Mbosso Afungukia Bifu Lake na Aslay

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema chini ya Label ya WCB amefunguka na kuweka wazi kuwa hali sio shwari kati yake na msanii mwenzake Aslay.

Mbosso ameweka wazi kwamba kwa sasa hayupo sawa na muimbaji mwenzake, Aslay ambaye awali alikuwa anafanya naye kazi katika bendi ya Yamoto Band.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Azam, alisema kuwa awali alikuwa anamsupport Aslay katika kazi zake ambazo amekuwa akizitoa lakini yeye amedai alikuwa hasapotiwi na muimbaji huyo.

Baada ya kumsupport Aslay kwa muda mrefu watu wakawa wananimbia mbona wewe unam-support halafu yeye haku-support? umem-follow mwenzako ameku-unfollow. Jifunze kubalance shobo, nikasema kumbe na mimi naonekana namshobokea ngoja na mimi nim-unfollow. Kwa hiyo sasa hivi kila mtu hana urafiki na mwenzake”.

Aslay na Mbosso walikuwa katika Kundi moja la Yamoto Band kwa miaka mingi Lakini walikuja kutengana  kutokana na sababu za kimaslahi ambapo Mbosso alijiunga na Label ya WCB.

Mbosso Aanika Siri Yake Kubwa Ya Udogoni

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB ambaye pia anayefanya vyema na wimbo wake wa ‘Hodari’  Mbosso ameanika siri yake kwamba alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kula ubwabwa na maharage kiasi kwamba kuna siku moja ulitaka kumtoa roho kwani alijikuta akivimbiwa kupitiliza.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mbosso alisema kuwa alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana ubwabwa na maharage kupita maelezo, ukipikwa nyumbani kwao alikuwa hachezi mbali na jikoni, mapema anakuwa amesharudi kwenye michezo yake tayari kusubiria mnuso.

Sijui ilikuwa ni uroho au nini, yaani nilikuwa napenda ubwabwa na maharage kiasi kwamba kuna siku nilivimbiwa sana, ilikuwa kila nikila sishibi, mwisho wa siku ikawa balaa, ikabidi mama achukue mwiko, akanipigapiga nao tumboni, hiyo ndiyo ikawa nafuu yangu, yaani ilikuwa balaa kwani watu walianza kwa kunipepea ikashindikana lakini nili­pata ahueni baada ya mama kunipa tiba hiyo”.

 

Diamond, Rayvanny na Mbosso Wapata Ajali Stejini Sumbawanga (+Video)

Msanii wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Diamond Platnumz na wasanii wenzake Rayvanny na Harmonize walipata ajali katika Steji ya Wasafi Festival iliyokuwa inafanyika mkoani Sumbawanga.

Shoo hiyo ilifanyika siku ya jana 9 Desemba katika uwanja wa Nelson Mandela ambapo wasanii hao walikuwa wanaperfom wimbo wao pendwa kabisa wa ‘Zilipendwa’ lakini ndipo balaa lilipotokea Baada ya wasanii hao kula mieleka.

Lakini baada ya kudondoka kwa Diamond akifuatiwa na Mbosso wasanii hao waliinuka na kuendelea na shoo na iliripotiwa kuwa hakuna Msanii aliyepata majeraha makubwa zaidi ya michubuko ya hapa na pale.

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale alitoa taarifa kuwa wasanii hao wanaendelea vizuri na hakuna aliyeumia.

Baada ya sakata hilo Kupitia ukurasa Wake wa Instagram, Diamond Platnumz aliposti video hiyo na kuandika:

https://www.instagram.com/p/BrK67ZVlDFX/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=d9geezbdwlgj

Mrembo Adaiwa Kunywa Sumu Kisa Mbosso.

Mrembo mmoja aliejulikana kwa jina ,la Sherry anadaiwa kunywa sumu kwa kulikosa penzi la msanii Mbosso ambae kwa sasa anafanya vizuri katika wimbo wa Hodari.

watu kutoka mtaani kwa mwanadada huyo anasema kuwa mwanadada huyo amekuwa akichanganyikiwa na msanii huyo kiasi kwamba  hata katika maa anaokaa watu wamekuwa wakimwita mrs mbosso na kama ukitokea ukamwita jina hilo anakuwa mwenye furaha ya kupitiliza.

Watoa ubuyu hao wanasema kuwa mwanadada huyo amekuwa akimsumbua sana msanii mbosso kwa kumtumia sms kila siku na hata alimuomba kuwa katika wimbo wake wa hoadri aweze kumtaka jina lake tu ili aweze kulizika.

Hata hivyo baada ya siku kadhaa wimbo huo kutoka, baadhi ya marafki zake walianza kumtani kwanini hakutajwa katika wimbo huo kama yeye ndio mrs mbosso, kwa hasira mwanadada huyo alikimbia na kwenda kununua sumu ya oanya na kuinywa lakini aliona hali inaanza kuwa mbaya alianza kulia na kusema kuwa alikunywa sumu.

Waliokuwepo karibu  pamoja na dada yake walimkimbiza katika hospitali moja hapo buguruni na kupumzishwa kwa masaa kadhaa.

Baada ya kutafutwa kwa mrembo huyo alikiri kuwa ni kweli lakini aliema kilichomuumiza zaidi ni vile marafiki zake walivyokuwa wakimsema na kumtania kuhusu swala hilo.

Hata hivyo mbossoa anasema kuwa hakuwahi kujua kuwa kuna watu wamekuwa na mapenzi ya dhati na yeye kiasi hicho.

 

Mbosso Alinisaidia Nilipotaka Kubakwa-Amber Lulu

Video queen na Msanii wa Bongo fleva Lulu Eugene maarufu kama Amber Lulu amefunguka na kudai Msanii mwenzake Mbosso kutoka WCB alimsaidia alipotana kubakwa miaka ya nyuma.

Leo ni siku ya kuzaliwa kwa Mbosso, Amber Lulu ni mmoja kati ya wasanii ambaye amemposti Kwenye mitandao ya kijamii na kumtakia heri lakini Kwenye posti yake Amber Lulu amemshukuru Mbosso na kutoa siri nzito.

Amber ameweka  wazi kuwa miaka ya nyuma Mbosso alishawahi kumsaidia alipokuwa anataka kubakwa Lakini pia hajawahi kumwambia mtu yoyote.

Kupitia ukurasa  wake wa Instagram, Amber Lulu ameandika:

Mbosso Afungukia Ukaribu Wake na Esma Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika Label ya WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Hodari’ Mbosso amefunguka na kuelezea uhusiano wake na Dada wa CEO wa WCB Diamond Platnumz, Esma Platnumz.

Mbosso na Esma wameonekana kuwa na ukaribu sana hasa Kwenye mitandao ya Jamii ambapo wamekuwa waki piga picha mara kwa mara na kuzirusha mtandaoni.

Kwenye mahojiano na waandishi wa Habari, Mbosso amesema Esma ni mshikaji wake sana na huwa wanaimba wote baadhi nyimbo na mara nyingi humfundisha kuimba pia hufikia kipindi hadi anamshawishi na yeye aweze kuimba yaani ajiingize kwenye mambo ya muziki.

Lakini pia mbali na kuongelea ukaribu wake na Esma lakini pia amekanusha vikali taarifa zilizokuwa zinasema kuwa yeye ana mahusiano na dada mwingine wa Diamond ambaye pia ni msanii Queen darlin,na kusema hama mahusiano nae kabisa.

 

“Najisikia Vibaya Kushindanishwa na Aslay”- Mbosso

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Hodari’ Mbosso amefunguka na kuweka wazi kuwa anachukia sana kupambanishwa na Aslay.

Mbosso na Aslay walikuwa pamoja katika kundi la Yamoto Band lakini baada ya kundi kuvunjika kila mmoja alienda njia yake lakini mashabiki wamekuwa wakiwapambanisha sana.

Mbosso amefunguka na kusema hakuna kitu kinachomsumbua na kumfanya ajisikie vibaya kama kuona anapambanishwa na Aslay kwa sababu anaona kabisa hawawezi kulingana kwa sababu Aslay ni kaka yake.

Hakuna kitu kinanifanya najisikia vibaya mara kwa mara kama nikaona nashindanishwa na Aslay, Mimi Aslay ni Braza angu, alafu isitoshe mimi nimeanza mziki kama Solo artist nina Miezi Tisa sasa lakini Aslay alianza muziki kama Solo artist tangu mwaka 2011 kwaiyo ni mkubwa sana kwangu mimi bado mchanga mno kwaiyo ukinifanisha naye unakuwa unamvunjia heshima yake na mimi sitaki iwe huvyo”.

 

Mbosso-Kuna Media Zilitaka Kunizika Nikiwa Hai

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka WCB anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Nadekezwa’ Mbwana Yusuf maarufu kama Mbosso amefunguka na kudai kuna kipindi baadhi ya media zilikataa kucheza kabisa nyimbo zake.

Mbosso amedai jambo hilo lilimkuta alipotoka katika kundi la Yamoto na kuwa Msanii wa kujitegemea ndipo alipokutana na vikwazi vya baadhi ya media kugoma kabisa kucheza nyimbo zake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mbosso alisema kwamba kipindi hicho kilikuwa ni kigumu kwenye maisha yake, kuna muda alikuwa hadi analia, lakini baada ya kuingia WCB, mambo yamebadilika kabisa na kila siku anaona muujiza mpya kwenye kazi yake ya muziki.

Kiukweli ninamshukuru Mungu anayetoa riziki. Ingekuwa inatolewa na binadamu pengine mimi nisingepata chochote kwa sababu kuna baadhi ya media zilikuwa hazichezi ngoma zangu, zilitaka kunizika nikiwa hai zikiamini kwamba siwezi na sitafika popote pale.

Lakini Mungu mkubwa, mambo yamebadilika na kwa sasa nipo kazini ninafanya kazi na wanamuziki watano wakubwa Afrika, na kila kitu kikikaa sawa nitaweka wazi”.

 

MbosoAfunguka Kuhusu Wimbo Wake na Kisanga cha Zari na Diamond.

Msanii Mboso amefunguka na kusema kuwa moja ya nyimbo zake ambazo aliwahi kuimba zamani na baadae kuurudia aliingia WCB ulipendwa sana na Diamond  kumbe ulikuwa unafanana na kisanga kikubwa kilichompta Diamond cha kutumiwa ua juesi na Zari the Bossy.

,boso anasema kuwa baada ya kuutoa wimbo huo February 9  ndipo Febraury 14 yalipotokea mambo ya ua jesi lakini wakati huo diamond alikuwa tayari anaupenda sana huo wimbo na ndie aliemuomba aurudie kuimba kwa sababu tayaria liashawahi kuimba akiwa Ya moto.

Hapana ni wimbo tu ambao umekutana na matukio, ni wimbo ambao nilishawahi kuimba hapo awali nilipokuwa ya moto , sasa nilipokuja kuingia WCB ni moja ya nyimbo ambazo bosi wangu alikuwa aizipenda sana na akaomba niurudie.sasa kipindi ninatoa wimbo huo ndio kisanga cha ua mwana mwekundu.

Mbosso Awakingia Kifua WCB Adai Sio Wanyonyaji Kama Madai Ya Mavoko

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Maromboso amefunguka na kuwakingia kifua WCB dhidi ya tuhuma za unyonyaji walizotupiwa na msanii Rich Mavoko.

Wiki iliyopita RIch Mavoko aliwaburuza WCB katika Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) na kuwatuhumu kwa unyonyaji kutoka na mkataba waliompa.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari Mbosso amefunguka na kudai yeye binafsi hajaona unyonyaji wowote WCB  hasa kwa upande wa mkataba wake Tena anaamini wamempa zaidi anachostahili.

Kiukweli kwa upande wangu tangu naingia WCB mpaka leo sijafikisha pesa ambayo wao wali invest kwangu kwaiyo nikiambiwa nanyonywa binafsi nitapinga kwa sababu mimi ndio naona nawanyonya kwa sababu mpaka leo hela waliyowekeza kwangu haijarusi na kuna wasanii wapo WCB mpaka leo pia hawajarudiasha hata nusu ya pesa kwaiyo ukiniambia WCB wananyonya wasanii nakuwa sikuamini labda uje na vigezo”.

 

Mboso Amtaka Rich Mavoko Aje na Ushaidi wa Unyonyaji wa Wasafi

Msanii kutoka WCB mbosso amefunguka kwa waandishiwa habari na kusema kuwa msanii rich  mavoko ambae amekuwa akitangaza kuwa WCB wanafanya kazi ya unyonyaji kwa wasanii wao ni uongo na kama kweli basi aje na kitu cha kuthibitisha maneno yake kama ni kweli.

Mbosso anasema kuwa kwa muda wote aliokuwa akifanya kazi wasafi mpaka sasa anaona kabisa kuwa hajarudisha hata robo ya kile alitakiwa kukirudisha kwa mambo ambayo amefanyiwa na WCB kwa muda wote.

mimi tangu nianze kuingiza kaz wasafi, sinaona kama nimerudisha mema niliyofanyiwa na WCB,  ile ela waliyowekeza kwangu bado sijarudisha hivyo nikiambiwa kuwa nina nyinya kwakweli binafsi nitakata kwa sababu naona mimi ndio ninawanyinya wao.

kwaio unaponiambia kuwa Mboso unanyinywa WCB basi uje na ushaidi kuwa nina nyonywaje.

Wasafi ina wasanii wengi sana ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya lebo hiyo lakini, Rich ni msanii wa kwanza kutoka WCB huku akisema kuwa sababu kubwa ni unyonyaji unaofanya na wasafi katika kufanya kazi na malipo lwa wasanii wao.

Mbosso- Ujana Ulinipelekea Kupata Watoto Katika Umri Mdogo

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Maromboso au maarufu kama Mbosso amekiri kuwa na watoto wawili katika umri mdogo ni matokeo ya balehe.

Mbosso ambaye kwa hivi sasa anaendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya “Nadekezwa” ni Baba wa watoto wawili ambao watoto wote wana umri sawa lakini ni mama tofauti.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mbosso amekiri kuwa pamoja na kila mmoja kuwa na mama yake lakini hana uhusiano na kama zao kwa sasa kila mmoja ameshaolewa.

Sipendi kuwa muongo na sitakuwa na dhambi ya uongo, huwa inatokea katika ukuaji (balehe) hususani sisi watoto wa kiume, kuna vitu utajizuia navyo lakini hutashindwa tu.

Kwa hiyo sitaki kuwa muongo, ilitokea ikawa hivyo nimekuwa baba nina watoto wangu wawili, tunaishi vizuri“.

Mbosso alianza muziki katika umri mdogo baada ya kujiunga Kwenye kundi la muziki la Yamoto Band miaka kadhaa iliyopita.

“Siwezi Kuingilia Mahusiano Ya Diamond”-Mbosso

Msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Maromboso almaarufu kama Mbosso ameweka wazi kuwa hawezi kuingilia Mahusiano ya Bosi wake Diamond Platnumz.

Diamond ambaye ni Mkurugenzi wa label ya WCB amekuwa kivutio sana Kwenye mitandao ya kijamii hasa linapokuja suala la Mahusiano Yake binafsi na Familia yake.

Mbosso ambaye alijiunga Rasmi WCB Miezi michache iliyopita amefunguka na kusema hawezi hata siku moja kuingilia Mahusiano binafsi ya Diamond.

Suala hilo liliibuka Kwenye mahojiano aliyokuwa anafanya na Sam Misago Tv, ambapo aliulizwa kama anaweza kumpa ushauri gani Diamond hasa linapokuja suala lake la Mahusiano.

Mahusiano Yake bwana Chibu daaah siwezi kumuingilia huko! Naomba niishie hapa siwezi kuingilia mahusiano yake, Unajua ndio displini niliyojiwekea kuna vitu naweza kuviingilia na kuna vitu siwezi kabisaa”.

Mapema mwaka huu mpiga picha maarufu wa Diamond anayejulikana kama Kifesi alifukuzwa kazi baada ya kuingilia Mahusiano ya Diamond baada ya kumshauri arudiane na Zari badala ya Hamisa.

Mbosso- Nyimbo Zangu Hazipigwi Redioni

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Maromboso au maarufu kama Mbosso ameongelea Kitendo Cha nyimbo zake kutopigwa na baadhi ya media.

Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz amekuwa kwenye mgogoro na baadhi ya vyombo vya habari hadi kupelekea nyimbo zake kufungiwa na vituo hivyo.

Wasanii wote ambao wako chini ya WCB wamekuwa wakibaniwa nyimbo zao kupigwa Kwenye Media hizo na Mbosso akiwa mmoja kati ya wasanii hao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Mbosso ameweka wazi kuwa ingawa  nyimbo zake hazipigwi na baadhi ya media lakini anashukuru zinadai kila vyema kwa mashabiki zake.

Ukizungumzia moja ya wasanii ambao hawakupata bahati ya kupata nafasi kubwa kwenye radio station, mimi pia naweza kusema nipo.

Sikupata bahati kabisa nyimbo kupigwa kwenye radio station lakini wananchi wamenipokea, wamesema Mbosso tunakusapoti, wamenisapoti nashuru leo nimefika nilipofika”.

Baada ya media zaidi ya nne kugoma kupiga nyimbo za Diamond na wasanii wote wa WCB, Diamond alifikia uwaumuzi wa kufungua Stesheni yao ya Wasafi Tv.

Mbosso Awalaumu Mashabiki Kwa Video Yake Chafu

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Maromboso au maarufu kama Mbosso ameelekeza lawama kwa mashabiki baada ya video yake kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Siku chache zilizopita video ilisambaa mtandaoni iliyomuonyesha Mbosso akiiwa stejini akitumbuiza kwenye shoo ya Kusi night huku akimbambia msichana mmoja katika staili za kimahaba.

Video hiyo ilisababisha mashabiki kumjia juu Mbosso huku wakiwarushia lawama WCB na kudai wamembadilisha Msanii huyo na kumfundisha tabia mbaya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Mbosso amefunguka hay kuhusu video ile:

Unajua watu wengi wanaamini mimi nimebadilika lakini hakuna kuna baadhi ya vitu vinachangia hasa kwenye shoo inakulazimu ufanye vitu fulani ili watu wafurahi kwaiyo unajikuta unafanya vitu fulani ili shoo ipendeze na watu wafurahi na mashabiki wawe na shangwe na wewe ndio inabidi uwape burudani mashabiki  zako”.

Lakini pia Mbosso amesisitiza kuwa yeye binafsi hakupenda kufanya vile ila kutokana na msukumo wa mashabiki waliokuwa wanampa ukumbini pale akajikuta akifanya vile.

NInastahili Kuwa Msanii Wa WCB- Mbosso

Mwanamuziki wa Bongo fleva Marombosso maarufu kama Mbosso ambaye amesainiwa chini ya label ya WCB amefunguka na kusema kuna muda utafika watu wote watajua kuwa anastahili kuwa msanii wa WCB.

Mbosso amefunguka hayo baada ya kuona kuwa anakosolewa sana na baadhi ya watu ambao wanaona kama hana kipaji kikubwa cha kuweza kuwa msanii wa label hiyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na TBC Fm, Mbosso amefunguka na kuongea mengi kuhusiana na uwezo wake katika label hiyo:

Kuna muda unaweza ukafanya kitu kwako wewe kipo sawa na unajaribu kukiwakilisha kwa njia iliyo sawa lakini inafikia hatua anaona hakiko sawa anafikia hatua hata ya kukutukana matusi, inafikia hatua mtu anakutukana mpaka matusi ya mama yako.

Lakini huwezi kumzuia mtu kufanya hivyo vitu ila kuna muda utafiki kila mtu atajua Mbosso kumbe anastahili kuwa WCB au anastahili kupewa hiki ambacho anapewa sasa hivi“.

Mbosso alijipatia umaarufu wakati alipokuwa katika kundi la Yamoto Band, Baada ya kundi hilo kuvunjika Mbosso alijiunga na timu nzima ya WCB rasmi mwaka huu tarehe 28 januari.