Lulu Diva Adai Hakuna Mwanaume Kama Idris

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maauru kama Lulu Diva ameibuka na kumwagia sifa kibao msanii wa sanaa ya vichekesho Idris Sultan na kudai kuwa hakuna mwanaume kama Idris Sultan.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lulu Diva aliandika kuwa hakuna mwanaume mzuri kama Mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Lulu Diva alitakiwa afafanue kwanini ameamua kumwagia sifa hizo Idris  alisisitiza kwamba, ameamua kuandika maneno hayo kwa sababu kaka yake huyo ni handsome (mzuri) na uzuri wake hauwezi kuufananisha na mwanaume mwingine yeyote Bongo.

Ndio ni kweli nimeandika hivyo kwenye akaunti yangu ya Instagram kwa sababu Idris ni handsome jamani kwani we huoni? Halafu kila siku mi’ huwa namw-ambia hata tukio-nana sema nikaona haamini ndio maana nikaposti kuonesha msisitizo”.

Lulu Diva aliweka wazi kuwa yeye na Idris ni ndugu kwa maana kuwa ni Mtoto wa mama mdogo na mama mkubwa

Msanii Kutoka Kenya Atangaza Kufa Kuoza Kwa Idris Sultan

Msanii wa muziki kutoka DRC Congo ambaye anafanya Shughuli zake za kimuziki nchini Kenya Alicious Theluji ametangaza kuwa amekufa ameoza kwa Mchekeshaji MBongo Idris Sultan.

Alicious ambaye amedai ameshindwa kujizua na hisia zake amefunguka na kudai kuwa kwa sasa hakuna mwanaume anayemvutia na kumpenda kama ilivyo kwa Idris Sultan.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha redio cha Citizen Kupitia kipindi cha Mseto East Africa, Alicious ameweka wazi kuwa Idris ni Crush Wake Lakini pia ni mtu ambaye anampenda sana.

Kwa sasa nipo Single, Idris Hivi karibuni nakuja Tanzania nina Media tour naomba unipokee Airport”.

Lakini pia mrembo huyo aliweka wazi vigezo vya nwanaume anayemtaka na kumtaja kabisa kuwa anamtaka Idris:

Navutiwa sana nadata, umeshawahi kuona mabega ya Idris wewe?”.

 

Idris Azungumzia kukutana na Wema

Msanii Idris Sultan amefunguka na kusema kuwa tangu  mwanadada wema sepetu  apungue mwili wake na muonekano mpya na hata kufungua duka lake la nguo  bado   hawajaonana kwa muda mrefu na hata muonekano wake huo mpya amekuwa akiuona kwenye  kwenye mitandao tu.

Idris anasema kuwa hawajawahi kukutana lakini amekuwa akimpigia simu na hata kumpongeza kwa sababu ya kufungua duka  la nguo za watoto.

Tangu Wema apungue sijawahi kukutana nae lakini nilimpigia simu kumpongeza kuhusu kufungua duka lake, ila tu kwa sasa kila mmoja amkuwa akifanya mambo yake.

Wawili hao waliwahi kuwa katika mahusiano kwa miaka kama miwili iliyopita, lakini kila mara ema anasema pamoja na kwamba wameshaachana lakini hawezi kumchukia Idris.

Idris Sultan Afungukia Tetesi Za Kujisogeza Kwa Mobetto

Staa wa filamu aina ya Komedi, Idris Sultan amefungukia tetesi zinazomkabili za kujisogeza kwa mwanadada anayetrend Hivi sasa kwenye Mitandao ya kijamii Hamisa Mobetto.

Tetesi hizo zilianza kusambaa Baada ya Idris kuonekana akikomenti sana kwenye picha za mrembo huyo mara tu Hamisa anapoposti picha zake basi Idris anekuwa akimuachia makopa tu.

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa, Idris kwa sasa ameamua kujipooza kwa Mobeto.

Wamekuwa wakiongozana kila kona kama kumbikumbi, ndiyo kwanza mapenzi yao yanachipukia“.

Baada ya tetesi hizo kusambaa, Gazeti hilo lilimsaka Idris ili kuupata Ukweli wa mambo kutoka kwake ambapo moja kwa moja alikana kabisa tetesi hizo na kumwaga povu:

Hebu acheni mambo yenu ya ajabu bwana kwa hiyo kila msichana nitakayeongozana naye basi ni mpenzi wangu? Halafu mmesahau kwamba mimi na Hamisa ni washkaji kitambo tu? Sasa kwa nini leo muanze kusema natoka naye? Muda mwingine watu wakikosa kazi ya kufanya huwa wanatunga tu vitu vyao”.

 

Idris Sultan Amwagia Misifa Kibao Shilole

Mchekeshaji na msanii wa Bongo movie Idris Sultan ameibuka na kumwagia sifa kibao Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole.

Siku ya jana ilikuwa ni siku ambayo Shilole alikuwa a ashehereka siku yake ya kuzaliwa na mastaa mbali mbali walimposti katika kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii.

Mmoja wapo ni Idris Sultan ambaye alimposti na kumuandikia ujumbe mzito ambapo ndani ya ujumbe huo alindika ni Jinsi gani msanii huyo ni mchapakazi na anajituma tofauti na mastaa wengine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris Sultan aliweka picha ya Shilole na kuandika ujumbe huu kumlenga Shilole:

Ana Nyumba, ana biashara zaidi ya tatu, ana watoto, ameolewa na ni maarufu na bado ana baby face, Mimi Nina kingereza tu. Tuendelee kuendekeza ujinga tutajua nani anamcheka mwenzake”.

Mbali tu kuwa msanii wa Bongo fleva na Bongo movie, Shilole pia ni mjasiriamali ambaye ni ana mgahawa wake anapouzia chakula pia anamiliki bidhaa zake mwenyewe kama vile Chili na nyinginezo.

Idris Sultan Alamba Shavu Nono

Muigizaji wa Bongo movie na komedian maarufu Idris Sultan amedaiwa kulamba shavu nono katika ulimwengu wa Burudani Baada ya safari yake ya nchini Afrika ya kusini.

Global Publishers wanaripoti kuwa Idris Sultan amealikwa kuhudhuria tamasha kubwa la  Komedi lililoandaliwa na Comedy Central, moja kati ya taasisi kubwa Duniani katika tasnia ya ucheshi na uchekeshaji linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Afrika Kusini.

Mwaliko wa Idris unakuja baada ya mafanikio makubwa katika Tamasha la Sex Tour ambalo liliwavuta maelfu  ya wapenzi wa comedy hapa nchini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na GPL, Idris alisema lilikuwa na lengo kuu la kuburudisha na kuelimisha watu katika maswala mbali mbali ya kijamii kwa kutumia Sanaa ya uchekeshaji.

Tarehe 1 Desemba, Idris Sultan aliandaa tamasha la kwanza la Sex Tour katika ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki jijini Dar ambapo watu zaidi ya 7,000 walihudhuria huku wengi wakilalamika kukosa ticket. 

Sex Tour imekua tamasha kubwa zaidi la comedy kuwahi kutokea nchini  Tanzania na kufananishwa na baadhi ya matamasha makubwa  ya muziki”.

 

Idris Aandika Barua ya Wazi kwa Mh Rais Baada ya Kufutwa kwa Sherehe za Uhuru

Mchekeshaji maarufu nchii ambae pia ni moja ya wahamasishaji wakubwa bongo Idris Sultani ameamua kumuandikia mh Rais barua ya kile anachokiamini baada ya kufutwa kwa sherere za kuhadhimisha kupatikana kwa uhuru wa Tanzania.

Idris anasema kuwa kufutwa kwa sherehe hizo kutaathiri sana hali ya uzalendo hasa kwa vijana na  watoto waliopo ambao bado wanahitaji kujua historia ya Tanzania.

Idris anasema kuwa anaogopa sana swala la kufutwa kwa sherehe hizo kwa sababu kuna fanya kuptea kwa uazlendo kidogo kidogo ukizingatia kuwa vijana hao ndio watakaokuja kufanya kazi katika ofisi za serikali bila kuwa na historia ya kile wanachokifanyia kazi.

Idris anasema kuwa pamoja na kwamba wanasema pesa za sherehe ziende kwenye matumizi muhimu kama afya lakini ni vigumu kulinganisha vitu hivyo vyote zaidi ya kuwa vinahitajika vyote na ndio maana  ni ngumu hata kuchagua kati ya kula na kupumua.

 

Idris Sultan Aandika Barua Ya Wazi Kwa Rais Magufuli Baada Ya Kufutwa Kwa Sherehe Za Uhuru

Mchekeshaji maarufu kwenye tasnia ya Bongo movie Idris Sultan ameibuka na kumuandikia barua ya wazi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Kwenye barua hiyo Idris ameongelea ishu ya kufutwa kwa sherehe za uhuru kwa mwaka huu na kudai kuwa sherehe hizo ni za muhimu sana kwani zinajenga ari ya uzalendo kwa vijana.

Idris kwenye barua hiyo fupi, aliyoichapisha kwenye mitandao ya kijamii ameeleza kuwa, sherehe hizo zinafaida kubwa kwa vijana ikiwemo kujenga uzalendo na kujua historia ya taifa lao.

Dear Mheshimiwa Raisi,

I love you work ethics na jinsi ulivyo na uchu wa maendeleo ndio maana nilikusapoti 2015. Nasema hayo ili ujue I’m with you mostly na akupendae sio mnafki. Hii nchi inapoteza wazalendo siku hadi siku na siwezi laumu kwasababu watu wanakosa passion.

This is a beautiful country tena sana ila watu wake hatujui uzuri wa hii nchi na tuipende vipi. Kutengeneza uzalendo kuna umuhimu wa kuijua historia yetu kwa undani. Ili watu waweke attention kwenye historia basi muhimu kuonyesha uzito wa matendo yaliyofanyika katika historia.

Kuonyesha uzito huo basi ni kuadhimisha makubwa yote yaliyofanyika katika historia. Kama nilivyosema juu “Tunapoteza wazalendo” vijana wadogo sasaivi wanakua wakiichukulia nchi poa poa tu. Hawajui uzito wa uhuru walionao kutembea kwenye hii ardhi.

Vitu kama hospitali ni muhimu sana ila natamani ingekuwa kwenye bajeti yake ya afya. Isifike wakati tuchague kati ya kusherehekea juhudi za kutafuta uhuru wa nchi na afya. Kila sula lina umuhimu wake. Ni ngumu kuchagua either ule au upumue. We need both.

I’m scared we are losing patriotism na kidogo kidogo tutatengeneza vijana wanaopata madaraka katika ofisi yako ila wataangalia maslahi yao tu. Yes inafika huko. It’s too late umefanya maamuzi na you’re the president ndio kauli ya mwisho ila naomba ulione hili katika jicho langu

Idris Sultan Awaacha Njia panda Mashabiki na Sex Tour

Mchekeshaji maarufu, idris sultana amewaacha mashabiki wake katika njia panda baada ya kuweka katika ukurasa wake wa instagram kuhusu tour wake mpya inayokaribia kufanyika hivi karibuni mwaka huu huku ikiwa haina maelezo yoyote.

Mashabiki wake walitaka sana kujuakuhusu tour hiyo ambayo idris mwenyewe ameiita sex tour huku mashabiki wake wakitaka kuua kujua sex tour hiyo inahusiana na nini hasa au kama ni sex kama inavyoaamnisha itakuwa ya  mtindo gani.

Katika ukurasa wake wa instargarm Idris aliandika kwa kuweka picha hii na kisha kusema kwa maneno “mbona itakuwa ishu sasa , #sextour2018..tunavaauhusika

Idris Sultan Atangaza Ajira Kwa Vijana 15 na Mshahara Wa Milioni 1

Mchekeshaji maarufu kwenye mitandao ya kijamii Idris Sultan amefunguka na kutangaza fursa ya kazi kwa vijana 15 wa Kitanzania.

Idris aliongea hayo siku chache zilizopita baada ya kufanikiwa kufikisha mashabiki milioni tatu katika ukurasa wake wa Instagram,

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris ameandika;

Nimefikisha 3 million followers instagram na kushukuru jamii kwa hilo nitawapa ajira vijana 15. Vijana watano kwa kila mmoja milioni. Pata kwa jamii rudisha kwa jamii. We help each other before they help us“.

https://www.instagram.com/p/Bpq0Py8nEyZ/?utm_source=ig_web_copy_link

 

Idris Sultan Afungukia Picha Yake Ya Utupu

Comedian maarufu na Muigizaji wa Bongo movie Idris Sultan amefunguka na kuiongelea picha yake ya utupu ambayo ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita.

Picha inayodaiwa kuwa ni Idris imekuwa ikisambaa sana mtandaoni Idris sasa anadai kuwa, ana imani aliyevujisha picha hiyo ni mchumba wake wa zamani na picha hiyo ni ya miaka miwili iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris ameandika haya:

Wanaonipenda wanajua mimi mtu wa aina gani, ndugu zangu wanajua mimi mtu wa aina gani, marafiki zangu, mchumba wangu ananifahamu vyema sana, mashabiki wangu wananijua sanaaa hadi wakati mwingine wanajua nini nitasema kabla sijasema. Kampuni zinazonidhamini zinafahamu mimi ni mtu wa aina gani. Hii ndio nguvu niliyo nayo, ni nguvu ya mapenzi”.

Idris anadai kuwa, watu wanaovujisha picha zake mtandaoni ni wenye nia mbaya wanaojaribu kuficha uchafu wao: Sasa ficheni uchafu wenu wa sasa kwa kuweka uchafu wangu wa miaka miwili iliyopita na mwone ni vipi Allah ataendelea kunibariki na mashabiki wangu… Sijutii, ni mitihani tu. Nakusamehe na nakuombea Allah akusamehe pia. Makosa yangu yatabaki kuwa yangu #NguvuYaMapenzi.

Diamond Amuweka Idris Katika Wakati Mgumu.

Mchekeshaji maaruf nchi Idris sultani amejikuta akiwa katika wakati mgumu kutokana na kile alichokifanya Diamond katika sku yake ya kuzaliwa ambacho kwa upande wake anaona kabisa kuwa haitawezekana kuwafanyia watu wa kwao.

Idris ambae pamoja na kumpongeza kwa hatua kubwa aliyoifikia ya kuwakumbuka wananchi wa sehemu alipotoka lakini pia anasema kuwa kitu alichokifanya Diamond kinamfanya yeye hashindwe kueleweka kwa watu wa arausha kwa sababu anaona kabisa kuwa hawezi kurudisha fadhira kama alizofanya diamond  na anaona kuwa kwa vitu anavyotaka kuwapelekea hakuna atakae muelewa.

Idris aliandika “kitu alichofanya diamond kimenifanya nishindwe kulala , najiuliza narudi vipi Arusha kugawa kilo mbili za mchele, elfu 20 ya luku, kisado cha mafuta ya kula  na tshirt ya sportpesa,wana watanipiga waniue.”

Ukiachana na kuwa wawili hao wameshapatwa na skendo za kuwa wanachangia wanawake lakini siku zote haijawahi kusikika kuwa wamekuwa na bifu au kukitana na kugombana aua kutupiana maneno , zaidi sana Idris amekuwa akiweka na maneno ya utani kutokana na kazi yake.

Idris Sultan Amuombea Msamaha Maua Sama

Msanii wa Bongo movie na Comedian maarufu Idris Sultan ameibuka na kumuombea msamaha Msanii wa Bongo fleva Maua Sama baada ya kuwekwa rumande kwa siku tatu.

Siku chache zilizopita Maua Sama na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown walitiwa nguvuni na jeshi la polisi baada ya video iliyowaonyesha wakiwa wanakanyaga pesa kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya kusambaa kwa video hiyo toka jumapili mpaka leo Soudy Brown na Maua bado hawajapata dhamana.

Idris Sultan ameibuka na kumuombea radhi Maua Sama na kuomba aachwe huru na Awe mfano wa kuigwa na jamii:

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris Sultan ameandika:

https://www.instagram.com/p/Bn6REJDhCPF/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1j9q2eztrp313

 

Idris Sultan Adaiwa Kumchukua Ex wa Diamond

Msanii wa Bongo movie na comedian maarufu Idris Sultan anadaiwa kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Ex girlfriend wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kumekuwa na tetesi kuwa Video vixen ambaye hakauki vituko Kwenye mitandao ya kijamii Irene Geofrey maarufu kama Lynn ana banjuka na Idris Sultan.

Tetesi za Mahusiano ya wawili hao zilianza juzikati ambapo watu wengi walipigia mstari baada ya mwanadada huyo kuposti picha ya Idris huku akiandika maneno ya kimahaba yalisomeka; “Babyboo baby boo bae.”

Baada ya Tetesi hizo kupamba moto Kwenye mitandao ya kijamii gazeti la Risasi Vibes, lilimsaka Lynn ambaye mara moja alikana kuwapo kwa Mahusiano hayo:

Unajua muda mwingine unaweza kuposti kitu halafu maneno yakajiandika yenyewe, sasa ndicho kilichonitokea na mimi sikutaka kufuta kwa sababu watu wangesema ni kiki.

Lakini Idris ni mshikaji wangu wa karibu sana na ninampenda anavyochekesha, watu wasinitengenezee mambo ambayo hayapo jamani“.

 

Steve Nyerere Amfananisha Idris na Fransis Cheka.

Mchekeshaji maarufu nchini  steve nyerere amefunguka na kusema kuwa watu wanakosea sana wanapotaka kumfananisha yeye na idrisa sultan kwa sababu hawawezi kulingana hata siku moja.

Wawili hao ambao wote ni wa tasnia ya uchekeshaji wamekuwa wakifanya vizuri comedy na kila mtu kwa style yake na huku kila mmoja akiwa na mashabiki wake.

Hata hivyo kutokana na jinsi idris amekuwa akitania sana wasanii wenzie katika mitandao ya kijamii na hata kutoa kituko cha skendo zinazondelea kumkabili steve nyerere, steve nasema kuwa haweiz kujibishana na idris kwa sababu wao ni watu wawili tofauti ni sawa na van dame na fransis cheka.

siwezi kushindana na idrisa maana kushindana na idrisa ni sawa na teke la van dame na fransis cheka, hivyo ni vitu viwili tofauti.

Idris Sultan Atangaza Ujio Wa Kipindi Chake Azam TV

Mchekeshaji na Muigizaji wa Bongo movie Idris Sultan ametoa habari njema kwa mashabiki zake baada ya kutangaza ujio wa kipindi chake kwenye Tv yako.

Idris alitangaza Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kipindi chake kilichokuwa kinaruka Kwenye ukurasa wake wa YouTube Kitaanza kuonekana rasmi ndani ya Wasafi Tv.

Nakumbuka wakati SIO HABARI ni show ndogo tu. Nilipoanza lengo kuu ilikuwa kujaribu kusema mambo makubwa na mazito ambayo wengi wanayajua, wanayasikia na labda hawataki kuyaongelea au wanaogopa. Haya mazito tuliyadadavua katika lugha nyepesi na ya kufurahisha na ujumbe ulifika. 

Show ilikaa mwezi tu kwenye TV nikaikatisha kwasababu niligundua ni kubwa kuliko nilivyoichora na ilibidi nifanye hivyo ili isianguke. Ilikua ni show nimelenga vijana tu ila kila jumatatu zilikaa familia kuangalia SIO HABARI. Wakubwa kwa wadogo. Haya niliyajua kwenye malalamiko baadhi ya watu wakisema samahani Idris punguza makali ya maneno tunaangalia na wazazi wetu “mnaogopa wazazi wataharibika au ?” Nilisema ila nikagundua nini kimesemwa bila wao kujua.This is not just a show anymore, hii ni sauti ya wengi wasioweza, ni kitu kimoja chenye ukweli mwingi kinachounganisha familia nzima na kumsikiliza mpuuzi mmoja anayetoa la moyoni. Wengi hamkushtukia show iliruka kwa mwezi mmoja tu.I’m proud to say SIO HABARI inarudi, wayyyyyy bigger than it ever was. Ilikuwa ndoto ikawa idea ikawa jaribio na sasa itakuwa a revolution kwenye ufunguaji wa fikra kwa kutumia lugha nyepesi tu “COMEDY”.. Vicheko itakuwa ni “Hahaha ila ni kweli”.. Soon on AZAM“