Mange Kimambi Ahusishwa Kesi ya Mwanafunzi wa UDSM.

Kesi ya mwanafunzi wa udsm Abdul Nondo ambayo iliendelea wiki iliyopita  huku shaidi upande wa jamhuri alitoa ushaidi na kusema kuwa mwanafuzni huyo aliwahikuwasiliana na mwanadada Mange Kimambi kabla ya tukio la kutekwa kutokea.

Mwana dada Mange kimambi ambae amekuwa ni moja ya wanaharakati wasiokuwa na taaluma maarumu kutokana na uwezo wake wa kuingilia katika kila idara na kukosoa au kusema ukweli ulioficha kuhusu kitu flani amehusishwa katika kesi hiyo ya mwanafunzi Abdul Nondo.

Shaihidi huyo anasema kuwa katika simu ya mshtakiwa walikuta baadhi ya barua pepe ambazo mwanafunzi huyo aliweza kumuandiki Mange Kimambi akimuelezea habari zake na kwamba yeye ndie alitoa tamko baada ya kutokea kwa kifo cha mwanafuzni wa NIT kifo kilichogusa mamilioni ya watanzania.

Lakini pia mtoa ushaidi huyo alisema kuwa ktaika barua pepe hiyo Abdul Nondo alimweleza mange kimambi kuwa amepata taarifa kuwa amekuwa akitfautwa kwa muda mrefu na ametakwa kutotembea ovyo .

Mange kimambi ambae amekuwa akitoa habari nyingi na matukio mengi hasa ya wasanii amekutwa na tetesi hiyo lakini hajatraka kuzungumzia chochote kuhusu hilo.

Mange Kimambi Amerudi Kundini , sasa ni Mwenzetu:-Afande MamboSasa

Kamanda wa kanda maarumu ya kipolisi ya Jijini Dar Es Salaam, ametoa wito kwa vijana wote kuacha kushabikia mambo yasiyokwa na uthibitisho  na bila kutambua madhara yake katika jamii.kamanda huyo anasema kuwa mwezi uliopita walikamata vijana wengi waliokuwa wakihasisha swala la maandamano ambalo lilianzishwa na mwana Dada Mange Kimambi lakini baada ya tarehe hiyo kupita mange kimambi ameanza tena kuipongeza serikali.

Ninawasihii sana vijana wa tanzania mnapokuwa mkishabiki vitu uwe kwanza mnaangalia pia na athari zake katika jamii zetu,,mnamo 26 february tulikamata vijana ambao walikuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuhamasisha swala a maandamano ambalo lilikuwa limeanzishwa na mwanaharakati mange kimambi.lakini sasa hivi mamnge anaipongeza serikali na tunampongeza pia kwa sababu bado anaipongeza serikali na amerudi kundini.

mange amekuwa akiwapotosha jamii lakini baaada ya kuona kuna watu wengi wanampuuza basi na yeye ameona ni bora arudi na kuipongeza serikali lakini watu tuliowakamata tuliwahoji na kuwapa dhamana.

Mwanaharakati mange kimambi amekuwa akihamasishwa vitu vingi katika jamii na watu wamekuwa mstari wa mbele kumuamini. lakini siku ya kumbukumbu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kulitokea tafrani kutokana na dada huyo kuwahamasishwa watu katika mitandao kuandamanaili kumpinga kiongozi  mkubwa wa nchi.

Mange- Wimbo Mpya Wa Ali Kiba Umebuma

Mwanaharakati wa mambo ya siasa Mtandaoni mwanadada Mange Kimambi amemlipua staa wa Bongo fleva Ali kiba na kusema wimbo wake mpya unaojulikana kama ‘Mvumo wa Radi’ umebuma vibaya mno.

Siku ya Ijumaa Ali Kiba aliachia wimbo wake mpya kwa mara ya kwanza Kupitia kipindi cha XXL ya Clouds Fm lakini wimbo huo umepatwa na masahibu na kudaiwa kufanyiwa figisu figisu na watu wasiojulikana Kwenye mtandao wa Youtube.

Mange ameibuka na kumpa za Uso Ali Kiba kuwa wimbo wake wa Mvumo wa radi umebuma lakini amemtaka asikate tamaa kwani wasanii wengi wanatoa nyimbo na zinabuma na hata akamtolea mfano Diamond na kudai Albamu yake ya A boy From Tandale ilibuma pia.

 

 

Ebitoke- Namchukia Sana Mange Kimambi

Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke amefunguka na kuweka wazi kuwa hampendi kabisa Mwanaharakati wa mambo ya siasa mitandaoni Mange Kimambi.

Kama utakumbuka siku za nyuma Ebitoke alishawahi kuingia Kwenye headlines baada ya Mange kutangaza kuwa Anatembea na bosi wa Timamu Tv ambaye ni mume wa msanii mwenzake Mama Ashura na hadi kusababisha Mama Ashura kufukuzwa.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Ebitoke aliulizwa anamchukuliaje Mange Kimambi na mara moja alitiririka jinsi anavyomchukia:

Yaani katika watu ambao siwezi kiwazungumzia ni huyo, Kwanza huyo Dada mimi simpendi, ameshawahi kuongia kwenye anga zangu lakini hata kabla ya hapo nilikuwaga simpendi.

Halafu siwezi kumkubali yule dada maana hanisidii kitu chochote mimi naona anawasaidia watu wengine, Mimi sipendi mambo yake na wala sikapendi na wala sipendi vimtu vinavyoongea sana “.

Lakini pia Ebitoke amesisitiza taarifa alizozieneza Mange hazikuwa na ukweli hata kidogo kwani yeye na Mama Ashura wako vizuri kabisa ingawa sio marafiki.

Hoja ya Mange kimambi Aibuka Tena Bungeni.

Mwanadada mange kimambi  mwanaharakati maaarufu anaekaa nchini Marekani lakini amekuwa akitetea na kuibua mamno mengi katika jamii hasa ya Tanzania, ameibuka tena kama hoja bungeni baada ya mbunge wa Ulanga Mh Mlinga kuitaka serikali kupitia mamlka ayake husika kushughulika na watu wote hasa katika mitandao ya kijamii wanaotukana viongozi wa nchi.

Mh Mlinga anasema kuwa kutoka na kuwepo kwa kurasa nyinngi zenye kufanya mambo hayo kumekuwa hakuna tena heshima wala cheo cha rais au viongozi wake kwa sababu viongozi wamekuwa wakitukwanwa bila kuogopa kitu.

matusi katika mitandao ya kijamii ni too much, haijulikani katika mitandao rais ni nani  au kiongozi ni nani, kumekuwa na akaunti nyingi zinatukana sana katika mitandao ya kijamii , IGP huko hapa tumekuwekea hizo nyota mabegani  ni nguvu, tumia nguvu zako ,mfano natoa akaunti zinazomtukana raisi ni pamoja na Kwinyara, Malisa gj, Yerico Nyerere na dada yao Mange Kimambi wamekuwa wakimtukana sana rais.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa viongozi kutaka mwanadada huyo kuchukuliwa hatua kwa tuhuma hizo ingawa kunamengipia mazuri ambayo mwanadada huyo amekuwa akiyafanya katika jamii, lakini yote yanaweza kutambulika kulinagana  na mamlaka husika.

 

 

Mange Amvaa Jokate Baada Ya Ali Kiba Kuoa Mwanamke Mwingine

Mwanaharakati wa siasa Mtandaoni Mange Kimambi amemvaa Jokate na kumtolea povu zito baada ya aliyekuwa mpenzi wake staa wa Bongo fleva Ali Kiba kuoa mwanamke mwingine.

Asubuhi ya Leo Ali Kiba Kumuoa mke wake Amina huko Mombasa nchini Kenya lakini Ex wake Jokate anashika headlines ambapo Mange amemjia juu Jokate huku akimcheka kuhusu hilo.

Mange amekuwa akiipinga ndoa hii kufanyika hivi sasa kwa hofu ya kwamba itazima haraka tu zake za Maandamano Lakini pia amekuwa katika vita na Jokate kutokana na Jokate kuwa chama tawala na alikuwa kiongozi.

Mange amemtolea povu zito Jokate huku akihusisha ndoa ya ALi Kiba ambapo kwenye ukurasa wa Instagram wa Jokate aliandika maneno haya:

Sina Uhakika Kama Mange ni Binadamu wa Kawaida.:-Dr.Tulia Ackson

Mh .naibu spika wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr Tulia Ackson amefunguka na kusema kuwa hana uhakika sana kama mwandada mabe ni mwana harakati na muongeaji katika mitandao ya kijamii kama ni binadamu wa kawaida.hivyo basi inakuwa ngumu sana kwake kum-judge mwanadada huyo kama anakosea au kama yupo sahihi.

sina uhakika kama na yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi au, kwaio nikikuana nae ndo nitajua nini cha kuzungumza ,lakini kwa yake ninayoyasikia ya hapa na pale kuhusu yeye sina uhakika sana kama na yeye ni binadamu wa kawaida kama mimi au sio ila nikipata nafasi ya kumuona nitazungumza nae.

siwezi sema kama anakosea kwa sababu sijajua yeye ni wa aina gani kama nilivyosema hapo awali,huenda hakosei kutokana na aina yake ya ubinadamu yaan species yake ni tofauti, kwaio kama spicies yake ni tofauti hapo huwezi kusema kuwa anakosea.

Maneno ya Dr Tulia yanaweza kuja baaada ya mwanaharakati huyo kuwa na mambo mengi sana anayoajua ambayo inawezekana kuwa mengine ni ukweli na mengine hayana ukweli lakini Mange siku zote amekuwa ni mtu wa kutoa taarifa mbalimbali ya kinachofanyika sehemu  mbalimbali , na ukiachana na mambo ya siasa anayoyafanya lakini pia amekuwa akitoa siri nyingi kuhusu wasanii na watu maarufu bongo.

Mange: Familia Ya Diamond Imemgeuza Wema Jinga Lao

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumwagia matusi mazito msanii wa Bongo movie Wema Sepetu baada ya kuzua maneno maneno jana kwenye mtandao wa Instagram.

Siku ya jana Wema alishika headlines za mitandao ya kijamii baada ya kuposti posti kadhaa zilizoamsha tetesi kuwa amerudiana na Diamond na alizidi kuzua maneno baada ya kuonekana akiwa na Esma huku wakiitana wifi.

Sio siri kuwa Wema na Mange wapo kwenye bifu kali tangu Wema afanye uamuzi wa kurudi CCM mapema mwaka jana akitokea Chadema na hata kuanzisha urafiki na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam jambo ambalo halikumfurahisha Mange.

Siku ya jana Mange amemtolea povu zito Wema na kumtuhumu anatumika kuleta drama zake na Diamond ilimradi wazime amsha amsha za maandamano na kudai amegeuzwa Jinga na familia ya Diamond.

Kupitia ukurasa wake Instagram, hili ndio povu la Mange kwa Wema:

Wema mjinga sana, mtu gani kutwa anatafuta attention za watu kwa mambo ya kijinga? Forever my wii my foot mbona Bi. Tukinao alivyokuwa nao mbona hawakukuita forever my wii? Yamewashinda kwa mganda ndio wamelikumbuka jinga lao. Janamke jinga halikui from CEO wa Endless Fame to mfanyakazi wa Wasafi Tv? Seriously wenzake wanasonga mbele lenyewe linarudi nyuma. Halafu hata halijistukii linaongea proudly kabisa “Sasa Diamond anaenda kuwa bossi wangu” from kuwa CEO mpaka kuwa mfanyakazi wa Diamond kama wakina Kifesi?”.

 

Hamisa Mobeto Akumbuka Wema wa Mange Kimambi.

Ikiwa  siku ya tarehe 4 March ni siku ya kumbukumbu ya mwanaharakati wa kimitandao Mange Kimambi , amepokea salamu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali huku yeye mwenyewe akisema kuwa hata baadhi ya upinzani wake waliweza kumtakia kheri ya siku hiyo ya kuzaliwa kwake.

Moja ya watu maarufu wanao-trend sana katika mitandao kwa sasa Hamisa Mobeto pia alikuwa ni mmoja walimtakia dada huyo kheri katika siku yake ya kuzaliwa lakini hii haitoshi kuelezea hisia zake hadi pale alipoamua kutoa shukrani zake za moyoni kuhusu mwanaharakati huyo na kwa jinsi alivyosimama nae kipindi cha matatioz yake.

Hamisa alimpongeza mwanadada huyo kwa siku hiyo lakini pia alimwambia kuwa anamshukuru sana kwai kipindi anapata matatizo ya kugombana na Zari na Diamond kila siki yeye hakuwahi kuonyesha kuchukia zaidi ya kumsapoti na kumtia moyo na hata wakati mwingine kutoa ushahidi wa ukweli kwa watu.

Happy birthday da mange @mangekimambi …wakati wengi waliniacha ulisimama nami  na pia wakati wngi walivyokuwa  hawaniamin you did..napenda kusema ahsante sana.

Mwenyezi Mungu ndo pekee anajua jinsi gani ulivyonipa nguvu  na ujasiri my dada.May Allah guide and protect you mama… na asante sana.-Aliandika Hamisa Mobeto katika ukurasa wake wa instagram.

Tukumbuke kuwa shukrani yake kwa Mange inakuja pale ambapo Hamisa alipokuwa akigombana sana na Diamond pamoja na zari kuhusu nani ni mmiliki halali wa mimba aliyokuwa nayo Hamisa, na hata mtoto alipozaliwa mange kimambi alishawahi kusema wazi kuwa mtoto ni wa Diamond Platinumz, siku zote ya vita kati aya pande hizi mbili Mange kimambi alikuwa akiandika posti za kumtia moyo Hamisa na ilipobidi kutoa ushahidi kwa kukandamizwa kwake Mange Kimambi aliweka ushahidi hadharani.

 

Wastara Amjibu Mange Kimambi Kuhusiana na Tuhuma Zake za Utapeli

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma amefunguka na kumpa majibu mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni Mange Kimambi baada ya kudai kuwa haumwi na anafanya maigizo.

Mange Kimambi alimtolea tuhuma nzito Wastara kuwa haumwi na anatumia pesa za michango kufanya biashara na hata alipofika India kwenye matibabu alirusha picha mtandaoni akiwa amechomwa dripu lakini Mange alisema dripu ile ilikuwa imechomekwa kisanii na ametapeli wananchi hela za michango.

Siku ya jana Wastara aliwatolea akitokea nchini India kwenye matibabu na kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 alimjibu mange Kimambi kuhusiana na tuhuma alizomrushia akidai kuwa ametapeli fedha za watu na serikali:

Kwanza siwezi nikamridhisha kila mtu kwa sababu mtu yule anayesema haya ni maigizo alafu kuna hamsini au ishirini wanamfuata hiyo tu inatosha kukuonyesha tofauti ya uelewa tulionao Watanzania Halafu watu wanasapoti kitu wasichokijua kisa tu Mange kawaambia sindano inaelekea chini lakini hajmwajafanya hata research kujua ukweli lakini siwezi kuwalazimisha wanielewe maana mwisho wa siku mimi na Mungu wangu ndio tunaujua ukweli wale wanaomuamini yule waache wamuamini cha msingi mimi nimetibiwa na nimerudi salama ingawa sijali na kabisa”.

 

Mange Kimambi Amtolea Uvivu Roma, ni Baada ya Kufungiwa na BASATA.

Mwanaharakati Mange Kimambi amefunguka na kuelezea jinsi alivyoipokea hukumu ya Roma kutoka kwa Naibu Waziri wa sanaa baada ya kuonekana kuwa nyimbo ya msanii huyo  inayojulikana kama kibamia kushindwa kuiboresha nyimbo hiyo na kukaidi agizo za kuondoa baadhi ya maneno.
Mange Kimambi ambae anasema kuwa hakutaa kulizungumzia swala hilo lakini mashabiki wamemuhamasisha kuongea hivyo kwaio ataongea kama vile lilivyo katika uhalisia.

                                                

Mange Kimambi anasema kuwa Roma alikuwa muoga sana katika kumtetea Mbunge Sugu ambae aliwekwa gerezani kwa shughuli za kisiasa ingawa alikuwa na bado  ni msanii mwenzao, Mange anasema kuwa Sugu ni moja ya wasanii jasiri waliweza kusimama bungeni na kutetea muziki wa hip-hop Tanzania,lakini pia Mange Kimambi anasema kuwa hawezi kumtetea Roma kwa hilo kwa sababu kipind yeye anatekwa Sugu alikuwa mstari wa mbele kumtetea Bungeni na kuhakikisha kuwa swala la kupotea kwake linashugulikiwa lakini cha ajabu Roma hakuwahi kufanya lolote pale Sugu alipokamatwa.

I think ni bora wasanii wanyooshwe ili wapate hasira.roma kumtetea sugu tu ni mpaka tumchambe kwanza  na sio kumtetea tu lakini pia hata kumpost ilikuwa anaandika caption as if  n mtu kavunja  sheria  akafungwa kawaida.yaani kama vile ambavyo watu walikuwa wakimpost kajala na lulu walipoenda jela..kama yeye kaamua kuwa muoga basi na sisi ni lazima tuwe waoga kumtetea yeye.mbona sisi tulimtetea yeye kwani hatukuwa na watoto na wajawazito, kwani sisi hatuwazi kufa na kuziachaje familia zetu?roma hata kwenye kesi ya sugu hakutokea, apambane mwenyewe.-Alifunguka Mange Kimambi.

 

 

Diva Ajifananisha na Mange Kimambi,Asema ni Mwanamke Mwenye Nguvu ya Ushawishi.

Mtangazaji wa kipindi cha ala za roho cha Clouds Radio kipindi pendwa kwa vijana Diva the bawse, amefunguka na kuelezea mapenzi makubwa aliyonayo kwa mwanaharakati anaevuma katika mitandao ya kijamii Mange Kimambi na kusema kuwa ni mwanadada mjasiri na mwenye nguvu kubwa ya ushawishi.Diva amesema kuwa mange kimbambi ni moja ya wanawake wenye akili za kipekee na mwenye  uthubutu wa kusema kile ambacho kina kuwa katika akili yake kwa kipindi hicho.

                                                                   

                                            mwanadada Diva the Bawse wa Clouds Radio.

Akiongea katika mahojiano na moja ya waandishi wanaofanya mahojiano na wasanii katika mtandao, Diva aliulizwa ni kitu gani kikubwa amekuwa akikipenda kwa Mange Kimambi ndipo alipofunguka na kusema haya .

Nampenda , yupo kama mimi,ana akili yake ya pekee yake tu kitu anachokiwaza kwenye akili yake ndicho anachokuwa anakisema kwa wakati huo.She is the most powerful womani in tanzania,unapozungumzia influencer she is number one kwakweli .Kila ukiamka asubui uwezi kuacha kuangalia amepost nini leo.She is like a sister to me,ana mambo mengi n pia anastyle yake ya kuandika stori zake kiasi kwamba anakuvutia kuendelea kuzisoma tu.

Mange kimambi ni moja ya wanawake wachache wenye wafuasi weni sana katika mtandao wa kijami hasa instagram kutokana kuwa mtoaji wa habari nyingi Tanznaia ingawa yeye mwenyewe haishi tanzania.amekuwa akiwahamasihsha watu wengi juu ya mambo mengi ingawa kwa sas hivi amejikita sana katika siasa.kKna mambo mengine ameuwa akiyatolea ufafanuzi na kuwafumbua watu juu ya mambo hayo.

Mange Kimambi: Diamond Ndio Alimuacha Zari

Tangu jana stori kubwa inayotawala kwenye mitandao ya kijamii ni kuvunjika kwa mahusiano ya Supastaa wa Bongo fleva na President wa WCB, Diamond Platnumz na mama watoto wake Mfanyabiashara Zari The Bosslady.

Siku ya Wapendanao Zari alitumia ukurasa wake wa Instagram kujulisha mashabiki zake kuwa yeye na Diamond wameachana lakini kikubwa zaidi alichoweka wazi Zari ni kuwa sio tu yeye na Diamond hawako wote bali yeye ndio amemwacha Diamond sababu ya kuchepuka ambapo aliandika:

There have been multiple rumors some with evidence floating around in all sorts of media in regards to Diamond constant cheating and sadly I have decided to end my relationship with Diamond..”.

Zari amejaribu kuweka wazi ijulikane wazi kabisa na  umma kuwa yeye ndio aliyemuacha Diamond kitu ambacho Mange ameibuka na kudai kuwa sio kweli na kudai Diamond ndio alikuwa wa kwanza kumuacha Zari kwa sababu alikuwa ameshamchoka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika maneno haya akimtuhumu Zari kwa kudanganya:

No no no honey, you didn’t leave Diamond, Diamond ndio alikuacha, mara ngapi Dogo alikuwa anakuonyesha kuwa hakutaki wewe ndio ulikuwa unamng’ang’ania? Ulivhotakiwa kusema leo ni kwamba umekubaliana na hali halisi kuwa dogo hatokaa kutulia kwa ajili yako. Wewe usituchezee akili eti umemuacha. Nyambaafu ulijua kuzaa fasta ndio kumkamata mwanaume! Umenyooooshwa”.

 

“Diamond Sio Mmiliki wa Diamond Karanga, Chibu Perfume Wala Wasafi Tv/ Radio”- Mange

Mwanaharakati wa mambo ya siasa mtandaoni, mrembo Mange Kimambi ameibuka tena na kumnyooshea kidole staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai yeye ni balozi tu sio mmiliki wa mali hizo.

Tangu siku za nyuma kuna habari zimekuwa zikienea kuwa Diamond sio mmiliki halali wa Diamond karanga na hata ilidaiwa kuwa karanga hizo zilikuwa zinaitwa Diamond karanga kabla hata ya kushikiliwa na Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika haya:

Hizi karanga zinaitwa Diamond karanga miaka na miaka, wamebadilisha rangi ya paketi na kurembesha ila jina la Diamond karanga ni la miaka yote ila zinatengenezwa na kampuni ile ile ya smart. Kilichotokea ni kwamba Joseph Kusaga alinunua ubia kwenye hicho kiwanda halafu akamleta Diamond aje amfanyie promotion na ndio maana wenye karanga zao baada ya tifu wametoa siri kuwa Diamond ni balozi wao tu”.

Lakini Mange hakuishia hapo pia amedai kuwa mali nyingine tunazozitambua kama za Diamond si zake ambazo ni perfume yake inayoitwa Chibu Perfume na pia vituo vya redio na televisheni anavyotegemea kuvizindua hivi karibuni vya Wasafi Tv na Radio ambapo Mange pia amesema;

Lakini pia Wasafi Radio na Wasafi Tv Joseph Kusaga ndio mmiliki wa asilimia 80 na Diamond anamiliki 20% ikimaanisha kuwa uwekezaji wote wa Wasafi Radio na Tv umefanywa na Joseph Kusaga. Lakini pia Wasafi Online ambayo wasanii wanatumia kuuza nyimbo zao 95% inamilikiwa na Kusaga. Chibu Perfume 100% inamilikiwa na Johainna Kusaga, mke wa Joseph Kusaga”.

Mpaka hivi sasa sio Diamond wala uongozi wake ulioongelea tuhuma hizo nzito zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii, ingawa kwa mtazamo wangu hata kama mali zote sio zake na yeye ni balozi tu haina shida ilimradi pesa inaingia kwenye akaunti kilichotakiwa ni kusema ukweli, Je wewe nini maoni yako? Tafadhali andika hapo chini.

Mange Kimambi Aibua Mapya Ugomvi wa Shilawadu na Mose Iyobo

Siku chache zimepita tangu kutokee ugomvi kati ya Moze Iyobo na waandaaji wa kipindi cha shilawadu(Soudy brown na Qwisar), ambapo baada ya waandaaji hao kutaka kufany interview na Aunty Ezekil kuhusu ugomvi aliokuwa nao na mrembo Tunda walifika katika pub yake na kumkuta Mose Iyobo ambae kwa inavyosemekana ni kuwa waandaaji hao walivamiwa na kupigwa vibaya na mzazi mwenzie na Aunty Ezekiel.

lakini wakiwa katikati ya kipindi cha shikawadu,Aunty Ezekiel aliwapigia simu waandaaji hao na kuwaomba radhi kuwa kitu hicho hakitajirudia lakini pia alimuombea mzazi mweznie msamaha na kusema atakapo rudi kutoka China watakuja kuyaongea na kuyamaliza.

Siku ya jana wasanii na wacheza dance wa wcb, walikuwa wakipost picha nyingi kuonyesha kuwa walikuwa pamoja na rc wa dar es salaam.ambapo baada ya picha hizo nyingi kusambaa katika mitandoa ya kijamii mange kimambi aliibuka na lake na kusema kuwa wasanii hao walialikwa kwa  mkuu wa mko kwa ajili ya kuwapongeza kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwapiga shilawadu.

Katika ukurasa wake wa Instagram Mange Kimambi aliandika,ndo wameenda kupongezwa na mkuu wa mkoa kwa kuwapiga shilawadu.ila sijui bashite angewafanya ni  shilawadu kama Magu angemruhusu  kuwanyoosha.

Ugomvi huo wa Mose na shilawadu unahusishwa na ugomvi kati ya shilawadu na mh makonda siku za nyuma na kusemekana kuwa kipigo cha shilawadu juzi ni kutokana na kutumwa na mkuu wa mkoa huyo ili kuwakomesha zaidi.

Hata hivyo bado kunaonekana vita ya  maneno inaendelea kati  kundi la wcb na waandaaji wa kipindi hicho huku wakitupiaa madongo gizani.

 

 

 

Mange Kimambi Apewa Siku Kadhaa Za Kuishi na Sheikh Mkuu

Mwanaharakati wa siasa mtandaoni mwanadada Mange Kimambi amejikuta ndani ya vita kali na sheikh Mkuu wa Dar es salaam Sheikh Alhad Musa Salim baada ya kumpa Mange siku kadhaa za kuishi duniani.

Sakata hilo lilianza siku chache zilizopita baada ya picha ya Sheikh huyo kusambaa mtandaoni iliyomuonyesha kama amekaa na mgombea CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia na wanachama wengine wa CCM na habari kusambaa mtandaoni kuwa alikuwa ametoka kuwapigia kampeni.

Baada ya picha huyo kusambaa Mange alimtolea uvivu na kumsema kuwa ni mnafki kwani ni siku chache zilizopita sheikh huyo alikuwa ametoka kuwasema Maaskofu waliokuwa wanaongelea siasa kwenye nyumba za Ibada yaani wanachanganya siasa na dini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange aliandika maneno haya:

Sio huyu sheikh majuzi aliwasema maaskofu waliomsema Raisi Magufuli kanisani na kusema wasichanganye dini na siasa yeye hapo anachanganya maharage na mahindi au? hana hata haya…haki wakina nabii Tito wapo wa dizaini nyingi”.

Baada ya maneno hayo aliyoandika Mange na maneno mengine kusambaa Sheikh Alhad aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kumtolea povu zito Mange. Sheikh Alhadi ameiongelea picha hiyo iliyosambaa mtandaoni na kusema picha hiyo ilipigwa Kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mtandaoni na kusema alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali ya raisi Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kusema Wema anautumia ulimi wake na mikono yake kutukana na kudhulumu watu na kuharibu heshima zao.

Sheikh huyo amesisitiza kuwa huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange Kimambi na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yoyote kwa ulimi wake na mikono yake kwa sababu amejihalalisha mwenyewe maangamizi kwa mikono yake amesema atamshtaki kwenye mahakama ya mbinguni.