Zari azua utata kwa kufanya hili kwenye kaburi la Ivan Ssemwanga

Zari Hassan amezua utata baada ya kuonekama akikaa juu ya kaburi ya aliyekuwa mume wake wa kitambo – Ivan Ssemwanga.

Ivan alifariki Mei akiwa Afrika Kusini alipokuwa akipata matibabu, mzazi mwenza wa Zari alizikwa kwao Kayunga, nchini Uganda.

Hatua ya Zari kuketi kwa kaburi ya Ivan imezua kelele kwenye mtandao wa jamii kwani kuna wale wanasema Zari haeshimu mwenda zake.

ray_officially: sasa huyu cameraman/women ulimwambiaje twende kwenye kaburi la ivan unipige picha au ulimuambiaje jaman@zarithebosslady

wisdomnelsonsalome: Jamani, kila mtu anastaili yake ya kuishi, unaweza ukawa na pesa lakini ukatumia kwa akili, wengine wakipata pesa anawaza kubadili nguo na mikoba, msimuhukumu mtu kwakile alicho penda. Wingine kutwaa kwenye majumba ya kupanga afu unamdc mwenzio kwann analife style ile ile, mwacheni boss Lady afanye anachopenda, mbona ninyi

homa_ya_jiji__: Daa hii picha inaujumbe mpana sana

dianamtenga: Wabongo wanafki jmn..watu huwatunaenda kuzika makaburini nawatu wa nakaa juu yamakaburi mara kibao..ila leo amekaa zari bc nizambi

 

Mahakama yaombwa kuamuru ufukuaji wa kaburi la Ivan Ssemwanga

Utata umezuka siku chache baada ya aliyekuwa mume wa Zari Hassan – Ivan Ssemwanga kuzikwa nyumbani kwa Kayunga, Uganda.

Kundi la Rich Gang ambalo lilianzishwa na marehemu, ulizua utata baada ya kumwaga pombe na kutupa pesa ndani la kaburi la Ivan.

Kitendo hicho kililazimisha familia ya Ivan kutafuta ulizi wa polisi kwa hofu kuwa wezi wengefukua kaburi la Ivan na kuiba jeneza lake na pesa zilizotupwa ndani ya karubi lake.

Soma pia: Polisi wa Uganda walinda kaburi la Ivan Ssemwanga

La kushangaza ni kuwa Mganda mmoja anayeitwa Abey Mgugu ameenda kotini kutoka koti iamuru ufukuaji wa kaburi la Ivan kwa msingi wa kutaka pesa zilizotupwa ndani la kaburi lake kutolewa na kurudishwa kwa matumizi.

Mgugu alisema kuwa kutupa pesa kwenye kaburi la Ivan kunadunisha fedha ya Uganda na nchi zingine ambazo pesa zao pia zilitupwa kwenye kaburi hilo.

 

 

Polisi wa Uganda walinda kaburi la Ivan Ssemwanga (Picha)

Ivan ssemwanga bado analindwa ata kwa kifo! Tishio la wezi kuiba geneza aliyozikwa nayo Ivan na pesa zilizotupwa kwenye kaburi lake, zimefanya familia yake kutafuta ulinzi kutoka kwa polisi.

Mwenda zake alizikwa kwa jeneza la bei kali ambalo lilinunuliwa Afrika Kusini. Kundi la Rich Gang lilitupa pesa nyingi ndani ya kaburi kabla ya jeneza liliyobeba mwili wa marehemu kushushwa kaburini.

Pesa zilizotupwa kwenye kaburi la Ivan

Soma pia: Kundi la Rich Gang yamwaga pombe na kutupa pesa kwenye kaburi la Ivan Ssemwanga

Pesa zilizotupwa kaburini na jeneza aliyozikwa nayo Ivan zimechangia familia ya mwenda zake kuhofia kuwa wezi wengefukua kaburi la Ivan na kuiba jeneza lake na pesa zilizotupwa ndani ya karubi lake.

Hi indo sababu ya familia ya Ivan kuamua kutafuta ulizi kutoka kwa polisi mbaka watakapozingira kaburi lake na ukuta.

Tazama picha za police wakilinda kaburi la Ivan hapo chini:

  

“Mshipa wake wa kichwa ulipasuka” Zari aeleze kilichomuua Ivan Ssemwanga huku akipinga kuwa aliwekewa sumu

Kumekua na uvumi kuwa kifo cha aliyekuwa mume wa Zari – Ivan Ssemwanga kilisababishwa na kuwekewa sumu. Zari amepinga uvumi huu.

Akiongea na Ayo TV, Zari alisema kiharusi (stroke) aliyokua nayo Ivan kilisababisha mshipa wa kichwa chake kupasuka. Alisema kupasuka kwa mshipa huo kulisababisha damu kumwagika kwenye ubongo wa Ivan na hii ndo ilisababisha kifo chake.

“Ivan was never poison, Ivan alikua na high blood pressure na hajawai kupima na if alipima he’s never taken it serious that he needs to take his medication. So what happened alipata stroke, vile alipata stroke high blood pia ikapanda. Now during the stroke akawa paralyzed one side of the body which is the left. And during the stroke venye imempiga, imempiga vibaya akapasuka vein in his head…in his brain…mshipa right? That thing in the head ikamwaga damu in his brain so daktari wakaniambia most of the patients like him, 80% of those patients like they die immediately. Wakaniambia 20% wenye wamebaki usually they die within a month and the other 10% hao…if they come back, if they make it wanakua fully dependent yani kumvalisha pampers, kumogesha, kumkulisha and things like that. So nkamuuliza ‘doctor what’s going on with my patient I wanna know’ akaniambia ‘look we are only trying to see what we can…wakamfanya operation to reduce the pressure on the brain ya ile damu lakini the operation also wasn’t successful because during the operation pressure ilikua inapanda inashuka inapanda inashuka and then also during the same operation he over bled so they didn’t continue with the operation because he was going die immediately, wakamrudisha in the ward to try stabilize him so that they can see if they can perform a second operation. So during that time when they were supposed to go back hali yake ikawa it’s just getting down and then towards the last day wakanipigia simu ‘look it’s not good you need to come and say goodbye because tumeona blood pressure kwanza ilipanda sana 220, normal blood is about 120/125. Ivan alikua 220 ilikua so bad ikakataa, sasa vile imeshuka ikashuka to 36 which was really bad. So wakatuambia come and say goodbyes tukasema our goodbyes tukarudi nyumbani because that day imepita nothing happened. Usiku around 2 o’clock on am…was it Tuesday or Wednesday 2am wakanipigia simu your patient has passed on, lakini during the day they had already told us that he’s on the process of passing on, wakatuambia no more visitors let him pass on, let his soul go in peace. It’s not poison, amekufa kwasababu of a stroke which ruptured vein in his brain coz a lot of bleeding, it was bad.” Zari alieleza.

Tazama mahojiano aliyofanya Zari kwenye video hapo chini:

Kundi la Rich Gang yamwaga pombe na kutupa pesa kwenye kaburi la Ivan Ssemwanga (Video)

Ivan Ssemwanga alikuwa mwanzilishi wa kundi la Rich Gang ambalo ni maarufu sana nchini Uganda kwa kufanya party za nguvu. Wanachama wa kundi hilo ni matajiri wakubwa ambao wanapenda sana maisha ya anasa.

Rich Gang walifanya ibada yao maalum kwenye kaburi la Ivan baada ya kanisa kufanya ibada ya maombi. Wanachama wa Rich Gang waliizingiza kaburi la mwanzilishi wao na kumwaga pombe ndani na pia kutupa pesa ndani la kaburi hilo.

Hii ilikua kabla ya jeneza la Ivan kuteremshwa kwenye kaburi lake. Waombolezaji waliskika wakishangilia wanachama wa Rich Gang walipokua wakitupa pesa kwenye kaburi la Ivan.

Tamaza video hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=nNtSSzHPZjY

Hii ndiyo sababu ya Diamond kukosa kuhudhuria matanga ya Ivan licha ya kudhibitisha awali kuwa angehudhuria

Akiongea kwenye kipindi ya The Trend ya NTV Kenya Ijumaa iliyopita, Diamond Platnumz alisema kuwa atasafiri kuenda Uganda kuhudhuria matanga ya Ivan Ssemwanga baada ya kumaliza show yake Nairobi.

“Well kwa ukweli ulikua ni wakati mgumu na mbaka saa hivi ni wakati mgumu kwasababu nlikua nko booked muda kidogo kuhusiana na Korogo festival, na msiba umetokea sasa kucancel tu ghafla show ya watu unajua inawezekana ukapata taswira tofauti, wengine wakachukua tofauti. Sikua na jinsi. So, lakini nliongea na mzazi mwenzangu (Zari) akanielewa, lakini nikimaliza hapa show tu na ntaenda Uganda kwasababu ya mazishi, kuzika. Baada ya hapo ndo ntarudi nyumbani,” Diamond alisema.

Lakini hata hivyo jana Simba hakuonekana kwa matanga ya Ivan, kwasababu gani? Meneja wa Diamond Sallam Sharaff alisema kuwa msanii huyo hangeweza kusafiri kwenda kumzika Ivan kutokana na ratiba kuingiliana.

“Kwenye mazishi hatujahudhuria, ilikuwa twende leo alfajiri lakini sasa kumbe wao wametoka usiku kwenda kijijini. Kwa hiyo nadhani ratiba yetu imeingiliana maana na sisi tulitoka Nairobi jana jioni.” Sallam alikiambia kipindi cha U-heard cha Clouds FM.

Skiza Sallam akielezea kwanini Diamond hakuweza kusafiri kuenda kumzika Ivan hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=elxy8DgyaFo

Simanzi nzito! Zari adondokwa na machozi kwa matanga ya Ivan Ssemwanga (Picha)

Aliyekuwa mume wa Zari – Ivan Ssemwanga alizikwa jana nyumbani kwao Kayunga, Uganda. Mwenda zake alisafirishwa kwao Jumatatu siku moja baada ya mwili wake kurudishwa Uganda kutoka Afrika Kusini.

Zari alihudhuria matanga hio kama mjane wa Ivan ingawa ndoa yao ilikua ishavunjika kitambo na ata Zari kuolewa na Diamond Platnumz.

Hata hivyo, Zari hakuweza kuficha uchungu aliyohisi kwa kupoteza baba wa watoto wake watatu, mrembo huyo adondokwa na machozi kwa matanga ya Ivan.

Wanawe wa kiume aliyowazaa na mwenda zake walijaribu kumtuliza lakini alishindwa kabisa kuzuia machozi kutiririka.

 

Zari awasili Uganda chini ya ulinzi mkali

Mkewe Diamond atamzika aliyekuwa mume wake Ivan Ssemwanga leo. Zari na wanawe watatu waliwasili Uganda kutoka Afrika Kusini Jumapili.

Ndege walioabiri kina Zari ndo pia ilibeba mwili wa mwenda zake. Zari alikua chini ya ulizi mkali alipowasili Uganda.

Mrembo huyo amekuwa akipigwa vita na familia ya Ivan huku wakidai kuwa anataka kupora mali ya mumewe wa kitambo.

Soma pia: Zari apigwa vita kwa maazimio yake ya kutaka kurithi mali ya aliyekua mumewe

Zaidi ya mabondia wawili walionekana wakimzingira Zari alipotua katika uwanja wa kimataifa wa Entebbe.

 

“Alikuwa na pesa nyingi, lakini ameshindwa kununua uhai” Waigizaji wa Bongo Movie waongea matope kuhusu kifo cha Ivan

Tofauti na wasanii wengine ambao walitoa salamu za rambirambi kufwatia kifo cha Ivan Ssemwanga, Steve Nyerere and Faiza Ally wameeleza hisia kali kuhusu kifo cha aliyekuwa mume wa Zari.

Waigizaji hao wa Bongo Movies wameongea matope kuhusu kifo cha Ivan, hisia zao kuhusu kifo cha mwenda zake zinaonyesha uadui tu.

“Alikuwa na pesa nyingi, alikuwa na uwezo wa kufanya chochote, alikuwa na uwezo wa kununua chochote lakini ameshindwa kununua uhai. Nimejifunza kitu kupitia wewe, tuishi vizuri na watu maana hakuna ajuaye kesho,” Steve Nyerere aliandika.

Steve Nyerere

“Binaadamu akikuchukia hata zuri kwake ni baya na ndio maana huwa na maisha yangu tu kama mimi bila kutaka kuwa yoyote, hakuna zuri mbele ya mtu mbaya. Unajua nini wala sijali naona upuuzi tu kama ya kipuuzi mengine yote yalio pita.

“Maisha yangu na wanangu yako kwenye mikono salama hata kushinda mikono yangu, yako kwenye mikono ya Mungu mwingi wa rehma. Leo Ivan na matajiri wengine wako wapi? Mali sio kila kitu kwenye maisha yetu tunahitaji amani, mapenzi, maelewano makubaliano.

Faiza Ally

“Nimetoka kwenye kutokua na mlo mpaka sasa namiliki milo, huo ni utajiri mkubwa maana kwanza ni kushiba akili ikae sawa ndio upange habari zingine, so at the end my heart is pure and that what give me amani ya moyo, hayo mengineyo tena yako nje ya uwezo wangu ni mipango ya Mungu, Faiza Ally aliandika.

 

Zari apigwa vita kwa maazimio yake ya kutaka kurithi mali ya aliyekua mumewe

Familia na marafiki wa Ivan Ssemwanga tayari wanampiga vita Zari Hassan kwa maazimio yake ya kutaka kurithi mali ya aliyekua mumewe.

Matukio haya yaliwekwa wazi na Big Eye ya Uganda ambayo ilimhoji mmoja wa marafiki wa Ivan. Chanzo cha habari hii kilisema kuwa Zari amevutana sana na Lawrence Kiyingi maarufu kama King Lawrence ambaye alitaka kupora mali ya Ivan.

King Lawrence ni mwandani wa Ivan na pia ni mwanachama wa kundi la Rich Gang ambayo ni maarufu sana nchini Uganda kwa kuhost parties za nguvu.

Rich Gang: King Lawrence (kushoto) na Ivan Ssemwanga (katikati)

Chanzo hicho kilieleza kuwa Zari and King Lawrence walitimuliwa hospitalini alipolazwa Ivan kwasababu walizua rabsha wakigombana kuhusu mali ya Ivan.

“At one point, these fights reached hospital and the two together with other family members had to be thrown out of hospital for the peace and sanity of the sick person. Ivan saw these fights, read some on Facebook but he just could not reply to anything. Someone had to hold the phone for him. And he had no reply just the hissing sounds. Deep down, he must have felt betrayed, used and abandoned by those he considered his closest,” Chanzo hicho kilisema.

Zari alionekana kwa video Instagram akigombana huku alisema kuwa mali ya mumewe wa kitambo ni ya watoto wake watatu aliyowazaa kama bado ni mke wa Ivan. Hii ilikua siku moja kabla ya Ivan kuaga dunia.

Zari na wanawe

Chanzo hicho pia kilisema kuwa Zari aliwaomba madaktari kuhairisha kutangaza kifo cha Ivan ili aweze kujipanga kable ya wanaomdulumu kuiba mali ya mume wake wa kitambo.

Mrembo huyo alitangaza mwenyewe kifo cha mumewe leo asubuhi baada ya kumaliza alichokuwa akifanya. Inasemekana Ivan aliaga dunia Jumanne asubuhi baada ya madaktari kudhibitisha kuwa viongo vyake kwa mwili vilifeli kufanya kazi.

 

 

Kwanini Diamond ameshindwa kupost chochote kumtakia hali aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Zari

Mume wa Zari Hassan wa kitambo – Ivan Ssemwanga amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini. Ivan alikibizwa hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa Kiharusi (kwa Kiingereza stroke).

Siku chache zilizopita Zari aliwaomba mashabiki wake wamuombe mpenzi wake wa kitambo ambaye ni baba wa watoto wake watatu.

Soma pia: Zari awaomba mashabiki wake wamuombee mume wake wa kitambo – Ivan baada ya kulazwa hospitali kutokana na ugonjwa wa stroke

Zari alipoenda hospitalini kumwona Iva

Akiongea kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, Diamond alieleza sababu zake za kukosa kupost chochote kumtakia hali Ivan Ssemwanga.

“Ni kweli mzazi wake Zari anaumwa, na yuko serious. Na kila siku huwa namuhimiza Zari akamuone mzazi mwenzie kwasababu najiuliza asingekuwa anaenda familia yangu ingemuonaje, kwa hiyo maskini dada wa watu kila siku huwa anaenda. Sijawahi mpigia simu kwasababu yuko serious sana na pia sikuweza kumpost kwasababu watu waneanza kusema labda natafuta kiki maskini ya Mungu kumbe wala,” Diamond alisema.

Diamond akiwa Clouds FM

 

Zari awaomba mashabiki wake wamuombee mume wake wa kitambo – Ivan baada ya kulazwa hospitali kutokana na ugonjwa wa stroke

Mume wa Zari Hassan wa kitambo – Ivan Ssemwanga amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini baada ya kuugua ugonjwa wa Kiharusi (kwa Kiingereza stroke).

Ugonjwa huwo hatari husababisha mwili kupooza kutokana na matatizo kwenye mishipa ya damu inayolisha ubongo.

Zari na Ivan walijaliwa kupata watoto watatu wa kiume kabla ndoa yao kusambaratika. Zari alidai kuwa Ivan alikua anamchapa na kumtesa akiwa mke wake – sababu ya yeye kumwacha.

Zari na wanawe

Ata hivyo Zari bado huzungumza na Ivan kwasababu ya watoto wao. Picha inayosambaa mitendaoni inaonyesha Zari akisimama kando ya Ivan ambaye amelazwa hospitalini.

Ivan akiwa hospitalini

Zari pia aliwaomba mashabiki wake kwenye Instagram wamuombee mume wake wa kitambo. Hakueleze zaidi kuhusu hasi ya Ivan.