Nandy Adai Yeye Ndio Msanii Mkali Wa Kike Bongo

Staa wa muziki wa Bongo fleva anayeendelea kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Ninogeshe’ Faustina Charles ‘Nandy’ ameibuka na kusema yeye ndio Msanii was kike anayeongoza Bongo.

Nandy amefunguka na kudai anaamini kuwa kwa sasa yeye ndio msanii wa kike ambaye amekuwa consistant na kushika chati za juice kutokana na ngoma anazotoa.

Kwenye Interview aliyofanya na Clouds Tv, Nandy amekiri kuwa yeye ni namba kwa kigezo cha namba ila anawaheshimu wale wote waliomtangulia kimuziki.

“Namba moja kwa Tanzania sasa hivi, au wewe unaonaje?, go with numbers, go YouTube, go Subscriber, go every where, go with numbers. Usiangalie tu nani anafanya nini, angalia numbers.

Kabla sijawa namba moja, namba moja yangu Lady Jaydee lakini bado nitamuheshimu, ni mkubwa amenitangulia. Yeyote yule ambaye amenitangulia lazima nimuheshimu kwamba ni mkubwa”.

Lakini pia Nandy amesema ingawa kuna wasanii wengi wakongwe anaowaheshimu kama Lady Jay Dee lakini haimaanishi wao watakaa Kwenye chati milele lazima wapishane kila mtu kwa nafasi yake atabeba chati.

Nandy Afanya Kufuru Apewa Mtaa Mahali anapokaa.

 

Nandy akiwa na moja ya viongozi wa mtaa huo.

Mwanadada Nandy anaendelea kuonekana mwenye mafanikio hasa baada ya kuonekana sehemu anayokaa kupewa mtaa wenye jina lake na balozi wa mtaa uo.akiwa kama msaani na kioo cha jamii watu wanaokaa katika mtaa huo wamemkubali na kumpenda na kuupa mtaa huo jina lake kama kumbukumbu.

katika video moja iliyoenea mtandaoni nandy alisikika akisema”asante sana balozi wangu kwa kunipa mtaani, ii ni kwa sababu ya kuisi na watu vizuri tangu nimefika hapa mkanikabithi plot na mpka sasa ivi mmeona kuna haja ya mimi kupewa jina la mtaa.”

Video Ya Ngono Yaendelea Kumtesa Nandy

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ameendelea kuandamwa na video yake ya ngono na aliyekuwa mpenzi wake Billnas.

Nandy ambaye kwa hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya Ninogeshe amekiri kuwa mpaka leo hii bado anapata kipindi kigumu kwa ajili ya ile video yake.

Nandy ambaye amekiri kuwa anatamani sana aweze kupanda usafiri wa umma maarufu kama daladala ili aweze kupata nafasi ya kukutana na mashabiki zake Uso Kwa Uso lakini ameweka iankuwa ngumu kutokana na ile video yake.

Kwenye mahojiano na Showbiz Xtra Nandy alisema kuwa, alipanga karibu mwezi mzima kufanya ziara hiyo ya kila sehemu atakayoenda atumie usafiri wa daladala ili aweze kupata nafasi nzuri ya kujua mambo mbalimbali ndani ya daladala na kuna wakati anazitamani stori za humo.

Nilipanga ndani ya mwezi mzima usafiri wangu uwe huo lakini mambo yakaingiliana na ya kusambaa ile video ya faragha kwenye mitandao ya kijamii, lakini bado dhamira yangu ipo nitafanya hivyo kwa sababu natamani kukutana na watu tofauti”.

Mwezi uliopita Nandy alipata fedheha hiyo baada ya video yake ya faragha na aliyekuwa mpenzi wake Billnas kusambaa Mtandaoni baada ya kukataa sio wapenzi kwa mara nyingi tu.

Nandy Ajiingiza Kwenye Ulimwengu wa Ujasiriamali (+picha)

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ameingia rasmi Kwenye ulimwengu wa ujasiriamali baada ya kutangaza bidhaa yake mpya.

Nandy amesema kuwa ameingia ubia na kampuni ya Grace Products inayojihusisha na utengenezaji wa sabuni za kuogea na vipodozi mbali mbali vya asili na yeye atakuwa ni moja ya wamiliki wa kampuni hiyo.

Nandy aliita waandishi wa habari kwa ajili ya kutangaza kuingia ubia na kampuni hiyo ya Grace Products na atakuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo na jina lake na picha zake zitatumika katika baadhi ya bidhaa hivyo kuwataka mashabiki zake wampe sapoti kwa kununua bidhaa hizo.

Ni wiki chache zilizopita Nandy aliongea na kumpongeza Ali Kiba kwa kinywaji chake cha Mo faya Lakini sasa ameamua kufuata nyendo zake.

Hizi ni baadhi ya Picha katika uzinduzi huo:

.

 

.

Nandy- Nategemea Kuolewa Hivi Karibuni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kwa Jina la usanii kama Nandy amefunguka na kuweka wazi kuwa anategemea Kuolewa hivi karibuni.

Nandy amefunguka Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi kuwa kuna mipango kabambe  ambapo ataolewa hivi karibuni huku akigoma kumwanika mchumba’ke akihofia nyakunyaku wa mjini.

Nimewaambia tu ninyi kwa sababu mmeniwahi kuniuliza, ukweli ni kwamba nitafunga ndoa soon, lakini kuhusu mwanaume wangu, naomba nisimwanike kwa sasa”.

Lakini pia Nandy ameongelea furaha yake aliyonayo kwa hivi sasa baada ya Kupitia kipindi kigumu kwenye maisha yake mwezi uliopita.

Unajua nimepita katika wakati mgumu sana, lakini sikumuacha Mungu kabisa na ndiyo maana hata haya yote yanayonitokea ya kupata mikataba na kufanikiwa hadi kununua gari ni kwa sababu kila kitu changu sasa kiko sawa kabisa”.

Mwezi uliopita Nandy aliposti a kipindi kigumu baada ya video yake ya ngono akiwa na mpenzi wake kwa kipindi hiko Billnas kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha kudhalilika kupita kiasi.

Nandy Adaiwa Kuhongwa Gari La Mamilioni

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT, Faustiana Charles maarufu kama Nandy amefungukia tuhuma alizotupiwa na kudaiwa kuwa gari aliliouza nalo sura hivi karibuni Kwenye mitandao ya kijamii amehongwa.

Wiki iliyopita kuna picha na video zilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Nandy akionyesha gari lake jipya alilodai amenunua hivi karibuni aina ya Mercedes Benz E-Class E320 CDI.

Lakini Kumekuwa na tetesi zinazosema kuwa Nandy amenunuliwa gari hilo kama zawadi na kigogo ambaye anamuweka mjini kwa hivi sasa taarifa ambazo Nandy amezikataa kata kata.

Kwenye Interview na Risasi Jumamosi, Nandy alisema kuwa, gari hilo alilinunua kwa zaidi ya shilingi milioni 70 za Kitanzania kwa jasho lake na hiyo ilitokana na kuingia mikataba na makampuni mbalimbali Tanzania yakiwemo ya michezo ya namba, shirika moja kubwa la ndege na mingineyo.

Watu wengi wanajua kuwa kuna mtu ameninunulia hili gari, lakini siyo kweli kabisa, mimi mwenyewe nina madili mengi ya kufanya na ndiyo yameniwezesha kupata fedha za kununua Benz, yaani kifupi ni jasho langu mwenyewe”.

Nandy Amekuwa akifanya vizuri na ngoma yake mpya ya Ninogeshe ambayo imeshika chati mbali mbali nchini.

Ninogeshe ya Nandy Yamfunika Ommy Dimpoz

Msanii wa kike Nandy ambae anatamba na wimbo wake wa Ninogeshe amkalisha chini msanii mkongwe pia Ommy Dimpoz na wimbo wake wa Yanje ambao pia ulitoka siku chache zilizopita,  nyimbo hizo ambazo zote zinaonekana kuwa zinazopendwa sana  na watu tangu zimetoka zimekuwa zikibadilishana nafasi kwa muda mrefu na sasa nandy amemkalisha ommy kwa nafasi moja.

Siku chache za nyuma msanii ommy dimpoz alisema kuwa hawezi kuangaika kufanya kiki ya kitu chochite ili kuweza kuifanua nyimbo yake ifanye vizuri, zaidi sana anaamini kuwa nyimbo zake za mwanzo zilishamtengenezea jina kubwa la kuweza kutoa wimbo wowote ili kuweza kuhit.

Nandy anakuwa moja y wasanii wa kike wanaofanya vizuri sasa katika muziki na kuwakalisha kina dada wengine wengi kutokana na kipaji chake ambacho amekuwa akikitendea haki.

Nandy Amnyooshea Mikono Ali Kiba Akiri Kumkubali

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT Nandy amekiri kuwa pamoja na mambo mengine yote na maneno yakiwekwa pembeni staa wa Bongo fleva Ali Kiba amemu-insipire sana kwa kinywaji chake.

Nandy amekiri kuwa hatua aliyofikia Ali Kiba ya kuingiza kinywaji chake mtaani ambayo ni Energy drink ni hatua kubwa sana ambayo imempa changamoto hata yeye ya kufanya makubwa zaidi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na The Playlist ya Times, Nandy amekiri kuwa kupitia Kiba ni vizuri wasanii wengi wakajifunza kuwa ni vizuri kuwekeza nje ya muziki.

Ameni-inspire kwa kinywaji kwa sababu ukiangalia the package ya kinywaji chake jinsi ilivyo ni project fulani ambayo ipo serious”.

Lakini pia Nandy ameongelea uwekezaji wa wasanii wengine kama Diamond Platnumz ambaye ni mmoja kati ya msanii Lakini pia mfanyabiashara.

Tunaambiwa nje ya kuimba tunatakiwa tuwekeze nje ya muziki wetu na ndicho hiki kaka zetu wanafanya ukimuangalia kama Diamond, Alikiba ni vitu ambavyo wanatuhamasisha”.

Kwa hivi sasa Nandy anafanya vizuri sana ngoma yake ya Ninogeshe inayoshika namba moja kwenye mtandao wa Youtube.

Makampuni ya Nguo za Ndani Yalinitafuta Kufanya Matangazo Lakini Nilikataa_Nandy

Mwanadada Nandy siku ya jana alikuwa na mahojiano na waandishi wa habari wa Clouds Media, na baada ya hapo alipata bahati ya kuongea na Millard Ayo ambapo Nandy alifunguka na kusema kuwa makampuni mengi yalimfuata ili kufanya nae kazi hasa ya kutangaza  kutangaza nguo za ndani.

Hii ilikuja baadaya nandy kuvujisha video akiwa amevaa nguo ya ndani tu akiwa na mpenzi wake Bilnass hivyo hiyo iliwafanya baadhi ya makampuni kuanza kumsumbua kufanya nae matangazo ya chupi.

Akiongea na millard ayo ,Nandy alisema

watu wa nguo za ndaniwalinitafuta sana,watu wengi sana na kuweka madau tofauti tofaut hadi na pedi walinitafuta pia , lakini siwezi kufanya kitu kama hicho kwa sababu hata kipindi kitu hicho kinatokea sikufanya kama makusudi  na nimeniumiza sana na kipo moyoni bado mpaka sasa.siwezi kuchukulia ilo kama fursa na mimi nikakaa na nikaanza kutangaza jamani chupi hii ni kama yangu.

Nandy anasema kuwa hawezi kufanya hivyo kwa ajili ya pesa kwa sababu ana vyanzo vingine vya kumpati apesa labda miaka mitano mbeleni kama mtu ataona kuwa chupi yake itampendeza ndipo atafanya baishara ya matangazo a chupi lakini sio sasa hivi.

Nandy- Nilitaka Kuacha Muziki Kisa Video Chafu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy amefunguka na kudai alikuwa tayari kuacha muziki baada ya ile video yake chafu kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki chache zilizopita Nandy aliwaacha watu midomo wazi baada ya video yake iliyomuonyesha akiwa kitandani na aliyekuwa mpenzi wake Billnas kivujishwa Kwenye mitandao ya kijamii.

Nandy amekiri kutaka kuacha muziki Kwenye mahojiano na Kipindi cha leo Tena cha Clouds Fm ambapo amezidi kufunguka haya:

Nilihisi kukata tamaa kuachana na muziki kabisa sikuona maana ya maisha. Lakini nilipofika BASATA walinipa ushauri na kunihoji binafsi sikuwa na picha mbaya nyuma katika maisha yangu kama kweli nilivujisha picha zile kwa ajili ya Kiki.

Hali yangu ilikuwa mbaya sana nilipoona ile video sikuamini kabisa macho yangu. Nilizidiwa na Pumu nikakimbizwa hospitali kifupi nilipata Brain Attack niliwaza kuhusu familia yangu nItamtazamaje mama na baba yangu?”.

Nandy jana aliachia wimbo wake mpya ulioandikwa na msanii mwenzake Aslay unaoitwa Ninogeshe.

Nandy Akana Kuvujisha Video Yake Ya Ngono

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy amekana kabisa taarifa zilizoenea kuwa yeye mwenyewe kwa mkono wake ndiye aliyesambaza video yake ya ngono na Billnas kisa kiki.

Wiki chache zilizopita Nandy na Billnas wali trend vibaya mno baada ya kuonekana kwenye video iliyovuja Mtandaoni wakiwa kitandani wakifanya mambo yao.

Kwenye mahojiano aliyofanya leo na kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, Nandy amekanusha kuwa video yake na Billnas haikuwa mpango wa kiki kama  wengi wanavyodhani na taarifa za kusambaa kwa video hiyo zilimuathiri kiafya kiasi cha kupoteza fahamu mpaka kukimbizwa hospitalini.

Ile video haikuwa kiki na wala sonata tabia ya kufanya kiki, wakati video inasambaa milioni huwa simu na meneja wangu kuniuliza na kiukweli baada ya kuiona ile video nilihisi sio mimi niliishiwa nguvu na uongozi wangu unasema niliishiwa fahamu kwa masaa kadhaa”.

Tangu video hiyo itokee nandy amekiri kuwa katika wakati mgumu kwani ni siku chache zilizopita kuna video iliyo trend ikimuonyesha akiangua kilio stejini hadi kushindwa kupiga shoo na meneja kumtoa stejini.

Nandy: Siyo Sahihi Kujirekodi Ukiwa Mtupu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy amefunguka a kuweka wazi kuwa kuvuja kwa video yake ya mahaba chumbani na aliyekuwa mpenzi wake Bilnass imemfunza mambo mengi ikiwemo sio vyema kujirekodi ukiwa uchi.

Sakata hili lilimkuta Nandy wiki iliyopita baada ya video yake akiwa chumbani na mpenzi wake Billnas wakiwa wamevaa nguo za ndani huku wakiwa nikaona ya kimahaba kuvuja mtandaoni na kusababisha tafrani.

Nandy amefungukia majuto yake kwenye mkutano na waandishi wa habari aliofanya alipotoka katika ofisi za mamlaka ya mawasiliano Tanzania na kuweka wazi kuwa amejutia sana kitendo hiko na sasa yupo tayari kushirikiana na serikali kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu:

Nipo Tayari kushirikiana na serikali kwa hilo lililotokea na kuelimisha wasanii, wanafunzi na jamii kwa ujumla najua watu wengi wanapitia hatua kama hizi na wengine hata hawajulikani lakini kwa kuwa limetokea kwangu Ilan najua kuna watu wengine wamefanya mambo kama haya na video zimeenda mitandaoni bila idhini yao”.

 

Diamond Akiri Kuwa Yeye ni Bingwa Wa Kiki na Drama

Supastaa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekiri kuwa yeye ni bingwa wa kutafuta kiki mitandaoni Lakini pia anajulikana kwa kuwa na drama zisizoisha.

Diamond amekiri hayo kwenye mkutano aliofanya na waandishi habari siku ya jana katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kujuzwa mambo kadhaa kuhusu sheria za mitandao.

Diamond ameongea hayo na kuomba radhi kwa mashabiki zake na serikali baada ya kuachia video mbili tofauti zilizomuonyesha akiwa na wanawake wawili huku akifanya matendo yaliyotafsiriwa kinyume na maadili ya Kitanzania.

Na mimi ni miongoni mwa mabingwa wa kiki, najikubali, najua kabisa drama ninazo kila siku lakini tunaziweka vipi zisiende kuwatia dosari viongozi ambao wanapambana kuhakikisha sanaa yetu inafika mbali,

Kwa sababu ikienda kwa mazingira ambayo yalikuwa yamezoeleka huko nyuma unawavunja moyo viongozi ambao wanapigania sanaa ifike mbali”.

Lakini pia kwenye mkutano huo pia Nandy aliomba radhi pia kwa kusambaza video yake ya chumbani na Billnas ambayo ilivuja wiki chache zilizopita.

Mh Mwakyembe Aagiza Nandy Kukamatwa

Mh Waziri wa habari na michezo, Harrison Mwakyembe ameagiza kukamatwa kwa msanii wa muziki wa kizazi kipya mwanadada  Nandy baada ya kusambaa kwa video zake chafu na kufikishwa kituo cha polisi kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi zaidi.

Majibu hayo yamekuja baada ya Mh  Goodluck Mlingwa  mbunge kutoka Morogoro alipouliza ni hatua gani za serikali zimekuwa zikichukuliwa ili kupambana na wasanii wanaweka picha za uchi na matuzi katika mitandao.

Hata hivyo, Mwakyembe amethibitisha kuwa mpaka sasa msanii Diamond Platinumz bado yuko polisi alikofikishwa tangu jana kwa ajili ya mahojiano baaada ya kuvujisha video akiwa na wanawake tofauti akiwa faragha.

Tulitunga sheria mwaka 2010 lakini tulikosa shaeria za kubana wasanii  katika maudhui hasa katika upande wa mitandao.tumeshazitunga hizo kanuni na sasa hivi zimeshaanza kufanya kazi.kuna baadhi ya vijana wamekuwa wakifanya uhuni uhni katika mitandao ya kijamii sana na tumeanza kuwafanyia kazi , yupo msanii Diamond Platinumz ambae  amefikishwa polisi tangu jana kutokana na kusambaa kwa picha zake chafu, hata hivyo pia binti nandy pia inabidi akamatwe ahojiwe..

Diamond Afikishwa Polisi Baada Ya Video Yake Kuvuja Mtandaoni

Mwanamuziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefikishwa polisi jana kwa ajili ya mahojiano baada ya kusambaa kwa video zake zisizo na maadili katika mitandao ya kijamii.

Jamiiforum wnaripoti kuwa hayo yalisemwa na Waziri wa habari, Michezo, Utamaduni na sanaa Dr.  Harrison Mwakyembe akiwa bungeni wakati akijibu swali juu ya kanuni za maudhi ya Mitandaoni aliloulizwa na Mbunge Goodluck Mlinga.

Aidha Dkt. Mwakyembe amesema Msanii Faustina Charles (Nandy) naye atahojiwa na Polisi kufuatia video yake ya faragha akiwa na Msanii mwenzake Billnass kusambaa mitandaoni.

Waziri Mwakyembe amesema kwa sasa wanaangalia  taratibu za kuwafikisha mahakamani.

Nandy Aomba Radhi Mashabiki na Jamii Nzima kwa Ujumla.

Mwanadada nandy kupitia ukurasa wake wa instagram amekubali kosa na kuwaomba msamaha watu wote walioiona na kuguswana hata kuharibu mahusiano yake na mashabiki.

Nandy ameomba msamaha baada ya kuvuja kwa video ilikuwa ukimuonyesha billnass na nandy wakiwa chumbani kitandani huku wakiwa katika hali ya kimahaba na kuvujisha siri waliokuwa wakiificha kwa muda mrefu kuwa wako katika mahusiano ya kimapenzi.

         Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi sana sana  ndugu zangu,familia yangu na rafiki zangu wote kwa kile kilichotokea,bado siki sawa naomba mniombee uzima.

Nandy na Billnass hawatokuwa wasanii wa kwanza Tanzania kuwa na skendo chafu ya ngono kwa kutupia picha hizo katika mitandao ingawa kila mmoja anakataa kukubali kosa la kuwa ndio chanzo cha video hiyo kuenea katika mtrandao.