Ray C ashangazwa na muonekano wa uso wake (picha)

Matumizi ya dawa za kulevya uliathiri mwili wa Ray C kwa njia nyingi. Mrembo huyo alinona sana alipokua akijaribu kuacha utumiaji wa mihadarati.

Watu wengi walifanya utani wakitumia picha za Ray C alipokuwa mnene. Mashavu zake haswa zilikuwa zimefura kama andazi.

Ray C aliamua kufanya mazoezi ili kurudisha umbo lake la kitambo. Mwimbaji huyo alishangazwa na muonekano wa uso wake alipoweka picha yake ya kitambo mtendaoni.

“Yesu Wangu!!!!Unajua Siamini!!Hivi na nyie mlikuwa hamniulizi haya mashavu vipi!!??wabaya sana nyie yaani!!! #yamudatuhiiwalaiiiiiinaifuta!!!!!” Aliandika Ray C.

 

Ray C ashindwa kuficha furaha yake baada ya Diamond kukiri hili

Rehema Chalamila maarufu kama Ray C ameishiwa na maneno ya kusema baada ya Diamond Platnumz kufunguka kuhusu nia yake kimuziki.

Diamond alisema nia yake ni kuinua wasanii wengi kumuziki kwani wao kama yeye wamelelewa kwa umaskini. Super star huyo alisema hayo akitangaza uzidunzi wa msanii mpya wa Wasafi.

“Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mwingine Mpya toka Mtaani, ndani ya @Wcb_Wasafi….. Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini… na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake….Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha…Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran?” Diamond aliandika kwa Instagram.

Ray C alifurahiswa na maneno ya Diamond kwa kiasi kwamba akaamua kumsifu kwenye mitendao ya kijamii. Alisema roho ya Diamond hauna ubinafsi kabisa.

“Wakitokea wasanii wakubwa kama wewe na wakawa na moyo kama wako basi muziki wetu utafika mbali sana…Kaa na huyu kijana japo nusu Saa tu,utaelewa kwa nini nasema haya!!Kuna Ro!!!!Na kuna RoHo!!!Jamaa ana Roho ya Peke Yake Maskini!!!!Na Mengi Moyoni natamani niongee lakini Haya Yanatosha mdogo wangu!!Kumbuka Mwenye Hii Dunia alishasema ,Mtoaji hupewa Zaid na Zaid…… Mungu akutangulie katika kila ufanyalo Inshallah…” Alisema Ray C.

 

Alichoapa Ray C kufwatia kifo cha Dogo Mfaume kutokana na dawa za kulevya

Ray C ako na uhakika kuwa akirudi kutumia dawa za kulevya atakufa bila shaka. Mwimbaji huyo alisema hayo akiongelea vifo vya wasanii walioago kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

Mrembo huyo haswa aliongelea kifo cha Dogo Mfaume, alisema kama bado hajapata somo kutokana na kifo cha Mfaume basi akipita tena ile barabara kitakachofata ni kifo chake.

Dogo Mfaume

Ray C aliapa kutorejea kwenye matumizi ya dawa za kulevya, alisema maamuzi ya kubadili mwendeno wa maisha yake ni yeye wenyewe.

“Kuna Muda nakaa na kujiuliza barabara ilikuwa na mvua kubwa sana na ukungu sana kiasi cha kushindwa kabisa kuona mbele!!!!Mbele magari mengine nayo yalitaabika KuFocus!La mbele kabisa alikuwamo Langa bahati mbaya lilipotea,Nyuma yake kulikuwa na la Ngwea Nalo pia lilitokomea mojakwamoja angali naliona,Hata la Whitney pia alieweza kukodi hata ndege lakini nae alipita hiyohiyo barabara na hakufanikiwa kupita!Na hili nalo la Mfaume limeenda zake sababu ni ileile ya balaa la mvua kubwa inayotishia Maisha….

“Najiuliza kwanini Mimi niwe hai Leo na barabara tuliipita wote na ni ileile ya kutisha!!Kama sijalipata somo mpaka sasa basi nikiipita tena ile barabara kitakachofata ni Kifo…………

“Ya Mungu ni makubwa mno tena Sana,Na kila sababu ya kusema Asante Mungu wangu……Ingawa njia yetu ni moja lakini Maamuzi ya kubadili mwendeno Wa Maisha yetu ni sisi wenyewe……..

“Ewe Ndugu unaetaabika Amua sasa……Sema No To Drugs.” Aliandika Ray C.

 

Jibu aliyotoa Ray C kuhusu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mbunge

Kuna uvumi nyingi kuhusu Ray C, mwimbaji huyo amesemwa mara mingi kwasababu amehushishwa na kashafa kadhaa wa kadhaa.

Hivi karibu kumekuwa na ubuyu kuwa mrembo huyo alijiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na mbunge ambaye ameoa.

Ray C

Ray C hata hivyo amekana uvumi huo, amedai kuwa hajawai kujihusisha katika uhusiano wa kimapenzi na mheshimiwa yeyota licha ya kufahamiana na wabunge mbalimbali.

“Kwanza kwa sasa mambo ya mapenzi nimeyaweka kando, niko bize na muziki wangu, akili na hisia zangu zote nimezielekezea kwenye kazi. Muziki ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Ray C.

 

Ray C: Kujiua kwangu lilikuwa ni wazo la mara kwa mara

Ray C amefunguka huhusu jinsi alivyotaka kujitoa uhai zaidi ya mara 10 kutokana na panda shuka za mkondo wa maisha.

Hit maker huyo wa ‘Unanimaliza’ alijiingiza katika utumiaji wa mihadarati miaka ya awali jambo ambalo lilisababisha afya yake kuzorota na ata kulemaza kazi yake ya kimuziki.

Akizungumza na Wikienda katika mahojiano maalum, Ray C alisema kuwa nia ya kujitoa uhai ilikuwa ikitokana na yeye kuamini kuwa hakua na njia nyingine ya kujinusuru.

“Kujiua kwangu lilikuwa ni wazo la mara kwa mara, inaweza ikawa hata zaidi ya mara kumi kutokana na kukata tamaa kabisa ya maisha huku nikijitazama nilivyokuwa msichana mwenye ndoto nyingi lakini nateketea nikijiona.

“Kuna wakati nilikata kabisa tamaa kuwa hakuna njia nyingine ya kunifanya nipumzike na tabu niliyokuwa nikipata zaidi ya kujitoa uhai ambao kwangu haukuwa na thamani na wala sikuwa ninajipenda tena hata kidogo,” alisema Ray C.

 

Ujumbe aliyotoa Ray C kwa Chid Benzi kuhusu utumiaji wa dawa za kulevya

Rapa Chid Benzi ni miongoni mwa wasanii ambao walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya. Afya yake Benzi ilikua ya kuogofya kabla ya menaja wake Diamond- Babu Tale kumpeleka Sober House kule Bagamoyo.

Chid Benzi akiwa amekonda alipoathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya

Ray C, ambaye pia aliathirika na dawa za kulevya, amemuombea Chid Benzi kwa Mungu ili aweze kutoka rasmi kwenye mtihani wa dawa za kulevya.

Mrembo huyo alimpa moyo Chid Benzi kwa ujumbe aliyotoa, alisema kuwa anaamini rapa huyo ataweza kushinda vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.

Ray C alisema anataka Benzi atoka rasmi kwenye mtihani wa dawa za kulevya kwasababu anataka kutoa wimba nyingine na yeye.  Ray C and Chid benzi walishawahi kutoa wimbo pamoja – ‘Nihurumie’.

Ray C Alimsifu Benzi na kusema rapa huyo yupo miongoni mwa marapa wakali zaidi Tanzania. Alisema pengo aliyowacha Benzi linaonekana.

“Chid benzi ni bonge la msanii na kwa upande wa Hip hop nadhani ni ‘one of the best artist’ na kwa sasa hayupo pengo lake linaonekana. Nampenda sana Chid Benzi  na ninamuombea sana kwa Mungu aweze kutoka katika janga hilo la madawa na akirudi natamani kufanya nae kazi nyingine. Aweke nia naamini atatoka.

“Binadamu wote lazima wapitie mitihani lakini tatizo mitihani hiyo lazima itakuwa inatofautiana. Haifurahishi kabisa kumuona mtu anateseka na matumizi ya dawa .Kama binadamu lazima uwe na nafasi ya kujifikiria kwa sababu hakuna mtu anayeweza kubebea ugonjwa au matatizo. Naamini Mungu aliyenisaidia mimi nikatoka kule atawasaidia wote siyo Chidi tuu bali wote wenye nia ya kuachana na yale mateso,” alisema Ray C.

Chid Benzi

 

Ray C amshukuru sana Naibu Waziri wa Afya – Hamisi Kigwangalla kwa kumtendea hili

Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa Afya na Mambo ya Wanawake, amewasihi Watanzania wote wampe Ray C support yao yote kuliko wakati wowote ule.

Kigwangalla alisema kila mtu hukosa na kila mtu anahitaji nafasi ya pili ile kuweza kurekebisha makosa waliofanya. Waziri huyo alisema Watanzania wanafaa wampe Ray C nafasi ya pili.

Hamisi Kigwangalla

“Na Mimi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Wanawake, kama #BaloziWaWanawake na kama Daktari niseme nimefurahishwa na kuvutiwa sana na jitihada anazofanya huyu dada @rayctanzania, nimeguswa na wimbo wake wa #Unanimaliza, na nimeona nimuunge mkono kwa kuwaomba wadau wote ambao mmekuwa naye siku zote mfahamu kuwa sasa anahitaji support yetu zaidi kuliko wakati wowote ule. Tumuunge mkono kwa dhati. Mungu atatujaalia kheir kwenye maisha yetu pia. Hakuna aliyekamilika. Sote tuna vipindi vyetu vya kuanguka Na kwa hakika tunahitaji ‘a second chance’ kila siku za maisha yetu! Hakuna anayeweza kujisimamia mwenyewe, sote tunahitaji mtu mmoja wa kutushika mkono na kutunyanyua pindi tunapoanguka! Kila la kheir Ndg. Rehema Chalamila. With our support, even the sky is not the limit! Keep on moving, keep on believing!” Hamisi Kigwangalla aliandika kwa Instagram.

Ray C alifurahiswa sana na maneno aliyosema  Kigwangalla, alimshuruku kwa dhati.

“Heshima kwako Mheshimiwa,Nashukuru sana kwa maneno yako ya Faraja baba.Bless Your Soul Sir ????  @hamisi_kigwangalla ,” Ray C aliandika.

Ray C

 

Dawa za kulevya kando, Ray C sasa yuko tayari kutawala kimuziki tena

Matumizi ya dawa za kulevya ndiyo ilisababisha Ray C kupoteza nafasi yake kama malkia wa nyimbo za Bongofleva na hatimaye kupoteza ushawishi aliokuwa nayo.

Ray C hatimaye ameebuka mshindi katika mapabano na matumizi ya dawa za kulevya. Katika mahojiano na Bongo5, Ray C alisema yuko tayari kutawala kimuziki tena.

Staa huyo wa kitambo alisema ako na nyimbo karibu kumi ambazo zitauzwa kwa tovuti la Wasafi.com punde atakapoziachilia.

Tazama mahojiano hayo kwenye video hapo chini:

Ray C hatimaye ampa jibu msanii kutoka Kenya – Ringtone aliyetaka kumoa

Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenya – Ringtone alitoa pendekezo akitaka Rehema Chalamila maarufu kama Ray C afunge naye ndoa.

Hii ilikua mwaka jana na Ray C hata hakumpa jibu. Ringtone ni msanii maarufu sana Kenya, amewahi fanya collabo ya nguvu na Christina Shusho. Wimbo wao ‘Tenda Mema’ bado ni hit kubwa sana.

Ringtone pia anadai kuwa msanii wa nyimbo za Injili mwenye utajiri mkubwa nchini Kenya. Ako na magari za kifahari na nyumba kubwa jijini Nairobi.

Ray C sasa amempa Ringtone jibu baada ya muda huo wote; akiongea na Mzazi Willy Tuva kenye kipindi cha Mambo Mseto ya Radio Citizen, Ray C alisema hawezi kubali Ringtone amuoe.

Ray C na Ringtone
Ray C na Ringtone

Mrembo huyo alikiri kuskia pendekezo la Ringtone kwenye mitendao lakini hakutaka kuongelea jambo hilo kwasababu hana haja nalo.

“Nilisoma hizo taarifa Kwa mitandao, namjua tu kama msanii kwanza wa Gospel, kwa hiyo nilishangaa sana ila ni mtu mzuri sana napenda anavyoshirikiana na wasanii wa Gospel wa Tanzania, ila hio haipo Kwenye ratiba yangu though,” Ray C alisema.

Ray C aliambia Mzazi Willy Tuva kuwa anampenda rais wa Kenya Uhuru Kenyatta and anaomba kukutana naye atakapoenda Kenya hivi karibuni.

Hatimaye Ray C akutana na Rayvanny na Diamond Platnumz

Mwimbaji mkongwe, Ray C, aliweza kukutane na wmibaji anayempenda sana Rayvanny hivi majuzi wakiwa HQ ya Wcb_wasafi baada kikao juu ya sanaa.

Kupitia mtandao wa Instagram, Ray C aliweka video yake na Rayvanny wakiimba na kulingana na tabasamu yake mwibaji huyu alikuwa ameeingojea siku hii kwa hamu na ngamu.

Kwa muda sasa Ray C amekuwa akitamani kufanya kazi na kijana huyu wa Wasafi records na hivi sasa kuna dalili kuwa wawili hao wanauwezo wa kuachilia nyimbo pamoja.

Ingawa Ray C alikuwa na shida na management yake, hivi sasa nyimbo zake zinawaweza kupatikana katika mtandao mpya wa wasafidotcom.

Mama Saida Karoli na Professor Jay pia walikuwa katika kikao hiki kilicho fanyika Jumanne iliyopita. Tazama video ya Ray C na Rayvanny hapa.

??????????

A post shared by Ray C (@rayctanzania) on Mar 14, 2017 at 1:06pm PDT