Babu Tale Aanika Ukweli Kuhusu Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Babu Tale amefungukia kwa mara ya kwanza tetesi zinazoendelea kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Rich Mavoko katimuliwa.

Tetesi hizi zilianza wiki chache zilizopita baada ya Mavoko kutoonekana Kwenye tangazo jipya la Trailer ya Wasafi reality show lililowaonyesha wasanii wote wa WCB na familia ya Diamond.

Kwenye mahojiano  na Ijumaa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp akiwa Marekani, Babu Tale alisema kwamba tetesi hizo siyo za kweli na Mavoko bado yupo WCB ila kipindi ambacho walikuwa wanachukua video ya Reality Show aliyoiposti Diamond ambayo ndiyo iliyozua maneno mwanamuziki huyo hakuwepo alikuwa kwao Mahenge, Morogoro kwenye msiba kwani alifiwa na dada yake.

Wakati tunarekodi hiyo video ya Reality Show, Mavoko alikuwa Mahenge kwao, alifiwa na dada yake kwa hiyo alikuwa kwenye msiba, lakini hizi siku zote yupo bize anashuti wimbo wake mpya na zamu inayokuja ni yake kuachia wimbo kwani sisi huwa tunaachiana muda wa kutoa nyimbo kwa hiyo sioni haja ya kuongopa kwamba hayupo WCB, kwa sababu hata asipokuwepo lazima itajulikana tu”.

Baada ya habari kuanza kusambaa Mavoko alimtafuta ili kuthibitisha taarifa hizo lakini alikataa kabisa kuongea na kutaka uongozi wake utoe majibu ya maswali hayo.

Mahakama Yatengua Hukumu ya Babu Tale.

Mahakama Kuu imetengua na kufuta amri ya kuwakamata na kuwafunga gerezani wakurugenzi wa Tip Top Connection Company Limited, Hamis Shaban Taletale maarufu Babu Tale na ndugu yake Idd.

Uamuzi wa kufuta amri hiyo ulitolewa juzi na Jaji Edson Mkasimongwa baada ya kujiridhisha kuwa haikuwa halali kutokana na mamlaka iliyoitoa kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Februari 16 naibu msajili wa mahakama hiyo, Wilbard Mashauri aliamuru Babu Tale na nduguye Idd wakamatwe na kupelekwa kifungoni katika Gereza la Ukonga kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya mahakama na Aprili 4 alitoa na kusaini hati ya kuwakamata.

Katika hukumu iliyotolewa na Jaji Agustine Shangwa Februari 18, 2016 ndugu hao waliamriwa kumlipa fidia ya Sh250 milioni, mhadhiri wa dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kutokana na makosa ya kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake

Show Za Diamond Zinajazwa na Wazungu na Wajamaica Sio Waafrika Pekee- Babu Tale

Meneja wa staa wa Muziki wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kueleza hali ya shoo za Diamond kwenye Tour ya ‘A boy from Tandale’ inayofanyika nchini Marekani.

Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa katika shoo zinazoendelea kufanyika nchini Marekani kwa sasa zinakuwa zinahudhuriwa na mashabiki wa mataifa mbali mbali kama wazungu na sio Waafrika tu kama ilivyozoeleka.

Kwenye mahojiano aliyofanya na JJ wa Jembe FM Babu Tale ambaye ameongozana na Diamond katika tour hiyo, amesema kuwa show za Diamond zimekuwa ni za watu wote na si wale kutokea Afrika pekee.

Ukiangalia clip ambayo ameposti Diamond utaona watu weupe kibao, nimeona wazungu kibao, Jamaica walikuwepo“.

Imekuwa ni Kasumba kuwa wasanii wanaoenda kufanya shoo nje ya nchi huishia kupiga shoo za sebuleni jambo ambalo Diamond amekuwa akilibadilisha kwani amekuwa akionekana akipiga shoo Kwenye kumbi kubwa na kujaza mashabiki kibao.

Meneja wa Diamond Aitibua Mahakama.

Meneja wa msanii Diamond Platnumz anaejulikana kama Babu Tale anazidi kuitibua mahakama baada ya kutakiwa kufika mahakamani wiki hii lakini kushindwa kufika kwa madai ya kuwa nje ya nchi huku akiwa alishakatazwa  kutoka nje ya nchi ikiwa kesi yake ikiendelea mahakamani.

Meneja huyo ambae alikuwa na kesi ya madai baada ya kampuni yake kufanya matangazo na baishara ya  kanda za dini za shekhe mmoja jijini dar es salam bila ridhaa yake na kuamuliwa kulipa fidia lakini alishindwa kulipa fidia na kutokomea kabisa.

HGata hivyo baada  ya kesi hiyo kuendelea kwa muda mrefu ilisogezwa mbele kwa siku kadhaa kutokana na kutokuwepo kwa wahusika hasa majaji waliokuwa wakishughulikia kesi hiyo.

Babu Tale alipewa masharti moja wapo ikiwa kutokusafiri nje ya nchi mpaka kesi hiyo itakapo kwisha lakini kesi yake ilipotajwa hapa mara ya mwisho babu tale alishindwa kuhudhuriwa kwa kupata dharura ya kusafiri.

 

Babu Tale Bado Anatusimamia Tip Top Pamoja na Kuwa Bize WCB- Dogo Janja

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kukiri kuwa Babu Tale bado anawasimamia wasanii wa Tip Top pamoja na kuonekana sana WCB.

Babu Tale ambaye kwa sasa ni Meneja wa staaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, lakini ni mmoja kati ya waanziloshi wa label ya kitambo ya Tip Top yenye wasanii nguli kama Madee, Dogo Janja, Kassim Mganga na wengineo.

Lakini tangu Babu Tale apate mafanikio katika label ya WCB Kumekuwa na tetesi kuwa amewatelekeza wasanii wote wa Tip Top baada ya kuonekana sana WCB tetesi ambazo Dogo Janja amezikana.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa hilo halina ukweli wowote kwani wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi.

Hapana sio kweli, Babu Tale anasimamia kazi zangu sana sana ila kwamba huku Tip Top sisi hatuko bize kama Wasafi ndio maana unaoa muda wote yupo kule, hatuna matukio.

Lakini nikiachia wimbo utaona redioni nitaenda na Babu Tale, so mimi sina matukio mengi ndio maana kwenye kazi zangu anakuwa mara chache sana pale ninapomuhitaji”.

Dogo Janja hivi sasa chini ya Label ya MMB (Manzese Music Baby) ambayo iko chini ya msanii mkongwe Madee Ali.

Kesi ya Babu Tale Yaonekana Kuwa Bado Ngumu.

Kesi inayomkabili meneja ya tip top connection babu tale bado inaonekana kuwa  ngumu kutokana na uzito wake baada ya wawili hao kuitwa tena mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.babu tale ambae anashitakiwa na mahakama akisimama kamammwakilishi wa tip top connection kwa kosa la kurudufu cd za mawaidha ya shekhe huyo bila ridhaa yake .

Hata hivyo hukumu ya kesi hiyo iliyowahi kutolewa hapo kabla ilimtaka babu tale kutoa fidia ya milion 250 kwa shekhe huyo lakini babu tale hakutekeleza swala hilo.

Kesi inazidi kuwa nzito kwa sababu hakimu aliyetoa hukumu hiyo inasemekana alisaidi hati ya hukumu hiyo akiwa amekwisha staafu na kwamba hata  msajili wa mahakama aliyesimamia kesi hiyo hana mamlaka ya kutoa hukumu ya kufungwa kwa mshtakiwa .

Hata hivyo baada ya mvutano wa muda mrefu, mahakama imepanga  kukutana tena na pande zote mbili juni 25 mwaka huu tena.

Tunawakataa Kwa Sababu na Wao Walitukataa.:-Babu Tale.

Meneja wa team ya wcb, babu tale amefunguka na kusema kuwa kuna baadhi ya media zilikuwa zimekwama kupiga nyimbo za WCB hapo mwanzo na sasa wanataka kurudi na kupiga tena na kutangaza habari zao, yeye anaomba waendelee kuacha kutoa habari zao wala lupiga tena nyimbo zao kwa sababu walshaamua kufanya hivyo.

tunaendelea kuwaomba waendelea kuwashinikiza wafanyakazi wao wasipige nyimbo zetu wala kutoa habari zet hivyo hivyo,hatutaki kuona wanapiga nyimbo zetu wala kurusha matangazo yetu,walitukataa mwanzo na sisi tunawakata kwa sabau walitukataa.

Hata hivyo Diamond aliwahi kusema kuwa katika tasnia waliopo michez ya kubaniana ipo sana kwa ivyo kwa upande wake hawezi kulaumu sana swala hilo.

WCB Wagoma Nyimbo Zao Kupigwa na Habari Zao Kuripotiwa na Baadhi Ya Media

Label au kundi linalofanya vizuri hivi sasa nchini WCB linaloongozwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz limetoa tamko rasmi la kuwataka baadhi ya media wasipige nyimbo zao.

Meneja wa label hiyo Babu Tale ametoa tamko hilo jana wakati akichonga na waandishi wa habari Kwenye uzinduzi wa Wasafi Tv Kwenye king’amuzi cha Startimes.

Babu Tale amevitaka vyombo vilivyokataa kupiga nyimbo zao Mwanzoni viendelee hivyo hivyo na hata visijaribu kuripoti taarifa zao.

Tunaendelea kuwaomba waendelee kushinikiza wafanyakazi wao wasipige nyimbo zetu.

Hatutaki kuona wanapiga nyimbo zetu wala kutoa habari zetu kwa sababu wao walitukataa mwanzo, tunawakataa kwa sababu wao walitukataa“.

Diamond amekuwa katika mgogoro mzito na Media mbali mbali ambazo zimekuwa hazipigi kabisa nyimbo zake ambazo ni Clouds Media na hata East Africa Radio na Tv.

 

Zari Sio Chanzo Cha Diamond Kukonda, Babu Tale Ataja Sababu Hizi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye pia ni CEO wa WCB amekuwa kwenye headlines sana na moja kati ya vitu vinavyo trend ni mwili wake kuisha.

Baada ya Diamond kuonekana anapungua mwili kwa kasi habari zilisambaa Mtandaoni kuwa kisa ni Zari ambapo ilidaiwa baada ya kumwagwa na Zari Diamond alipata mawazo sana na hata kudaiwa eti sahivi hapati matunzo aliyokuwa anapata wakati yupo na Zari.

Lakini Meneja wa Diamond, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa sababu za Diamond kupungua mwili kwa muda mfupi kuwa ni kukosa muda wa kulala kutokana na jukumu zito la ujio wa Wasafi TV.

Kuna baadhi ya watu wanasema msanii wangu anapungua mimi na nenepa navimba, Kama hamjui Media sio kitu kidogo, wakati tunaanza tulijua ni kazi ndogo, kwa miezi sita non stop msanii wangu analala masaa mawili tu, kwa sababu ya kuandaa hiki mnachokiona machoni mwenu.. Wiki mbili za mwanzo tukawa tunakasirika kwa nini anafanya kazi ngumu, ilipofika mwezi tukawa tunaona  ana-loose weight (kupungua uzito) na bado kazi zinaendelea tukawa tunashangaa ana nia gani huyu”.

Lakini pia mwana Familia wa Diamond mwenyewe,ambaye ni dada yake Esma aliwahi kunukuliwa akisema kaka yake kapungua kwa kumiss penzi la Zari.

Nikki wa Pili Atupa Dongo kwa Babu Tale, ni Baada ya Kwenda South kwa Zari

Msanii wa Hip-Hop nchini, Nikki wa Pili amemtupia dongo Babu Tale baada ya babu tale kwenda afrika ya kusini na kurudi huku akitangaza kuwa lengo lake ku ilikuwa ni kwenda kumbebeleza zari ambae ni zazi mwenzie na diamond ili kurudiana na diamond.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, Nikki wa Pili alisema kuwa kazi ya babu tale kutumwa haijaanza leo ameanza kutumwa tangu akiwa kijana enzi hizo anatumwa na kaka yake ku-burn CD  na sasa hivi anatumwa na Diamond kubembeleza ndoa.

babu tale alikuwa akitumwa empty CDs na majani  pale bongo records ili ku-burn CD s za wasanii wa kaka yake,siku hizi natumwa akabembeleze ndoa SAUZI…. kweli swala la uadilifu katika utumishi  linaendelea.

Babu Tale Adai Hata Akichepuka Mke Wake Hawezi Kumuacha

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kama Babu Tale amefunguka na kudai kuwa anajua hata akichepuka mke wake hawezi kumuacha.

Wikiendi iliyopita Babu Tale alisafiri kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na mzazi Wenzake Zari baada ya kutokiwa Kwenye maelewano kwa miezi kadhaa.

Lakini tangu akiwa S.A kumekuwa na  taarifa Mtandaoni zinazodai kuwa Babu Tale amezaa mtoto na mwanamke mwingine na kumtelekeza mtoto huyo bila matunzo yoyote.

Baada ya taarifa hizo watu walimjia juu Babu Tale kwa kukimbilia kurekebisha maisha ya Diamond ilihali ya ndoa yake na mkewe  yanamshinda.

Basi Babu Tale kawamwagia povu wale wote wanaoeneza taarifa na kusema yeye na mke wake wametoka mbali wako pamoja kwa zaidi ya miaka 17 hivyo mke wake hawezi kumuacha hata afanye kosa gani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale alimwaga povu hili:

 

Nay wa Mitego: Babu Tale Kaiba Wazo Langu La Kuwapatanisha Diamond na Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amemjia juu Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale huku akidai yeye ndio aliyetoa wazo la kuwapatanisha Diamond na Zari.

Mwanzoni mwa wiki hii Babu Tale alifunga Safari kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na Zari kitendo ambao Nay amekiri kuwa ni kizuri lakini amehoji kwa nini amesubiri mpaka yeye atoe wazo hilo alafu ndio na yeye aende.

Babu Tale Alipoenda South Africa kumuombea Diamond msamaha

Kwenye na mahojiano na Risas Mchanganyiko, Nay wa Mitego amemtolea povu hilo Babu Tale:

Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli”.

Siku video ya wimbo wa Iyena ulipotoka Nay alimshauri Diamond aachane na Hamisa na arudiane na Zari na hata kumuhaidi atasaidia kumuombea msamaha na kuwapatanisha.

Nay wa Mitego: Babu Tale Kaiba Wazo Langu La Kuwapatanisha Diamond na Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amemjia juu Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale huku akidai yeye ndio aliyetoa wazo la kuwapatanisha Diamond na Zari.

Mwanzoni mwa wiki hii Babu Tale alifunga Safari kwenda nchini South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha Diamond na Zari kitendo ambao Nay amekiri kuwa ni kizuri lakini amehoji kwa nini amesubiri mpaka yeye atoe wazo hilo alafu ndio na yeye aende.

Babu Tale Alipoenda South Africa kumuombea Diamond msamaha

Kwenye na mahojiano na Risas Mchanganyiko, Nay wa Mitego amemtolea povu hilo Babu Tale:

Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli”.

Siku video ya wimbo wa Iyena ulipotoka Nay alimshauri Diamond aachane na Hamisa na arudiane na Zari na hata kumuhaidi atasaidia kumuombea msamaha na kuwapatanisha.

Nilishawahi Kumshauri Hamisa Kuhusu Mahusiano Na Diamond Kabla:-Babu ale

Kwa sasa meneja  huyu alifunguka na kusema mazio kuhusu mahusiano ya msanii wake na mwana dada hamisa mobeo ambapo alisema kuwa kabla hamisa hajaanza mahussiano na diamond aliwahi kumwambia kuhusu kuwa na ahadhari juu ya mahusiano hayo kabla.

,Babu Tale amesema kabla ya Hamisa kuzaa na Diamond alishawaonya kwani wakati huo Diamond alikuwa katika mahusiano na Zari. “Kabla Hamisa hajapata ujauzito, tulikuwa tuna-shoot video ya Salome nikamwambia Zari sio adui yako, kama una mapenzi na Diamond mpende ila kama unataka kumkomesha, kamkomeshe Lulu, ila kama unataka kufanya hivyo haipendezi,” amesema. “Nikamwambia pia Diamond kama unafanya ujana, inatakiwa pia uangalie ujana wako yule demu (Zari) amekuja huko from nowhere amekuzalia mtoto pia,” Tale ameiambia Wasafi TV.

Moja ya sababu alizoeleza Zari kuwa zilichangia kuachana na Diamond Platnumz ni kitendo cha kuzaa na Hamisa Mobetto. Babu Tale kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini kuhakikisha Diamond na Zari wanamaliza tofauti zao.

haa hivyo Babu Tale ilisemekana kuwa maekwenda  Afrika ya kusini kwa ajili ya, kufanya usuluhishi wa maaioz ya Zari na Diamond  hivyo bado majibu hayajakuwa wazi.Haa hivyo baadhi ya picha zimekuwa zikionyesha meneja huyo yuko nyumbani kwa Zari na familia yake.

Babu Tale- Sijaenda South Africa Kurudisha Penzi la Diamond na Zari

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kudai hakuenda nchini South Africa Kurudisha Penzi la Diamond na Zari.

Wikiendi iliyopita habari ya mjini ilikuwa Zari na Diamond baada ya video ya wimbo wa iyena kutoka ukiwaonyesha wawili wakifunga ndoa mwaka jana wakati bado wapenzi.

Babu Tale alitengeneza headlines baada ya kutangaza anaenda nchini South Africa kwa ajili ya kwenda Kurudisha Penzi la Diamond na Zari baada ya kutengana kwa zaidi ya Miezi minne sasa.

Lakini baada ya kufika nchini humo ambako ndipo Zari anaishi na watoto wake Babu Tale ameweka wazi kuwa hajaenda Kurudisha Penzi lao bali ameenda kuwapatanisha wawili hao ili waweze kulea watoto wao.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Babu Tale amesema ameona ni vyema wawili hao wakaelewana kwa manufaa ya watoto wao:

Kilichonileta  huku ni kuwasuluhisha matatizo yao wayaweke pembeni ili waweze kulea watoto wao, of course nimeongea sana na Zari nikamwambia kama mnataka kurudiana kimapenzi it’s up to you lakini mimi ningependa kuona wewe na Diamond mnapatana ili  watoto waweze kuwa karibu na nyinyi na ikitokea tupo South Africa ni rahisi kupita kusalimia watoto na kama watoto wamemiss Baba unampigia simu”.

Diamond na Zari wamekuwa na uadui fulani tangu wawili hao walipoachana Miezi michache iliyopita ambapo Zari alimtuhumu Diamond kwa kutowaona watoto wake kwa miezi mitano kutokana na wao kukosa maelewano.

Sifanyi Shoo Mwezi wa Ramadhan;-Tunda Man

Msanii Tunda Man amefunguka na kusema kuwa mwezi huu mtukufu wa ramadhani ni mwezi wa toba na sala hivyo hata siku moja katika mwezi huu hawezi kufanya kazi yoyote ya sanaa kwa sababu muda mwingi anakuwa katika swala.

Tunda Man anasema hiki ndicho kipindi cha kufanya toba na kumrudia Mwenyezi Mungu na pia kumshukuru kwa kila kitu .

Mimi mwezi huu mtukufu huwa naacha kila kitu, hata mtu aje na show ya milioni mia 2 sifanyi shoo, na nina swali sala zote tani ilimradi tu nimtumikie mwenyezi Mungu anisamehe madhambi yote niliyoyafanya.

Hata hivyo Tunda Man anasema kuwa kesi inayomkabili babu tale kwa sasa haimuhusu bali ilitakiwa kuwa ya Abdul Bonge lakini Abdul Bonge hayupo

Ile kesi haimuhusu kabisa Babu Tale , ile kesi ilikuwa ya abdul bonge na Abdul Bonge ni marehemu sasa, kwa kuwa wale ni tip top connection basi ile kesi hata mimi inanihusu.