Zari na Hamisa Wameingia Tena Kwenye Bifu Kali Baada Ya Kurushiana Maneno Mazito Mtandaoni

Wazazi wenza wa Msanii Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto wameingia tena kwenye bifu zito baada ya kila mmoja kumrushia maneno mwenzake mtandaoni.

Kisa cha ugomvi huo kilianza siku chache zilizopita baada ya Zari na Hamisa kujikuta wana sherehe siku moja nchini Uganda Jana hapo ndipo mashindano yalipoanza huku kila mmoja akijinadi atakuwa juu zaidi huku wakisaidiwa na timu.

Party hizo mbili zilifanyika Jana usiku kwenye kumbi mbili tofauti lakini kwa wakati mmoja. Baada ya party hizo picha zilianza kusambaa mtandaoni huku kila mmoja akijitahidi kuonyesha kuwa alikuwa na nyomi kubwa kuliko mwenzie.

Baada ya muda warembo hao wawili walianza kurushiana maneno katika mtandao wa Snapchat na Instagram huku kila mmoja  akimtambishia mwenzie kuwa amepata mafanikio zaidi ya mwenzake lakini pua walifikia hadi hatua ya kurushiana maneno ya kashfa.

Zari ameibuka akumrushia maneno haya Hamisa kupitia kurasa yake ya Snapchat:

Kuna tofauti kubwa Kati ya tembo na mbu, baraka juu ya  baraka Asante Mungu, Watu wenyewe ni maslay cartoons, wezi wa wanaume za watu wanataka waishi kwa kutegemea child support lakini wapi hawawezi kushindana na mimi, wameenda mpaka kisutu lakini wameambulia patupu”.

Baada ya kurushiwa maneno hayo Hamisa alishindwa kuvumilia kwani na yeye amefunguka ya kwake na kumrushia Zari madongo:

Siwezi kubishana na bibi yangu, Mimi nina umri wa binti yako wa kwanza unemzidi mama yangu miaka 3…Mama yangu amenifundisha kuheshimu wakubwa walionizidi alafu ungejiamini wako angetulia…alaku wewe endelea kulilia kuvalishwa pete wakati mwenzako mume wa mtu tayari”.

 

Hamisa Afunika Kwa Mapokezi Aliyopata Nchini Uganda (picha na video)

Mwanamitindo na muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto ambaye pia ni mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz ameingia nchini Uganda na amepokelewa kama staa wa mbele vile.

Hamisa Mobetto ameingia nchini Uganda Jana mchana kwa ajili ya kuhost au kusherehesha sherehe inayoenda kwa jina la Gal Power Party: Women empowerment itakayofanyika Leo tarehe 21 December.

Latino kinachovutia zaidi party hiyo itafanyika siku moja na wakati mmoja na mke mwenzie au hasimu wake Zari the boss lady ambaye na yeye yupo nchini Uganda kwaajili ya kuhost party yake Zari All White party. Lakini pia kivutio ni kuwa kundi la Rich Gang lililokuwa linaongozwa na Ivan aliyekuwa mume wa Zari limeamua kwenda kwa Hamisa.

Hizi ni baadhi ya picha kuonyesha mapokezi mazito aliyopata Hamisa nchini Uganda Jana:

 

 

 

 

 

 

 

 

Wanigeria Wamtolea Hamisa Mobetto Povu Zito Baada ya Kusema Yeye Mzuri Kuliko Wao

Mwanamitindo na muigizaji maarufu Bongo Hamisa Mobetto ambaye pia ni mama mtoto wa mwanamuziki Diamond Platnumz, ametolewa povu zito na Wanigeria baada ya kudai kuwa yeye ndio msichana mrembo Nigeria.

Wikiendi hii Hamisa alisafiri kwenda nchini Nigeria ambako aliweka wazi kuwa ameenda kufanya kazi za mitindo na designer Mkubwa nchini humo. Ambapo Hamisa aliandika kuwa amealikwa na mbunifu huyo wa mavazi kwaajili ya kupiga picha na kumtangazia mavazi yake.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa aliweka picha yake ambayo alikuwa anarembwa na time yake lakini maneno yaliyosindikiza picha ndio yaliyozua utata na kusababisha Wanigeria kumjia juu na kumpa kichambo cha haja.

Hamisa aliandika maneno haya;

The Most Beautiful girl in Nigeria is Tanzanian”.

Baada ya kuandika maneno hayo yaliyomaanisga kuwa msichana mzuri nchini Nigeria ni msichana wa Kitanzania, hapo ndipo mtandao wa udaku mtandaoni wa nchini Nigeria unaoitwa Instablog9ja, ulizinyaka habari hizo na kuzirusha kwenye ukurasa wao wa Instagram jambo lililozua tafrani kwani Wanigeria wamemchamba Hamisa hadi akaweka ukurasa wake wa Instagram private.

Wanigeria walieleza kuwa wamekerwa na Hamisa kwenda nchini kwao na kuanza kuwadharau wanawake wa nchi hiyo na kujiona kuwa yeye ndio msichana mzuri wakati kuna wasichana wengi ambao ni Wanigeria.

 

 

Hamisa Amefunguka Kuhusu Bifu Lake na Lulu

Mwanamitindo na muigizaji wa Bongo movie, Hamisa Mobetto amemzungumzia muigizaji mwenzake Elizabeth ‘Lulu’ Michael aliyehukumiwa wiki iliyopita miaka miwili jela pamoja na uhusiano wao.

Siku za nyuma Hamisa na Lulu walikuwa na bifu kubwa tu ambalo lilitokana na wao kugombania mwanaume mmoja ambaye ni Majizzo. Hamisa alikuwa na uhusiano kwanza na Majizzo ambao ulipelekea kuzaa mtoto mmoja lakini baadae tena Majizzo aliachana na Hamisa na kuanzisha uhusiano na Lulu kitendo kilichopelekea mwanzo wa bifu la warembo hao wawili huku Hamisa akimtuhumu Lulu kwa kumuibia bwana ake hali iliyopelekea wawili hao kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya Lulu kuhukumiwa Hamisa aliwashtua wengi baada ya kujishusha na kudai anamuonea huruma na hadi kufikia hatua ya kudai kuwa anampenda Lulu. Kitendo hiki kiliwaacha watu wengi midomo wazi na kwenye mahojiano na Millard Ayo alifunguka yafuatayo kuhusu uhusiano wake na Lulu:

Mimi kumposti Lulu ni kitu kidogo sana kwa sababu mwanangu Fantasy anapokuwa kwa baba yake Lulu naye anakuwepo ikimaanisha kuwa ni mama yake mdogo au mama wa kambo kwa mwanangu, lakini watu wanapenda tu kukuza mambo kwenye mitandao ya kijamii just because people don’t see each other doesn’t mean wana ugomvi mwisho wa siku mimi sina ugomvi na mtu na isitoshe nilivyo mposti Lulu ilikuwa ni kwa nia njema kabisa na kusema ukweli nimeumia Lulu kufungwa kwa sababu hata nilikuwa nikisafiri najua kabisa Fantasy nikimuacha na baba yake kunakuwa na mwanamke anamuangalia ambaye ni Lulu kwa sababu mimi siamini sana wafanyakazi wa ndani”.

Hamisa alifunguka hayo baada ya watu wengi kumuita mnafki baada ya kumuongelea vizuri Lulu lakini baadae alionekana kamualika kwenye sherehe yake Mama Kanumba ambaye anajulikana kama ni Hasimu Mkubwa wa Lulu.

Hamisa Mobetto: Najua Watu Wataniona Mnafki Lakini Nampenda Lulu

Mwanamitindo na mzazi mwenza wa Mwanamuziki Diamond, Hamisa Mobetto amefunguka tena kuhusu kesi ya Lulu Michael na kudai kuwa anampenda sana Lulu ingawa anajua watu wengi watamuona kama mnafki.

Lulu na Hamisa siku zote wamesemekana kuwa maadui kutokana na Lulu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Majizzo ambaye ni baba wa mtoto wa kwanza wa Hamisa aitwaye Fantasy. Habari za chini ya kapeti zinadai kuwa hapo zamani Hamisa na Lulu walikuwa marafiki lakini urafiki huo uliingia doa na kugeuka maadui baada ya Hamisa kuachana na Majizzo kisha Lulu kuanza kutembea naye.

Lakini juzi baada ya kifungo cha Lulu, Hamisa alimuandikia Lulu ujumbe huku akidai kuwa atamiss. Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Tv, Hamisa amedai kuwa pamoja na hayo yote bado anampenda Lulu:

Namjua Lulu and then namjua Mama Kanumba na upande wa Kanumba, miaka miwili nyuma mimi na Lulu tulikuwa na ugomvi ambao kila mtu anajua sababu sio lazima niongee hapa lakini linapotokea jambo kama hili lililomkuta Lulu  ambalo sio zuri ukaongea kitu fulani wapo watakaochukulia kwa nia mbaya au wakakuona mnafki ila kwangu mimi sina naye tatizo naweza sema kuwa nampenda hasa amekuwa mtu mzuri kwa mwanangu yaani Fantansy ukimuonesha tu picha ya Lulu anafurahi anajua ni anti yake”.

Baada ya Hamisa kuandika ujumbe wa kumlilia Lulu alipofungwa miaka miwili watu wengi waliibuka na kumuita mnafki kwa kile walichodai kuwa Hamisa amesubiri mpaka Lulu amefungwa ndo kusema hawana ugomvi.

 

 

Baada Ya Kuzikosa Pesa Za Diamond, Hamisa Mobetto Kaja Na Hili

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka mara baada ya habari kusambaa kuwa mahakama imetupilia mbali madai yake, ametangaza kuja na duka lake la kuuza nguo.

Mara baada ya kujifungua mtoto wa Diamond miezi mitatu iliyopita, Hamisa na Diamond waliingia katika mgogoro ambao ulipelekea Diamond kukataa kutoa pesa kwa ajili ya kumuhudumia mtoto kitu kilichomsukuma Hamisa kutafuta wakili wa kumwakilisha na kuenda kumfungulia kesi ya madai Diamond Mahakamani Kisutu.

Siku ya Ijumaa, tarehe kumi kesi hiyo ilitupiliwa mbali na hakimu mkazi Kisutu kwa kile kilichodaiwa kuwa ni makosa katika hati ya awali ya mashtaka ambapo wakili wa Mobetto, Good luck Walter alidai kuwa karani wao alikosea kuchapa hati hiyo ikiwa ni kosa la kibinadamu kabisa.

Kwa kipindi kirefu mashabiki wamekuwa wakimtupia vijembe Hamisa kuwa ni mwanamke asiyetaka kujishughulisha kuwa hana kitu hana biashara yoyote zaidi ya kutegemea matunzo kutoka kwa baba za watoto wake Majizzo na Diamond.

Lakini mapema wiki hii kupitia ukurasa wake wa instagram tayari Hamisa amefunguka na kudai kuwa Ana mpango wa kufungua duka lake hilo la nguo na pia amekataa tuhuma alizokuwa anarushiwa kuwa amejibweteka tu kwani tayari ana biashara zake tangu siku nyingi ambazo watu wengi hawazijui.

 Instead of being rich at once it is better to be poor first, kwa takribani miaka minne sasa nimekuwa nikifanya biashara ya kuuza nguo (kitu ambacho watu wengi hawakijui) Imekuwa ndio biashata inayonilisha na kunitunza mimi na familia yangu, nilikuwa napiga picha naweka nguo zangu kwa baadhi yq maduka yenye majina makubwa hapa mjini wananiuzia na ninapata pesa kwa njia hiyo, watu wengine walikuwa wananidhihaki sana kwa kusema oh ananipa picha tu ndio anachojua bila kujua kinachoendelea. Ata ourclosettz ilikuwa mali yangu lakini hakuna anayejua. Sasa habari njema nimeaua kufungua duka langu mwenyewe litakaloitwa Mobettostyles naomba support yenu tafadhali”.

Mange Afunguka Kuhusiana na Ugonjwa Uliompata Hamisa na Kumpa Shavu Baada Ya Kushinda Tuzo

Mshawishi wa mambo ya siasa mtandaoni, Mange Kimambi ameibuka na kumtetea mrembo Hamisa Mobetto baada ya kugubikwa na skendo baada ya kusemekana amechanganyikiwa.

Tangu wiki iliyopita habari zilienea mtandaoni kuwa mzazi mwenxie na Diamond, Hamisa Mobetto amechanganyikiwa na kile kilichohusishwa na Imani za kishirikina huku watu wengi wakidai kuwa Hamisa ametupiwa uchawi na hivyo kusababisha yeye kuwa kama chizi.

Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange alifunguka kuwa habari za Hamisa kuchanganyikiwa kwa kulogwa zinasambazwa na maadui tu bali ukweli ni kuwa Hamisa alikuwa anaumwa malaria:

Hamisa alipatwa na malaria kaliii ikapanda hadi kichwani, ila hadi hivi sasa anaendelea vizuri. Hizi stori za kuwa amegeuka chizi and so forth ni chumvi tupu zimeongezwa…..But its true alikuwa anaumwa na ishu ni malaria kali ambayo ilipanda kichwani, ila sasa hivi anaendelea vizuri tuendelee kumuombea”.

Pia Mange alimpongeza Hamisa kwa kushinda tuzo aliyokuwa anagombania na washiriki wengine. Ambapi Mange aliandika

“Hongera kwa kushinda tuzo Toto”

Jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa alitangaza kuwa ameshinda tuzo aliyokuwa anawania;

 

Well…. what can I say? team Hamisa Mobetto we won babies Thank you a guys soo sooo much for your votes Ahsaaanteni saana stardqt awards thank you babies, Ila nini tuzo yetu kuifuata iko pale pale”.

 

 

Hamisa Mobetto Anaumwa Gonjwa Zito, Inadaiwa Kachanganyikiwa

Mwanamitindo na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto anadaiwa kuwa yupo katika kipindi kigumu kwani inasemekana kuwa anaumwa na amechanganyikiwa na kilichomtokea kinahusishwa na imani za kishirikina.

Wiki iliyopita mtandao wa Global Tv uliripoti kuwa umati wa watu ulikusanyika nyumbani anakoishi Hamisa na mama yake Mbezi beach Jogoo, alifunga mtaa baada ya kusemekana kukutwa kwa vitu vinavyohusishwa na imani za kishirikina jambo lilotisha wengi.

Baada ya sakata hilo kutokea majirani waliita vyombo vya habari na kudai kuwa vitu vilivyokuwa vinaonekana viliwatia shaka maana vilikaa kama vifaa vya uchawi si uchawi baadhi ya vitu hivyo vilivyofungwa kwenye kabrasha vilikuwa ni Nazi, ndizi, hirizi dalili zote za mambo ya kishirikina.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mama mzazi wa Hamisa aliwaomba watu wamuombee mwanaye ambapo aliandika maneno haya kutoka katika kitabu kitakatifu cha Quran na akiwasihi watu wamuombee binti yake:

Good and Evil deeds are not equal, Repel evil with what is better; then you will see that one who was once your enemy has become your dearest friend (Qur’an 41:34) pray for my adorable daughter Hamisa.

Watu mbali mbali wamedai Hamisa anaumwa lakini haumwi malaria au taifodi Bali amedata kabisa na inasemekana mpaka muda huu amepelekwa kwa mashekhe ambao wanamuombea visomo mbali mbali huku mama yake akizidi kuwasihi wait waendelee kumuweka kwenye maombi yao ingawa familia yake haijatoa tamko lolote kutokana na afya yake .

 

Familia Yaingilia Kati Bifu La Zari Na Hamisa

Hakuna ubishi kuwa Zari adui yake mkubwa hivi sasa ni Hamisa hiyo ilianza tangu siku Hamisa alivyoanza kutembea na Diamond huku akijua wazi kuwa ni baba watoto wake.

Bifu hilo lilianza rasmi mwaka 2015 pale ambapo Zari alipata taarifa kuwa Hamisa anatembea na Diamond. Bifu lilipamba moto miezi miwili uliopita baada ya Zari kugundua kuwa Diamond amezaa na Hamisa na hapo walianza kurushiana vijembe mtandaoni

Zari na Hamisa wamedaiwa kuwekwa kitimoto ili waache kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii, gazeti la Risasi limeelezwa kwa nyakati tofauti kila mmoja aliwekwa kitimoto na ndugu wa msanii wa mzazi mwenzao na kutakiwa waache malumbano hayo mtandaoni kwani hayaleti picha nzuri kwao ukizingatia kosa limeshafanyika na amekiri hadharani.

Walichoelezwa ni kwamba tu waache kutupiana vijembe mtandaoni kwani wao hivi sasa hata kama hawata kuwa wake wenza lakini tayari Diamond ana damu yake kwa Hamisa, ameshakiri aliteleza na kujikuta kwenye uhusiano naye hadi kufikia hatua ya kuzaa naye. Mtoto ameshazaliwa na ni damu ya msanii na mwisho wa siku atalazimika kumpa mahitaji yake kama mwanaye hata kama hataendeleza mahusiano na mwanaye”.

Chanzo hiko ambacho ni mwana familia wa karibu aliendelea kutiririka kuwa sasa hivi wanashukuru Mungu, kwani warembo hao wawili kila mmoja kwa wakati wake ameelewa somo na hivyo kuacha kurushiana maneno maneno kwenye mitandao ya kijamii maana zamani ilikuwa haipiti siku mbili bila kutibuana mitandaoni.

Hamisa Mobetto na Vera Sidika Wavurugana Kisa Zari

Hamisa Mobetto na Mrembo kutoka Kenya Vera Sidika maarufu kama Queen Vee, wameingia katika vita ya maneno mtandaoni kisa ni Zari.

Sakata hili lilianza baada ya Hamisa ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya kukutana na Vera na kumrekodi wakati wanasalimiana na kisha kutuma hiyo video Snapchat. Tendo hilo liligeuka ugomvi kwani inajulikana wazi kuwa Vera ni rafiki kipenzi wa Zari ambaye ni hasimu mkubwa wa Hamisa (kwani wote wamezaa na Diamond)

Baada ya Video hiyo kusambaa mtandaoni mashabiki wa Zari walimjia juu Vera kwa kitendo chake cha kuwa na urafiki na Hamisa wakati ni adui wa shoga yake Zari. Baada ya kuona hilo ndipo Vera alipoingia mtandaoni na kuanza kujitetea kuwa hana urafiki na Hamisa bali alisimama kumsalimia mtu mwingine aliyekuwa na Hamisa na hakujua kuwa anarekodiwa na Hamisa.

Vera amedai hana urafiki na Hamisa na anashangaa kwanini alimpiga picha bila ruhusa.

Baada ya kuona hivyo Hamisa alimjia mjuu Vera na kudai kuwa aache uongo kwani alijua wazi kuwa alimrekodi na kabla hajaituma video ile alimuonyesha na akakubali, pia Hamisa amedai Vera alimuomba amtafutie mashabiki Tanzania pia alimualika Nyumbani kwake akamtembelee yaani kwa kifupi walikuwa mashoga ila saivi anamruka kwaajili anamuogopa Zari.

Hamisa amchana kuwa kwa sababu ana urafiki na Zari hana haki ya kumsema vibaya

Sakata halikuishia hapo kwani Hamisa alimrushia maneno Vera kuwa ni mtu mzima ovyo mwenye maziwa fake na kajichubua na Beta kamsema Hamisa kwa kitendo chake cha kuzaa na wanaume wenye hela ili wamsaidie maishani kwani hana kazi yoyote.

Vera akimchana live Hamisa
Hamisa akimpa makavu Vera

Mpaka sasa Zari hajachangia lolote juu ya bifu hili je unahisi nani yupo sahihi?

 

 

 

Baba Diamond Amshauri Zari Amvumilie Diamond Kwa Mapungufu yake

Baba mzazi wa Mwanamuziki Diamond Platnumz Mzee Abdul ameibuka na kumshauri Zari aendelee tu kumvumilia Diamond kwa makosa aliyoyafanya.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Mllard Ayo Baba Diamond alipoulizwa akikutana na Zari atamshauri nini kuhusu mtoto wake ndipo aliposema kuwa atamshauri awe mvumilivu.

Baba Diamond amesema;

“Kwanza awe mvumilivu kwani mtoto wa kiume anakua mtu wa kudanganywa, mpotofu na ilimradi kashaambiwa kuna mke mwenzie basi awe mvumilivu ila kikubwa tu kuwe na heshima na adabu Zari kama Zari na Hamisa kama Hamisa waheshimiane wawe pamoja waangalie maisha tu yanaenda kama kawaida”.

Pia Mzee Abdul aliendelea kusema:

“Zari mi namwambia asipende kuwasikiliza waswahili ilimradi aangalie yake yanamwendea vizuri na Hamisa naye asipende kusikiliza ya Waswahili akae aangalie yake aendelee vizuri maana sisi waswahili kila neno linakuwa baya kwetu hamna neno zuri na mara nyingi tunakuwa hatupendani kupendeana mema mtu anapenda mwengine haaribikiwe asemwe tu, ila wakae pamoja tu waangalie haya maisha leo tupo kesho hatupo”.

Baba Diamond pia alimuomba Zari kama kuna uwezekano basi apewe nafasi awaone wajukuu zake akimaanisha Latiffah na Nilllan ambao amekiri hajawahi kuwaona kutokana na kutokuwa na  uhusiano mbovu na mtoto wake Diamond.

Baba Diamond aliongeza;

“Mi napenda kumwambia Zari nikiwa mimi kama mimi Baba Diamond aniletee wajukuu zangu kwanza niwaone au sio lazima nianiletee anaweza hata akaniambia sehemu gani naweza niweze kuenda kuwaona wajukuu zangu”.

Mange: Wote Wanaomkosoa Hamisa Kuzaa na Diamond Wanamuonea Wivu

Mchambuzi na mdau mkubwa wa Siasa mtandaoni Mange Kimambi amewajia juu wale wote wanaomsakama Hamisa Mobeto kwa kitendo cha kuvujisha picha na video za faragha wakiwa na Diamond.

Tangu sakata Diamond na Hamisa litokee watu mbalimbali wamekuwana mitazamo tofauti kuhusiana na kilichotokea huku watu wengi wameenda upande wa Diamond na kumsakama sana Hamisa na kumuita majina mabaya kwa kitendo chake cha kuzaa na Diamond huku akijua wazi kuwa yuko kwenye uhusianao na Zari.

Mange amekuja juu na kuwasema wotw wanaomsema vibaya na kumuona kama shujaa kwa kitendo chake cha kuhakikisha kuwa Diamond anamkubali mtoto wao hadharani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliongea yafuatayo:

“Hamisa usikae kujutia ulichokifanya, acha waongee but you did the right thing for your child hao wanaosema haujui kula na kipofu ndo magolddiger, wewe ungekuwa golddiger ungekaa kimya ule vyako kimya kimya lakini uliamua kumpigania mwanao bila kujali. Najua ulijua tangia mwanzoni kuipeleka issue public itamuuzi Diamond lakini hata baada ya vitisho alivyokupa still uliamua  kufanya ulichokifanya. Umemsaidia sana mtoto wako unajua watu hawajui watoto wa kufichwa na baba zao wanaishije? hao watoto wana kuwa messed up maisha yao yote.Anapita nje ya jumba la babake lakini hawezi ingia kwasababu siri itajulikana hata kama baba yake anawasiliana naye kwa kuficha still itamsumbua mno mtot kujiuliza why yeye anafichwa wenzie hawafichwi yeye alikosa nini. na kibaya zaidi siku baba akifa mirathi hapati kitu kwa sababu baba hajawahi kumtambulisha lakini leo hii Diamond akifa Dylan atapata mirathi sawa na Tiffah kwa hilo hongera Hamisa”.

Pia Mange amemwambia Hamisa wale wote wanaomsema kwa kuzaa na Diamond wanamuonea wivu kwasababu wanajua mtoto wake ataishi maisha mazuri bila wasiwasi na pia wanaona wivu kwasababu Hamisa tayari amezaa na mmiliki wa stesheni ya EFM Majizzo ambaye pia ni tajiri kwahiyo wanajua wazi kuwa baba wote wa watoto wake wawili ni watu wenye uwezo kifedha.

Zari Amsamehe Diamond,Wamerudiana (picha ndani)

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu sakata la Diamond na Zari lichukue nafasi, baada Diamond kuwa na mahusiano ya siri na Hamisa kufikia hatua ya kumzalisha mtoto na kumkubali mtoto na Zari kutumia mitandao ya kijamii kudai kuwa hajamsamehe hatimaye Zari amemsamehe mpenzi wake.

Tarehe 23 jumamosi ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Zari  ambapo Diamond kwa kupitia ukurasa wake wa instagram aliweka ujumbe huu:

“Uzuri na urembo pengine ningetembea baadhi wanao pia. Lakini akili hekima pamoja na roho yako ya kwenye shida na raha kwangu ndio kitu pekee kinachonifanay nikupende na kukuthamini zaidi kadri siku zinavyozidi kuenda…wanaposema kwenye kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke imara hawamaanishsi anapika na kuosha vyombo hapaana ni mwanamke mwenyekuwa bega kwa bega na mpenziwe kwenye shida na raha…Happy birthday General”.

Siku hiyo kimya kimya Diamond alisafiri mpaka Afrika ya kusini ambako Zari yupo na kuweka picha mtandaoni akicheza na watoto wao Latifah na Nillan. Baada ya muda waliweka video na picha mbalimbali wakiwaonyesha wapendanao hao wakikumbatiana na kuweka wazi kuwa wamerudiana.

Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwa Diamond na Zari:

1. Diamond na Zari wakienda kwenye sherehe ya Zari (Birthday dinner)
2. Diamond akiwa amelala na binti yake Latifah
3. Diamond akiwa anacheza na mtoto wake Nillan (Daddy son moments)

Pamoja na hayo yote yaliyotokea Zari amekiri kuwa ameamua kumsamehe Diamond ili waendelee kulea familia yao ikiwemo watoto wa Ivan, kwani Diamond ameshakuwa baba kwao na pia Diamond alikiri kutorudia kosa tena.

Shilole Amponda Hamisa na Kumsifia Zari

Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole Kiuno amefungukia suala la Hamisa na Zari na kuweka neno lake. Kama ilivyokuwa kwa wasanii wengi wametoa maoni yao juu ya jambo hili Shilole pia amefunguka na kuonyesha wazi yupo upande wa Zari na kumponda Hamisa.

Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole amefunguka kuwa kitendo alichofanya Hamisa kimewadhalilisha wanawake wote kwani  amemtumia mtoto wake kutafuta kiki.

Shilole amefunguka;

“Mwanamke asiyejielewa ndio hutumia mwili wake kujidhalilisha na kuwatumia watoto malaika wasi na kosa kutafuta kiki. Mwanaume akikupenda atakuweka ndani atakuthamini. Kinyume na hapo mtatumiana kwa maslahi yenu binafsi. Ukiwa mwizi unakuwa hata na heshima kwa mwenye mali yake ya nini mpaka udhalilishwe na mwanaume ijulikane hupendwi ila umetumiwa tu. Vinginevyo hata huduma unayopata kwa wiki utaisikia bombani. Kwani haiwezekani mwanamke kufight na kutulia na watoto wako mpaka utengeneze drama? Hebu tubadilikeni jamani huu ni u GOLD DIGGER unatudhalilisha tu. Aggh mi nakereka tu hebu niendelee na umama ntilie wangu au sijui na mimi nitafute wababa wa watoto wangu tuanza drama”.

Kwa upande mwingine Shilole amemposti Zari na kumuonyesha yuko upande wake na anamkubali yeye. Shilole kaweka picha ya zari na maandishi “Ijumaa Kareem! Mashallah umependeza wifi”.

Zari na Hamisa Wazidi Kuvurugana Kisa Diamond

Baada ya kumalizika kwa utata wa muda mrefu baada Diamond kukiri kuwa ni baba  wa mtoto wa Hamisa, mashabiki walidhani sakata hilo limeisha na halitasikika tena lakini imekuwa tofauti na matarajio ya wengi kwani picha ndo kwanza kama linaanza kwani sakata hilo limechukua sura mpya.

Zari na Hamisa ambao kwa sasa wote ni mama watoto wa Diamond wameonyeshana chuki kwa kupitia mtandao wa kijamii Snapchat,huku wakiweka wazi  kuwa tusitegemee kuwaona wakiwa marafiki mda wowote kuanzia sasa. Hamisa kwa kudhani kuwa mtoto wake Dylan ameshakuwa na undugu na watoto wa Zari na Diamond Nillan na Tiffah akaamua kuwafata (follow) kwenye instagram kwakutumia ukurasa wa Dyla lakini Zari hakufuraishwa hivo kwa kupitia Snapchat akamwambia Hamisa amuachie watoto wake na wazimu wake unahitaji kupelekwa hodi ya machizi

Kupitia Snapchat Zari aliandika;

“Laki 2 stop following my kids lol, Your obsession needs a mental institution. Like hell?”.

Baada ya kuona hivyo Hamisa ilibidi awa-unfollow watoto wa Zari na kuandika haya kwenye Snapchat;

“Na kama kuna mwanamke mwingine unampenda zaidi yangu…….Bai mwambie mzaa chema shkamoo”.

“Waambie waliopanga mwenye nyumba kaja ndani……Ana meremeta”.

Ingawa watu wengi wangependa kuwaona wanawake hawa wanapatana kwa sababu tu ya watoto wao kwani wote baba yao ni mmoja hivyo wakiwa na maelewano angalau watoto watakua wakijuana kama ni ndugu.

Zari Ajibu Mapigo Baada ya Sakata la Jana

Baada ya Msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ kukiri kuzaa mtoto na mwanamitindo Hamisa Mobetto, hatimaye mama watoto wake Zarinah Hassan azidi kumuweka njia panda juu ya uhusiano wao.

Mwanamama huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameeleza kupokea ushauri uliotolewa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii. “Watu wakiamua kuchepuka au kudanganya ni sawa na kujipotezea muda, ingawa wanahisi wanakuchezea wewe, hivyo usikate tamaa na kujilaumu wewe kwa ajili ya makosa ya watu wengine, maisha lazima yaendelee.

“Mambo yaliyotokea hayawezi kunipungizia hadhi yangu, usijilaumu kwa mambo yaliyotokea, zingatia malengo yako na kufanya maisha yako yaendelee”.am edema Zari.

Amesema kuwa yale yote yaliyosemwa katika sakata hili yanabaki yalivyo na muda huu anaamua kuyaweka kando na kuelekeza nguvu zake katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Sakata hili limeibuka siku moja baada ya ya Zari kujibu mapigo katika mtandao wa Snapchat akionya asihusishwe na kitendo alichokifanya Diamond, cha kuzaa na Hamisa Mobetto.

Awali Katika maelezo yake mwanamuziki Diamond alisema kuwa ameshazungumza na mpenzi wake huyo kuhusiana na  mtoto aliyezaa na Hamisa na kwamba ameelewa na  hakuna tatizo tena.