“Nilikuwa Siwezi Kupanda Stejini Bila Kutumia Madawa Ya Kulevya”- Ray C

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amefunguka na kuelezea kipindi kigumu alichopitia wakati ameathirika na madawa ya kulevya.

Ray C ambaye kwa sasa anaishi nchini Kenya na kufanya kazi zake kimuziki amefunguka alipohudhuria kongamano la madawa ya kulevya Mombasa.

Ray C alipata  nafasi ya kuongelea kuhusu madawa ya kulevya kutokana na yeye kuwa muhanga mkubwa wa madawa hayo ambapo kwa sasa amekiri kuacha  kutumia madawa.

Ray alifinguka kuwa ilifika kipindi akawa mtumwa wa madawa ya kulevya kiasi ya kwamba alikuwa hawezi kupanda hata stejini kutumbuiza bila kutumia madawa ya kulevya.

Addiction took three of the best of me. I was heartbroken. My brain was taken away by drug use. My brain was not working because there was something else in my brain telling me I could not perform on stage without drugs, that I could not do anything without drugs. I could not go anywhere without drugs, therefore I was a prisoner in my own soul. Wengi wanaoingia kwenye madawa, watu wanaathirika maini kwenye madawa, watu wanatumia sindano pamoja wanapata HIV, wanawake wanajiuza ili mradi aweze kupata pesa aweze kukidhi ule utegemezi wake”

Tangu Ray C aache kutumia madawa ya kulevya ameonekana kufanya vizuri zaidi na hata kurudi kufanya muziki.

Wembamba Ndio Dili, Unene Uchafu:- Ray C

Mwanadada aliyewahi  kwa muda mrefu katika game la muziki na baadae kupotea kwa muda(RAY C) amefunguka na kusema kuwa mwili wake ambao ulikuwa ukionekana mkubwa sana kutokana na kunenenpa sana na kupoteza uhalisia wake wa hapo awali ulimtesa sana na kwamba ilikuwa iafikia hatua mbaya ya kupata ugonjwa wa shinikizo la damu ndipo aliposhauriwa na daktari kupunguza mwili huokabla hajakutana na hatari ya ugonjwa huo.

naomba niwashauri wale vibonge kuwa wembamba ndio dili , unene ni  uchaafu tu kwani hata kujisugua bafuni ni kazi,ukipindisha tu mkono mgongoni unahema kama unafanya jogging  kumbe unaoga tu binafsi sitaki kabisa kuusikia unene.

Baada ya matatizo aliyoyapa ray c mwili wake ulikuwa mnene sana na kusababisha kufanya mazoezi na kupunguza vyakula vya mafuta ili kupunguza mwili wake.

Ray C na Rostam Wala Shavu Kutoka Kwa Msanii Wa Kenya

Raper wa muziki kutoka Kenya Khaligraph Jones siku ya jana aliachia rasmi albamu yake.

Albamu hiyo aliyoipa jina la Testimony 1990 ina nyimbo zipatazo kumi na saba na habari njema ni kwamba ndani ya nyimbo hizo kuna wasanii watatu wa Bongo fleva walioweka mkono humo.

Wasanii wa Bongo fleva ambao watasikika Kwenye Albamu hiyo ni pamoja na Msanii mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila ‘Ray c’ aliyeimba wimbo unaoitwa ‘Aisee’ na kundi la Rostam linalounda na Stamina na Roma.

Roma na Stamina watasikika katika albamu hiyo Kupitia kibao chao cha ‘Now you know’.

Hii inaonyesha ni jinsi gani muziki wetu wa Bongo fleva unavyozidi kukua kila siku na hata kufika kabisa mbele na kimataifa zaidi.

Ray C Azitaka Media Zisipige Nyimbo Zake Akifa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amezijia juu Media za Bongo (Vyombo vya habari) huku akiwataka wasipige nyimbo zake akifa.

Ikiwa ni siku moja tangu msanii wa Bongo fleva Sam Wa Ukweli aage dunia, Ray C ametupa Dongo kwa baadhi ya vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikipiga nyimbo za msanii huyo tangu jana ilihali alipokuwa hai hazikupigwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ray C amesema kuna baadhi ya media zina mambo ya kibafki kwani msanii ukiwa hai hawa pogo nyimbo zako ila ukishakufa tu ndio wanaanza kupiga jambo alilolipinga na kusema yeye akifa wasipige nyimbo zake:

Media za Bongo bwana! Kufa leo uone nyimbo zako zitapigwa wiki nzima hata zile ambazo hazijatoka studio lakini! Tusapotiane tukiwa hai pia….Nikisha kudai hata msihangaike kunipa promo….Maana hakutakuwa na maaana Tena RIP Sam”.

Msanii Sam wa Ukweli alifariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kuugua kwa kipindi cha mwezi mzima malaria na UTI sugu.

Rafiki Yako Akikusaliti Tupa Kule Usithubutu Kuwa Naye Karibu- Ray C

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila ‘Ray C’ Kiuno bila mfupa amefunguka na kuwapa ushauri mashabiki zake kuwa endapo kuna rafiki yako amekusaliti achana naye.

Ray C ambaye hapo nyuma amewahi kufunguka kuhusiana na usaliti uliopata mara baada ya kuingia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ambapo alifunguka kuwa watu wote aliodhani kuwa ni marafiki zake walimsaliti na alibaki amesimama mwenyewe.

Ray C ametumia ukurasa wake wa Instagram kufikisha ujumbe huo ambao ameonyesha pia unamhusu na yeye:

Ukiona rafiki kakugeuka, usije thubutu kuwa naye karibu tena huyo ni zaidi ya nyoka. Tena bora Nyoka ukikutana naye harembi kujifanyisha mzuri kwako, anakugonga tu fasta kabla hujamdhuru kuliko huyo anayejifanya kwako mzuri na ukiondoka tu anakung’ong’a”.

Ray C alisindikiza ujumbe huo kwa neno Chefu si kidogo. Hivi sasa Ray c anatamba na wimbo wake Rudi Kidogo na anafanya sana matamsha yake nje ya nchi kama Kenya, South Africa na kwingineko.

Ray C Amkingia Kifua Diamond Platinumz.

Msanii wa muziki wa bongo fleva alikuwa amepotea kwa muda mrefu lakini sasa amerudi katika game Rehema Chalamila maarufu kama Ray c, amefunguka na kusema amekuwa akisikitishwa sana na watu wanaokuwa wanamuandama sana msanii mwenzake Diamond Platinumz.

Ray C anasema kuwa watu bwanamuongelea diamond vibaya na kuacha kuangalia mazuri na makubwa aliyoyafanya katika muziki wa tanzania kwa kuwakomboa na kuukomboa muziki huo.ray c anasema kuwa kama mtu ana macho hana haja ya kuambiwa ni  kiyu gani daimond  amefanya kukuza na kuuboresha muziki wa tanzania zaidi ya kumpongeza na kumfanya apate moyo wa kuendelea kufanya.

Ray c anawaomba  wanaomsema Diamond vibaya kuiga mfano kutoka Nigeria jinsi watu wa huko wanavyofanya kusapotiana kimuziki ili ukue.

ninaumiaga sana ninapoona  watu wanamuongelea vibaya huyu mtoto,amfanya mapinduzi makubwa sana huyo mtoto.kama una macho unaona kabisa .muziki wa tanzania sas ahivi  unafika mbali sana sababu ya watu kama hawa.Nigeria  wanafika mbali sana kwa sababu wanasapotiana  lakini sijui kwa nini tanzania tunapenda kuzodoana,kushushana,kuchukiana, dah yaaani huyo alieanzisha social media mungu na amlaani.

Kwa kipindi hiki kifupi Diamond amekumbwa na mambo mengi na maneno mengi katika mitandao yanayomsema vibaya ambapo baadhi ya wachambuzi wakuwa wa habari na muziki pia wamekuwa wakisema kuwa mambo hayo yanaweza kumshusha au kumuangusha kabisa Diamond kimuziki, ukianza familia, mapenzi na hata mashabiki wamekuwa mstari wa mbele kumshambulia Diamond kimuziki.

 

Ray C Amuomba Raisi Magufuli Apitishe Sheria Ya Mpya Kuhusu Ndoa

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila au maarufu kama Ray C ameibuka na kumuomba Raisi Magufuli kupitisha sheria iyakayoangalia mahusiano ya kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume.

Ray C alifunguka haya kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya jana ambapo aliweka picha ya Raisi John Pombe Magufuli na kumuomba ahahakikishe kuwa Tanzania kuna kuwa na sheria ambayo itahahakikisha kuwa mwanaume na mwanamke wasiwe na mahusiano ya kimapenzi hadi pale watakapofunga ndoa ili wanawake wengi wapate nafasi ya kuolewa.

Ray C amefunguka hayo kwa kile alichodai kuwa wanaume wengi wana tabia ya kuchezea wasichana na wa watu na mwisho wake wanawaacha solemba bila ndoa na badala yake wanaishia kuoa wasichana wengine.

Ray C aliandiika maneno haya machache katika ukurasa wake wa Instagram:

Mzee mimi nina shida moja hawa wanaume hapa nchini wanajifanya wajuaji sana! ombi langu kwako kwa mwaka huu ni hili! Naomba upitishe sheria kama ya Sultan Qaboos wa Oman! Hakuna mahusiano kati ya mwanamke na mwanaume mpaka pale watakapofunga ndoa. Na yeyote atakayekutwa na mwanamke iwe hotelini au guest house bila cheti cha ndoa wapelekwe wote segerea. Nadhani itasaidia sana kwani wanawake wengi wataolewa badala ya kuishia kuwa manungayembe! Utakuwa umewanyoosha sana hawa wanaume wetu nadhani tutaweza kuheshimiana”.

Ray C ameongea hayo kuhusu ndoa na mahusiano ingawa yeye binafsi alishaweka wazi kipindi cha nyuma kidogo kiwa kwa sasa hana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote kwani mahusiano ya kimapenzi  yamesha mpotezea sana muda wake kipindi cha nyuma.

Huu Ndio Ushauri Ambao Ray C Amempa Recho Kizunguzungu

Mwanamuziki mkongwe wa bongo fleva. Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliyejipatia umaarufu miaka ya nyuma kama ‘kiuno bila mfupa’ kutokana na staili zake za kucheza kwa kukata viuno, ameibuka na kumpa ujumbe mzito msanii mwenzie Rachel Kizunguzungu.

Uhusiano wa ukaribu kati ya Rachel na Ray C ulianza tangu pale Rachel alipoweka hisia zake wazi kwa Ray C na kufunguka kuwa anavutiwa sana na mwanadada huyo na hata uimbaji wake. Rachel aliimba nyimbo za Ray C na hata watu kumfananisha naye kitu ambacho Ray C alikubaliana naye na hata kupanda naye stejini mara kadhaa.

Miaka ya hivi karibuni Rachel alikuwa kimya kimziki na habari zilisambaa kuwa alikuwa anajihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, habari inayoendana na ya Ray C kwani na yeye alidumbukia kwenye matumizi ya madawa ya kulevya lakini amekiri hivi sasa ameacha na amerudi kwenye muziki anakofanya vizuri.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C amemwambia Rachel asikate tamaa ya kurudi kwenye muziki baada ya matatizo kwani hata na yeye alipita huko huko:

Kuna watakaokwambia hufai na kuna watakaokwambia umefeli na kuna watakaokukatisha tamaa na kutamka kwako waziwawaziwazi kuwa wakati wako umeisha huwezi tena kuna watakao amua kutokukusapoti! Nilishatamkiwa hivyo vyote nisingekuwa najitambua ningekuwa nimeshakata tamaa kabisa ya kuingia studio usiyumbishwe na mwanadamu na wala usifikirie hata siku moja kuwa huwezi kwa sababu unaweza na Recho umebarikiwa sauti, sasa amka tena simama kama Recho, usikate tamaa mwaka 2018 ni wako gemu bado liko wazi kabisa nikihesabu wasanii Wa kike wanaofanya vizuri hata wanne hawafiki nafasi yako bado iko pale pale”.

 

Ray C Alinidhalilisha Sana Kwa Maneno Yake- Nandy

Mwanamuziki kutoka Jumba la sanaa la Vipaji THT, Nandy ameibuka na kudai kuwa alivunjika moyo kwa maneno ya udhalilishaji aliyoambiwa na msanii mwenzake Rehema Chalamila au maarufu kama Ray C.

Wiki chache zilizopita wasanii hawa wawili waliingia katika vita kali ya maneno mtandaoni baada ya  Nandy kutumia/ kuimba nyimbo za Ray C katika tamasha la Fiesta ambapo hakulipwa kwenda kuimba. Ray C alimjia juu Nandy na kumwambia asitumie nyimbo zake kuingiza pesa kwani na yeye ni mwanamuziki hivyo anaweza kuimba nyimbo zake mwenyewe, jambo ambalo halikumpendeza Nandy ambaye alidai kuwa Ray C alikuwa na taarifa kuwa ataimba nyimbo zake kwani walikuwa wote THT kwenye mazoezi.

Nandy alipohojiwa na Dizzim Online, alisisitiza ya kuwa maneno yale aliyoyaongea mtandaoni yalimdhalilisha sana kama msanii

Sikuwahi kufikiria kama Ray C angeweza kupaniki kama alivyo paniki kwani hata mimi alinishangaza, baada ya yeye kuandika vile kwenye instagram, management yangu ilinipigia ili initulize kwa sababu kusema ukweli nilipaniki na nilijisikia vibaya sana pale watu walivyo nifata na kuanza kunitukana kwamba niimbe vinyimbo vyangu viwili na mambo mengine kitu kilichonidhalilisha sana pia kwa sababu nilivyoimba ile nyimbo sikuimba kwa ubaya ilikuwa ni kwa nia nzuri tu ya kuburudisha mashabiki zangu”.

Tangu ishu hii itokee Nandy amekuwa mtu wa kuizungumzia sana akionyesha kuwa hakufurahishwa hata kidogo tofauti na Ray C ambaye hajawahi kuongelea suala hili hata mara moja

Nimejaribu Kumtumia Meseji Lakini Hajajibu, Nandy Aongelea Nia Yake Ya Kumuomba Msamaha Ray C

Mwanamuziki wa Bongo fleva mrembo Nandy ameongelea nia yake ya kutaka kumtafuta Ray C ili waweze kumaliza tofauti zao licha ya Ray C kumuwekea ugumu.

Mwanzoni mwa wiki hii Ray C hakumkopesha Nandy kwani alimjia juu kwa kitendo chake cha kuimba nyimbo zake bila ruhusa yake kwenye tamasha linaloendelea la fiesta. Ray C aliweka wazi kukerwa na kitendo hicho hasa kwa sababu yeye mwenye nyimbo hakualikwa kwenda kushiriki tamasha hilo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo, Nandy amefunguka ya moyoni kuhusu ishu hiyo name meseji aliyomtumia Rayc lakini hajaijibu:

Kiufupi ni kwamba tu niliposti clip ya nyimbo ya Mez B ambayo amemshirikisha dada angu Ray C ambayo tuliimba mimi na Ben pol na tulifanya hivyo kwasababu ilikuwa ni season ya kukumbuka malegend wa bongo fleva kwaiyo haikua kwa nia mbaya sasa nilishangaa kwa nini alichukulia vibaya mimi kuimba ile nyimbo yake hadi kupelekea mashabiki zake kunitukana sana lakini sikuishia hapo niliandika kama kumuelewesha na kumtaka radhi kwenye Instagram pia nilimwandikia meseji ya kawaida private nikamuuliza kwa nini kaamua kunifanyia hivi? Na ni siku gani nilishawahi kukutana naye sikumsalimia? Nikamwambia mbona mi nilikusapoti kukutangazia nyimbo yako ilipotoka lakini hata asante hukutoa! Lakini nilikuja kugundua hata mwaka jana nilivyoimba nyimbo yake hakupenda ingawa alikuwepo kwenye mazoezi na hata mashairi mengine mwenyewe alinisaidia”.

Nandy alimalizia kwa kudai kuwa amemsamehe Ray C na atachukua ushauri wake wa kuimba nyimbo zake mwenyewe kwani hata fiesta kupata kazi ni kutokana na watu kuvutiwa na  nyimbo zake mwenyewe na siyo nyimbo za Ray C au msanii mwingine yeyote.

Ray C Amuonya Nandy Kutumia Nyimbo Zake Kwenye Show

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva ambae kwa muda takribani miaka minne alikuwa kimya kutokana na athari alizozipata kwa matumizi ya madawa ya kulevya Rehema Charamila maarufu kama Ray C ameibuka na kuwalalamikia wasanii ambao wamekuwa wakitumia nyimbo zake katika show bila kumshirikisha  au kumnifaisha na chochote kutoka katika nyimbo hizo,

Msanii huyo aliandika maneneo hayo katika ukurasa wake wa instagram akimlenga zaidi msanii wa kike ambae pia kwa sasa anafanya vizuri katika tasnia ya muziki , Nandy ambae amekuwa akiimba nyimbo za Ray C katika matamasha ya Fiesta ambayo yanaendlea kwa sasa yakizunguka nchi nzima, Nandy amejuwa ni moja wa wasanii amabo huimba nyimbo za wasanii wengine majukwaaani huku wakibadilisha kidogo muonekao (melody)wa nyimbo hiyo.kumbe swala hilo limemkwaza msanii menye nyimbo hizo.

Ray C aliandika”jamani hii tabia sio nzuri kabisaa!! sijafa bado, kama mnaona umuhimu wa  sauti yangu kwenye shoo zenu muwe mnaniitaga basi,sina cancer ya koo kushindw kuziimba  hizo nyimbo!! nandy hii ni mara ya mwisho ukipanda fanya kazi zako.hii ni mara ya pili ujue, mashabiki zangu hamuwatendei haki, idont like it! sipendi maana hata tukigongana  muda mwingine hata salamu hamnipi , staki maozea ‘niliimba tusitafutiane pisha sio presha tena’#sipendiunafki #nawewetena #mnaninilakini #kilamtuapaterizikiyakeyajasholake” aliandika Ray C

Ray c ambae analalamika na kuona kuwa wasanii wenzie wanakuwa kama wanafaidika na nyimbo zake wakati yeye mwenyewe yupo na anauwezo wa kuimba nyimbo zake, ivyo waache kuimba kama wanataka shoo za nyimbo izo basi waangaike kumtafuta na kumualika katika shoo ilia akutane na mashabik wake mwenyewe.Kitu kingine kinachomkwaza Ray C ni jinsi ambavyo baadhi ya wasanii wanapokuta mitaani huwa wanashindwa hat kusalimiana.

Rehema Chalamila ni mmoja wa wanadada wa zamani waliokuwa wakitumia sauti na kiuno chake vizuri katika muziki na alikuwa akiitwa’ kiuno bila mfupa’  baadhi ya nyimbo zake ni  Uko wapi,Sogea sogea, Wanifuata nini na hivi karibuni alitoa wimbo unaojulikana kama Unanimaliza ikiwa ni wimbo wake wa kwanza tangu arudi katika game la muziki baaada ya kukaa kwa muda mrefu.

 

Sitaki Unafki Amesema Ray C Baada Ya Nandy Kuimba Nyimbo Zake Bila Ruhusa

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Rehema Chalamila amemjia juu msanii mwenzake Nandy baada ya kutumia nyimbo zake bila ruhusa.

Ray c alionekana kukasirishwa na kitendo cha Nandy kutumia nyimbo zake kwenye tamasha linaloendelea la Fiesta licha ya yeye kutokualikwa kushiriki tamasha hilo. Ray C aliyepumzika kimuziki kwa miaka mingi kutokana na kuingia kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya amerudi na kibao chake ‘Unanimaliza’ kinachofanya vizuri hivi sasa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray C alimfungukia Nandy yafuatayo:

Jamani hii tabia sio nzuri kabisaa! Sijafa bado!  Kama mnaona umuhimu wa sauti yangu kwenye shoo zenu muwe mnaniitaga basi! Sina Kansa ya koo ya kushindwa kuziimba hizo nyimbo Nandy hii ni Mara ya mwisho ukipanda Fanya kazi zako! Hii ni mara ya pili ujue, Mashabiki zangu hamuwatendei haki ujue! I don’t like it sipendi, Maana hata tukigongana salamu saa nyingine hamna kwaiyo sitaki mazoea! Niliimba tusitafutiane visa tena pisha sio tena presha, sitaki unafki na wewe Tena, mna nini lakini? Kila mtu apate riziki kwa jasho lake”.

Baada ya kuona povu la Ray c na mashabiki kumjia juu Nandy kwa kitendo alichofanya Nandy aliomba radhi;

Dada angu Ray c, kama wote tulivyosema kabla ya kuimba juzi, mimi ni mmoja wa wasanii wanaokukubali kama msanii uliyetufungulia njia ya mziki wetu ulipo, sitaacha kukuheshimu na kukukubali  kwa hilo  wewe na wengine wengi tu. Siamini kukusifia na kukuenzi ni lazima uwe umekufa hapana nafanya jambo hili zuri kwa moyo wangu mzuri Kama ulivyomuenzi Mama mwanahela kwa nyimbo zake. Heshima yangu kimuziki kwako itabaki siku zote kama nilivyoimba nyimbo za wasanii Kama king kiki, mwasiti, Yemi Alade na Recho”.

Ray C alionekana kukerwa na kitendo cha Nandy kulipwa kushiriki tamasha la fiesta na kutumia nyimbo zake wakati yeye mwenye nyimbo hajalipwa kushiriki tamasha hata moja.

“Jaydee ana mapenzi ya kweli” Ray C afunguka kuhusu uhusiano wake na Lady Jay Dee

Ray C alizungumzia uhusiano wake na Lady Jaydee katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni na Mwanaspoti. Mrembo huyo alimsifu Jaydee kwa kuwa na mapenzi ya kweli.

Ray C alisema kuwa Jaydee alimwonyesha upendo sana katika kipindi alipokuwa ameathirika na utumizi wa dawa za kulevya.

“Jaydee ana mapenzi ya kweli kwa msanii mwenzake. Hataki kuona anaanguka…ninampenda sana kwa moyo wake wa upendo,” Ray C alisema.

Mrembo huyo pia ushauri wake kwa matumizi ya dawa za kulevya, alisema kuwa serikali inafaa ijitahidi kutoa elimu mashuleni kuhusu athari za kutumia dawa za kulevya.

“Mie naiomba tu Serikali ijitahidi kutoa elimu mashuleni kuhusu athari za kutumia dawa za kulevya, kwani wengi wanaoathirika kwa sasa ni vijana tena wadogo na wengine ni wanafunzi na hao wanafunzi hutumia muda wa mapumziko kutumia dawa hizo hivyo kupewa elimu ni muhimu kwani hawajui athari zake wanajiingiza kama mimi nilivyojiingizaga bila kujua,” anasema.

 

Ray C afunguka kuhusu kuibiwa kwa ukurasa wake wa Instagram

Ray C amepoteza ukurasa wake wa Instagram uliokuwa na wafuasi zaidi ya laki tano. Mrembo huyo amefunguka na kusema kuwa akimpata aliyehack account yake atakipata cha mtema kuni.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa radio, Ray C alieleza kukerwa kwake na aliyehack ukurasa wake wa Instagram.

“Mwizi aliyedukua (hack) akaunti yangu amenirudisha sana nyuma kwani nimeshindwa kufanya matangazo ya video ya wimbo wangu, matokeo yake nimetumia nguvu kubwa sana nilipouachia. Nikimkamata huyo mtu aliyenifanyia hivyo cha kwanza nitamnasa kofi kwa kunipa kazi cha pili lazima nimfikishe polisi na mwisho wake ni Segerea. Siwezi kuendelea kuvumilia watuibie halafu waendelee kukaa mitaani kwani watatutesa sana.

“Mimi akaunti yangu haijapotea kabisa kwani naiona ikiweka matangazo mbalimbali yaani nikimkamata sitamwambia anipe asilimia kumi bali atatoa pesa yote kwani nitahesababu tangazo la kwanza mpaka la mwisho ili kujua ni kiasi gani cha pesa anatakiwa anipe maana wameshazoea,” Ray C alisema.

 

Siri anayotumia Ray C kunoa makali yake kimuziki itakushangaza sana

Ray C ameachana na mambo ya kutumia dawa za kulevya kabisa, kwa sasa akili yake yote iko tu kwa mambo ya muziki pekee.

Mrembo huyo alifunguka na kusema kuwa hana hamu na mambo ya mapenzi kwasababu ya malengo yake kimuziki.

Soma pia: Ray C atoa sababu ya yeye kuwa single

T Fighter, mmoja wa mameneja wa Ray C, pia amefunguka kuhusu siri ambayo mrembo huyo anatumia kunoa makali yake kimuziki.

Akiongea na Planet Bongo ya EA Radio, T Fighter alisema Ray C ako na uwezo wa ajabu kwani yeye hushinda studio kwa siku mbili mfululizo akirekodi ngoma zake.

“Tukienda studio tunakesha hata siku mbili, mimi nishazoea nikienda studio nakaa lisaa limoja naondoka ila yeye akiingia studio anakaa siku mbili anarekodi nyimbo tatu au nne kali,” T Fighter alisema.

 

Ray C atoa sababu ya yeye kuwa single

Ray C hana haraka na mapenzi, muimbaji huyo amedhibitisha haya hivi karibuni ambapo pia alitoa sababu zake za kutaka kuwa single bado.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL ya EATV, Ray C alisema hana muda na mwanaume yeyote kwani malengo yake ni kuvuma tena kwa kutoa ngoma kalikali.

Ray C alieleza kuwa alipoteza muda mingi kwa kujihusisha na mahusiano ambayo haikumpeleka kokote, alisema akili yake sasa iko kwa kazi tu.

“Mimi hapana sipo kwenye mahusiano na mtu yeyote, kwa muda niliopoteza, hakuna tena muda wa kupoteza wa kumpa tena mtu mwingine naona kama muda umenipita sana, kwa hiyo akili yangu ipo kwenye kazi. Sioni kama ninaweza nikashare muda wangu na mtu mwingine, sina hata hizo feeling kwa bahati mbaya sana,” amesema Ray C.