Kauli ya Dogo Janja Yawashtua Mashabiki.

Katika ukurasa wake wa twitter msanii Dogo janja amewashtua mashabiki zake baada ya kuweka ujumbe ambao kidogo umeashiria kama mtu aliyekataa tama kabisa na maisha hivyo kujikuta akiongea vitu vinavyoashiria kutaka kupoteza uhai.

Msanii huyo ambae hapa karibuni lizivuma tetesi kuwa alilazwa huku sababu kubwa ikiwa ni presha na mshtuko alioupata baada ya kugomabana na mke Irene uwoya ambae wamefunga ndoa mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo Dogo janja alipoulizwa kuhusu maneno hayo alikri kuyaandika huku akisema kuwa hiyo ni baadhi ya mistari katika nyimbo yake mpya huku akikataa kuongelea swala la yeye na mkewe.

Dogo Janja Atoa Sababu ya Kutobadili Jina Lake.

Msanii dogo janja amefumguka na kusema kwa pamoja na kwamba kwa sasa ameshakuwa na watu wamkuwa wakisema kuwa jina hilo halistahilitena kutokana na ukweli kuwa umri wake umeshakuwa , yeye anakataa na kusema kuwa hawezi kubadili jina hilo kwa sababu tayari hiyo ni brand na hawezi kuipoteza kwa sababu ameifanyia kazi kwa muda mrefu sana.

kama tukiangalia kwa nchi nyingi  duniani , wasanii wanakuwa na viunganishi vya majina ambavyo baada ya umri flani kuviondoa kwa sababu vinakuwa tayari havipaswi kutumika kutokana na umri wake na ndivyo inawezekana ilitakiwa kwa dogo janja kutokana na neno DOGO haliendani tena na umri wake sasa.

Dogo janja anasema ‘mimi ni forever young, dogo janja ni brand ambayo ilitengenezwa kwa miaka 9 sasa kwaio kwangu ni biashara ukiachana na udogo au ukubwa wangu.kwaio hiyo ni biashara ambayo inajitegemea.

 

Dogo Janja Asema Hana Bifu na Young Killer Wala Young Dee.

msanii wa bongo fleva dogo janja amefunguka na kukanusha tetesi zinazosambaa kuwa yeye na wasanii wenzanke young dee na young killer wamekuwa na kutokuwa na maelwano ya muda mrefu kitu ambacho sio cha kweli hata kidogo.

Dogo janja ameyaongea hayo alipokuwa katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa na EATV.

Sijawahi kuwa na ugomvi na msanii yoyote hapa nchi kwa sababu mimi ninapita katika njia yangu na wao sio njia ya mtu mwingine yoyote.kwaio watu wanaamua kufanya hivyo  na kuweka ule u-young lakini hakuna ukweli owowte kuhus sisi kuwa na ugomvi.

Upande wetu siis nje ya muziki tunayo maisha yet tofauti kabisa,kwaio huwa tunakutana na tunafanya tunayoyafanya kwa  amani tunakutana sana na huwa tunataniana sana na hawaniwezi mimi kwa matani na wao wanajua hilo.

Hata hivyo Dogo janja amefunguka na kusema kuwa hakuna changamoto anayoipata katika swala la muziki kwa sababu wenzake wamekuwa waki-ra na yeye akiimba hivyo hakuna changamoto.

Matumizi ya Kinga Yamzuia Dogo Janja Kupata Mtoto.

Msanii wa bongo fleva anetamba sana kwa sasa na wimbo wake wa Banana dogo janja ambae pia ni mume wa msanii wa filamu nchini irene uwoya , amefunguka na kusema kuwa  kabla hajaoa ilikuwa ni vigumu sana kwake kupata mtoto kutokana na wosia aliwahi kuachiwa na baba yake.

Akijibu swali aliloulizwa na mashabiki kuhusu  idadi ya watoto alionao mpka sasa , Dogo Janja anasema kuwa hana mtoto na wala hajwahi kusingiziwa mtoto katika maisha yake ya ujana .

sijawahi kusingiziwa mtoto maisha yangu yote ,kwa sababu mimi napenda sana kutumia kinga,alafu na marehemu baba yangu aliwahi kuniambia kuwa nisipate mtoto nje ya ndoa.kwa sasa nimeona kwaio siwezi kuendelea kutumia kinga na panapo majaliwa basi tutapata mtoto soon.

Dogo Janja Ataja Ngoma Ambayo Haikubali Kutoka Kwa Madee

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuanika jina la ngoma kutoka kwa Msanii mwenzake Madee Ali.

Dogo Janja ameitaja ngoma ya Madee ‘Hip Hop haiuzi’ kama moja ya nyimbo za Msanii huyo ambazo hajawahi kuzikubali kabisa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kwetu Flavor cha Magic Fm Dogo Janja ametaja ngoma ya Madee ‘Hip Hop Haiuzi’ kama wimbo ambao hakupendezwa nao kabisa pindi ulipotoka.

Kipindi hiyo unatoka nipo chuga, nachana sana na masela. Nikaona huyo vipi, masela wanasema huyu waki labda hasije chuga, tutamfanyia kitu mbaya”.

’Hip Hop haiuzi’ ni nyimbo ya Madee ambayo ilizua gumzo sana miaka ya nyuma ambapo wasanii wenzake ambao wanafanya muziki wa Hop Hop walimjia juu MAdee baada ya kuuponda muziki wao wa hip hop.

 

Belle 9- Dogo Janja Ndio Anatakiwa Kuchapwa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Belle 9 ameibuka na kudai kama kuchapwa anatakiwa kuchapwa Dogo Janja sio yeye.

Wiki iliyopita Dogo janja Kwenye Interview yake alisema Belle 9 anahitaji kuchapwa viboko 70 baada ya kusema Hamuelewi na hata nyimbo zake anzoimba huwa hazielewi.

Kwenye mahojiano na Enews ya EATV, Belle 9 amemjibu Dogo na kusema inabidi achapwe yeye kwani nyimbo yake mpya ya ‘Banana’ ni ngoma ya kihuni na hajaielewa:

Nilivyosema msanii ambaye simuelewi ni Madee sikuwa na maana mbaya na samahani kama wamekasirika lakini niliongea kwa uzuri maana ni msanii ambaye huwa namuangalia.

Kusema ukweli nilivyosikia anasema nichapwe viboko nilicheka sana na huenda tunatofautiana kufikiria na labda kwa mazingira aliyokulia yeye anaona kuchapwa viboko kunaweza kumbadilisha mtu ila sio pointi sana maana mambo yamebadilika.

Halafu kama ni viboko anatakiwa achapwe yeye kwa nyimbo anazoimba zenye  utata kwani nyimbo iliyopita alivaa kama mwanamke na nyimbo yake mpya ya Banana anaimba sijui your my Banana na wote tunajua Banana ina maana gani”.

 

Tip Top Haijafa Ila Majukumu Ndio Mengi- Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dogo Janja ameibuka na kuongelea suala la kundi la Tip Top Connection kuvunjika ambapo amedai halijavunjika bali kila msanii ana majukumu mengine.

Kundi kwa Tip Top Connection liliwahi kuvuma sana na kufanya vyema sana miaka ya nyuma na liliundwa na wasanii kama Madee, Kassim Mganga, Keysha, Dogo Janja na wengineo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dogo Janja amesema kuwa sio kweli kuwa kundi hilo limekufa kutokana na kwamba hawatoi wimbo wa pamoja bali majukumu mengine na muda vimewatenganisha.

Tip Top ipo pale pale, umri na majukumu sio watu tena wa kukusanyana masikani tena ndio kitu ambacho watu wanakuwa wanapishana sana lakini Tip Top ipo na inafanya.

Watu wanazungumza kwa sababu hakuna wimbo wa kundi nahisi ndio chanzo cha watu kuzungumza hivyo”.

Wasanii ambao walikuwa wanaunda kundi hilo wamesambaratika huku kila msanii akiwa anafanya muziki wake ingawa wamekuwa wakionekana pamoja Kwenye matukio mbali mbali pamoja kama Kwenye Harusi ya Dogo Janja.

Dogo Janja- Belle 9 Amemkosea Sana Madee

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Dogo Janja anayefanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Banana’ amedai kuwa Msanii mwenzake Belle 9 amemkosea sana Madee hivyo anahitaji kuadhibiwa.

Wiki chache zilizopita Kwenye mahojiano na Jembe FM ya jijini Mwanza Belle 9, alimtaja Madee kama rapa wa Tanzania ambaye haelewi nyimbo zake kabisa anaona kama mzugaji kwani anaona ni msanii ambaye anatoa ‘beat’ tu na sio wimbo.

Katika interview na Enews ya East Africa Tv, Dogo Janja amemjia juu Belle 9 kwa kumwambia kuwa amekosea sana kumbeza msanii mkongwe kama Madee ambaye ameshawahi kutoa ngoma kali nyingi hata kabla ya Belle 9 kujulikana kwenye muziki.

Kitu cha kwanza hata yeye Belle 9 kuna vitu anafanya kuna watu huwa hawamuelewe, hata mimi mwenyewe kuna wanangu kibao huwa wananiambia bora Nuruely. Alichokifanya Made kwenye muziki, Belle 9 hata robo hajafikia.. Respect a legend, waheshimu wakongwe, waheshimu wazee sio busara kutukana wakongwe.

Kakosea amemkosea mzee, anatakiwa apigwe 70 bomani (wamasai hapo wamenielewa) ukivunja sheria au ukimkosea mkubwa au mzee unatakiwa uchapwe fimbo 70 mbele ya wanabomani wote.. Madee mpole sana ndio maana wanamuonea. ni mkongwe anayezeeka na heshima zake”.

 

Rayvanny Amwagia Povu Zito Dogo Janja

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Rayvanny amemwagia povu zito msanii mwenzake Dogo Janja na kumtaka ampe heshima yake.

Siku chache zilizopita Dogo Janja alimtaja Rayvanny kama msanii ambaye hajui kuvaa Kwenye Interview yake na Wasafi Tv na kujitolea kumvalisha.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Rayvanny amejibu tuhuma hizo na kusema kuwa Dogo Janja anakosea kusema hivyo kuni kuna tofauti kati ya mtu kujua kuvaa na mtu kupendeza.

Kuna tofauti kati ya kuvaa na kupendeza, mtu akikuambia hujui kuvaa, anakosea, labda akuambie hujui kupendeza.

Cheni yake ambayo anaivaa sasa hivi, aliivaa Dully Sykes kwenye wimbo wa Sugar Mami. Kwa hiyo ukija kusema eti una uwezo wa kumvalisha Rayvanny hajui kuvaa, no!, unanikosea heshima kwa sababu mimi nimeenda sehemu nyingi nimeona watu wanavaa vitu tofauti”.

Dogo Janja ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Banana’ ambayo imeendelea kushika namba moja Kwenye mtandao wa YouTube.

Dogo Janja Aponda Mavazi Ya Rayvanny

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Banana’ Dogo Janja amedai msanii kutoka label ya WCB Rayvanny anamuangusha sana Kwenye suala la mavazi.

Siku za nyuma Dogo Janja ameshawahi kuachia ngoma maalumu kwa ajili kuvaa na kupendeza Inayoitwa ‘Ukivaaje unapendeza”.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kama  akipata fursa ya kumvalisha Rayvanny atafanya hivyo.

Nikiambiwa msanii ambaye niwe namvalisha namchagulia mavazi, nitamchagua Rayvanny huwa ananiangusha sana sometimes.

Kuna muda huwa anapatia halafu kuna muda unaweza ukatema mate kule, anaweza akala njano juu mpaka chini”.

Dogo Janja yupo katika Media Tour kwa ajili ya kutangaza rasmi Single yake mpya ‘Banana’ inayoendelea kufanya vizuri Kwenye chati mbali mbali.

Babu Tale Bado Anatusimamia Tip Top Pamoja na Kuwa Bize WCB- Dogo Janja

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kukiri kuwa Babu Tale bado anawasimamia wasanii wa Tip Top pamoja na kuonekana sana WCB.

Babu Tale ambaye kwa sasa ni Meneja wa staaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, lakini ni mmoja kati ya waanziloshi wa label ya kitambo ya Tip Top yenye wasanii nguli kama Madee, Dogo Janja, Kassim Mganga na wengineo.

Lakini tangu Babu Tale apate mafanikio katika label ya WCB Kumekuwa na tetesi kuwa amewatelekeza wasanii wote wa Tip Top baada ya kuonekana sana WCB tetesi ambazo Dogo Janja amezikana.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa hilo halina ukweli wowote kwani wamekuwa wakishirikiana kwa mambo mengi.

Hapana sio kweli, Babu Tale anasimamia kazi zangu sana sana ila kwamba huku Tip Top sisi hatuko bize kama Wasafi ndio maana unaoa muda wote yupo kule, hatuna matukio.

Lakini nikiachia wimbo utaona redioni nitaenda na Babu Tale, so mimi sina matukio mengi ndio maana kwenye kazi zangu anakuwa mara chache sana pale ninapomuhitaji”.

Dogo Janja hivi sasa chini ya Label ya MMB (Manzese Music Baby) ambayo iko chini ya msanii mkongwe Madee Ali.

Dogo Janja Atoa Darasa kwa Wanawake Wasidanganyike.

Msanii Dogo Janja amewataka wadada kutodanganyika na wanaume na kuwa nao makini kwa sababu wanaume wengi wamekuwa wakitumia uongo kuwanasa wanawake na wakishawapata baadae wanawake wanaanza kujutia maamuzi yao.

dogo janja anasema kuwa wanaume wengi so wakweli kama ambavyo wanawake wanavyozani lakini wanapokuja huja na njia nyimgi zinazowafanya wadada waamini kuwa mwanaume anamtaka anaongea ukweli,dogo janja ameyaongea hayo alipokuwa akizungumza na kipndi cha DADAZ kinachorushwa na  EATV.

Unajua vijana wegi ni waongo sana tena hasa wanaume ni waongo sana,ogopa sana mwanaum anaekufata na gari , heshimu anaekufata na mguu maana anakuwa yuko real.anakueleza kuwa anakupenda na maisha yangu yako hivi na hivi , ninaweza kuatafuta nikapata au nikakosa kuliko anaekufata na kukupeleka huku mara kule mara akununulie wigi la laki 8,mwishowe ananza kukopa na kukuongopea.

Dogo janja ameamua kujitolea mfano yeye mwenyewe na kusema kuwa wakati anamfata Irene alimwambia ukweli kuwa hana kitu kikubwa na kwamba uwezo wake ni wa kawaida tu.

Alichojifunza Dogo Janja Kupitia Video ya Nandy na Bilnass Kuvuja.

Msanii Dogo Janja amefunguka na kusema kuw kutokana na kitendo alichokutana nacho Nandy amejifunza kuwa wasanii wengi hawana ushirikianao katika kupatwa kwa matatizo kwa wasanii wenzao zaidi ya kuwa wanashuapalia mambo.

Kupitia matukio mawili makubwa ambayo  ya roma kutekwa na nandy kuvujisha video inamfundisha tabia za wasaniiwengine huku akisema kuwa kwa tukio la nandy wasanii wengine wamefurahishwa na tukio ilo na walikuwa wakiomba sana Nandy aweze kufungiwa kama adhabu ili iwe faida kwao kwa kupata show.

Nahisi ninaweza kumaindiwa leo na wasanii wenzangu lakini ni lazima mtu aanze ndio hili donda ndugu litapona.wasanii sis ni masinchi sana na baada ya hii ishu ya nandy ndo nimepata uhakika , kipindi cha isu ya roma nilikuwa nikiona baadhi ya watu kwenye makundi walikuwa wakisema atakoma eeh amezoea huyo , lakini pia jana na juzi nimekaa nabaaadh ya wasanii wakubwa wanasema bora hili limetokea kwa nandy maana na spidi ya show zitapungua , bora baraza wamfungie kidogo hata miezi 6 ili apotee kidogo.walikuwa wanapiga stori kama utani lakini moyoni nimefikiria sana.

wasanii tuache roho mbaya wote sisi ni maskini tu na wote tunahangaikia ugali, tukipata ajali kazini tusiombeane mabaya.vita iwe kwenye kazi tu.

 

Dogo Janja Kuwa Video Queen Kwenye Video ya Niki Mbishi

Baada ya kushambuliwa sana katika mitandao ya kijamii kuhusu nymbo yake ya wayu wayu ambayo imekuwa gumzo baada ya yeye mwenyewe kutokea kama video queen, msanii Dogo Janja ajibu kwa kashfa  maneno ya msani mwenzake Niki Mbishi kuwa hata kama yeye atamwajiri kutokea katika video yake kama video queen kwake ni sawa na hana shida na hilo.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Nikki mbishi aliandika “dogo janja ni video queen’ na ndipo dogo janja hakutaka kuwa nyuma kujibu kwa kusema kuwa ni kweli yeye ni video queen na hata akitaka atokee katika nyimbo yake pia anaweza kutokea.

Chupa lako ukitaka niktokee wewe onana na manejiment yangu tu gharama zangu wala sio ghali,-  Alijibu dogo janja na kutasfiriwa kuwa yupo tayari kufanya hata hivyo katika video ya Nikki wa pili.

Tangu kutokea kwa video hiyo, Dogo Janja amekuwa katika wakati mgumu wa kukutana na maneno ya kshafa sana ilhali muziki ni sanaa ambayo imekuwa na uhuru wa kuwa wabunifi kila siku.

Dogo Janja Awatolea Povu Zito Wanaoiponda Ndoa Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Dogo Janja amewajia juu watu wote ambao bado wanaiponda ndoa yake na Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya.

Ndoa hii imezidi kutengeneza headlines kila kukicha pamoja na kwamba ilifungwa mwaka jana mwishoni na ndio ilikuwa stori ya kufungia mwaka lakini bado mpaka leo hii Ndoa hiyo imebaki kuwa gumzo.

Dogo Janja amedai kuwa amechoshwa na watu wote wanaomsema vibaya kuhusu ndoa yake na Kwenye mahojiano na Enews Dogo Janja amesema nyimbo yake ya Wayu Wayu ni ujumbe kwa wale watu wote wanaomsema vibaya kwa kufunga ndoa na Uwoya.

Walitokea watu walikuwa na kejeli na nini mimi naonekana kidagaa sina chapaa wananitukana nini lakini mwisho wa siku nawakanyaga kama soksi zangu ilikuwa kama sehemu ya kufikisha maudhui kwa watu waendelee kuheshimu mahusiano ya mtu wasiangalie utofauti wowote kwenye mahusiano kinachotakiwa sana ni upendo kama watu mnapendana mnaheshimiana hivi vitu vingine ni vitu vya kawaida”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Dogo Janja alimtolea povu zito Rapa Young Tusso aliyemwambia ameidhalilisha Arusha kwa kuvaa kama mwanamke kwenye video yake ya Wayu Wayu, Dogo Janja amesema hamfahamu Young Tusso na itakuwa vizuri kama ataendelea kuwa shabiki wake.

Nimemzidi Dogo Janja Kila Kitu Labda Yeye Kanizidi Dhambi:- Uwoya

Msanii wa bongo movie nchi irene uwoy amefunguka na kusema kuwa wala hajali watu wanaosema kuwa amemzdi mwanaume aliyemuoa miaka mingapi kwa sababu yeye anachojali zaidi ni mapenzi na wala sio kitu kingine.

Irene Uwoya ameyasema hayo leo alipokuwa katika mahojiano na kipindi cha Leo tena  cha Clouds Radio  alipokwenda yeye na mumewe huyo.Irene anasema kuwa kwake umri ni namba tu kwa sababu  hata kwa hao wanaume wenye kulingana nao umri hawakuweza kumpa kile alichokuwa anakitaka.

Ni kweli nimemzidi  umri na sio umri peke yake hata vitu vingine nimemzidi labda yeye kanizidi dhambi(Akiongea kiutani), Kwangu umri ni namba maana nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na watu ambao wamenizidi umri au tupo sawa lakini sikupata nilichokuwa nakitaka lakini kwa mume wangu nimekipata, 
Toka nimeolewa watu wengi wamekuwa wakisumbua japo hapo mwanzoni walikuwepo lakini kwasasa kuna aina ya watu ndiyo wamekuwa wakisumbua kwa kuhisi sababu Abdul kanioa basi hata wao wanaweza kupata nafasi hiyo

Irene anakiri kuwa katika mahusiano yake yote aliyowahi kuwa nayo, dogo janja ndio mwanaume aliyeweza kumpa kitu ambacho hajawahi kupata kwa mwanaume yoyote na wala sio ela bali ni mapenzi ya dhati.

Sijaolewa na dogo janja kwa sababu ya pesa,kuna vitu vingi ambavyo nimevutiwa kutoka kwake .Kwanza nilipenda mara ya kwanza alivyokuja na kuni-approch.Dogo Janja amenipa kitu ambacho wanaume wote niliokuwa nao walishindwa kunipa.