Yaliyojiri Mahakamani Kwenye Kesi ya Wema Sepetu.

Siku ya jana tarehe 12 march mwaka 2018, Wema Sepetu alionekana tena katika viwanja vya mahakama ya kisutu akiwa na mama yake na watu wake wa karibu kusikiliza kesi yake inayoendelea juu ya madawa ya kulevya iliyoanza tangu mwaka uliopita.

Akitoa ushahidi wa kesi hiyo , mjumbe wa shina  namba 39 anapokaa Wema Septu ametoa ushahidi wa siku ya upekuzi wa kesi hiyo na kusema kuwa siku ya tukio la kupekuliwa kwa nyumba ya Wema Sepetu hakukutwa na bangi bali ilikuwa ni kipisi cha sigara.

Shahidi huyo aliejulikana kama Alphonce  aliyaongea hayo katika mahakama ya kisutu mbele ya Jaji Thomas Simba akisaidiana na wakili wake  Costantine Kakula na kusema kuwa  alikuwepo na alishiriki katika kupekua nyumba ya wema na walikutana na kipisi cha sigara. Alphonce anasma kuwa ingawa haujui bangi ikiwa katika matumizi lakini alishawahi kuona siku moja akiwa mkoani shinyanga ikiwa shambani.

 

Mama Kanumba Afunguka Kulizwa na Wema Sepetu

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba ‘Florah Mtegoa’, Mama Kanumba amefunguka na kudai kuwa Wema Sepetu amemfanyia kitu mbaya hakutegemea.

Mama Kanumba amedai kuwa hivi karibuni aliwasilisana na Wema Sepetu na kukubaliana wakutane na ndipo Wema alipomuita nyumbani kwake Salasala jijini Dar es salaam lakini amedai alipofika getini hakufunguliwa geti.

Inadaiwa kuwa majirani waliokuwa maeneo hayo walimuona mama huyo akiwa amesimama kwa muda mrefu bila kufunguliwa na wamekiri kuwa ni tabia ya Wema kutofungua geti la nyumbani kwake kama huna appointment yoyote kwake.

Kwenye Interview aliyofanya na gazeti la Ijumaa, Mama Kanumba alifunguka na kukiri kuwa jambo hilo lilitokea ambapo aliongea na Wema hivi karibuni kwa simu ambapo walikubaliana aende nyumbani kwake na ndipo alipokodi bajaji mpaka kwake na alipofika alikuwa akigonga geti walinzi walimwambia hawajapewa maagizo yake na alikuwa akimpigia simu hapokei.

Jamani inauma nyie mtu nimekubaliana naye vizuri unakodi bajaji mpaka kwake kulivyo mbali lakini hajali wala hapokei simu nikaamua kuondoka zangu”.

Mama Kanumba amedai kuwa walikuwa na maongezi ya kawaida tu kwani alikuwa mkwe wake na alikuwa anampenda lakini pia amefunguka na kusema amesikitishwa kwani mpaka hivi sasa hajaombwa radhi na Wema.

Wema: Zari Alimuacha Diamond Kwa Mambo Aliyomfanyia Huko Nyuma Sio Kisa Mimi

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amefunguka na kusema anaamini Zari alimuacha Diamond kwa mambo yao waliyotofautiana kipindi cha nyuma lakini sio kisa yeye alimkumbatia.

Baada ya Zari kutangaza kumuacha Diamond alifanya Interview na BBC Swahili na aliweka wazi kuwa amemuacha aliyekuwa mpenzi wake supastaa wa Bongo fleva Diamond kwa sababu ya yeye kukumbatiana na Wema kwenye party.

Wema na Diamond walikuwa pamoja kwa miaka kadhaa huko nyuma na wamekuwa na tabia ya kuachana na kurudiana hata Diamond amedaiwa kuchepuka kwa wapenzi wake wapya na Wema hivyo alivyoonekana tu Wema wanakumbatiana ikaonekana tayari.

Lakini Wema amekataa tuhuma za Zari kuwa amemuacha kisa yeye Kwenye Interview aliyofanya wikiendi iliyopita na Bongo 5 Wema Alitalia maneno haya juu ya suala hilo:

Zari alikuwa ana sababu nyingi sana za kupanick za nyuma za Diamond za mambo yao wenyewe lakini sio hiyo ya juzi ya mimi kumkumbatia Diamond kama rafiki atakuwa ana jingine”.

Lakini pia Wema aliweka wazi kuwa pamoja na yeye na Diamond wameachana kipindi kirefu kilichopita lakini bado wana chemistry ambayo haiwezi kuisha.

Wema alipotakiwa kumshauri kitu chochote Zari alifunguka na kusema kuwa hawezi kuwa mshauri wa Zari kuhusu Mahusiano yake na Diamond.

“Mimi na Diamond ni Marafiki Hakuna Kingine Kinachoendelea”- Wema

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amesisitiza na kusema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Diamond zaidi ya urafiki na ukaribu wa kawaida.

Tetesi za wawili hawa kurudiana ziliibuka mwezi uliopita baada ya Wema kuibuka kwenye moja ya party za WCB na kuanza kukumbatiana na Diamond kimahaba kabisa na ishu hii ilizidi kupamba moto baada ya Zari kukiri kumuacha Diamond kisa kumkumbatia Wema.

Diamond na Wema Enzi za mapenzi yao

Tangu sakata hilo Diamond ameshakataa tuhuma hizo na kusema yeye na Wema ni marafiki tu hawana uhusiano mwingine wowote na Wema pia ameibuka na kuthibitisha hilo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Wema alifunguka na kusisitiza kuwa yeye na Diamond wamebaki kuwa marafiki wa karibu tu:

Mimi na Diamond ni marafiki ni marafiki wazuri, nadhani kinachowafanya wengi washangae ni kwa sababu mimi na yeye tulikuwa hatuongei kwa muda mrefu tangia tulivyoachana lakini sahivi tumeamua kukua na we decided to just put all those things behind us na maisha yaendelee kwaiyo hakuna cha kushangaza mimi kuongea naye au akinikaribisha kwenye party za WCB lakini kilichowashangaza ni mimi kuenda kwenye partu akaja kunisalimia mimi and Diamond we did not kiss nilimhug I hug my friends”.

Wema ameendelea kusisitiza kuwa yeye na Diamond ni marafiki tu hakuna cha zaidi na mambo aliyofanya na Diamond pale anaweza kufanya na mtu mwingine yoyote ambaye ni rafiki wa kawaida.

Wema Azidi Kumwaga Sifa Kwa RC Makonda

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amezidi kumwagia sifa na kuonyesha kumkubali sana mkuu wa moja wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.

Wema Sepetu na RC Makonda walisemekana kuwa kwenye bifu hii ilikuwa mwaka jana baada ya Makonda kumtaja Wema kwenye listi ya watu wanaotumia madawa ya kulevya na kisha Wema kufiki uamuzi wa kuhama Chama na kuhamia Chadema.

Mwaka jana mwishoni kabisa disemba Wema alitangaza kurudi CCM na siku chache tu baada ya kurudi CCM Wema alionekana pamoja na RC Makonda wako pamoja wakipiga stori na hata kupiga picha na kuziweka mtandaoni.

Tangu hapo Wema kaheuka shabiki namba moja kwa Makonda yaani humwambii kitu kuhusu Makonda na jana usiku kupitia ukurasa wake wa Instagram alimuweka Makonda na kumuandikia ujumbe uliopita gumzo:

And he keeps doing what he does best….My RC…. Mtumishi wa Mungu….Hujalazimishwa Kupenda lakini….Gudnyt world”.

 

Baba Dimpozi Afananisha Malezi ya Ommy na Tatizo la Wema

Baba mzazi wa Ommy Dimpoz ambae juzi alifunguka na kusema kuwa hataki kusikia wala kumuona mwanae huyo akija katika mazishi yake siku ya kifo chake kwa sababu mtoto huyo amekuwa hamjali hata kidogo kipindi cha uhai wake ilhali mtoto huyo sasa hivi ana hali nzuri kimaisha na anashindwa kumkumbuka baba yake.

Swala la wazazi kulalamika kuhusu watoto wao hasa wasanii limekuwa sio swala geni katika tasnia kwa sababu tatizo hilo limekuwa likiibuka kila kukicha na kama utakumbuka ni hivi juzi juzi tu baba mzazi wa msanii mkubwa Dimaond Platinumz alitamka maneno ya hasira sana kwa mtoto wake huyo wa kiume.

Baba Ommy Dimpoz anasema kuwa pamoja na kwamba anahisi kosa lake ni kutokujihusisha na malezi ya Ommy Dimpozi kipindi cha ukuaji wake lakini anaamini kuwa hata swala la kumleta Duniani tu ilikuwa ni swala tosha la mtoto huyo kumjali na kuheshimu.

Hata hivyo baba Ommy Dimpoz anasema kuwa amekuwa akisikia jinsi Wema Sepetu ambavyo  anahangaika kupata mtoto lakini mwisho wa siku unaweza kukuta mtoto huyo  akashindwa kumsaidia mama yake lakini hiyo haibadilishi swala ya yeye kuwa mzazi.

mfano kama nikifa leo wala asije kunizika au kukanyaga Tabora , kwanza akija atasema nani amefariki, watampiga maana kipindi niko hai tu wala hanijali.Ni kama Wema Sepetu sasa hivi anavyohangaika kutafuta mtoto siku hakimpata hata kama hawezi kumsaidia lakini bado atamshukuru Mungu tu na mimi ni hivyohivyo, huwa namshukuru Mungu kuwa nimemleta Ommy Duniani.-Alifunguka baba huyo.

Wema Sepetu Adaiwa Kutumia Bangi Kama Starehe

Kesi ya muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu imeendelea kuunguruma kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu ambapo Wema anakabiliwa na kesi ya kukutwa na msokoto wa bangi.

Siku ya jana shahidi wa tatu upande wa mashtaka anayejulikana kwa jina la Mary amefunguka na kuieleza mahakama kuwa mshatakiwa Wem Sepetu alimwambia kuwa anatumia bangi kama starehe tu.

Mary amedai kuwa tarehe 4 February 2017 alipewa maelekezo na mkuu wake wa kazi amtoe Wema mahabusu na kumpeleka nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya ukaguzi, amedai kuwa walipokuwa njiani alimuuliza kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kuuza madawa ya kulevya Wema alijibu kuwa hauzi madawa bali anatumia bangi kama starehe.

Shahidi huyo amefunguka kuwa siku hiyo tukio walienda kufanya ukaguzi kwenye nyumba ya Wema huko Kunduchi Ununio ambapo alikutwa na misokoto ya bangi na alikiri mara ya mwisho kuvuja bangi ilikuwa siku ya jumatatu.

Kesi ya Wema imehairishwa na itasikilizwa tena tarehe 12 na 13 ambapo mashahidi watendelea kutoa ushahidi.

Akaunti ya Instagram ya Wema Sepetu Yarudishwa Baada ya Kushikiliwa Zaidi ya Mwezi.

Kwa muda mrefu msanii wa bongo movie na aliyekuwa mrembo wa Miss Tanzania mwaka 2006  Wema Sepetu ilikuwa imeshikiliwa na watu wasiojulina na hata kubadilisha matumizi ya akaunti hiyo na kumfanya madame Wema Sepetu kutokuwa karibu na mashabiki wake kwa muda mrefu.

Akaunti hiyo ambayo ilichukuliwa na kuanza kutumika kwa baishara ambazo Wema Sepetu hakuwa anazifanya imerudishwa baada ya mafundi na watu wa karibu wa mwanadada huyo kuangaika sana na kufanikiwa kuirudishwa kwake.

Upoteaji wa akaunti hiyo ya Wema Sepetu ulizua ugomvi na uadui kati ya Wema Sepetu na mwanaharakati Mange Kimambi kwa kile kilichodaiwa kuwa Wema Sepetu alikuwa akimtuhumu Mange Kimambi kuwa ndie alikuwa ameshikiria akaunti hiyo.

Akitihibitisha kurudi kwa akaunti yake Wema Sepetu aliposti katika akaunti hiyo na kuandika”alhamudulilah am baaaack…this time for real…thank you Tizzo wangu.”

 

Zari: Wema Amevuruga Penzi langu na Diamond

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Zarinah Hasssan ‘Zari the Bosslady’ amerudi tena kwenye headlines mwishoni mwa wiki hii baada kufanya Interview kwa mara ya kwanza baada ya kutangaza kumuacha Diamond rasmi.

Siku ya Valentine’s Zari aliushangaza uma wa watu baada ya kutangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa ameamua kumuacha mpenzi wake na Baba watoto wake kwa kile alichodai ni michepuko imesababisha.

Lakini Zari ametaja sababu kubwa ambayo imepelekea yeye kuachana na Diamond ni mpenzi wake wa zamani (Ex wake) Wema Sepetu.

Wiki chache zilizopita video na picha zilizomuonyesha Wema na Diamond wakikumbatiana na kushikana hadharani kwenye party ya WCB.

Zari amefunguka mengi Kwenye mahojiano aliyofanya na BBC Swahili nchini Uingereza, London ambapo ameweka wazi alifikia uamuzi wa kumuacha Diamond baada ya kuona picha na video akiwa anakumbatiana na Wema Sepetu kusambaa kila kona Kwenye mitandao ya kijamii:

Kwanza hakuwa ametegemea mimi kuposti vile Instagram kutangaza kumuacha kwa sababu nilikaa mwenyewe muda mrefu nikafikiria mwishowe nikaamua tuishie hivyo”.

Zari amezidi kufunguka na kueleza kuwa walikuwa katika jitihada za kuuweka uhusiano wao kwenye mstari ulionyooka baada ya usaliti aliomfanyia uliompelekea kuzaa na Hamisa lakini alimuumiza zaidi alivyoona video akiwa anakumbatiana na Wema kwenye mitandao ya kijamii.

Unakaa leo unasikia hiki kesho unasikia kile kukumbatiana na ma-EX kwenye public kufanya vitu vya kunidhalilisha mimi na watoto wangu na unaona kabisa sio sawa na mtu ukiamua kuwa na familia unatakiwa vitu vingine unataka kama nimeshakukubali kuwa wewe ni msanii kutakuwa kuna vitu vingine unafanya lakini kuna vitu unatakiwa uweke stop ili kuiheshimu familia yako”.

Zari amefunguka na kusema baada ya kuona Diamond anapiga picha anakumbatiana na Wema kwenye social media aliamua kumblock kila sehemu hivyo alikuwa hana mawasiliano naye ya aina yoyote kuanzia hapo mpaka siku ya Valentines alipoamua kumuacha.

Zari amefunguka na kusema tangu amuache Diamond Kwenye Instagram hajawahi kuongea naye Tena wala kuwasiliana naye wala hajawaona watoto wao.

Wema Sepetu Aingilia Kati Ugomvi wa Zari na Diamond

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu ameingilia kati na kutoa yake ya moyoni kuhusu kinachoendelea hivi sasa kati ya wapendanao Diamond na Zari.

Wiki iliyopita siku ya Valentine’s Day Zari alishangaza wengi baada ya kutangaza kumbwaga aliyekuwa mpenzi wake na baba watoto wake Diamond huku akidai sababu kubwa ni skendo na uchepukaji wake uliokithiri.

Tangu waachane Wema amekuwa akitajwa sana na watu mbali mbali huku tetesi zote zikidai kuwa Wema amerudi kwa Diamond jambo ambalo limekuwa likisemwa kwa muda mrefu tangu kabla hata Diamond hajaachana na Zari.

Wema amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na uhusiano wa Diamond na Zari na kuzungumzia hasa kinachoendelea hivi sasa baina yao ambapo kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online Wema alisema yafuatayo:

Kama kweli wameachana basi wayamalize tu na maisha yaendelee ingawa mapenzi hayaingiliwi warudiane ili walee watoto wao kwa pamoja”.

Lakini pia Kwenye interview hiyo aliyofanya na Dizzim Online Wema alifunguka kuhusiana na Account yake ya Instagram ambayo imeibiwa kwa wiki kadhaa sasa ambapo amesema kuwa anawaomba mashabiki zake kuwa na moyo wa subira kwani bado anaendelea  na jitihada za kuirudisha mikononi mwake.

 

 

 

 

Picha za Wema,Esma na Wcb Zazua Mjadala Mitandaoni.

Huku bado mahusiano ya kimapenzi katika ya Diamond na Zari yakiwa bado hayajakaa sawa baada ya Zari kusema kuwa hana mapezni tena na Diamond Platinumz kutokana na kuwa na tetesi nyingi za kuwa na wanaume tofauti tofauti, huku upande wa pili mambo yanazidi kupamba moto kutokana na ukaribu walionao Wema Sepetu na Esma Platinuzm .

Wema Sepetu ambae ni miss tanzania inasemekana kuwa ni ndo chanzo kikubwa cha kuwafanya Zari na Diamond kuachana baada ya kuonekana kuwa karibu na Diamond siku za hivi karibuni anazidi kuoneka kuwa karibu na wasanii wa wcb na  dada yake Diamond ambae pia siku za nyuma ilisemekana kuwa hayupo kribu na kaka yake wala aliyekuwa wifi yake (Zari) kwa madai kuwa wawili hao walikuwa wana mgogoro.

Tetesi za Esma kuwa na chuki na Zari zinaanza kuthibitika kwa sababu ya ukaribu mkubwa aliyonao na wema ambapo hapo mwanzo kipindi mwanadada huyo amegombana na Diamond hawakuwa kama walivyo sasa na hata kuanza kuonekana katika events mbalimbali za lebo hiyo.

wakioenaka kuwa karibu siku ya uzinduzi wa club ya Rommy Jonnes inayojulikana kama Octagon, Wema Sepetu alikuwa karibu na kila msanii kutoka wcb, huku kampani yake kubwa ikiwa na Esma ambae ni dada yake na Diamond.

                                                                

Wema sepetu akiwa na wasanii wa wcb.

                                                                        

                                                                Alichoweka Esma snapchart

 

                                                         Alichokipost Wema snapchart .

Kesi ya Wema Sepetu Yahairishwa Tena

Kesi inayomkabili msanii wa bongo movies Wema Sepetu iliyokuwa imesikilizwa mara nyingine tena jana, imeharishwa tena mpka hapo February 26 mwaka huu.

Wema Sepetu ambae aliwasili jana viwanja vya mahakama ya Kisutu akionekeana asiye na wasiwasi akiingia kwa madoido katika mahakama hiyo huku  akiwa na wakili wake mpya Albert Msando baada ya yule aliyekuwa nae mwanzo kumbaga (Peter Kibatala) waliwasili pamoja na kuingia mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo.

Hata hivyo baada ya kesi hiyo kusoma, moja ya mashaidi aliewasilisha ushaidi wa mkojo wa Wema kutoka kwa mkemia mkuu huku wakili wa Wema akimuoji maswali yaliyomfanya shaidi huyo kuwa na kigugumizi muda mwingine.

Hata hiuvyo shaidi huyo amekiri kuwa wakati wa kufanya upekuzi katika nyumba ya Wema hawakufanya upekuzi katika chumba anacholala Wema zaidi ya chumba chake cha kulalia na chumba cha dada wa kazi ambapo walikutana na misokoto miwiwli ya bangi huku mmoja ukionekana kuwa ulishatumika.

Shaidi huyo ambae ni Inspecta wa polisi alipoulizwa kuhusu ni muda gani walitumia kukaa nje ya ofisi ya mkemi mkuu kusubiri sampuli ya mkojo wa wema alijibu kuwa hakumbuki muda  huo.

Kesi hiyo ya wWema inayomkabili kuhusu madawa ya kulevya itasoma tena February 26 na 27 mwaka huu.

Wema Sepetu Afika Mahakamani na Wakili Mpya,ni Alberto Msando

Baada ya wakili aliekuwa nae mara ya kwanza katika kesi inayomkabili ya madawa ya kulevya kumtema na kumuacha njia aliyekuwa akijulikana kama Peter Kibatala leo hii msanii wa bongo moviea  na aliyewahi kuwa Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu ameripoti leo katika kusikiliza kesi hiyo akiwa na mwanasheria mpya.

wema sepetu ameingia  mahakama ya kisutu akiwa na mwanasheria wake huyo mpya maarufu anaejulikana kama Albert Msando kwa ajili ya kusikiliza muendelezo wa kesi hiyo ambayo tangu imeanza bado inaendelea kusikilizwa huku kesi za wasanii wenzie zikiwa tayari zilishakwisha.

Wema anaendelea kusikiliza kesi hiyo ambapo anatuhumiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumvani kwake ununio mwaka 2017 wakati wa sakata la kamata kamata ya wasanii na watumiaji wa madawa ya kulevya, kampeni iliyoanzishwa na Mh. Makonda.

                                                 

                     Wema akiingia mahakamani na mwanasheria mzoefu Albert Msando.

                                                

                                             

                    Wema akiwa mahakamani hapo akisubiri kesi yake kuitwa.

Nilishamwambia Wema Atakuja Kupata Mtoto- Chuchu Hansy

Muigizaji wa Bongo movie Chuchu Hansy ameonekana kumkingia kifua msanii mwenzake wa Bongo movie, Wema Sepetu kuhusu suala lake la kuzaa mtoto.

Kwa kipindi kirefu Wema amekuwa akiweka wazi hisia zake juu ya watoto na kusema kuwa anapenda kuwa na mtoto siku moja lakini pia ameweka wazi wakati mgumu ambao amekuwa akipata katika jitihada za kupata mtoto.

Kipindi cha nyuma Wema alishawahi kuweka wazi kuwa miaka ya nyuma alishawahi kutoa mimba ya aliyekuwa mpenzi wake kwa kipindi hiko msanii Marehemu Kanumba, lakini tangu aweke wazi taarifa hiyo amekuwa akisakamwa mtandaoni na maadui zake ambao kila siku akimposti mtoto basi watamsema kwa nini hazai na vitu vingine.

Sikh ya birthday ya mtoto wa Ray na Chuchu anayeitwa Jayden , Wema alimposti mtoto huyo kwenye ukurasa wake Instagram jambo lililozua balaa kwani mashabiki walimvamia na kuanza kumnanga na kumuita mgumba tasa na majina mengine.

Kitendo kile hakikukaa vizuri na Chichi ambaye kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa TV alifunguka yafuatayo:

Kusema kweli zile comments zilikuwa nyingi sana lakini nyingi zilikuwa ni za kumuumiza mtoto kawekwa pale badala ya kusema happy birthday Jaden mtu anamuandiki liukurasa kabaisa maneno ya kumuumiza sijui mgumba sijui tasa hayo nimaisha na ni kipindi tu wao sio Mungu kama walimsema Ray ni tasa lakini leo hii Mungu kawaonyesha kampa mtoto kwaiyo na Wema asubiri kwa sababu siyo tasa alishabeba mimba mara ya kwanza lakini nilishamwambia Wema wewe utakuja kupata mtoto lakini sio pale unapohitaji wewe pale Mungu atakapopenda upate”.

Mama Diamond Amkingia Kifua Wema.

Mama mzazi  wa msanii Diamond Platinumz amekuwa ni mzazi anakuwa mstari wa mbele katika kumsapoti mtoto wake na hata kufikia hatua ya kugombana na mashabiki wake katika mitandao pale anapoona kuwa mtoto wake anakuwa ameandamwa sana.

Wikiendi hii kulikuwa na party ya kumtambulisha msanii mpya katika kundi  la wasafi ambapo mwandada Wema Sepetu alikuwa ameharikwa katika party hiyo.Swala la uwepow a mwandada huyo lilizua gumzo kubwa kwa mashabiki wake na hata kuanza kumtukana Wema na familia ya Diamond kwa kusema kuwa wamekuwa wakisapoti uchafu anaofanya ndugu yao.

Kwa kuonyesha kuwa hajali maneno hayo ya watu mama Diamond alipost moja ya video zilizosambaa sana katika mitandao ambayo ilikuwa ikiwaonyesha Wema na Diamond wakiwa katika muonekano wa kimahaba na kuandika kuwa watu waongee tu lakini wao wanapiga hela.

 Katika ukurasa wake wa instagram mama yake diamond alionyesha kuwa aamekuwa hakiyaona maneno yao lakini wao wanaingiza hela kupitia amneno yao.kwa herufi kubwa nyie hongeeni,chambeni cc tunapiga hela.

Ikiwa bado kuna lile fukuto la Zari kumwambai mAma Diamond wahame madale na kwamba wamuachie Diamond guest house ikiwa ni dongo kubwa kwa Doiamnd , hakuna aliyetaka kuamini kuwa mama Ziamond angeweza kuandika hivyo kwa kumtetea diamond na mtoto wae ilhali wengi waliamini kuwa mama huyo yuko upande wa zari ambae kwa sasa inasemkana kuwa hana mahusiano mazuri na mzazi mwenzie Diamond Platinumz.

Hizi Ndio Picha na Video Mpya za Wema Sepetu Zilizozua Gumzo

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu amerudi tena kwenye vichwa vya habari huko kwenye mitandao ya kijamii kwani amekuwa akitrend tangu Jana usiku yote kwa sababu ya picha mpya.

Wema ametupia picha hizo na video alizopiga kwa ajili ya fashion line inayoitwa Mac Couture ambayo Wema amefanya kazi ya kuwatangazia magauni yao.

Baada ya picha hizo kusambaa Wema aligeuka kivutio kutokana na jinsi lile gauni lilivyomtoa na kupelekea kila mtu kuweka neno lake juu ya vazi hilo.

Hizi ni baadhi ya picha na video zilizozua makubwa huko Instagram: