Wema Ashindwa Kuzuia Hisia Zake kwa Ommy Dimpoz

Mwanadada Wema Sepetu ameshindwa kuzuia hisia zake baada ya msanii Ommy Dimpoz kutoa wimbo mpya ambao umeanz akufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya habari,aliomshirikisha Sayi Shey kutoka Nigeria unaojulikana kwa jina la yanje.

katika ukurasa wake wa instagram wema sepetu aliandika”kimya kingi kina mshindo  nkubwa, ngoma imebabmba hataree.sijui kwa sababu ni aina ya muziki ninayoipenda labda ,, forever bae umamaliza wallahy ..this one is just amazing..

Wema sepetu na ommy dimpoz walishawahi kufanya kazi pamoja na hata habari kusambaa kwamba waliwahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi, uhusiano uliopo kwa sasa kati awema na Diamond pia unaweza kuwashangaza wengi kwanini Wema ameweza kumpongeza wema kwa sababu Ommy na Diamond kidogo mambo hayako sawa.

Wema na Wenzake Wapata Deal Nono Star Time.

Mwanadada Wema Septu na baadhi ya wasanii wenzake kutoka tasnia ya sanaa ya bongo movies na muziki pia wamechaguliwa na star time kuwa mabalozi wa Star Time kwa kutoa elimu na kutangaza michuano ya kombe la dunia itakayo fanyika mwaka huu huko nchini urusi huku star time ikiwa ni moja ya kampuni itakayorusha michuani hiyo kwa lugha ya kiswahili.

Nina washukuru sana star times, kwa kuona fani zenu na ufanisi wetu wakaamini kuwa tunaweza kutumia hii platform kutangaza world cup kupitia star times kwa mwaka huu 2018.natambua ukubwa na uzito wa kazi iliyopo mbele yetu , kwangu hii ni kama kazi nitatumia fursa hii  kama kazi nyingine ninayoifanya kwa kushirikiana na team wema na team zangu zingine kubwa sana kufanikisha kazi hii.

tutafanya kazi ya kuelimisha watu na watazamaji kwa kuwaambia jinsi gani wanaweza kuangalia michuano hii ya kombe la dunia kupitia star time kwa mara ya kwanza kwa lugha ya kiswahili.

Huu ni mwanzo mzuri kwa wasanii hao hasa Wema Sepetu ambae tuzo alizozipata mwaka huu zinaendelea kumfungulia milango ya mafanikio zaidi.

Wema Sepetu Atoa Kauli Ya Kifo Chake

Msanii wa filamu za Bongo movie Madam Wema Sepetu amerudi tena Kwenye headlines huku safari hii akishangaza watu wengi baada kusema akifa anataka watu wapendeze Kwenye msiba wake.

Msanii wa Bongo fleva Shilole alisema kuwa siku ya msiba wake anataka aagwe Kwenye Msikiti na sio Leaders Club ambako watu wanakaa na kunywa na kufanya starehe nyingine.

Wema naye ameibuka na kudai kuwa akifa anataka Kwenye msiba wake watu wapendeze wavae vizuri na wafurahie maisha aliokuwa anaishi Lakini pia anataka jeneza lake lipambwe kwa maua ya pinki.

Napenda sana siku ya mazishi yangu waombolezaji wawe kwenye muonekanao mzuri na pia sehemu ambayo mwili wangu utafikia pawe pamepambwa vizuri kwa maua ya pinki yanayovutia,” alisema Wema“.

Staa huyo alifunguka zaidi kuwa kwenye mazishi yake hayo baada ya familia, mtu mwingine ambaye anataka awe mstari wa mbele kwenye mazishi yake ni staa mwenziye, Aunt Ezekiel na kudai kuwa yeye ndio ataweka ua wa kwanza kwenye kaburi lake kabla ya staa mwingine yeyote.

 

Mama Kanumba Amwagia Povu Zito Wema Baada Ya Kugoma Kuigiza Naye

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu alifunguka hivi karibuni na kuweka wazi kuwa miaka ya nyuma wakati yupo Kwenye Mahusiano na Marehemu Steven Kanumba alimwambia hataki mama yake aigize.

Tangu Kanumba aage dunia miaka michache iliyopita mama yake mzazi na yeye ameingia Kwenye sanaa ya Bongo movie na hivi sasa ameshaigiza Movie kadhaa.

Siku chache zilizopita Wema Sepetu alifanya mahojiano na Global Publishers ambapo aliulizwa kama atakuwa tayari kushirikiana Kwenye filamu na Mama Kanumba ndipo Wema alitoboa kuwa hawezi kwa sababu  Kanumba alikataa mama yake kuigiza.

Baada ya taarifa hizo kusambaa Mama Kanumba ameibuka na kumtolea povu zito Wema na kudai kuwa sababu pekee ambayo ilimfanya mwanaye amkataze kucheza filamu ni kwa sababu alikuwa anamuangalia yeye na kumtunza lakini hivi sasa hana msaada hivyo inatakiwa aigize.

Kanumba alisema hayo kwa kuwa alikuwa ananitunza yaani ananinunulia vyakula na kunilipa mshahara kila mwezi kama mfanyakazi lakini sasa hayupo, je Wema alitaka nishike bakuli nikaombe barabarani au? Maana kulima siwezi hivyo naona tu bora niigize ili niweze kujikimu kimaisha”.

 

Kanumba Alikataa Mama Yake Kuigiza, Siwezi Kuigiza Naye

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuigiza filamu moja na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kwani Mwenyewe hakutaka mama yake ajiingize Kwenye sanaa.

Wema ameanika hayo huku akisisitiza kuwa kipindi wakati Kanumba yuko hai alimweleza Wema ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kamwe hataki mama yake ajiingize kwenye Bongo movie.

Wema alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambao walimuuliza endapo yupo tayari kucheza filamu na Mama Kanumba ambaye hivi sasa amegeukia sanaa hiyo:

Hapana, siwezi kwa sababu Kanumba alikuwa hataki mama yake aigize na hata mimi alishaniambia, sasa nitavunja makubaliano yetu mimi na Kanumba”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Wema alikataa tuhuma alizorushiwa na Mama Kanumba kuwa alipownda nyumbani kwa Wema hakufunguliwa geti badala yake aliishia kuchomeshwa mahindi:

Jamani…kwanza siku hiyo mimi sikuwepo kabisa, niliambiwa tu alikuja na kwa nini nifanye hivyo sasa“.

 

Hii Ndio Sababu Ya Wema Kutohudhuria Mazishi Ya Agnes Masogange

Wikiendi iliyopita marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’ aliagwa na wasanii wenzake wa Bongo movie pamoja na Bongo fleva kwenye viwanja vya Leaders Club.

Lakini Wema Sepetu alizua gumzo baada ya kitohudhuria siku hiyo wasanii wote walipoenda kisha mwili na hata wasanii waliposafiri kwenda Mbeya kwenda kumzika.

Hapo mwanzoni kuna taarifa zilikuwa zinaenea na kudai kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka Wema  asihudhurie mazishi ya Masogange ni kwa sababu ya bifu lili kuwepo kati yake na marehemu.

Baada ya Tetesi hizo kuenea gazeti la Risasi Mchanganyiko lilimsaka Neema Ndepanya ambaye ni meneja na mtu wa karibu wa Wema ambaye alifunguka haya:

Wema alikuwa na nia ya kufika msibani kabisa na alikuwa ameshajiandaa lakini ilishindikana baada ya kuugua tumbo la ghafla ikabidi aahirishe tu, pia Mbeya alishindwa kusafiri maana Jumatatu ambayo ndiyo mazishi ya Masogange alikuwa anatakiwa kuhudhuria mahakamani kwenye kesi yake inayoendelea”.

Agnes Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao Mbeya ambako alizikwa jana Aprili 24, 2018 kijijini kwao Utengule, Mbalizi.

Wema Atangaza Ujio Wa Lipstick Zake Baada Ya Kufungiwa

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Wema Sepetu amerudi kwa kasi ya ajabu katika ulimwengu wa Biashara ya lipstick baada ya kufungiwa kwa muda na biashara kusimama.

Wema alikuja na bidhaa hizo kwa mara ya kwanza miaka michache iliyopita lakini baadae zilikuja kufungiwa na TFDA kwa kukosa vigezo vya Kutumia na binadamu.

Wema amerudi Tena bidhaa hizo ambapo atakutana na mashabiki wake pamoja na wakazi wote wa Arusha kwa siku mbili mfululizo kuwauzia bidhaa zake mpya za Lipsticks ambazo mashabiki wake walizimiss kwa miaka miwili.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema amesema kuwa ataanza kuuza bidhaa hizo mkoani Arusha kwa siku mbili kuanza tarehe 26 hadi 27 Aprili 2018, ambapo yeye mwenyewe ndiye atakayekuwa anahudumia wateja watakaokuwa wanahitaji huduma, katika duka la Kubrasadiki.

Good News For you, Tunakuja week hii tar 26 na 27… Tutakuwepo kwenye Duka la Wakala wetu Mkubwa wa Arusha @kubrasadiki @kubrasadiki @kubrasadiki. Na nitakuuzia Lipstick mwenyewe… Cant wait kumeet warembo wangu…. Alhamis na Ijumaa hii Ladies & Gents”.

 

Monalisa Afungukia Bifu La Wema na Riyama

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amefunguka na kuongelea bifu lililosemekana lili kuwepo kati ya waigizaji wawili wa Bongo movie ambao ni Wema Sepetu na Riyama Ally.

Wiki chache zilizopita Wema alichukua tuzo ya Muigizaji bora wa kike kwenye Bongo movie Kupitia Tuzo za SZIFF ambayo alishindanishwa na wasanii wengi kama Riyama.

Baada ya Riyama kukosa tuzo ile alifanya Interview na kituo kimoja cha redio na alimwaga machozi live  kabisa huku akidai kuwa yeye alistahili kupata tuzo ile na kuwataka SZIFF wamuombe radhi kwani kukosa kwake tuzo ni Kumdhalilisha.

Baada ya kuongea maneno hayo moja kwa moja ilivhukuliwa kuwa Riyama amejijengea bifu na Wema Sepetu kwani ni sawa na alisema kuwa Wema hakustahili kupata tuzo hiyo.

Lakini Riyama na Wema walizima tetesi hizo za kuwa na bifu baada ya kupiga picha pamoja wakiwa Airport walipoenda kumpokea Monalisa ambaye alikuwa ametoka kuchukua tuzo yake nchini Ghana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm Monalisa alifunguka haya kuhusiana na maneno yaliyosemwa kati ya Wena na Riyama:

Kwanza niseme nilivyofika pale sikutegemea kuona watu lakini nilivyoshuka nikakutana na wasanii wenzangu, nilijisikia furaha sana..

Nilifurahi kuawaona, sidhani kama Riyama kamlalamikia Wema nyie tu ndio mnachukulia vibaya, Riyama alikuwa na malalamiko yake na mimi ninayafahamu toka siku ya kwanza”.

 

Wanaume Watano Wamejitokeza Wanataka Kunioa- Wema

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kueleza jinsi wanaume wanavyomiminika kwao kutaka kutoa posa ili wamuoe.

Wema amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda ambapo amedai kuwa kuna muda wanaume watano tofauti walienda kutoa posa kwao lakini aliwakataa wote:

Walijitokeza karibu wanaume watano wanaenda, kwa mama kupeleka barua kinachotokea mama ananiita, ananiuliza mimi, sikubali kwa sababu siwezi kuolewa na mtu ambaye simjui au sijakaa naye“.

Lakini kuhusu Kuolewa hivi sasa Wema amejibu hawezi kuweka wazi lakini ana mpenzi wake ambaye anampenda lakini hawezi kumuweka wazi kwani amekuwa mtu mzima siku hizi.

Wema amefunguka na kumpongeza msanii wa Bongo fleva ambaye pia ni rafiki yake wa karibu Ali Kiba kwa kufunga ndoa hivi karibuni ambapo amesema:

Ninampongeza sana kwa mwanamuziki mkubwa kama yeye kufanya jambo hilo amejijengea heshima kubwa sana, lakini ninaamini mke yupo popote ni jinsi tu Mungu alivyokupangia wapi utampata“.

“Hamisa Aliniongelea Maneno Mabaya, Sio Rafiki Yangu”- Wema

Staa wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amefunguka kuhusu uhusiano wake na Baby mama wa Diamond, Hamisa Mobetto na kusema hana bifu naye lakini pia sio rafiki yake.

Kama utakumbuka siku za nyuma Wema na Hamisa walikuwa vizuri tu Tena walikuwa marafiki wakubwa lakini Ghafla kuna taarifa zilienea kuwa Wema anataka kukodi watu wakumchamba Hamisa.

Lakini pia ilisemekana chuki ya ghafla kutoka kwa Wema kwenda Hamisa ilitokana na taarifa zikivyosambaa kuwa Diamond alikuwa anachepuka na Hamisa kipindi chote alivyokuwa na Mahusiano na Wema.

Wema amewafungukia Global Publishers, Ijumaa Wikienda na kusema yeye hana bifu na Hamisa ila alimchukia pale aliposikia anamuongelea vibaya kwa watu hapo ndio urafiki wao uliishia:

Sina bifu na Hamisa ila siyo rafiki yangu kabisa kwani kuna maneno aliniongelea mabaya sana, tena siyo kwa kuambiwa, kwa kusikiliza sauti, sasa nikaona huo ni unafiki kwa hiyo nikaona kila mtu achukue muda wake na hata tukikutana kila mtu na hamsini zake“.

Wema alipoulizwa kuhusu Zari aliweka wazi kuwa hana tatizo na Zari Tena anampenda.

Najua Tabia Za Diamond Nikiwa Naye Atanisumbua Sana- Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu kwa mara nyingine amejibu tetesi zilizozagaa kuwa amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Tetesi za Wema kurudiana na Diamond zilianza kuapmba moto Miezi michache iliyopita baada ya Zari kutangaza kuwa alimuacha Diamond baada ya kumuona amekumbatiana na Wema huku akidai wamerudiana Tena.

Lakini Wema siku zote amekuwa akikataa tetesi hizo na kusisitiza kuwa Diamond ni rafiki yake wa karibu tu. Lakini Siku mbili hizi imedaiwa Wema alibeba ujauzito wa Diamond jambo ambalo amelikataa na kusema tayari ana mpenzi wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Wema ameweka wazi kuwa hawezi kurudiana na Diamond kwani anajua tabia zake lakini pia amesema hata akitaka kumuoa hawezi kukubali:

Yaani Diamond, hata aache kila kitu akaniambia sasa Wema nataka kukuoa sitakubali kabisa Alafu nilimpenda zamani, lakini siyo sasa kwa sababu Nasibu nimekaa naye miaka miwili. Najua alivyo na hatanisumbua sana kwa sababu mimi nilimwacha CK kwa ajili yake, matokeo yake akatoka na Meninah (msanii wa Bongo Fleva) na meseji nilizibamba. Kwa hiyo hata kwenye ndoa hawezi kubadilika.

Lakini pia Wema amejitetea kuhusu suala la yeye kuonekana anaenda nyumbani kwa Diamond Madale ni jambo la kawaida kwani alienda kwenye swimming party aliulizwa tu na Diamond kama rafiki yake.

Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Mimba Iliyotoka Na Muhusika Wa Mimba Hiyo

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka kuhusu janga lilompata hivi katibuni baada ya kuweka wazi kuwa mimba aliyokuwa amebeba kwa mara ya pili imetoka Tena.

Wema amekuwa muwazi sana juu ya kipindi kigumu  akijaribu kutafuta mtoto kwani sio mara ya kwanza kwa Wema kuweka wazi kuwa amepata miscarriage kwani miaka michache iliyopita mimba yake na Idris Sultan ilichoropoka.

Wiki iliyopita Wema Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka wazi machungu yake baada ya kuandika kuwa kwa mara ya pili mimba aliyokuwa amebeba imetoka tena.

Mara moja baada ya habari hizo kusambaaa tetesi nazo zilianza kutembea kuwa muhusika wa mimba hiyo hakuwa mwingine bali ni staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye alisemekana kuwa na Mahusiano naye.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Wema amekataa tetesi hizo na kudai Diamond hakuwa muhusika wa mimba hiyo kabisa na kumtaja mwanaume mwingine:

Hakuna ukweli wowote, ni ya mtu mwingine kabisa Diamond ni Hakuna lolote ila ni mshkaji wangu ambaye si unajua tumezoeana sana!”.

Lakini pia Wema aliweka wazi kuwa mimba yake iitoka muda mrefu uliopita ila aliweka wazi wiki iliyopita:

Kusema ukweli hiyo mimba imetoka karibia mwezi na nusu hivi umepita lakini kilichotokea Mimi niliweka picha moja ya mwanamke mwenye tatizo kama langu la kushika mimba kisha inatoka ndipo nikaandika; ‘My Life Story’.  

Hapo ndipo watu walichukulia kama nimepatwa na janga hilo kwa wakati huu, lakini ukweli ni jambo lililonipata mwezi na nusu uliopita“.

 

Mahakama Yamtaka Wema Sepetu Kujibu Kesi Yake Ya Madawa Ya Kulevya

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amezidi kuwa katika wakati mgumu kwani kesi yake ya madawa ya kulevya inaendelea kuunguruma na halikumfurahisha kamtaka kujibu kesi hiyo mahakamani.

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu imesema Wema Sepetu na wenzake wawili wanaokabiliwa na tuhuma za kutumia madawa ya kulevya wana kesi za kujibu hivyo wataenda kujitetea mahakamani kuanzia mei 14 na 15 2018.

Wema Sepetu alifunguliwa kesi hiyo mwaka jana mwanzoni baada ya kukutwa na misokoto kadhaa ya bhangi nyumbani kwake na kwa kipindi cha muda mrefu kesi yake imekuwa ikiendelea kusomwa kwenye mahakam ya hakimu mkazi Kisutu.

Maznat Ampa Moyo Wema Sepetu Kuhusu Mtoto

Moja ya wanawake jasiri na maarufu nchi katika sekta ya mitindo na urembo Maznat bride amefunguka na kumpa moyo mwanadada Wema Spetu amabe kila siku amekuwa akionyesha kilio chake cha kupata mtoto lakini ombi lake limekuwa hakujibiwi,.

Wiki iliyopita wema aliweka picha akionyesha kusinoneka kutokana na mimba yale kuharibika . kitu kilichowaumi za watu wengi na kumuonea huruma kwa mapito anayopitia.

Katika ukurasa wake wa instagram,maznat alimwambia Wema kuwa kila mtu upewa kitu kulingana na muda ambao mungu amempangia hivy wala hasikate tamaa.

kuitwa mama sio lazima uzae, ukifika tu umri wa kiutwa aunty, mamdogo, shangzai au mama mkubwa ina maana wewe tayari ni mama, kuwa mama siyo lazima uingie labour , miminashukuru mungu kwa sababu nimezaa nimelea watoto wangu na wsio wangu na katika hayo nimejifunza kupenda watoto kwa dhati na pasipo kubagua.nimejifunza kuwa ukiwapenda kwa uendo wa kweli kabisa na wao watakupenda hivyo hivyo bila kubagua.lakini pia nilijifunza kuwapenda watoto yatima na kujitoa shiling yangu ya mwisho bila hata kuwajua wazazi wao.tena nikajitoa kwa moyo wangu wote na nguvu zangu zote  wala sikutaka kuwaza.

mungu ni msiri sana mdogo wangu wema sepetu @wemasepetu anajua nini kinamstahili nani na kwa muda gani, muda wa mungu ukifika atakufanyia suprise na faraja ya ajabu.atakupa kile moy wako unataka.atakutunuku zawadi ya ajabu, na ya kipekee, jipe moto al  its well, eeeh mungu na kila mwanamke apate hata katoto kamoja.

TCRA Watoa Onyo Kali kwaTimes Fm Na Clouds Fm

Kamati ya maudhui ya TCRA wametoa adhabu na onyo kali kwa vituo viwili vya habri vya times fm na Cloud fFm baaada ya kuonekana kurusha vipindi vilivyoshindwa kufuata maudhui ya utangazaji.times fm ambao walitangaza mahojiano ya msanii Diamond Platinumz ambae alifunguka na kuongea majibu yaliyoonyesha kujibu kwa dharau uamuzi wa Naibu Waziri wa habari baada ya nyimbo yake na baadhi ya wasanii wenzake kufungiwa.

Times Fm kupiti akipindi chake na muda ule wanapaswa kumuomba Naibu Waziri Mh Juliana Shonza msamaha kwa maneno achafu yaliyotamkwa na msanii huyo na kutaruhusu kutoka katika jamii na kuwaomba msamaha jamii kwa ujumla.

Lakini pia Clouds Fm wamepewa onyo kali baada ya kutoa taarifa iliyokinzana mizani kati ya Roma na Mh. Naibu Waziri wa Habari baaada ya Roma kufungiwa kutokufanya kazi kwa miezi sita.

Wema Sepetu: Tuzo Zangu Zimewatoa Povu na Sasa Nina Hasira Ya Kufanya Kazi Nzuri

Msanii wa Bongo movie Wema sepetu amefunguka tena kuhusiana na wasanii wenzake kumtolea povu baada ya kujishindia tuzo mbili kamamsanii bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Wasanii kama Batuli na Irene Uwoya wameweka wazi kuwa hawajapendezwa na kitendo cha Wema kushinda tuzo ya msanii bora wa kike na kuamini kuna wasanii  wengine wanaofanya vizuri kuliko wao kwenye tasnia hiyo.

Baada ya povu hilo Wema amewajia juu wasanii hao na kuwataka waache wivu kwani yeye amestahili tuzo hiyo kwa movie yake ya heaven sent kwani imeleta changamoto kwa wasanii wenzake.

Kwenye Interview aliyofanya na Millard Ayo Wema alifunguka haya:

Kwanza kikazi kidogo tu cha heaven sent kimeleta maneno haya kwaiyo wamenitia hasira na pia wamenifanya nione kuwa mimi ni tishio kwao alafu huyo mtu ambaye anaongea nimesha fanya naye kazi alafu tumeshawahi kuwa karibu mimi sina tatizo na yeye nashangaa kwa Nini imekuwa hivi halafu nimeshafanya naye movie na nimmnyoosha kwenye kazi ambayo tumefanya lakini sijawahi kusema kitu chochote kibaya juu yake”.

Wema ameongeza kuwa kinachosababisha mpaka mambo yanakuwa hivi ni wasanii wa Bongo movie kuoneana wivu Ambao unasababisha kunakuwa hakuna umoja kati yao hali inayosababisha tasnia hiyo kurudi nyuma.