Diamond Hana Pesa, Nimeshakuwa na Wanaume Wenye Pesa-Zari

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari’ ameibuka na kumtupia dongo zito mzazi mwenzake huyo na kusema hana pesa.

Zari na Diamond walikuwa kwenye mahusiano kwa miaka minne na walifanikiwa kuzaa Watoto wawili Lakini Penzi Lao liliingia shubiri mapema mwaka jana Baada ya Diamond kuchepuka na Hamisa na kuzaa naye mtoto.

Tangu waachane sio siri Diamond na Zari hawajawahi kuwa na mahusiano mazuri na siku ya Leo ameweka wazi kuwa Diamond hana pesa kama watu wengi wanavyosema.

Zari alifunguka hayo alipoulizwa na shabiki kama Diamond asingekuwa tajiri na maarufu basi Zari asingeweza kuwa naye kwenye mahusiano, Swali ambalo Zari alijibu kuwa Diamond hana pesa.

Siongei haya ili kuonekana na roho mbaya Lakini nimeshawahi kuwa na wanaume wenye pesa nyingi na yeye hayupo kwenye hao watu kwaiyo sikuwa naye Kwajili ya pesa na umaarufu. Wanaume zangu wote niliowahi kutembea nao ni matajiri lakini bado sijapata ambaye hatakuwa anabadilisha wanawake”.

 

Babu Tale- Sijaenda South Africa Kurudisha Penzi la Diamond na Zari

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kudai hakuenda nchini South Africa Kurudisha Penzi la Diamond na Zari.

Wikiendi iliyopita habari ya mjini ilikuwa Zari na Diamond baada ya video ya wimbo wa iyena kutoka ukiwaonyesha wawili wakifunga ndoa mwaka jana wakati bado wapenzi.

Babu Tale alitengeneza headlines baada ya kutangaza anaenda nchini South Africa kwa ajili ya kwenda Kurudisha Penzi la Diamond na Zari baada ya kutengana kwa zaidi ya Miezi minne sasa.

Lakini baada ya kufika nchini humo ambako ndipo Zari anaishi na watoto wake Babu Tale ameweka wazi kuwa hajaenda Kurudisha Penzi lao bali ameenda kuwapatanisha wawili hao ili waweze kulea watoto wao.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Babu Tale amesema ameona ni vyema wawili hao wakaelewana kwa manufaa ya watoto wao:

Kilichonileta  huku ni kuwasuluhisha matatizo yao wayaweke pembeni ili waweze kulea watoto wao, of course nimeongea sana na Zari nikamwambia kama mnataka kurudiana kimapenzi it’s up to you lakini mimi ningependa kuona wewe na Diamond mnapatana ili  watoto waweze kuwa karibu na nyinyi na ikitokea tupo South Africa ni rahisi kupita kusalimia watoto na kama watoto wamemiss Baba unampigia simu”.

Diamond na Zari wamekuwa na uadui fulani tangu wawili hao walipoachana Miezi michache iliyopita ambapo Zari alimtuhumu Diamond kwa kutowaona watoto wake kwa miezi mitano kutokana na wao kukosa maelewano.

Wema Sepetu Yupo Tayari Kushuhudia Ndoa Ya Diamond na Zari

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameshangaza watu wengi baada ya kufunguka kuwa anatamani a Ex wake Diamond Platnumz na Baby mama wake Zarinah Hassan wafunge Ndoa.

Wema alifunguka hayo baada ya video ya wimbo wa Iyena wa Diamond kutoka siku ya Ijumaa ambapo ndani yake yupo Zari kama video queen ambapo ndani ya video hiyo wanafunga ndoa.

Wema alimtaka Diamond kufanya kweli na kumuoa mama watoto wake huyo ambapo aliandika maneno haya Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli. Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri”.

Hili suala limewaacha watu vinywa wazi kidogo k sababu hasa ukiangalia kuwa Zari aliweka wazi kuwa alimtosa Diamond baada ya video kusambaa zilizomuonyesha Diamond na Wema wakikumbatiana Kwenye kumbi za starehe Miezi minne iliyopita.

Zari Amchana Diamond Baada Ya Kugoma Kuwaona Watoto Wao

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameingia vitani na mzazi mwenzake mfanyabiashara Zarinah Hassan baada ya kumtuhumu kwa kutokwenda kuwaona watoto wao na kutojua wanaishije mpaka hivi sasa.

Diamond na Zari walikuwa Kwenye Mahusiano kwa miaka minne na zaidi lakini mwaka huu mwezi wa Pili Zari alivunja Mahusiano yao baada ya kuchoshwa na michepuko ya Diamond lakini alisisitiza kuwa watabaki marafiki kwa ajili ya watoto wao.

Lakini sasa urafiki huo umeelekea ukingoni kwani Zari amempa makavu Diamond na kumtaka aende akawaone watoto wao kwani watoto hawajamuona Baba yao kwa miezi kadhaa sasa.

Zari amemtolea povu hilo Diamond Kupitia ukurasa wake wa Snapchat ambapo amewatolea maneno pia mameneja wake na kuwataka wamshauri msanii wao akawaone watoto wao kwani watakuwa wameshaanza hata kumsahau Baba yao:

 

“Wema na Jokate Wameungana Ili Kumshusha Alikiba”-Harmorapa

Msanii wa Bongo fleva  anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa amewatolea povu tena warembo wengine ambao ni Wema Sepetu na Jokate Mwegelo  na kudai ni wadangaji na wameungana ili kumshusha Alikiba.

Wiki iliyopita baada ya kutoa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ watu wengi walijitokeza na kumpongeza Diamond kwa hatua aliyofikia na warembo kama Wema na Jokate nao walimpongeza kitendo ambacho inaelekea hakikumfurahisha Harmorapa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa aliwatolea povu zito Wema na Jokate kwa kudai kitendo chao cha kumpongeza Diamond ni kwa nia ya kutaka kumshusha Ali Kiba:

Naona hawa wadada na wadangaji wengine wameungana ili kumshusha King Kiba. Nawachana nyie wadangaji mwenye kupewa uwezo kapewa tu nyie bora mkazane na uwezo weny mliopewa wa kudanga. Mnafikiri mkiposti kazi za Diamond ndio mnuumiza moyo KingKiba? Ndio maana mmchezewa mmeachwa Jojo umechezewa na King Kiba umeachwa kaenda kuoa mtoto chokoleti huko Moombasa eti hasira zako umezihamishia huko kwa Chibu, na liwema nalo limechezewa likaachwa nafasi ikachukuliwa na African beauty Zari aliyelishinda kila kitu kuanzia uzuri m, followers mpaka pesa eti likaanza kumtongoza king kiba ili limkomeshe Mondi, KIng nae akapita nalo akalitema likaona lirudi kumwaribia Zari ndoa yake nalenyewe limeungana kumharibia Alikiba”.

 

Familia Ya Diamond Imecharuka Baada Ya Zari Kuwapeleka Watoto Kanisani

Familia ya msanii wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, inadaiwa kuja juu na kutofurahishwa na kitendo cha Zari kuwapeleka watoto wao kanisani.

Zari na Diamond waliachana mwezi uliopita lakini katika Mahusiano yao walifanikiwa kupata watoto wawili ambao ni Latiffah na Nillan ambao wanaishi na kama yao Africa ya kusini.

Habari zilizoifikia gazeti la Amani zimedai kuwa siku chache baada ya Zari kuonekana akiwapeleka watoto wake wote kanisani siku ya Jumapili kimewacharua familia ya Diamond ambao ni way mini wa dini ya kiislamu hivyo moja kwa moja wanataka watoto wao wafuate dini yao.

Gazeti la Amani linaripoti kuwa mwanafamilia mmoja  wa familia ya Diamond ambaye aliomba jina lake lisiandikee gazetini amesema kama familia wamekasirikishwa na suala hilo kwani walijua labda wataenda mara moja tu lakini imekuwa kila jumapili:

Awali Zari alipotupia picha ya kwanza ikionesha ameenda kanisani na watoto, tuliona labda ni maombi ya mara moja na pengine haiwezi kuwa tatizo lakini kadiri siku zinavyozidi kwenda, tunaona amekomaa na kanisani sasa tunaona kama inaweza kuja kuwa tatizo hapo baadaye na watoto wakawa njia panda.

Si unajua wale watoto ni waislamu kwa sababu siku zote watoto huwa wanafuata kwa baba, sasa baadaye watakaporudi kwa Diamond na wakawa wameshazoea kwenda kanisani itakuwaje?” 

Baada ya kupewa taarifa hiyo gazeti hilo lili Fanta jitihada ya kumtafuta Diamond na Mama Diamond ambao wote hawakupatikana lakini walipomsaka Baba Diamond Abdul Juma aliweka wazi kuwa kama familia hawajafurahishwa na kitendo cha Zari kuwafundisha kuhusu mafundisho ya Kikristo pekee.

Hatukatai dini ni dini tu lakini kilichotushtua ni kwa nini tunaona anawapeleka upande mmoja tu.
Unajua hata kama yeye ameamua kurudi kwenye Ukristo lakini watoto anapaswa kuzungumza na mwenzake ili waamue pamoja”.

Baba Diamond alimalizia kwa kutoa msimamo mkali kuwa, kama familia watamsisitiza Diamond azungumze na mzazi mwenzake na waangalie uwezekano wa kuwapeleka watoto hao madrasa ili pia waifahamu dini ya baba yao.

Natafuta Pesa Sina Muda wa Kutafuta Mpenzi Mpya- Zari

Zari ameibuka na jipya tena huku safari hii akisisitiza kuwa wale wanaume wakware wote waliopanga foleni kusubiri penzi la Zari hawana nafasi kwani hana muda wa kuwa na mpenzi kwa sasa.

Zari alitangaza kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, mwezi uliopita lakini tangu hapo Kumekuwa na tetesi nyingi juu ya Zari kupata mwanaume mwingine wa kuchukua nafasi ya Diamond.

Kupitia kurasa yake ya SnapChat siku ya jana Zari ameweka wazi kuwa haitaji mpenzi kwa sasa baada ya marafiki zake kumtumia ujumbe uliosema “Kama mwanaume wako akienda kutafuta vimada  wenye msambwanda mpya inabidi umkumbushe kuwa na wewe msambwanda wako mpya kwa mwanaume mpya”.

 

Zari amedai kuwa marafiki zake wanamtumia meme hizo kama vijembe kwa EX wake lakini amejibu kuwa hataki mwanaume mpya kwa sasa:

Marafiki zangu siwawezi hivi kwanini wamekazana kunionyesha hizi Mambo lakini hazinifai mimi….. Nahitaji kutafuta pesa mpya na sihitaji mwanaume kwa muda huu samahani!!!!”.

 

Njama Anazofanya Zari Kuwaondoa Watoto kwa Diamond.

Haijawahi kuwa kesi kwa wazazi kugombana lakini watoto wakabaki katika hali  ya kawaida na malezi yakaendelea. siku zote haiwezekana kumnyima baba mtoto kama baba hajwakana na anaendelea kuwahudumia.

Baada ya Zari kugombana na kutangaza rasmi kuhusu kuachana na Diamond Platinumz ameanza mikakati mipya ya kuwaweka watoto wake bali na familia ya Diamond  kwa kuwapeleka kanisani.Hii imezua gumzo sana katika mtandao wa kijamii kwa wle walioona picha za caption za watoto hao katika page zao.

Katika kurasa za mitandao ya kijamii hasa instagram , jana siku ya jumapili waliweka caption za kuwaonyesha kuwa wanaenelekea kanisani,katika page ya Princesstiffah aliweka picha na kuandika “stepping into church like…”  na pia katika ukurasa wa Prince Nillan nae aliandika “had swimming plans after church but looks like cloudy sunday”

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Zari kuonekana kuwapeleka watoto hao kanisani ilihali baba wa watoto wake (Diamond platinumz )   dini yake sio ya kwenda kanisani, na shida inakuja pale ambapo ameazna kuonekana akiwapeleka kanisani watoto hawa baada ya kugombana na baba yao.

Swali limekuwa kwa mashabiki kuwa je, Diamond mwenyewe anaona hayo yakitokea, au ameruhusu na ndio maana hata mama anapata mwanya wa kuweka wazi swala la watoto wake kwenda kanisani.

Wema: Zari Alimuacha Diamond Kwa Mambo Aliyomfanyia Huko Nyuma Sio Kisa Mimi

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema anaamini Zari alimuacha Diamond kwa mambo yao waliyotofautiana kipindi cha nyuma lakini sio kisa yeye alimkumbatia.

Baada ya Zari kutangaza kumuacha Diamond alifanya Interview na BBC Swahili na aliweka wazi kuwa amemuacha aliyekuwa mpenzi wake supastaa wa Bongo fleva Diamond kwa sababu ya yeye kukumbatiana na Wema kwenye party.

Wema na Diamond walikuwa pamoja kwa miaka kadhaa huko nyuma na wamekuwa na tabia ya kuachana na kurudiana hata Diamond amedaiwa kuchepuka kwa wapenzi wake wapya na Wema hivyo alivyoonekana tu Wema wanakumbatiana ikaonekana tayari.

Lakini Wema amekataa tuhuma za Zari kuwa amemuacha kisa yeye Kwenye Interview aliyofanya wikiendi iliyopita na Bongo 5 Wema Alitalia maneno haya juu ya suala hilo:

Zari alikuwa ana sababu nyingi sana za kupanick za nyuma za Diamond za mambo yao wenyewe lakini sio hiyo ya juzi ya mimi kumkumbatia Diamond kama rafiki atakuwa ana jingine”.

Lakini pia Wema aliweka wazi kuwa pamoja na yeye na Diamond wameachana kipindi kirefu kilichopita lakini bado wana chemistry ambayo haiwezi kuisha.

Wema alipotakiwa kumshauri kitu chochote Zari alifunguka na kusema kuwa hawezi kuwa mshauri wa Zari kuhusu Mahusiano yake na Diamond.

Msanii Kutoka Kenya Atangaza Nia Ya Kumuoa Zari

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka Kenya anayejulikana kama Ringtoneapoko amefunguka na kudai yupo tayari Kuwa na Zari baada ya kutangaza kuachana na Diamond.

Wiki iliyopita siku ya Wapendanao Zari alitangaza kuwa ameamua kumuacha Baba watoto wake na mpenzi wake Diamond huku akisisitiza kilichompelekea kufikia uamuzi huo ni Diamond kuzidisha michepuko.

Baada ya tukio hilo Kumekuwa na maneno mengi yamekuwa yanasemwa huku linalowatatiza wengi ni kama kweli wawili hao wameachana kwani Kumekuwa na maneno mengi yanasemwa huku ikidaiwa wawili hao wanatafuata kiki na hawajaachana jambo ambalo Zari amelikataa.

Huku drama ya Diamond na Zari ikiwa inaendelea msanii Ringtoneapoko kutoka Kenya amejitokeza na kusema anataka kumuoa Zari huku akidai amesikitishwa na kitendo ambacho Zari amefanyiwa na Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ringtoneapoko aliandika ujumbe huu kwa Zari:

Leo tumenunua ng’ombe 42 ambazo tumepanga kupeleka Uganda kwa waking Zari wakati ukifika. Na kieleweke vyema kama mwanaume hajalipa mahari huyo msichana bado sio wake. Ama namna gani???? Na please mwambieni Diamond asimtolee Zari wimbo aende atoe mahari kama all serious. For us tupo tayari kwenda Uganda na tulipe hatuogopi tunafunga na kumuomba Mungu atupe ushindi”.

 

Ney wa Mitego Amchana Diamond Baada ya Kuachwa na Zari

Msanii wa Bongo fleva Ney wa Mitego amemtolea povu zito msanii mwenzake Diamond Platnumz baada ya mpenzi wake Zari kutangaza rasmi kuwa amemuacha kutokana na michepuko kuzidi.

Jana usiku Zari aliwashtua watu wengi baada ya kuweka wazi kuwa ameamua kimya cha Diamond kutokana na kuzidi kudhalilishwa na taarifa za yeye kuwa na michepuko mingi huku mambo yaliyokuwa yanatokea kwenye mitandao ya kijamii yalikuwa yanamuumiza.

Kumekuwa na skendo nyingi mtandaoni za Diamond kuchepuka na wanawake kadhaa huku pia kumekuwa na uthibitisho wa vitendo hivyo lakini kwa muda mrefu Zari alionekana kuvumilia na kumsamehe mpenzi wake huyo lakini safari hii inaelekea maji yalimfika shingoni.

Baada tu ya Zari kutangaza kumwaga Diamond mashabiki walianza kumlaumu Diamond kwa kumuacha mrembo kama Zari aende kwa tabia yake ya kuendekeza michepuko moja kati ya watu hao ni msanii Ney wa Mitego.

Nay kumtolea povu zito Diamond kwa kumuacha mtoto mzuri kama Zari ambaye ana pesa zake na badala yake kuendekeza michepuko ambayo hainam maana ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay wa Mitego alitoa povu hili:

Wanasema chozi la aliyetendwa haliendi bure mwanangu Diamond, Omna sana Mungu akuonyeshe njia la si hivyo utapotea… umempoteza mwanamke ambaye hana njaa ana maisha yake binafsi alichokuwa anataka ni mapenzi yako tu sikatai kuwa hakuna mwanaume asiyekuwa na tamaa lakini ulifeli kufanya uchafu wako wazi wazi”.

Baada ya kutoa povu hili imeonyesha wazi kuwa Nay wa Mitego na Diamond hawana urafiki mzuri kama waliokuwa nao mwanzoni ambapo siku za nyuma kulikuwa kuna habari zikidai kuwa wamekorofishana.

Zari Kwa Mama Diamond ” Fanya Tuhame Madale Guest House Tumwachie Mwanao”.

Mzazi mwenza na mpenzi wa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari the Bosslady’ ameendelea kukaa kwenye vichwa vya habari baada ya kuachia bomu jingine.

Tangu Hamisa aachie picha zilizomuonyesha alikuwa anajiachia Nyumbani kwa Diamond Madale na hata ofisini kwa Diamond sasa imekuwa fasheni kwa wasichana kujipiga picha wakiwa Madame na kisha kuzisambaza mtandaoni.

Wiki iliyopita kuna msichana anayetambulika kwa jina la Mila ambaye video yake akiwa Nyumbani kwa Diamond, Madale kusambaa mtandaoni na kusababisha tafrani hadi kupelekea Zari kupaita Madame Guest house yaani nyumba ya kulala wageni.

Zari ameonyeshwa kuwa bado ana kinyongo na Diamond kwa tuhuma za wanawake kwenda kujiachia Nyumbani kwao Madale wakati yeye akiwa nchini South Africa.

Lakini pia inaonekana mpaka sasa ishu hiyo ya Diamond kupeleka wasichana kulala Madale bado inamkera Zari kwani ameendekea kuiongelea baada ya kumwandiki mama mzazi wa Diamond kuwa wahame Madale guest house na wamuache mwanaye ambaye ni Diamond peke yake, Zari alimwandiki Mama Diamond ujumbe huu:

Fanya tuhame guest house tumwachie mwanao”.

 

 

Kabla ya sakataa hili la wiki iliyopita halijaishaa vizuri Zari kamuongeza Zari na skendo jingine la kukumbatiana na Wema na mpaka sasa haijajulikana vipi uhusiano wa Diamond na Zari upoje ingawa Diamond ameshasema hawezi kuiacha familia yake.

Diamond Platnumz: Nampenda Zari na Siwezi Kumuacha

Mwanamuziki machachari wa Bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kudai kuwa anampenda sana mpenzi wake Zari na hawezi kumuacha.

Wiki iliyopita ilikuwa ni wiki ya Diamond kwani alikuwa akitawala vichwa vya habari vyote kwenye mitandao ya kijamii sababu ya uhusiano wake na mama watoto wake Zari.

Baada ya habari kusambaa kuwa Diamond ana uhusiano wa kimapenzi na mrembo anayeitwa Tunda kuna tetesi zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diamond na mpenzi wake Zari wameachana.

Siku chache zilizopita Diamond alitua nchini Rwanda ambako ameenda kwa ajili ya kutambulisha bidhaa zake za Chibu perfume na Diamond karanga, bidhaa ambazo tayari ni maarufu sana nchini Tanzania, Kenya na Uganda.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari (press conference) nchini Rwanda, Diamond alifunguka kuhusu suala linalozungumzwa sana mtandaoni nalo ni uhusiano wake na Zari kwa hivi sasa ambapo Amesisitiza kuwa ana mwanamke mmoja tu ambaye ni Zari na anampenda sana na hategemei kumuacha.

Lakini pia Diamond amefunguka na kutaja idadi ya watoto aliokuwa nao na amesema kuwa ana watoto watatu ambao ni Tiffah na Nillan aliozaa na Zari na Dylan aliyezaa na Hamisa. Hii imetokana na wanawake wengi kujitokeza na kudai kuwa wamezaa na Diamond.

Diamond alimalizia kwa kuongelea album yake mpya inayoitwa ‘A boy from Tandale’  ambayo anategemea kuitoa tarehe 23  mwezi wa pili ambapo kwenye albamu hiyo amewashirikisha wasanii wakubwa kama Rick Ross.

“Ati Madale State Lodge, au Madale State House?” Zari Aendelea kumpiga Madongo Diamond

Mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari’ ambaye pia ni mpenzi na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amejikuta anashindwa kuvumilia kinachoendelea mtandaoni na kumtupia madongo mpenzi wake.

Tangu wiki hii inaanza stori iliyotawala mitandao ya kijamii ni uhusiano uliopo baina ya Diamond na mrembo Tunda. Tangu mwanzo wa wiki kilichokuwepo ni tetesi tu na maneno ya watu yaliosemwa mpaka Jana video iliyosambaa mtandaoni ilitomuonyesha mdogo wa Tunda akijiachia Nyumbani kwa Diamond Madale.

Ifahamike kuwa nyumba ya Diamond iliyopo maeneo ya Madale ilibatizwa jina la ‘State house’ ikimaanisha mjengo wa raisi/ Ikulu na Guest House ikimaanisha nyumba ya kufikia wageni.

Baada ya stori ya Jana kutoka kuwa msichana huyo amejirekodi akitembea Madale lakini pia Hamisa na yeye ameshajirekodi akiwa Madame inaelekea uzalendo ulimshinda Zari ikabidi amrushie dongo hill la kuhoji endapo  nyumba hiyo bado ni jumba la raisi au imekuwa ni guest house?

Zari alihoji hayo kupitia ukurasa wake wa Snapchat na kuandika:

Ati Madale state lodge or Madale state house? Kuna mtu alikuwa anauliza akipanda Bajaji anashukia wapi? Mama yangu sio state house Tena….”.

 

Tetesi za Diamond kutembea na Tunda zimekuwa zikisikika mjini hapa kwa muda mrefu lakini wote wawili wamekuwa wakizikana lakini pia hivi sasa kuna habari zinazodai kuwa Tunda ni mjamzito na Diamond ndiye baba mtoto ingawa ni taarifa tu ambazo hazijathibitishwa na Tunda wala Diamond.

Zari Asitisha Mahojiano na Vyombo Vya Habari Baada Ya Maswali Ya Diamond na Hamisa Kutawala

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa msanii Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ amesitisha mahojiano yake na kituo cha redio cha Capital FM na stesheni zote baada ya kuchoshwa na maswali ya maisha yake binafsi.

Zari amekuwa kwa wiki moja sasa nchini Uganda na amefanya media tour katika vituo mbali mbali kwa ajili ya kutangaza party yake ya Zari All White Party, lakini Jana kabla ya shoo yake alisitisha mahojiano na kituo cha Capital FM kwa like alichodai anaulizwa maswali ambayo yapo kibinafsi Sana na hapendelei kuyajibu bali yuko interested na kuongelea kazi zake zaidi kuliko maisha yake binafsi.

Kutokana na drama zinazoendelea mtandaoni kati ya Diamond, Zari na Hamisa kila radio station aliyoenda Zari amefunguka mengi sana juu ya kinachoendelea kati yake na Diamond na usaliti aliofanyiwa na mzazi mwenzake huyo baada ya kuzaa na Hamisa miezi michache iliyopita.

Kupitia page yake ya snapchat Zari aliujulisha umma wa Uganda kuwa hataweza kuendelea na mahojiano na vituo mbali mbali vya redio kutokana na kukwepa drama zinazokuja na maswali yanayoulizwa na waandishi wa habari kuhusu maisha yake binafsi kwani anachotaka kuzzungumzia ni Zari, watoto wake na biashara zake tu.

Nimeamua kuhairisha kufanya interview na vituo vyote vya habari kutokana na kuulizwa maswali ambayo mengi ni binafsi sana na sipo tayari kwa drama zinazofanyika na ninaamini kuwa drama ni kwa ajili ya watu wenye drama ila mimi naangalia maisha yangu watoto wangu na  biashara zangu, lakini natarajia kumuona kila mtu usiku wa lao kwa ajili ya Zari All White Party”.

Kwenye interview zote alizofanya Zari nchini Uganda amekuwa muwazi sana kwa kile kilichotokea kati yake na Diamond na Hamisa jambo lililozua maneno maneno mengi kwenye mitandao ya kijamii.

Tahiya Amuomba Msamaha Zari Baada Ya Video Yake Yenye Utata na Diamond Kusambaa (video)

Mwanamitindo na mrembo anayejulikana kama Tahiya amekiri kuwa alimuomba msamaha mpenzi wa Diamond, Zari baada ya video yao kusambaa.

Wiki chache zilizopita video clip iliyomuonyesha Tahiya akiwa na mkali katika muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz wakiwa wamekumbatiana kimahaba kusambaa na kusababisha sintofahamu. Baada ya kuhojiwa Tahiya alikataa kuwa na uhusiano wowote na Diamond huku akidai kuwa Diamond ni ndugu yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Tahiya aliweka wazi kuwa yeye ndugu wa Diamond kwahiyo hakuna kitu chochote kinachoweza kuendelea baina yao na anamuheshimu Zari kama make halali Diamond;

Unajua mimi nina ukaribu na Diamond kwa hiyo watu walivyoniona kwenye birthday yake na mimi kuwa karbu naye watu wakachukulia vibayq ila kitu watu hawajui Diamond ni mtu poa sana ni mtu wa famiia, hata Zari hakuwa na neno na ile video ila zaidi ya hapo watu wanatakiwa wajue kuwa namheshimu sana Zari na pia namheshimu Diamond na kwa ujumla nawaheshimu kama mume na mke na kama Zari amechukulia vibaya ile video naona ni muda nimuombe msamaha kwa ile video, ila sikutegemea Kama watanzania wanaweza kuikuza ile ishu”.

Pia Tahiya alikataa tuhuma alizorushiwa kuwa alionekana amelala nyumbani kwa Diamond Madale .

Hii ndio Video ya Diamond na Tahiya iliyozua haya yote: