Hatimaye Diamond Amuweka Mtoto Wake na Hamisa Mtandaoni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz anayefanya vizuri na kibao chake cha kwangwaru ametengeneza gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha ya mtoto wake na Hamisa.

Hatimaye kwa mara ya kwanza Diamond ameposti picha ya kwanza ya mtoto wake Dylan ambaye amezaa na Hamisa.

Tangu Dylan azaliwe kulikuwa na mgogoro kati ya Diamond na Hamisa hii ilitokana na Hamisa kuanika video na picha zao za faragha Wakati huo Diamond alikuwepo na Ex wake Zari.

Tangu hapo kilichofuata kilikuwa ni kurushiana vijembe Mtandaoni na kupelekana mahakamani na hata Hamisa alisema kuwa Diamond alikuwa hataki kumuona mwanaye na hata kumuhudumia.

Lakini tangu taarifa za Diamond na Hamisa kurudiana zienee inaelekea mambo yamekuwa tofauti kwani Diamond amesemekana hata kumuona mtoto wake na hata jana kwa mara ya kwanza aliweza kumposti mtoto wake Kwenye ukurasa wake wa Snapchat:

 

Video za Mahaba Kati ya Diamond na Hamisa Zazua Gumzo (video)

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na amerudi upyaa Kwenye headlines baada ya video zake za mahaba na Baby mama wake msanii Hamisa Mobetto kusambaa mtandaoni siku ya jana.

Wawioi hao wamesha wazi kuwa maarui siku za nyuma baada ya Hamisa kusambaza picha zao wakiwa pamoja baada ya Diamond kukataa kuwa hajazaa naye lakini baadae walimaliza tofauti zao mahakamani.

Lakini jana Diamond na Hamisa wameonekana pamoja katika chumba kimoja huku wakikumbatiana na kushikana kitendo kilichoibua maswali mengi kwani kiukweli haijajulikana kama wapo pamoja au ni kiki.

Hizi ni baadhi tu ya video zinazowaonyesha wakiwa pamoja:

 

 

“Unajiona Mzuri na Mdogo Lakini Huwezi Kupata Mwanaume Wako” Zari Amrushia Hamisa Dongo

Mfanyabiashara na mzazi mwenza wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ amerudi tena kwenye headlines baada ya kumua kufumua bifu lake na baby mama mwingine wa Diamond, Hamisa Mobetto.

Inaelekea bifu la wazazi wenza wa Diamond  limerudi upyaaa kwani Zari kaamua kulianzisha tena baada ya kimya kirefu juu ya suala hilo na tofauti tulivyodhani kuwa huenda wamemaliza tofauti zao kama ambavyo Diamond na Hamisa walivyomaliza mahakamani.

Siku ya jana Zari kutumia mtandao wa SnapChat alimrushia Hamisa madongo upya kama ilivyokuwa siku za nyuma ambapo ameongelea kuhusu suala la Hamisa kuzaa na Diamond na pia taarifa za Hamisa kuchumbiwa na Diamond.

Siku za nyumba Hamisa ameshawahi kudokeza kuwa aliwahi kuchumbiwa au kuvalishwa Pete ya uchumba na Diamond na hata kuna taarifa zilienea kuwa huenda Diamond na Hamisa walifunga ndoa habari ambazo hazijawahi kuthibitishwa.

Mzuri, Mdogo lakini pamoja na hayo yote huwezi kupata mwanaume wa peke yako…..Eti amekuvalisha pete ya uchumba lakini hajawahi kukubali wala kukukubali hadharani! Dada jiangalie sana ….Anafanya Interview redioni eti mwenye mimba atoke blah blah”.

 

Lakini ni pia Zari ametangaza ujio wa kipindi chake kitakachoonyesha maisha yake halisia (reality show)  kitakachoitwa Life of Zarithebosslady ambacho mashabiki wake watapata kuona kila kitu kuhusu maisha yake.

 

Angalia Picha Mpya za Mtoto wa Diamond na Hamisa

Miezi michache iliyopita Diamond na mzazi mwenzake Hamisa hawakuwa kwenye sehemu nzuri kiuhusiano walikuwa kwenye bonge la bifu huku Hamisa akidai Diamond anagoma kumuhudumia mtoto wake.

Ugomvi wao Ulianzia pale Hamisa alipoweka hadharani picha zao za chumbani na kisha kuuambia ulimwengu mzima kuwa alikuwa ana uhusiano wa kimapenzi na Diamond na amezaa naye kitu kilichomfanya Diamond afanye Interview na Clouds na kukiri kuzaa na Hamisa.

Tangu hapo wawili hao walikuwa maadui wanarushiana maneno mtandaoni na Diamond kugoma kumlea mtoto wake lakini wiki chache wawili hao walimaliza tofauti zao mahakamani na kusameheana na kudai wamerudi kama familia kwa ajili ya kumlea mtoto wao.

Siku ya jana pia Hamisa aliweka picha za mtoto wao mtandaoni na Diamond alionyesha ushirikiano na kurepost, Hizi ni baadhi ya picha za mtoto wao anayejulikana kama Daylan:

 

 

 

 

Hamisa Mobetto: Nimefurahia Maamuzi ya Mahakama

Siku ya jana supastaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mzazi mwenzake mwanamitindo Hamisa Mobetto walifika tena mahakama ya Kisutu kwa ajili ya muendelezo wa kesi iliyofunguliwa iliyofunguliwa na Hamisa dhidi ya Diamond.

Walifika mahakamani hapo kwa ajili ya kuweka rekodi ili mahakama na ustawi wa jamii waweze iwe na kumbukumbu ya usuluhishi wao mara ya mwisho na ahadi zao walizowekeana.

Baada ya kutoka mahakamani msanii Diamond alifunguka na kuongea na waandishi wa habari na alifunguka yafuatayo:

Labda tu cha kuzungumza kama nilivyosema mara ya mwisho tuliitwa kwa ajili ya usuluhishi na wala sio kesi ilikuwa tunaangalia ni kwa namna gani tutamlea mtoto vizuri tukalifanya hilo likakaa sawa kwaiyo leo tulikuwa tunaweka rekodi ili hapa ustawi na mahakama wawe na kumbukumbu sahihi ili kesho na keshokutwa kisije kikazungumzwa kitu kingine cha uongo lakini mwisho wa siku tumlee mtoto wetu akue maana anaweza akaja akawa kiongozi mkubwa hapa nchini”.

Lakini pia Hamisa aliongea na Millard Ayo Tv ambapo aligunguka na kusema amefurahishwa na maamuzi ya mahakama:

Kwa kweli maamuzi ya mahakama nimeyafurahia kwa sababu ni maamuzi ambayo pande zote mbili tulijadiliana na tukakibaliana nayo nashukuru tu kila mtu ameridhika na maamuzi hayo na yamekwisha”.

Baada ya kumaliza kesi hii Diamond na Hamisa wamekiri kumaliza maneno yao ya mitandaoni na kujikita katika kumlea mtoto wao, Tuwatakie kila la kheri.

Diamond na Hamisa Warudi Mahakamani Tena Leo

                                         

                               Diamond akiwa anaingia mahakamani mapema leo.

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini na boss wa kundi la WCB, Diamond Platinumz ameonekana leo tena mahakamni na mzazi mwenzie Hamisa Mobeto. Ambapo wiki iliyopita walikuwa  mahakamni hapo kwa ajili ya usuhuishi wa kesi yao ya matunzo ya mtoto wao.

Hata hivyo wiki iliyopita wawili hao baada ya kutoka mahakamani walikiri na kusema kuwa kesi hiyo imeenda poa na walishakubaliana kumlea mtoto huyo kwa pamoja na kwa kushirikiana hivyo hakuna tena malumbano ya malezi kati yao kuhusu  mtoto wao.

Diamond na Hamisa waliponekana leo mahakamani , taarifa zinasema kuwa waliamua kuja mahakamni hapo kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya makubaliano na usuluhishi wao ili baadae isije kusumbua au kuonekana kuwa ni waongo.

Diamond alisema kuwa  mara ya mwisho kukutana haikuwa kesi bali ilikuwa ni kufanya usuluhishi ambapo leo tumekuja kuweka rekodi ya makubaliano hayo ili yasije yakazushwa mengine ya uongo na kweli.

Wawili hao walifikia hatua ya kupelekana mahakamani baada ya msanii huyo kutokuwa na maelewana na hamisa ambae ameweza kupata nae mtoto mmoja wa kiume  na kushindwa kuwa anatoa ela ya matumizi kwa ajili ya mtoto wake.

Hamisa Mobetto Azidi ‘Kuwaka’, Angalia Picha Zilizoibua Tetesi za Hamisa na Diamond Kurudiana

Mwanamitindo, muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amezidi kukamata headlines huko kwenye mitandao ya kijamii.

Hamisa amezidi kupendeza na kuwa mcharo wa hali ya juu hii inatokana na kuanza kupata kazi ndani na nje ya nchi ambazo zinamuingizia kipato fulani na inaonekana kabisa maisha yake yamebadilika.

Baada ya tetesi kusambaa kuwa Hamisa ameshinda kesi yake mahakamani dhidi ya Diamond wiki iliyopita ambapo inadaiwa kuwa mahakama ilimuamuru Diamond kutoa pesa ya matumizi kwa ajili ya malezi ya mtoto wao.

Baada ya kesi hiyo kuisha na Diamond kuthibitisha kuwa wamepatanishwa na hivi sasa hawana ugomvi wowote, tetesi zilianza kutembea kuwa Hamisa na Diamond wamerudiana ndio maaana wamemaliza zile tofauti zao mahakamani fastaa na ndio maana Diamond kakubali kutoa pesa kirahisi.

Siku ya jana tetesi za Hamisa kurudiana na Diamond zilizopita kupamba moto mtandaoni baada ya kusambaa kwa picha na video zilizomuonyesha mpiga picha wa Diamond anayeitwa Lukamba ambaye amekuwa ni mpiga picha ambaye ana mpiga picha Diamond na timu nzima ya Wasafi lakini pia amekuwa akimpiga picha Zari na hata akienda South Africa amekuwa akifikia nyumbani kwa Zari.

 

Hiyo picha hapo juu inamuonesha photographer Lukamba ambaye ni mpiga picha wa Diamond akiwa na Hamisa huku tetesi zikisambaa kuwa alitumwa na Diamond akampige picha lakini Lukamba kwa chini akiwa kwenye picha ya pamoja na Zari.

Hamisa Mobetto Amefunguka Haya Baada ya Kusuluhishwa na Diamond

Msanii na mwanamitindo maarufu Hamisa Mobetto amefunguka baada ya kusuluhishwa na mzazi mwenzake supastaa wa Bongo fleva Diamond Platnumz mahakamani siku ya jana.

Baada ya vita ya mitandaoni kuendelea kwa miezi kadhaa tangu mtoto wao azaliwe pande zote za familia zao zimekuwa zikionyesha kukwaruzana huku Diamond na Hamisa kuonyesha kutoelewana kuhusu mambo yao mbali mbali.

Siku ya jana Hamisa na Diamond wote walifika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwenye mahakama ya watoto ambapo waliitwa ili kumalizia kesi hiyo Hamisa na Diamond wote waliongelea kuhusu kusuluhishwa na kupatana kwao.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv, Hamisa alifunguka yafuatayo;

Leo sana sana kulikuwa kuna kama suluhisho na mwisho wa kesi na kila kitu that’s why ilibidi wazazi wote wawili ilibidi tuwepo na tuonekane tupo pale na kuyamaliza, ilikuwa ni kuhusu kumuhudumia mtoto na vitu vingine kwaiyo tumeshakubaliana kuwa atamhudumia mtoto wake na hivyo yaani.

Kama ilivyokuwa kwa watu wengi kila mtu alikuwa anataka kujua endapo Hamisa kapata kiasi alichokuwa anataka kwa mwezi milioni 10, Hamisa alisema haya:

Hayo ni mambo ya kifamilia siwezi kusema ila hata kama ikiwa milioni mia ni sawa tu kama mzazi ana uwezo sawa tu haina tatizo kwa sababu mwisho wa siku inategemeana na uwezo wa mzazi ila kiasi cha pesa tulichokubaliana siwezi kukisema kwani sitakiwi kukitaja kwa sababu ni mambo ya kifamilia zaidi.

Unajua kwenye familia kuna pande mbili upande wa mama na upande wa baba hawa watu kwa kujua au kutokujua hawakuwepo pale wakati mtoto anatengenezwa au hawajui njia gani aliyotengenezwa  but kila mtu anakuwa na la kusema mwishowe inasababisha makelele ila nashukuru yameisha hakuna mzazi anayependa mtoto wake kusemwa vibaya”.

Hamisa amehitimisha kwa kusema hana ugomvi na Diamond na ana imani huu utakuwa mwanzo mzuri wa kuendelea kumlea mtoto wao lakini pia amesisitiza kuwa hana mpango wa kuolewa kwa sasa kwani haamini masuala ya ndoa na ndio maana amezaa nje ya ndoa.

“Mimi Sina Tatizo na Hamisa” Amefunguka Diamond Baada ya Mahakama Kuwasuluhisha

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya uhusiano wake na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto baada ya kumaliza tofauti zao mahakamani jana na Diamond kudai hana tatizo na Hamisa.

Siku ya jana tarehe 8 mwezi wa 2 Diamond na Hamisa walifika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa ajili ya kusikiliza shauri la malezi ya mtoto wao anayejulikana kama Abdul Naseeb au Dylan.

Tangu mtoto huyu azaliwe kumekuwa na maneno mengi na tuhuma mbali mbali zikirushwa kwa pande zote mbili yaani upande wa baba na Mama huku kila mmoja akimlaumu mwenzake kuhusu malezi ya mtoto wao.

Baada ya kutoka mahakamani Diamond aliongelea kesi yao ilivyoenda na kuonyesha kufurahishwa na matokeo ya kesi hiyo ambapo kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv alifunguka yafuatayo:

Kila kitu kimeenda vizuri kwani tulichokuwa tunafanya ni kuwekana sawa ili kila mmoja ajue majukumu yake mimi kama Baba nijue nafanyaje na yeye kama mama hivyo hivyo, Alafu ile haikuwa ni kesi ndio maana unaona hatukuenda hata kizimbani tulikaa tu chini tukazungumza na kila mtu azungumze anataka nini yote ili tujue tunamleaje mtoto wetu katika malezi yaliyo bora.

Mnajua mkiwa na ugomvi kila mmoja anaongea lake kwaiyo leo tulikuwa tunawekana sawa ili tumlee mtoto wetu akue katika misingi iliyo bora, alafu hivi viasi vya pesa tunavyotaja mitandaoni mara oh mimi nataka milioni 10 tunakuwa tunazungumza tu lakini kiukweli mtoto anataka malezi mengi kuna wakati mwingine kama mwanao una uwezo wa kumpa hata milioni mia ila hautampa kwa sababu ulishaandikiwa milioni 10 hiyo haimsaidii mtoto lakini tumeweka mazingira mazuri na nimeweka kiasi kizuri ambacho kitaweza kumsaidia aweze kukua ni mtoto wangu na pia kwenye maisha kuna kupanda na kushuka”.

Diamond alipata kutaja kiasi alichopangiwa kutoa kwa mwezi na kusisitiza ni mambo ya kifamilia lakini pia ameongelea kumaliza tofauti zake na Hamisa na kusema kuwa yeye na Hamisa hawakuwa na bifu lolote bali kuna pande zilizokuwa zinawachochea.

Hamisa Mobetto Akiri Kulimiss Penzi la Diamond

Mwanamitindo na msanii wa Bongo movie, Hamisa Mobetto amekiri kulikumbuka penzi la mzazi mwenzake ambaye ni staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Hamisa na Diamond walikiri kuwa na mahusiano ya siri kwa miaka tisa mpaka yalipomwagwa wazi mapema mwaka jana walipozaa pamoja mtoto wao wa kiume anayeitwa Dully au Dylan.

Baada ya mahusiano yao kuwa hadharani wawili hao waligeuka maadui kwenye mitandao ya kijamii kwani Hamisa aliingia kwenye migogoro kadhaa na mpenzi wa Diamond na mzazi mwenzake Zari.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu kuhusiana na mahusiano yake Hamisa amewashangaza wengi siku chache zilizopita baada ya kuandika ujumbe ulioashiria kabisa umemlenga mpenzi wake wa zamani Diamond.

Ambapo kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Hamisa maneno yalioashiria yeye kumkumbuka mpenzi wake wa zamani:

Sometimes i miss you but my heart no longer hurts like it used to, I miss you but I don’t want you back..sijui nimwamini nani kwenye safari ya penzi  langu nimkabidhi usukani akawe dereva wangu maana majanga nalilia kisicho changu..kwenye nyumba ya kupanga nadai kodi wenzangu”.

Baada ya kuandika ujumbe huo watu wengi walimjia juu kwa kutangaza amemiss Diamond wakati anajua fika ana familia na mwenyewe kwa maneno yake amekiri kuwa analilia kisicho chake.

Hamisa alipotafutwa na chanzo kimoja cha habari kuhakikisha endapo ujumbe huo umemlenga Diamond hakupatikana lakini mama mzazi wa Hmisa anayejulikana kama Mama Mobetto alifunguka yafuatayo kuhusiana na mwanaye kumkumbuka Diamond:

Jamani sisi mambo hayo kwenye mitandao mda huu hatuna tena hata mwanangu ameshayasahau hayo mambo badala yake yupo bize na mambo yake mengine..michakato yetu sisi ni kutafuta pesa na si mengine na wala hatutaki kumsikia huyo Diamond”.

 

Zari Asitisha Mahojiano na Vyombo Vya Habari Baada Ya Maswali Ya Diamond na Hamisa Kutawala

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ amesitisha mahojiano yake na kituo cha redio cha Capital FM na stesheni zote baada ya kuchoshwa na maswali ya maisha yake binafsi.

Zari amekuwa kwa wiki moja sasa nchini Uganda na amefanya media tour katika vituo mbali mbali kwa ajili ya kutangaza party yake ya Zari All White Party, lakini Jana kabla ya shoo yake alisitisha mahojiano na kituo cha Capital FM kwa like alichodai anaulizwa maswali ambayo yapo kibinafsi Sana na hapendelei kuyajibu bali yuko interested na kuongelea kazi zake zaidi kuliko maisha yake binafsi.

Kutokana na drama zinazoendelea mtandaoni kati ya Diamond, Zari na Hamisa kila radio station aliyoenda Zari amefunguka mengi sana juu ya kinachoendelea kati yake na Diamond na usaliti aliofanyiwa na mzazi mwenzake huyo baada ya kuzaa na Hamisa miezi michache iliyopita.

Kupitia page yake ya snapchat Zari aliujulisha umma wa Uganda kuwa hataweza kuendelea na mahojiano na vituo mbali mbali vya redio kutokana na kukwepa drama zinazokuja na maswali yanayoulizwa na waandishi wa habari kuhusu maisha yake binafsi kwani anachotaka kuzzungumzia ni Zari, watoto wake na biashara zake tu.

Nimeamua kuhairisha kufanya interview na vituo vyote vya habari kutokana na kuulizwa maswali ambayo mengi ni binafsi sana na sipo tayari kwa drama zinazofanyika na ninaamini kuwa drama ni kwa ajili ya watu wenye drama ila mimi naangalia maisha yangu watoto wangu na  biashara zangu, lakini natarajia kumuona kila mtu usiku wa lao kwa ajili ya Zari All White Party”.

Kwenye interview zote alizofanya Zari nchini Uganda amekuwa muwazi sana kwa kile kilichotokea kati yake na Diamond na Hamisa jambo lililozua maneno maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii.

Hamisa Mobetto Amefunguka Haya Baada Ya Tetesi za Kuonekana na Diamond Dubai

Mwanamitindo na muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto kwa mara nyingine tena ameingia kwenye vichwa vya habari baada ya tetesi kuenea kuhusiana na uhusiano name baba mtoto wake Diamond.

Mwishoni mwa wiki iliyopita habari zilienea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diamond na Hamisa wameonekana pamoja nchini Dubai ambapo Diamond alikuwa anashiriki kwenye tamasha la One Africa Music Festival, huku sababu ya Hamisa kuenda Dubai ikiwa haijajulikana bado.

Picha mbali mbali zilisambaa mtandaoni zilizoashiria kuwa Diamond na Hamisa walikuwa katika eneo moja huku watu wakidai kuwa wamewaona pamoja kitendo ambacho kiliibua maswali Mengi kutokana na kuwa kiukweli Diamond yupo katika uhusiano na mama watoto wake na mpenzi wake Zari ambaye kwa sasa yupo nchini South Africa.

Mwishoni mwa wiki hii Hamisa alikuwa kwenye uzinduzi wa filamu yake inayojulikana kama ‘Zero player’ aliyocheza hivi karibuni katika mahojiano na Millard Ayo Tv alifunguka yafuatayo kuhusu tetesi hizo na uhusiano wake na mzazi mwenzie Diamond:

First of all kitu ambacho watu wanatakiwa wajue Mimi na Naseeb ni mtu na mzazi mwenzie yaani tumezaa mtoto sasa sijui kwanini watu wana-make a big deal wakisikia Hamisa kakutana na Diamond yaani hicho ni kitu ambacho watu wanatakiwa wazoee tu kwani ni baba wa mtoto wangu na mimi ni mama wa mtoto wake lakini hapana sikukutana na Naseeb Dubai watu sijui wamepata wapi hizo stori ama wamefikiria kitu gani ila kiukweli hata kama ningekutana naye ingekuwa kwa ajili yangu mimi na yeye kujua siyo watu wengine kujua”.

Pia Hamisa alifunguka na kudai kuwa yeye hana ugomvi wowote na familia ya Diamond hasa mama yake na Diamond kwani anamheshimu sana na pia anaamini mtu mzima hakosei lakini pia amedai anaelewa kama Zari anamchukia lakini yeye hana tatizo naye.

Inasemekana Hii Ndio Picha Iliyowaunganisha Diamond na Hamisa Dubai

Mwanamuziki Diamond Platnumz amerudi tena kwenye skendo na mzazi mwenzie Hamisa Mobetto baada ya habari kusambaa mtandaoni kuwa walikuwa wote nchini Dubai.

Wiki chache zilizopita Diamond alienda Nchini Uingereza, London ambako alikuwa na shoo lakini siku ya pili baada ya kufika huko Zari naye alitoka South Africa na kwenda kuungana naye London ambapo waliweka picha mtandaoni wakila bata na kufanya media tours.

Mapema wikiend hii mrembo Hamisa Mobetto alisafiri kutoka Tanzania kuelekea Dubai ingawa hakuweka wazi sababu ya kwenda nchini humo. Baada ya Diamond kutangaza kuwa anaenda Dubai kwa ajili ya kufanya tamasha la One festival, hapo ndipo maneno yalipoanza kuwa Diamond na Hamisa wako wote ingawa hakuna aliyekuwa ana uhakika hivyo yalibaki kuwa maneno maneno ya watu mtandaoni.

Kushoto: Diamond na Salaam SK wakiwa pamoja na mrembo huyo Kulia: Hamisa akiwa pamoja na mrembo huyo.

Leo kwenye mitandao wa kijamii kuna picha inayosambaa ikimuonyesha msichana ambaye haijajulikana kuwa ni rafiki wa karibu wa Hamisa tu au ni shabiki aliyeomba kupiga picha na Diamond na akapiga picha na Hamisa jambo lililowafanya watu wengi wahisi kuwa wawili hao walikutana na walikuwa eneo moja usiku huo.

Je unahisi Diamond na Hamisa walikuwa pamoja au ni maneno ya watu wanaotaka kuwagombanisha Diamond na Zari.

Tafadhali toa maoni yako hapo chini.