Hamisa Mobetto Afunguka Mazito Juu Ya Familia Ya Diamond

Mwanamitindo na Msanii wa muzik wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Madam Hero’ Hamisa Mobetto ambaye pia ni mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka mazito juu ya Familia hiyo.

Hamisa ambaye amekuwa hana maelewano mazuri na familia ya Diamond kwa muda mrefu sasa hasa baada ya kuachana na Diamond wiki chache zilizopita ameongea mazito juu ya familia hiyo.

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Hamisa amedai kwamba Mama Diamond alimpigia simu akimtaka arudiane na mtoto wake mara baada ya kuachana naye.

Mama Diamond alinipigia simu nirudiane na Diamond, lakini mawifi ndio hivyo tena”.

Lakini pia Hamisa ameongelea sakata la kumblock Diamond Kwenye akaunti ya mtoto wao Dylan:

Diamond hajielewi, nimem-block insta ya mtoto kwa sababu anashindwa hata kujisitiri, hadi anamuhusisha mtoto kwenye mambo yake, nakosa deal kibao za mtoto kisa mambo yake”.

Hamisa amekiri kuwa ni sauti yake iliyosikika na kusemekana kuwa alikuwa anaongea na mganga lakini amesisitiza kuwa yule Kwenye simu hakuwa mganga bali alikuwa ni shekhe:

Sauti ilikuwa ya kwangu, hakuwa ni mganga alikuwa ni Sheikh kwaajili ya dua, ni vitu vya kawaida sana lakini walirekodi”.

 

 

“Mabifu Hayalipi Tanzania” Hamisa Mobetto Afungukia Bifu Lake na Ray C

Mwanamitindo na Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuongelea bifu lake na msanii mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila Ray C.

Mobetto na Ray C waliingia kwenye sintofahamu siku za nyuma na kujikuta wanarushiana maneno ya kejeli na baadae mashabiki na wapambe wao kujikuta Kwenye vita ya maneno.

Lakini siku ya juzi Ray C alilimaliza bifu hilo baada ya kumposti Hamisa na nyimbo yake mpya na kusema amani itawale juu yao na kumtakia Mrembo mafanikio mema katika ulimwengu wa muziki.

Kwenye mahojiano na East Africa Television, Hamisa amefungukia bifu lake na Ray C na kuweka wazi kuwa hawezi kuwa na bifu na mtu maana kibongo Bongo mabifu ya wasanii hayalipi:

Unajua huyo dada sijawahi kumuona live yaani na Mwanzoni sikujua kama ananiongelea mimi man sikuwahi kumjibu lolote kuhusiana na hilo na binafsi napenda mziki wake kwaiyo kama ameposti video yangu nashukuru, Unajua nchi za wenzetu wakiwa na mabifu wanatengeneza pesa lakini huku kwetu hakuna faida”.

Lakini pia alipoulizwa kuhusu Tanzania Sweetheart Wema Sepetu, Hamisa amekataa kabisa kuliongelea na kusisitiza hana maelewano mzuri na Wema hivyo hawezi kusema chochote kuhusu yeye.

Hamisa Mobetto Atangaza Kuingia Kwenye Muziki Rasmi

Mwanamitindo na Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Hamisa Mobetto ametangaza ujio wake rasmi katika tasnia ya Bongo fleva baada ya kuendelea kufanya vizuri na wimbo wake wa kwanza.

Hamisa Mobetto ameachia video mpya ya wimbo wake wa ‘Madam hero’ na mara moja wimbo huo umeweza kufanya vizuri sana na kushika namba moja katika mtandao wa Youtube.

Kwenye mahojiano na East Africa Television, Mobetto amefunguka na kusema hakutegemea mapokezi aliyoyapata kutoka kwa mashabiki lakini atajikita Kwenye tasnia hiyo ya uimbaji kutokana na mafanikio anayoyapata hivi sasa.

Kusema ukweli sikutegemea kama itapokelewa vizuri kiasi hicho, kwani wimbo huo niliurekodi siku nyingi tangia mwaka jana na nilikuwa sina uhakika kama nitautoa kwani sikujua kama mashabiki watanielewa lakini nafurahi na ninashukuru Mungu umekubalika”.

Lakini pia Mobetto amekiri kuwa pamoja na mapikezi makubwa aliyoyapata kutoka kwa mashabiki na wadau wakubwa wa muziki ataendelea kufanya shughuli zake nyingine kama kawaida Ikiwa ni pamoja na mitindo na Bongo Movie.

Hamisa Mobetto Amewaacha Mbali Aslay, Mbosso na Maua Sama

Msanii wa Bongo fleva na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto amezidi kufanya vyema katika ulimwengu wa muziki baada ya video yake kushika namba moja Kwenye mtandao wa Youtube.

Hamisa Mobetto ambaye ndio kwanza ametoa Single yake ya kwanza inaitwa ‘Madam Hero’ ameonekana kung’aa mara baada ya video yake hiyo kufanya vyema zaidi.

Mpaka muda huu video hiyo inatrend namba moja Kwenye mtandao wa kijamii wa Youtube kwa Tanzania na kukimbiza video za wasanii wakali wanaofanya vizuri nchini kama Mbosso na ngoma yake ya Hodari, Aslay na wimbo wake wa Kwatu na Maua Sama na kiokote.

https://www.instagram.com/p/Bn7_OvDltew/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=19m8x137scjmh

Hii sio mara ya kwanza kwa Mobetto kusikika akiimba ameshasemekana kuweka vocal Kwenye ngoma ya Jibebe ya Diamond Platnumz.

Ray C Amaliza Bifu Lake na Hamisa Mobetto

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila Maarufu kama Ray C ameonekana kumaliza bifu lake na Mwanamitindo Hamisa Mobetto baada ya kuposti video yake mpya.

Ray C na Mobetto wameahawahi kukwaruzana siku za nyuma ambapo Ray C alimponda Hamisa kwa mavazi yake ambayo alikuwa anauza Dukani kwake na kuyaita fake jambo lililopelekea mashabiki wa Hamisa kumvamia na kusababisha varangati.

Lakini Baada ya muda kupita Ray C ameonekana kumaliza bifu hilo baada ya kuposti video mpya ya Hamisa ya wimbo wake wa Madam hero na kuwataka mashabiki zake wakaangalie wimbo huo na kumsapoti Mobetto.

kuonyeshwa kuwa ameguswa na Kitendo hicho Hamisa alimshukuru Ray C na hata kutaniana kuhusu nguo za zilizowagom mbanisha.

 

Mobetto Hawezi Kuwa Tanzania Sweetheart ni Wema Peke Yake-Maimartha Jesse

Mtangazaji maarufu na mfanyabiashara Maimartha Jesse ameibuka na kumkingia kifua Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu na kudai hakuna kama yeye.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na mjadala Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Hamisa Mobetto amekuwa akipambanishwa na Wema Sepetu na watu hata kusema title ya Wema ya Tanzania Sweetheart anatakiwa apewe Mobetto kwani ndio anapendwa kuliko Wema.

Katika interview aliyofanya na Global Publishers, Maimartha amesema hakuna na hatatokea mrembo mwingine anayependwa na kukubalika kama Wema hivyo wanaompigia debe Mobeto kwamba ndiye anayekubalika sana kwa sasa wanajisumbua tu.

Wema ndiye Tanzania Sweetheart, hakuna wa kufanana naye na hatatokea mwingine kama yeye, hii ni namba nyingine, wanaosema Mobeto anamzidi ni waongo na hawajafanya tathmini zao vizuri, Wema anapendwa na kila mtu kuanzia watoto hadi wazee“.

Pamoja na kutokea kupingwa na kuchukiwa na mashabiki siku za hivi karibuni mpaka kutakiwa kuacha kujiita Tanzania Sweetheart Mrembo Wema Sepetu amegoma kuachia jina hilo na kusisitiza yeye ndio Sweetheart wa East Africa nzima.

Irene Paul Afungukia Bifu La Zamaradi na Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Irene Paul amefunguka na kupima uzito bifu lililopo kati ya rafiki yake kipenzi Zamaradi Mketema na Hamisa Mobetto.

Wiki chache zilizopita Zamaradi na Mobetto waliingia Kwenye bifu zito mara baada ya kutokea sintofahamu Kwenye mavazi ambayo Zama aliyavaa kwenye arobaini ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Irene alisema Zamaradi alipoingia kwenye ugomvi na Mobeto hivi karibuni kisa kikiwa mshono wa nguo aliyovaa kwenye arobaini ya mwanaye, yeye aliamua kujiweka pembeni kwa sababu aliogopa kuchukuliwa hatua za kisheria kwani serikali kwa sasa haitaki mchezo.

Si unajua tena siku hizi sheria za mtandao, unaweza kujifanya kimbelembele yakakukuta mazito kwa hiyo niliona nikae pembeni licha ya kwamba Zamaradi ni rafiki yangu sana kwa sababu nilifahamu pia wawili hao wangeweza kumalizana bila tatizo lolote”.

 

Meneja Wa Mobetto Adai Mteja Wake Hajatetereshwa na Skendo Ya Uchawi

Meneja wa Msanii wa Bongo movie na mwanamitindo Hamisa Mobetto, Beatrice Ndungu amefunguka na kuweka wazi kuwa Hamisa hajatetereshwa na skendo ya uchawi.

Siku ya jana Hamisa Mobetto aligubikwa na skendo nzito mara baada ya voice notes kuvuja zilizothibitisha kuwa alikuwa anafanya maongezi na mganga wa kienyeji.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Meneja wa Mobetto ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba Mteja wake anapitia kipindi kigumu kwa yale yanayoendelea Kwenye mitandao ya kijamii lakini ni mwanamke jasiri na anajua nini anafanya hivyo yuko vizuri kabisa.

Mitandao ya kijamii inakuja na mambo  mengi mengine mazuri na mengine mabaya lakini nahisi kila kitu ni vile utapokea na kujibu kwa sababu maneno hayaishi watu wanaongea lakini cha muhimu ni vile unajionyesha mbele ya watu kwa majibu yako.

 

Hamisa ni mtu mmoja jasiri mpaka kuna vitu ambavyo ni binafsi sana mimi kama meneja siingilii lakini ninachoamini ni msichana jasiri na amepitia vitu vingi sana na hivyo alivyopitia amefika hatua nzuri inayopelekea makumpuni mengi kumtaka kwa ajili ya kutangaza bidhaa zao na kuna vitu vingi zaidi vinakuja”.

Lakini pia Meneja huyo amesema Mobetto amefungua ukurasa mpya na hayo mambo ameshaachana nayo na hivi sasa anaangalia mambo mengine hivyo mashabiki zake wakae mkao wa kula.

“Unaonekana Hushindwi Hata Kumuua Mama Yangu” Diamond Amshukia Hamisa Baada Ya Skendo Ya Uchawi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemshirikisha mzazi mwenzake Hamisa Mobetto baada ya skendo za kumloga kwa waganga kupamba moto.

Sakata hilo limetokea baada ya voice note zilizomuhusisha Hamisa na mama yake wakiwa wanazungumza na mganga kusambaa Kwenye mita ya kijamii.

Kwenye voice note hizo Hamisa anasikika akimuomba mganga amfanyie dawa ambayo itamfanya Diamond ampende na amuoe na Mama Diamond na Familia yake imkubali kama zamani.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Diamond amefunguka kuhusu sakata hilo na kumwagia povu zito Hamisa:

Unapotaka kwenda kwa mganga uniroge mimi na mama yangu, unaonekana wewe haushindwi hata kumuua mama yangu, kama unawaza sijui nikupe nyumba. Voice notes zinasambaa sambaa hata mimi nilitumiwa, ninazo unasikia kitu halafu unajua huyu ni yeye, halafu nikamwambia huyu ni wewe.

Watu kuna vitu wanaongea ongea halafu wanajaribu kuvipindisha aonekane Mama yangu na dada yangu wana matatizo, mama yangu na dada yangu hawawezi kuwa na matatizo. Halafu hao watu wako unaowatuma wakatukane nimeshakuona ukiwatuma wakatukane kwa watu wengine kwa sababu pia uliwatuma pia wamtukane na Zamaradi”.

Wiki hii dada wa Diamond Platnumz, Esma aliandika ujumbe mrefu kukanusha taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao kwamba wameandaa voice note kwaajili ya kumchafua Hamisa Mobetto.

Esma Akana Tuhuma Za Kula Njama Za Kumchafua Mobetto

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka na kuandika waraka mrefu wa kukana tuhuma zinazomkabili yeye na kama yake za kumchafua Hamisa Mobetto.

Siku mbili hizi kuna taarifa zilienea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Hamisa Mobetto ameenda kwa mganga wa kienyeji kwa nia ya kuwatengeenezea dawa Familia ya Diamond impende na yeye aolewe na Diamond.

Lakini kuna taarifa nyingine ziliibuka kuwa voice note ambaye Esma na Mama Diamond walisema ilikuwa ni Hamisa Akiongea na mganga ilikuwa ya uongo na inasemekana voice note hiyo ilikuwa imepikwa na Mama Diamond kwa nia ya kumchafua na kumpoteza Mobetto.

Baada ya Tuhuma hizo Esma ameibuka na kudai kwamba yeye pamoja na mama yake hawawezi fanya kitu kama hicho kwa Mobetto.

Dada bora ukae kimya halafu unapata zambi kumshilikisha Mwenyezi Mungu ktk swala km hili kuongopa vitu mbona sie wenyewe tupo Kimya au ndio mnatapatapa embu mjitulize jamani hata MUNGU HAPENDI kwani ye ndio Muamuzi plz naomba msinitungie uongo wa kijinga jinga mlichokifanya wenyewe mnakijua na nafsi zinawasuta sipendi kuniingiza ktk uongo wa kijinga msijisafishe kutaka kuchafua watu. Huyo huyo mama mnaotaka awapende kutwa mnachamba na kumtungia uongo naombeni mkitaka kuweka uongo wenu bora mniweke mimi sio mamaangu. MLICHOFANYA MNAKIJUA
#temporarypost?#mfaMajiHamuishiKutapatapa”.

Lakini pia Esma aliongeza:

Katika maisha ni vema kukaa kimya pindi ukikosea na hasa ukijua wazi kuwa nimekosea ila ukijaribu kufuta au kusawazisha kosa kupitia njia za wasiogusa maisha yako ujue kosa linazaa kosa…Ungetulia maana watu wameshiba vielelezo na ushahidi 100%”.

 

Mange Amkingia Kifua Mobetto Dhidi Ya Familia Ya Diamond Kufuatia Tuhuma Za Uchawi

Mwanaharakati wa mambo ya siasa na mdau wa mitandao ya kijamii Mange Kimambi amemkingia kifua Hamisa Mobetto baada ya familia ya Diamond kumuandama na skendo za ushirikina.

Mama Diamond na Esma Platnumz wamemtuhumu Hamisa kwa uchawi ambapo wamedai kuwa alienda kwa mganga kwa nia ya kumloga Mama Diamond na Esma ili wampende na aolewe na Diamond.

Mange ameibuka na kumtetea Hamisa dhidi ya tuhuma hizo na hata kuwatupia maneno ya shombo familia ya Diamond na Wema Sepetu ambaye pia ameonekana kumsema na kumtupia vijembe Hamisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BnMqWQFFRTt/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1d4duzu19snyf

Mobetto, Barnaba na Shilole Wala Shavu Kampeni Ya Be Smart

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Barnaba Boy Classic na Shilole pamoja na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto wamekula Shavu baada ya kuteuliwa mabalozi wa TCRA.

Wasanii hao wameteuliwa na Baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano (TCRA CCC) kuwa mabalozi wa kampeni ya Be smart inayojihusisha na kuelimisha vijana kuondokana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii mashuleni.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari wasanii hao wamefunguka kupata shavu hilo nono Lakini pia nafasi watakayo cheza kama mabalozi:

https://www.instagram.com/p/BnGMZYTlrt8/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=13yt54nc81jzx

Mobetto- Sina Ubaya na Wanawake Wanaomtaka Diamond

Mwanamitindo na msanii wa Bongo movie Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi kuwa hana ubaya na wanawake ambao wanamtaka Baba mtoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Hamisa na Diamond wamefanikiwa kuzaa pamoja mtoto mmoja wa mwaka mmoja anayeitwa Dylan wakat Diamond ana watoto wengine wawili na mwanamama Zarinah Hassan.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Hamisa amefunguka wakati alipoulizwa kuhusu Msanii wa Bongo fleva Pretty Kind ambaye aliwahi kuweka wazi mapenzi yake kwa Diamond na baadaye kulalamika Hamisa kachukia hadi kamblock:

Hamisa amekana kumblock Pretty Kind na kudai yeye hana ubaya na mwanamke yoyote anayemtaka Diamond ambaye anasemekana kuwa ni mpenzi wake:

Kwanza kabisa nilikuwa simjui na hata kumsahau huyo mtu mwenyewe halafu sijamblock kwa sababu ya Diamond kwa sababu kuna wanawake kama milioni tano wote wanamtamani huyo huyo mtu mmoja sasa sasa kama ndio hivyo nitawablock watu wangapi Jamani?

Pretty Kind kuna Maneno machafu na mabaya aliyaongea kuhusu mimi alinichafua sana halafu mimi ni brand simjui nikaona huyu naye katokea wapi? Nikamblock Maisha Yangu yaendelee kwa amani wa Nini mtu anayenipa kero”.

Pretty Kind alifunguka kuwa kama akitaka kutoka kimapenzi na Diamond anaweza akampata kwa sababu yeye ni mzuri na ana vigezo vyote vya kutokataliwa na Diamond.

Mama Mobetto: Nitamsapoti Mwanangu Kwa Kila Jambo

Mama mzazi wa Mwanamitindo Hamisa Mobetto, Shufaa Rutaginga maarufu kama Mama Mobetto amefunguka na kuapa kuwa upande wa mwanaye na kumsapoti katika mambo anayopitia.

Mama Mobetto amedai hata kama watu watamtenga mtoto wake yeye atakuwa katka upande wake na kumsapoti kwa kila jambo kwani anajua uchungu wake kama mama.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Mama Mobetto amefunguka kuwa, watu wakiendelea kumzushia mwanaye mabaya na kumsema kila kukicha kazi yake yeye siku zote ni kumpa moyo na kumsihi asikate tamaa.

Kazi yangu kubwa kwa mtoto wangu ni kumpa moyo na kumuonesha ni jinsi gani ninampenda maana naamini ni changamoto tu anapitia, lakini zitaisha na zitamfanya kusimama imara”.

Hamisa amekuwa akipata wakati mgumu Kwenye mitandao ya kijamii tangu azae na Diamond kwani Familia ya Diamond imekuwa ikiweka wazi kumchukia lakini pia mashabiki wa Zari wamekuwa wakimpa kipindi kigumu.

Wema Aingilia Bifu La Zamaradi na Mobetto

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amejikuta Tena katika headlines za social media baada ya kuingilia kati bifu linalo trend hivi sasa kati ya Zamaradi Mketema na Hamisa Mobetto.

Zama na Mobetto waliingia Kwenye bifu hili baada ya kutifuana kuhusu mshono wa vazi alilovaa Zamaradi Kwenye 40 ya mtoto wake wiki chache zilizopita.

Zamaradi aliandika waraka mrefu wa kurasa tatu ukieleza namna alivyosikitishwa na maneno yanayosambaa mitandaoni kuwa alipewa mshono na Mobeto kwa lengo la kushonewa, lakini akauchukua na kwenda kuushona kwa mtu mwingine huku akimwaga chati zote za WhatsApp walizokuwa wakitumiana.

Lakini pia kwa Mobeto naye aliibuka na kupinga vikali waraka huo. Wakati hayo yakiendelea, Wema kupitia ukurasa wake alinunua ugomvi kwa kuandika; Tuendelee ama tusiendelee’.

Meneja wa Wema, Neema Ndepanya naye hakukaa kimya, aliingilia kati na kumkingia kifua Wema kwa kuandika waraka wake. “Kiki za kuchafuana zilishapitwa na wakati, hakuna kitu kibaya duniani kama kuwa mnafiki, yaani nachukia mtu anajifanya kila wakati anaonewa yeye tu,”

.

Hamisa Mobetto Alamba Shavu La Milioni 60 Kupitia Ubalozi

Msanii wa Bongo movie na Mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto amelamba shavi Nono baada ya kuteuliwa kuwa balozi wa Prima hair.

Global Publishers wanaripoti kuwa Hamisa Mobetto  analipwa shilingi milioni 5.7 kwa mwezi (zaidi ya milioni 60 kwa mwaka) leo Agosti 8, 2018, baada ya kuingia mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa balozi wa kiwanda kinachotengeneza nywele (rasta) cha Prima Afro, kilichopo Tabata, Matumbi jijini Dar.

Hamisa Mobetto alitangaza habari hiyo njema Kupitia mkutano wake aliofanya na waandishi wa habari ambapo aliweka wazi kuwa kampuni hiyo walikuwa wakimchunguza  nguvu yake kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kunichunguza, walinifuata ofisini kwangu tukazungumza, nikausoma mkataba na kuangalia masharti yao na kiwango wanachotaka kunilipa niliporidhia tukapanga siku ambayo ni leo nikasaini”.