Wema Sepetu Aendelea Kukwepa Habari Za Kukatwa Utumbo

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu alijikuta katika wakati mgumu mapema wiki hii baada waandisha wa habari kumbana kuhusu taarifa zake za kukatwa utumbo nchini india.

Baada ya Wema kushindwa kufika mahakamani  chache zilizopita kuna taarifa zilienea kuwa Wema alienda India kwa ajili ya kukatwa utumbo ili apunguze unene aliokuwa.

Lakini tangu mwanzoni Wema amekuwa akikataa taarifa hizo na kudai yeye ni mzima lakini alikiri kiwa alienda India kwa ajili ya matibabu kutokana na ugonjwa mwingine ambao hajauweka wazi.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Wema alikubali kuwa alikuwa anaumwa lakini aligoma kuweka wazi alikuwa anaumwa ugonjwa gani hasa:

Ni kweli hapa katikati nilikuwa anaumwa lakani namshukuru Mungu nimepona. Siwezi kuzungumzia nilikuwa naumwa nini hiyo ni privacy yangu, sasa kama video mliiona ndio ni kweli nilikuwa naumwa lakini kuhusu ugonjwa hapana”.

Habari ya Wema kukatwa utumbo ili kupunguza mwili ilipamba moto Wikiend iliyopita baada ya kuonekana akiwa amepunguza kilo za kutosha tu Kwenye mashindano ya Miss Morogoro.

Wema Adaiwa Kuzama Ndani Ya Penzi Zito

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amedaiwa kuwa ndani ya Penzi Zito na mfanyabiashara Lawrence Masanja maarufu kama ‘R.a.h.u.r’.

Gazeti la Ijumaa wanaripoti kuwa tetesi za uhusiano wa Wema na R.a.h.u.r zilianza kuibuka miezi kadhaa iliyopita kwenye mtandao wa Instagram baada ya Wema kuibuka mshindi wa Muigizaji Bora wa Kike na Chaguo Bora la Watu kupitia tuzo zilizofahamika kama Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF).

Ujumbe huo ulisomeka:

People’s choice & Best Actress, Ni category kubwa sana. Hongera kwa ushindi huo, you deserve, i’m proud of you. #Maso.”

Baada ya Ujumbe huo Wema alijibu:

I’m glad i made you proud my love. It won’t stop, I promise you”.

Mapema wiki hii, R.a.h.u.r aliibua gumzo lingine kwa kuonesha picha ya fedha na kuelekeza mashabiki wake kuwa anaelekea Morogoro ambako inaaminika Wema pia atakuwa mkoani humo kwa ajili ya mashindano ya urembo yanayotarajiwa kufanyika wikiendi hii.

R.a.h.u.r

Baada ya Tetesi hizo kupamba moto gazeti hilo lilimsaka R.a.h.u.r ambaye alifunguka:

Kiukweli mimi huwa sipendi media,” alijibu. Alipoendelea kubanwa zaidi, aliingia mitini“.

Lakini Wema naye aliposakwa na gazeti hilo alikana Mahusiano hayo na kudai ni marafiki tu.

Mimi huyo ni mshkaji wangu tu wala hakuna kinachoendelea”.

 

Hukumu Ya Wema Sepetu Kusomwa Ijumaa

Hukumu ya Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu imesogezwa mbele mpaka mapema wiki hii siku ya Ijumaa ambapo itasomwa Tena.

Wema ameweka wazi kuwa hukumu hiyo iliyotangazwa kutolewa leo imehairishwa kutokana na hakimu kutaka muda zaidi wa kuweza kufanya uchunguzi wa kina.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Wema amefunguka haya kuhusu hukumu yake:

Hakimu kasema kuna vitu ambavyo anatakiwa kuvifanyia uchunguzi zaidi kwa undani hivyo amesema mpaka Ijumaa ndio atatoa hukumu”.

Mwaka jana Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili mnamo tarehe 23 Aprili 2018 walikutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana kukabiliwa na kesi ya kutumia Madawa za kulevya.

Wema ni Mzuri na Ana Umbo la Asili:-Neema Ndepanya

Mwanadada Neema Ndepanya ambae ni moa ya wasanii wa bongo movies lakini pia menea wa mwanadada wema sepetu amefunguka na kumtetea Wema Sepetu kwa kusema kuwa watu wamekuwa wakimzushia Wema kuwa ana fake umbile lake lakini hiyo sio kweli kwa sababu wema ni mzuri na ana umbile la asili.

Hayo yote yanakuja baada ya mwanadada Wema Sepetu kusemekana kuwa alikwenda ne na tetesi zikidai kuwa ni kutokana na kuwa na umbile kubwa lenye manyama uzembe mengi yaliyomchosha hivyo alikwenda nje kwa ajili ya kufanya upasuaji ili kupunguza mwili huo.

Meneja huyo alikanusha safri hiyo ya Wema na kusema kuwa alikwenda kufanya check -up ya mwili wake na sio vinginevyo.

Wema ana umbile la asili hawezi kwenda kokote kutengeneza umbile lake,wema ni mzuri na ndivyo alivyo zaliwa kwaio kama ku-maintain atamaintaini tu kwa kufanya mazoezi na vitu vingine, lakini nje alikwenda kufanya mazoezi kwa ajili ya afya yake tu.

 

Brown Mauzo Yupo Tayari Kuwa Spea Tairi Kwa Wema Sepetu

Msanii maarufu kutoka Mombasa Kenya Brown Mauzo amefunguka na kudai ana mapenzi mazito kwa Muigizaji wa Bongo movie Supastaa Wema Sepetu.

Kwenye mahojiano yake na kipindi cha Enews cha East Africa Tv, Brown amesema kuwa amekuwa akivutiwa sana na Wema Sepetu na yupo tayari muda wowote kumuoa mrembo huyo hata kama ikibidi awe spea tairi.

Mimi namzimia sana Wema Sepetu kwa bahati mbaya sijawahi kuonana naye namzimiaga sana, kila mtu anasema ukweli kutoka moyoni kila shetani na mbuyu wake. Licha ya kwamba alikuwa na nani sijui na nani ila mimi nipo tayari kumuoa, na popote atakapokuwa namwambia mimi nampenda na nataka kumuoa.. hata kama akiwa na mtu mwingine mimi nipo tayari hata niwe spea tairi”.

Brown amemwagia Wema Misifa kibao huku akidai ni mwanamke ambaye amekaa na ameona anafaa kuwa mke wake wa ndoa.

Brown Hana Hadhi Ya Kutembea na Wema Sepetu- Kelechi

Msanii wa muziki anayefanya kazi zake  Mombasa Kenya, Kelechi amefunguka na kudai msanii mwenzake Brown Mauzo hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu.

Siku chache zilizopita Brown Mauzo aliibuka na kufunguka juu ya mapenzi yake kwa msanii wa filamu Tanzania Wema Sepetu na kudai anataka kumuoa jumla jumla.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Kelechi amefunguka na kudai Brown hawezi kumuoa Wema Sepetu wala hata kumuhudumia hawezi:

Huyu Brown ni mtoto mdogo sana hawezi kumpata Wema Sepetu alafu isitoshe ni Dogo sana kwa Wema na pia hana hata hadhi ya kuwa  naye kimapenzi”.

Lakini pia Kelechi amedai Brown amekimbia Mombasa na kurudi Tanzania baada ya kutembea na mke wa Meneja wake.

Wema Atangaza Rasmi Kumaliza Bifu Na Muna

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ametangaza Kumaliza rasmi bifu lake na aliyekuwa rafiki yake wa siku nyingi Muna Love ili waishi kwa Amani na Upendo.

Wema amefunguka hayo siku ya  Jumamosi, Julai 7, 2018 katika viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar wakati wa kuaga mwili wa mtoto Muna, Patrick aliyefariki dunia Nairobi nchini Kenya, Julai 3 na kuzikwa siku ya Jumamosi katika Makaburi ya Kinondoni.

Pole zangu ziende kwa wazazi wa Patrick ambao ni Muna na Patrick, Muna ni rafiki yangu wa muda mrefu, nisingemjua Muna basi nisingemjua Patrick. Nilimpenda sana Patrick, japo sijabahatika kupata mtoto lakini nafahamu maumivu mnayopitia kwa kupoteza mtoto wenu“.

Muna pole sana, najua ulivyompenda Patrick, na mapenzi yako kwake ndiyo yametufanya hata sisi tuwe hapa leo, mimi huwa napenda sana watoto, najua hakuna mzazi anayependa kumzika mwanaye, ninaamini Mwenyezi Mungu atakupa nguvu wewe na baba Patrick.

Ninaomba tuyaache ya mitandaoni, najua mtoto wenu atafurahi huko aliko akiona mnaupendo na hakuna mgawanyiko kama huu ambao tumekuwa tukiuona. Muna unajua nakupenda na nitaendelea kukupenda, yaliyopita si ndwele tugange yajayo”.

Miaka miwili iliyopita Wema na Muna waliongia Kwenye bifu zito Kwenye mitandao ya kijamii na hata kuvunja urafiki wao.

Hata Baba Yake Muna Tulimzika kwa Peter:-Wema Sepetu

Mwandada wa sepetu amefunguka na kuzungumzia  mkanganyikounaoendelea kati ya familia mbili za wazazi wa patrick ambapo wazazi hao wawili wamekuwa wakigombania maiti ya mtoto aliyefariki hivi karibuni.

akiwa kama rafiki ya muna hapo awali kabla hawajagombna a, wema sepetu anaelezea sababu kubwa iliyomfanya yeye na mama yake kwenda kuhani msiba na kusubiria maiti nyumbani kwa peter mwananyamala na sio mbezi kwa muna kama mama mzazi wa mtoto anavyosema.

alielezea sababu iliyomfanya aonekane katika msiba ni kwaba aliwahi kuishi na patrick kwaio hawezi kuacha kuja kwenye msiba kwa sababu ameishi na mtoto na msiba umemuuma sana.

ki ukweli msiba umeniuma sana kwa sababu patrick ni mdogo na alikuwa akinijua na nimeishi nae muda mrefu but hivyo vingine sijui.

Lakini pia akielezea kuhusu mahali sahihi msiba unapotakiwa kuwepo, Wema anasema kuwa yeye ameamua kuja kwa peter kwa sababu anavyojua yeye misiba ya muna imekuwa ikifanyika pal na hata msiba wa baba yake muna ulifanyika hapo.

mimi sijaongea na Muna chochote kuhusu msiba lakini nimekuja hapa kwa sababu misisba yote tunafanyia hapa , hata msiba wa baba yake muna tulifanyiaga hapa na tulizika hapa kwaio hayo mengine mimi sijajua

Meneja Ajikanyaga Kuhusu Ugonjwa wa Wema Sepetu

Meneja wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu anayejulikana kama Neema Ndepanya amejikuta akikosa cha kujibu baada ya kuulizwa kuhusu hali ya kiafya ya Wema Sepetu.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi nyingi Kwenye mitandao ya kijamii zinazodai Wema alienda nchini India wiki chache kwa ajili ya kukatwa utumbo.

Wema na uongozi wake walikataa tetesi hizo na kusisitiza kuwa yeye ni mzima wa afya lakini taarifa hiyo imeingia doa baada ya video yake ikimuonyesha anaumwa hoi hospitali kusambaa mtandaoni.

Baada ya kuvuja kwa video hiyo,Risasi Jumamosi lilimsaka Wema ili kupata ukweli juu ya afya yake lakini kama kawaida yake simu iliita bila kupokelewa na lakini walipompigia Meneja wake alipokea na kujikanyaga na kupata kigugumizi:

Jamani nipo mbele ya watu hapa siwezi kuongelea suala hilo nitakutafuta baadaye tuongee”.

Lakini alipotafutwa hakutaka kuongea tena Lakini pia Mama Wema alipotafutwa alidaiwa kuporomosha matusi ya nguoni bila majibu yoyote.

Gigy Money Asema Hamjui Wema Sepetu

Mwanadada Gigy Money ambae hakosi kuwa na drama kila siku anasema kuwa hamjui mwana dada Wema Sepetu na kwamba yeye ndie msani pekee wa kike ambae anafanya vizuri kwa sasa kuliko msanii mwingine yoyote hapa bongo .

Akiongea kwa kujiamini gigy money anasema kuwa kutokana na madili anayoyapata sasa hivi yanayomuingizia hela hakuna msanii wa kike wa kumlinganisha nae wa sasa.

Swala la gigy money kuwa akisema hawajui baadhi ya mastaa hapa bongo liekuwa la kawaida kwake kutokana na kuwa na tabia ya kusema hivyo mara kwa mara kwa baadhi ya mastaa wakubwa .

Gigy money  ambae baada ya kujifungua alianza kufanya kazi na kusaini mikataba mbalimbali  ya kumuingizia pesa ansema kwa sasa hakuna msanii wa kike bongo anaemfikia.

Wema Atoa Shukrani kwa Niaba ya Rc Makonda

Mwanadada wema sepetu amejitokeza katika ukurasa wake wa instagram na kuwashukuru wananchi wote wenye imani na Rc Makonda  kwa kufikisha followers million moja katika ukurasa wa kiongozi huyo ambae kwa upande wake anasema kuwa ni moja ya viongozi wanaopendwa sana na watu na ni kiongozi wa kwanza kufikisha idadi hiyo ya wafuasi.

katika ukurasa wake wa instagram, wema sepetu aliandika “ndugu zangu wapendwa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kumfikishia follower 1m  mr dar es sallam….hongera kakangu kwa kufikisha 1m followers, umebreak record ya viongozi wote wenye flowers wengi ..unakubalika kakangu…wasiokukubali tunajua matatioz yao…ila mi ugomvi siwezagi”

Wema Sepetu na makonda kwa sasa wamekuwa karibu kama kaka na dada ukiachilia mbali sakata la madawa ya kulevya na kesi yake inayoendelea ambayo  ni kampeni iliyoanzishwa na Rc huyo.

Yasemekana Wema Sepetu Mgonjwa Sana.

Kuna  video inasambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonyesha Wema Sepetu akiwa mgonjwa na akiwa maeneo ya hospitali ,habari zinazosambaa zinasema kuwa wema sepetu amelazwa katika hospitali moja wapo huko jijini Dar Es Salaam huku sababu kubwa ikiwa bado haijajulikana kuwa ni nini.

Hivi karibuni kuna habari zilisambaa kuwa mwanadada huyo alikwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kukata utumbo ili kupunguza mwili.

Taarifa zilizowahi kutolewa na mwanadada Mange Kimambi zinasema kuwa Wema Sepetu aliamua kusafiri na kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupunguza uzito na mwili mkubwa.

 

 

Kajala- Sina Urafiki na Wema, Nina Marafiki Wapya

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja amefunguka kuhusu urafiki wake na msanii mwenzake Wema Sepetu na kudai kwa sasa hawana urafiki tena.

Wema na Kajala walikuwa marafiki wakubwa sana mara baada ya Wema kumlipia Kajala shilingi milioni 13 katika kesi yake lakini urafiki huo ulivunjika baada ya Kajala kumsaliti Wema na kumuibia mwanaume wake.

Baada ya uadui wa miaka kadhaa mwaka jana Wema na Kajala walionekana kulimaliza bifu lao baada ya Wema kumtumia Kajala salamu za siku ya kuzaliwa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers  Kajala anaweka wazi kuwa hana urafiki na Wema na kusisitiza ana rafiki yake mwingine ambaye amemtaja:

Kuhusu suala la urafiki wangu na Wema yameshapita hayo na mimi kwa hivi sasa nina marafiki zangu wengine kabisa na rafiki yangu kipenzi ambaye anajua mambo yangu yote ni Lamata”.

Lakini pia Kajala alikataa Tetesi za kutaka Kuolewa na Kigogo hivi karibuni lakini amekiri ana mpango wa unalipa Kwenye mjumba wake wa kifahari.

Meneja Wa Wema Akana Tetesi Za Wema Kukatwa Utumbo

Meneja wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Neema Ndepenya amekana tetesi zilizoenea Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema amekatwa utumbo.

Wiki iliyopita Mwanaharakati wa siasa Mtandaoni Mange Kimambi aliuambia uma wa Watanzania Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa Wema amekatwa utumbo.

Mange alidai kutokana na kuzidiwa na uzito mkubwa (ubonge) Wema alipata ofa ya kwenda nchini India kwenda kukatwa utumbo kwa ajili ya kupunguza kilo.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Neema alisema habari hizo zilizozagaa mtandaoni si za kweli bali ni za nia ya kumchafua staa huyo kitu ambacho wao wamekipuuzia.

Unajua kuna habari nyingine unasikia wala kichwa chako hakiwezi kuuma hata kidogo kwa sababu ni za kizushi, Wema alikwenda India kwa matibabu yake binafsi”.

Wema alikwenda nchini India hivi karibuni na kuzua gumzo baada ya kushindwa kuhudhuria kesi yake ya madawa ya kulevya katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar na ndipo ilipotoka taarifa ameenda kufanyiwa upasuaji lakini haijajulikana ni upasuaji gani alienda kufanyiwa.

Wema Aanza Kujitetea Mahakamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imeaza kusikiliza utetezi wa mshtakiwa ambaye ni muigizaji, Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili, Angelina Msigwa na Matrida Abass, baada ya mahakama hiyo kuwaona wana kesi ya kujibu katika mashtaka yanayowakabili ya kutumia dawa za kulevya.

Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. ambapo wote kwa pamoja wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.

Watuhumiwa hao wameanza kujitetea mbele ya Hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na washtakiwa hao wanatetewa na wakili Alberto Msando ambaye alikuwa akiwaongoza katika kuwauliza maswali juu ya nini wanafahamu kuhusiana na tukio hilo kuanzia Februari 4, 2017 hadi walipofikishwa polisi.

Kwa nyakati tofauti watuhumiwa hao wameeleza kila kitu wanachokifahamu juu ya tukio hilo ambapo hakimu Simba alikuwa akiandika kile walichokuwa wakieleza.

Kwa upande wa mashtaka, umeongozwa na wakili wa Serikali, Constantine Kakula, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 16 mwaka huu ambapo hakimu atatoa uamuzi.

Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4 mwaka huu, nyumbani kwao Kunduchi Ununio , Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam.

Wema Afika Mahakamani Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Nchini India

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu alifika mahakama ya Kisutu siku ya jana baada ya kutoka nchini India Kwenye matibabu na kufanyiwa upasuaji.

Wema anakabiliwa na kesi ya kutumia madawa ya kulevya na kesi yake imekuwa ikiendelea kusikilizwa tangu mwaka jana.

Wema alifika na wafanyakazi wake wawili wanaokabiliwa na kesi ya kutumia dawa ya kulevya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,  wataanza kujitetea Juni 19, mwaka huu.

Wema na wenzake walipaswa kuanza kujitetea leo Juni 13 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba,  na kwa upande wa mawakili ni Cosstantine Kakula wa Serikali na Wakili wa Utetezi, Albert Msando.

Lakini hata hivyo watuhumiwa hao walishindwa kujitetea siku ya jana kutokana na kwamba Hakimu Simba alikuwa na kazi nyingine na kesi imeahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu ambapo washtakiwa wataanza kujitetea.