Wema Sepetu: Kanumba Umebadilisha Maisha Yangu Milele Nitalienzi Jina Lako

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka mazito katika siku ya kumbukumbu ya marehemu Kanumba ambaye alifariki miaka mitano iliyopita.

Wema alikuwa Kwenye Mahusiano ya kimapenzi na Steven Kanumba mwaka 2007 baada ya kutwaa taji la Miss Tanzania na baada ya hapo Kanumba ndiye aliyemuingiza katika fani ya kuigiza kwenye Bongo movie.

Mara kwa mara Wema ameweka wazi kuwa walipokuwa Kwenye Mahusiano ndipo Kanumba alimshawishi Wema aingie kwenye filamu na kusema aliomshirikisha kipaji chake hata kabla yeye mwenyewe hajaona, Wema na Kanumba walicheza pamoja filamu kadhaa.

Siku ya Jumamosi ilikuwa ni Kanumba Day ambapo ilikuwa ni maadhimisho ya kifo chake na Wema alitumia ukurasa wa Instagram kumkumbuka Kanumba na kutupia picha kadhaa ambapo zilisindikizwa na ujumbe mzito wa kumbukumbu:

 

Dude Azunguzmia Ushindi wa Wema Sinema Zetu

Msanii mkongwe wa bongo movie Kulwa Kikumba maarufu kama Dude amezungumza hisia zake kuhusu wasanii mbalimbali waliopata mnafasi ya kushinda tuzo za sinema zetu wikiend iliyopita hasa kwa upande wa Wema sepetu ambae watu wengi walikuwa wakilalamika kuwa inawezekana msanii huyo atakuwa amependele wa sana na kuachwa kwa baadhi ya wasanii.

Hata hivyo baada ya Wema kushinda tuzo hizo aliweza kupata kampuni ambayo ameingia nayo mkataba na kuweza kumuuzia filamu yake ya Heaven sent ambayo  imempa tuzo.

Dude anasema kuwa ushindi wa mwema umetokana na kura nyingi alizozipata kutoka kwa mashbiki ambao wamekuwa wakimuna tu kwa vile alivyo bila kuangalia kama kuna kitu anaweza ndani ya sanaa, na pia walikuwa wakimpigai kwa sababu ya kumsikia tu lakini hawakuangalia ubora wa kazi zake.

Mpoki alishawahi kushinda  award za kili kwa kategoria ya muzii wa asili na kumshinda wanne star na Mrisho Wpoto na hiyo ndio faida ya  kura za mashabiki, na hapo ndio kweny tatizo.sikatai wema kushinda lakini  tatioz linakuja kwa waandaaji wa tuzo za nje  wanweza  kumsikia wema ameshinda nchini wakampeleka kule  atafeli maan ni ukweli ulio wazi kwamba Wema hawezi kuwazidi wengine kama wakina Riyama.–Aliongea dude alipokuwa akizungumza na AMANI.

Wema Sepetu Apata Dili Nono, ni Baada ya Kuonekana SZIFF

Msanii wema septu ambae aliingia katika headline wiki hii baada ya kupokea tuzo za sinema zetu kupitia filamu yake ya heaven senr amepata dili nono na kusaini =mkataba na kampuni moja ya kusambaza filamu zake inayojulikana kama Auguster.

Mkataba huo umesainiwa leo katika ofisi za Azam Tv na kuhudhuriwa na watu mbalimbali akiwepo mwandishi na mtayarishaji na rafiki wa karibu wa star huyo Neema Ndepanya.

Wema anasema kuwa tangu kutolewa kwa movie hiyo mashabiki wake walikuwa wakiipata movie hiyo kupitia applicatuon yake tu na hakukuwa na DVD za filamu hiyo lakini sasa hivi wataanza kuipata kupitia huko.

Wema anasema kuwa uamuzi wa kampuni hii kusaini nae mkataba unakuja pale ambapo filamu hiyo  imeweza kupata tuzo mbili hivyo kuonekana ni moja ya filamu bora pia.

Baada Ya Kushinda Tuzo Mbili Wema Sepetu Alamba Shavu Hili Tena

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amelamba  shavu jingine siku ya jana baada ya kutangaza kuwa filamu yake ya Heaven sent itauzwa kwa mfano wa DVD ili kuwafikia watazamaji wengi.

Wema alijishindia tuzo mbili wikiend iliyopita kutoka katika tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) ambazo ni Muigizaji bora wa kike 2018-2019 na People’s choice Award (Chaguo la watu).

Lakini inaonekana huo ulikuwa mwanzo tu wa baraka za Wema kwani jana kwenye mkutano na waandishi wa habari Wema ametangaza kupata dili jingine na Azam Tv likiwa ni Kusambaza movie yake kwenye mtindo wa DVD.

Tangu movie ya wema imetoka mapema mwaka jana amekuwa akiiuza filamu hiyo kwa mtindo wa digitali kumaanisha amekuwa akiuzia filamu hiyo Kupitia App yake ya Wema Sepetu inayopatikana kwa simu za Android.

Wema amehaidi kufanya filamu full time na kuhakikisha analeta mambo mazuri katika tasnia hii ya Bongo movie lakini pia Kumekuwa na tetesi kuwa mwezi wa Sita ana mpango wa kuzindua filamu yake aliyoigiza na Van Vicker.

Wema Aweka Ahadi Nzito kwa Rc Makonda.

Msanii Wema Sepetu amejibu kwa kishindo cha kuweka ahadi pongezi kubwa aliyopewa na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda baada ya siku  ya jana Mh huyo kumpongeza Wema kwa kushinda tuzo za sinema zetu kupitia filamu yake ya heaven sent.

Wema amemshukuru sana makonda kwa kumtia  moyo na kumfariji sana kwa kipindi hiki ambacho anahitaji sana kuwa anafarijika ili kufanya vizuri zaidi.

lakini pia naomba nikuahidi sitakuangusha ,maana kumuangusha RC wako nako sio pambe kabisa

Wema pia anaendelea kwa kusema kuwa katika tasnia hiyo ya filamu kwa sasa wanataka watu wanaojielewa na wanaotaka kufanya kazi na sio watu wanaokurupuka na kuongea mambo bila kudadavua.

Yote yanawezekana , wasanii ni watu wenye wadhifa mkubwa sana,najivunia kuwa mmoja kati yaonajua hata wewe unajivunia sana kuwa kati yetu sisi,ukiwa kama mlezi na kutuongoza kila leo kutaka tufike sehemu nzuri na inshallha tutafika.”

RC Paul Makonda Amwagia Misifa Lukuki Wema Sepetu

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameshindwa kujizuia na kumwagia Misifa Lukuki msanii wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kujishindia tuzo ya muigizaji bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Tangu Wema ashinde tuzo hiyo siku ya jumapili Kumekuwa na maneno maneno mengi hasa kutoka kwa wasanii wenzake wa Bongo movie ambao wameona kuwa hajastahili kushinda tuzo hiyo.

Paul Makonda amemwagia sifa hizo Lukuki Wema na kuwajia juu wale wote wanaoziponda tuzo hizo zilizoandaliwa na Azamu Tv na kudai watu hao hawana hata uwezo wa kuandaa tuzo za kuku.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Paul Makonda alimwagia Wema sifa hizi:

Naomba picha uliopokea Tunzo kwa sababu nimesikia maneno maneno kwa watu wasioweza hata kuandaa tuzo za kuku. Hongera Azamu Tv mmefanya kuliko hata matatajio ya watu. Endeleeni kufanya vyema ili mwakani mpokee tuzo tena na wale wenye kukosa endeleeni kukosa ili mwakani mkose tena. Huu ndio Utamaduni unaofanya wenye kufanikiwa wachukiwe na wenye kuchukia kujifariji kwa maneno bila kuweka bidii katika kazi”.

 

Esha Buheti Amtetea Wema Sepetu Baada Ya Kuambiwa Hastaili Kushinda Tuzo

Msanii wa Bongo movie Esha Buheti amewajia juu wasanii wote wa Bongo movie wanaodai kuwa Wema Sepetu hakustahili kushinda tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Siku ya Jumapili pale Mlimani City hall Kulikuwa kuna ugawaji wa tuzo za Sinema Zetu (SZIFF) kwa wasanii wa filamu za Bongo movie na moja kati ya wasanii waliopata tuzo kubwa ni Wema Sepetu aliyejinyakulia tuzo ya msanii bora wa kike na Gabo aliyejipatia msanii bora wa kiume.

Kitendo cha Wema kushinda kiliibua hisia za wasanii wengi walioona Wema hajafanya movie nyingi mpaka kuweza kustahili kushinda tuzo hiyo na moja kati ya waaanii hao ni Irene Uwoya ambaye aliweka wazi kuwa Gabo alistahili tuzo ile lakini sio Wema.

Esha ameibuka na kumkingia kifua Wema na kusema hamna haja ya kumuonea wivu kwani wasanii walivyoambiwa wapeleke kazi zao kwa ajili ya kushindanishwa waligoma ila wachache waliopeleka kama Wema na Gabo wamefanikiwa kuibuka kidedea.

.

 

Aliyoyasema Wema Baada ya Kupokea Tuzo

Malikia wa bongo movies, Wema Sepetu juzi aliweza kupokea tuzo kwa kushinda vinyang’anyio mbalimbali huku filamu yake ya heaven sent ikiwa imemsaidia kupata tuzo hizo.

hata hivyo baada ya kupokea tuzo hiyo akiwa palple jukwaani wema alipata nafasi ya kuzungumza juu ya tuzo hiyo ndipo aliposema kuwa kuna baadhi ya kundi la watu wamekuwa wakitaka kumuangusha na kuonekana hafai bongo movies wakati amekuwa akijitahidi kufanya kazi.

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru alla’h sub’banah wata’Allah  kunifikisha hapa nilipo..najua kuna mambo mengi yamefanyika kwa ubaya ila yeye ndio amekuwa tumaini langu kubwa..namshukuru sana mama yangu mzazi na familia yangu kwa ujumla  na kusimama na mimi bega kwa bega katika kila kitu

Hata wiki moja haijapita tangu kupokea kwa tuzo hizo, baadhi ya wasanii wa bongo movies wameanza kukwaruzana na kutupiana vijembe kuwa Wema amependelewa na haikuwa haki yake.

Mwanadada Kutoka Kenya Ajitolea Kumsaidia Wema kupata Mtoto.

Ni muda mrefu sasa umepita tangu mwanadada wema sepetu akiwa analalamika na kuonyesha kiu yake ya kupata mtoto , baadhi ya watu wamekuwa wakimuonea huruma na wengine kumsema na kumtukana lakini mwanadada huyo hajawahi kuacha kuonyesha kiu yake ya kutaka kupata mtoto.

Akiongea katika chaneli ya EATV,Wema anasema “kwakweli nimekuwa nikitamani kupata mtoto hata leo kwa muda sasa tangu nikiwa na miaka 24 hadi leo nina miaka 29

Hata hivyo moja ya warembo kutoka kenya aliyekuwa akiishi dubai anaejulikana kwa jina la 2g diva, amejitolea kumsaidia wema kupata mtoto ili kuweza kutimiza ndoto zake za muda mrefu.

Katika moja ya video zilizovuja mtandaon zikimuonyesha dada huyo akiongea anasema kuwa ” wema sepetu darlin suluhisho tunalo, may be unaenda kuwa mama soon

 

 

Wema Sepetu Awagarazaga Wasanii Wenzake Wa Bongo movie

Muigizaji wa bongo movie Wema Sepetu amewagaraza vibaya wasanii wenzake wa Bongo movie baada ya kunyakua tuzo mbili katika tuzo za filamu ziitwazo Sinema Zetu Film Awards.

Wema amejinyakulia tuzo hizi kama msanii bora wa kike 2017-2018 kupitia tuzo za Sinema Zetu zilizoandaliwa na Azam TV.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema amefunguka haya kuhusiana na tuzi hizo:

 

Wema Havai Nguo za Ndani- Muna Love

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Muna Love amefungukia tuhuma ambazo zimekuwa zikimuandama kwa muda mrefu kuhusiana na urafiki wake na Wema Sepetu.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi mbali mbali kuhusu sababu za kuvunjika urafiki wa Wema Sepetu na Muna.

Kama utakumbuka miaka ya nyuma Wema alikuwa na urafiki hasa na Muna walikuwa wanaonekana pamoja kila sehemu Lakini urafiki huo ulivunjika ghafla na kila mmoja alishika njia yake na kuendelea na maisha yake.

Lakini baada ya kugombana ilisemekana kuwa Wema aligundua kuwa Muna ni mshirikina na alikuwa anamuendea kwa waganga na kibaya zaidi ilisemekana kuwa Muna alikuwa anaiba nguo za ndani Wema (chupi).

Tuhuma hizo za kuiba nguo za ndani za Wema zilisambaa sana lakini juzi Kwenye mahojiano aliyofanya na Shilawadu ya Clouds Tv, Muna alikana tuhuma hizo na kudai hawezi kuiba nguo za ndani za Wema maana mtu mwenyewe havai nguo hizo.

Ngoja niongee ukweli kwa sababu nimeokoka nguo za ndani hizo ambazo wanasema alikuwa havai inakuaje nachukua nguo za ndani ya mtu ambaye alikuwa havai”.

Kwenye mahojiano hayo Muna alikiri kuwa hana tatizo na Tunda na hakutaka kabisa kuongea sana kuhusu mzazi mwenzake Casto Dickson.

Shabiki Amuandikia Wema Barua, Amtahadharisha Kuishi Maisha Magumu Baadae.

Moja ya wadau wa sanaa na shabiki wa sanaa nchini aliejulikana kama Dr Modest  Mkali amemwamndikia wema barua ya wazi na kumwambia kuwa huu ndio wakati wake wa kutengeneza jina na maisha yake ya baadae yeye na ndugu zake hasa mama yake mzazi ambae mara nyingi wazazi ndio tegemeo lake.

Shabiki huyo amesema kuwa kuja haja gani Wema kuwa na magari ya kifahari kama hana hata kiwanja au nyumba ya kuishi,kuna faida gani kama anaweza kuanzisha kampuni kubwa iliyokuwa ikiajiri watu wengi na baadae ikafa alafu akaanza yeye kuajiriwa na watu wengine.

Shabiki huyo amemtaka Wema kuwa makini ili maisha yake yasije yakawa kama ya Kanumba ambae aliweza kutengeneza jina kubwa lakini leo hii tangu amefariki mama yake amekuwa ni mtu wa kuangaika tu na kuona picha za matangazo na kuanza kulia lia.

unanunuaaje gari la milliona 40,kama huna kiwanja au nyumba ya kuishi, unataka ustar wakati vitu muhimu katika maisha huna,timiza kwanza basic needs ndio uje kwenye luxury needs.tatizo sisi watanzania tunataka kwanza luxury ndipo tunakuja na basic sasa inakuwa tayari ni too late.matokeo yake tunajikuta tukiishi maisha mabovu kama kina flani flani, hivi inakuingia kailini kweli kwamba mtu kama wema sepetu ambae alikuwa CEO  wa endless fame leo hii anenda kuwa mfanyakazi wa wasafi alafu anaona fresh tu, kama sio kukosa malengo ni nini/

wasanii tuamke jamani, sasa hivi mamake kanumba amekuwa akina picha za mwane analia lia  tu, hakuna wa kumsaidia , angalia uisje kumtesa mama yako kipindi utakapo kufa! 

Mange: Familia Ya Diamond Imemgeuza Wema Jinga Lao

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumwagia matusi mazito msanii wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kuzua maneno maneno jana kwenye mtandao wa Instagram.

Siku ya jana Wema alishika headlines za mitandao ya kijamii baada ya kuposti posti kadhaa zilizoamsha tetesi kuwa amerudiana na Diamond na alizidi kuzua maneno baada ya kuonekana akiwa na Esma huku wakiitana wifi.

Sio siri kuwa Wema na Mange wapo kwenye bifu kali tangu Wema afanye uamuzi wa kurudi CCM mapema mwaka jana akitokea Chadema na hata kuanzisha urafiki na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam jambo ambalo halikumfurahisha Mange.

Siku ya jana Mange amemtolea povu zito Wema na kumtuhumu anatumika kuleta drama zake na Diamond ilimradi wazime amsha amsha za maandamano na kudai amegeuzwa Jinga na familia ya Diamond.

Kupitia ukurasa wake Instagram, hili ndio povu la Mange kwa Wema:

Wema mjinga sana, mtu gani kutwa anatafuta attention za watu kwa mambo ya kijinga? Forever my wii my foot mbona Bi. Tukinao alivyokuwa nao mbona hawakukuita forever my wii? Yamewashinda kwa mganda ndio wamelikumbuka jinga lao. Janamke jinga halikui from CEO wa Endless Fame to mfanyakazi wa Wasafi Tv? Seriously wenzake wanasonga mbele lenyewe linarudi nyuma. Halafu hata halijistukii linaongea proudly kabisa “Sasa Diamond anaenda kuwa bossi wangu” from kuwa CEO mpaka kuwa mfanyakazi wa Diamond kama wakina Kifesi?”.

 

“Wema na Jokate Wameungana Ili Kumshusha Alikiba”-Harmorapa

Msanii wa Bongo fleva  anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa amewatolea povu tena warembo wengine ambao ni Wema Sepetu na Jokate Mwegelo  na kudai ni wadangaji na wameungana ili kumshusha Alikiba.

Wiki iliyopita baada ya kutoa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ watu wengi walijitokeza na kumpongeza Diamond kwa hatua aliyofikia na warembo kama Wema na Jokate nao walimpongeza kitendo ambacho inaelekea hakikumfurahisha Harmorapa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa aliwatolea povu zito Wema na Jokate kwa kudai kitendo chao cha kumpongeza Diamond ni kwa nia ya kutaka kumshusha Ali Kiba:

Naona hawa wadada na wadangaji wengine wameungana ili kumshusha King Kiba. Nawachana nyie wadangaji mwenye kupewa uwezo kapewa tu nyie bora mkazane na uwezo weny mliopewa wa kudanga. Mnafikiri mkiposti kazi za Diamond ndio mnuumiza moyo KingKiba? Ndio maana mmchezewa mmeachwa Jojo umechezewa na King Kiba umeachwa kaenda kuoa mtoto chokoleti huko Moombasa eti hasira zako umezihamishia huko kwa Chibu, na liwema nalo limechezewa likaachwa nafasi ikachukuliwa na African beauty Zari aliyelishinda kila kitu kuanzia uzuri m, followers mpaka pesa eti likaanza kumtongoza king kiba ili limkomeshe Mondi, KIng nae akapita nalo akalitema likaona lirudi kumwaribia Zari ndoa yake nalenyewe limeungana kumharibia Alikiba”.

 

Chemical, Wema Ndani ya Movie Moja.

Wasanii wa tasnia ya muziki na filamu nchi kwa pamoja Wema Sepetu na Chemical wameamua kuungana na kufanya kitu cha tofauti na kukileta kwa mashabiki wao ili kuendelea kutoa burudani lakini pia kufanya baishara yao upande wa sanaa kuweza kuwalipa.

Akiongelea swala hilo , Chemical amesema kuwa yeye na Wema Sepetu watafanya kazi katika movie moja lakini sababu kubwa ni baada ya kufanya wimbo wa mary mary ndipo walipoamua kumchagua  Wema kuvaa uhusika na kuto muvi yenye  jina la wimbo huo  kwa sababu za kibiashara.

Aliipenda story na kuna watu  wa karibu yake waliongea  nae kibiashara , kwaio sio kwamba tumeangalia tu jina kubwa la msanii hapana,kwaio tuliamua kumfuata Wema Sepetu kibiashara tu.

mimi sio msanii wa bongo movie ila mimi ni msanii wa muziki kwaio mimi nimefanyatu kama by the way.

Muvi hiyo ya mary mary itakuwa ni toleo la wimbo wa Chemicaal unaoitwa Mary Mary ambao unaelezea maisha ya msichana na mapito anayopitia.Ambapo Chemical aliamua kumchagua wema kuvaa uhusika huo kwa sababu za kibiashara kama alivyosema mwenyewe.

Wema Sepetu Akiri Kuponzwa na Madawa.

Msanii wa maigizo na filamu nchini Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa ameshindwa kabisa kupunguza ukubwa wa mwili wake kwa sababu ya kutumia madawa kwa muda mrefu lakini anajitahidi kuacha madawa hayo kwa sababu anatamani kupunguza mwili wake.

Akiyaongea hayo alipokuwa anamjibu Ray C katika ukurasa wake wa instagram baada ya  Ray C kumshauri yeye pamoja na Shiloleh kujitahidi ili kupunguza miili yao kwa sababu  wanakoelekea ni kubaya wakati wana uwezo wa kupunguza miili yao kama vile yeye alivyoweza kufanya.

Kutokana na ushauri huo wa Ray C kwa Wema Sepetu ndipo Wema alipoamua kumjibu Ray C kwa kumwambia kuwa anatamani sana kukonda lakini sio yeye ni madawa ndio yanayomfanya hivyo lakini atajitahidi ili aweze kuacha.

yaani mimi sielewi jamani,, sio mimi dada yangu…..dawa zinaniponza mimi na ninaziacha.-Alijibu Wema Sepetu.

Hata hivyo comments ya Ray C haikuishia hapo kwa sababu alimwambia kuwa njia iliyo bora ni kuacha kuzitumia dawa hizo tu na kuweka mambo sawa kwa sababu endapo atafuata masharti mazuri ya kupunguza mwili atarudia hali yake ya zamani na atapata matokeo mazuri kabla ya mwaka kuisha.

Pole wangu inabidi uzikatae maana hakuna namna,inawezekana kabisa niamini mimi. a good trainer, a proper diet , less than a year utaniambia.Najua unaweza Wema Sepetu.–Aliandika Ray C