Wema Arejea Kutoka Kwenye Matibabu Nchini India

Mwana dada aliyewahi kuwa miss tanzania mwaka 2006 wema sepetu ameripotiwa kurudi kutoka india alipokwenda kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matatizo yanayomsumbua kwa muda sasa.

wema amnae aliripotiwa  wiki chache zilizopita mahakamani alipotakiwa kwenda kusikiliza kesi yake ya madawa ya kulevya ndipo mama yake aliposema kuwa mwana dada huyo alishindwa kufika kutokana na kupata safari ya ghafla  ya kwenda nje kwa matatibabu.

alipokuwa akiongea na waandishi wa habari, meneja wa Wema Martin Kadinda ansema kuwa wema amereja kutoka india lakini hawezi kuongea mambo mengi kwa sasa kutokana na kuwa bado hayupo vizuri.

wema amerejea lakini kwa sasa hawezi kuzungumza  kwenye simu,anahitaji kupumzika kwa sababu amefanyiwa upasuaji ila anaendelea vizuri.

ninachoweza kukwambia ni upasuaji mdogo na ndio maana alikwenda peke yake,ninatumia nafasi hii kuwajulisha kuwa wema anaendelea vizuri.

Amber Lulu- Aslay Ameshawahi Kufaidi Penzi La Wema Sepetu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Jini Kisirani’ Amber Lulu amefunguka na kupasua kuwa Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameshawahi kufaidi penzi la staa wa Bongo fleva Aslay.

Amber Lulu, ametoboa siri ya Wema Sepetu na Aslay kuwa wapenzi miaka ya nyuma lakini pia amedai waliwahi kuishi pamoja kinyumba kama mke na mume.

Wiki iliyopita Amber Lulu alianika hadharani kuwa yeye na Aslay walishawahi kuwa Kwenye Mahusiano pale alipoanika orodha ya wanaume ambao ameshawahi kubanjuka nao.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Amber Lulu ameweka wazi kuwa kipindi alipokuwa na Aslay alisikia pia alikuwa na Wema Sepetu aliyekuwa anaishi naye nyumba moja kitendo kilichofanya Mahusiano yao yasiwe serious:

Kipindi hiko nilikuwa undergrad nikawa nasikia Aslay alishakuwa na watu wengi nasikia alishakuwa na Wema Sepetu na wakakaa nyumba moja na wakapika na  kupakua halafu mimi kipindi hiko bado kabisa nilikuwa nanyapia nyapia”.

Amber Lulu amedai kuwa Aslay alikuwa ni fundi mzuri sana kunako mausuala ya sita kwa sita huku pia akitumia sifa hiyo kumtofautisha na Mbongo Fleva mwingini, Young D ambaye nae pia alikuwa mpenzi wake lakini hakuwa fundi sana kama ilivyo kwa Aslay.

Wema Sepetu Yupo Tayari Kushuhudia Ndoa Ya Diamond na Zari

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameshangaza watu wengi baada ya kufunguka kuwa anatamani a Ex wake Diamond Platnumz na Baby mama wake Zarinah Hassan wafunge Ndoa.

Wema alifunguka hayo baada ya video ya wimbo wa Iyena wa Diamond kutoka siku ya Ijumaa ambapo ndani yake yupo Zari kama video queen ambapo ndani ya video hiyo wanafunga ndoa.

Wema alimtaka Diamond kufanya kweli na kumuoa mama watoto wake huyo ambapo aliandika maneno haya Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli. Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri”.

Hili suala limewaacha watu vinywa wazi kidogo k sababu hasa ukiangalia kuwa Zari aliweka wazi kuwa alimtosa Diamond baada ya video kusambaa zilizomuonyesha Diamond na Wema wakikumbatiana Kwenye kumbi za starehe Miezi minne iliyopita.

Mirror- Sipo Chini Ya Wema Lakini Nampenda Sana

Staa wa Bongo fleva Mirror aliyetamba na nyimbo zake kali kama Baby na One and Only ametangaza rasmi kurudi kwenye gemu.

Mirror alijizolea umaarufu baada ya kusainiwa chini ya Endless Fame ya mwanadada wa Bongo movie Wema Sepetu.

Baada ya kimya kirefu Mirror ameifungukia Millard ayo Tv na kuweka wazi kuwa alikuwa amepata ajali kubwa ya gari lakini hivi sasa anaendelea vizuri na yupo tayari kurudi kwenye gemu.

Mirror ameweka wazi kuwa kwa hivi sasa amefanikiwa kupata management mpya ambayo ndiyo itakayohusika na kusimamia kazi zake na mara tu mwezi mtukufu utakapoisha basi staa chia Rasmi wimbo wake mpya.

Lakini pia Mirror amekana tetesi zote zilizosambaa kuwa amegombana na Wema Sepetu na Petit Man na kusema hana ugomvi na Wema na anampenda kama Mama yake na hata hivisasa akitaka ushauri kuhusu kazi zake basi anamtafuta Wema na Petit.

Mirror- Sipo Chini Ya Wema Lakini Nampenda Sana

Staa wa Bongo fleva Mirror aliyetamba na nyimbo zake kali kama Baby na One and Only ametangaza rasmi kurudi kwenye gemu.

Mirror alijizolea umaarufu baada ya kusainiwa chini ya Endless Fame ya mwanadada wa Bongo movie Wema Sepetu.

Baada ya kimya kirefu Mirror ameifungukia Millard ayo Tv na kuweka wazi kuwa alikuwa amepata ajali kubwa ya gari lakini hivi sasa anaendelea vizuri na yupo tayari kurudi kwenye gemu.

Mirror ameweka wazi kuwa kwa hivi sasa amefanikiwa kupata management mpya ambayo ndiyo itakayohusika na kusimamia kazi zake na mara tu mwezi mtukufu utakapoisha basi staa chia Rasmi wimbo wake mpya.

Lakini pia Mirror amekana tetesi zote zilizosambaa kuwa amegombana na Wema Sepetu na Petit Man na kusema hana ugomvi na Wema na anampenda kama Mama yake na hata hivisasa akitaka ushauri kuhusu kazi zake basi anamtafuta Wema na Petit.

Wema Sepetu Amesafiri Nchini India Kwa Ajili Ya Matibabu

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amedaiwa kwenda nchini India kwa matibabu baada ya kushindwa kufika mahakamani mapema leo.

Wema ambaye anakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya alitakiwa kufika mahakamani leo tarehe 29 May ili kuendelea kusikiliza kesi yake lakini hakufika.

Taarifa za kutokuwepo kwa Wema nchini zimetolewa na mama mzazi wa Wema Sepetu, Mariamu Sepetu ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba yake kwa ajili ya kutoa taarifa.

Mama Wema alitoa taarifa hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani ambapo wakili alishangazwa na taarifa hizo na kudai kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba mahakama isimamie sheria.

Baada ya kutoa maelezo hayo Mama Wema akatoa nyaraka za binti yake za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji.

Mpaka sasa haijajulikana nini zaidi Wema anaumwa au amekwenda Lini nchini India.

Esma- Wema Ndio Ana Mapenzi Ya Kweli Alimpenda Naseeb Sio Diamond

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amemwagia sifa kibao aliyekuwa wifi yake Wema Sepetu kwa kudai ndio mwanamke aliyempenda kweli Diamond.

Kama utakumbuka Wema na Diamond walikuwa wapenzi kwa muda mrefu tangu Wema alipokuwa Miss Tanzania kwa kipindi hiko Diamond alikuwa ndio anaanza muziki.

 

Esma alianza kwa kumposti  Wema na  kuanza kumsifia kuwa amependeza na mavazi yake ya kinigeria ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka posti:

Baada ya posti hiyo kuzua gumzo baada ya Esma kuendelea kuitana wifi na Wema hata baada ya Wema kuachana na kaka yake Diamond, na Esma alifunga kazi kwa kumwagia sifa Wema huku akikiri yeye ndio wifi aliyempenda kweli Diamond kwani alianza naye mapenzi wakati hana kitu mpaka leo staa.

Wema uwifi hauishi leo wee ndio forever wiii wa kihistoria mtoto wa watu unajua kuishi ulimpenda Naseeb na sio Diamond”.

 

Pamoja na kwamba Wema aliachana na Diamond muda mrefu uliopita lakini amekuwa bado karibu sana na familia yao.

Wema Augua Ghafla Mahakamani

Mwanadada wema sepetu siku ya leo alitakiwa kusimamam na kujiteta katika kizimba cha mahakama ya kisutu kuhusu ksi yake ya madawa ya kulevya mabavyo inaendelea mahakamanai hapo.wakili wa serikali ameimabia mahakama mbele ya hakimu mkazi thoams simba kuwa wema na wenzake walitakiwa kutokea mahakamani hapo siku ya leo ili kuanza kujitetea kuhusu kesi yao lakini imeshindikana kutokana na mwana dada huyo kuwa mgonjwa.

Mama mzazi wa  Wema Sepetu alifunguka na kuiambia mahakama kuwa wema sepetu alifika mahakamani hapo asubui lakini muda aliokuwa akisubiri kuingia mahakamani alianza kuumwa ghafla  kwa kujisikia vibaya na kuanza kutapika hivyo kushindwa na kuondoka.

Baada ya maelezo hayo , hakimu simba thomas alihairisha kesi hiyo mpaka May 29 na kusema kuwa washtakiwa hao wanapaswa kujianda kwa kujitetea.

Washitakiwa wengine wanaoambatana na wema ni pamoja na matilda abbas pamoja na angelina msigwa mabao walikutwa na kiwango kidogo cha madawa ya kulevya  na mengien kuyatumia.

Hii Ndio Sababu Iliyomzuia Wema Kufika Kwenye Uzinduzi Wa Filamu Ya Aunty Ezekiel

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kutaja sababu iliyomfanya mpaka asiweze kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Aunty Ezekiel.

Siku ya Jumapili Aunty Ezekiel alikuwa anafanya uzinduzi wa filamu yake fupi ya dakika 20 inayoitwa MAMA pale Kwenye ukumbi wa Cinema Mlimani City.

Wema Sepetu ambaye mwanzoni alitoa taarifa ya kuthibitisha kuwa atakuwepo eneo la tukio kumpa sapoti Aunty Ezekiel ambaye pia ni rafiki yake kipenzi kabisa hakuonekana mpaka shughuli inaisha.

Siku ya jana Wema aliweka wazi kuwa sababu kubwa iliyomfanya mpaka asihudhurie shughuli hiyo ilikuwa ni kucheleweshwa na Mama yake mzazi ambaye alikuwa naye na hivyo kujikuta kapitisha muda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wema aliandika:

I was soooo Ready for MAMA Short Film But My MAMA Took my Time aswell… Nikachelewa…???,”

Hata hivyo Aunt Ezekiel alipohojiwa na Mwananchi Digital sababu za Wema Sepetu kushindwa kufika katika uzinduzi huo alisema ni kutokana na gauni la mrembo huyo alilotakiwa kuvaa kwenye uzinduzi huo lilikuwa bado lipo kwa fundi halijamalizika kwa sababu ya kukatika kwa umeme.

Wema: Hamisa ni Mdogo Wangu Lakini Mazoea Yamezidi

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuongelea uhusiano wake na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto huku akidai kuwa ni mdogo wake ila mazoea yalizidi hivyo aliamua kumuweka kando.

Siku za nyuma Wema na Hamisa walikuwa marafiki sana kwa miaka mingi na hata ni mara nyingi Hamisa amekuwa akisikika akimuita Wema dada yake.

Lakini urafiki huo uliingia shubiti siku za nyuma baada ya Wema kutaka kumtumia watu wampe kichambo Hamisa na hata kudai sababu ya wawili hao kutofautiana ni baada ya kumsikia Hamisa akimsema maneno mabaya.

Kwenye Interview yake na Global Tv, Wema amefunguka kuwa Hamisa ni mdogo wake lakini alizidisha sana mazoea hivyo ilibidi amuweke kando ili heshima iwepo:

Mimi hamisa ni kama mdogo wangu, hivyo yaani waga nasema kila siku Lakini sometimes mazoea yakizidi sana sijui huwa inaleta mushkeri kwaiyo inabidi kila mtu abaki kwenye mipaka yake ili ajue hapa natakiwa nipitilize au hapa nisipitilize”.

Watu wengi walihusisha Wema kugombana na Hamisa na Diamond lakini Wema aliweka wazi kuwa aligombana na Hamisa kwa sababu alimsikia anamsema vibaya kwa watu.

Wema Sepetu Alamba Shavu Nono Na Tatu Mzuka

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameendelea kuwa na mwezi mzuri kwani siku chache baada ya kupata ubalozi wa Kombe la Dunia na Star Times siku ya jana Wema alilamba dili nono na Tatu Mzuka.

Siku ya jana Kampuni ya The Network ambayo inahusika na kuendesha Michezo ya namba ya Tatu mzuka, imetangaza kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na Wema.

Akizungumza Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatu Mzima Sebastian Maganga, alisema ushirikiano wao na Wema ni mpango mkakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania ili kuboresha maisha yao.

Kusudi kubwa la Tatu Mzuka kuingia makubaliano na Wema, ina lengo la kutaka kusambaza fursa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo ili kuboresha maisha yao ya kila siku”.

Lakini pia Wema aliyepata shavu hilo alifunguka na kusema:

Nina hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha bidhaa hii mashabiki zangu wote na Watanzania kwa ujumla wao ili waweze kujitengenezea fursa nyingi za kuboresha maisha yao  kupitia kwangu.

Baada ya Heaven Sent, Wema Awaanda Washabiki wake kwa Kikubwa Zaidi.

Mwanadada Wema Sepetu amewataka mahabiki zake kukaa mkao wa kula kwa kazi kubwa na nzuri zaidi kwa sababu baada ya Heaven sent ambayo imeshinda tuzo mbili na kumletea heshima anawahaidi watu kuwa kazi itakayo kuja itakuwa kubwa zaidi kwa sababu sasa hivi yeye na team yake wanapika vitu vizuri.

Wema Sepetu aliandika”heaven sent imekuja na imeshinda tuzo, so it agood thing,tutegemee vitu vikubwa zaidi kama nilivyosema hapo awali kuwa kuna kitu kinatoka hapo june , naomba tukae mkao wa kula nadhani kitabadilisha taswira ya tasnia ya filamu nchini, kuna project za kutikia mji.

Baada ya wema kushinda tuzo hizo imekuwa kama njia ya kumfungulia mafanikio kwa sababu amepata madili mengi katika makampuni mbalimbali .

Ommy Dimpoz- Sijawahi Ku-date na Wema ile Ilikuwa ni Kiki Tu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Omari Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi hata siku moja kutoka kimapenzi na Wema Sepetu.

Kipindi cha nyuma ilishawahi kusemekana Kuwa Ommy Dimpoz na Wema Sepetu walikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi hasa baada ya picha zao kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Tetesi za Ommy dimpoz na Wema kuwa kwenye mahusiano zilizidi pale ambapo alionekana na Wema Kwenye chumba wakiwa wamelala ambapo baadae ilikuwa kujulikana walikuwa location kwa ajili ya kushoot wimbo wa Wanjera ambao Wema alikuwa ni video queen.

Lakini Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Ommy Dimpoz amethibitisha kuwa zile zilikuwa ni kiki tu kwa ajili ya project zao.

No, Sijawahi ku-date na msichana yeyote maarufu hapa Bongo, sijawahi.“

Lakini pia Ommy Dimpoz amesisitiza kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na msichana yoyote ambaye ni staa kwa Bongo.

Hivi sasa Ommy Dimpoz anafanya vizuri sana na wimbo wake wa Yanje aliomshirikisha Msanii Seyi Shay kutoka Nigeria, wimbo inaoshikilia nafasi ya kwanza Kwenye mtandao wa Youtube.

 

Wema Amtumia Salamu Hajis Manara

Msanii Wema Sepetu, ametuma salamu kwa mkuu wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Manara, na kutamba kwa kusema, klabu ya Yanga ndio timu kubwa na yenye mafanikio hapa nchini na kitendo cha kufungwa na Simba katika mchezo wa April 29 ni sehemu ya mchezo tu.

Akiongea na waandishi wa habari leo Mei 02 wakati wa kutambulishwa kama balozi wa Startimes kueleka kombe la dunia, Wema amesema yeye ni mpenzi mkubwa wa timu Yanga na hata katika kuchukua ubingwa timu hiyo imefanikiwa zaidi kuliko wapizani wao simba.

Mpelekeeni salamu Haji Manara, anajua kabisa kwamba Yanga tumechukua ligi (kuu bara) mara nyingi sana, kwa hiyo wao (Simba) kutufunga juzi ni changamoto, katika ubingwa huwa tunawachapa kilasiku”, amesema Wema

Haji Manara na msanii Wema Sepetu wamekua na tambo za maneno kuhusu timu za Simba Yanga hususani katika mitandao ya kijamii.

Akiongelea kuhusu nchi wakilishi wa bara la Afrika katika michuano ya kombe la dunia Wema amesema, bado kuna changamoto kubwa kwa nchi hizo kufanya vizuri katika michuano hiyo ukilinganisha na mataifa ya bara la Ulaya.

Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Kipindi Chake Wasafi Tv

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuelezea mipango yake  aliyonayo kuhsu  kipindi chake  kinachotarajiwa kurushiana ndani ya Wasafi Tv.

Kama utakumbuka siku za nyuma kidogo Wema aliweka wazi kuwa hana Mahusiano ya kimapenzi na Diamond bali atakuwa na uhusiano wa kikazi naye kwani atakuwa bosi wake.

Wema alitangaza kuwa atakuwa na kipindi ndani ya Wasafi Tv ambayo imeanza kurushiana matangazo yake wiki chache zilizopita.

Wema amefunguka hayo kwenye press conference aliyofanya jana na kuweka wazi kitakuwa ni kipindi cha kawaida na sio reality show kama ilivyokuwa mwanzoni kwenye EATV.

Kitakuwa ni kipindi cha tofauti tutakuwa wanadada watatu. Sitapenda kuweka wazi zaidi lakini haitakuwa reality show, kama itakuwa ni reality show nitaweka kwenye App yangu.

Bado hatujaanza ku-shoot kwa sababu sasa hivi bado wanafanya majaribio, kwa hiyo ile process nzima ya vipindi bado haijanza, so content zipo pale pale na tutaanza ku-shoot hivi karibuni”.

 

Faiza Ally Amchekelea Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Faiza Ally ameshindwa kuzuia hisia zake na kuchekelea baada ya Wema kupata ubalozi wa Star Times siku ya jana.

Siku ambayo Zari alikuja Tanzania baada ya kupata ubalozi wa bidhaa mbili tofauti Faiza alitoa povu zito na kulalamika makampuni hayo kwa nini yametoa nafasi hiyo kwa mtu ambaye sio Mtanzania.

Faiza Ally alilalamika kwa nini wanatoa ubalozi kwa mtu ambaye ni Mganda halafu wanaacha mastaa kibao ambao ni Watanzania ambao wanaweza kabisa kufanya jukumu hilo.

Siku ya jana Wema Sepetu na wasanii wenzake kadhaa wamelamba dili nono kutoka Kwenye kampuni ya Star Times na kwa kuwa mabalozi wao wote waliowachagua ni Watanzania Faiza amechekelea uchaguzi wa Wema Sepetu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza amemuandikia ujumbe huu Wema wa kumpongeza: