Diamond Platnumz adaiwa kodi ya zaidi ya Sh. milioni 400

Hitmaker wa Nasema Nawe Diamond Platnumz amejipata kwenye matata baadaya mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia kudai kuwa msanii huyo anadeni la Sh. milioni 400 analodaiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza bungeni Maulid Mtulia aliweka wazi kuwa msanii huyu amekuwa akikwepa kulipa TRA kitu ambacho wasanii wakubwa kama yeye hufanya. Mazungumzo haya yalifanyika bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Diamond Platnumz anadaiwa pesa hizi kwani yeye ni mmoja wa wasanii ambao wanaoingiza pesa nyingi kupitia nyimbo zake lakini inaonekana muimbaji huyo amekuwa akikwepa kupeana pesa hizi kama inavyohitajika kila mwezi.

Hata hivyo Diamond Platnumz hajazungumzia swala hili ambalo limewaacha Watanzania kama wameshangaa.

Diamond Platnumz awaandikia barua wasanii wanaokosoa nyimbo zake

Diamond Platnumz hivi karibuni aliwaandikia wasanii wenzake barua huku akiwasihi wanapoandika nyimbo zao lazima wawe na malengo ya kuwafikia watu wengi na sio watanzania peke yao.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Diamond aliandika huku akitoa mfano wa muziki wake. Kulingana na alichaondika Diamond Platnumz alisema kuwa muziki wake umemfungulia njia za kupiga show nchini ambazo yeye hakuwa anajua anaweza kufika.

Mkali huyu wa bongo aliandika kusema

Leo ningependa nitoe ujumbe huu kwa wasanii wenzangu pendwa… Siku hizi mjini kila mtu anajifanya yeye soko la Muziki analijua sana na bingwa wa kuelekeza na kukosoa nyimbo za watu….Pasipo kujua kuwa kila nyimbo ina soko lake na kila mwanamuziki anapotoa nyimbo anakuwa na malengo ama plan ambayo ameidhamiria…leo ntakupostia baadhi ya nyimbo ambazo wakati nazitoa zilidharauliwa, zilipingwa sana na wanaojifanya wajuaji wa Muziki… pasipo kujua kuwa dhamira ama nini yalikuwa malengo yangu….kwakuwa nilikuwa na imani na kufahamu nikifanyacho basi nikawa nawaekea tu neno #MALENGO na leo hii nyimbo hizo ndio sababu kubwa ya mimi kuwa na Show za nchi ambazo kiukweli sijawai tegemea fika na kufanya show za Uwanjani….. sababu yangu kubwa leo ni kuwasihi wasanii wenzangu kuwa mnapokuwa na kitu ambacho mnamalengo ama target nacho msiogope kukisimamia…lakini pia kuwajuza kuwa kila kanda ina maadhi ya muziki wake ambao unaupenda, hivyo ukitaka kufanikiwa kushika kanda zote usiogope kufanya Muziki tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina “UKIMUONA” Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi zingine… #SimbaInZambia

Diamond Platnumz amuandikia Ray C ujumbe kumpa moyo wa kutokata tamaa katika muziki wake

Ni wengi ambao hawakudhania kuwa Ray C atarudi kufanya muziki tena baada ya kupotea ndani ya madawa ya kulevya. Hata hivyo mrembo huyu amewafurahisha wengi ambao hawakuwa wamekata tamaa kwake.

Mmoja wa hawa ni Diamond Platnumz ambaye amemwandikia ujumbe wa kumtia moyo huku akimsihi kuendelea na muziki wake japo ya kukawia sana bila kutoa nyimbo.

Kupitia mtandao wa Instagram Diamond aliandika kusema…

Ray C

Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali…. Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya….

Diamond aliendelea kwa kusema,

Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku? @rayctanzania

Hata hivyo Ray C ameonyesha kuwa hanamipango ya kuacha muziki tena na kuna uwezekano wa kuenda mbali hivi karibuni.

Mashabiki wa King Kiba wamtolea Barakah the Prince hasira baada ya kumpost Chibu

Ingawa Baraka the Prince alifanya wimbo na King Kiba Nisamehe haamanishi kuwa hawezi msupport Diamond Platnumz. Hata hivyo hivi sivyo mashabiki wa Kiba wanavyofikiria. Hivi Karibuni muimbaji huyu wa Bongo, Baraka the Prince aliupost wimbo mpya wa Diamond Platnumz na kilichofuatia ni matusi kutoka team Kiba.

Soma: Baada ya kufanya collabo na King Kiba, Barakah The Prince aeleza changamoto alizopitia

Barakah The Prince
Barakah The Prince

Mashabiki wengi ambao wamekuwa wakicomment kwa picha hii wanashangazwa na Baraka kupost wimbo huu kwa sababu wengi wanajua Baraka yuko kwenye lebel moja na Alikiba.

Kama mnavyoelewa Kiba na Diamond wamekuwa na beef kwa muda sasa kwa hivyo Baraka asingeweza kupost chochote kuhusu Diamond Platnumz, wengine wamecomment kwa kutopendezwa na post hiyo wengine wamepost kumpongeza.

Kupitia Instagram Barakah the prince aliandika kusema…

Chanzo cha kutengenezewa maden na makaka poa..ila mama alinifunza kukaa kimya..eeehh mungu niokoe vita

Alichosema Mamake Hamisa Mobeto baada ya Zari Hassan kumtolea mwanawe povu

Maneno yamemfika kooni mamake model Hamisa Mobeto baada ya picha kusambaa mitandaoni ikidaiwa bintiye amechora tatuu ya Diamond Platnumz.

Picha hiyo ilizua kero ikuluni,Madale kwa Diamond Platnumz na mpenzi wake Zari Hassan,hadi matusi na maneno yakaporomoshwa kumchafua Hamisa Mobeto.

Hamisa Mobetto
Hamisa Mobetto

Kuhusu stori hii, mamake Mobeto ameshindwa kujizuia.Na inasemekana amejikuta ashamtolea povu hatari sana Zari Hassan kwa sababu ya matusi aliyomtunukia Hamisa.

Akizungumza na gazeti la Global Publishers,mamake Mobeto alisema,’hakuna wakati mgumu kama kuona mtoto wake huyo anazungumziwa vibaya kila wakati katika mitandao ambapo wakati mwingine siyo jambo la kweli zaidi ya kumchafua tu.

Hamisa, Diamond na Zari
Hamisa, Diamond na Zari

Jamani mimi kama mzazi, sidhani kama kuna mzazi yeyote anayeweza kuvumilia kuona mwanaye kila mara yuko kwenye midomo ya watu au kuongelewa vibaya kwenye mitandao ya kijamii kwa vitu ambavyo hajafanya,” alisema.

“Unajua unapomuona Hamisa (Mobeto) amenyamaza, kila wakati wanatafuta kumuwekea jambo baya, kitu ambacho siyo sahihi, mimi sijawahi kuiona hiyo tatuu wanayosema zaidi ya kuona kuwa wanampandikizia maneno tu ya kumchafua, sipendezwi kabisa na tabia hiyo,” amemalizia huku akiwa na uchungu mwingi.

Mashabiki wamponda Diamond Platnumz baada ya kuonyesha cheni zake za mamilioni

Ni kweli kuwa Diamond Platnumz anapesa nyingi hadi imembidi kununua cheni na pete ambazo alilipia Tsh 158 millioni. Alipost picha hizi kupitia mtandao wake wa Instagram hata hivyo si mashabiki wengi walifurahia kitendo hiki na kuacha comments ambazo zilimfanya Diamond Kuwajibu.

Mashabiki hawa walionelea kuwa Diaomond Platnumz angetumia pesa hizo kuwasaidia maskini ambao hawana hata nyumba za kuishi wala chakula cha kula. Diamond na yeye pia aliwajibu kwa kuwatajia mambo ambayo ameweza kufanya kuisaidia jamii ili kuwajulisha kuwa hakuwa mtu selfish.

Aliandika kusema…

Nimejenga nyumba 5 mwaka janaIringa, Misikiti miwili mmoja Morogoro pia nyingine Mtwara na Madrasa tegeta na nyumba ya Imamu mbili na sadaka mbali mbali sasa unataka nitoe ela zote sadaka nami nisifurahishe nasfi? Hebu niombe radhi kwa hilo.

Comment yake ata hivyo haikuwafurahisha mashabiki hao waliondelea kumponda na kumwambia kuwa amekuwa mtu mwenye kiburi na kuwa amesahau alikotoka. Je wewe waonaje?

Diamond Platnumz awaonyesha mashabiki wake Pete na cheni mpya alizozinunua Tsh 158 million

Kweli Diamond Platnumz sio mtu wa mchezo. Mwimbaji huyo wa Tanzania ameaacha mashabiki wake kama wameduwaa baada ya kuonyesha pete na cheni zake mpya alizozinunua millioni 158 pesa za Tanzania.

Ata hivyo hii sio mara ya kwanza ya huyo muimbaji kuaonyesha baadhi ya vitu anavyovimiliki vya thamani ya juu. Kupitia mtandao wake wa Instagram aliandika kusema…

Thanks God for my new GOLD & DIAMONDS collection…i never thought i would be able to hang 50,000$ on my neck

Aliendelea kumshukuru mungu akisema kuwa kila siku anapata baraka amabazo ata yeye mwenyewe haamini kuwa angepata. Kwenye picha nyingine aliandika kusema…

“Thanks God for your daily blessings never thought i would be able to walk with 22,000 $ on my Hand!!!… jus get inspired @sallam_sk don’t hate.”

Tazama hizi cheni na pete hapa chini.

Diamond afunguka kuhusu wimbo wake anao udhamini sana

Diamond Platnumz anajivunia hits kadhaa alizozitoa tangu aanze kuimba. Wimbo wake ‘Mbagala’ ndio ulio mfanya ajulikane Afrika Mashariki.

‘Number One’ ilifanya Diamond ajulikane barani Afrika, Davido alitoa remix na Diamond baadaya ya kuupenda wimbo huo.

Lakini hata hivyo ‘Mbagala’ na ‘Number One’ sio wimbo ambazo Diamond ana dhamini sana kama hit yake ‘Kamwambie’.

Hit maker huyo anasema ‘Kamwambie’ ndio wimbo wake ambao ulimtambulisha kwenye Bongo fleva na ata kumfanya kushinda tuzo kadhaa.

“This song called #KAMWAMBIE , it’s the song which introduced me to the Bongo flavour Market 7 Years back….it also Made me Win Triple Awards, Song of the Year , R&B song of the Year and Upcoming artist of the year,” Diamond aliandika.