Rammy Galis Kumkatia Fungu La Pesa Mtoto wa Masogange

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis ambaye alijizolea umaarufu kipindi cha nyuma baada ya kuwa Kwenye uhusiano wa kimapenzi na Marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.

Rammy Galis amefunguka na kudai kuwa amekusudia kumpa fungu la pesa Sania ambaye ni mtoto wa Marehemu Agnes mara baada ya kuzindua filamu aliyoigiza naye.

Kwenye mahojiano na Planet Bongo ya East Africa Radio, Rammy amesema atahakikisha fungu hilo la pesa atamkabidhi mtoto Sania mwenyewe kutokana na kazi aliyofanya mama yake kwenye filamu hiyo:

Kwanza nisingependa kutangaza rasmi kiasi ambacho kitamfikia kwa sababu sijui filamu mauzo yake yatakuaje lakini mimi kama Rammy galis nitatoa kile ambacho Mungu atanibariki katika filamu hii, kutakuwa na asilimia kadhaa ambayo nitaiweka kwa niaba ya mtoto”.

Lakini pia Rammy Galis ameweka wazi kuwa anasubiri Kwanza muda upite ili watu wasahau machungu ya msiba ndipo akafanye uzinduzi maana asije akaambiwa anatafuta kiki.

Agnes Masogange aliaga dunia wiki chache zilizopita baada ya kuugua ghafla.

Familia Haitapewa Michango Ya Marehemu Masogange-Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya Agnes Masogange amesema pesa za rambi rambi zilizochangwa hazitapewa kwa familia.

Siku ya jana familia ya Masogange ililalamika kuwa hwajaona hata senti ya fedha ambayo wasanii wa Bongo movie waliochanga kwa ajili ya kumsomesha mtoto wa marehemu anayeitwa Sania.

Steve Nyerere amefungukia tuhuma hizo za kutokabidhi pesa hizo kwa ndugu wa Masogange na kusema kuwa pesa hizo haziwezi kukabidhiwa kwa familia.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv, Steve Nyerere amesema pesa hizo ambazo ni kiasi cha shilingi milioni mbili zimechangwa kwa ajili ya kumsaidia mtoto atakapoanza shule hapo mwakani.

Lakini pia Steve ameitaka familia ya Masogange iendelee kushukuru kwa mchango waliotoa kwa ajili ya kumzika ndugu yao na waache kuulizia Michango  ya pesa kwani sio ya kwao bali ni pesa za mtoto.

Familia Ya Agnes Masogange Yadai Haijapokea Michango Ya Marehemu

Familia ya marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ imelalamika kuwa haijapokea michango yoyote iliyokusanywa kipindi cha msiba wiki chache zilizopita.

Ndugu wa marehemu Agnes Masogange wakiwemo wifi zake ambao ndio wanaishi na mtoto mmoja wa Marehemu anayeitwa Sania wamesema hawajapata taarifa zozote juu ya fedha ambazo zilichangwa na Kamati ya wasanii kwa ajili ya malezi ya mtoto.

Kwenye mahojiano waliofanya na Planet Bongo ya East Africa Radio, mmoja wa ndugu hao aliyejitambulisha kwa jina la Sada, wamesema hawajapata taarifa zozote kutoka kwa kamati hiyo iliyoundwa na wasanii ambayo pia ilisimamia kwa kiasi kikubwa mazishi ya Agnes.

Toka tumekuja hatujapata taarifa yoyote bado hatujawasiiana nao mpaka dakika hii labda mpaka tuwatafute”.

Lakini pia familia hiyo imesema ina mpango wa kuendelea kumlea mtoto huyo kwani hata kipindi cha uhai wa mama yake  walikuwa wanamlea.

 

Agnes Masogange Alikuwa Mtu Wa Watu- Young Dee

Staa wa Bongo fleva David Genzi maarufu kama Young Dee amefunguka na kusema kuwa marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ alikuwa mtu wa watu sana.

Ikiwa imepita wiki moja sasa tangu Masogange aage dunia mastaa wenzake bado wanaendelea kumkumbuka na kumlilia huku ikionekana wazi kabisa kuwa itakuwa ngumu kuziba pengo lake.

Kwenye mahojiano na Championi Jumatano, Young Dee alisema kipindi cha uhai wake, Masogange alikuwa ni mtu wa watu ambaye alikuwa hapendi ugomvi na hajawahi kusikia akigombana na mtu japo yeye hajawahi kufanya naye kazi.

Japo sijawahi kufanya naye kazi, lakini alikuwa mtu wa watu kwani sijawahi kusikia akigombana na mtu yeyote, kwa sasa wasanii tuendelee kumuomba Mungu na tuachane na maovu pia tuwe wamoja kwani hujui lini utakufa“.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita kwenye Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua Ugonjwa wa Nimonia na upungufu wa damu mwilini na kisha kuzikwa wiki hii siku ya Jumatatu kijijini kwao Mbeya.

Shilole- Mama Yangu Alinifunza Kujitoa Kwenye Matatizo Ya Wengine

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema Mama yake alimfunza kujitoa Kwenye matatizo ya binadamu wengine.

Shilole ambaye alijizolea sifa kubwa Kwenye msiba wa msanii wa Bongo movie Agnes Masogange ambapo alionekana akishughulika kupika chakula na wanawake wengine Kwenye msiba.

Shilole baadae aliweka wazi kuwa alipofika tu msibani hapo badala ya kwenda kukaa pembeni na wasanii wenzake alienda jikoni kujiunga na wanawake wengine na kuanza kupika chakula.

Shilole ameweka wazi Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hivyo ndivyo alivyo siku zote kwani mama yake alimfunza kujitoa kwa ajili ya matatizo ya watu wengine:

Kabla mama yangu hajafariki aliniambia sifa ya binaadamuu! Kujitoa kwa wenzio hasa Kwenye matatizo kwani raha zipo tu. Pumzika kwa amani mama yangu japo uliniacha nikiwa na miaka saba hekima zako bado nazifata”.

 

Chegge- Nimeumizwa na Kifo Cha Agnes Masogange

Mwanamuziki wa Bongo fleva Said Juma ‘Chege Chigunda’ ameongelea kifo cha msanii wa filamu na video queen Agnes Gerald ‘Masogange’ na kusema hatokaa amsahau mrembo huyo.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao Mbeya ambako alizikwa jana Aprili 24, 2018 kijijini kwao Utengule, Mbalizi.

Chege aliyasema hayo juzi Jumapili alipokuwa Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar katika kuuaga mwili wa Masogange aliyefariki ghafla baada ya kupungukiwa damu.

Kiukweli msiba umeniumiza kama msanii kwani sisi ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva wa mwanzomwanzo kumtoa Masogange kimuziki, kifupi sitamsahau na nawapa pole ndugu na wanafamilia”.

 

Niligombana na Mwanangu Kisa Mambo Ya Usanii- Mzee Gerald

Baba mzazi wa marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ Anayeitwa Mzee Gerald amefunguka na kueleza kuwa alikuwa akigombana sana na mwanaye ambaye alikuwa anamsihi aachane na mambo ya sanaa.

Agnes alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kwa mara ya kwanza baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Msanii wa Bongo fleva Belle 9 Masogange ambao ulipelekea mpaka yeye kuitwa Agnes Masogange Lakini pia marehemu alikuwa ameanza kuwa muigizaji wa Bongo movie.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers kwa mara ya kwanza tangu amzike mwanaye hapo jana, Mzee Gerald amefunguka haya kuhusu binti yake:

Mwanangu alikomea kidato cha pili lakini hata kidato  cha pili hakumaliza kwa sababu ya matatizo. Kuna wakati nilikorofishana naye nikamwambia mimi mambo ya usanii sitaki, akanijibu, ‘sasa baba mimi nitafanya kazi gani wakati unafahamu tangu niko kanisani nilikuwa naimba kwaya?’ Baada ya muda tulikutana tena, tukalimaliza suala hilo, nikamruhusu“.

 

Irene Paul Ana Matatizo Yake Binafsi- Rammy Galis

Muigizaji wa Bongo movie Rammy Galis ameibuka na kujitetea baada ya sakata lake la kutuhumiwa kuigiza amezimia na msanii mwenzake Irene Paul kwenye msiba wa Agnes Masogange.

Siku ya Jumapili pale Leaders Club ambako Marehemu Agnes Masogange alikuwa anaagwa kuliibuka kizaazaa baada ya Rammy kupoteza fahamu hali iliyopelekea abebwe na kupelekwa kwenye gari kwa ajili ya huduma ya kwanza.

Lakini baada ya sakata hilo msanii wa Bongo movie Irene Paul alishangaza watu wengi baada ya kuamua kumshambulia Rammy na kumtuhumu kwa kujifanyisha na kupeleka maigizo msibani na kudai alikuwa hajazimia bali alikuwa anatafuta kiki.

Kwenye mahojiano na Dizzim Online, Rammy amejitetea kuwa kitu kilichomfanya azimie ilikuwa ni kuchoka baada ya kusimama kwa muda mrefu hivyo kuishiwa nguvu kabisa lakini pia ameweka wazi kuwa Irene Paul ana matatizo naye tangu siku nyingi:

Mimi sina matatizo na Irene kwa sababu kwanza Mungu alinijalia mini kuwa mwanaume na yeye kuwa mwanamke kwaiyo siwezi kubishana na mwanamke lakini huyu ana matatizo yake binafsi kwa sababu hata tukiwa location tumegombana sana na ninaweza kusema alikuwa ana matatizo na marehemu pia kwa sababu aliwahi kuniambia unaishi na mtu unajua nani anamlipia kodi? Kwa kweli iliniuma sana”.

 

Zari Amkumbuka Agness Masogange Amefunguka Haya Kuhusu Kifo Chake

Kifo cha Video Vixen na msanii wa Bongo movie Agnes Gerald maarufu kama Masogange kimewagusa wengi hasa kwa sababu alikuwa mrembo mdogo tu.

Moja kati ya watu walioguswa na kifo hiko ni Baby mama wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ambaye amemlilia marehemu Agnes Masogange.

Zari ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambao ameonesha kuguswa na msiba huo ambao amekiri kuwa alikuwa anafahamiana na marehemu ingawa hawakuwa marafiki sana lakini alikuwa mtu wa kumsalimia na kumjulia hali.

 

Ali Kiba na Diamond Uso Kwa Uso Kwenye Msiba Wa Masogange

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na hasimu wake namba moja msanii mwenzake Ali Kiba wamekutana Uso Kwa Uso kwenye viwanja vya Leaders Club hapo jana.

Jana Kwenye viwanja vya Leaders Club mwili wa Marehemu Agnes Masogange ulikuwa unapewa heshima ya mwisho kabla ya kwenda  kuzikwa kijijini kwao Mbeya wiki hii.

Wasanii kibao walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho na moja wapo walikuwa mahasimu wa siku nyingi Diamond na Ali Kiba ambao walionekana kupeana mkono jambo lililozua minong’ono msibani hapo.

Lakini pia Harmonize alionekana hana tatizo kukaa karibu na Ali Kiba high table wakati misa ya msiba huo inaendelea, hii inaonyesha ni jinsi gani kuna ukweli pale Diamond aliposema WCB haina bifu wala tatizo na Ali Kiba.

Aliyekuwa Mpenzi wa Agnes Masogange Azua Kizaazaa Msibani

Muigizaji wa Bongo movie Rammy  Galis Aliyekuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Marehemu Agnes Masogange amezua timbwili jana baada ya kuzimia msibani.

Jana katika viwanja vya Leaders Club Agnes alikuwa anaagwa na Wasanii Wenzake mbali mbali kabla hajasafirishwa kwenda Mbeya kwa ajili ya maziko.

Rammy alikuwa na Mahusiano ya kimapenzi na Agnes siku za nyuma kidogo na katika hali ya kawaida alifunguka na kueleza ni kwa jinsi gani msiba huo ulivyomgusa hadi kupelekea kuzimia wakati akiaga maiti.

Rammy alizua kizaazaa baada ya kuzimia na lube way kupelekwa kwenye gari lakini mkono alionekana kama bado ameshikilia vitu vyake jambo lilipolekea wengi kudai ulikuwa ni usanii tu.

Msanii mwenzake wa Bongo movie Irene Paul amemtolea povu zito Rammy na kudai alikuwa anatafuta kiki kwa kuigiza kuwa amezimia wakati ni wazi kabisa alikuwa anaigiza.

Hali ya Rammy baada ya Kuzimia

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Irene Paul alimtolea povu hili Rammy:

 

Marehemu Agnes Masogange Ameagwa Leaders Club Jana (Picha)

Aliyekuwa msanii wa Bongo movie na video vixen Agnes Gerald au maarufu kama Masogange aliyefariki dunia siku ya Ijumaa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugonjwa wa pumu, ameagwa jana leaders club jijini Dar es Salaam.

Agnes ameagwa jana na wasanii wenzake pamoja na mashabiki zake tayari kabisa kwa ajili ya kusafirishwa na kupelekwa mkoani kwao Mbeya kwa aajili ya mazishi.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio yaliyotokea jana Leaders Club:

 

 

.
.