,  hii ilithibitisha tetesi kuwa inawezekana wawili hao kwa sasa ni wapenzi.

 

 

Zari Kuanika Maisha Yake Kwenye Jarida la True Love.

Mwanamama Zari the Bossy ataonekana katika jarida la true lovehuku jarida hilo likisadikika kuongelea maisha yake yote ya biashara na mapenzi katika jarida hilo.

Jarida hilo ambalo lina Cover picha  ya mwana dada Zari the bossy , litaanza kuuzwa hivi karibu na kusambazwa kwa  watu mbalimbali  na nchi mbalimbali huku watu wakifaidika kujua maisha yake halisi na familia yake na maisha yake ya mapenzi.

Muonekano wa  Cover la jarida la True love.

 

Ikiwa Mwaka Umepita Tangu Kifo Chake, Zari Bado Anamlilia Ivan

Mwanamama kutoka uganda Zari The Bossy ambae alibahatika kupata watoto wawili na diamond platnumz, wikiendi hii alizua gumzo mitandaoni kutokana na kile alichokiandika kuhusu machungu yake kwa mwanaume wake wa kwanza kabisa ambae wikiendi hii ambapo Ivan anakaribia  kutimiza mwaka mmoja tangu alipofariki mwaka uliopita.

Zari na Ivan walifanikiwa kufunga ndoa na kupata watoto watatu lakini walikuja kuachana na kisha kujiingiza katika mahusiano na Diamond Platinumz, ameonyesha kumlilina ivan kila siku kutokana na maneno yake aliyoyandika siku hiyo.

ni vigumu kuamini kuwa ni takribani mwaka sasa umepita tangu ulipotutoka , naona kama jana,hakuna siku ambayo inapita bila kukuombea  na mama yako.roho yako ziendelee kupumzika kwa amani,hakika siis waja hutoka mbali- Aliandika zari katika ukurasa wake wa instagra,m akiwa ameweka picha ya ivan akiwa amembeba mtoto wao wa kiume kipindi akiwa mdogo.

Ivan alifariki mwaka 2017 may 25 na kwa sasa anakaribia kutimiza mwaka lakini zari anaonekana bado kum-miss na kujali uwepo wake katika kulea familia na kuendesha maisha ya watoto wao.

 

Irene Paul :Tanzania Inahitaji Zari Wake

Msanii wa bongo movie Irene Paul amewataka wasanii kuacha kuwa wanalalamika wanapoona wasanii wakubwa na wajasiriamali kutoka nje wanakuja Tanzania na kuchukua nafasi zao za umaarufu na biashara badalka yake wakae na kufikiria mtu huyo ana nini ambacho ni special ili na wao waweze kujitengeneza.

Irene anasema kuwa kuna haja kubwa sana kwa watanzania kutengeneza Zari wake ili kuweza kufix matatioz na malalamiko yanayokuwa yanatokea katika nafasi za baishara.

Irene Zaul anasema kuwa njia nzuri ni kuangalia nini Zari anafanya na sifa gani makampuni yanataka mpaka kumtumia zari na kisha kutengeza zari wao ili waweze kuziba nafasi inayozibwa kila siku na zari kutoka nje ya nchi.

Haya yanakuja baada ya hivi karibuni Zari kutoka Uganda na kuja Tanzania na kusaini dili la pampers kutoka nchini na kuwaacha wasanii wengi hasa wa kike kulalamika na kusema kuwa kwanini makampuni inachukua wageni na kuacha wazawa.

Idris Amtaka Diamond Kumpigia Magoti Zari

Mjasiriamali na mchekeshaji maarufu nchini Idris Sultani amabe kila linalotokea siku zote huwa aachi kuaa nalo moyoni ni lazima atatafuta namna ya kuliongelea na mara nyingi zaid uongea kwa utani lakini ujikuta akifikisha ujumbe kwa unaemhusu.

Akijitahidi kukumbushia ahadi ya Diamond siku za nyuma aliposema kuwa hatakaa kuona zari anamwacha hata siku moja na kama itatokea mwanamama huyo akataka kumuacha basi ni lazima atatafuta njia ya kumuomba msamaha na hata kama itakuwa ni kwa kupiga magoti kutoka Tanzania mpka Afrika ya Kusini.

Wobongo ni wanafiki sana utasikia ooh idris siku ile ya white party 2015 alimchomea kwa kumwambia zari kuwa embu  muone jamaa yako anavyokumbatia fans wake , mi nakuambaia hata hiyo mimba uliyobeba sio ya kwake  ni ya demu mwingine kakudanganya.

by the way shem ninaanzisha kilimo cha black roses sijui unataka  shares? mond naomba upige yale magoti  uliotuhaidi, unashindwaje kumganda wakati mganda.

Wakati msanii Diamond anapata skendo ya kuzaa na hamisa mobeto kulitokea pia mgogoro kati ya Diamond na mzazi mwenzie huyo, ambapo Diamond aliweza kutangza katika vyombo vya habari kuwa kama Zari atamuacha basi atatembea kwa magoti kutoka hapa mpka anapoishi huko Afrika ya Kusini.

Zari aliamua kutoa tamo la kuachana na mzazi mwenzie baada ya kusema kuwa amechoshwa na tabia ya kusikia skendo za michepuko ya Diamond kila siku hivyo ni lazima afanye vitu kulingana na status yake aliyonayo katika jamii.

Zari The Bossy Atangaza Kuachana na Diamond Rasmi

Mwanamama mjasiriamali na mwenye jina kubwa Tanzania na Uganda pia Zari The Bossy ametangaza rasmi kuachana na mzazi mwenzie  Diamond Platinumz kwa madai kuwa amekuwa akisikia habari na tetesi nyingi zinazomkabili mzazi mwenzie huyo hivyo haoni haja ya kuendelea nae.

Ikiwa jana ni siku ya waapendanao inayosherekewa kila mwaka kwa wale wanaopendana, Zari alimau kuonyesha sikitiko lake la moyo kwa kuonyesha kuwa upande wake yeye hakuna Valentines bali ni maumivu  ya mapenzi yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Maamuazi ya Zari yanakuja baada ya kuwa na habari nyingi mbaya zinazoendelea katika mitandao kuhusu mwanaume aliyekuwa nae katika mahusiano kuwa na mahusiano na wanawake wenmgine wengi tofauti tofauti , na kwa muda mrefu mwanamama huyo hakutaka kuongelea swala hilo hadi pale jana alipoona kuwa ndio muda muafaka wa kutangaza rasmi ingawa kuna wengi waliosema kwa hawezi kuchukua uamuzi huo kwa sababu mara ya kwanza diamond alipotembea na Hamisa Zari  aliweza kumsamehe.

katika ukurasa wake wa instagram , huku akiweka ua jeusi kuashiria hakuna upendo, Zari The Bossy alisema amuamua kufanya hivyo ili kulinda heshima na utu wake kwa jamii inayomzunguka na kumjua kama bossy lady, lakini hataendelea kuwa mama bora kwa watoto wake wanne wa kiume na mmoja wa kike na kuwafundisha heshima siku zote.

Kwa kuongezea Zari anasema kuwa siku zote ataendela kuwa Bossy Lady na kuwahamasisha wengine kufata njia zake za kufanikiwa.Pia katika maisha yake alishakutana na changamoto nyingi lakini ndizo zinzazomfanya hazidi kukomaa.

Katika yote Zari anasema kuwa pamoja na kwamba anaachana na Diamond,haimaanishi kuwa yeye sio baba wa watoto wake bali wanaachana kimahusiano lakini wataendelea kuwa na mahusiano kama wazazi.

Understand that this is very difficult for me to do.There have been some multiple rumors some with evidence floating all around medias  in regards to Diamond cheating’s and I Sadly  have decided  to end my relationship  as my  RESPECT,INTEGRITY,DIGNITY  and WELL BEING  can not be compromised.we are separate as partner and not as  parents.This does not reduce me a self-made as individual and as a caring mother and the bossy lady you have become to know. I will continue to build as mogul, I will inspire the World of women  become boss ladies too. I will teach my four  son to always respect women and teach my daughter what self-respect means.Unlike I have been in entertainment industry for 12 years  and through all my challenges   I come out with victory because  I am a winner  and so are  all of you Zari  supporter.HAPPY VALENTINES

Baada ya Kukosana na Diamond, Zari Apeleka Watoto Kanisani.(video)

Mwanamama aliyebahatika kupata watoto wawili na msanii mkubwa Tanznaia  Diamond Llatinumz ameonekana akiwa kanisani  na watoto wake wawili ambao amezaa na msanii huyo.maswali yamekuwa mengi baada ya video hiyo kuvuja na kuacha maswali mengi kuwa inawezekana ndio ukawa mwisho wa mawasiliano katika ya Zari na Diamond na kuachanishwa kwa watoto wake.

Maswali yamekuwa mengi kwa sababu msanii Diamond ni wa dini tofauti hivyo kama Zari anataa kuwafunza dini watoto hao basi ilipaswa kuwapeleka msikitini kama dini ya baba yao inavyotaka lakini zari ameonekana katika video hiyo akiwa kanisani tena watu wakisifu na kuabudu.

 

Hivi karibuni Zari na Diamond wamekuwa wakitupiana maneno katika mitandao ya kijamii huko zari akionekana kuumizwa zaidi na matendo ya mzazi mwenzie hyo kwa tetesi kuwa diamond amekuwa na uhusiano na mwanamke mwingine tena tofauti na wale wa nyuma mwanamama huyo aliyekuwa nao.

Kajala Na Zari Wasemekana Kuwa Na Siri Nzito

Ikiwa ni kama wiki imeshapita tangu kufanyika kwa harusi ya  Rommy Jons ambae ni Dj  wa msanii maarufu na mkubwa Tanzania Diamond Platinumz  ambae pia ni ndugu yake ambae wamekuwa wakifanya kazi pamoja , siri imevuja kuwa katika watu waliohudhuria akiwemo Kajala na mzazi mwenzie na Diamond anaejulikana kama Zari The Bossy wamekuwa wakikwepana na hilo lilionekana live siku ya harusi.

Wanawake hao ambao kila mmoja amekuwa nguli katika mitandao kwa nafasi yake na warembo wamesemekana kukwepana hasa Kajala ambae aliamua hadi kutoka kabisa katika sherehe hiyo  baada ya kuona kuwa kitendo cha yeye kwenda mbele kingemkutanisha kwa karibu na Zari The Bossy.

Katika harusi hiyo kuna wakati ambapo Mc aliwahitaji baadhi ya watu mbele kwa ajili ya ufunguzi wa champaign  mabapo kati ya watu hao walitajwa ni pamoja na Zari na baadae alimuita kajala ili aweze kujumuika pale mbele kwa ajili ya kufungua shampeni lakini kitu cha ajabu na ambacho si cha kutegemea Kajala aliamka na kupitia mlango wa nyuma na kutokomea kusiko julikana ilhali sherehe ikiwa bado haijaisha na kuwaacha watu wakisubiri kutokea kwake.

Hata hivyo baada ya kajal kutafutwa ili kuweza kuthibitisha hilo alikubali kuwa ni kweli aliamua kuondoka kwa sababu alikuwa hataki kuonana na baadhi ya watu, swali linakuja kwanini alikwenda kwenye harusi ilihali alijua hataki kuonana na baadhi ya watu na akiuja kabisa ni harusi ilipaswa kuhudhuriwa na watu maarufu, lakini pia kwanini iwe katika kipindi cha ufunguzi wa shampeni tena baada ya kuitwa mbele yeye na Zari.

ni kweli nilikwenda kwenye hiyo harusi  na nikaitwa mbele lakini niliamua tu kuondoka zangu kwa sabau sikutaka  kuonana na baadhi ya watu  .-Alifunguka Kajala.

Wawili hao hawajawahi kusikika kuwa wamegombana hata siku moja hivyo kama ni maadui basi kuna kinachoendelea kati yao ambacho hakijawahi kuweka wazi na watu hao wawili  na kuamua kufanya siri kwa maslahi yao binafsi.

Mitandao Ya Kijamii Uganda Yamuumbua Zari

Mama mzazi wa watoto wa Diamond platinumz, Zari the boss ambae pia  anaejulikana kwa utajiri mkubwa Afrika mashariki kutokana na utajiri mkubwa alioachiwa na baba wa watoto wake wa kwanza  Ivan The Don, Zarina Hassan Tlate maarufu kama Zari The Bossy ameumbuliwa na baadhi ya mitandao ya kijamii nchini uganda baada ya kuamua kuweka wazi sehemu asili ambayo alizaliwa mwanamama huyo.

Zari The Bossy ambae amekuwa akipiga picha zenye kuonyesha utajiri wa magari nyumba na vitu vingi vyenye thamani ameripotiwa kuwa ameshindwa kabisa kupaendeleza nyumbani kwao kijijini ambako ndio asili yake.

Zari ambae hivi karibuni alitajwa kama moja ya wanawake matajiri wakubwa nchini Uganda anasemeka kuwa uku Uganda katika kijiji chao kinachojulikana kwa jina la  Jinja hakuna kitu chochote cha maana alichokifanya huku mahali anapoishi yeye na familia yake jijini South Africa ikiwa inaonekana ni ya kitajiri sana.Zari amekuwa akijinadi sana majumba na magari yake yaliyopo Pretoria na Kampala lakini amekuwa akisahau kuwa kuna sehemu aliyozaliwa ambayo pia inatakiwa iendelezwe.

Katika baadhi ya kurasa za mitandao nchi Uganda ziliorodhesha hata mali ambazo mwanamama huyo amekuwa akimiliki na kusema

Zari amekwa akiposti picha akiwa na magari kama Ferrari ,Hummer H2, Lamborgin, na hata Mercedez Benz lakini kitu cha ajabu ni kwamba ukioyeshwa nyumbani kwao huko Jinja lazima utakata kama hapo ndio kwao kwa sababu kwa fedha alizokuwa nazo mwanamama huyo alipaswa kabisa kupatengeneza kwao.Na hata sisi waandishi tunaandika hivyo ili kumkumbusha kuwa ana kwao na mkataaa kwao ni mtumwa wala hatufanyi hivi kwa ubaya wowote ule

Wakielezea historia ya maisha ya mwanamama huyo, mtandao mmoja wa kijamii uliandika kuwa “Mama mzazi wa Zari aliolewa zamani huku Jinja nchi Uganda lakini baadae mama na baba na mama wa Zari walitengena hivyo mama mzazi wa Zari aliamua kuondoka na kuanza kuwalea watoto wake wote nane akiwemo Zari akiwa peke yake, na kuamua kuamia Kampala akiwa na Zari, katika kutafuta Zari alianza kuangaika lakini ikiwa na kutembea na wanaume ili kuweza kujikimu kimaisha ndipo alipokutana na  Ivan The Don na kumjengea mama yake ghorofa iliyopo Munyonyo jijini Kampala.

Ukiachana na utajiri mkubwa alioachiwa na mumewe ambao amezaa nae watoto watutu, Zari pia anajishughulisha na biashara za urembo pamoja na kuanda events za Zari All White Party ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki.