Irene Paul Atoa Ushauri Kwa Mastaa Kuhusu Kujichubua

Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul ameibuka na kuwapa ushauri wasanii Mbali mbali ambao wamekuwa wakijichubua na kuwataka kuepuka gharama hizo kwa kuwa asilia.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Irene alisema amekaa na kujitathimini na kugundua kuwa hatumii gharama kubwa kununua nywele za bei mbaya au kutumia madawa ya usoni, lakini bado anaonekana mrembo.

Ukitaka kuniangalia kuanzia kichwani hadi ngozi yangu situmii gharama hata kidogo, naamini mastaa wengine wakiamua kuwa jinsi walivyo watapendeza na wataepuka gharama ambazo si za muhimu“.

Wasanii wengi wamekuwa waliweka wazi gharama kubwa wanazotumia kuhakikisha wanakuwa warembo ikiwemo krimu za bei mbaya Lakini pia mawigi.

Irene paul apigana location

Mwanadada i=UIrene paul na Mary mawigi wanaripotiwa kupigana walipokuwa location walipouwa wakifanya kazi yao.Wawili hao ambao walikuwa wakifanya kazi ya huba, walisgindwa kuelewana katika baadhi ya mambo na ndipo irene alipoamua kumsukuma mary na Mary kushindwa kuvumilia na kumpiga vibao  na ndipo varangati lilipoanza.

Wawili hao walishindwa kumaliza tofauti zao na kuamua kuondoka sehemu ya kufanyia kazi kwa muda huo.

Hata hivyo baada ya kutafutwa na kuulizwa kuhusu tetesi hizo, wawili hao kila mmoja kwa nafasi yake alishindwa kutoa majibu ya kueleweka huku mary akishangaa ni nani amevujisha ubuyu huo na kusema wao ni wakubwa wanajua jinsi ya kuyatatua.

Kwa upande wa irene paul hakupokea simu ya mwandishi na hata ulipotumwa ujumbe alionekana kuuusoma lakini hakujibu.

Irene Paul- Siwezi Kumlazimisha Mtoto Wangu Kuwa Msanii

Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul ameibuka na kuweka wazi kuwa ingawa yeye ni Msanii na anaipenfa kazi yake Lakini hawezi kumlazimisha Mtoto Wake awe hivyo pia.

Irene Paul amefunguka hayo alipokuwa anamuongelea Mtoto Wake mdogo Wake kike anayeitwa Wendo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Irene aliongelea mipango ya mwanaye na kama endapo atafuata nyayo za mama yake na yeye kuwa msanii.

Unajua mwisho wa siku staa ni mimi, yeye si staa hivyo napenda aishi maisha yake mwenyewe anayoyapenda, ajifunze vitu tofautitofauti, akifika umri mkubwa atachagua la kufanya mwenyewe na staili ya maisha yake mwenyewe kwani wakati huo huenda na mimi nitakuwa si staa tena”.

Hivi sasa Irene Paul anang’ aa kwenye tamthiliya ya Huba ambayo inarushwa na kituo cha DSTv ambapo amecheza Sambamba na wasanii wengine.

Mtoto Wangu Amebadilisha Maisha Yangu- Irene Paul

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Paul amefunguka na kuweka wazi Jinsi Mtoto Wake wa kwanza alivyoweza kubadilisha maisha yake na kumpa Furaha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti pa Ijumaa, Irene Paul amefunguka na kuweka wazi Jinsi binti yake anayeitwa Wendo alivyoweza Kumbadilisha kabisa maisha yake:

Kuna vitu vingi sana, yaani sijui nisemeje lakini kifupi maisha yangu yote yamebadilika kwani kuwa mama ni kitu kingine tofauti na usichana”.

Irene ameweka wazi kutokana na Upendo alionao kwa mwanaye hajawahi muacha na Dada wa kazi kabisa:

Kwanza unavyoniona mimi toka mwanzo sikupenda mwanangu akae nyumbani na dada wa kazi, nilitaka kumuangalia mwanangu hatua kwa hatua, hata mama yangu mwenyewe alinishangaa na ndivyo hivyo nikiwa na kazi zangu anakuwepo mama yangu au ndugu yangu“.

Lakini pia Irene ameweka wazi mipango yake ya kuongeza mtoto mwingine katika siku zijazo.

Ndio, nina mpango huo kwani kama unavyoona nina mmoja tu, Mungu akinibariki mwingine nitashukuru”.

 

Maisha ya Sasa Hayahitaji Mwanamke Mzuri Bali Mwenye Akili :-Irene Paul

Mwanadada kutoka katika kiwanda cha bongo movies Irene Paul amefunguka na kusema kuwa kwa maisha ya sasa jinsi yalivyo  hapahiytajiki kuangalia uzuri wa mwanamke ni upi zaidi ya kujua kama mwanamke ulienae ana akili na anaweza kukusaidia katika  maisha.

kwa kujitolea mfano yeye mwenyewe anasema kuwa , amekuwa mtu wa kuchukia sana kutegemea kila kitu kutoka kwa mwanaume hivyo anapambana kila kukicha ili waweze kuasaidiana kimaisha kwa vitu vidogo vidogo.

akiongea na dizzim online, Irene anasema “tunaenda kisasa zaidi, maisha ya sasa hayataki mwanamke mzuri hata kidogo,  maisha ya sasa yanataka mwanamke mwenye akili, mwanamke anaeweza kutafuta,mimi nikiwa kama mke na kama mama siwezi kumtegemea mme wangu kunileta kila kitu, iswezi kusema kuwa yeye ndio afanye kila kitu, vitu vingine tunasaidiana.”

Irene Paul Afungukia Bifu La Zamaradi na Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Irene Paul amefunguka na kupima uzito bifu lililopo kati ya rafiki yake kipenzi Zamaradi Mketema na Hamisa Mobetto.

Wiki chache zilizopita Zamaradi na Mobetto waliingia Kwenye bifu zito mara baada ya kutokea sintofahamu Kwenye mavazi ambayo Zama aliyavaa kwenye arobaini ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Irene alisema Zamaradi alipoingia kwenye ugomvi na Mobeto hivi karibuni kisa kikiwa mshono wa nguo aliyovaa kwenye arobaini ya mwanaye, yeye aliamua kujiweka pembeni kwa sababu aliogopa kuchukuliwa hatua za kisheria kwani serikali kwa sasa haitaki mchezo.

Si unajua tena siku hizi sheria za mtandao, unaweza kujifanya kimbelembele yakakukuta mazito kwa hiyo niliona nikae pembeni licha ya kwamba Zamaradi ni rafiki yangu sana kwa sababu nilifahamu pia wawili hao wangeweza kumalizana bila tatizo lolote”.

 

Irene Paul , Haogopi Kuzeeka kwa Sababu ya Kuzaa.

Mwanadada kutoka bongo movies Irene Paul amefunguka na kusema kuwa  bado anategemea kuzaa na kuongeza mtoto wa pili na wala hana wasiwasi wa kusema kuwa atazeeka kwa sababu ya kuzaa kwa sababu anaamini kuwa bado ana nguvu ya kuzaa.

Irene anayasema hayo kutokana na ukweli kwamba wanawake wengi hasa katika tasnia yao wamekuwa na tabia ya kuogopa kuzaa  kwa sababu ya kuogopa kupoteza muonekano wao , lakini kwake hilo sio tishio hata kidogo.

sina hofu ya kuendelea kuzaa kwamba labda nitapoteza muonekanao wangu, au  nitapoteza ustaa wangu,Ninachojua ni kwamba watoto wanakufanya akili yako kuchangamkaa , na kila mtu kwa sasa anajivunia kuwa na watoto wake ni tofauti na pale zamani watoto walikuwa wanafichwa.

 

“Wasanii Tupunguze Kiki Tufanye Kazi Zaidi”- Irene Paul

Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul ameibuka na kuwashauri wasanii wenzake kuachana na kiki na kuanza kufanya kazi zao za sanaa kwa nguvu zaidi.

Wasanii wengi wamekuwa na mtindo wa kutengeneza skendo fulani (kiki) ziwe za kimapenzi au bifu lakini skendo zitakaziweza kuwaletea attention fulani kutoka Kwa vyombo vya habari au mitandao ya kijamii ili watakapotoa kazi zao zifanye vizuri.

Irene Paul amewataka wasanii wenzake kuacha kuzidisha sana kiki kama njia ya kutafuta attention kwani inakuwa inaharibu kazi zao kwani jitihada hivyo ya kiki wangeielekeza katika kutengeneza kazi Debye unitary basi mambo yangekuwa mazuri;

Nafikiri tumesha hustle sana Kwenye hii gemu kwa njia tofauti na umri haurudi nyuma bali unasogea so I think it’s about time tufanye kazi zaidi kwani ndio kitu pekee kilichobaki.

Waliojiuza wamejiuza sana na waliokaa uchi wamekaa uchi sana na waliotengeneza skendo wametengeneza skendo za kutosha lakini wamepata nini out of it?.

Lakini pia Irene Paul amewataka Bongo movie wenzake waelekeze nguvu zao Kwenye kufanya kazi zaidi ili kuitudisha Bongo movie Kwenye ramani:

Umefika wakati tufanye kazi Bongo Movie Industry sio ya kipindi kile wakati inaanza kuna mapinduzi makubwa twende na wakati Tanzania tuna vipaji lakini tuna lack Knowledge na ubunifu kwaiyo cha muhimu kufanya kazi kwa bifu bidii ili kufika malengo”.

 

Irene Paul Amkingia Kifua Muna

Msanii wa filamu za Kibongo, Irene Paul ameibuka na kumkingia kifua mwanadada Muna Love na kudai watu lazima waheshimu hisia za watu na kuweka mawazo yao pembeni.

Suala hili  limekuja baada ya sakata lililozuka jana baada ya Muna kufanya maongezi na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa Peter sio Baba wa marehemu Patrick na kumtaja Casto kama Baba Lakini pia aliweka wazi kuwa nyumba anayoishi Peter ni ya kwake na hati zote.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Irene Paul amemtetea Muna na kuwaomba watu wamuache aongee anachotaka kuongea kwani bado yupo kwenye maonbolezo ya mtoto wake.

Mimi nina mawazo kama walivyo watu wengine lakini ningependa tuheshimu hisia za Muna kama mzazi ambaye ni muhusika Mkuu wa mtoto aliyefariki na Kwenye maisha kila mtu ana jinsi ya ku-deal na stress kuna wengine wanapenda kuongelea matatizo yao na wengine wanapenda kunyamaza kwaiyo lazima tuheshimu mawazo ya watu”.

Kikao hiko cha Muna na waandishi wa habari hakikuaa vizuri na baadhi ya watu waliohisi ni mapema sana kuzungumza kwani mwanaye amekufa wiki mbili tu zilizopita na mmoja kati ya watu hao ni msanii Shilole:

Irene Paul “Hakuna Harusi Inayozidi Ndoa Nzuri”

Mwanadada Irene Paul ambae tangu amefunga ndoa na kupata mtoto amekuwa akijitenga sana na skendo katika mitandao ya kijamii huku akijitaidi sana kuwa akitoa ushauri kwa wasichana wengine kutulia na kujitaidi kuficha maisha yao .

Katika ukurasa wake wa instagram, Irene aliandika caption yenye kutoa ushauri kwa watu wanaotaka kufunga ndoa au waliopo katika ndoa kuhusu swala la kuwa wakiamini sana na kufuata maneno ya marafiki bila kujua kuwa siku ndoa yako itakapo haribika hakuna anayeweza kuinganisha zaidi ya wewe na mwanaume wako, Irene aliandika

tamani kupata ndoa nzuri kuliko harusi nzuri,harusi ni yako na wote wanaokujua na wasiokujua pia , wanakuja na kuondoka katika harusi yako , lakini ndoa ni yako pekee yako na mpenzi wako , hakuna harusi inayozidi ndoa nzuri”

Irene Paul Ana Matatizo Yake Binafsi- Rammy Galis

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis ameibuka na kujitetea baada ya sakata lake la kutuhumiwa kuigiza amezimia na msanii mwenzake Irene Paul kwenye msiba wa Agnes Masogange.

Siku ya Jumapili pale Leaders Club ambako Marehemu Agnes Masogange alikuwa anaagwa kuliibuka kizaazaa baada ya Rammy kupoteza fahamu hali iliyopelekea abebwe na kupelekwa kwenye gari kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Lakini baada ya sakata hilo msanii wa Bongo movie Irene Paul alishangaza watu wengi baada ya kuamua kumshambulia Rammy na kumtuhumu kwa kujifanyisha na kupeleka maigizo msibani na kudai alikuwa hajazimia bali alikuwa anatafuta kiki.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Rammy amejitetea kuwa kitu kilichomfanya azimie ilikuwa ni kuchoka baada ya kusimama kwa muda mrefu hivyo kuishiwa nguvu kabisa lakini pia ameweka wazi kuwa Irene Paul ana matatizo naye tangu siku nyingi:

Mimi sina matatizo na Irene kwa sababu kwanza Mungu alinijalia mini kuwa mwanaume na yeye kuwa mwanamke kwaiyo siwezi kubishana na mwanamke lakini huyu ana matatizo yake binafsi kwa sababu hata tukiwa location tumegombana sana na ninaweza kusema alikuwa ana matatizo na marehemu pia kwa sababu aliwahi kuniambia unaishi na mtu unajua nani anamlipia kodi? Kwa kweli iliniuma sana”.

 

Kitambaa cha Mkononi Cha rammy Champotoa Povu Irene Paul

Mwanadada Irene Paul ameonyeshwa kutkupendezwa na picha iliyosambaa sana katika mitandao ya kijamii inayomuonyesha rammy galis ambae  aliwahi kuwa mpenzi wa Agness Masogange  na aliyewahi kucheza nae filamu moja wapo inayoiywa hukumu ambayowalifanya pamoja kipindi wakiwa wapenzi.

Ukiachana na maneno mazito aliyoyaongea rammy alakini pia katika kuaga mwili wa marehemu ,Rammy alionekana kushindwa kuhimili maumivu na kuishiwa nguvu kabusa hivyo kupewa msaada  na watu waliokuwa karibu nae,

Hata hivyo, picha hiyo inamuonyesha mwanaume huyo akiwa amebebwa na watu huku akiwa ameshikilia kitambaa chake mkononi ndipo watu walipoanza kupata maneno ya kongea na kusema kuwa rammy alikuwa anaigiza kuumizwa na msiba huo kwa sababu mtu aliyezimia asingeweza kukuishikilia kitambaa hicho bali angekidondosha.

Katika ukurasa wake irene aliandika”Maskini pamoja na kuzimia lakini aliweza kushika  vitu vyake,wote tumeguswa na  lakini pia tusifanye misiba ya wenzetu kama sehemu ya kujipatia kiki,tuheshimu misiba hiyo kama kweli tunakuwa na nia ya kuwasundikiza mwenzetu kwa upendo , na zaidi tujue kutofautisha kati ya location za filamu na dunia ya kweli,

kuna vitu vinakera na vinachefua sana , i sorru to say umebichefua leo..na bora ungejua jinsia ya kike angalau..ningelala na hili likiwa limenikaba, pumzika kwa amani AGNESS.

                                         

Irene Paul Azidi Kumwagia Sifa Zari

Muigizaji wa Bongo movie Irene Paul amezidi kumiminia sifa Zarinah Hassan ‘Zari’ na kudai mrembo huyo anajua kutengeneza jina lake na pia anajua kufanya biashara.

Irene Paul amewataka wasanii wenzake waache kumuonea wivu Zari kwa Dili alilolipata la Softcare na badala yake wajiulize wanafanya nini ili hata kampuni kubwa ziwaangalie wao wanawake Kwanza.

Lakini pia Irene amedai kuwa Zari ni staa mkubwa sio tu nje ya Bongo bali hata nchini kwetu na kudai hajaona bado hajamfikia kwa uwezo wake wa kuweza kuwa kiwango cha juu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Irene alizidi kumiminia sifa hizo Zari na kusema yafuatayo:

Ni staa mkubwa, anajua kumaintain jina lake, simuoni staa wa kumshinda yeye Bongo”.

Wiki iliyopita Zari alipata dili na kampuni ya Softcare kwa ajili ya kuwa balozi wa bidhaa zao za pampasi kitendo kilichowakera watu wengi baada ya kampuni hiyo kumpa dili hilo Mganda wakati kuna Madura staa wa kibongo kibao wangeweza kuwa mabalozi.

Irene Paul :Tanzania Inahitaji Zari Wake

Msanii wa bongo movie Irene Paul amewataka wasanii kuacha kuwa wanalalamika wanapoona wasanii wakubwa na wajasiriamali kutoka nje wanakuja Tanzania na kuchukua nafasi zao za umaarufu na biashara badalka yake wakae na kufikiria mtu huyo ana nini ambacho ni special ili na wao waweze kujitengeneza.

Irene anasema kuwa kuna haja kubwa sana kwa watanzania kutengeneza Zari wake ili kuweza kufix matatioz na malalamiko yanayokuwa yanatokea katika nafasi za baishara.

Irene Zaul anasema kuwa njia nzuri ni kuangalia nini Zari anafanya na sifa gani makampuni yanataka mpaka kumtumia zari na kisha kutengeza zari wao ili waweze kuziba nafasi inayozibwa kila siku na zari kutoka nje ya nchi.

Haya yanakuja baada ya hivi karibuni Zari kutoka Uganda na kuja Tanzania na kusaini dili la pampers kutoka nchini na kuwaacha wasanii wengi hasa wa kike kulalamika na kusema kuwa kwanini makampuni inachukua wageni na kuacha wazawa.