Muna Love Arudi Tena Vitani Na Baba Patrick

Rose Alphonce maarufu kama ‘Muna Love’ amerudi tena kwenye headlines ikiwa ameingia tena kwenye mvutano na aliyekuwa mume Wake Peter Komu ‘Baba Patrick’ huku Safari hii wakipelekana

Gazeti la Ijumaa linaripoti kuwa Muna Love alikwenda mahakamani ili kudai talaka yake na kugawana vitu ambavyo walichuma pamoja walipokuwa wote.

Unajua ninamshangaa sana Muna, amekwenda mahakamani, anasema ile nyumba ni ya kwake, lakini wauzaji wa kile kiwanja wapo na kama haitoshi hadi mafundi waliojenga wapo kwa hiyo tuiachie mahakama ifanye kazi yake. Talaka sawa, kama yeye ameamua, siyo mbaya kwa kuwa hawapo pamoja kwa kipindi kirefu. Kwa hiyo kama anadai talaka ni sawa tu, kwa kuwa tunasikia anahitaji kuwa huru na pengine anataka kuolewa na mwanaume mwingine”.

Baada ya tetesi hizo Gazeti la Ijumaa Lilimsaka Peter ambaye alifunguka haya kuhusu tetesi hizo:

Ni kweli nilikwenda mahakamani Magomeni (Dar) na Muna. Anataka mgawano wa mali na talaka. Ninachojua talaka zina process (taratibu) zake, lakini kesi ni tarehe 20 ya mwezi ujao (Februari) hivyo Muna anatakiwa afike na mashahidi“.

Muna na Peter waliingia kwenye mgogoro tangu walipofiwa na mtoto wao, Patrick ambapo kuliibuka mkanganyiko na sintofahamu ya kujua baba halisi wa mtoto kufuatia uwepo wa baba mwingine, Casto Dickson.

Muna Afungua Patrick Foundation ya Mwanae.

Mwanadada Muna love amefanikiwa kufungua Foundation yake itakayo itwa Patrick Foundation ambayo itakuwa na kazi ya kusaidia watoto wenye matatizo mbalimbali katika jamii huku lengo kubwa ikiwa ni kwa ajili ya kuwasaidia  na pia kumkumbuka mtoto wake.

Muna amekuwa akiguswa sana na kutokuwepo kwa mtoto wake huyo ambae  alifariki mwaka huu, hivyo Muna aliamua kufanya hivyo kama kuguswa na watoto wanaoteseka mitaani .

Dhumuni la muna inadhihirika sana pale aliapoanza kutembea mikoa mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto hao  waliopo mitaani na wale walio wagonjwa ambao wamekuwa wakikosa misaada ya kiafya na pia kielimu.

 

 

 

Muna Awachana Wanaotaka Kujua Undani wa Maisha Yake.

Msanii wa Filamu chini, amefunguka juu ya watu wanaotaka kujua kila kitu katika maisha yake moja ya maswali hayo ni kuwa anafanya kazi gani na hela anatoa wapi? Muna kupitia ukurasa wake wa Instagram, amechapisha kuwa inatakiwa wajiulize amewezaje kupita katika moto mkali wa maumivu na kwa muda mchache yuko imara.

“Kama mwanamke unaejiamini lazima ujitambue wewe ni nani?Na unataka nini?Haijalishi umeumizwa kiasi gani na umekosa tumaini kwa ukubwa gani. Kuwa na furaha ni jukumu lako wewe mwenyewe,” amesema Muna.

“Hili swali kila siku mnaniuliza sijui hufanyi kazi ila unaela ?sijui mliziona wapi? unafanya biashara gani? , kila kitu mnataka kujua naomba Jambo moja ambalo mnatakiwa hasa kujua ,mjiulize nimewezaje kupita kwenye moto mkali na wamaumivu kwa Muda mchache na niko imara ?, mnazani ni mimi peke yangu ningeweza au nigejikwamua hapana , kuna mkuu kuliko wanadamu ndiyo anaenipa Jeuri na kufanya vile nyinyi mnavyoniona mpaka kuna wakati na mwambia Baba mi nakosa cha kuwajibu hawa zaidi ya kuwambia kwa Yesu kutamu.na apo Baba Ameni busti tu bado ajaachilia vya kuwashangaza ndo mtaelewa…. Njooni kwa Yesu mfurahi milele.”

Wolper Amwaga Povu Zito Kisa Muna

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamitindo maarufu Jacqueline Wolper amejikuta akiporomosha mvua ya matusi pale alipoulizwa kuhusu sakata la Muna.

Muna ametawala vichwa vya habari kwa wiki kadhaa kufuatia skendo yake ya kumtelekeza mtoto wake wa kwanza anayeitwa Brian na majibizano a familia yake Kwenye vyombo vya habari.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Jacqueline Wolper amewajia juu watu wanaoingilia ugomvi wa familia za watu wanaowaona Kwenye mitandao ya kijamii.

Watu wa Instagram ni washenzi na hawajielewi, tena ni wapuuzi na wapumbavu. Kazi kufuatilia maisha ya watu tu, kwa nini wasimuache Muna mambo yake na familia yake, kila mtu abebe msalaba wake”.

 

Sakata La Muna Kutelekeza Mtoto Lachukua Sura Mpya

Siku mbili zilizopita stori iliyotawala Kwenye mitandao ya kijamii ni Tetesi za Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Rose Alphonce maarufu kama Muna Love.

Global Publishers waliripoti kuwa ndugu wa karibu wa Muna ndio wamemnyooshea kidole kwa kitendo chake cha kumtelekeza mtoto wake Nyumbani kwao Moshi.

Baada ya taarifa hizo kuzagaa Mtandaoni Muna alikana kabisa na kusisitiza wanaosambaza taarifa hizo wana nia moja tu ya kumchafua ili aonekane mbaya.

Siku ya leo Muna Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kuwa Mtu ambaye amesambaza taarifa hizo yuko mikononi mwa polisi na ambaye amemtuma ni mama yake mzazi na dada yake:

 

Muna Akumbwa na Skendo Ya Kutelekeza Mtoto

Msanii wa nyimbo za Injili Rose Alphonce Nungu maarufu kama Muna Love amejikuta katika skendo nzito ya kutelekeza mtoto wake wa kumzaa.

Global Publishers wanaripoti kuwa pamoja na Muna kunukuliwa akisema kwamba Patrick alikuwa mwanaye pekee, lakini nyuma yake kuna madai kuwa alizaa mtoto mmoja wa kiume (jina linahifadhiwa kimaadili) mwenye umri wa miaka 13.

Katika mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Ndugu yaka na Muna alimwaga ubuyu kuwa, kitendo cha Muna kutangaza kuhudumia watoto wa watu wengine huku akimuacha mtoto wa kumzaa akiwa analelewa na watu wengine, kinawakwaza ndugu walio wengi.

Tunashangaa sana Muna huwa hamtambulishi kabisa mtoto wake mkubwa na nasikia alisema aliwahi kuzaa mtoto akafa wakati mtoto yupo hai na anatakiwa apate upendo kutoka kwa mama yake.

Kinachouma ni kwamba Muna sijui ataishi maisha ya kuigiza mpaka lini ilihali anawasaidia watoto wenye matatizo, hatukatai ni wajibu yeye kusaidia, lakini amwangalie na mtoto wake ambaye alimtoa katika tumbo lake. “Mtoto huwa anawaambia wenzake shuleni kuwa mama yake mzazi ni Muna na wenzake wanamwambia mbona hawajawahi kumuona akija kumwangalia? Mtoto anaishia kulia tu.

Baada ya Tuhuma hizo gazeti hilo lilimsaka Muna ili kupata ukweli wa mambo ambapo amekana kabisa taarifa hizo:

Hakuna Mtu Aliyeumizwa na Msiba Wa Patrick Zaidi Yangu-Muna

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili na mdau mkubwa wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amefunguka na kusema hakuna mtu aliyeumizwa na msiba wa mtoto Patrick Zaidi yake kama mama.

Muna amefunguka kutokana na maneno ambayo amekuwa akikumbana nayo Kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wamekuwa wakimponda kutokana na maamuzi yake ya kutumia Kifo Cha mwanaye kama ushuda kanisani.

Siku ya leo Muna alifanya mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza Tamasha lake la Kidini litakalofanyika siku ya Jumamosi na aliweka wazi kuwa atatoa ushuhuda wake kuhusu Kifo Cha mtoto wake Patrick.

Kwenye mahojiano na vyombo vya habari, Muna alijibu tuhuma za kumtumia mtoto wake ambapo alifunguka:

Kwanza hakuna mtu anayeweza kusema ameumizwa na Kifo Cha Patrick zaidi ya mama mzazi na mimi tangu niingie Kwenye wokovu naamini hakuna mtu atakayeweza kuishi milele kila nafasi itaonja mauti lakini mimi natumia mwanangu ili kubasdilisha watu Ikiwa mimi mwanangu amenibadilisha nilikuwa mtu wa ajabu nilikuwa natukana na kufanya mambo mengi ya ajabu lakini niangalie leo hii nilivyobadilika”.

Mtoto wa Muna, Patrick alifariki dunia miezi michache iliyopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

 

Muna Apewa Maono Ya Kusaidia Jamii na Marehemu Patrick

Msanii wa Bongo movie na mdau mkubwa muziki wa Bongo fleva Rose Alphonce maarufu kama Muna Love amefunguka na kutaja sababu ya yeye kujikita katika kusaidia jamii kwa sasa.

Muna amefunguka baada ya kuonekana akijikita sana katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na magonjwa ni katika kumuenzi mtoto wake aliyeaga dunia mwezi uliopita.

Kwenye mahojiano na gazeti la Amani, Muna alisema kwa sasa watu wengi wamekuwa wakimuona akifanya shughuli mbalimbali za kusaidia wenye uhitaji, kazi ambayo ataifanya kwa kadiri ya uwezo wake wote kumuenzi marehemu mwanaye.

Nafanya hivi kwa sababu ni maono toka kwa Mungu, pia naona ndio njia pekee ya kumuenzi mtoto wangu kwa sababu yeye alikuwa na upendo na watoto wenziye, ilikuwa ukimpa kitu ale, hawezi kula lazima ampe na mwenziye na hata kama kipo kimoja basi yeye hatakula atampa mwenziye“.

Patrick mtoto wa Muna aliugua mwezi uliopita nchini Kenya alipoenda Kwenye matibabu baada ya kuugua kwa kipindi kirefu.

Sina Mpango wa Kuzaa Baada Ya Patrick Kufariki- Muna

Msanii na mdau mkubwa wa Bongo fleva Muna Love amefunguka na kuongelea maisha baada ya Kifo Cha mwanaye Patrick aliyefariki mwezi uliopita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Zikiwa zimepita siku 40 tangu Mtoto wa Muna Patrick afariki Dunia, Muna anafunguka

Kwenye mahojiano na Global Publishers Muna amefunguka kuwa pamoja na kuwa 40 ya Patrick ilikuwa jana lakini yeye sio mtu wa kuweka 40 kwa sababu ni Mlokole:

Kwanza watu wafahamu mimi sina 40, nimeokoka na mwanangu kashaenda kwa baba yake nimemaliza, ila kwa sasa mimi bado nafunga tu mpaka nielekezwe nini cha kufanya lakini nashukuru nimeshaanza kuhudumia watoto wenzake ambao tayari wameanza kupata matibabu, nashukuru sana Mungu kwa hilo“.

Lakini pia Muna alifunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuzaa mtoto mwingine:

Pengo kwangu hakuna nimeshasema Patrick, kamaliza kazi yake aliyotumwa na baba na mimi sasa hivi sina mpango wa kuzaa mtoto mwingine kabisa, nafanya kazi ya baba kwanza, ninachofanya sasa hivi ni kuwasaidia watoto wenzie matibabu basi”.

Muna amekana vikali Tetesi za kutaka Kuolewa na Joel Lwaga na kudai ni maneno maneno ya watu yeye hana mpango wa Kuolewa kwa sasa.

Muna Afunguka Kuhusu Ugawaji wa Nguo za Marehemu Patrick.

mwanadada muna love amefunguka na kuongelea swala linalosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu ugawajiwa nguo za mtoto wake aliyeafriki wiki chache zilizopita huku watu wakisema kuwa marehemu ameacha nguo nyingi sana kiasi kwamba wanashangaa muna atazipeleka wapi nguo hizo.

Huku watu wakijaribu kuraka kufuata mila na desturi za kawaida za kifamilia za kitanzania kuwamba kila baada ya 40 ya marehemu basi mali na kila alichoacha marehemu kinaweza kugawiwa kwa watu au kukabidhiwa mtu kwa ajili ya kukitunza , kukiendesha au kukimiliki basi hii ni tofaiuti kna kile anachokiamini muna kuhusu kila alichokiacha mtoto wake.

Muna ansema kuwa ajui chochote kuhusu 40 katika msiba kwa sababu ameshazika na amemaliza , anackofanya sasa ni kueneza neno la mung na kutoa ushuhuda, lakini pia hawezi kugawa nguo za mtoto wake hata kama zipo nying kwa sababu mtoto wake aliacha maona na inabidi yafuatwe hivyo haweiz kugawa nguo.

mimi ni mkristo , na mambo ya 40 siyajui, ninachojua mimi ukimaliza msiba tu unaendelea na mambo yako na kuhusu mavazi ya mwanangu sitayagawanya kwa sababu mwanangu aliacha maono na maono yake lazima yafuatwe.-Aliongea Muna akiwa nchini Kenya aliposema kuwa yupo katika kazi ya kulitukuza neno la Mungu.

“Muna ni Mwanamke Shupavu Sana”- Joyce Kiria

Mtangazaji wa kipindi cha ‘Wanawake Live’ na mpiganaji wa haki za wanawake Joyce Kiria amemkingia kifua Muna Love na kumtaja kama mwanamke shupavu.

Siku chache zilizopita Muna amekuwa akikosolewa sana baada ya kuonekana amerudi Kwenye maisha yake kama kawaida baada ya Kifo Cha mwanaye Ikiwa zimepita wiki chache tu.

Mashabiki wamemjia juu Muna kutokana na mavazi yake ambayo amekuwa akivaa na hata kuposti picha Kwenye mitandao ya kijamii na kuendelea na maisha yake kama kawaida.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Joyce Kiria amedai Muna yuko sahihi kwa hivi sasa anavyotoka na kuonekana kwenye mitandao kabla ya kumaliza 40 ya mtoto wake aliyefariki kwa sababu hana sababu ya kuendelea kulia na kujifungia ndani kama watu wanavyomtaka.

Mimi binafsi nampongeza sana kwa kile anachokifanya sasa hivi, inaonekana jinsi gani alivyo shupavu maana bila hivyo basi angekuwa anaishi kwa maumivu makali tena ya kumsababishia athari ndani ya moyo”.

Mashabiki walimjia juu Muna baada ya kuamua kuongea na waandishi wa habari siku chache baada ya Kifo Cha mwanaye na sasa ameonekana nchini Kenya na kuendelea na maisha yake kama kawaida wakati mtoto wake hjafikisha siku 40 tangu afariki.

 

Baada ya Msiba Mzito, Muna Aanza Kujirudisha Mitandaoni,

MUIGIZAJI Muna Love ambaye hivi karibuni alipata msiba kwa kuondokewa na mtoto wake, Patrick, amefunguka na kusema kila binadamu hupitia magumu lakini haimanishi kwamba Mungu anakuwa amekuacha badala yake anakufanya uwe imara na kumwonyesha shetani kwamba ‘wewe ni mtoto wake’.

Muna ametoa kauli hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram na kumshukuru Mungu kwa yote aliyomtendea huku akisisitiza kwamba ataendelea kumtumikia muumba wake milele.

“Mungu anawapenda watu wote bila kujali wewe ni nani na unatabia gani mbele zake …na atatumia njia anazojua ili zikufikie na umtambue urudi kwake ukazaliwe upya… na hata pale anakupa jaribu sio kama hakupendi au anataka akuumize hapana, anakupa jaribu na pia anajua utaliweza na hatoweza kukuacha kamwe atakupa na njia za kupita.

“Mungu kwenye kila jaribu lile la aina yoyote jua yupo nyuma yako na anakukomaza ili kumuonyesha shetani kua wewe ni mtoto wake na anajivunia wewe sasa ,usiwaze kumuhukumu Mungu au kuumia kwanini umepitia hilo bali mshangilie na kumtukuza uone matunda atakayokupa ????????

“Asikudanganye mtu Mungu awezi kukuacha upitie gumu bila kukupa njia na roho mtakatifu akakuongoza asante Mungu wangu nitakutumikia milele,” amesema Muna.

 

Ray c Ampongeza Muna, Amwambia Ametua Mzigo.

Baada ya muna kuongea yaliyopo moyoni mwake kuhusu swala la marehemu mtoto wake Patrick   kusema wazi juu ya baba wa mtoto wake kuna watu waliongea mengi kila mtu akim-judge  Muna kwa lake huku wengine wakisema kuwa ameyafanya mapema sana mambo hayo alitakiwa kusubiri mpaka 40 ya mtoto huyo  ipite ndio aongee hayo.

Lakini wapo waliomtetea na kumuona kama alichokifanya labda kinaweza kumsaidia kukaa kwa amani lakini pia labda kingeweza kufunga midomo ya baadhi ya watu waliokuwa wakimhukumu bila kujua kwa nini yalitokea yaliyotokea.

Ray c ameguswa na maamuzi ya Muna na hivyo aliamua kuongea kuhusu swala hilo la kumpongeza kwa kumwambia kuwa aloichokifanya kimeweza kumuondolea mzigo wa maumivu yake aliyokuwa nayo kuhusu mtoto wake.

Una uhuru wa kuwa muwazi pale unapoona mambo fulani yamekuumiza au hayajakaa sawa,kuongea kuna kufanya nafsi yako inakaa sawa,safi muna ninaamini kuna kamzigi flani umekatua  kutoka kwenye moyo…good job.

“Mimi na Wema Tutaenda Kumtembelea Muna Labda Tufukuzwe”- Steve Nyerere

Muigizaji wa Bongo movie Steve Nyerere ameweka wazi kuwa hana kinyongo na Muna hata baada ya povu alilomtolea Povu Kwa waandishi wa habari Lakini ameshapanga kwenda kumtembelea.

Sakata hili lilianza wiki chache Kwenye msiba wa mtoto wa Muna ambapo Steve alionekana kuingilia mambo ya kifamilia ya Muna na kutangaza Kwenye mitandao ya kijamii taarifa ambayo Muna amedai haikua ya kweli.

Lakini siku ya jana Steve ametangaza kumsamehe Muna na kudai anajua hiki ni kipindi kigumu kwa Muna kwani bado anamuomboleza mtoto wake hivyo haoni sababu ya kuweka kinyongo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Steve  amedai kuwa yote ambayo ameongea Muna siku ya jana kuhusu yeye sio ya kweli na tayari ameshamsaheme ambapo amepanga safari ya kwenda kumtembelea akiwa na Wema Sepetu.

https://www.instagram.com/p/BlaXDuthZLR/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1lebqzhdtqbzi

Steve Nyerere Afungukia Sakata Lake na Muna Atangaza Kumsamehe

Muigizaji wa Filamu za kibongo na kiongozi wa Kamba hiyo Steve Nyerere ameibuka na kuongelea sakata lake yeye na Muna na kutangaza kuwa ameamua

Muna alipoongea na waandishi wa habari, alikanusha baadhi ya taarifa ambazo zilitolewa na Steve Nyerere zikidai kuwa muigizaji huyo amekubali kushirikiana na Mumewe Peter Komu katika kumzika mtoto Patrick ambaye Muna amekanusha kuwa sio wa Peter bali ni wa Casto Dickson.

Steve alifunguka siku ya jana Kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo ameamua kupangua hoja zote zilizotolewa na Muna ambazo zinamuhusu yeye.

Kwanza nimpe pole dada yangu Muna kwa kupita katika kipindi kigumu sana, kwa kuondokewa na mtoto. Tulikuwa tumejipanga kwenda kumuona, tukaambiwa kwa waliokoka huwa hawana 40, lakini kwa mzazi lazima kuwepo na 40. Mimi siyo mjinga wa kukurupuka tu kutangaza kuhusu msiba bila kuambiwa na wahusika wa msiba, sikukurupuka, mimi ni mtu mzima, nina familia na watoto, nilipewa maagizo hayo na Muna mwenyewe akiwa na ‘mumewe’ Joel Lwanga wakiwa Kenya, alinipigtia simu.

Nimemsikia akizungumza maneno mazito, eti nyumba anayoishi Peter haina hati, kama haina hati basi itakuwa ni ya serikali wakachukue nyumba yao. Anatukandamiza na kutoa voice, ametoa hisia zake kwa Watanzania, ametufundisha sisi vijana na wazee. Tukisema tufuatilie tutakuta mtoto uliyemsomesha hadi chuo kikuu ni wa mlinzi, mwanamke mwenye busara lazima awe na staha, ndoa siyo kitu cha mchezo jamani.

Nimemsamehe Muna kwa sababu hajui kama anachokizungumza anakifahamu. Hili liwe funzo kwa dada zetu, mimi nimemsamehe hata nikikutana naye asiogope kunisalimia, Shilole naye amemsamehe, usipoimamini biblia utamwamini sheria”.

Irene Paul Amkingia Kifua Muna

Msanii wa filamu za Kibongo, Irene Paul ameibuka na kumkingia kifua mwanadada Muna Love na kudai watu lazima waheshimu hisia za watu na kuweka mawazo yao pembeni.

Suala hili  limekuja baada ya sakata lililozuka jana baada ya Muna kufanya maongezi na waandishi wa habari na kuweka wazi kuwa Peter sio Baba wa marehemu Patrick na kumtaja Casto kama Baba Lakini pia aliweka wazi kuwa nyumba anayoishi Peter ni ya kwake na hati zote.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Irene Paul amemtetea Muna na kuwaomba watu wamuache aongee anachotaka kuongea kwani bado yupo kwenye maonbolezo ya mtoto wake.

Mimi nina mawazo kama walivyo watu wengine lakini ningependa tuheshimu hisia za Muna kama mzazi ambaye ni muhusika Mkuu wa mtoto aliyefariki na Kwenye maisha kila mtu ana jinsi ya ku-deal na stress kuna wengine wanapenda kuongelea matatizo yao na wengine wanapenda kunyamaza kwaiyo lazima tuheshimu mawazo ya watu”.

Kikao hiko cha Muna na waandishi wa habari hakikuaa vizuri na baadhi ya watu waliohisi ni mapema sana kuzungumza kwani mwanaye amekufa wiki mbili tu zilizopita na mmoja kati ya watu hao ni msanii Shilole: