Harmorapa afungua roho na kusema anataka kumoa Wema Sepetu

Wema Sepetu anatajika kwa kupenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mstaa; aliwai kuwa na uhusia na Ali Kiba, Diamond and Idris Sultan.

Kwa sasa Wema hana mshikaji yeyote na hii ndio sababu ya Harmorapa kujitokeza na kusema kwamba angependa kumoa Wema.

Harmorapa

Msanii huyu amefungua roho na kusema kama angekubaliwa na Wema basi atatangaza ndoa mara moja.

“Napenda kusema ukweli ulio jificha moyoni mwangu tangu siku nyingi kutokana na jinsi ninavyo sumbuliwa na hisia za kimapenzi kwa mrembo @WEMASEPETU,tangu naanza kumfaham wema sepetu na kumwona kweny tv akigombea umiss tz mwaka 2006 nilitokea kumpenda sana na kupata hisia za kumwoa endapo ntampata basi tu ndo vile nilikua sina uwezo wa kuonana nae wala kukutana nae kwa sababu ya position nilio kua nayo enzi hizo nauza pochi mwenge?nakumbuka kipind kile #WEMASEPETU wamemkata kweny uchaguz wa wabunge wa viti maalum niliumia sana,hadi skupatwa na usingiz nakumbuka niliamka saa 9 za usiku gheto na kuelekea mwenge kulangua mikoba kwa sababu ya kuiuza kipindi npo maeneo ya mwenge rafiki yangu alie kua na smart na alikua akifaham ni kiasigani namkubari #wemasepetunga alinipa taarifa kua #sepetunga anaingia dar kutokea dodoma baada ya jina lake kukatwa Ukwel nilisema lazima nikampokee na dhawadi nimpatie, bas nikaingia zangu kurangua mikoba nilibahatika kupata mkoba mmoja mzuri sana Akili ikanijia kua ule mkoba nmpe dhawad #kiumizaRohoYangu sikuuza nikauhifadh baadae nikafunga gori langu mapema nikaelekea kumpokea #kiumizaRohoYangu baada ya madam kufika niliangaika sana ili nimpatie ile dhawad ya mkoba bahati mbaya niligongwa na bodaboda kweny mguu wa kushoto na skufanyikiwa kumpa ila hadi leo ule mkoba nnao endapo siku nikipata fursa ya kukutana nae ntampatia huo mkoba.

“Ila nachukizwa sana na vijana walio uchezea moyo wa #sepetunga wakina #Mrblue, #diamond,#idrisa na wengineo nawachukia sana kwa kuufanya moyo wa @WEMASEPETU kama danadana na kuwalaum juu.

“Pia nawaonya wale wote mnao mlinganisha #Zarithebosslady na #WEMASEPETU mnakosea sana wema sepetu n mzuri mno kuliko #zarithebosslady sio kwamba #Mamatee n mbaya hapana mamatee ni mzuri ila hajamfikia #wemasepetu.

“Yote ya yote naombeni mumfikishie Taarifa hizi #WEMASEPETU Mwambieni nampenda sana endapo nikampata hato chukua hata wiki kwangu ntamvisha pete na kufunga ndoa nae juu na kumtunza kwa hali yoyote ile,” Harmorapa aliandika.

 

Picha Hizi ni Ishara tosha kuwa Wema Sepetu ni Binti Mrembo Zaidi Tanzania

Ingawa ni mwanamke ambaye amekuwa na scandals mingi, ni kweli kuwa Wema Sepetu ni binti ambaye ameumbwa kama malkia na ambaye anatambulika Afrika Mashariki na wengi.

Alipoanza career yake kama model sio wengi walidhania kwamba binti huyu angeleta mabadiliko mengi katika burudani ya Bongo. Wema Sepetu si model tu bali mwigizaji na kwa hivi mwanasiasa.

Hata hivyo, yeye ni fashion killa na mwanamke ambaye anajitambua. Akitembea mitaani watu wengi huduwaa kutokana na urembo alionao.

Nimeweza kupata picha kadhaa kama mfano kuonyesha mbona Binti huyu anaurembo watu wengi hutamani. Ingawa hukubaliani na mimi, pia ni sawa kila mtu ana maoni yake. Tazama picha hizi hapa.

 

Mama Wema Sepetu kudaiwa kuleta masaibu mengi katika ndoa ya Msama

DAR ES SALAAM: Hatari! Mama mzazi wa muigizaji mkubwa wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, Miriam Sepetu anadaiwa kuitikisa ndoa ya mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Msama, Risasi Mchanganyiko limepewa mchongo mzima.

ANA KWA ANA NA CHANZO Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na ishu hiyo, mtikisiko huo mkubwa ulitokea ndani ya familia ya muandaaji huyo wa matamasha ya Injili baada ya mkewe kukuta ujumbe mfupi wa maneno katika simu ya mumewe, hivyo kusababisha mtafaruku.

“Sijui hasa nini kilitokea, lakini nilicho na uhakika nacho ni kuwa ndoa ya wawili hao ilikuwa katika majaribu makubwa wakati huo, maana kulionekana kuwepo kwa mawasiliano ya mara kwa mara baina ya Msama na Mama Wema, kitu ambacho mkewe alishindwa kuelewa. “Msama alijitahidi sana kupooza mambo kwa kujaribu kumuweka sawa mkewe, lakini bado ikawa ngumu hadi baadhi ya marafiki wa karibu wa pande

WAANDISHI WETU, RISASI zote mbili walipoingilia kati na kuliweka sawa jambo hilo na hivyo kupoa,” kilisema chanzo hicho. Chanzo hicho kilisema wakati mmoja katika mtafaruku huo, wanandoa hao walikuwa hawazungumzi, kitu ambacho kilitishia sana uhai wa ndoa hiyo. Baada ya kupata taarifa hizo, Risasi Mchanganyiko lilifanya juhudi kubwa za kuwatafuta wawili hao, likifika ofisini na nyumbani kwa nyakati tofauti lakini mara zote likiambulia patupu. Hata hivyo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Msama alipatikana kupitia simu yake ya mkononi.

HUYU HAPA ALEX MSAMA

“Ni kweli, ndoa yangu ilipata mtikisiko mkubwa sana kwa sababu ya Mama Wema, mke wangu alikuta mawasiliano baina yangu na yule mama kwenye simu, akaja juu. Alikuwa akiniuliza huyu ni nani na kwa nini nawasiliana naye mara kwa mara.

“Nilikuwa nawasiliana naye mara kwa mara kwa sababu nilikuwa na biashara naye. Unajua kuna kipindi nilitaka kununua nyumba yake, nikawa wakati mwingine ninampa hela kidogokidogo, sasa katika biashara kubwa kama ile ni lazima mtakuwa mnawasiliana mara kwa mara.

“Mke wangu alipokuwa anaona meseji nyingi kutoka kwake, akawa anahisi kuna kitu, lakini nilijitahidi kumweleza kuwa ni kwa sababu ya biashara tu, hatimaye alinielewa, mambo yakaisha na sasa kila kitu kiko vizuri,” alisema Msama. Mke wa Msama ni mtangazaji wa kituo kimoja cha Redio, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam.

VIPI KUHUSU PESA ZAKE?

Risasi Mchanganyiko lilimuuliza Msama hatima ya fedha zake za maudhiano ya nyumba ambazo hivi karibuni alilazimika kutumia Polisi ili kumkamata, baada ya kudai kuwa mama huyo alichukua fedha, lakini badala yake akamuuzia mtu mwingine.

“Hapa ni lazima niwe mkweli, siwezi kukubali huyu mama achukue tu fedha zangu kirahisi atoweke, ninasikia faili lake tayari limeshafika kwa Mwendesha Mashtaka wa serikali, ninachotaka mimi ni vyombo vya sheria kufanya kazi yake ili haki itendeke.

“Sitakubali mazungumzo, maana watu kama hawa wapo wengi sana hapa mjini, wanafanya mambo makusudi, wakitegemea huruma, siwezi kuwa na huruma na mtu ambaye anadhani udanganyifu ni jambo zuri, suala hilo ninataka limalizike mahakamani,” alisema Msama ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Habari ya Msama Media Group.

MSAKO WA MAMA WEMA

Mbio za kumsaka Mama Wema zilishika kasi na kulifikisha Risasi Mchanganyiko hadi nyumbani kwake, Sinza Mori, lakini msichana aliyefungua mlango alisema mwanamama huyo, aliyegonga vichwa vya habari wiki chache zilizopita kufuatia sakata lake na Steve Nyerere, hakuhitaji kuonana na mtu yeyote kwa wakati huo.

Kuona hivyo, waandishi wetu walimtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya mkononi, lakini licha ya kuonyesha kuwa ujumbe huo ulifika na kusomwa, hakurudisha majibu.

TUJIKUMBUSHE

Alex Msama na Miriam Sepetu wamejikuta wakiingia katika mtafaruku baada ya kushindwa kuelewana katika suala lao la mauziano ya nyumba ya mama huyo iliyopo Sinza Lion.

Taarifa za awali zilizoandikwa na gazeti hili, zilisema mama huyo alitaka kuiuza nyumba hiyo kwa Msama, lakini mfanyabiashara huyo alichelewesha malipo na kumfanya aiuze kwa mtu mwingine. Hadi anafikia uamuzi wa kufanya biashara na mtu mwingine, inadaiwa kuwa tayari alikuwa ameshachukua kiasi cha shilingi milioni 16 kutoka kwa Msama.

Moja kwa moja kutoka Risasi mchanganyiko

Huu ndio ujumbe mirror aliutoa kwa Wema Sepetu baada ripoti kutokea kwamba Wema alimtenga alipopata ajali

Leo katika show ya U heard ya clouds FM, Saudi Brown alibahatika kuongea na mirror ambaye anaendelea kupona kutokana na ajali aliyoipata ya gari.

Mirror anayedaiwa kutelekezwa na Management yake wakati anajiuguza hadi kupona kutokana na kupata ajali ya gari na alizungumzia hiyo ishu mara ya kwanza.

wema sepetu

“Hamna, mimi sina matatizo na mtu, Madam sina tatizo naye hakuwahi kuja kunitembelea nyumbani sijajua labda yupo busy na kazi zake ila sina tatizo naye japo kuna wasanii kibao wamekuja kunitembelea. Watu wengi sana, ila sina noma na mtu yoyote” – Mirror.

Wema Sepetu amsifu Martin Kadinda katika ujumbe alioamwandikia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa

Aliyekuwa manager wa Wema Sepetu, Martin Kadinda hivi leo amesherekea siku yake ya kuzaliwa na kama kawaida marafiki wake wa dhati wamekuwa wakimpost kwenye Instagram huku wakimsherekea leo.

Wema Sepetu ni mmoja wa marafiki waliompost Martin Kadinda. Katika ujumbe wake, Wema Sepetu alimsifu Martin na kumfungulia roho katika ujumbe wake uliowaacha mashabiki na tabasamu. Aliandika kusema,

Wema sepetu akiwa na Martin Kadinda

The World Knows How I feel about You… I have nothing more to add to dat… I love you more everyday than yesterday… (Mi nakupenda Leo kuliko Jana, ?) Happy Birthday wa kwangu mimi apa…. Wa Sunny, Wa Sunshine, Kaka manager wa kwanza kabisa duniani… Yaani hapa natafuta maneno mapya mapya ambayo sijawahi kukwambia ila najikuta nakosa maana yote nishamalizaga… Basi wacha niache kutype….

Wawili hawa wamekuwa marafiki kwa miaka mingi na ata baada ya Martin kuanza biashara zake, bado wako pamoja kama ndugu na dada.

Kimeumana! Wema Sepetu amkana rafiki wake wa dhati Zena Abdallah

Wema Sepetu na rafiki wake wa karibu Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ sasa hawana uhusiano mwema baina yao tena. Hii ilibainika baada ya mdau mmoja kuweka picha ya Jike Shupa wakiwa pamoja na Wema na kusema ni marafiki.

Wema alijibu kwa upesi na kumkana Jike Shupa hadharani kwamba siyo rafiki yake.

“Wema kafuta urafiki na James Delicious sasa hivi kaunda urafiki na msagaji Jike Shupa, dada una marafiki wabovu hawaendani na hadhi yako, angalia wewe…,” aliandika mdau huyo.

Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ na Wema Sepetu

 

Risasi Jumamosi inaeleza kwamba uhusiana baina ya Wema na Jike Shupa uligonga mwamba kutokana na watu kuzungumza mengi kuhusu Jike Shupa huku wakimkataza Wema kuendelea kuwa na ukaribu naye kwa kile wanachodai kwamba tabia zake siyo nzuri.

“Watu wamekuwa wakimpigia Wema kelele za kuacha ushosti na Jike Shupa kwa sababu ya tabia zake maana kila mara amekuwa akionekana akifanya vitendo vya ajabu hadharani kama kunyonyana ndimi na wanaume tofautitofauti, kubadili wapenzi kila kukicha huku akihusishwa pia na usagaji,” Risasi Jumamosi iliripoti.

 

“Mkome kunihusisha na watu wasio jua kitu chochote kuhusu maisha yangu” Wema Sepetu awaonya mashabiki

Mrembo Wema Sepetu ambaye sasa ameingia kwenye siasa hici juzi aliwaonya mashabbiki ambao wamekuwa wakimhusisha na mambo yasiyo na mbele au nyuma.

Kupitia mtandao was Instagram Wema Sepetu aliandika ujumbe mrefu huku akiwaomba mashibiki wakome kumfikiria kuwa yeye anamahusiano na Kibabude. Wawili hawa walikuwa wanashukiwa kuwa wanamahusiano baada ya kuonekana wakiwa pamoja mara kadhaa.

Wema aliandika kusema…

They Say Silence is The Best Weapon but sometimes Silence can mislead you…. Just sometimes though…. Anyways, Y’all better stop involving me with people who dont know a pinch abt my life… Im a People’s person, Talking to everyone & laughing with everyone is what I do… Mwisho wa siku hakuna binadamu aliekamilika chini ya jua… Y’all know Im a sweetheart like that… So lets nat misunderstand one another…. I hope we are Clear…. If there is anything anyone would like to ask then Download my app and subscribe…. I just cant wait for iOs users to join our Family…. There’s gon be sooo much FUN….!!!

Kibabude ata yeye amekana kuwa mpenzi wa Wema na akaelezea kuwa kwa hivi sasa amerudiana na mama watoto wako. Kwa hivyo kwa sasa hataki drama mitandaoni itakayo vunja familia yake.

Mwendesha mashtaka akaribia kukamilisha uchunguzi wa kesi ya Wema Sepetu kuhusu biashara ya mihadarati

Upelelezi wa kesi ya Wema Sepetu kupatikana na bangi unakaribia kukamilika. Msanii huyu maarufu wa filamu za Bongo alikamatwa na polisi mapema Februari baada ya kupatikana na misokoto ya bangi nyumbani kwake.

Wema Sepetu aliachiliwa kwa dhamana Februari 6 baada ya kuzuiliwa jela kwa muda wa siku sita. Kesi yake ilitajwa mahakamani lakini mwendesha mashtaka aliomba mahakama impe muda kukamilisha upelelezi.

Wakili wa serikali Constantine Kakula alieleza mahakama (Jumatano) kwamba upande wa mashtaka ulikua katika hatua za mwisho kukamilika upelelezi wao.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, hakimu wa mahakama ya Kisutu aliuhimiza upande wa mashtaka wajitahidi kuukamilisha upelelezi, kesi hio imeahirishwa hadi Aprili 11, 2017.

Wema Sepetu na meneja wake Martin Kandinda wakitoka mahakamani