Rayvanny Awashangaa Wanaomtuhumu Kujichubua

Msani Ray Vanny amekanusha taarifa za mitandao na kurasa za udaku kuwa kwa sasa ameanza kujichubua.

Akiongea na waandishi wa habari wa  Ijumaa Wikienda, Rayvanny alisema kuwa anashangaa maneno hayo yanatoka wapi kwani katika maisha yake haja­wahi kuwaza kufanya hivyo na anachoamini yeye watu watakuwa wanaongea kwa sababu ya muonekano wake kwenye picha.

“Jamani mimi hizo tabia nimezianza lini tena? Yaani walimwengu hawakosagi cha kusema, unajua kuna picha ambazo zikitupiwa mtandao­ni naonekana mweupe sana na nyingine zinakuwa zime­toka vibaya, hapo watu ndiyo huanza kusema nimejichibua, kitu ambacho siyo kweli,” alisema Rayvanny.

Hivi karibuni msanii huyo aliposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa ana­toka kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, ambapo picha hiyo ilionesha magoti yake ni meusi tofauti na sehemu nyingine za mwili wake hivyo kuwafanya wadau kudhani amejichubua.

Kevin Gates Awakubali Diamond Platnumz na Rayvanny

Msanii wa muziki wa Hip hop kutoka pande za Marekani Kevin Gates ameonekana kuikubali nyimbo mpya ya Rayvanny na Diamond Platnumz Baada ya kuonekana akiwa anaisikiliza.

Kevin Gates ambaye alishawahi kutamba na ngoma kibao ikiwemo ‘Out The Mud’ ameposti kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram, akisikiliza ngoma ya Tetema.

Tetema imeendelea kuvunja rekodi kuanzia kuwa nyimbo ya kwanza Tanzania kutazamwa mara milioni moja ndani ya mastaa 17 Mpaka kufikisha watazamaji milioni 3 ndani ya siku tatu.

 

Tetema Ya Diamond na Rayvanny Yavunja Rekodi

Wimbo mpya unaofanya vizuri Hivi sasa ‘Tetema’ ulioimbwa na wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny umevunja rekodi Mpya Baada ya kufikisha watazamaji milioni moja ndani ya mastaa 17.

Wanamuziki Diamond Platnumz na  Alikiba ni baadhi ya waliofanikiwa nyimbo zao kutazamwa mara milioni moja kwa muda wa masaa 24.  Mpaka wakati huu wimbo huo umetazamwa mara milioni 1.2.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameshukuru mashabiki zake kwa kuangalia wimbo huo mara milioni moja:

Tumekoma Hatuwezi Kurudia Tena Makosa-Babu Tale

Meneja wa Kampuni ya Wasafi (WCB) Babu Tale amekiri kuwa adhabu waliyopewa wasanii wake Diamond na Raymond Mwakyusa’ Rayvanny kufungiwa miezi miwili, imewafundisha na hawatarudia tena.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la mwananchi, Babu Tale ameweka wazi kuwa adhabu waliyopata Diamond na Rayvanny imekuwa somo kwao wote na hawatorudia tena makosa.

Kwa kweli kwa muda wote ambao wasanii wetu walikuwa wamefungiwa pamoja na kusitishwa kwa tamasha letu la Wasafi, tumejifunza mengi, hatuna budi kuishukuru BASATA na serikali kwa ujumla tunachowahaidi ni kwamba tumrjifunza mengi na hatutarudia tena”.

Diamond na Rayvanny walifungiwa mwaka jana Desemba 15 na kuzuiwa kufanya maonyesho ya nje na ya ndani hata hivyo Wiki chache zilizopita BASATA Ilitangaza kuwafungulia rasmi.

 

Rayvanny Ataja Kilichomsibu Mpaka Kupaka Rangi Nywele

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Music Label ya WCB, Raymond Mwakyusa maarufu kama Rayvanny amefunguka na kumtaka kilichomsibu Mpaka kubadilisha muonekano Wake.

Hivi karibuni Rayvanny ameonekana na muonekano Mpya kichwani kwani Mbali tu ya kusuka Rasta Lakini pia amezipaka rangi ya Bleach na kuonekana tofauti.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Rayvanny amesema kuwa kwa kawaida msanii anatakiwa kuwa na muonekano wa tofati tofauti na ndicho alichokifanya kwa sasa.

Muda mwingine msanii unatakiwa uwe unabadilika sio panki kila siku. Mtaanza matusi yenu toa, toa, sitoi huo ndio muonekano wangu”.

Msanii huyo anayefanya vyema na kibao chake cha Paraanawe amepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki zake ambao hapo Mwanzoni walikuwa wanavutiwa kwa kuwa na nywele fupi za kawaida tofauti na Diamond na Harmonize ambao walikuwa wanasuka na kubleach nywele.

Wakikupa hi Tu Wablock :- Rayvanny Amuomba Fahyma

Msanii kutoka kundi la wcb Rayvanny ,  amefunguka na kumuomba mama mzazi wa watoto wae fayma kuwa muaminfu na hata kama atatokea mtu kumtaka na kumtongoza basi akatae kabisa naikibidi amblock wala asimsikilize anataka nini.

Rayvanny na mama watoto wake wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu sasa na hata kupitia mambo mengi ikiwa pamoja na kukaa mbali kila mtu kwa muda kutokana na ugomvi unaotokea katika mahusiano lakini wawili hao mpaka sasa wameweza kuwa pamoja.

hata hivyo Rayvanny tayari alishamtambulisha mwanamke wake nyumbani ingawa hawajafunga ndoa lakini alisema yuko mbioni kufanya hivyo, kupitia ukurasa wake wa instagram  Rayvanny alimumba mama huyo kwa kusema “itaniuma sana siku pumbavu wakiniibia, …mama jilinde ukipewa hii tu wewe bulooock …”

 

Rayvanny Atoa Shukrani kwa BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ameishukuru Bodi ya Baraza la sanaa Taifa (BASATA) kwa kuwaruhusu kuendelea na show zao nje ya nchi licha ya kufungiwa.

Rayvanny na Diamond Platnumz walifungiwa na baraza hilo kufuatia kutumbuiza wimbo wao uitwao Mwanza licha ya wimbo huo kufungiwa. Hiki ni kile alichoandika Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram;

“Nichukue Nafasi Hii Kushukuru Basata, Hususani Bodi Ya Basata Kwa Kutupatia Ruhusa Ya Kufanya Matamasha Tulioyafanya Nchini Comoro , Nairobi Na Mombasa. Matamasha Tulitakiwa Tusiyafanye Kutokana Na Makosa Tuliyoyatenda Ila Kwa Upendo Wenu Mlituruhusu Kuyafanya.

“Nitoe Shukurani Zangu Za Dhati Kwenu Maana Bila Nyie Kutupa Ruhusa Ni Mengi Yangetukuta Vijana Wenu, Lakini Pamoja Na Yote Yaliotokea Kwetu Ni Kama Darasa La Kujua Wapi Tulipoteleza, Ili Mbeleni Lisijirudie Kosa Kama Tulilolifanya.

“Tuna Ahidi Kua Vijana Bora Na Mfano Kwa Jamii Hususani Katika Maadili Naamini Basata Na Bodi Ya Basata Mnatupenda Vijana Wenu Na Mnatamani Kuona Tunafika Mbali Katika Sanaa, Tunaomba Sana Hekima Zenu Katika Hili Vijana Wenu Tuendelee Kuchapa Kazi Kama Anavyosisitiza Mh. Rais Magufuli

Rayvanny Atoa Sababu ya Kubadili Nywele.

Msanii kutoka katika kundi la Wcb amefunguka na kusema kuwa sababu kubwa iliyompelekea maa kutaka kubadili muonekano wake ni kwa sababu anataka kuwa na muonekano tofauti tofauti kama msanii kwa ajili ya kubadili radha kwa mashabiki wake pia.

Rayvanny anasema ‘Muda mwingine msanii unatakiwa kubadilika sio kila siku panki tu ,  na ninajua karibuni taanza matusi yenu na kuniambia toa, toa, toa lakini sitoi huu ndo muonekano wangu kwa sasa.”

Wasanii hwa kutoka katika kundi hili kwa sasa  wamekuwa kama wameambizana kwa sababu wote wamebadili muonekano yao kichwani.

BASATA Wakanusha Taarifa Za Kuwafungulia Diamond na Rayvanny

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha taarifa za kuwafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wanaotumikia adhabu ya kutojihusisha na muziki kwa muda usiojulikana baada ya kufanya makosa mbalimbali ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Taarifa hiyo imekuja baada ya msanii Diamond kutangaza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jana kuwa wameruhusiwa kufanya tamasha la muziki, Wasafi Festival’  nchini Kenya.

Siku chache zilizopita wasanii hao kupitia mtandao wa Instagram Walionekana wakifanya mkutano na waandishi wa habari nchini Kenya kutangaza maonyesho yao yanayoendelea, lakini alifajiri taarifa ya Basata ilisema kuwa hawajatoa ruhusa kwa wasanii hao.

Baada ya kauli hiyo kutoka kwa wasanii hao kutoka WCB, BASATA walitoa tamko lao na kusema:

Ikumbukwe kuwa Desemba 18 tuliwafungia kutojihusisha na sanaa kwa kipindi kisichojulikana kwa kuimba kwa makusudi wimbo Mwanza tulioufungia kwa sababu za kimaadili,

“Baraza linasisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao, pia linawaonya kuacha kutoa taarifa za uongo kabla halijawachukulia hatua kali zaidi,” imeeleza barua hiyo.

 

Diamond na Rayvanny Waomba Msamaha BASATA na Serikali Baada Ya Kufungiwa

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka Katika Label ya WCB Diamond Platnumz na Rayvanny ameibuka na kuomba Radhi kwa serikali na BASATA siku chache Baada ya kufungiwa.

Wiki iliyopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walitangaza kuwafungia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny Baada ya kukaidi amri yao na Kuperfom wimbo wa Mwanza uliofungiwa kwenye tamasha lao la Wasafi Festival.

BASATA Walitangaza kulifungia tamasha la Wasafi Festival na pia kuwataka wasanii hao kutoperfom katika nchi nyingine yoyote pamoja na kwamba walishapanga kwenda Kuperfom Nchini Kenya.

Lakini Wasanii hao wameomba msamaha Kwa BASATA na Serikali kwa ujumla na kuomba wasemehewe adhabu yao waliyopewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameposti kipande hiki cha video kinachoonyesha wasanii Hawa wakiomba radhi:

https://www.instagram.com/p/BroqbY3j9YE/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1uqh6m3umbdj1

Diamond Platnumz na Rayvanny Wafungiwa Kufanya Show Ndani na Nje Ya Nchi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Rayvanny kutokea katika Label ya WCB wamefungiwa rasmi kutofanya show ndani na nje ya nchi kwa muda usiojulikana.

Baraza la  Sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza kuwafungia Diamond na Rayvanny Baada wawili hao kukiuka masharti waliyopewa.

Taarifa  iliyotolewa leo Desemba 18, 2018 na BASATA,  imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Kwa upande mwingine, BASATA  wamefuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linalotarajiwa kufanyika nje ya nchi baada ya kuzunguuka kwenye baadhi ya mikoa hapa Tanzania.

Imeelezwa kuwa wimbo wa Mwanza ndio uliowaingiza matatani, baada ya wasanii hao wikiendi iliyopita kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi Festival jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.

Lynn Akiri Kuvutiwa na Rayvanny na Dogo Janja

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Irene Godfrey Louis maarufu kama Lynn ameibuka na kuweka wazi kuwa wasanii waliomvutia kwenye Sanaa ni Mastaa wa Bongo fleva Rayvanny na Dogo Janja.

Wiki mbili ziizopita Lynn aliingia rasmi kwenye tasnia ya Bongo Fleva kwa kutambulisha wimbo Wake Mpya ‘Chafu’.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Lynn alisema kwa kipindi kirefu alikuwa na nia ila alikosa mtu wa kumshauri, lakini baada ya kuwasikilizisha nyimbo zake, Rayvanny na Dogo Janja walimtia moyo kuwa anaweza.

Muziki ni moja ya malengo yaliyokuwa ndani yangu, lakini ndoto zangu niliona kama zinakufa kutokana na baadhi ya watu kunikatisha tamaa. Lakini ilikuwa tofauti kwa Rayvanny na Dogo Janja ambao walinipa moyo kuwa naweza ndipo nikatoa wimbo wangu haraka”.

Lyyn ambaye ameachia ngoma inayokwenda kwa jina la Chafu na kusifia mapokezi kuwa ni mazuri kuliko alivyotegemea hivyo amepanga kuachia mwingine fasta.

 

 

BASATA Kuwashughulikia Diamond na Rayvanny Baada Ya Kupiga ‘Mwanza’

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) linefungukia kitendo cha Wasanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Rayvanny kuperfom wimbo wao wa Mwanza ambao umefungiwa.

Mwezi uliopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) walitangaza kuufungia rasmi wimbo wa ‘Mwanza’ kwa madai kuwa wasanii hao wamekiuka maadili ya Kitanzania kwa maudhui ya wimbo huo.

Diamond aliimba wimbo huo alioshirikishwa na Rayvanny jana Desemba 15, 2018 katika tamasha la Wasafi lililofanyika jijini Mwanza jana, huku maelfu ya mashabiki wakimshangilia na kumfuatisha alivyokuwa akiimba. Mkali huyo wa Bongo Fleva aliimba wimbo huo  akiwa pamoja na Rayvanny.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Katibu mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza alifungukia ishu hiyo na kusema:

Nimepigiwa simu kuhusu hii kitu. Niko Arusha kikazi nimeshawasiliana na mwenyekiti wa bodi (ya Basata).

Basata itakuja na majibu muafaka kwani hapa (Diamond) kaonyesha kiwango cha juu cha dharau kwa baraza, bodi, wizara (Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo) na Serikali kwa ujumla”.

 

 

Diamond, Rayvanny na Mbosso Wapata Ajali Stejini Sumbawanga (+Video)

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Diamond Platnumz na wasanii wenzake Rayvanny na Harmonize walipata ajali katika Steji ya Wasafi Festival iliyokuwa inafanyika mkoani Sumbawanga.

Shoo hiyo ilifanyika siku ya jana 9 Desemba katika uwanja wa Nelson Mandela ambapo wasanii hao walikuwa wanaperfom wimbo wao pendwa kabisa wa ‘Zilipendwa’ lakini ndipo balaa lilipotokea Baada ya wasanii hao kula mieleka.

Lakini baada ya kudondoka kwa Diamond akifuatiwa na Mbosso wasanii hao waliinuka na kuendelea na shoo na iliripotiwa kuwa hakuna Msanii aliyepata majeraha makubwa zaidi ya michubuko ya hapa na pale.

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale alitoa taarifa kuwa wasanii hao wanaendelea vizuri na hakuna aliyeumia.

Baada ya sakata hilo Kupitia ukurasa Wake wa Instagram, Diamond Platnumz aliposti video hiyo na kuandika:

https://www.instagram.com/p/BrK67ZVlDFX/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=d9geezbdwlgj

“Natamani BASATA Waniruhusu Kuperfom Mwanza”- Rayvanny

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny ameibuka na kuwaomba tena BASATA wampe ruhusa ya kuperfom wimbo wa Mwanza stejini.

Wiki chache ziliopita Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liliufungia rasmi wimbo wa ‘Mwanza’ wa Rayvanny aliomshirikisha Diamond Platnumz kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kwa kuimba matusi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Rayvanny alisema angetamani sana kwa mara ya kwanza apafomu Wimbo wa Mwanza katika jukwaa la Wasafi Festival lakini anashindwa kutokana na adhabu ya Basata ya kuufungia wimbo huo ambao yeye anakiri kuwa hakuutunga kwa nia ya kupotosha watu bali kuburudisha.

Kiukweli natamani sana wangeniruhusu tu japo nipafomu katika shoo zangu maana mapokezi ya huu wimbo ni makubwa mno mpaka yananifanya nitamani kuupafomu katika jukwaa la Wasafi Festival Jumamosi hii”.

WCB wanategemea kupigwa bonge la shoo kwenye tamasha Lao la Wasafi Festival linalotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumamosi hii tarehe 24 mkoani Mtwara.

Diamond Aiangukia BASATA Aomba Japo Kuperfom ‘Mwanza’ Stejini

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameibuka na kuiomba ruhusa Baraza la Sanaa kutumia wimbo wake walioufungia wa Mwanza kuperfom stejini.

Wiki chache zilizopita wimbo wa ‘Mwanza’ ulitoka lakini mara moja BASATA waliufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kwa kubeba ujumbe wenye lugha ya matusi.

Lakini Diamond Platnumz amefunguka na kuwaomba Basata kuutumia wimbo wao ba Rayvanny wa Mwanza kwenye tamasha lao la Wasafi Festival 2018.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram Diamond ameandika hayo.