Zari Aamua Kumuiga Wema Kwa Hili

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amemuiga Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu kwa jina.

Ikiwa jina la Tanzania Sweetheart bado lina utata ambapo Wema Sepetu na  Hamisa Mobetto bado wako vitani kwa ajili ya Jina hilo na Zari naye ameibuka na lake.

Zari na yeye ameamua kumuiga kwa kujiita Uganda’s Sweetheart. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Snapchat, Zari aliweka picha yake na kuambatanisha na maneno hayo ya Uganda’s Sweetheart hali ambayo ilisababisha gumzo mitandaoni.

Mh! Bi dada naye kaona amuige Wema kwa kujipa jina la Sweetheart, makubwa,” alichangia mmoja wa wadau wa mtandao wa Instagram baada ya kipande hicho cha picha kusambaa.

Hata hivyo Zari hakutoa maelezo yoyote kama kujiita vile ilikuwa ni kwa ajili ya utani au kweli alimaanisha kutaka kuwa Uganda Sweetheart.

Tazama Jinsi Zari Alivyofanya Birthday Party Ya Kifahari Uganda

Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ ambaye ni mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefanya party la kifahari nchini Uganda.

Zari ambaye alisheherekea Birthday yake tarehe 23 Sepetemba lakini aliungana na Familia yake inayoishi nchini Uganda kwa ajili ya Kusheherekea na ndugu zake na marafiki.

Sherehe hiyo iliyofanyika katika hoteli ya kifahari ilihudhuriwa na marafiki na ndugu kadhaa wachache ambapo watu maarufu walikuwa ni pamoja na  Captain Mike Mukula, dada wa Zari, Aly Alibhai na mkewe, Sylvia Wilson Namutebi.

Umri Wa Zari Wazua Balaa Kwenye Mitandao Ya Kijamii

Umri wa mwanamama Zari Hassan ‘Zari The Bosslady’ umekuwa tena mjadala Kwenye mtandao wa kijamii baada ya kudaiwa kudanganya umri wakr hivi karibuni.

Wikienda iliyopita ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa wa kwa Zari na sherehe yake alienda kuifanya nchini Uingereza, London lakini inasemekana aliwekwa Kwenye mahojiano kwa masaa kadhaa na kisa kikitajwa ni umri wa Zari.

Inadaiwa kuwa umri wa Zari uliopo Kwenye Cheti cha kuzaliwa na uliopo kwenye passport ya kusafiria ni tofauti ambapo Zari amedai ana miaka 38 ikimaanisha amezaliwa mwaka 1980 lakini kuna taarifa zinadai amezaliwa 1978 na nyingine mwaka 1975.

Mange Kimambi Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa kitendo cha Zari kudanganya umri kumemletea matatizo kwani kuna uwezekano wa kuzuiliwa kuingia Uingereza kwa miaka mitatu.

Umri wa Zari imekuwa ukioeta utata kwa muda mrefu huku baadhi ya watu wakidai Zari hana miaka 38 Anayodai anayo jambo ambalo ameshawahi kulikataa siku za nyuma.

Zari Ni Hodari Wa Mapenzi- Diamond Platnumz

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amesuka gumzo siku ya jana Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuimba kipande cha wimbo chenye maneno “Zari hodari wa Mapenzi”.

Diamond ambaye alikuwa Kwenye Mahusiano na Zari kwa takribani miaka minne mpaka walivyimwagana mapema mwaka huu aameibuka na kusifia ujuzi wa mapenzi wa mama watoto wake huyo.

Diamond amesema maneno yake Kupitia kipande cha video Kilichomuonyesha akiimba wimbo mpya wa Msanii kutoka WCB Mbosso uitwao ‘Hodari’ ambapo ndani yake amemtaja Zari kama Hodari wa mapenzi.

Lungi Amcharua Gigy Money Kisa Zari

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Lungi Maulanga amemwagia povu zito msanii wa Bongo fleva Lungi Maulanga kisa Mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Zari The Bosslady.

Lungi ameibuka na kudai hakufurahishwa na maneno yaliyotolewa na Gigy Money na kuelekezwa kwa Zari siku chache zilizopita baada ya wawili hao kuingia kwenye majibizano ya Mtandaoni.

Kwenye Interview yake na gazeti la Ijumaa, Lungi alisema amekuwa akikerwa mno na Gigy ambaye amekuwa akitoa kauli ya kuwa yeye ni mzuri na mrembo kuliko Zari, jambo ambalo siyo kweli kwani msanii huyo hawezi kumfikia hata robo mwanamama huyo ambaye ni raia wa Uganda mwenye makazi yake nchini Afrika Kusini.

Huyo Gigy alipata jina kwa kukaa utupu, lakini Zari ni mwanamke mpambanaji na ana pesa zake siyo anadanga, sasa namshangaa huyo mtoto kujilinganisha naye.

Ni bora hata mimi nikajilinganisha naye kwa sababu hapa nina watoto wanne, lakini bado ninaonekana mrembo.

Sina hata tumbo, lakini yeye mtoto mmoja tu utadhani anao zaidi ya watano, namsihi anyamaze na aache kutafuta kiki kupitia jina la Zari maana siyo levo zake”.

Gigy Money alimwagia povu zito Zari mara baada ya kutoa kaulia ambayo mwenyewe aliamini ilikuwa imelenga kumdhalilisha.

Natamani Kuzaa na Mtoto Kwanza wa Zari – Gigy Money

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amemtolea povu zito Mzazi mwenza wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady.

Gigy alianza kumtolea povu Zari wiki iliyopita Kwenye mitandao ya kijamii baada ya Zari kudai hataki kuwekwa kundi moja na Gigy.

Lakini inaonekana kama bifu la Gigy kwa Zari halijaisha kwani ameendelea kumuongelea mbovu Kwenye mitandao ya kijamii ambapo sasa ameibuka na kudai anataka kuzaa na mtoto wa kwanza wa Zari ili awe bibi wa mtoto wake.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Gigy amemwagia povu hili Zari:

Zari mimi nakuahaidi kitu kimoja lazima ni we na mtoto wako wa kwanza ili uwe bibi wa mtoto wangu halafu ndio utaniheshimu na ndio maana sitaki kuongea sana maana atakuwa mama mkwe wangu na hatoamini kwa njia yoyote ile mwanangu atakuwa mrithi wa hizo hela anazoringia na kama siwezi kuwa Bosslady kwa njia moja basi nitakuwa hata kwa urithi”.

Zari ni mama wa watoto watano ambao watoto wake watatu wa kiume alizaa na Marehemu Ivan na watoto wake wawili wadogo amezaa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Gigy Money Amtolea Povu Zito Zari Adai Sio Type Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Kiki ni Gigy’ amemwaga povu zito akilielekeza dhidi ya Baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond, Zarinah.

Gigy amemrushia maneno makali ya kejeli Zari baada ya Zari kutaka asihusishwe na Gigy siku chache zilizopita.

Sakata zilianza baada ya Zari kuposti picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa anazindua chuo ndipo shabiki mmoja alimtag Gigy baada ya kuona Gigy ametajwa Kwenye page yake Zari alisema ni kama amedhalilishwa kuhusishwa kwa njia yoyote na Gigy Money.

Kwenye mahojiano na Bongo stars, Gigy Money amemwagia povu zito Zari:

 

 

“Bongo Movie Kwenda Kwenye Birthday Ya Tiffah Ilikuwa ni Kiki Tu”- Shamsa Ford

Msanii wa Bongo movie Shamsa Ford amefunguka na kupasua kuwa habari ya wasanii wa Bongo movie  kama Wema, Aunty, Shamsa, Faiza, Maimatha na Wolper Kwenda Kwenye party ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu.

SIku chache zilizopita Kwenye 40 ya mtoto wa Zamaradi, Babu Tale aliwaalika Bongo Movie kwa ajili ya kwenda South Africa Kwenye party ya Tiffah South Africa Lakini mara moja Zari aliwapiga stop.

Baada ya mgogoro wasanii hao kila mmoja ameonekana kughaili Kwenda huku wengine wakidai kulikuwa hakuna Safari bali ilikuwa ni kiki tu.

Gazeti la Amani, liliamua kuwasaka baadhi ya mastaa waliokuwemo kwenye kamati hiyo ambapo kila mmoja aliongea la kwake kama ifuatavyo;

Faiza Ally alisema kuwa alijua wazi kuwa hatakwenda kwa sababu Zari ‘alishamblock’ siku nyingi kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mimi baada ya kutangaziwa vile tu nilijua siwezi kwenda kwa sababu Zari alishaniblock siku nyingi, sasa huwezi kwenda kwa mtu ambaye alishakublock na alivyosema maneno yale ndio kabisaaa”.

Maimatha wa jesse alidai kuwa hawezi kwenda kwa sababu hakuipenda tabia ya Zari kuwaambia kuwa watakwenda kumchafulia nyumba.

Sikuipenda kabisa tabia ya Zari, yeye angeacha akaona kama kweli tutaenda au la lakini kabla hata siku hajizafika akajibu palepale, ya nini kwenda? Nimemshangaa maana hajui kama kwake tungeenda ingekuwa na faida sana hata kujitangaza kibiashara“.

Shamsa Ford yeye alidai kuwa anachojua lile tangazo la wao kwenda Sauz kwenye sherehe ya Tiffah ilikuwa ni kiki tu wala hakukuwa na ukweli wowote.

Unadhani mchezo kuwasafirisha watu wote wale, ile ilikuwa ni sehemu ya kiki tu, wala siendi mimi”.

 

Zari Aweka Pembeni Tofauti Zake na Hamisa na Kumtumia Dylan Salamu za Birthday

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameweka tofauti zake pembeni na Mzazi mwenza mwingine wa Diamond Hamisa, na kumtakia heri mtoto wake Dyalan.

Zari na Hamisa walikuwa kwenye vita kali tangia Zari alipoginfua Diamond kamsaliti na kuzaa na Hamisa wakati wakiwa Kwenye Mahusiano kimapenzi.

Lakini sasa Zari anaonekana kuweka pembeni tofauti hizo hasa linapokuja suala la watoto kwani amemtumia salamu za Birthday Dylan na kukiri yeye ni mtoto na hana makosa.

Kwenye mahojiano hayo na kituo kimoja cha habari nchini Uganda ambapo Zari anategemewa kuwa JAJi katika mashindano ya Miss Uganda, amefunguka na kusema hana kinyongo na Dylan kwani ni mtoto ambaye hana makosa na sio kosa lake yuko pale:

Siku ya Jumatano ilikuwa Birthday ya Dylan mtoto wa Diamond na Hamisa na Zari alimtumia salamu Hizi:

Happy birthday Dylan, Hope you have the best in life and Mummy Z loves and no matter what the public says it was never your fault you were just caught up in it and you happened and i know the internet will torment you and say you were a child who came to break another woman’s family but no matter what you are here and I hope you grow up to be something big”.

Shamsa Ford, Faiza Ally na Maimatha Wamburuza Zari Mtandaoni

Mrembo  Zarinah Hassan maarufu kama Zari The Bosslady amejikuta katika vita kali ya maneno katika mitandao ya kijamii na wasanii wa Bongo movie ambao ni Shamsa Ford, Faiza Ally na Maimatha Jesse.

Bifu kati ya Zari na Wasanii hao lilianzia katika suala zinazoendelea la kuhudhuria birthday party ya Tiffah ambapo Zari aliwachana wasanii hao na kudai kuwa wasiende Sauzi maana watachafua nyumba.

Wasanii hao walionyesha kutofurahishwa na kauli hiyo na kumtolea povu zito ambapo Faiza Ally alifikia hatua ya kumuita Zari mshamba kutoka Uganda:

.

https://www.instagram.com/p/BmNO1hVB20g/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1k3ud2823hr96

 

“Sina Mpango wa Kwenda SA Kwenye Birthday Ya Tiffah” Povu la Wema Kwa Zari

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amemwaga povu zito na kudai hataenda Kwenye Birthday party ya Tiffah nchini South Africa.

Wema amefunguka na kusema kuwa hawezi kwenda Afrika Kusini kwenye party ya mtoto huyo kama walivyoalikwa Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika:

God Bless The Next Big Thing… Like Father Like Daughter. On August 6th, A Star was Born… ??????. Msije mkadhani kwenye Party naenda. Wala siendi. I jus wished the lil angel Dats it…!!! ??? #SinagaHianaMie . Maana hamkawii”.

Povu hilo limekuja siku chache baada ya Zari kumwambia Live kabisa Wema na kundi lake la Bongo movie kuwa hawataki nyumbani kwake maaana watamchafulia Nyumba.

Diamond na Zari wanategemea kumfanyia Tiffah bonge la sherehe huko nchini South Africa.

“Mimi Sio Level Zenu, Msiniringanishe na Vinuka Mkojo”- Zari

Baby mama wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amekuja juu na kumwaga povu zito siku ya jana na kuomba asilinganishwe na vinuka mkojo.

Povu hili la Zari limekuja siku chache baada ya kupishana Kauli na wasanii mbali mbali kutoka Bongo Movie ambao walitakiwa kwenda nchini South Africa kwa ajili ya birthday ya mtoto wa Diamond, Tiffah.

Zari aliwaambia wasanii kama Wema Sepetu, Aunty Ezekiel, Maimatha na kamati nzima ya Zamaradi kuwa hataki waende South Africa kwenye birthday ya Mtoto wake kwani watachafua nyumba yake.

Siku ya jana pia Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Zari aliwamwagia povu hili watu ambao hawakuwataja majina lakini hakutaka kulinganishwa nao.

Ati sijui A or B, mimi sio level zenu I worked hard for my name, Am not a social climber. Hatuuzi sura tu, tunapambana na  msiniringanishe na vinuka mkojo vwenu, mxiuuu.”.

.

 

 

 

Familia Ya Diamond Yadaiwa Kugoma Kwenda Kwenye Birthday Ya Mtoto Wa Hamisa

Familia ya staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz imedaiwa kugoma kabisa kuhudhuria Birthday party ya mtoto wa Diamond aliyezaa na Hamisa Dylan.

Global Publishers wanaripoti kuwa Familia hiyo inadaiwa kususia mwaliko huo ambao ni wa Birthday ya Mtoto wa Mobetto na inadaiwa kuwa bize zaidi na maandalizi ya birthday ya Tiffah itakayofanyika South Africa.

Chanzo makini kilieleza kwamba familia ya Diamond imegomea kwenda kwenye bethidei inayoandaliwa na Mobeto kwa ajili ya Dylan ambaye pia ni mtoto wa mwanamuziki huyo inayotarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu.

Unaambiwa familia ya Diamond haitaki kusikia mtu anayeitwa Mobeto maana hawampendi hivyo licha ya kwamba Dylan amezaliwa mwezi mmoja na Tiffah lakini wao wako upande mmoja wa Tiffah“.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Esma Platnumz ambaye ni dada wa Diamond amesema  kuwa hawezi kwenda kwenye birthday ya Dylan kwa sababu hawajawahi kualikwa kwenye sherehe zao hata siku moja, hivyo hawawezi kwenda wala hawatarajii kusogea.

Hivi ushawahi kuona klina Hamisa wanatualika kwenye ishu zao hata kidogo? Hivyo hatuwezi kwenda hata kidogo wala hatutarajii kabisa“.

Kumekuwa na maswali mengi juu ya birthday ya mtoto wa Hamisa na Diamond ambaye pia ana birthday hivi karibuni kwani  inayosikika ni  ya Tiffah na siyo Dylan ambaye pia ni mtoto wa Diamond.

Wema Amjibu Zari “Hatukuomba Kuja South Africa”

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameamua Kuvunja ukimya na kumjibu Zari na kumwambia kiroho safi tu wao hawakuomba kwenda South Africa kwenye birthday ya Tiffah bali walialikwa.

Sakata hilo lilianza baada ya siku ya juzi Meneja wa WCB, Babu Tale kuwakaribisha kamati nzima ya watu walioshughulikia 40 ya mtoto wa Zamaradi ambayo ilijumuisha wasanii mbali mbali wa Bongo movie ikiwemo Wema Sepetu na Aunty Ezekiel kwenye birthday ya Tiffah.

Birthday party ya mtoto wa Diamond na Zari inatarajiwa kufanyika mwezi ujao na wana mpango wa kufanya bonge la party kwaiyo WCB waliamua kuwalipia tickets kamati hiyo ili waende South Africa kwa ajili ya party hiyo.

Lakini Zari hakutaka kabisa watu hao waende kwani siku ya jana alizua gumzo baada ya kubadilisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hataki watu waende kwa sababu watamchafulia nyumba yake kwaiyo wabaki huku huku Tanzania.

Basi baada ya maneno hayo kutoka kwa Zari Wema alishindwa kujizuia kwani alimjibu kuwa asipanik kwani wao hawakuomba huo mwaliko bali walipewa tu na WCB.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Wema aliandika:

Sema nasikia kama safari ya SA imeleta mtafaruku mtaa fulani…….Jamani hatukuomba halafu kiroho safi tu….”.

 

 

Aunty Ezekiel Awatolea Povu Wanaohoji Ukaribu Wake na Zari Pamoja na Wema

Msanii filamu za kibongo Aunty Ezekiel amemwaga povu kwa mashabiki Kwenye mitandao ya kijamii ambao wamekuwa wakimsema na kumuita Yuda kwa kitendo chake cha kuwa na ukaribu na Wema pamoja na Zari.

Mashabiki Kwenye mtandao wa Instagram ambao wamegawanyika Kwenye team Wema na Team Zari wamekuwa wakimpiga majungu Aunty na kumuita Yuda msaliti baada ya kutangaza kwenda nchini South Africa kushiriki birthday ya Tiffah.

Kwenye mahojiano na gazeti la na Amani, Aunty alisema majungu hayo yameanza mitandaoni baada ya kusikia amealikwa kwenda kwenye bethidei ya mtoto wa Zari, Tiffah inayotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao lakini kamwe majungu hayo hayamsumbui.

Ifike mahali tufunge mjadala, kila siku ni Aunt kuwa karibu na Zari, Wema kama ni bethidei nitaenda tu. Hawa wote ni marafiki zangu sasa siwezi kubagua kwa kuwa eti Wema aliachana na Diamond wakati kule kwa kina Diamond pia kuna mpenzi wangu Iyobo na isitoshe Zari ni wifi yangu kwa upande mwingine“.

Kwa miaka mingi Zari na Wema wamekuwa kama paka na panya kwa ajili ya kugombea penzi la Diamond kwaiyo kitendo cha Aunty kusema anaenda Kwenye sherehe ya mtoto wa Zari kiliwashangaza watu wengi hasa kwa sababu Aunty rafiki yake kipenzo ni Wema.

Diamond Kuwakutanisha Wema na Zari Nchini South Africa

Ikiwa siku zinakaribia kuelekea birthday party ya mtoto wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Bosslady Zarinah Hassan, Diamond anatarajiwa kuwakutanisha Zari na Wema nchini Afrika ya Kusini.

Diamond Kupitia uongozi wa label yake ya WCB imetangaza kusafiri na Wema Sepetu ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wanakamati wa birthday party ya Tiffah Dangote.

WCB wamesema wataisafirisha kamati hiyo kwa kuwa wameipenda na wanaona ni jambo zuri kwenda kushiriki nao kwenye shughuli hiyo. Mastaa wengine ambao wanaunda kamati hiyo ni Shamsa Ford, Shilole, Irene Paul, Irene Uwoya, Lamata, Kajala Masanja pamoja na wengine wengi.

Wema pamoja na wanakamati wengine ambao siku ya jana walikuwa wanakamati katika arobaini ya mtoto wa Zamaradi wamepokea mualiko huo uliowasilishwa na Meneja wa Diamond Babu Tale.

Diamond ameitaja Birthday party ya Tiffah  kama  sherehe ya mwaka ambapo pia amehaidi kuwalipia mashabiki kadhaa kwa ajili ya kwenda kuhudhuria.