Jumbe Athibitisha Kufanya Mazungumzo na Rayvanny Kabla Ya ‘Siri’ Kutoka

Msanii mkongwe wa muziki wa lumba nchini Mzee Jumbe amefunguka na kukiri kuwa walishakutana na msanii Rayvanny kwa ajili ya kufanya mazungumzo nae kabla ya kutoa wimbo wake wa Siri ambao amrudia baadhi ya sehemu ya wimbo huo wa mzee huyo.

Mzee Jumbe amesema kuwa katika kurudia wimbo huo, Rayvanny na uongozi wake walimwita na kuongea nae vizuri na hata kumlipa kiasi cha pesa kizuri ambacho ameridhika nacho na kumruhusu kufanya wimbo huo kwa amani kabisa.

Akiongea kwa furaha na kuthibitisha hilo, Mzee Jumbe amesema kuwa amefurahi kuona Rayvanny ameutendea haki wimbo huo na anasema kuwa sababu kubwa ya kukubali Rayvanny kufanya wimbo huo ni kwa sababu anajua kuwa kundi la Wasafi na wasanii wake wanafanya kazi nzuri.

Wamenilipa vizuri na Rayvanny ameufanyia  haki wimbo huo na nimekubali kwa sababu ninajua kazi nzuri sana wanayoifanya wasanii kutoka kundi la wasafi.

Mzee Jumbe ametoa shukrani zake za dhati kwa lebo ya wasafi na kusema kuwa anaona fahari kuona wamemkumbuka na kuukumbuka wimbo wake kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiupa kisogo wimbo huo.

Ukitaka kuona hata katika video ya wimbo huo,nimetoka na huo ndio uungwana , mtu anatumia kazi yako na anakushirikisha  mwenyewe na hata kama wasipokulipa unapata faraja.nashauri wasanii wengine wa kizazi kipya wafanye kazi na wasanii wakongwe ili wapate madini ya muziki  na muziki wao utadumu  , kama utakumbuka wimbo huu nimeuimba miaka mingi iliyopita lakini mpaka leo unafanya vizuri.

Mzee Jumbe ansema kuwa aliutoa wimbo wake mwaka 2001,na hata wimbo wa Rayvanny alishauri uitwe mapenzi ya siri lakini wakaona bora wauite siri.

Rayvanny: Baada ya Kufanya Kazi na Jason Derulo Chochote Kinaweza Kutokea na ‘Migos’

Mwanamuziki kutoka kundi la WCB Rayvanny amefunguka kuhusu experience yake ya kufanya kazi na Jason Derulo na mpango wake wa kwenda mbele zaidi na kufanya kazi na kundi la Migos.

Rayvanny amerudi juzi kutoka nchini Marekani alipokuwa ameenda kupiga show katika miji ya Washington na Minneapolis. Alipokuwa nchini alishare picha iliyomuonyesha akiwa studio na moja ya wasanii wakubwa duniani Jason Derulo na kuweka wazi kuwa anafanya kazi kwenye moja ya nyimbo zake.

Tumezoea kuona wasanii wa Africa wengi wanawafata mastaa kuomba washiriki kwenye nyimbo zao lakini ni mara chache sana kwa msanii mkubwa kumuweka msanii kutoka Africa kwenye nyimbo yake lakini Rayvanny amefanya hivyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online Rayvanny amefunguka kuhusiana na kolabo aliyofanya na Jason Derulo Lakini pia mipango yake ya kufanya kazi na kundi kubwa kutoka Marekani la Migos:

Mimi na Jason Derulo tulikutana kwenye Coke studio akawa mshkaji wangu sana nina namba yake tunachat baadae nilivyoenda LA Marekani nikaenda Nyumbani kwake na pia mpaka Leo bado nachat naye kwaiyo ni mtu ambaye yuko humble na ninajifunza vitu vingi sana kutoka kwake na pia ni msanii ambaye yuko very busy kila siku anarekodi na yupo busy lakiningoma niliyofanya itatoka siku so nyingi lakini pia tuna mpango wa kufanya ngoma na Migos tumeshawatumia cover tunasubiri wapate muda wa kuingalia then naweza nikasafiri kwenda Marekani kufanya nao ngoma”.

 

Familia Ya Rayvanny Yasambaratika .

Baada ya kuweka picha yenye caption ya kuijiita single mother , mwanadada mrembo ambae pia ni video queen katika video mbalimbali lakini pia  ambae alitokea katika video ya Rayvanny ya kwetu iliomfanya akatambulika zaidi.baada ya kutokea katika video hii  wawili hao walijikuta wameingia katika mahusiano ya kimapenzi yaliyowapelekea mpaka kupata mtoto mmoja  wa kiume.Lakini wawili hao wameonekana wakisambaratika na kuachana kabisa baada ya kutupiana maneno katika kurasa zao za instagram.

Mwandada huyo baada ya kuweka picha hiyo , mzazi mwenzie Rayvanny aliamua kumjibu na kumwambia kuwa kwa sababu ajishajiita single mother anaomba abadilishe na jina lake la mwisho ambaol alikuwa akilitumia lililokuwa likimtuambulisha kuwa ni mpenzi wa Rayvanny.Mwanadada huyo ambae alikuwa akijiita Fayvanny baada ya kuchukua jina la mwisho kutoka kwa Rayvanny ameombwa kubadilisha jina hilo na mzazi mwenzie huyo baada ya kusemekana kuwa wameachana.

Hata hivyo katika account ya instagram ya mwanadada huyo amebadilisha jina hilo na  kujiita Fayma_96 na kufuta baadhi ya picha alizokuwa akipiga na mzazi mwenzie huyo, hata hivyo katiak ukurasa wa Rayvanny mwenyewe amefuta picha zote alizokuwa amepita na mzazi mwenzie ambae alikuwa akikaa nae katika nyumba moja kama mke na mume.

Fayhma na Rayvanny walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume anaejulikana kwa jina la Jaydan ambae umri wake hajafikisha hata mwaka mmoja tangu amezaliwa.

Mapenzi ya wasanii wengi yamekuwa yakiishia ukingoni na kuacha watoto wao wakilelewa katika mazingira mabovu.Kama wamegombana basi kama mashabiki wanawaomba waongee na kupatana ili kulea mtoto mabe bado ni mdogo mwenye huitaji wa malezi ya wazazi wote wawili.

 

ray vanny kuwakalisha magwiji kwenye tuzo za Uganda Entertainment Award

Msanii wa bongo fleva, chini ya lebel kubwa nchini Tanzania ya WCB mwenye single mpya inayokwenda kwa jina la ‘chuma ulete’ Ray vanny hivi juzi ametwaa tuzo kubwa nchini uganda inayojulikana kama Uganda Entertainment Awards ‘UEA17’.katika kipengele cha African Act of the Year .

katika kipengele icho ambacho ray vanny alikuwa anagombania na wasanii wengine wakubwa kama Davido,Wizkid ,na Vennessa Mdee  ambao wote ni wasanii wakubwa barani Africa na ray vanny aliibuka kidedea.Raymond amekuwa akionesha mafanikio kwani pia ni miezi michache tu ametoka  kushinda tuzo ya BET

Tunamtakia ray vanny kila lenye kheri katika kazi za muziki na pongezi nyingi ziende kwake.

Rayvanny arejea kuishi maisha ya ufukara

Msanii Rayvanny amewaza taswira ya yeye kuwa kufara, staa huyo wa Wasafi ameongelea taswira hii kwenye wimbo wake mpya ‘Chuma Ulete’.

Ray anaonekana akiishi maisha ya ufukara kwenye video yake mpya, alionekana akiteseka huku kungangana kupata riziki .

Staa huyo wa Wasafi aliachia wimbo wake mpya kwa YouTube, tazama video hio hapo chini:

Diamond, Victor Wanyama wamtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa

Rapa Ambwene Allen Yessayah maarufu kama AY anasherekea siku ya kuzaliwa kwake leo Julai 2017. AY amefikisha miaka 36 leo.

Mastaa wengi wamemtakia AY heri ya siku ya kuzaliwa kwake, rafiki wake wa karibu Victor Wanyama alikua miongoni mwa wale waliomtumia jumbe mapema.

AY na Victor Wanyama

“Happy bday big boss @aytanzania have a good one bro,” Victor Wanyama aliandika.

Diamond na Rayvanny pia walimtumia AY jumbe:

“Big Birthday wish to Msoja wange @jahprayzah and my Legend Brother @aytanzania …. Long Life!!” Diamond Platnumz

“HAPPY BIRTHDAY KAKA LAO @aytanzania Mungu Akupe maisha marefu yenye Mafanikio zaidi,” Rayvanny

 

Rayvanny aisuta Basata kwa kukosa kuenda kumpokea katika uwanja wa ndege

Rayvanny alipewa mapokezi ya kirais alipowasili Tanzania kutoka Marekani. Staa huyu wa Wasafi alishinda tuza la BET na kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda tuzo hilo.

Diamond, Harmonize, Babu Tale na mamia ya mashabiki walijitokeza kwa wingi kumlaki Rayvanny katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere.

Rayvanny ata hivyo ameisuta Basata kwa kukosa kuenda kumlaki katika uwanja wa ndege, alisema bodi hio ya sanaa nchini haikuonyesha picha nzuri na hatua yao.

“Kwa mafano, mimi nilivyochaguliwa kama BASATA walikuwa wameona. Wao ni wazazi walikuwa na chochote cha kusema lakini wakisema kwamba wanasubiri niende mimi mwenyewe au tunasubiri watuambie au hatuwezi kwenda kwa sababu hatujaambiwa. Wale ni wakubwa kwetu ni wazazi wetu tunategemea kwamba wanakuza sanaa yetu na sisi tunawaangalia wao walitakiwa kuwa kipaumbele sisi kutusaidia,” Rayvanny alisema.

Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza akiongea na Clouds FM alitetea bodi hilo kwa kusema kuwa Basata haikupata ratiba ya Rayvanny.

“Hakukuwa na mawasiliano mazuri alivyokuwa amekwenda na ujio wake lakini tungekuwa tunaifahamu ratiba yake Baraza kama ilivyo ada huwa hatuna budi ya kwenda kumpokea Airport, kwanza inaleta heshima. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kusema tusingeenda kumpokea ni kwamba mawasiliano hayakuwepo tangu anaenda na pia ningependa nikumbushe wasanii wanavyokwenda nje ya mipaka ya Tanzania ni vizuri tukaagana ili tukajua ratiba ikoje hata wakirudi tuwapokee,” Godfrey Mngereza alisema.

 

Rapa kutoka Kenya -Khaligraph aondoa video yake na Rayvanny kwa YouTube

Rapa Khaligraph Jones kutoka Kenya alimshirikisha Rayvanny kwa wimbo unaoitwa ‘Chali Ya Ghetto’ ambao uliwekwa YouTube mwezi moja uliopita.

Kutolewa kwa wimbo huo YouTube kumewashangaza watu wengi kwani ‘Chali Ya Ghetto’ ulikuwa na zaidi ya views laki moja.

Akiongea na Mseto East Africa, Khaligraph alieleza kuwa alitoa wimbo huo ile aiweke kwenye channel nyingine ya YouTube.

“Yes it’s true I pulled it down but it will be uploaded on another channel” Khaligraph Jones alisema.

 

Zari asherekea ushindi wa Rayvanny

Rayvanny aliwasili Dar jana kutoka Marekani ambapo alituzwa katika tuzo la BET. Muimbaji huyo alishinda katika kitengo cha Best International Viewers Choice Award.

Zari, ambaye hakua amesema lolote kuhusu ushindi wa Rayvanny, alisherekea ushindi wa Ray kwa kumpongeza kwa kupeleka Afrika Mashariki katika kiwango kingine

“Traffic imepunguka? We are so proud of you, you took East Africa and Africa in general on another level regarding the music industry. Be blessed @rayvanny cc @diamonplatnumz the Godfather of @wcb_wasafi where hits? are made,” Zari aliandika.

Wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki walimpongeza Rayvanny kwa ushindi wake. Jua Cali kutoka Kenya alisema ushindi wa Rayvanny unaupa sifa muziki wa East Afrika kwa kuutangaza zaidi.

“Unajua dream yetu sisi wote ni kupeleka ngoma za East Afrika huko nje. Unajua competition ziko nyingi sana, tunapigana na watu wa South Africa, West Africa, Marekani, watu wa Europe and the moment kuna msanii wetu anashiunda tuzo kama hiyo, kwa sababu hiko ni kitu kikubwa sasa kinaweka East Afrika mahali pazuri especially kwanza kiswahili. Unajua mimi ni mtu wa wa Kiswahili so nikiona msanii anaimba kwa Kiswahili na ameshinda inapendeza sana,” Jua Cali alisema akiwa katika Citizen Radio.

Jua Cali

 

“Kuna kipindi nilikosa hata nguo za kuvaa” Rayvanny asimulia safari yake kimuziki baada ya kushinda tuzo la BET

Rayvanny alifunguka kuhusu maisha yake ya awali kabla ya yeye kuwa mtu mashuhuri na kupata hela. Staa huyo wa Wasafi aliamua kuongea kuhusu maisha yake ya awali baada ya kushinda tuzo la BET.

Ray alimshukuru sana Madee ambaye alisema alimsaidia sana wakati bado alikua fukara, staa huyo aliishi na Madee alipokuja Dar kutafuta riziki.

“Nakumbuka Miaka Sita Iliyopita ndio kipindi Ambacho nilikutana na Unaemuona mbele yangu.kipindi hicho Sikujua nilichonacho pia sikujua Wapi nianzie na nini nifanye.Kilikua kipindi kigumu sana Kwangu sababu nilikua Mgeni Dar as salam.Lakini kaka angu @madeeali Alisimama namimi Kila Alipokua Akienda Alienda na mimi na hii yote ni baada yakuniona mnyonge Nisie na msaada.Nilijuana na Wadau na baadhi ya wasanii Kupitia kaka angu @madeeali Pia Alikua akinipeleka studio nakunishauri Vitu vingi sana vyakimaisha na mziki pia nakusisitiza kua Nisikate tamaa.

Rayvanny na Madee

 

“Nimepata Uzoefu Mkubwa wakutumbuiza mbele ya kundi la watu kutoka kwake.Kuna kipindi nilikosa hata Nguo zakuvaa Alikua akinipa hata nguo alizokua akizipenda yote kunistiri mdogo wake.Nakumbuka kuna kipindi Akasema mdogo wangu Ray jifunze gari,nikamkatalia nakumwambia kwamba mimi ntaendesha Wapi gari na Ntakuja lini kupata gari.Akaniambia mdogo wangu Unakitu Ambacho kitakusaidia baadae yote yatawezekana.Alianza kunifundisha Gari yake japo nilikua naigongesha gongesha kwenye mashimo sababu nilikua sijui lakini Alinivumilia hadi nikajua Pia Nikawa mjanja wavitu vingi na kujiamini kisa yeye.Siku Nilipomwambia Naenda Wasafi nilijua hatonielewa Lakini Ndio Alikua mstari Wa mbele mambo yangu yafanikiwe nae Akichangia mpaka #Raymondtiptop Akawa #Rayvanny Hadi leo Hii Tumechukua Tuzo kubwa duniani #BETAwards MUNGU AKUBARIKI KWA MOYO HUO HUO SINA CHA KUKULIPA MUNGU PEKEE NAKUSHUKURU WEWE NA FAMILIA NZIMA YA SENEDA…. HUU MWANZO MUNGU MWEMA @madeeali” Rayvanny aliandika.

Diamond: Ilibidi nipunguze kasi nyimbo zangu zisiwaue kina Harmonize, Rayvanny

Diamond ameeza kwanini alikosa kupata uteuzi wa tuzo la BET mwaka huu. Hit maker huyo wa ‘Marry You’ amewahi kuteuliwa mara mbili (2014 na 2016) kuwania tuzo hilo kwa kitengo cha Best International Act: Africa.

Akiongea katika kipindi cha XXL ya Clouds FM jana, Diamond alieleza kuwa alipunguza kasi yake kimuziki mwisho wa mwaka jana ili akuze kina Rayvanny, Harmonize na wasanii wengine.

Alieza kuwa msanii kupata uteuzi wa BET ni lazima aachilie nyimbo mfululizo na yeye aliwacha kutoa ngoma nyingi kwani kama angefanya hivyo nyimbo zake zingewaua kina Harmonize, Rayvanny na wengine.

“Mwakani lazima niingie, unajua kuna kitu kimoja…lazima uishi kwa plani na malengo…Na ukiangalia mwaka juzi mwishowe mbaka mwaka jana ulikua ni mwaka kuhakikisha nawashika vijana wa Kitanzania nao wasikike katika muziki. Na ili wasikike ilibidi mimi nipunguze kasi yangu kwasababu mimi naachilianga tu mawe, ilibidi nipunguze mawe niwashindirie tu hao mawe kina Harmonize, sijui kina nani Ray… wote…kwasababu nikiingia itakua ni mtafaruko. Ukiangalia mitaa ingine nimeanzisha lebo kuna nyimbo kama tatu, nyimbo zangu zingine ni mishirikisho tu. Ilibidi nipunguze kwasababu mimi najua nikiweka nyimbo na hawajakua na nguvu nyimbo zangu zitawaua. Na zile nomination zinataka mtu aachilie ngoma mfululu,” Diamond alisema.

Tazama mahojiano hayo hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=K_fRN6xFS8o

Ujumbe wa Wema Sepetu kwa Rayvanny ambao umewasisimua mtendao wa kijamii

Wasanii na raia wa kawaida wanampigia debe Rayvanny kushinda tuzo la BET – Viewer’s Choice Best New International Act.

Washidi watatuzwa terehe 25 Juni katika ukumbi wa Microsoft, jijini Los Angeles, Marekani. Waliochaguliwa wanapigwa kura na wale ambao watapata kura nyingi ndo watashinda tuzo walizoteuliwa.

Wasanii wa Bongo wamekua wakiwaomba wafwasi wao wampigie kura Rayvanny ili aweze kushinda tuzo hizo la kimataifa.

Ujumbe ya Wema Sepetu kwa Rayvanny akiwaomba watu wampigie kura umesisimua mtendao wa kijamii. Mrembo huyo aliambia Rayvanny tarayi yeye ni mshindi, alisema Rayvanny anastahili kabisa.

“Its Jus a Nomination But To Me You are Already a Winner…. Well Deserved…!!! V-Vanny Boy…!!!! ???????? #IPickRayVanny …. Nd it doesn’t stop here… Keep the Votes Going… ??????” Wema Sepetu aliandika.

 

Rayvanny aachia wimbo mpya aliyoshirikiana na mfalme wa rap kutoka Kenya (Video)

Hii ni mara ya pili Rayvanny kufanya kolaba na msanii kutoka Kenya. Mwimbaji huyo wa Wasafi alishirikiana na Bahati kuachia wimbo unayoitwa ‘Nikumbushe’ ambayo ni hit kubwa Kenya.

Rayvanny tena ameshirikiana na msanii mwingine kutoka Kenya anayeitwa Khaligraph Jones. Wawili hao wametoa wimbo unaoitwa ‘Chali Ya Ghetto’.

Khaligraph hudai kuwa yeye ndiye mfalme wa hip hop nchini Kenya. Tazama video ya wimbo wao mpya hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=9pIYpVNeNfQ

Alichosema Rayvanny baada ya kuteuliwa kuwania tuzo la BET 2017

Diamond Platnumz amekosa kupata uteuzi kuwania tuzo la BET 2017 lakini Rayvanny ameteuliwa katika kitengo cha ‘Best International View’s Choices’ akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika katika kitengo hicho.

Rayvanny aliambia Ayo TV alikuwa studio akirekodi ngoma mpya ndo habari ikamfikia kuwa ameteuliwa kuwania tuzo la BET.

Diamond ata hivyo hajateuliwa kuwania tuzo la BET 2017; hit maker huyo wa ‘Marry You’ amewahi kuteuliwa mara mbili (2014 na 2016) kuwania tuzo hilo kwa kitengo cha Best International Act: Africa.

Tazama orodha hio hapo chini uone wasanii kutoka Afrika ambao waliteuliwa kwa kitengo cha Best International Act: Africa 2017:

Best International Act: Africa

AKA (South Africa)

BABES WODUMO (South Africa)

DAVIDO (Nigeria)

NASTY C (South Africa)

STONEBWOY (Ghana)

TEKNO (Nigeria)

WIZKID (Nigeria)

MR EAZI (Nigeria)

 

Alikiba ako na beef kubwa sana na Diamond lakini anapenda nyimbo za wasanii kutoka Wasafi

Alikiba na Diamond hawali chungu moja kwasababu kadhaa wa kadhaa, hata hivyo Kiba hana beef na wasani wengine kutoka Wafasi.

Hit maker huyo wa ‘Aje’ ameonekana kwenye video akifurahia and kuimba wimbo wake Rayvanny ‘Kwetu’ akiwa kwa gari.

Rayvanny pia amewai kusikika akisema kuwa hana tatizo lolote na Alikiba. Alisema kuwa yeye humchangamia Kiba kokote wakutanapo.

“Alikiba huwa nikikutana naye napiga naye stori, tunasalimiana tunacheka, ananiambia kuwa nafanya kazi nzuri, hatujawahi kuongea sana. Ikitokea siku naweza kufanya naye kolabo kwasababu ‘end of the day’ wote tunafanya muziki ni biashara pia, mashabiki wetu wanapenda kuona ‘combination’ za watu tofauti tofauti, hata nikikutana naye hatufungiani vioo,” Rayvanny aliambia Clouds FM kitambo.

Rayvanny