Wema Sepetu Ajuta Kuchora Tatoo

Msanii wa bongo movie ambae haishi kusema kwenye mitandao kila siku  Madame Sema sepetu amefunguka na kusema kuwa katika vitu anavyochukia katika mwili wake ni tatoo kubwa aliwahi kuichora maeneo ya shingoni.

Wema Sepetu  anasema kuwa hiyo ni moja ya tatoo zake za mwanzo kabisa alizowahi kuchora na wakati anachora hakuwa anafikiria kitu sana lakini tatoo hiyo iliyopo shingoni ni kubwa kuliko na imekuwa ikimkera sana kwa sasa.Hata huvyo Wema anasema kuwa tatoo iyo ambayo imetapakaa shingoni  waktai anachora alimwambia mchoraji  achore na iyonekane shingoni hivyo mchoraji aliamua kuchora umbo kama la mjusi anatamani kuifuta lakini anaogopa maana anaambiwa kufuta tatoo  kunasababisha maumivu sana.

“Natamani sana kuifuta tatoo hii ila nasikia vibaya na pia niliambiwa kufuta tatoo inaumwa sana, lakini ingekuwa uwezo wangu wala hata isingekuwepo mpaka sasa” alisema Wema Sepetu

Ukiachana na tatoo iliyopo shingoni ambayo madame wema sepetu anataka kuifuta, wema ni mmoja wa watu wenye tatoo nyingi sana katika mwili wake na zimekuwa zikiongezeka kila leo.

Watu wengi sana wamezua tabia   ya kuchora michoro ya tatoo mwilini , baadhi yao uchora michoro ya  tatoo za majina ya watu wao wa karibu au watu wanaowapenda. Ingawa pia inaweza kuleta  shida  pale wale watu wanaowapenda wanapokuwa wamegombana nao  au kuitilafiana wengi ujikuta wakiangaika kuziondoa na kuishia kuchora michoro ya maua au michoro isiyo eleweka.

Ikiwa ni kama moja ya urembo mwilini tatoo inaweza kuchora ya muda mfupi kulingana na mahitaji yako, inasemekana kuwa kuchora tatoo ya moja kwa moja kwenye ngozi uweza kusababisha kansa ya ngozi, hivyo kwa urembo wanaohitaji wanapaswa kufikiria njia mbadala zaidi ya hiyo, lakini pia inakuwa shida  pale unapotaka kuiondoa.

Team-Wema Wakiri Kumchoka Wema Sepetu

Mashabiki wanaojitolea kum-support  wema sepetu wamekuja juu na kumtupilia mbali msanii huyo, Wema ni mwanadada wa bongo movies ambae  ana mashabiki wengi sana katika mitandao ya kijamii uhusani instagram, wakiandika katika ukurasa  wa instagram moja ya viongozi wa team hiyo anaijiita wemaselfies, amefunguka na kusema kuwa wamechoka tabia za madame wao.

Mashabiki hao wamelalalmika na kusema kuwa kwa muda mrefu sana Wema amekuwa kimya hana kazi yoyote mjini, hatoi hata movie yoyote kila siku kuahidi lakini hakuna kinachokamilika, wakatolea mfano wa movie mojawapo ambayo Wema Sepetu aliitangaza kwa muda mrefu aliomshirikisha Van Vicker lakini mpaka leo movie hiyo haijatoka na mashabiki wakiwa wamekaa wanaihusibiri.

Hata hivyo team hiyo inalalamika na kusema kuwa kwa muda  Wema amekuwa akifanya mambo ya aibu lakini wamekuwa wakimsapoti sana wala hawalipwi chochote zaidi ya mapenzi kwa msanii huyo lakini kitu cha kushangaza ni kwamba wanapofanya jukumu la kumwambia wanaishia kugombana na msanii huyo.

Wakimtolea mfano na kumfananisha na Huddah the boss kutoka Uganda, team hiyo inasema kuwa Wema amekuwa mtu wa kuanzisha biashara lakini zinakuwa zinakufa kwa mfano wa biashara yake ya lipstick haijulikani mpaka leo iko wapi wakati watu kama  Huddah wameanza hivi juzijuzi lakini sasa hivi wako mbali na biashara zao.

Mashabiki wa Wema wamekuwa watu wa kukata tamaa kutokana na tabia ya Wema kuendelea kujipendekeza kwa Wasafi na boss wao Diamond wakati mapenzi yao yalishaisha siku nyigi ingawa yeye mwenyewe anasema kuwa hana kinyongo na Diamond, kitu ambacho Team wema wanatafsiri ni kama kumbembeleza Diamond na familia yake, wakamtolea mfano na mwanadada Penny ambae pia alikuwa ni mpenzi wa Diamond lakina alipoachana nae aliamua kufunga milango yote ya mawasiliano na kuwa karibu na msanii huyo.

Haya yote yatakuwa yamesababishwa na tabia ya msanii huyo kuwa anafanya mambo ya aibu huku team zake wakimtetea huku wakijua kuwa mambo mengine sio sahihi kwa msanii wao kuyafanya, hivi karibuni kuna baadhi ya picha zilizosambaa kwa zaidi ya awamu mbili tofauti zilionyesha picha za Wema akiwa faragha na mwanaume.Lakini pia kumekuwa na tetesi kuwa mwanadada huyo kuwa bado na mahusiano na msanii Diamond ingawa yeye mwenyewe alikanusha tetesi hizo.

 

 

Picha Zilizovuja Zikimuonyesha Wema Sepetu na Mume Wa Mtu Zazua Gumzo

Muigizaji na mlimbwende Wema Sepetu, amejikuta katika wakati mgumu tena Jana usiku baada ya picha za faragha na bwana ake kuvuja mtandaoni.

Picha hizo zilizovuja zimewaonyesha wakiwa bafuni kwenye mahaba mazito. Inasemekana jina la mwanaume huyo ni Bakari Kila na kwa habari za chini ya kapeti zinadai kuwa mwanaume huyo ameoa na ana familia.

Picha za Wema na Bakari

 

 

Kupitia chanzo cha Global Tv inasemekana kuwa aliyevujisha picha hizi ni mtu wa karibu wa Wema kwani inavyoonekana hapo Wema ndiye alikuwa anapiga picha hizo. Mtu huyo aliyevujisha alisikika akiongea:

Achana na skendo ya unga inayomtafuna bwana wa Wema sahau kabisa zile picha zilizovuja Wema akiwa na Bakari mimi ninazo picha mpya wakiwa bafuni full mahaba, Wema ndani ya kanga moja huku wakipigana mabusu moto moto”.

Habari zilizopo zinadai kuwa kuna janga kubwa linaendelea baina yao, inasemekana kuwa bwana huyo wa Wema sio tu mume wa mtu bali pia ni muuza madawa ya kulevya na inavyosemekana kwa sasa yupo jela mjini Moombasa, Kenya.

Pia inasemekana kabla ya kutupiwa rumande bwana Bakari alikuwa na mkwanja mrefu sana ambao uliweza kumtuliza Wema mpaka akatulia na kuacha makeke ya mjini.

Pia picha hizo zimeonekana kuwakera sana mashabiki wa Wema hadi kuishia kumtolea mapovu makali.

Wema Sepetu Kwenda Nairobi Kwa Ajili Ya Tundu Lissu

Akiwa kama mmoja wa watu walikuwa mstari wa mbele sana katika kufanya kampeni katika mitandao ya kijamii ili kuchangia ela za matibabu kwa ajili ya mbunge wa Singida kupitia chama cha upinzani Chadema, mwanadada mrembo na anaependwa na watu Wema Sepetu aonyesha wazi hisia zake za furaha baada ya mwanaharakati huyo kutoka ICU.

Tundu Lissu ambae alikuwa ICU kwa muda wa takribani mwezi sasa tangu iliporipotiwa kuwa hali yake ni mbaya baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana alipokuwa nyumbani kwake Dodoma na kuhamishwa kwa matibabu nchi Kenya, jana kwa mara ya kwanza ameweza Kuongea na wananchi wanaomsapoti na kuonyesha kuwa yeye anaendelea vizuri.

Wema Sepetu alikuwa ni mmoja kati ya watu wengi maarufu walioonyesha jinsi gani wamefurahishwa na hali ya mbunge huyo kutengemaa na amehaidi kupanga safari ya kwenda Nairobi kwa ajili ya kwenda kumjulia hali mbunge huyo huku akisema kuwa alikuwa anaogopa kwa muda mrefu kwenda kumuona kwa sababu hasingeweza kuvumilia kumwangalia akiwa na yale maumivu kitandani kama ilivyokuwa ikiripotiwa na watu wa karibu waliokuwa na mgonjwa huyo hospitali kuwa hali yake ilikuwa ni mbaya.

Katika ukurasa wake wa instagram , Tanzanian sweetheart aliandika”What doesn’t kills you always makes you stronger,and you will come baq stronger than you have ever been, Our True Leader…our Hero..sasa naweza  andaaa safari ya Nairobi kuja kukuona …. I couldn’t bare to see  you in pain…This picture just melted my heart…..God sure is Good…All the time #ATrueLeader#OurOnlyHope#OurHero#SuperMan”  aliandika Wema Sepetu

Taaarifa za kuendelea vizuri kwa mwanaharakati huyo zimegusa watu wengi kwa namna tofauti huku wengine wakizidi kumuombea ilia aendele kupona haraka, hata hivyo Wema bado anafanya kampeni za fedha za matibabu kwa sababu bado kuna pesa zinahitajika ili kuendeleza matibabu ya mbunge huyo.

Ikumbukwe kwamba Wema alipoamua kuingia katika siasa  alikuwa ni mmoja wa wasanii waliokuwa  wakiisapoti Chama Cha Mapinduzi lakini hivi karibuni Wema Sepetu aliamua kubadilisha msimamo wake na kubadilsh upepo na kuingia Chadema.

Wema Sepetu Akana Tetesi Za Kulala Madale

Mwanadada mrembo kutoka Tanzania ambae amejizolea umaarufu na upendo mkubwa kutoka kwa watanzania kwa muda mrefu bila upendo huo kuchuja, Wema Sepetu amefunguka na kuongelea tetesi na scandal iliyokuwa ikimkabili kuwa alikuwa akionekana kulala madale kwa Diamond  huku  akikana kuwa maneno hayo ni uongo na hakukuwa na  kitu kama icho.Mwanzoni mwa mwezi huu mwanadada huyo alikumbwa na tetesi za kuonekana madale , huku watu wakimtuhumu kurudisha majeshi kwa msanii huyo mkubwa kutoka Tanzania Diamond Platinumz na kuwa birthday party aliyofanya msanii huyo iliandaliwa na Wema Sepetu lakini alikuwa akijificha ficha ili watu wasijue  na kumuona kwani walikuwa wakifanya kuwa siri.

Akiongea na Ijumaa wikienda, Wema Sepetu alisema watu wamekuwa na tabia ya kuzusha sana kuhusu taarifa ambazo zinakuwa hazina ukweli wowote,”unajua kuna habari zingine zinaweza kukushangaza sana, kwenye kumbukumbu zangu madale niliwahi kukanynga kipindi nyumba ndio inajengwa kwa sababu kipindi hicho nilikuwa bado nina mahusiano na diamond,lakini siku hizi za karibuni sijawahi kukanyaga huko kabisa, “

Wema pia anashangazwa na tabia ya watu kuwa na tabia ya kuzua mambo bila kuwa na uhakika wa kile wanachokiongea na hajui maneno hayo huwa yanatokea wapi,”mimi huwa sielewi  wanapokuwa wanazungumza hivyo viyu huwa inakuwaje,yaani nashndwa kabisa kujua” alifunguka mwanadada huyo.

Hata hivyo Wema alisema kuwa watu wanaokuwa wanasema maneno ambayo yanakuwa sio ya kweli wanakuwa wanahatarisha sana mahusiano ya watu tofaui kwa sababu Diamond sasa hivi ana mtu wake kwaio inakuwa haileti picha nzuri kwa watu,watu wanashindwa kuelewa kuwa kwa sasa kila mtu ana mahusiano yake , hivyo kusema vit kama hivyo ni kuharibiana mahusiano tu,  ambao unaendelea kwa sasa hivi kwa kila mmoja,hakuna kitu kibaya kama watu kkuvunja mahusiano yao kwa sababu ya maneno ya kusikia,ambayo hayana ukweli ndani yake. Aliongezea Wema

Diamond na Wema Sepetu walikuwa wapenzi zaidi ya miaka mitatu imepita sasa lakini bado kumekuwa na tetesi za mara kwa mara kuwa wawili hao bado wanaendeleza mahusiano ilihali Diamond tayari ana mwanamke mwingine ambae alishazaa nae watoto wawili.

Wema Sepetu na Mange Kimambi Wamesaidia Kukusanya Zaidi Ya Milioni 60 Kwaajili Ya Matibabu Ya Lissu

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi na Muigizaji wa bongo movie Wema Sepetu wametajwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kama watu wanaozidi kuchangia kwenye matibabu ya mbunge wa Singida mjini Tundu Lissu.

Tundu Lissu alipigwa risasi mwezi uliopita na watu wasiojulikana akiwa mkoani Dodoma kwaajili ya kuhudhuria vikao vya bunge vilivyokuwa vinaendelea. Tangu hapo amelazwa mjini Nairobi Kenya.

Kwenye kikao alichofanya Jana na waandishi wa habari Mh. Mbowe aliwataja Mange na Wema kwa mchango wao mkubwa:

Naomba niwashukuru Watanzania wanaoishi nje ya nchi kwa michango yao ya dhati naomba nimshukuru Dada yetu Mange Kimambi anayeishi nchini Marekani kwa kuanzisha account ya ‘go fund me’ iliyowezesha kukusanya dola za kimarekani elfu ishirini na tisa na mia saba sawa na shilingi za Kitanzania milioni sitini , tunatambua mchango wa Mange na Wema Sepetu katika kuhamasisha Watanzania kuchangisha pesa hizo  kupitia mitandao ya kijamii, hivyo tunapenda kuendelea kuheshimu wajibu waliochukua”.

Pia Mh. Mbowe aliwahakikishia kuwa Tundu Lissu anaendelea vizuri kwani ameshatoka ICU na sasa anakula mwenyewe bila mirija na kupumua bila oksijeni.

Mange na Wema walitumia ushawishi wao kuwaomba watu waendelee kumchangia Mh. Tundu Lissu na kwa kiasi kikubwa watu waliitikia wito na kuzidi kutoa walicho nacho.

 

 

Wema Ni Mkorofi Kutoka Ndani -Martin Kadinda

Mwanamitindo maarufu nchi Martin Kadinda ambae pia ni mtu wa karibu wa Wema Sepetu, amefunguka na kusema tabia za Wema ambazo inawezekana mashabiki wake  wamekuwa hawajui kuhusu yeye.Martin Kadinda anaasema kuwa kwa watu wasiomjua wanaweza kusema Wema ni mpole lakini ukweli ni kuwa Wema ni mkorofi sana kuliko vile watu wengi wanavyoweza kuamini.

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, mwanamitindo huyo amesema kuwa  Wema Sepetu yupo tofauti sana na vile watu wanavyomfikiria na kumuona kwenye mitandao ya kijamii, kwa sababu yeye anamjua Wema vizuri kuliko mtu yoyote na hivyo huwa anajua kabisa pale anapogombana na mtu kuwa Wema ameguswa wapi mpaka amefikia hatua ya kuongea maneno hayo.

wema ni mkorofi kutoka ndani kabisa,lakini huwa anajitahidi kadri ya uwezo wake na nguvu zake zote ili ukorofi ule usionekane,lakini pia akiamua kukorofisha anakorofisha kwelikweli,kuna matukio mimi nakisikia anafanya tu najua kabisa hapa wema ameguswa wapi” Alisema Martin

Hata hivyo Martin anaendelea kusema kuwa Wema Sepetu ni mwanadada ambae ana moyo wa huruma sana na anapenda sana kuongeza marafiki kiasi kwamba huweza kumuamini mtu yeyote hata kama bado hajamjua vizuri  “lakini pia kitu kingine ambacho Wema anacho ni open door,milango ya moyo wake iko wazi sana, na yuko wazi kiasi kwamba anaweza kumuamini mtu yeyote,mtu yeyote anaweza kuaj kwake na akwa rafiki yake na akalala hata kwake” aliongea Martin Kadinda

Martin ambae amekuwani mtu  karibu zaidi na Wema kuliko mtu yeyote yule, amekuwa ni moja ya watu wanaojitahidi kumuongelea sana Wema hasa pale watu wanaongea maneno tofauti na vile alivyo,kuna kipindi Martin alishawahi kusikika akisema kuwa  ni vigumu kufanya kazi na Wema kwa sababu Wema ni mtu asiyekuwa kiakili, amekuwa ni mtu wa kupaniki sana anapokutana na jambo.

Ukiachana na kuwa mwanamitindo na Designer wa Wema kwa kipindi cha nyuma, Martin pia alishawai kuwa meneja wa Wema Sepetu lakini baadae walisitisha kazi hizo na sasa wamebaki kuwa marafiki tu.

 

Wema Sepetu Amjia Juu Soudy Brown Kisa Mama Yake

Muigizaji wa Bongo Movie Mrembo Wema Sepetu amemjia juu mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu Soudy Brown baada ya kumrekodi Mama yake.

Siku ya Jumanne kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM Soudy alimpigia Mama Wema Simu kwaajili ya mahojiano baada ya kumkosa Wema kwa Simu, Kitendo hicho cha kumpigia Simu na kumhoji Mama yake kilimkera Wema na kumjia juu Soudy.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema alimtolea povu Soudy;

“There is limits to everything…Sipendi kabisa when people involve my mother kwenye mambo ambayo hata hayamhusu…Niachie Mama yangu Soudy I don’t like when you bother her like dat only kumrecord alafu uje kumuanika like that…Hivi Soudy huna mama wa kumfanyia like that?sasa basis like da way huwezi kumfanyia mama ako basi usiwafanyie mama wa wenzako..Have some respect at least”.

Baada ya povu hilo la Wema, Soudy Brown alimuomba Wema msamaha na kukiri kosa hilo na mashabiki wa Wema pia walionesha kukerwa na kitendo hicho.

Mapya Yaibuka, Nillan si wa Diamond, Wema Arudisha Majeshi Madale

Kadri siku zinavyozidi kusonga ndivyo mambo yanazidi kuwa mengi,kuna mengi yanayokuwa yamejificha  ambayo inawezekana kweli yakawa yanafanyika au watu katika  mitandao wanakuwa wanazusha tu, baada ya tetesi nyingi kuwakumba , Dari na diamond na kufikia hatua mpaka ya kutokuwa na mahusiano mazuri, bado tetesi hizio zinazidi kuwaandama wawili hao .Inasemekana kuwa  kuna taarifa za kuvuja kwa siri nzito kutoka kwa watu wa karibu wa Diamond bila yeye mwenyewe kujua.

Leo katika mtandao wa kijamii wa instagram muda mfupi uliopita kumekuwa na tetesi mpya kuhusu taarifa kuwa mtoto wa pili wa kiume wa Diamond Platinumz anaejulikana kama Nillan sio wa kwake na kuwa eti katika kipindi ambacho Diamond alikwenda kufuatilia maswala ya kipimo cha DNA na baada ya kuthibitisha kuwa mtoto huyo sio wa kwake ndipo alipoamua kunyamaza na icho chiko kilicholeta mtafaruku mkubwa kati ya mama na baba wa mtoto huyo.

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, Mange Kimambi ambae amekuwa akionekana mtu mwenye ujua  siri nyingi za watu wengi, Mange alitoboa undani huo na kusema kuwa Diamond alipokwenda  Afrika ya Kusini  kushereka birthday ya Mama Tiffah alikwenda na kufanya DNA na  iliyoonyesha kuwa mtoto huyo w akiume  ambae ilikuwa ikisemekana kuwa ni wa diamond sio wa kwake kwa mujibu wa vipimo vya DNA.Hata hivyo Mange anasisitiza kuwa baadhi ya watu wa karibu wa msanii huyo wamekuwa wakijua siri iyo lakini wamekuwa wakinyamaza ili kulinda heshima ya msanii hyu ambae kwa muda mrefu amekuwa akikanusha taarifa hizo.

Kwa upande mwingine pia , kuna tetesi kuwa kwa sasa msanii Diamond Platinumz amerudiana na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu ambae walikuwa katika mahusiano kwa muda wa miaka kama minne nyuma .Tetesi hizo ambazo hazina ukweli bado zinadai kuwa Wema Sepetu amekuwa akionekana nyumbnai kwa diamond muda mwingi sasa na hata katika mfululizo wa sherehe za kusherkea sikukuu ya kuzaliwa kwa msanii diamond Wema Sepetu ndie alieandaa moja ya sherehe hizo.

 

Hawa Ndio Mastaa Waliomtakia Wema Birthday Njema (picha ndani)

Ikiwa jana ilikuwa siku ya kuzaliwa ya Mrembo Wema Sepetu mwigizaji wa filamu za bongo movie na moja ya watu maarufu sana nchini, Watu wengi walijitokeza kumtumia salamu za pongezi mrembo huyo ikiwemo mastaa mbalimbali.

Wafuatao ni baadhi tu ya mastaa waliotuma salamu zao;

1. Ali Kiba

Mwanamuziki Ali kiba kama rafiki wa karibu wa Wema alimtumia salamu njema za birthday.

2. Diamona Platnumz

Pamoja walikuwa wapenzi zamani lakini wakaachana Diamond na Wema wamebaki kuwa marafiki wazuri hivyo alimtumia salamu hizo za birthday.3. 

3. Idris Sultan

Idris na Wema wamekuwa marafiki wazuri pamoja na kutokuwa pamoja kimapenzi lakini Idris alimtumia Wema ujumbe wa birthday

4. Jokate

Mrembo Jokate Mwegelo na yeye alimtumia rafiki yake Wema salamu njema za birthday.

5. Aunty Ezekiel

Muigizaji Aunty na yeye alimtumia ujumbe huu wa birthday Wema.

6. Zamaradi Mketema

Mtangazaji Zamaradi na yeye alimtumia ujumbe wa birthday rafiki yake Wema Sepetu.

7. Esma Platnumz

Dada yake na Diamond naye ambaye amekuwa rafiki wa Wema alimtumia salamu hizo za birthday.

8. Hamisa Mobetto

Mrembo Hamisa Mobetto naye alimtumia dada yake salamu za birthday njema.

Hao ni baadhi tu wa mastaa waliojitokea kumtumia salamu hizo za hadhara kwenye mtandao wa instagram jana.

Mfahamu Vizuri Madame Wema Isaac Sepetu

Wema Abraham Sepetu,alizaliwa tareh 28 Septemba mwaka  1988,  Wema ni mwanamitindo, muigizaji na pia  ni mjasiriamali, mwaka 2006 Wema alishinda taji la Miss Tanzania.

Wema ni mtoto wa nne na wa mwisho katika familia ya mzee Abraham Sepetu, elimu yake yote Wema Sepetu amesoma katika shule ya  ‘Academy International’ iliyopo jijini Dar Es Salaam, na baadae kwenda Malaysia alipoenda kusomea uongozi wa biashara.

Ukiachana na elimu yake na ushindi alioupata katika ulimwende , Wema ni muigizaji wa filamu nchini Tanzania , ni mmoja wa wasanii wakubwa na wakongwe ambao bado wanaendelea kufanya vizuri katika tasnia, moja wa watu wa karibu waliogundua kipaji cha Wema  ni marehemu Steven Kanumba, huku akionekana kucheza nae vizuri katika baadhi ya movie ikiwepo ‘The Point of no Return’.Na hivi karibuni  alizindua movie mpya ya ‘Heaven Sent’

Wema amekuwa moja ya wasanii wa kike wenye ushawishi mkubwa sana wa watu hasa katika mtandao, ni mwanadada mwenye moyo wa kupendwa na watu lakini ameonekana kuwa siku zote ni mvumilivu pamoja na matatizo mengi anayokumbana nayo.Mara nyingi amekuwa akisema vibaya lakini haonyeshi kujali kwa maneno ambayo watu wamekuwa wakimsema.

Msanii huyo bado hajabahatika kuolewa lakini ameshapitia katika mahusiano na baadhi ya wasanii maarufu kama Mr.Blue, Diamond Platinumz, Charls Baba, T.I.D, na wengi maarufu lakini kwa sasa mahusiano yake hayawekwa wazi sana ingawa kuna tetesi za kuwa na mpenzi mpya ambae sio maarufu.

Akiwa kama msanii na kipenzi cha watu wengi, inaweza  kusemekana kuwa Wema ndio msanii wa kwanza Tanzania kuwa na kundi la watu wanaompenda katika mtandao linalojulikana kama “team wema”, ambao wamekuwa wakimsapoti karibia katika kila anachokifanya lakini pia ndio watetezi wake wakubwa mara mashabiki wasiompenda wanapomuandama.

Katika upande wa uajsiriamali, wema alikuja na bidhaa yake ya lipstick iliyojulikana kama “Kiss by Wema Sepetu”, ambayo iliopoingia sokoni ilipendwa sana na wanunuzi, Wema pia alikuwa na kipindi cha Tv show ambacho kwa sasa kimesimama kidogo.

Inawezekana ikawa ni hitaji lake lakini sio muhimu sana kwa sasa, kwa muda Wema amekuwa akiandika katika mitandao juu ya kuomba Mungu ili apate mtoto, ambapo wanawake wengi kwa umri kama wake wamekuwa na watoto sasa,ikiwa leo ni siku anayoadhimisha siku ya kuzaliwa kwake basi tunamuomba Mungu amtimizie haja ya moja wake na mafaniko kwake.HAPPYBIRTHDAY WEMA!!!

Picha Ya Wema Na Bwana Mpya Yazua Utata Kwa Mashabiki

Ikiwa ni kama desturi sasa kwa baadhi ya wasanii kuvujisha picha za siri wakiwa faragha na wapenzi  wao , na inaonekana kama ni jambo la  kawaida wakati swala la mapenzi ni siri kati ya   watu wawili, hivi karibuni zimeibuka picha nyingine zikimuonyesha msanii wa Bongo Movie, malkia wa urembo, kipenzi cha wengi mwenye majina lukuki Wema Sepetu akiwa na mwanaume mpya . Msanii huyo ambae tangu kuwepo kwa picha hizo katika mitandao hajaamua kujibu kitu chochote lakini imekuwa ikileta tafrani kwa baadhi ya mashabiki huku wengine wakimpongezana na  kumsifia kuwa na mahusiano  huku wengine wakimponda na kumtukana na kumwambia kuwa ni bora hasithubutu kuvujisha picha hizo hadharani.

Msanii huyo ambae pia amepitia mahusiano ya mapenzi na wasanii  na watu wengi  maarufu katika tasnia ya sanaa hasa katika bongo fleva ikiwepo Diamond Platinumz, TID, Mr.Blue kwa  kipindi cha nyuba na hivi karibuni alikuwa akitoka na  mshindi wa big brother kutoka Tanzania Idris Sultan haonekani kukoma na tabia ya kuweka mahusiano yake wazi ilhali mahusino yake mengi ya kimapenzi yamekuwa hayadumu kwa muda mrefu.

Wapo baadhi ya washabiki wamekuwa wakisema kuwa picha hiyo ni moja ya sehemu za movie yake mpya ambayo itatoka hivi karibuni, lakini baada ya waandishi wa habari kufatilia na kupata video clip ya picha hiyo ni dhahiri kuwa picha iyo hausiani na utengenezaji wa filamu yoyote ya msanii huyo.Hata hivyo katika video clip iyo kuna baadhi ya maneno yanayosikika Wema Sepetu akiongea huku akiwa kama anamponda moja ya mabwana zake aliowahi kuwa na uhusiano nao wa kimapenzi huko nyuma.

Hata hivyo , hii ina maanisha nini kwa baadhi ya wasanii ni kusema kuwa hawana privacy, au kwa sababu wao ni wasanii basi kila kitu kinakuwa wazi, baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiandiak maoni kwa msanii huyo wakimtaka aongele kuhusu picha hizo na atoe uthibitisho wa kile kinachosemwa katika mitandao.Wema ni moja kati wa mastaa wa kike ambao wamekuwa wakisema na kutukanwa sana na mashabiki  katika mitandao kwa karibia kila tukio analolifanya , linaweza kuwa zuri au baya.

Martin Kadinda Afunguka Kuhusu Ugumu Anaopata Kufanya Kazi na Wema Sepetu

Mbunifu wa mavazi Martin Kadinda ambaye pia ni meneja wa Msanii wa Filamu na Mwanamitindo Wema Sepetu amefunguka kuhusu changamoto anazopata kufanya kazi na mtu maarufu kama Wema Sepetu.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha East Africa Martin aliweka wazi kuwa anapata wakati mgumu sana kufanya kazi na Wema kwasababu hakui kimawazo kutokana na wakati unavyozidi kwenda. Amesema licha ya kuwa anampenda sana Wema na kuwa ni mtu muhimu kwenye maisha yake iwe kwa sababu ya kazi au bila kazi bado ataendelea kumheshimu   kwani tayari wana uhusiano mzuri sana.

Martin aliendelea kusema;

“Changamoto kubwa kwangu unajua Wema ni mtoto hakui, yaani miaka inakwenda bado yupo vile vile kikubwa ni kuweza kumtengenezea  mazingira ili kesho na kesho kutwa aweze kuheshimika. Unajua Wema ana maisha yake binafsi na vitu vyake anavyovipenda kwa hiyo ninachokifanya zaidi ni kuweza dhibiti mambo yake binafsi yasimfanye kesho na kesho kutwa kushindwa kupata ugali wake wa kila siku”.

Wema ni moja kati ya msanii anayependwa sana na Watanzania kutokana na Urembo wake lakini pia  ana kundi kubwa la mashabiki wanaojiita #teamwema. Hivi sasa Wema amejiingiza kwenye biashara zaidi ambapo anauza pia bidhaa mbalimbali za urembo pia hivi karibuni amefanya filamu yake mpya inayoitwa ‘Heaven sent’ ambayo inafanya vizuri sana sokoni

 

 

Bifu Jipya Laibuka Kati ya Wema Sepetu na Batuli

Waigizaji wa Bongo movie nchini Wema Sepetu na Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ waliowahi kuwa marafiki wazuri hapo zamani na kisha kutibuana kisa fedha za kampeni za CCM walizopiga kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, wameibuka tena na bifu hilo jipya.

Warembo hao waliokuwa na ukaribu na urafiki uliopitiliza hadi kufikia hatua ya kuvaa nguo sare urafiki wao uliingiwa na dosari mapema mwaka huu na kupelekea urafiki huo kuvunjika. Lakini toka wamemaliza urafiki huo kumekuwa na maneno ya chini chini ambayo wamekuwa wakirushiana.

Batuli aliyekuwa kimya kidogo kwa miezi hii aliibuka na kusema kuwa Wema Sepetu hawezi kutamba kwenye filamu pasipo kuwepo marehemu Kanumba. Batuli ameyasema hayo mara baada tu ya Wema kuachia filamu yake mpya inayoitwa ‘Heaven sent’ aliyoifanya na mwigizaji mwenzake Gabo. Wema aliyeingizwa na kwenye sanaa na marehemu Kanumba na kutoanaye  filamu kadhaa zilizofanya vizuri sokoni.

Wema ni moja kati ya supastaa anayeongoza kwa kubadilisha marafiki kwani amekuwa na urafiki na wasanii wengi kama Kajala ambaye aligombana naye baada ya Kajala kumuibia Wema mwanaume, Kuna Auntyezekiel ambaye urafiki wao uliisha baada ya Aunty kuanzisha urafiki na Zari ambaye ni hasimu wa Wema na rafiki yake wa mwishoni alikuwa Munalove lakini naye pia walitifuana baada kumkamata uchawi na kumtuhumu kuwa alikuwa anamuonea wivu.

 

Kajala, Wolper na Harmonize Waingia Katika Bifu Zito

Mastaa wawili wa Bongo movies Kajala Masanja na Jacqueline Wolper wameingia katika bifu zito baada ya maongezi kwa njia ya video ‘video call’ baina ya Kajala na mpenzi wa zamani wa Wolper mwanamuziki Harmonize kuvuja mtandaoni na kuibua makubwa.

Kajala alikuwa akizungumza kwa njia hiyo ya kisasa na Harmonize ambae alionekana akila tunda aina ya apple kitandani kwake huku na Kajala akiwa kitandani kwake, baadaye Harmonize aliirusha picha hiyo mtandaoni na kusababisha minong’ono ya chini chini kusambaa. Picha ile ilimkera Wolper ambaye ametoka kuachana na Harmonize miezi si mingi na Kajala pia ni rafiki yake hivyo ilipelekea Wolper kuandika maneno yafuatayo kwenye picha ile: “Yaani nimekaa hapa mwenyewe nimewaza mapenzi ya siku hizi yana drama mno, mara leo huyu mara kesho yule”. Akijua wazi Kajala ameumizwa na kitendo hicho. 

Wema Sepetu naye aliingilia kati ishu hiyo na kuandika maneno chini ya picha hiyo “Be carefully my baby huyo nyakunyaku asije akapita maana keshaambiwa mlango uko wazi”. Maneno hayo yalionekana kumuuma Kajala ambaye mara moja alikimbilia mabatini kituo cha polisi kwenda kumshtaki Harmonize kwa kitendo chake cha kuweka picha hiyo mtandaoni na kuleta tafsiri kuwa huenda wawili hao ni wapenzi kitu ambacho sio cha kweli, na yeye amepewa RB No/ KJN/ 73/2017 Jalada la uchunguzi

Kajala amesema;

“Nimemshtaki Harmonize ili ajue mimi sio mtu wa mchezo  kila wakati, maana ile video tulikuwa tukizungumza kawaida kwa nini aisambaze ili iweje kama sio kuchafuana huko”.

Kajala aliongeza kuwa anawashangaa wasanii wenzake Wolper na Wema kuingilia vitu kama hivyo kwa sababu wanaona kama yeye ni wakula mizoga yao. “Mimi nashangaa hivi wamenionaje, wanafikiri mimi ni wakula  mizoga yao nini wanayoiacha, wamenishangaza sana”.

Harmonize aliwasili kituoni hapo na kwa mujibu wa chanzo kinachoaminika kutoka kituoni hapo, Mwanamuziki huyo alijitetea kuwa sio yeye aliyeweka picha hizo mtandaoni bali ni mwanamke wake wa kizungu ndo aliyemtumia mtu mwingine kwa nia ya kutaka kumjua Kajala.

Ukweli kuhusu biashara ya Wema kupigwa stop

 

Msanii Wema Isaack alikuja na biashara mpya ambayo wakidada wengi waliipenda kwa sababu ya uzuri wa bidhaa za mrembo huyo, Wema ambae aliaanza kwa kuzitambulisha lipstick zake zilizojulikana kama Kiss by Wema Sepetu zilipoingia kwa mara ya kwanza Tanzania wakidada walizigombania kama njugu sokoni hivyo bidhaa hiyo kuisha, shida imekuja katika kuendeleza bidhaa hizo kwa kuagiza mzigo mara ya pili ambapo kumekuwa na tetesi mbaya kuhusu bidhaa hizo.

Kumekuwa na tetesi kuwa biashara hiyo inaweza kufa kutokana na mzigo mpya ambao umeagiza umepigwa stop kisa tu bidhaaa hizo zinaonekana hazina ubora kama mwanzo.Tetesi hizo zinasema kuwa kutokana na kupendwa kwa lipstick izo sokoni ndio maana mzigo wa pili ulitengenezwa haraka bila kujali ubora wowote,  na ni hatari kwa matumizi ya watu hivyo bidhaa hizo kukatazwa kuingia sokoni.

Lakini pia zipo tetesi kuwa inawezekana kuna watu wanaotaka kuchafua jina la msanii huyo  kwa kusambaza tetesi hioz au kuingia mzigo fake kwa kutumia jina la Madame ili tu  kumuharibia msanii jina.

Hata hivyo alipokuwa akitoa maelezo ya uwepo wa tetesi hizo katika kituo cha EATV , meneja mpya wa Madame Wema Sepetu aliejulikana kwa jina la  Happy  Shame  amesema mzigo huo haupo sokoni kwa sasa kwasababu  msimu wa kuangiza mzigo mpya bado  na sio kweli kwamba mzigo umezuia kwa sababu hauna ubora .

“Hicho kitu sijakisikia na wala sijatumia katika email yangu  kwamba lipstick zimezuiwa . Hivi vitu vinaenda na msimu , muda wake ukifika tutaziachia  kwaiyo hakuna ukweli  isipokuwa kuna baadhi ya vitu  tunavikamilisha baadae mzigo utatoka” anasema Happy Shame.

Hivyo basi uwepo wa tetesi za kusimamishwa kwa bidhaa za lipstick za Wema Sepetu zinaweza kuwa  si za kweli ilhali meneja wa msanii huyo amethibitisha kuja kwa bidhaa hizo endapo taratibu za uingizaji wa bidhaa hizo nchi utakamilika, hivyo kwa wateja waliokuwa wanasubiri bidhaa hizo wanaweza kutokwa na wasiwasi kwa kusikiliza pia maneno ya meneja.