Ujumbe wa Roma Mkatoliki kwa wasanii wa Bongo: Muache kutegemea media

Roma Mkatoliki ametoa ujumbe kwa wasanii wa wenzake, staa huyo anayetamba kwa wa wimbo mpya ‘Zimbabwe’ amewataka wasanii wa Bongo waache kutegemea media kupush ngoma zao.

Akiongea na The Playlist ya Times FM, Roma alisema kuwa kuna baadhi ya wasanii ambao wanapata upendeleo wa ngoma zao kupata airtime katika media.

Rapa huyo alionya kuwa mtindo huo ni hatari kwani wasanii hao wanapobwagwa na media mara nyingi huwa wanavyoshindwa kuishi kabisa.

“Yeah, off course asilimia mia moja kuna wasanii wanabebwa na media na pale media inapokata mirija utaona the way wanavyoshindwa kuishi kitu ambacho si kizuri, nashauri mtu atumie kipaji chake halafu aweze kujua at any time unaweza ukabwagwa na media halafu ukatakiwa usimame wewe kama wewe sasa kitaa unacho?, kwa sababu mimi naamini cha kwanza kitaa. Kitaa kikikuelewe media ni bless tu, utakuta ni Miaka minne/mitano wimbo wangu haujaingia kwenye chart za top ten lakini nikidondoka kwenye show na huo wimbo, bwana wee!!, kwa hiyo ile show yangu ya Mbagala ndio top ten yangu,” Alisema Roma.

 

Nay Wa Mitego: Nliumizwa sana na maneno ya Roma Mkatoliki

Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay Wa Mitego amefunguka kuhusu bifu yake na Roma Mkatoliki iliyoonza baada ya Roma kutekwa nyara miezi kadhaa iliyopita.

Roma aliongea maneno ya kumkashifu Nay Wa Mitego mara baada ya yeye kuachiliwa na watu waliomteka nyara akiwa na wenzake kwa studio yake.

Nay Wa Mitego

Nay ata hivyo hana machungu na Roma, rapa huyo alisema yeye bado anamtakia mema Roma hata kama maneno aliyosema juu yake yalimuuma sana.

“Roma anatakiwa ajue kwamba mimi ni mmoja kati ya wasanii ambao walishinda kutwa nzima kwenye studio yake ya Tongwe Records na kituo cha polisi, toka siku aliyotekwa hadi siku aliyopatikana, lengo likiwa ni kutaka kujua tunasaidiana vipi ili aweze kupatikana. Akitaka kuthibitisha hilo amuulize mkewe, lakini nikashangaa baada ya kupatikana eti akanikashifu, kila nikikumbuka inaniumiza, sema mimi ni mwanaume siweki vitu rohoni, na pia nimeipenda sana ngoma yake ya Zimbabwe, Roma ni rapa mkali, sina kipingamizi juu ya hilo,” amesema Nay Wa Mitego.

Roma Mkatoliki

 

Mke wa Roma amchana mrembo aliyemkalia Roma akitumbuiza jukuwaani hivi karibuni

Kuolewa na msanii ni kitu ngumu sana kwani unapaswa kuwa na subra ya kuelewa kuwa hiyo pia ni kazi. Hata hivyo mke wa Roma ameonyesha kukerwa na mwanamke aliyemkalia Roma wakati alipokuwa akipiga show yake ya kwanza tangu tokeo lake la kutekwa miezi kadhaa iliyopita.

Mrembo huyu alifunguka kuhusu tekeo hilo kupitia mtandao wake wa Instagram huku akisema kuwa alitamani sana kupanda jukwaani kumshusha yule binti….aliandika kusema,

 

Kuwa Na Mume Msanii Wakati Mwingine Ni #Stress Nyie Acheni Tu Jamani!!!
.
.
Aaaf kuna vibinti ndiyo kama vinafanya makusudi

Kama Huyu!!!
Nilitamani Nipande Jukwaani Nikamshushe.
Sijui Hata alivyombeba alimpeleka wapi!!!!
.
.
Aaaah Ntafanyaje Mie Na Ndiyo Kazi Inayonifanya Niende Saloon!! .
.
By the way uliua…Show nzuri kama kawaida yako
Cc @usimsahau_mchizi_roma@usimsahau_mchizi_roma

Hata hivyo mashabiki wengi walimuunga mkono huku wengine wakimwambia kuwa mambo Kama hayo hutendeka lakini ikiwa Roma ni wake hakuna mwanamke yeyote anaweza kumchukua.

Tazama video hiyo hapa;

https://youtu.be/VA66Muo5-KE

Roma aweka wazi kuwa amewasamehea na kuwasahau waliohusika na kutekwa kwani

Roma ambaye ni msanii wa hiphop bongo alitekwa miezi kadhaa iliyopita lakini akapatikana baada ya siku kadhaa kitu ambacho yeye Kama mwanadamu hajaweza kusahau.

Hivi karibuni akizungumza na Times FM, Roma alifunguka kudai kuwa tangu awachiliwe serikali ya Tanzania haikumsaidia kwa njia yoyote. Msanii huyu alisema kuwa familia, marafiki na mashabiki ndio walisimama na yeye hadi kupona kwake. Alipoulizwa ikiwa Serikali ilimjulia hali wala kumshughulikia alijibu kwa kusema,

“Lahashaa! Hapana juu kwa juu tuu polisi, polisi Mwananyamala PF3 sijui nini ile, baada ya pale nikajiongoza mimi mwenyewe na familia yangu,so ikawa hivyo tuu“

Hata hivyo Roma alisema kuwa ameshawasamehe na amewasahau wote waliohusika na kutekwa kwake.

“Yaliyopita yamepita tunasamehe,tunasahau waliohusika Mungu atawahukumu na mkono wake na Mungu atupe neema uvumilivu na neema ya kuwasamehe…Lakini usidanganyike na mtu anakwambia sijui alikuja akatoa bugana lake au sijui akatoa hela ya panadol, Lahashaa!“

Roma Mkatoliki arejelea kazi yake ya ualimu

Watu wengi hawakua wanajua kazi aliyokuwa akifanya Roma Mkatoliki kabla ya kujiunga na sanaa. Rapa huyo anarudi shuleni kwa muda mfupi.

Roma alikua mwalimu wa somo la Hisabati kabla ya kuamua kuanza kuangusha mistari kwa ngoma zake za kuvutia.

Rapa huyo alienda kufunza hisabati katika shule ya msingi ya Mchikichini iliyopo Mbagala-Kibondemaji jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Showbiz Xtra kabla ya kuelekea shuleni, Roma alisema kuwa ameamua kuchukua nafasi hiyo kwanza kujikumbushia kazi yake ya ualimu.

“Somo la hisabati ni miongoni mwa masomo yanayotengwa sana na wanafunzi wengi hivyo basi nikiwa kama mwalimu niliyepitia kufundisha somo hili, nimeona vyema kuhamasisha wanafunzi walipende na kuliamini. Nitagawa vitabu vya hesabu kwa wanafunzi wa darasa la saba na pia kuwafundisha somo hilo. Kila mmoja nitahakikisha amehamasika na somo hili na kulipenda kama masomo mengine,” alisema Roma.

 

Roma Mkatoliki aeleza kwanini muziki wake sio chanzo cha yeye kutekwa nyara

Rapa Roma Mkatoliki na wenzake walitekwa nyara wiki kadhaa zilizopita wakiwa kwenye studio. Kupotea kwa Roma kulizua utata, watu wengi waliamini kuwa muziki anaoufanya Roma ndo ulikua chanzo cha yeye kutekwa nyara.

Roma alisemekana kuwa aliukosoa serikali kupitia mistari zake kwa wimbo wake, watu wengi walihusisha tukio la kupotea kwake na muziki anaoufanya.

Lakini akizungumuza katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, Roma alikana dhana hilo. Alisema muziki wake hauvunji sheria yoyote.

“Kwanza niweke sawa, naamini katika muziki ninaofanya na naamini sijafanya kitu kibaya, sivunji sheria na wala siongei maneno mabaya

“Naumia sana nikiona mtu anautafsiri vibaya muziki wangu. Mimi sifungamani na upande wowote, hata ukiniuliza kadi ya chama mimi sina kadi ya chama chochote. Kwa sababu nikichukua kadi ya chama chako utasema nimekuwa mwanafamilia wako wewe ni baba ukikosea nitakunyooshea vipi kidole?. Kwa hiyo napata sana ukakasi nikiona watu Roma wanamtafsiri tofauti, naumia sana,”alisema Roma.

“Nliamini kuwa sitakuwa na wewe” Mke wa Roma Mkatoliki aeleza hofu iliompata baada ya bwana wake kupotea

Wiki chache zilizopita Roma Mkatoliki alitekwa nyara na watu wasiojulikana alipokua kwenye studio. Msanii huyo aliachiliwa huru baada ya wasanii kulalamika.

Soma pia: Roma Mkatoliki aelezea yote yaliyomfanyakia baada ya kutekwa

Mke wa Roma Mkatoliki, Nancy, alisherekea siku ya kuzaliwa kwake Jumapili hii Aprili 23. Nancy aliongelea kupotea kwa mumewe.

Alisema kuwa alikata tamaa kumpata mume wake baada ya siku kadhaa kupita bila kuskia lolote kutoka kwa polisi ama watu waliomteka nyara mumewe.

Nancy na Roma Mkatoliki

“lifika wakati nilikata tamaa na kuamini kuwa sitakuwa na wewe katika sikukuu ya kumbukumbu yangu ya kuzaliwa ya mwaka huu!! Lakini Mungu Baba Wa Mbinguni akasema no. #MyBirthday2017,” aliandika Nancy kwenye Instagram.

 

Mke wa Roma Mkatoliki azungumza mara ya kwanza baada ya mumewe kutekwa

Ni wiki chache tu kutoka Roma Mkatoliki awachilie huru baada ya kutekwa na watu asiyewatambua.

Alitekwa kwenye sttudio yake lakini baada ya kulalamika kwingi kwa wa Tanzania akaachiliwa.

Sasa amo nyumbani ana pumzika na mke wake Nancy Mshana amezugumza kwa mara ya kwanza kutoka muwewe atekwe.

Mrembo huyo ametumia maneno ya kwenye Biblia kutoka katika kitabu cha Yeremia kufikisha ujumbe wake kwa watu ambao wamemfanyia ubaya mume wake na kusema kuwa na wao watakutwa na mabaya hayo.

“(Yeremia 30:16-17) Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo. Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya jeraha zako, asema Bwana.Ameen” Alinukuu mke wa Roma Mkatoliki.

Bali na hilo amewashukuru wa Tanzania wote ambao wamesimama na familia yake wakati huu mgumu.

Mke wa Roma aeleza alivyozunguka vituo vyote vya polisi kumtafuta mumewe ambaye hajulikani aliko

Mke wa Roma, Nancy amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya mumewe, Roma kupotea. Kulingana na stori mitandaoni kuna fununu kuwa Roma na rafiki yake walichukuliwa na polisi wakiwa studio za Tongwe Record Masaki jijini Dar es Salaam.

Kama Watanzania wenzake Nancy hafahamu alipo mumewe ambaye ni baba ya mtoto wake, Ivan. Akizungumza na wanahabari, Nancy ameeleza kuwa amemtafuta mume wake katika vituo vya polisi lakini kila andako hakuna anayerecords za Roma Kutiwa mbaroni. Alisema,

Mimi kama mke wa Roma mara ya mwisho niliwasiliana na mume wangu jana saa kumi na mbili jioni, akaniambia anaelekea Tongwe Records kwajili ya kazi zake za kila siku. Baada ya hapo sikuwa nampata tena kwenye simu lakini nikachukulia ni kawaida tu simu imezima, nimekuja kuamka saa 7 nikapokea simu kutoka kwa rafiki yake akaniambia uko na Roma nikamwambia hapana alikuwa Tongwe, akaniambia kuna taarifa kwenye mitandanao na mimi nikaingia nikakuta hizo taarifa kama walizopata watu wengine. Baada ya hapo nikaanza kutafuta watu wa kunisaidia, baadhi ya ndugu zangu wameangaika vituo vyote vya polisi Roma hayupo, hadi sasa hivi sifahamu yuko wapi, kwa ufupi sina ninachokijua wala ninachokifahamu. Jitihada zangu za kutafuta kwenye vituo vyote vya polisi nimemaliza.

Hivi sasa watanzania kwa ujumla wameungana mikono katika jitihada za kumtafuta Roma ambaye mpaka sasa hajulikani aliko.

“Uoga ni uzembe” Babu Tale amtaje anayemlaumu kwa kupotea kwa Roma Mkatoliki

Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wamepotea bila ya yeyote kujua nani aliwateke, wamepelekwa wapi na nia yao ni ipi.

Wasanii wengi wamehofia usalama wa Roma na wenzake kwasababu hata polisi hawajui nani aliwateka. Watu wengi kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Roma Mkatoliki

Babu Tale, meneja wa Diamond, ameweka wazi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ndiye anafaa kulaumiwa kwa kupotea kwa Roma.

Babu Tale amemtaka Makonda awaeleze Watanzania kule Roma alipo, anasema kuwa yeye ndiye kiongozi wa kamati ya usalama Dar es Salaam kwahivyo anafaa ajue Roma alipo.

Paul Makonda

Uoga ni uzembe me nazani mwenye jukumu la kujua Roma yupo wapi ni Mkuu wa koa sababu yeye ndio kiongozi wa kamati ya usalama ya mkoa sasa ikiwa tumezunguka vituo vyote vya polisi na mwenzetu atumuoni nani wa kumfuata kumwambia tunamtaka mwenzetu kama sio @paulmakonda me naanza hili bila uoga mkuu wa mkoa naomba utusaidie kutuambia mnzetu @roma2030 alipo. Tukutane Tongwe mida hii me nipo kwa foleni wakuu #uogauzembe#freeroma,” Babu Tale aliandika kwa Instagram.

 

Diamond, Babu Tale, Vanessa Mdee, Professor Jay wahofia usalama wa Roma Mkatoliki na wenzake waliotekwa usiku wa Jumatano

Rapper Roma Mkatoliki na vijana wengine walitekwa usiku wa Jumatano wakati walipokuwa studio ya Tongwe Records. Watu wasiojulikana walipotea na Roma na wenzake.

Mpaka sasa bado hakuna anayejua wamekamatwa na nani na kwa kosa gani, na pia bado haijafahamika wamepelekwa wapi. Lakini watu kwenye mitandao ya kijamii wanahusisha kitendo hiki na masuala ya siasa yanayoendelea nchini hivi sasa.

Roma Mkatoliki

Wasanii kadhaa wamekashifu kitendo hicho:

Professor Jay: ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!

Diamond: Wakati mwingine natafakari sijui hata wapi tunaelekea… lla kwakuwa Mwenyezi Mungu ndio Mpangaji wa yote basi naamini hata hili litapita tu… Mwenyezi Mungu aipe nguvu familia ya @roma2030 na wanamziki wenzetu wote ambao hadi sasa haijajulikana walipo..

Vanessa Mdee: Wherever you are, God is Bigger than, Stronger than, Realer than all the other forces that be. Stay UP brother @roma2030 #VivaRoma #FreeRoma #FreeMoni roho inauma na nimetoka kumsikiliza mkeo redioni hajui hata ulipo sasa ndiyo nini ?????is this where we are at now? Ma studio yanavamiwa, watu wanakamatwa kama wanyama pori. Aaaarrrrgh

AY: Vyombo husika vifanye uchunguzi wa haraka tujue hali za wasanii wenzetu wako kwenye hali gani..@romamkatoliki Mungu yupo pamoja nanyi awaepushie lolote baya.. @tongwerecords @j_murder_tongwe

Babu Tale: Baba wa familia kupotea kama kuku na sisi wadau kuishi kupost tu hii sizani kama itatusaidia tuamke sote kwa pamoja saa sita mchana tukutane Tongwe Record tujue mstakabal wa mwenzetu @professorjaytz @efm_93.7 @cloudsfmtz #freeroma

 

Baada ya Nay wa Mitego, Wasanii wengine wawili mashuhuri kukamatwa

Huzuni imejaa Tanzania nzima baada ya ripoti kutokea kwamba wasanii wengine wawili walikamtwa usiku tulioamkia.

Roma mkatoliki alikamatwa jana kwenye Tongwe Records na mpaka wakati huu hakuna anayejua akuwepo.

“Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..

Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!” professor Jay alitangaza kwenye instagram.

Wasanii wengi ikuwepo Nay wa Mitego wamekashifu tendo hilo.