Mwana Fa Awaombea Msamaha Wasafi

Hamisi Mwinjuma maarufu kama Mwana FA ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), leo amefika katika ofisi za Baraza hilo kuwaombea msamaha WCB.

Juzi, Basata waliwalima WCB adhabu ya Sh. Milioni 9 kutokana na wimbo wa ‘Mwanza’ uliofanywa na Ray Vanny akimshirikisha Diamond Platinumz. Pamoja na adhabu hiyo, Basata waliufungia wimbo huo kutopigwa kwenye vituo vya runinga na redio. Pia, iliwataka WCB kuuondoa wimbo huo kwenye YouTube na kutoutumia katika matamasha yoyote.

Akizungumza muda mfupi baada ya kumaliza kikao na watendaji wa Baraza hilo, Mwana FA amesema kuwa amewaombea msamaha WCB na kwamba anaamini adhabu hiyo itapunguzwa, ingawa sharti la kwanza ni kwa uongozi wa lebo hiyo ya muziki kuandika barua ya kuomba radhi.

Mimi nilichofanya ni kuwaomba watendaji wa Baraza, kuona hii adhabu tunaweza kufanya nayo nini isiwaumize. Pengine kuna makosa labda yamefanyika lakini tuone namna ambavyo tutawaadhibu bila kuwaumiza,” alisema FA.“Watendaji wamenielewa na wamesema kwamba uongozi wa Wasafi na wasanii wao wanatakiwa kuandika barua kuomba radhi na kupunguziwa adhabu. Na ninaamini adhabu haitakuwa kama ambavyo imetolewa jana,” aliongeza.

Msanii huyo ambaye ni miongoni mwa wasanii wawili pekee wanaounda Bodi ya Wakurugenzi ya Basata, alisisitiza kuwa alienda kuwaombea msamaha wasanii hao kama mtu binafsi na msanii lakini sio kama mjumbe wa Bodi.

Alisema kuwa Watendaji wa Baraza wana mamlaka ya kutoa adhabu hiyo bila kuingiliwa na mtu yeyote na kwamba suala hilo lingeifikia Bodi endapo tu wasanii walioadhibiwa wangeamua kukata rufaa

Diamond Awaomba BASATA Waruhusu Wimbo Wao Upigwe Muda Wa Usiku Watoto Wakiwa Wamelala

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameibuka na kuliangukia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liruhusu japo wimbo wao na Rayvanny upigwe usiku watoto wakiwa wamelala.

Siku ya jana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kutokana na maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo hiyo.

Diamond ameibuka na kulalamikia uamuzi huo wa BASATA na kuwaomba wafikirie na kutafuta njia ya kuiacha nyimbo hiyo kuendelea kupigwa kwenye kumbi za starehe na ipigwe mida ya usiku watoto wakiwa wamelala Lakini pia ameomba wimbo huo urudishwe kwenye mtandao wa YouTube.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqHLwGaFvfE/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1j577yw2ugopk

https://www.instagram.com/p/BqHM7WhlEou/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=retbexv8i8mf

 

Rayvanny Afunguka Baada Ya Wimbo Wake na Diamond Kufungiwa na BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny amefunguka kwa Mara ya kwanza tangu wimbo wake wa ‘Mwanza’ aliomshirikisha Diamond Platnumz kufungiwa.

Siku ya jana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kutokana na maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo hiyo.

Rayvanny ameibuka na kulalamikia uamuzi huo wa BASATA na kusisitiza kuwa haikuwa maana yao kuimba matusi katika wimbo huo Bali ni Sanaa iliyotumika na kupelekea watu mawazo yao kufika huko.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqG9rwonTtl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=mo32cxhbwmsv

https://www.instagram.com/p/BqG-WAGHFKG/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=109chbj8a1coh

Queen Darleen Ajibu Tetesi Za Mama Yake Kufungwa China Kisa Madawa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na First Lady wa WCB Mwanahawa Abdul maarufu kama Queen Darlene amefunguka na kukana tetesi za mama yake kuwa kifungoni nchini China.

Miezi michache iliyopita kuna tetesi zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mama yake Mzazi na Queen Darlene amekamatwa nchini China Baada ya kukutwa na madawa ya kulevya na hivyo yupo jela akisota.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers juu ya ishu hiyo, Darleeen aliweka wazi kuwa, aliposikia hata yeye alishtuka na kwamba ni uvumi tu kwani mama’ke yupo hapa nchini na hapendi mambo ya mitandao.

Mama yangu kafungwa China? Niliposikia nilishangaa sana kwani mama yangu yupo na mtu akitaka anione nimpeleke nyumbani”.

Licha ya Queen Darlene kuwa na mama tofauti na msanii mwenzake na kaka yake Diamond Platnumz lakini Wana baba mmoja ambaye ni Mzee Abdul Juma.

Babu Tale Aweka Wazi Hali Ya Kiafya Ya Hawa Kwa Sasa

Meneja wa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Babu Tale ameweka wazi kuwa Mwanadada Hawa Saidi ambaye alikuwa anatibiwa nchini India anaendelea vizuri.

Hawa alikuwa na tatizo la ini ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini na Babu Tale ndio alipewa jukumu la kusimamia matibabu yake nchini India kwa kuwa gharama zote za matibabu alizitoa Diamond Platnumz.

Hawa alikuwa na tatizo la ini ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini na Babu Tale ndio alipewa jukumu la kusimamia matibabu yake nchini India kwa kuwa gharama zote za matibabu alizitoa Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Babu Tale amesema wazi kabisa kwa sasa Hali ya Hawa inaridhisha kabisa tofauti na siku chache zilizopita kabla ya kupata matibabu:

Diamond aliweka wazi kuwa ametumia zaidi ya milioni 490 kumtibia Hawa ambaye miezi michache iliyopita alikuwa hoi kitandani nchini Tanzania.

Jaquar Amtolea Povu Zito Harmonize

Msanii Jaquar kutoka  Kenya ameibuka na kumtolea Povu Zito msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize Baada ya kushindwa kupiga shoo nchini humo.

Wikiendi iliyopita Harmonize alitakiwa kufanya shoo mjini El Doret nchini Kenya lakini alihairisha kufanya shoo hiyo Baada promota kushindwa kumlipa pesa waliyohaidiana.

Kitendo cha Harmonize kushindwa kupiga shoo kiliwauzi mashabiki wengi ikiwemo Mbunge wa jimbo la Starehe Jaquar ambaye kwenye mahojiano na Kipindi cha Mambo mseto alifunguka:

“Ni tukio la kuhuzunisha lakini mimi NAMSHTUMU sana Harmonize….wakenya wamemsupport sana, wamesupport wasanii wa nje sana. Wengine wanatumia pesa zao kupiga simu, kurequest nyimbo zao. Mimi mwenyewe siwezi nikakosa kupanda stage sababu ya balance ambayo promoter amebakisha na ni kitu nilikuwa nafanya. Kwanza nadeal na mafans wangu.

Kama Mimi ningekuwa Harmonize Saturday ningeenda kwa stage niambie watu samahani nimechelewa lakini kwa sababu mumenifikisha mahali nimefika saa hii mimi nitaperform lakini promoter hajanilipa…vitu zingine nitadeal nazo baadaye sababu bila nyinyi nisingekuwa Harmonize pale niko. Unapata kuna fans wametoka mbali hadi Eldoret kwa sababu yake. Sometimes unafaa kuanglia mafans Kwanza”.

 

Babu Tale-Tumeshaanza Kuwasiliana na Uongozi Wa Ali Kiba

Meneja wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi mipango yao ya kumpata msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Siku ya Jana kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz aliweka wazi mipango yao  ya kumpata Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye shoo yao.

Lakini sasa Meneja wa Diamond Babu Tale anafunguka kuhusu jitihada zao za kuwasiliana na Kiba ambapo amekiri kuwa hana mawasiliano na Kiba lakini anaelewana sana na meneja wake anayeitwa Seven.

Siongeagi na Alikiba kivile, mimi naongeaga na meneja wake maana alishawahi kunisaidia sana, lakini kuhusu inshu ya Wasafi Festival Sallam ameshaanza kuwasiliana na uongozi wa Alikiba”.

Baby Tale ameweka wazi kuwa siku ya uzinduzi wa Wasafi festival pamoja na wasafi fm mbali ya kuwepo kwa mipango ya kumpata Ali Kiba lakini pjs atakuwepo msanii Konki konki konki master Dudu baya katika tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Wasafi media.

Mwarabu Fighter Afunguka na Kueleza Alivyoteseka Kufanya Kazi Kwa Diamond

Bodyguard aliyejizolea umaarufu Bongo baada ya kufanya kazi kwa staa wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika magumu aliyopitia kufanya kazi kwa Diamond.

Katika mahojiano aliyofanya na mtandao wa Bongo 5, Mwarabu Fighter amefunguka na kuanika mazingira magumu aliyopitia wakati anafanya kazi kwa staa huyo:

Nilikuwa nakatwa mshahara nikichelewa kwenye tukio siku unaenda kupokea mshahara unakuta hata laki na nusu hakuna halafu unakutana na kijikaratasi kikieleza na kukupa ufafanuzi kuwa siku fulani ulichelewa pia unakumbuka siku fulani?”.

Lakini pia Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa kuna baadhi ya siku za mapumziko alizokuwa anatakiwa apumzike nyumbani alikuwa anapigiwa simu aende kazini na kupewa dakika  kumi au kumi na tano.

Mwarabu Fighter ameweka wazi kuwa wakati anafanya kazi kwa Diamond aliishia kupata ajali ya pikipiki mara nne katika harakati za kuwahi kazini.

Babu Tale Aweka Wazi Hali Ya Hawa Baada Ya Upasuaji Wa Moyo

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale ambaye yupo nchini India kwa ajili ya kusimamia matibabu ya Msanii wa Hawa Said ameweka wazi kua anaendelea vyema baada ya upasuaji.

Hawa amefanyiwa upasuaji wa moyo chini ya madaktaru bingwa watano na sasa Babu Tale anasema Mrembo huyo amepata fahamu baada ya kufanyiwa upasuaji huo mkubwa.

Baada ya opersheni hiyo kufanyika Babu Tale ameandika:

 

Babu Tale Afungukia Matibabu Ya Hawa Nchini India na Ugonjwa Unaomsumbua

Meneja wa Msanii mkubwa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kutaja ugonjwa unaomsumbua Msama Hawa na kudai sio ini kama ilivyoaminika hapo Mwanzoni.

Wiki iliyopita Babu Tale aliondoka na Hawa kwa ajili ya kwenda kufanyiwa matibabu nchini India baada ya Diamond kujitolea msaada wa zaidi ya Milioni 450 kwa ajili ya matibabu yake.

Babu Tale ametoa taarifa kuwa  Hawa atafanyiwa upasuaji wa moyo jioni ya leo Lakini pia Wataalamu wameangalia kila kitu na hawajaona tatizo kwenye Ini kama iliyokuwa inaripotiwa awali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Babu Tale ameandika:

Asante Mungu tumefika salama India na tumefanya vipimo vyote upya salama na jibu lililotoka kwa wataalamu kwa asilimia 95% awajaona tatizo linalohusiana na ini kwa mgonjwa ila ni moyo ndio uliokua unapelekea mgonjwa kujaa maji mwilini ivyo basi kutaitajika kufanyika upasuaji mkubwa ambao utakua na uangalizi mkubwa wa wataamu then wametuakikishia baada ya hapo mgonjwa atapata nafuu na inawezekana izo 5% zilizobaki itakua poa na tatizo la ini alitokuwepo kikubwa tunaomba mtuombee dua na msiache kumuombea pia @diamondplatnumz apatenguvu ya kuendela kumsaidia kwa maana kutoa ni moyo. Kikubwa sana naomba tumuombee Hawa coz anaingia kwenye upasuaji mkubwa na hii ni atua ya yeye kua salama. Mungu tusimamie”.

 

Mavoko- Sina Tatizo na WCB, Niko Tayari Kupiga Nao Kazi

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Richard Martini maarufu kama Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo kabisa na uongozi wake wa zamani WCB.

Miezi michache iliyopita Rich Mavoko alitangaza Rasmi kujiengua Kwenye Label ya WCB alipokuwepo kwa miaka kadhaa kutokana na matatizo ya Kimkataba.

Leo hii Rich Mavoko yupo chini ya uongozi mpya ambao hajauweka wazi Lakini pia ameachia nyimbo zake kadhaa kama Ndegele, Hongera, Naogopa na Navumilia.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kuondoka WCB lakini hana tatizo nao:

Unajua watu wengi wanashindwa kuelewa, sikuondoka WCB kwa ugomvi kule hata kidogo ni mambo tu ya kawaida ya kimuziki lakini sina tatizo na yeyote yule”.

Lakini pia Mavoko ameweka wazi kuwa kama itatokea WCB watakuwa tayari kufanya naye kazi hivi sasa basi yeye hana tatizo:

Sina tatizo kabisa, tutakaa chini na kuzungumza si ni biashara tu?”.

 

Aikah Afunguka Kuhamia WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Kutoka katika kundi la Navy Kenzo Aikah Marealle amefunguka na kuongolea taarifa za kuhamia WCB.

Baada ya kutoa hit single ambayo inaendelea kufanya vyema mpaka sasa ‘Katika’ waliomshirikisha Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuliibuka tetesi kuwa Nahreel na Aika wamehamia chini ya WCB.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers , Aika  amesema kuwa, amekuwa akisikia kwa watu wengi juu ya kuhamia WCB mara baada ya kuachia wimbo wao  na Diamond jambo ambalo halina ukweli.

Yaani watu wengi wanasema nimehamia WCB lakini ukweli ni kwamba tuna meneja anayetokea huko anaitwa Sallam na amekuwa akitusimamia sasa sijui hayo mengine yanatokea wapi.

Nilikaa na mwenzangu tukatunga Wimbo wa Katika tukaona ni vizuri tukamshirikisha Diamond ndiyo ikawa hivyo sasa nashangaa hao wanaoungaunga maneno”.

Tetesi hizo za Kuhamia WCB zilipamba moto mara baada ya Msanii kutoka WCB Harmonize kusema wazi kuwa wasanii hao wanahamia Kwenye Label yao taarifa ambazo Navykenzo walidai ulikuwa ni utani.

Diamond Amkabidhi Mpiga Picha Wake Gari Jipyaa

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemfanyia bonge la surprise mpiga picha wake anayejulikana kama Lukamba baada ya kumkabudhi gari jipya.

Diamond amempa gari aina ya Toyota Alteza Lukamba siku ya Ijumaa iliyopita alipoenda kutoa msaada Tandale, ambapo Diamond alifunguka:

Lukamba anakaa Bunju, kuna kipindi alikabwa na kuchukuliwa hadi laptop sasa leo nampatia gari,”

Baada ya kukabidhiwa gari hilo, Lukamba alimuandikia Diamond ujumbe huu Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Hadi Sasa Nimekosa Maneno Ya Kuandika Yatakayoweza Kubeba Hisia Zangu Za Furaha Niliyonayo,Nimekuwa Nikiandika Na Kufuta Kila Neno Ninaloandika Naona Halijitoshelezi Nahisi Halina Uzito Kuelezea Kilichopo Moyoni Mwangu….. Bro @diamondplatnumz umekuwa msaada sana kwa Sisi vijana maskini wenzako, Mungu azidi kukupa moyo wa kidogo unachopata kugawana na wenzako, pia nishkuru uongozi wa @wcb_wasafikwa kudhamini kidogo changu hii imenipa moyo sana wa kuzidi kujituma zaidi na zaidi
God bless you simbaaa ????????????@diamondplatnumz”.

 

Rich Mavoko Afungukia Bifu Lake na WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake na Label yake ya zamani ya WCB.

Rich Mavoko ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba ameondoka katika Label hiyo lakini hana tatizo lolote na CEO wa Label hiyo Diamond Platnumz.

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Rich amesema kuwa kilichotokea mpaka akaondoka Kwenye Label hiyo sio ugomvi bali muda wa kufanya Biashara ulifikia kikomo hivyo sasa wapo vizuri.

Lakini pia Rich Mavoko amemtaka meneja wa WCB Sallam SK kuwa na busara na heshima ni baada ya Meneja huyo kusema Mavoko hajarudisha hata robo ya pesa waliyowekeza kwake na kumtengeneza kama Brand:

Unajua Kwenye masuala ya kumzungumzia Rich Mavoko unazungumzia Brand ambayo ilikuwepo kwaiyo uliichukua kwa nia ya kufanya nayo biashara sasa umesema hajarudisha sasa na huyo mwenye talent atakuwa amepata?”.

Mavoko aliendelea kutiririka na kumwaga povu zito:

Mimi sitaki kuongelea sana hivi vitu kwa undani kila mtu anatakiwa kuheshimu kitu cha mwenzake ndio tuanze kuongeleana na kuongeleana vitu vibaya ni kutafuta mtu kujitetea”.

Diamond Athibitisha Nafasi ya Mavoko Kupata Mrithi.

Ikiwa ni baada ya kupelekana BASATA, ndipo mkataba wa msanii Rich mavoko ulipofutwa katika lebel ya wasafi, msanii wa lebel hiyo ambae pia ni bosi katika kundi hilo Diamond Platinumz amethibitisha kuwa  kuna mpnago wa kusajiri msanii mwingine katika lebo hiyo ili kuziba pengo aliloliacha Rich mavoko.

Rich mavoko ambae alikuwa msanii katika kundi hilo ameondoka katika kundi  hilo huku akitoa tuhuma nzito kuhusu lebo hiyo kuwa wamekuwa wakinyonya wasanii na kwamba hakuna haki katika lebo hiyo na hata mikataba yao imkuwa ya unyonyaji.

Mbali na maneno ya Rich wasanii wnegine kutoka katika lebo hiyo walikataa skendo hiyo na hata ukiangalia wasanii wengi nje ya wasafi wamekuwa waktamani kuingia katikalebo hiyo kutokana na masiha wanayoishi wasanii hao katika umoja huo.

Wasanii Wanaofanya Vizuri Tanzania Wanatoka WCB- Babu Tale

Meneja wa staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi kuwa wasanii wote wanaofanya vizuri Kwenye gemu kwa sasa wanatoka WCB.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Babu Tale amedai hata watu wanune au waumie lakini ni ukweli usiopingika kuwa WCB ndio Label yenye wasanii wakali kwa sasa:

Wasanii wetu wote wanafanya vizuri,” alisema Babu Tale. “Wasanii wanaofanya vizuri nchini Tanzania kwa kipindi hichi wanatoka Wasafi iko wazi ukinuna ukiumia wasanii wanaofanya vizuri kwa kipindi hiki Wanatoka Wasafi”.

Babu Tale amepingana na vikali na baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakisemwa kuhusu mikataba ya WCB ambapo mapema wiki hii Mkurugenzi wa vipindi EFM, Sebo aliishauri kampuni hiyo kupitia upya mikataba ya wasanii wao kwani kitu ambacho kimetoka kwa msanii Rich Mavoko kwenda kulalamika BASATA hakikuleta picha nzuri kwa taasisi kubwa kama WCB.

Babu Tale amesisitiza kuwa Mikataba ya WCB ipo vizuri na wasanii wake wanaridhika na wanafanya kazi nzuri na ndio maaana wanatoa wasanii wakali na kazi zenye ubora:

Hatuna mpango wa kupitia mikataba wa wasanii wa WCB, mikataba ya wasanii wetu wote haina matatizo, kama unavyoona wasanii wetu wote wanafanya vizuri“.