“Kukua Kwa Sanaa Haimaanishi Lazima Wasanii Waimbe Matusi, Tubadilike”-Mwana FA

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kuchana Mwana FA amesema kuwa kukua kwa sanaa nchini sio lazima wasanii watunge nyimbo zenye maudhui machafu au video zenye muonekano mbaya kwenye jamii, bali ni kufanya kazi kwa bidii na kwa kufuata kanuni na sheria.

Mwana FA amefunguka hayo alipokuwa anaongelea sakata linalokamata headlines hivi sasa la Wimbo wa Rayvanny na Diamond kufungiwa kutokana na kudaiwa kukiuka maadili ya Kitanzania.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mwana FA alifunguka haya zaidi:

Mimi napenda kuwashauri wasanii kuwa wanapotoa kazi zao wahakikishe wanatoa nyimbo ambazo zitaburudisha Lakini pia zisivuke mipaka ya kuharibu jamii kwasababu ukuaji wa Sanaa sio lazima wasanii watukane kwenye nyimbo au wawe uchi kwenye video zao hapana tubadilike kuna njia nyingi sana zilizo kwenye maadili”.

Mwana FA amesema hayo jana Novemba 14, 2018 muda mfupi baada ya kutoka BASATA ambako alienda kuwaombea msamaha wasanii wa WCB, Diamond na Rayvanny kuhusu kufungiwa wimbo wao wa Mwanza

Diamond Awaomba BASATA Waruhusu Wimbo Wao Upigwe Muda Wa Usiku Watoto Wakiwa Wamelala

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameibuka na kuliangukia Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) liruhusu japo wimbo wao na Rayvanny upigwe usiku watoto wakiwa wamelala.

Siku ya jana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kutokana na maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo hiyo.

Diamond ameibuka na kulalamikia uamuzi huo wa BASATA na kuwaomba wafikirie na kutafuta njia ya kuiacha nyimbo hiyo kuendelea kupigwa kwenye kumbi za starehe na ipigwe mida ya usiku watoto wakiwa wamelala Lakini pia ameomba wimbo huo urudishwe kwenye mtandao wa YouTube.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqHLwGaFvfE/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1j577yw2ugopk

https://www.instagram.com/p/BqHM7WhlEou/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=retbexv8i8mf

 

Rayvanny Afunguka Baada Ya Wimbo Wake na Diamond Kufungiwa na BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny amefunguka kwa Mara ya kwanza tangu wimbo wake wa ‘Mwanza’ aliomshirikisha Diamond Platnumz kufungiwa.

Siku ya jana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) lilitangaza kuufungia wimbo huo kwa madai ya kukiuka maadili ya Kitanzania kutokana na maneno yaliyoimbwa kwenye nyimbo hiyo.

Rayvanny ameibuka na kulalamikia uamuzi huo wa BASATA na kusisitiza kuwa haikuwa maana yao kuimba matusi katika wimbo huo Bali ni Sanaa iliyotumika na kupelekea watu mawazo yao kufika huko.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameandika:

https://www.instagram.com/p/BqG9rwonTtl/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=mo32cxhbwmsv

https://www.instagram.com/p/BqG-WAGHFKG/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=109chbj8a1coh

Rayvanny Awasihi Wasanii Wenzake Kusaidi Wagonjwa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Rayvanny ameibuka na kuwapa wasanii wenzake ambapo amewataka kuwa na moyo wa kusaidia wagonjwa ambao wapo mahospitalini.

Rayvanny amefunguka na kutoa ujumbe wa kuhamasisha watu wasanii na Watanzania wengine waweze kujitoa japo kidogo ili kuwasaidia wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali Hospitalini.

Rayvanny amefunguka hayo baada ya kutembelea katika Hospitali ya Muhimbili kumjulia hali mama  aliyekuwa anasumbuliwa na jicho kutoka Mbeya, ambaye wiki iliyopita video zake zilisambaa mtandaoni zikimuonesha akiomba msaada wa matibabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny ameandika;

Nashukuru Mungu Leo Nimepata Nafasi Kutembelea Hospitali Ya Muhimbili, Kumuangalia Yule Mama mwenye tatizo la jicho. Kwangu Leo imekua kama darasa na Sehemu Ya kujifunza, kutokana na Hali Ya ndugu zetu pale Hospitali.Nilienda Kwa Ajili Ya Yule Mama lakini nikajikuta naenda Kwa Wodi Nzima…. KIDOGO NILICHOKUA NACHO NIKASAIDIA WODI NZIMA…. Maana Ya Mimi kupost Sio kujikweza Ila nikukumbushana Kwa Kidogo Tunachokua nacho Tusiache kusaidia ndugu zetu wenye Magonjwa,Matatizo mbalimbali na Wasiojiweza…. MUNGU AWABARIKI”.

Mke Wangu Hata Akitembea Uchi Sawa tu ;- Rayvanny

Msanii kutoka kundi la WCB  Rayvanny amefunguka na kusema kuwa kwa Dunia ya sasa hivi swala la mavazi kwake  halina shida sana  kwa sababu anajua kuwa Dunia ya sasa hivi mambo ya mavazi kila mtu anachukulia vile anavyoona yeye hivyo hata kama mke wake atavaa nguo za utupu kwake ni sawa tu.

Rayvanny ambae amekuwa akionekana kutulia sana katika swala la mahusiano na mwanamke aliekuwa nae tangu kipindi bado jina lake halijawa kubwa anasema kuwa  mavazi hayatasfiri tabia ya mtu kwa sababu kama mtu ana tabia ya uhuni hata akivaa dela au ushungi basi atakuwa hivyo hivyo hawezi kubadilika.

mtu akiwa mhuni hata vae dela au ushungi muda wote kama kupata wanaume atapata tu, na mavazi kwa sasa hayatasfiri tabia ya mtu lakini ni vile tu mtu anavyovutiwa na muonekano wako.Mimi hata siku moja siwezi kumpangia mke wangu avae nguzo za namna gani vyovyote atakavyo  vaa fresh tu hata aseme kuwa atatoka utupu mi niko poa.

 

 

Rayvanny Athibitisha Kuwa Sababu ya Kusainiwa kwa Mboso WCB

Msanii Rayvanny amefunguka kuwa aliwahi kumshawishi Diamond Platnumz kumsaidi Mbosso ndani ya WCB, Kipindi hicho ambacho msanii huyo alikuwa bado hajasainiwa sehemu yoyote baada ya kutoka Ya Moto band,

Rayvanny amefunguka hayo alipoulizwa anajisikiaje wimbo ‘Jibebe’ ndio ameandaliwa Challenge badala ya wimbo wake Chombo ambao ndio ulikuwa kwenye mipango hiyo hapo awali. “Mbosso Lava Lava ni watu ambao walinikuta Wasafi na pia nilikuwa nawaambia msikate tamaa kila kitu kinaenda sawa. Na nilikuwa naongea na Diamond bhana Mbosso yupo vizuri lakini hana Management  tumsaidiae, mimi ndio nimelazimisha hadi Mbosso amefika pale,” amesema Rayvvnny.

Kabla ya Mbosso kuingia WCB alikuwa akifanya vizuri na kundi la Yamoto Band, wakati Rayvanny kabla ya kusainiwa kwenye lebo hiyo alikuwa Tip Top Connection ingawa hakupata nafasi ya kusikika sana

Kutembea na Wanawake Wengi Maarufu Wala Sio Dili:-Rayvanny

Mwanamuziki kutoka katika kundi la Wcb , Rayvanny amefunguka na kuwa tofauti na watu wengine hasa wasanii wenzake na hawa wale wa katika laevbo yake baaada ya kusema kuwa kwa upande wake haoni kama ni dili kutembea na wanawake tofauti tofauti .

Alipoulizwa kwanini yeye amekaa katika mahusiano na mwanamke aliyezaaa nae kwa muda mrefu tena bila kuwa na skendo wala kiki za ajabu ajabu kama anavyofanya bosi wake, Rayvanny anasema kuwa kwa uande wake maisha yake ni kama ya watu wengine na hataki kutafanya kuwa magumu kwa kuishi maisha ya kisanii sana.

mimi naishi maisha yangu na nina jichukulia kama watu wengine wa kawaida tu, niko sawa na watu wote na wala sitaki kuishi kama vile mimi ninaishi dunia nyingine sitaki kujistress, sio ishu kuwa na wanawake maarufu, mara huyu mara yule.sitaki kuja kujuta baadae.

Rayvanny Asitisha Ushindani Wa Kimavazi na Wasanii Wenzake

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka. WCB Rayvanny anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Chombo’ ameibuka na kutangaza Kumaliza ushindani wake wa kimavazi na wasanii wenzake huku akitaoa yeye ndio mshindi.

Sakata hili lilianza baada ya Dogo Janja kumtaja Rayvanny kama mmoja wa wasanii ambao haelewi anavaaga nini kwani hajui kujipangilia na kupendeza kitendo kilichomkera Rayvanny.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Rayvanny amesema kuwa anaamini ushindani upande wa mavazi anabaki kuwa yeye ni mwenye ujuzi na yuko katika viwango vya kuvaa vitu vya gharama zaidi hivyo hahitaji tena kushindana.

Akizungumzia hatua ya kutotaka tena kujihusisha na ushindani wa mavazi, Rayvanny aliongeza kuwa kwa sasa ana mambo mengi ya maana ya kufanya ikiwemo kujikuza zaidi kimuziki na kuandaa maisha mazuri ya mwanae JayDan kwa sasa na siku za Usoni.

Rayvanny ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chombo’ ambapo ametangaza ujio wa video siku yoyote kuanzia hivi sasa.

 

Rayvanny Afungukia Suala la Rich Mavoko Kutimuliwa WCB

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Rayvanny amefunguka kuhusu Tetesi za Msanii mwenzake Rich Mavoko kutimuliwa kutoka katika label hiyo.

Tetesi za Mavoko kutimuliwa WCB zilianza kusambaa mwezi uliopita baada ya kutoonekana Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na WCB ambao ulijumuisha wasanii wote wa label Lakini pia Mavoko hajaonekana Kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Rayvanny amesema hawezi kuliongelea sana suala hilo kwa sababu sio msemaji lakini amesema Rich Mavoko bado yupo na huwa wanawasiliana naye mara kwa mara:

Ujue sisi tunachekiwa kwenye group, leo kuna tukio hili na hili, so ukiona huyo kakosa ni masuala ya uongozi sana labda angekuwepo Diamond au Babu Tale angeweza kuongea sana lakini Mavoko yupo Wasafi kila siku.

Anakuja, anajiunga kwenye vitu lakini yeye kutokuja siku ile sijui sababu, kama kuna vitu vinavyoendelea ni yeye na uongozi. Mimi siwezi kuongea sana kwa sababu Mavoko ni mwanangu tunaongea tunachati, tunarekodi ngoma zetu“.

Lakini Hata hiyo Babu Tale alieleza kuwa siku hiyo Rich Mavoko alikuwa aki-shoot video ya wimbo wake mpya na kushindwa kuhudhuria.

Rayvanny Amwagia Povu Zito Dogo Janja

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Rayvanny amemwagia povu zito msanii mwenzake Dogo Janja na kumtaka ampe heshima yake.

Siku chache zilizopita Dogo Janja alimtaja Rayvanny kama msanii ambaye hajui kuvaa Kwenye Interview yake na Wasafi Tv na kujitolea kumvalisha.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Rayvanny amejibu tuhuma hizo na kusema kuwa Dogo Janja anakosea kusema hivyo kuni kuna tofauti kati ya mtu kujua kuvaa na mtu kupendeza.

Kuna tofauti kati ya kuvaa na kupendeza, mtu akikuambia hujui kuvaa, anakosea, labda akuambie hujui kupendeza.

Cheni yake ambayo anaivaa sasa hivi, aliivaa Dully Sykes kwenye wimbo wa Sugar Mami. Kwa hiyo ukija kusema eti una uwezo wa kumvalisha Rayvanny hajui kuvaa, no!, unanikosea heshima kwa sababu mimi nimeenda sehemu nyingi nimeona watu wanavaa vitu tofauti”.

Dogo Janja ameendelea kufanya vizuri na ngoma yake mpya ya ‘Banana’ ambayo imeendelea kushika namba moja Kwenye mtandao wa YouTube.

Dogo Janja Aponda Mavazi Ya Rayvanny

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Banana’ Dogo Janja amedai msanii kutoka label ya WCB Rayvanny anamuangusha sana Kwenye suala la mavazi.

Siku za nyuma Dogo Janja ameshawahi kuachia ngoma maalumu kwa ajili kuvaa na kupendeza Inayoitwa ‘Ukivaaje unapendeza”.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kama  akipata fursa ya kumvalisha Rayvanny atafanya hivyo.

Nikiambiwa msanii ambaye niwe namvalisha namchagulia mavazi, nitamchagua Rayvanny huwa ananiangusha sana sometimes.

Kuna muda huwa anapatia halafu kuna muda unaweza ukatema mate kule, anaweza akala njano juu mpaka chini”.

Dogo Janja yupo katika Media Tour kwa ajili ya kutangaza rasmi Single yake mpya ‘Banana’ inayoendelea kufanya vizuri Kwenye chati mbali mbali.

Rayvanny na Fayma Kufunga Ndoa.

Msanii wa muziki kutoka lebel ya WCB Rayvanny ametangaza kufunga ndoa na mzazi mwenzie ambae pia ni mpenzi wake wa siku nyingi fayma .

Rayvanny anaweza kuwa msani wa kwanza kutoka katika lebel hiyo Kutangaza kufunga ndoa na kama ndoa hiyo itakamilika basi pia atakuwa msanii wa kwanza kufunga ndoa na kukaa katika mahusiano yaliyodumu na yasiyokuwa na drama katika lebel hiyo.

Siku za nyuma kidogo msanii huyo aliwahi kuweka oicha nyingi zikimuonyesha akiwa amekwenda nyumbani kwao Mbeya ambapo alikwenda kumtambulisha mpenzi wake huyo na mtoto wao wa kiume.

Rosa Ree is My Favorite Wangu ;-Rayvanny

Msanii wa uziki kutoka wcb  , rayvanny amefunguka na kueleze kwa undani kwanini msanii rosa ree ndio msanii pekee wa kike katika remix ya wimbo wake wa pochi nenen ambayo inapangwa kutoka hivi karibuni.

Rayvanny anasema kuwa amekuwa akivutiwa sana na muziki wa rosa ree na pia katika iwmbo huu rapper pekee angeweza ku-fit kutokana na wimbo ulivyo , alikuwa ni rosa ree na sio mwingineyo.

nawakubali wasichana na wasanii wote wanao-rap lakini rosa ree ni my favorite wangu ,naweza kusema kuwa nilimuona yeye anafaa kutokana na kwamba aina ya wimbo wenyewe wa pochi nene.

ukimsikia anavyo sound kama Nick Minaj sio Nick Minaj hivi,nikaona kabisa kwenye bit kama lile ataleta vibes sana  na ndio maana niliamua kumuweka yeye.

Katika remix ya wimbo huo watakuwepo wasanii kama khaligraph jones, godzilla, rosa ree, izzo business,country boy na wakorintho.

 

Rayvanny Ampigia Salute Alikiba

Mwanamuziki anaefanya vizuri katia anga za muziki Raymond maarufu kama Rayvanny kutoka kundi kubwa nchini WCB amefunguka na kusema kuwa kati ya wasanii wakali anaowakubali nchini ninpamoja na alikiba pamoja na kwamba msanii huyo ni mshindani mkubwa wa bosi wake Diamond Platinumz.

Akiongea na Global online tv, Rayvannya ameorodjesha wasanii wakubwa tanzania ambao anafurahi jinsi wanavyofanya kazi hasa kujituma na kupeperusha bendera ya taifa na kusema kuwa wasanii hao ni pamoja na Diamond platinumz, Alikiba pamoja na Vannesa mdee ambao wamekuwa kama nembo ya taifa.

Katika hali ya kawaida amshabiki wengi wamekuwa wakihisi kuwa wasanii wengine wanapaswa kumchukia Alikiba kwa sababu tu amekuwa mshindaniwa siku nyingi wa bosi wao lakini , wcb imefika sehemu wanaonekana kuona kuwa bifu za wasaniihazijengi na ndio maana kwa sasa wanaonekana kujitahidi kuepukana na maneno ya uchochezi kutoka kwa mashabiki.

 

Dayna Nyange Afunguka Kukoshwa na Rayvanny

Mwanamuziki wa kike wa Bongo fleva Dayna Nyange anayefanya vizuri na ngoma yake ya Salesale amefunguka na kusema amefurahishwa kwa kiasi kikubwa na msanii mwenzake wa Bongo fleva kutoka WCB Rayvanny.

Dayna amesema amekoshwa na msanii mwenzake Rayvanny hii ikiwa ni baada ya kumtaja katika nyimbo yake inayofanya vizuri ndani na nje ya Bongo ‘Makulusa’ ambao amemshirikisha msanii kutoka South Africa anayejulikana kama Dj Maphorisa.

Kwenye wimbo huo wa Makulusa kuna kipande ambacho Rayvanny amemtaja Dayna Nyange ambapo mashairi yake yanaimba hivii “Kipotabo kama Dayna, ana shepu ya birika she got ice cream China, hips from America My baby she is finna”.

Kipotabo Dayna Nyange

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Kupitia kipindi cha The playlist, Dayna alidai labda pengine Rayvanny alimtaja kutokana na vitu anavyovifanya kuendana na ngoma hiyo.

Unajua Dayna amekuwa Kipotabo kwa muda mrefu hajawahi kuongezeka kwaiyo naamini Rayvanny akaona ngoja nimuweke Dayna kwa sababu huyu baadae hawezi kuja kunipa shida , na mimi kwa upande wangu nilifurahi sana japo kila nilikuwa nje ya nchi na sikutegemea kama alikuwa anaweza kufanya kitu kama hicho kwa sababu sikuwa na ukaribu naye kihivyo so I was happy”.

 

Rayvanny Awavuta Jason Derulo na French Montana Kwenye Bongo Fleva

Msanii maarufu wa Bongo fleva kutoka label maarufu Bongo WCB, Rayvanny amezidi kudhihirisha uwezo wake baada ya jana kuachia ngoma yake inayoitwa ‘Tip Toe remix’ aliyoshirikishwa na Jason Derulo huku ndani yake akiwepo French Montana.

Jason Derulo ni msanii maarufu sana nchini Marekani lakini hivyo hivyo rapa maarufu French Montana mwenye Makazi yake nchini Marekani lakini mwenye asili ya Africa kutoka katika nchi ya Morocco.

 

Ngoma ya Jason Derulo ya ‘Tip Toe’ ni moja kati ya ngoma zake ambayo imefanya vizuri na kufikisha jumla ya watazamaji milioni 66 katika mtandao wa YouTube baada ya kuona mafanikio hayo ndipo alipoamua kutoa ‘Remix’ yake ambayo ndio hiyo aliyomshirikisha Rayvanny na French Montana.

Msanii huyo mkali wa wimbo wa kwetu alitangaza kutoka kwa nyimbo hiyo jana ambapo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram maneno haya:

God is good all the time, big thank you to my brother Jason Derulo for this amazing opportunity, Africa to the world, let’s go”.

Miezi michache iliyopita Rayvanny alienda nchini Marekani kwa ajili ya kufanya kazi na Jason Derulo lakini pia alisema atafanya kazi na kundi la Migos muda wowote. Hii hatua kubwa katika kuukuza mziki wetu wa Bongo fleva hakika hongera kwa Rayvanny kwa jitiahada zake.