“Mwaka 2018, Nilitimiza Ndoto Zangu”- Vanessa Mdee

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee maarufu kama ‘Vee Money’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mwaka 2018 ulikuwa mwaka mzuri sana kwani alitimiza Ndoto zake nyingi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Ijumaa Showbiz, Vanessa alisema mwaka 2018 alitimiza baadhi ya ndoto zake ikiwemo kuzindua albam yake ya Money Mondays na viatu vyake ya Bora Star by Vanessa Mdee.

Mwaka 2018 ulikuwa poa sana kwangu, namshukuru Mungu nilitimiza baadhi ya ndoto zangu ikiwemo kuzindua albam yangu ya Money Mondays na viatu vyangu vya Bora Star by Vanessa Mdee, naomba Mungu azidi kunifanikishia zaidi na zaidi mwaka 2019“.

Lakini pia Vanessa habanero mpango wa kuishia hapo kwani 2019 ana mipango makubwa zaidi kibiashara kwani hapo baadae anategemea kuja biskuti cha chokoleti zitakazoitwa Vee Choc.

https://www.instagram.com/p/BnGAQ2FByh2/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1dcqd85ipi7mo

Vanessa Mdee na Ndoto Yake Ya Kusambaza Viatu Vyake Afrika

Staa wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ameibuka na kuweka wazi kuwa Hivi sasa Ndoto Yake kubwa ni kuviona viatu vyake vinasambaa Afrika nzima.

Vanessa ambaye hivi karibuni alizindua bidhaaya viatu vyake vya kike hususani kwa wanafunzi, amesema yupo kwenye mchakato wakuvisambaza Afrika nzima.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Vanessa Mdee amesema kuwa moja ya mikakati ya kupanua soko la bidhaa za viatu vyake ni kuviuza  nje ya Tanzania.

Nategemea brand yangu kuipanua zaidi na ili ikue nategemea kupata masoko katoka nchi mbalimbali za Afrika, lengo ni kuwafikia wanafunzi wengi wa shule za kiafrika“.

Viatu hivyo vinapatikana katika maduka  mbali mbali nchini Tanzania na vinafanya vizuri kwenye mauzo  yake sokoni.

Vanesaa Mdee Afunguka Kuogopa Kufunga Ndoa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amefunguka na kuweka wazi kuwa anaogopa sana kufunga ndoa licha ya kwamba umri Wake alionao unamruhusu kufanya hivyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Vee Money alisema licha ya kwamba ana umri wa miaka 30 kwa sasa, lakini hajawaza kuolewa kwa sababu anaogopa atabanwa na majukumu ya ndoa na kushindwa kufikia malengo aliyonayo.

Vanessa Na Mpenzi Wake Jux

Umri wangu umefikia wa kuingia kwenye ndoa, lakini siwezi kwani nina malengo makubwa ambayo bado sijayatimiza hadi sasa hivyo nahofia nikiingia kwenye ndoa kuwa nitabanwa na kushindwa kuyatimiza, maisha ni malengo hivyo siwezi kukurupuka tu, nikishayatimiza hayo malengo ndipo nitaingia kwenye ndoa“.

Vanessa amekuwa kwenye uhusiano wa miaka mingi na Mpenzi Wake ambaye pia ni Msanii wa Bongo fleva Juma Jux.

Nedy Music Afungukia Mipango Ya Kolabo na Vanessa Mdee

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nedy Music amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kufanya kolabo na msanii mwenzake wa Bongo fleva Vanessa Mdee ‘Vee Money’.

Nedy Music ambaye amekamata headlines kwa siku kadhaa sasa Baada ya kujishindia tuzo za Afrimma zilizofanyika nchini Ghana ameweka wazi Kama ana mpango wa kufanya kolabo na Vanessa Mdee.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Nedy Music amesema si kweli kwamba walifanya kolabo nchini Ghana walipokutana Kama tetesi zinavyosambaa kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa.

Hapana sijafanya kolabo na Vanessa Mdee nchini Ghana na kama kutakuwa na kolabo itafanyika nchini Tanzania”.

Nedy Music na Vanessa Mdee walikutana na nchini Ghana ambako wote wawili walikuwa wamechaguliw kushiriki tuzo hizo lakini Vanessa hakuweza kupata tuzo hizo na Nedy alifanikiwa kijinyakulia tuzo moja.

“Ruby Inabidi Ujifunze Kula na Kipofu”-Vanessa Mdee

Msabii wa muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee maarufu Kama Vee Money ameibuka na kumtaka Msanii mwenzake Ruby kujishusha kwa watu na kupunguza kiburi.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tuhuma dhidi ya Ruby kuwa ni mgumu kufanya naye kazi kwani Ana kiburi kupitiliza kwaiyo inakuwa ngumu kwa wasanii wenzake na wadau kufanya naye kazi.

Siku ya jana Mange Kimambi alimchana Ruby kuhusu taarifa za kuwa mjeuri na kiburi mbele ya watu wanaomsaidia na kudai Ana kipaji sana lakini hafanikiwi kwa sababu watu wengi hawataki kufanya naye kazi kwa ajili ya kiburi chake.

Vanessa Mdee naye ameibuka na kumpa ushauri Ruby na kumtaka ajishushe anapokuwa na watu ili azidi kufanikiwa zaidi.

Kupitia Instagram, Vanessa Mdee amemuandikia maneno haya Ruby:

Leo nimekutana na Ruby na tumeongea sana kuhusu hii ishu yake, Nakupenda sana Ruby tupige kazi mama kula na kipofu, kuna muda mwingine jifunze kukaa kimya halafu acha muziki wako uongee zaidi fanya kwa manufaa yako na Mtoto wako”.

Ruby anatarajia kujifungua Mtoto Wake wa kwanza muda  wowote kuanzia sasa kwani hapo alipo ana  ujauzito wa miezi kadhaa.

Vanessa Mdee Afunguka Baada Ya Kuimba Nyimbo Ya Kihindi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee ameibuka na kuanika ugumu alioupata baada ya kuandika na kuomba wimbo wake wa Kihindi unaoitwa ‘Vaishnav Jan’.

Katika mahojiano yake na Risasi Vibes, Vanessa amedai kuwa alifuatwa na ubalozi wa India ambao upo Tanzania ili autunge na kuuimba wimbo huo kwa ajili ya kutumika kwenye maadhimisho ya miaka 150 ya kufariki kwa baba yao wa Taifa, Mahatma Gandhi ambayo hufanyika kila mwezi Oktoba huko India.

Orijino wa wimbo huu umefanywa na msanii wa kwao wa zamani sana wa kike, sasa katika kuadhimisha miaka hiyo 150 wakaona watafute mtu mbadala wa kufanya kava kwa ajili ya kucheza pamoja na video ndipo wakanipata mimi,” alisema Vee Money na kuongeza“.

Kwa hiyo kutokana na fursa hiyo nikafanya wimbo nikiongoza na mwalimu wa lugha ya Kihindi na tukashuti video ndogo ambayo ipo Youtube. Ilikuwa kazi kwani Kihindi sijui lolote hata ukinitukana lakini kwenye kuimba nimefanya vizuri na tayari nimepokea barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje India, Swaraj akinipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanya“.

Baada ya kuimba wimbo huo serikali ya India ilimtumia barua  ya shukrani na kuonyesha kufurahishwa na wimbo ule.

Vanessa Mdee Amaliza Bifu Lake na Mimi Mars

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money amefunguka na kuweka wazi kuwa ameamua kumaliza bifu lililokuwepo kati yake na mdogo wake ambaye pia ni msanii mwenzake Mimi Mars.

Vanessa Mdee ameweka wazi kuwa yeye pamoja na ndugu yake huyo kama ilivyokuwa katika familia yoyote kulikuwa na migongano lakini amefikia uamuzi wa kumaliza bifu hilo na kwa sasa wako vizuri.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Vanessa Mdee Vanessa amesema kuwa ameamua kumaliza tofauti kati yake na ndugu yake huyo kwa kuwa wao ni ndugu hivyo hakuna maana yoyote wao kutofautiana.

Naona ni jambo jema kwa kuwa mimi na mdogo wangu tulikuwa hatupo pamoja kutokana na sababu tu ambazo hazina msingi. Kwa hiyo nimeona tumalize bifu letu na tuendelee kupeana sapoti katika kazi zetu japokuwa kila mmoja anafanya muziki wake“.

 

Vanessa Mdee Amfariji Maua Sama “Usijali Utatoka Tu”.

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee amefunguki ishu ya Msanii mwenzake Maua Sama kuwekwa Ndani kwa siku tano mfululizo bila ya dhamana.

Maua Sama anewekwa  ndani tangu siku ya Jumapili mpaka leo hajapata dhamana baada ya kuonekana kwenye video clips akiwa anakanyaga  pesa huku akicheza wimbo wake wa ‘Iokote’.

Vanessa ameibuka n kumtaka Maua kuwa mjasiri na kumtaka kuwa mvumilivu kwani siku si nyingi atatoka na akisha toka watacheka na kusahau yote yaliyotokea.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa Mdee kamuandikia ujumbe huu:

https://www.instagram.com/p/Bn8Tpg3CHhO/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=rtlm6iay8rzk

Gigy Money Azimikia Figa Ya Vanessa Mdee

Msanii wa Bongo fleva Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa anavutiwa sana umbo la msanii mwenzake Vanessa Mdee.

Moja kati ya vitu ambavyo vilitengeneza headlines kuhusu Gigy Money ni kupungua ghafla kwa mwili wake na kuzua tetesi kuwa anaumwa na maneno mengine mengine.

Lakini Kwenye mahojiano na Clouds Fm, Gigy Money amesema hivi sasa anajithidi kupunguza mwili wake ili aweze kutumbuiza vizuri jukwaani kama anavyofanya Vanessa Mdee.

Kuna muonekano wa show tofauti na picha za Instagram mimi sasa hivi ni performer, huwezi kwenda jukwaani una limwili lako tu. Kwa hiyo mtu unatakiwa na mwili fulani hivi”.

Do you look Vanessa akiwa ana-perform, how do you feel unaoana kabisa machachari, anaweza kuwa na bendi, anaweza kuinua mguu, unafurahi, sio mtu shabiki anasubiri utikise makalio tu”.

Siku chache zilizopita Gigy Money alikiri kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka apungue mwili ni mapenzi ambapo alikuwa anaumizwa na penzi la Baba watoto wake Mo J.

Barnaba- Nikikutana na Vanessa Tunatengeneza Mziki Mzuri

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barnabas Elias ‘Barnaba Boy Classic’ amefunguka na kuweka wazi kuwa kila akikutana na msanii mwenzake Vanessa Mdee basi wanatengeza hits tu.

Barnaba anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chausiku’ aliyomshirikisha Vanessa Mdee amedai yeye na Vanessa wana chemistry fulani Inayovutana mpaka kutengeneza nyimbo kali.

Barnaba alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, amedai kuwa mashabiki zao wenyewe wanafahamu wakikutana yeye na Vanessa nini kitatokea ndio maana wanafanya vizuri:

Mashabiki wanajua mimi nikikutana na Vanessa kuna mambo mazuri yanakuja, sisi tuna chemistry ya pamoja, sauti zetu zimekuwa zikikutana pamoja kuna mambo mazuri yanatokea”.

Lakini pia Barnaba ameweka wazi kuwa kwa sasa mashabiki wameshachoshwa na kelele wanataka mziki mzuri:

Hii inaonyesha kazi ni nzuri watu wanapenda muziki mzuri, watu wamechoshwa na makelele wanahitaji muziki mzuri, na ukweli kazi na sio maneno maneno”.

 

G.Nako Atabiri Yeye Na Vanessa Mdee Watafika Mbali Zaidi na ‘Wet’

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap kutoka kundi la Weusi G Nako ametabiri ngoma yake na Vanessa Mdee inayoitwa Wet kufanya vizuri.

Ngoma ya Wet iliyoimbwa na Vanessa Mdee kumshirikisha G Nako inayopatikana kwenye albamu ya vanessa imeendelea kufanya vizuri na kushika chati mbali mbali nchini.

G Nako amefunguka Kwenye mahojiano na Jembe Fm na kudai kuwa tangua wanatoa wimbo huo walikuwa wameshautabiria makubwa sana kwani walijua ni ngoma kali.

Ni wimbo nzuri toka tulivyoureekodi, wakati albamu bado inaendelea kutengenezwa ilionyesha ni moja ya nyimbo zitakuja kufanya vizuri kwenye albamu.

So nafikiri mafanikio bado yataendelea kuwa makubwa na tunasubiri mafanikio mengine makubwa zaidi na mimi bado nashukuru kwa watu wote ambao wanaendelea ku-support”.

Video ya wimbo wa Wet unaendelea kusimbua kwa sababu ya ubunifu uliotumika Lakini pia umefanywa nchini Tanzania na producer Mtanzania tofauti na trend ya wasanii wengi siku hizi kupenda kushoot video zao nchi za nje kama South Africa na kwingineko.

Msanii Tox Star Akiri Kumkubali Vanessa Mdee

Msanii anayejulikana kama Tox Star amefunguka na kusema Katika wasanii wa kike kibongo Bongo basi kwa Vanessa Mdee ndio kafika.

Msanii huyu alipata umaarufu alipotoa wimbo uitwao Pretty Girl, aliomshirikisha Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’, ulimtambulisha vyema kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva.

Lakini baada ya kutoa hits chache chini ya uangalizi wa Ostaz Juma na Musoma kama  Kitaani akimshirikisha Dully Sykes lakini baadae msanii hiyo alipotea Kwenye ramani.

Kwenye Interview aliyofanya na gazeti la Risasi, Tox Star alifunguka kuwa hakuna msanii Bongo anayrmkubali kama Vanessa Mdee:

Vee Money. Kiukweli huyo dada ninamzimia sana na siku moja nitafanya naye kazi. Nikibahatika mashabiki wangu watauona ule wimbo wa mwanamuziki kutoka Marekani, Nelly uitwao Dilema ukirudi tena kivingine“.

Msanii huyo ametoa ngoma mpya  ijayo kwenda  jina la chukua ambao amedai ndio utamrudisha Kwenye chati tena.

Vanessa Mdee Azidi Kupata Mafanikio na Albamu Yake Ya ‘Money Mondays’

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee amezidi kufanya vizuri na albamu yake ya ‘Money Mondays’ kwani albamu hiyo imetajwa kuwa ndio inaongoza Afrika Mashariki nzima.

Kupitia mtandao wa Boomsplay ambao unahusika na upakuaji wa nyimbo kadhaa umeweka wazi kuwa Albamu hiyo ndio kinara kupitia mitandao yao ya kijamii ambapo wameandika ujumbe huu:

Hongera nyingi sana kwake @vanessamdee kwa kuwa na albamu namba moja kwa mauzo na kusikilizwa, ukanda wa Afrika Mashariki nzima ! Wewe kama shabiki wake mkubwa uliyewezesha hili, tunakupa pongezi pia na endelea kuipa support “Money Mondays” kila siku!”.

Vanessa Mdee alionyesha kufurahishwa na taarifa hiyo kwani alitumia ukurasa wake wa Instagram kushukuru mashabiki zake kwa kuweza kupakua wimbo mpaka kufanya uwe namba moja:

Thank you Asante Sana for making #MoneyMondaysTheAlbum the NO 1 ALBUM in East Africa @mdeemusicofficialmmetishaaaaaa @boomplaymusic_tz@boomplaymusicke @boomplaymusicngwith over a million plays/streams. #SwimmingInJesusJuice #BestFansInTheWorld.”

 

Diamond Amwagia Sifa Kibao Vanessa Mdee

Msanii wa bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameibuka na kumwagia sifa kibao msanii mwenzake Vanessa Mdee na kudai ni mpambanaji sana.

Diamond alifunguka hayo baada ya Vanessa kuwekwa na Wasafi Tv kama Women Crush Wednesday ambapo walimshukiru mchango wake katika Bongo fleva.

Diamond aliandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alifunguka kwa kumtumia ujumbe huu wa shukrani Vanessa:

Vanessa ni moja kati ya waaanii wa kike Kwenye Bongo fleva anayefanya vizuri sana kitaifa na kimataifa na hata albamu yake ya Money Mondays aliyotoa mapema mwaka huu bado inafanya vyema.

Vanessa Mdee Amesema Hana Mpango Wa Kwenda Kufanya Kazi Zake Nje Ya Nchi Tena

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee anayefanya vizuri kwa hivi sasa na kibao chake cha ‘Wet’ amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kwenda nje ya nchi kutengeneza video kwani hapa Bongo kuna madirector wakali.

Vanessa Mdee amefunguka na kudai kuwa kutokana na maprodyuza wa video za muziki kujitambua na kuanza kutengeneza kazi nzuri, hakuna haja ya kutoka nje kwa sasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Showbiz Xtra, Vanessa  ametambulisha  video yake ya wimbo namba tisa unaopatikana kwenye albamu yake hiyo uitwao Wet aliomshirikisha G Nako, aliongeza kwamba hata akiwa na hamu ya kufanya kazi na prodyuza wa nje atahakikisha anamleta Bongo ili ashirikiane na maprodyuza wa ndani kufanya kazi.

Kwa sasa kiukweli tutabanana hapahapa. Mambo ya kutoka nje huku maprodyuza wetu wanafanya kazi nzuri sioni kama ni kitu kizuri kwa sasa, binafsi kazi nyingi nitafanyia Bongo”.

Ni kawaida kwa mastaa wengi wa Bongo kama Diamond, Alikiba, Vanessa, Navy Kenzo kwenda kutengeneza video zao nchi za nje kama South Africa ambazo wamedai kuna madirector wazuri kabisa wa video lakini hivi sasa tunajivunia na vya kwetu kama Vanessa.

Vanessa Mdee Akumbwa na Skendo Ya Utapeli

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee amejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyoshewa vidole na kudaiwa kuwa ni tapeli baada ya watu waliouza albamu yake ya ‘Money Mondays’ kudai hawajaliowa.

Mwezi uliopita Vanessa aliachia albamu yake ya kwanza alioyoiita jina la Money Mondays. Albamu ambayo iliuzwa kwa njia zote yaani kidigitali kumaanisha kipitia mitandao mbali mbali ya kuuzia muziki Lakini pia kwa DVD yaani CD zilizouzwa mtaani.

Stori Hizi za kutapeli wauzaji wa albamu yake zimekuwa zikisikika chini chini lakini siku ya jana kwenye kipindi cha XXL ya Clouds Fm Soudy Brown aliongea na mwanadada aliyejitambulisha kama Jacky Tarimo aliyedai kuwa wamefanya kazi ya kuuza albamu hiyo kwa siku ishirini lakini wakiombwa walipwe wanakataa.

Kwenye mahojiano hayo mdada huyo alidai kuwa walikuwa wanataka  kufanya kazi mara mbili kwa wiki na kila siku ni shilingi elfu 15 na walifanya kazi kwa siku 15 lakini hawajaliowa hata senti mpaka muda huu.

Vanessa Mdee alipotafutwa ili kujibu tuhuma hizo hakupokea simu na meneja wa Vanessa anayeitwa Tahiya alikataa kujibu chochote kuhusu tuhuma hizi.