Babu Tale Aachiwa Huru Rasmi

Mkurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection na Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale ameachiwa huru rasmi baada ya kusota rumande kwa Siku mbili.

Tale alifikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar, juzi Jumatano Mei 23, 2018 kufuatia kesi yake anayodaiwa na Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Tsh. Milioni 250 ambapo kesi hiyo iliahirishwa baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo mahakamani hapo.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Babutale ameachiwa kutoka Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam tangu jana Alhamisi na sasa yupo uraiani japo haijafahamika iwapo yupo nje kwa dhamana au vinginevyo.

Wakili wa Sheikh Mbonde Afunguka, Babu Tale Anaweza Kukaa Mahabusu Kwa Muda Usiojulikna

Wakili wa Sheikh Mbonde amefunguka na kusema kuwa inawezekana kabisa meneja wa Tip Top connection Babu Tale akakaa rumande kwa muda usiojulikana kutokana na kushindwa kufikia kwa muafaka kati  yao hasa baaada ya alitoa amri ya kukamatwa kwake kutokuwepo mahakamani hapo.

Akielezea hali ilivyokuwa, wakili huyo alisema kuwa hata baada ya kukaidi amri ya mahakama kwa muda mrefu,Babu Tale alipofikishwa mahkamani alipewa muda wa kuyazungumza madai hayo na aliyemshitaki lakini walishindwa kuelewana na ndipo hakimu aliposema Babu Tale anapaswa kumsubiri naibu msajili wa mahakama kuu atakaporejea kutoka safari.

Katika kesi hiyo, wakili huyo anahadithia kuwa babu tale na Sheikh Mbonde walikubaliana  kurekosi masomo ya kiislamu na kisha kuauza kwa jamii lakini baadae  Babu Tale alimkatia mawasiliano Sheikh huyo na kumwambia kuwa amhairisha kufany kazi hiyo hivyo atafute mtu mwingine wa kufanya hivyo.

Hata hivyo Sheikh Mbonde alipokwendaDodoma alikutana na video hizo aina ya DVD baadhi ya sehemu zikiwa zinauzwa  ndipo alipomua kufikisha swala hilo mahakamani.

Kesi ya Babu Tale Yahairishwa, Arudishwa Tena Rumande

Mkurugenzi wa kampuni  ya Tip Top Connection Babu Tale mapema leo alifikishwa mahakamani kufatia kesi ya madai dhidi ya Sheikh Hamis Mbonde baada ya Babu Tale kutumia masomo ya Sheikh huyo katika maswala yake ya kibiashara bila kuwa na hati miliki kutoka kwa mwenyew.

Babu tale ambae alikamatwa tangu siku mbili zilizopita amekuwa akifikishwa mahakamani hapo  lakini  hakimu aliyetoa hati ya kukamatwa kwake hayupo hivyo kufanya kesi hiyo kuhairishwa.

Babu tal alipewa hukumu ya kulipa fidia ya shilingi milion 250 lakini hakufuatilia hukumu hiyo kwa muda tangu mwaka 2013 na ndipo  hakimu alipotoa hati ya kukamamtwa kwakwe tangu february mwaka huu lakini mtuhumiwa amekuwa akikosekana kila anapotumia hati ya kufika mahakamani au kukamatwa.

Mameneja Wa Diamond Wadaiwa Kuhusika na Kusambaza Video Ya Ngono Ya Nandy

Kama utakumbuka mwezi uliopita jiji zima lilizizima baada ya video ya ngono iliyomuhusisha msanii wa Bongo fleva Nandy na Billnas kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha skendo kubwa kwa wasanii hao.

Chanzo cha video hiyo hakikujulikana kwa sababu Nandy na Billnas wote walikataa kuhusika na kusambazwa kwa video hiyo lakini aliyeiweka video hiyo Mtandaoni ni kurasa ya Udaku inayojulikana kama UdakuTz.

Sasa tangu wikiendi iliyopita kuna taarifa zilizodai kuwa mmiliki wa kurasa hiyo ya udaku ametekwa na watu wasiojulikana kwani familia yake haijui alipo, mpaka jana ambapo ilidaiwa alichukuliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano juu ya kuvuja wa  video ile ya Nandy na Billnas.

Lakini taarifa iliyotolewa jana na mtangazaji wa Clouds Fm Soudy Brown ni kuwa mmiliki wa kurasa hiyo yupo kituo cha polisi na Kwenye mahojiano hayo amewataja watu waliompa video hiyo avujishe ambao walikuwa ni mameneja wa Diamond ambao mi Salaam SK na Babu Tale.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Soudy Brown aliweka posti hii:

Mpaka sasa haijajulikana kama Watajwa hapo juu  ambao wote ni mameneja wa Diamond wameshatiwa mbaroni au bado.

Lakini pia haijawekwa wazi ni vipi Msanii Diamond anahusika vipi katika hilo lakini yote hii inarudi katika bifu la Diamond na Clouds Media.

Madee Amefungukia Tuhuma za Babu Tale Kuitelekeza Tip Top Baada ya Kuhamia WCB

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Madee Ali amefunguka na kutoa mtazamo wake juu ya taarifa ambazo zimekuwa zikienea kwamba Babu Tale ameitelekeza Tip Top Connection na kuhamia WCB.

Tangu zamani Babu Tale alijulikana zaidi kwa kuwa meneja wa wasanii wa kundi la Tip Top Connection lililoundwa na wasanii kama Madee, Tundaman, Kassim Mganga, Keisha na wengineo.

Lakini baadae alianza kumsimamia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na label nzima ya WCB na kuanzia hapo akaanza kutuhumiwa kwa kuitelekeza Tip Top baada ya kuona anapata mafanikio zaidi WCB.

Madee amefunguka juu ya hilo alipokuwa anafanya mahojiano na Sam Misago na kudai sio kweli hajawatekeleza kwani bado wanafanya naye kazi:

Babu Tale bado tunafanya naye kazi Tip Top Connection na bado anaangalia kila kinachotokea Tip Top na hapo hapo bado Babu Tale ni meneja wa WCB”.

Madee amekiri kuwa maneno maneno yanayosemwa mtaani hayana ukweli wowote watu wanazusha hayo kwa sababu wanataka kusikia kuwa wana ugomvi lakini hakuna bifu wala hakuna tatizo kazi inaendelea kama kawaida.

WCB Wazidi Kurushiana Mpira Skendo ya Mjengo, Babu Tale Afunguka Kuununua Kwa Bilioni 1

Kundi na moja kati ya label kubwa ya mziki nchini ya WCB inayoongozwa na mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz imezidi kujikuta kwenye maji ya moto kuhusiana na skendo inayowazunguka hivi sasa ya nyumba.

Wiki iliyopita Diamond alitangaza kuwa amenunua mjumba kwa bilioni 1 ambayo itatumika kama makao makuu ya label yao ya Wasafi Classic Co. Lakini pia ndio makao ya stesheni mpya ya redio na TV zinazotarajiwa kufunguliwa na Diamond hivi karibuni.

Lakini utata ulikuja jitokeza pale ambapo habari zilitoka na kudai kuwa in fact mjengo ule hawakuununua kwa bilioni 1 bali waliupangisha kwani mmiliki wa mjengo huo yupo jela kwa sasa.

Babu Tale ambaye ni meneja wa Diamond amefunguka na kudai kuwa mjengo ule hawajaununua kama taarifa zilivyosambaa lakini pia hawapo tayari kulizungumzia jambo hilo kwa madai kuwa wanangojea muongozo kutoka BASATA.

Hatujanunua nyumba, tungesema kama tumenunua ila hatujawa tayari kuongea lolote muda ukifika tutaongea kwa sababu sisi tupo chini ya BASATA hatuwezi kuongea bila wazazi wetu BASATA kuwepo kwaiyo tunasubiri BASATA wakiwa tayari tutaita media ofisini kwetu”.

Suala hili zima la nyumba hii limechanganywa zaidi na madalali walioshughulikia Nyumbani hiyo kwani dalali aliyesimamia Nyumbani hii anayejulikana kama Scober au dalali mwanamke amedai kuwa Diamond alinunua mjengo huo kwa shilingi Bilioni moja lakini pia alidai ufunguzi rasmi wa men go huo utakuwa February 2 jambo ambalo Babu Tale amelipangua kwa kudai “Aliyekwambia February 2 ni nani ni mimi ni fela ni nani? Scober anaongoza WCB? Unataka kumsikiliza Scober unanisikiliza Mimi, hatuko tayari kuzungumza”.

Babu Tale Kamchana Ruby Kuwa Siku Akigundua Tatizo Lake Akajirekebisha Basi Heshima Yake Itarudi

Mdau mkongwe katika sanaa ya Bongo fleva Babu Tale na maarufu zaidi kwa kuwa meneja wa mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amefunguka na kumchana msanii Ruby kuhusu tatizo alilonalo.

Ruby ambaye ni mwanamuziki wa Bongo fleva alifanya vizuri zaidi na vibao vyake mbali mbali siku za nyuma kidogo kwa kipindi cha mwaka mzima Ruby amekuwa kimya bila ya kutoa ngoma yoyote zaidi ya kuonekana kwenye mitandao ya kijamii jambo alilolieleza kuwa amechukua mapumziko kidogo.

Mziki wa Ruby ulianza kulega lega pale alipoamua kujitoa kwenye jumba la vipaji Tanzania (THT) ambapo sanaa yake mwanzoni kabisa aliianzia kwenye jumba hilo lakini mwishoni alipishana kidogo na mabosi zake huko THT  na kuamua kujiengua.

Siku ya Jana kuna video clip iliyomuonyesha Ruby akiimba wimbo wa dini wakusifu kwa hisia kali ambapo wasanii mbali mbali walikiri kuikubali sauti yake na kukikubali kipaji chake wakiwemo Kajala, Jacqueline Wolper, Shetta, na pia Babu Tale.

Babu Tale kupitia ukurasa wake wa Instagram aliiposti video hiyo na kuisindikiza na ujumbe uliomtaka Ruby kujua anasumbuliwa na ugonjwa gani kulitatua na kisha atapata heshima yake kwenye muziki anaofanya:

Fundi Sana we binti siku ukijua unaumwa nini na ukaamua upone basi ujue heshima ya wote wanao kuchukulia poa itarudi kwako Helena mama mimi nakuzimia unajua hilo mimi ni mmoja wa watetezi wako popote ulipo mama”.

Hii ndio video clip ya Ruby iliyozua gumzo siku ya Jana mtandaoni:

 

Meneja Wa Diamond ‘Babu Tale’ Ana Hatihati Ya Kuswekwa Rumande

Meneja wa Diamond, Babu Tale amejikuta katika upande mbaya wa sheria baada ya yeye na ndugu yake Iddi Tale Tale kushindwa kulipa fidia ya shilingi milioni 250 kutoka katika kampuni ya Tip Top kwenda kwa Mhadhiri wa dini ya kiislamu. Sheikh Mbonde juu ya kosa la matumizi ya kanda za mahubiri ya kiislamu kibiashara bila ruhusa.

Mwaka Jana mwezi februari, mahakama kuu kanda ya Dar es salaam iliwataka Babu Tale na Iddi Tale Tale kama Wamiliki wa kampuni ya Tip top walitakiwa wamlipe fidia Sheikh Mbonde fidia ya milioni 250 na juni mwaka huu mahakama iliamuru Wakurugenzi hao waweke wazi thamani za kampuni hiyo na kama watashindwa kutaja mali za kampuni basi wao watalipia fedha hizo au mali zao binafsi kukamatwa na kuuzwa endapo hawatakuwa na fedha za kufidia.

Pia kama hawana mali yoyote basi watakamatwa na kufungwa gerezani kama wafungwa wa kesi ya madai kwa mujibu wa sheria.

Katika hati ya madai ya kesi hiyo namba 185 ya mwaka 2013, Sheikh Mbonde aliingia makubaliano na kampuni hiyo ya kutumia kazi sake za mawaidha kwakuzalisha, kurekodi na kuzisambaza. Vile vile makubaliano mengine yalikuwa kulipia gharama za kurekodi masomo na mafundisho ya mihadhara yake, kumnunulia gari, kumjengea nyumba na kugawana faida za mauzo vitu ambavyo havikutimizwa.

Babu Tale motoni baada ya kumpigia debe mwanasiasa kutoka Kenya

Meneja wa Diamond – Babu Tale amejikuta pabaya baada ya kujiingiza katika siasa ya nchi jirani ya Kenya ambayo itawachagua viongozi wao Agosti 8.

Watu katika mtandao wa Instagram walimvamia Babu Tale baada ya meneja huyo kumpigia debe mwanasiasa – Julius Owino maarufu kama Maji Maji anayewania kiti katika kata ya Embakasi jijini Nairobi.

Maji Maji alikuwa rapa kabla ya kujiunga na siasa, anajulikana kwa hit song yake ‘Unbwogable’ ambayo aliimba na mwenzake Gigi Gidi.

Post aliyoweka Babu Tale kwa Instagram kumpigia debe Maji Maji ilikera watu wengine ambao walimtaka aache kujihusisha na siasa Kenya.

Hafidhplatinumz: Poa poa meneja

vankempes_:Safi

kibugikayzach: Wajuaje mambo ya kenys

misskilungya: U can’t deal with Kenyan politics….. just vanish from them and do music dude…!!

laqwisher: Nchi yako imekushinda ukavamie ya jirani hembu piga kampeni bashite aoneshe vyeti original na piga kampeni haki itendeke rais wako amtumbue bashite na sio Kuwapotosha wakenya wewe huwezi wachagulia kiongozi wakuwafaa na atae watendea haki kama umeshindwa kusimama na watz kung’oa bashite

shikumilcah: @babutale weeee hatari thats my home ground MCA @majimajikenya

 

Babu Tale akerwa kwasababu mke wake ashindwa kupata ajira

Meneja wa Diamond- Babu Tale amekerwa na hali ya maisha Tanzania – ukosefu wa ajira ndo chanzo cha Babu Tale kuikemea serikali.

Babu Tale amesema kuwa amejaribu kutumia kila mbinu kumtafutia mkewe ajira lakini mbaka sasa hajafanikiwa licha ya kuwa na shahada.

Meneja huyo alisema kuwa shahada aliyopata mkewe imesalia kabatini nyumbani kwani ameshindwa kupata ajira kabisa.

“Msomi wangu bado yupo nyumbani na degree yake ipo kabatini nakumbuka nilisema ajira kamlete ila kwake imekua ngumu pamoja na connection zote nilizo nazo bado mtiani na hivi serikali imetangaza juu ya miaka 30 ajira hakuna pesa yangu imeenda bure IFM ?????” Babu Tale aliandika kwa Instagram.

“Uoga ni uzembe” Babu Tale amtaje anayemlaumu kwa kupotea kwa Roma Mkatoliki

Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wamepotea bila ya yeyote kujua nani aliwateke, wamepelekwa wapi na nia yao ni ipi.

Wasanii wengi wamehofia usalama wa Roma na wenzake kwasababu hata polisi hawajui nani aliwateka. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Roma Mkatoliki

Babu Tale, meneja wa Diamond, ameweka wazi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ndiye anafaa kulaumiwa kwa kupotea kwa Roma.

Babu Tale amemtaka Makonda awaeleze Watanzania kule Roma alipo, anasema kuwa yeye ndiye kiongozi wa kamati ya usalama Dar es Salaam kwahivyo anafaa ajue Roma alipo.

Paul Makonda

Uoga ni uzembe me nazani mwenye jukumu la kujua Roma yupo wapi ni Mkuu wa koa sababu yeye ndio kiongozi wa kamati ya usalama ya mkoa sasa ikiwa tumezunguka vituo vyote vya polisi na mwenzetu atumuoni nani wa kumfuata kumwambia tunamtaka mwenzetu kama sio @paulmakonda me naanza hili bila uoga mkuu wa mkoa naomba utusaidie kutuambia mnzetu @roma2030 alipo. Tukutane Tongwe mida hii me nipo kwa foleni wakuu #uogauzembe#freeroma,” Babu Tale aliandika kwa Instagram.

 

Baraka the Prince azua uvumi baada ya kufanya hili

Uvumi umezuka katika mitendao ya kijamii baada ya mwimbaji Baraka the Prince kuonekana na meneja wake Diamond – Babu Tale.

Baraka ameongelewa sana baada ya kupost picha kwenye mtandao wake wa Instagram kama yuko na Babu Tale.

Wengi wa mashabike wake Baraka the Prince wanadhani staa huyo anajiunga na kambi la Diamond Platnumz – Wasafi Records WCB.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakicomment kwenye picha hiyo wakisema kuwa Babu Tale anamshawishi Baraka kujiunga na Wasafi.

Kuna wale pia wanaodhani Babu Tale anataka Baraka the Prince aweke wimbo zake katika tovuti la wasafi kama wasanii wengi (wasio sajiliwa na Wasafi) walivyofanya.

 

Meneja wa Diamond Babu Tale amrarua mmiliki wa kampuni ya Global Publishers Eric Shigongo

Eric Shigongo alianza mgogoro na Wafasi alipodai kuwa Diamond anaingizwa shimoni na Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam.

Soma pia: “Diamond anapelekwa kwa shimo na watu watatu” Mmiliki wa kampuni ya Global Publishers aonya

Babu Tale amemjibu Eric Shigongo kwa Instagram:

“Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kwenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya… baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo insyagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako…

“Siku zote nimekuheshimu na Sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata..ila kesho ukawaambie vizuri waamdishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wengine na watu mbalimbali…

Babu Tale

“Tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu… Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond… ila sie kaa kimya… na kujifanya unazungaa eti unatushauri… kweli mtu unasema unampenda unamshauri instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?… Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini?…na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya Harmonize DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi “kupost tumepost… ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilika na kutak asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa…tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa…

“Hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na mashabiki zao hii ndio kuwaeka wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe… mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula madawa…yote kutafuta sababu msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kumbomoa msanii kupitia magazeti yako…tafadhali heshimu heshima yetu kwako…”Mh Magufuli tafadhali ulipo kaza legeza, ona wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoot vidogo vyao….”

Eric Shigongo na Diamond

 

 

Hili ndilo jibu Babu Tale Meneja wa Diamond alimpa Waziri wa Utalii baada ya kuwaambiwa atangaze Tanzania bure

Ikiwa kuna biashara Diamond Platnumz anadai kuinyakua, ni ile ya kutangaza nchi yake lakini wizara ya utalii haiko tayari kumpea hela zozote kufanya hiyo kazi.

Na waziri Prof. Jumanne Maghembe alihakikisha jambo hilo alipomjibu meneja wake Babu Tale. “Wasanii wetu wenye majina makubwa watangaze tu Tanzania, Tanzania ni nchi yao sio lazima mpaka waambiwe waje tukae pamoja  tupange mikakati na tuangalie ni kitu gani anaweza kufanya na watusaidie kutangaza utalii wetu” alisema.

Hapo ndipo Babu Tale alijibu kwa kueleza hivi:

“Duh hapa sijui mimi mshamba au sijamuelewa vizuri Mh Waziri kuhusu kuitangaza Tanzania mimi kwa akili yangu fupi naona watu wa nchi jirani wanatafuta wasanii watanzania kutangaza nchi zao hapa kwetu tunaambiwa tuombe ili tutoe msaada mh sasa hela ya wizara inaenda wapi???? >>>>> Babu Tale

“Cha ajabu unaweza ukaambiwa uitangaze nchi halafu utapelekwa mbugani bure duh. Ninachojua kila sekta inamfuko sasa hili eneo la utalii mfuko upo wapi mimi naendelea kuuliza mfuko wa kuitangaza Tanzania kwa nia nzuri na mazuri yaliyopo umewekwa wapi??>>> Babu Tale

“Leo wasanii wengi wanakimbilia hata kufanya video zao nje ya nchi sababu ukitamani kufanya kitu nchini inakuwa kama mtu anakukomoa usifanye. Hvi Samatta anavyofunga magoli wangewaza kumvalisha bendera ya tanzania nguo yake ya ndani pale anapofunga goli avue watu waone duniani kuna nchi inaitwa Tanzania ingekuwa je?>>> Babu Tale

“Sina nia mbaya ila tuamke kweli kuitangaza nchi yetu na sio wahusika waifuate sekta husika wakati kila sekta inakitengo cha matangazo na wanajua nani wakupewa jukumu #mtazamochanya #Tanzania #”