Shilole Afungukia Anachotamani Kufanya Kabla Ya Mwaka Kuisha

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva na mjasiramali Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa anatamani sana mwaka huu usiishe kabla ya kuhamia Kwenye mjengo wake.

Mwezi uliopita Shilole aliweka wazi mjengo wake wa kifahari anaojenga kwa pesa anayopata Kupitia Muziki anaofanya na biashara zake kama kuuza chakula (Restaurant).

Kwenye moja ya Interview aliyofanya hivi Karibuni na gazeti la Dimba, Shilole, ambaye amekuwa akifanya vyema kupitia biashara yake ya chakula, amesema kikubwa anachofanya kwa sasa ni kuona ndani ya mwaka huu biashara hiyo inamwingizia pesa za kuweza kujenga nyumba yake.

Natamani sana nifikie kile nilichokusudia, nashukuru mpaka sasa naweza kusema biashara yangu inanilinda vya kutosha, nimefanya vingi kupitia chakula”.

Shilole amesisitiza kuwa lengo lake kuu ni kumaliza mwaka huu huku biashara zake zikiwa zimefanikiwa kwa asilimia 90 sambamba na kuhamia kwenye mjengo wake.

Natamani Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Igunga- Shilole

Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kwa Jina la usanii kama Shilole amefunguka na kudai na kuwa anatamani kuwa mkuu wa Wilaya ya Igunga.

Shilole ambaye ni Msanii na mfanyabiashara amedaiwa kutokana na kwamba anakubalika sana katika jamiii anaona kuwa atafaa kuwa kiongozi wa watu wake wa Igunga.

Shilole amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv ambapo ametiririka haya:

Natamani sana siku moja nikawe kiongozi kwetu Igunga nikapate kuweza kuiongoza Wilaya yangu na natamani sana Igunga ikawa jiji tena kwa sababu nimetoka nayo mbali hata kama nisipokuwa Mkuu wa Wilaya nataka kuwa hata diwani”.

Lakini pia Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kwamba sio kiongozi kwa sasa lakini ameshafanya mambo mengi Igunga ikiwemo ameitangaza na kila mtu anapajua Igunga.

 

Mastaa Wanaoficha Watoto Wataumbuka: Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na mfanyabiashara maarufu Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema wasanii wanaoficha watoto watakuja kuumbuka.

Maneno hayo yamesemwa mara baada ya sakata la Msanii Muna Love kutawala vichwa vya habari baada ya kudaiwa kumtelekeza mtoto wake wa kumzaa mwenyewe.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Shilole amesema hakuna siri duniani na wasanii wa kike ambao wamekuwa wakiwaficha watoto wao na kusema hawajawahi kuzaa au walizaa wakafa, ipo siku wataumbuka, pia wanatakiwa kutambua kuwa wanakosa riziki kwa sababu ya kuwaficha malaika hao wa Mungu.

Hakuna siri duniani, ipo siku Mungu atawaumbua wote wanaodanganya kwamba hawana watoto au wamekufa, kuficha malaika hao wanakosa riziki ambazo wangepata kupitia wao, jamani wanawake wenzangu badilikeni, kuwa na mtoto au watoto siyo kashfa ni baraka maana wapo wanaotafuta wanakosa“.

Shilole amekuwa mmoja kati ya wasanii ambao wameweka wazi kukerwa na baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakifanywa na Muna kuanzia msiba wa mtoto wake Patrick mpaka sakata lake la kumkataa mtoto.

Emmanuel Mbasha Amshukia Shilole Baada Ya Kuomba Msaada Kwa Raisi

Msanii wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha amejikuta akimwagia povu zito Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, baada ya kuomba msaada kwa Raisi.

Siku chache zilizopita kuna video clip iliyosambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Shilole akimlilia Raisi Magufuli pesa kwa ajili ya kumsomesha mtoto wake.

Mbasha aliamua kuwatolea uvivu watu wote maarufu wanaomuandama Rais Magufuli kwa kutaka msaada wa mali ile hali wana uwezo kifedha, ikiwemo Shilole ambaye anafanya kazi za sanaa na mjasiriamali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbasha aliandika ujumbe huu:

 Habari za mda huu . Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya watu wanaopenda kutumia vibaya huruma ya raisi wetu, haswa wasanii wa bongo movie. Jamani sera ya raisi wetu ni kila mtu afanye kazi na ndiyo maana slogan yake inasema “HAPA KAZI TU” Ukifanya kazi na kujituma kama sisi mbona maisha ni mazuri tu hapa Tanzania jamani, ila ukipenda mteremko ndiyo inaweza kuku cost ????. Dada yangu Shilole, yaani juzi tu umepost bonge la jumba hapa kila mtu akafurahia na kukupongeza hadi mie nilikupongeza, japokuwa wiki moja kabla ya hapo kuna kijana alikuwa anadai pesa zake za pili pili?.???. Leo nileshangaa kuona clip inasambaa ukilia na kuomba raisi akusaidie kukusomeshea mtoto, sitaki kukupinga ila nakuuliza na kukushauri. Jambo ambalo nakuuliza ni kwamba, Je ! Umesahau kuwa elimu ni bure kuanzia chekechea hadi form four ? Je ! Huyo unaetaka asomeshwe yuko darasa la ngapi dada yangu? Mimi nadhani vitu vingine tungevipima kabla ya kuamua kuchukua hatua. Hebu jiulize, leo raisi akikulipia ada ya mwanao unadhania hawa watoto wa maskini kabisa ambao hawana hata makazi watajisikiaje kama sio kutaka kubebeshana lawama ?

Mimi nadhani wasanii tutumie majina yetu kusaidia jamii isiyojiweza na sio kutafuta mteremko. Kweli marafiki zako wote umeshindwa hata kuwakopa kimya kimya hiyo pesa ya ada kisha uwarejeshee kidogo kidogo pale biashara inapokwenda sawa ? Mimi nadhani hichi ulichokifanya ulistahili kukifanya kwa niaba ya mtu ambaye hana jina wala connection kama zako ili utumie jina lako kumuombea msaada kwa raisi, na siyo mwanamke mpambanaji kama wewe.mie nadhani ungeandika andiko ambalo ungempelekea raisi na ukaomba akudhamini ili upate pesa Bank 400 Ml au Zaidi ukakopeshwa na ukafungua hotel kubwa na pia utakua umetengeneza ajira kwa vijana wenzetu kuliko hilo wazo,Pia kumbuka juzi tu tulikuwa na msiba kule Chato nadhani badala ya kuibuka leo na kutaka msaada angarau ungejitokeza na rambirambi kidogo ili ikuwekee mazingira mazuri ya kuja kukiwakilisha hichi kilio chako hapo baadaye. Haya ni maoni yangu kama Mtanzania huru, sitaki povu hapa jamani. Kamati yangu ya kublock kaeni mkao wa kura.kama unaweza kuzunguka na Ttcl nchi nzima.kajifunze kwa @munalove100 basi”.

Baada ya kusoma ujumbe huo Shilole alijibu kwa maneno machache tu Nakuheshimu sana kaka yangu please tulinde heshima yetu”.

Mobetto, Barnaba na Shilole Wala Shavu Kampeni Ya Be Smart

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Barnaba Boy Classic na Shilole pamoja na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto wamekula Shavu baada ya kuteuliwa mabalozi wa TCRA.

Wasanii hao wameteuliwa na Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) kuwa mabalozi wa kampeni ya Be smart inayojihusisha na kuelimisha vijana kuondokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii mashuleni.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wasanii hao wamefunguka kupata shavu hilo nono Lakini pia nafasi watakayo cheza kama mabalozi:

https://www.instagram.com/p/BnGMZYTlrt8/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=13yt54nc81jzx

Shilole Atoa Asaini Dili Nono na Kampuni Ya TTCL

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amezidi kuomba mafanikio baada ya kusaini Dili jipya na Kampuni ya simu ya TTCL.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole amethibitisha kupata Dili hilo na kuandika:

Asanteni sana TTCL Tanzania kwa kuniamini na kunipa Nafasi hii! Mkataba umeshasainiwa. Asante Kaka yangu Waziri kwa kuniamini pia. Sasa turudi Nyumbani mashabiki zangu. #RudiNyumbaniKumenoga .Wakati ndio huu! @ttcl_corporation“.

https://www.instagram.com/p/Bm0cvIaBpo5/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=la6k12w6e88h

Hili ni dili la pili kwa mwaka huu kwa msanii Shilole kusaini, mwezi uliopita alisaini dili la ubalozi na British Council ambalo mwenyewe alidai kuwa ni dili nono.

Shilole Awasihi Uwoya na Wema Wafuate Nyayo Zake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na mfanyabiashara Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewapa somo wasanii wenzake Wema Sepetu na Irene Uwoya.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Shilole amewataka mastaa hao wa kike kuacha maisha ya kuigiza mitandaoni ambapo wanaonekana wamependeza kwa kuvaa nywele zenye thamani ya shilingi milioni moja na zaidi huku wakiwa hawajafanya la maana litakalowasaidia maishani.

Nawasihi wasanii wenzangu wote siyo Wema na Uwoya tu, wapambane na waithamini shilingi mia moja maana unakuta mtu ananunua nywele za shilingi milioni moja na hana hata kiwanja hebu jiulize hapo angenunua mifuko ya simenti angepata mingapi, jamani wasanii wenzangu jitahidini kufanya mambo yatakayowasaidia katika maisha ya mbeleni.

Inashangaza sana kuona msanii anafariki msiba unaenda kufanyika kwa shangazi yake kwa sababu kuna nyumba nzuri, kwa nini tusijikwamue sasa hivi angali tuna nguvu ili baadaye tuwe na cha kujivunia jamani, inabidi tubadilike zama za kujianika mitandaoni na nywele za mamilioni zimepitwa na wakati”.

Lakini pia Shilole alitoa siri ya mafanikio yake iliyomuwezesha kujenga mjengo huo wa thamani:

Hii nyumba nimejenga kwa fedha nyingi ambazo mpaka sasa sijui jumla ni gharama kiasi gani maana sijajumlisha na fedha hizo nilikuwa kila nikipata hela kidogo nanunua simenti au mchanga na vifaa vingine hivyo mpaka nikae chini niangalie risiti nianze kuzijumlisha”.

 

Nuh Mziwanda Adai Na Yeye Alichangia Kununua Mjengo Wa Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nuh Mziwanda ameibuka kuwa ana yeye pia aliweka mkono Kwenye kununua Mjengo mpya wa Shilole aliouanika Kwenye mitandao ya kijamii.

Ikiwa ni siku chache zimepita tangibly shilole aanikr Mjengo wenye thamani ya zaidi milioni 90 anaoujenga hivi sasa, aliyekuwa mpenzi wake Nuh Mziwanda amedai na yeye pia ana chake Kwenye Mjengo huo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv, Mziwanda amedai pamoja na kwamba alishiriki kununua Mjengo huo wakati wa Mahusiano yao lakini amesem hawezi akaomba arudishiwe pesa sababu hawapo wote:

Ni kweli ule mjengo tulinunua wote Wakati tupo pamoja, nakumbuka tulikuwa na hela tukaenda mpaka kule tukamalizana na yule jamaa yaani mishe mishe zote tulikuwa wote tunanunua nyumba na kukamilisha kila kitu”.

Lakini pia Mziwanda amedai hawezi kumdai SHilole Pesa zake alizochangia Kwenye ule mjengo sababu yeye ni mwanaume:

Hapana siwezi kwa sababu yule mtoto wa kike ujue alafu mimi nilikuwa mwanaume kama Baba sasa nikianza kudai nilichangia hiki na kile inakuwa haileti picha nzuri yule ni mtoto wa kike muache atunzwe”.

Baada ya kuweka wazi mjengo wake Shilole aliweka wazi amejenga nyumba ile kwa nguvu zake bil msaada wa mwanaume yoyote na kusema ile sio nyumba ya mume wake Uchebe bali amejenga kwa ajili ya watoto wake.

Shilole Aanika Mjengo Wake Wa Thamani

Staa wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameweka wazi Mjengo wa thamani ambao anajenga hivi sasa kwa kipato cha muziki na kuuza chakula.

Shilole ni msanii ambaye ametoka mbali kimaisha kwani alianza harakati za kutafuta riziki kupitia kuigiza Bongo Movie mpaka Bongo fleva na sasa anamiliki mgahawa wake wa chakula.

Lakini pamoja na kuanza harakati za maisha kama mama ntilie wa watoto wawili lakini leo hii Shilole ameanika mjengo wake mpya Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika:

https://www.instagram.com/p/BmsSdHzBON3/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=9a8zoul98xo

“Shilole Angetaka Kiki Angeenda Beach na Uchebe Wake na Kuvua Nguo Zote”-Nay Wa Mitego

Msanii wa MuzikiSana wa Bongo fleva Nay wa Mitego amemjia juu Msanii mwenzake Shilole baada ya kuingilia kati sakata la Muna na kumrushia maneno katika Interview mbali mbali.

Nay ameibuka na kumkingia kifua Muna na kumtolea povu Shilole na kudai anatafuta kiki Kupitia ishu ya Muna na hana lolote kingine linalomsumbua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nay wa Mitego alimuandikia ujumbe huu Shilole:

Shiloleeee Zainabuuu nadhani ulimiss tu Media dada yangu nadhani umefanikiwa kwa kiasi chake. Ulichokosea ni ishu uliyoingilia yaani gear  yako. Sioni alichokosea huyo unayemuita mdogo wako Muna ameongea mengi ambayo watu walitaka kujua nini kilichokuwa kinamsumbua Patrick.

Sasa ungetaka kiki mngeenda Beach na Uchebe wako mnavuana nguo zote alafu mbapiga picha halafu mnaposti bila hata caption halafu mtaona kiki yake ingekuwa noma.Lakini hili la Muna umejichoresha tu umeonekana ulikuwa unatafuta…..Mtazamo wangu tu”.

Sakata kati ya Muna na Shilole lilianza baada ya Muna kufanya Interview na kuweka wazi kuwa Casto ndiye Baba halali wa marehemu mtoto wake Patrick na mambo mengine ambayo yalionekana kutompendeza Shilole.

Kitabu Cha Mapenzi Cha Shilole ‘Broken Heart’ Chazua Gumzo

Msanii maarufu wa Muziki na mjasiriamali Shilole a.k.a Shishi Baby ametangaza ujio wa Kitabu chake kiitwacho Broken Heart alichoandika na mwandishi chipukizi Jackson Fute.

Shilole akiwa na Mwandishi wa Kitabu, Jackson Fute

Taarifa ya Kitabu hicho alizianika Instagram alipoweka picha za yeye na mwandishi huyo wakiwa na mameneja wao Mc Carter na Viola Julius wakisaini mkataba wa makubaliano.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole pia aliandika:

Kabla ya kitabu hakijatoka tunaweka mambo sawa. Kisheria zaidi leo nimemalizana na na Jackson Fute kuhusiana na Kitabu Chetu cha Broken Heart”.

Kitabu hicho kimezua maswali mengi sana kwani mpaka hivi sasa hakuna anayejua nani hasa ataandikwa Kwenye Kitabu hicho cha mapenzi kama atakuwa Nuh Mziwanda au Uchebe.

Lakini pia Shilole ameweka wazi kuwa Kitabu hicho kitatoka siku yoyote kuanzia sasa kwani uandishi wa Kitabu umekwisha kamilika.

Usiri wa kilichoandikwa ndani ya Kitabu hicho ndio kinatupa hamu ya kutaka kujua na kukisoma, tusubiri taarifa zaidi ya uzinduzi wa Kitabu hicho.

Shilole- Siwezi Kuwacheza Watoto Wangu

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kwa jina la usanii kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi kuwacheza watoto wake.

Shilole ambaye ni mama wa watoto wawili wa kike ambao alizaa na mwanaume ambaye alifariki wiki chache zilizopita, amekataa kuwacheza intangibles watoto hao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha  Break cha Clouds TV Shilole amesema kuwa ingawa katika kabila lao (Wanyamwezi) wana utamaduni huo hawezi kuruhusu kwa wanae.

Siwezi, sasa hivi hatuna watu wakubwa ambao wapo, sinaunajua zinakuwaga kama familia. Lakini zamani mambo hayo ndio yalikuwepo tofauti na sasa”.

 

Ndoa Haijazima Muziki Wangu- Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa ndoa yake haijaweza kuzima  hata kidogo muziki wake.

Shilole alifunga ndoa ya siri na mume wake Asharaf Uchebe mwaka jana mwishoni lakini tangu hapo hajasikika Tena akiwa na Wimbo Mpya ambapo imedaiwa ndoa imembana kufanya Muziki Tena.

Kwenye mahojiano aliyofanya na vyombo vya habari Kwenye shoo ya Davido mwishoni mwa wiki iliyopita, Shilole amesema amebanwa tu na biashara  nyingine nje ya muziki lakini sio ndoa yake:

Sio kweli, mimi ningekuwa nimepungua kwenye game usingenifanyia interview sasa hivi. Sio kweli nina kazi nyingi za kuniingizia fedha kuliko muziki”.

Wimbo wa mwisho wa Shilole kutoa unaitwa Kigori ambao ulitoka August 07, 2017 ambao ulikuwa ni Miezi kadhaa kabla ya ndoa yake.

Shilole ameweka wazi kinachombana ni biashara zakke nyingine ambazo ni mgahawa wake wa Shishi Food na pia anamiliki chili yake na hivi karibuni anakuja na kitabu chake.

 

Shilole Kugombea Ubunge

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amedaiwa kuwa mbioni kugombea ubunge miaka ya baadae.

Taarifa hiyo imesemwa na msanii wa muziki Bongo fleva  Mr Kesho ambaye amemshirikisha Shilole kwenye wimbo wake mpya ‘Nakudata’, ameweka wazi kuwa mrembo huyo anamipango ya kuwania uongozi kupitia siasa kuongoza wananchi.

Mr Kesho amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Bongo 5 ambapo amedai kuwa Shilole sio msanii wa kufanya Muziki maisha yote bali ana mipango mwingine ya kuwa kiongozi:

Kusema ukweli sidhani kama Shilole anaweza kufanya Muziki mpaka miaka mitano mbele mimi nanavyoona ni kama ana ndoto sana za kuwa kiongozi Tena kiongozi wa siasa akaongoza wananchi naweza sema 2020 tunaweza tukamuona Bungeni na mimi namuombea afike huko maana ni mtu Powa sana na ana uthubutu”.

Miaka ya hivi karibuni limekuwa jambo la kawaida kwa wasanii na mastaa mbali mbali kupenda kuingia kwenye mambo ya siasa kwani tumeshawaona wasanii wawili ambao wameshafanikiwa kuingia bungeni ambao ni Mr. Sugu na Profesa Jay Lakini Shilole hajathibitisha taarifa hizi rasmi.

Shilole Amwaga Machozi Baada Ya Kupewa Tuzo na Aunty Ezekiel

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amejikuta akibubujikwa na machozi baada ya kupewa tuzo ya Mama bora na staa wa Bongo movie Aunty Ezekiel siku chache zilizopita.

Kwenye mahojiano na Showbiz, Aunty alisema ameamua kumpatia zawadi hiyo siku ambayo alikuwa akizindua filamu yake ya Mama kutokana na Shilole kuwa ni mama bora ambaye siku zote amekuwa akitafuta pesa kwa shida ili wanaye wasome vizuri.

Kwenye siku hii muhimu nikaona itakuwa sio jambo baya kama mimi na timu yangu nzima nikamzawadia huyu mtu (Shilole), sijui niseme tuzo ya mama bora au zawadi ya mama bora, kwasababu kwa upande wangu yeye ni mama bora, ni mtu ambaye anatafuta sana, anafanya kazi kwa shida sana ili watoto wake wasome kwenye shule za gharama na mtu huyo ni Shilole”.

Baada ya kupewa tuzo hiyo ya heshima ya mama Shilole alifunguka kuwa ni jambo jema na la heshima kwa mtu kumtambua kama mama bora:

Nilikuwa shocked kuona Aunty Ezekiel kanichagua kuwa mama bora, nililia kwa furaha kuona pia msanii mwenzangu ameweza kunitunuku, namshukuru sana, na hii imenipa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa nguvu zangu zote”:

Shilole ni moja kati ya Wanawake watafutaji sana kwani amewalea watoto wake watatu mwenyewe kwa biashara zake kuanzia muziki mpaka kuuza mama ntiliye.

Snura Afungukia Bifu lake na Shilole

Mwanamuziki wa Bongo fleva Snura Mushi Majanga amefunguka kuhusu uwezo wa bifu lake na msanii mwenzake wa Bongo fleva Shilole.

Kwa muda mrefu kumekuwa na habari za kuwepo kwa bifu kati ya Shilole na Snura huku siku za nyuma wasanii hao walionekana wakibishana na hata kurushiana maneno.

Lakini Snura amedai hivi sasa hakuna bifu kati yake na Shilole kwani mambo yaliyotokea siku za nyuma yameachwa huko na hivi sasa wameendeleea mbele

Snura alifunguka hayo Kwenye mahojiano na Bongo 5, ambapo amedai hata tuzo yake aliyopewa na Aunty Ezekiel yeye ndio alimpokelea na akampelekea.

Sina beef hadi juzi kwa Aunt mimi sindonimempokelea zawadi, yeah, hatuna bifu na nimempelekea”.

Snura kwa sasa anatamba na ngoma ‘Vumbi la Mguu’ baada ya kufunika na Zungusha ambayo alimshirikisha Christian Bella.