Harmorapa- Nimeumizwa Sana na Kitendo Cha Wema Kutangaza Ndoa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa amefunguka na kuweka wazi kuwa hisia zake zimeumizwa baada ya mwanamke anayempenda kutangaza Kuolewa na mwanaume mwingine.

Harmorapa ambaye amekuwa muwazi tangia Mwanzoni kuwa anampenda Wema na kutamani kuwa naye kimapenzi ameonekana kukata tamaa ya kuwa naye baada ya Wema kutangaza ndoa na mpenzi wake PCK.

Harmorapa ameeleza kuwa labda haikupangwa kwa yeye kuwa na Wema Sepetu ndio maana hadi sasa hajafanikiwa kuwa naye, hivyo amenyoosha mikono juu kuhusu hilo.

Siku chache zilizopita Wema alimuanika hadharani mpenzi wake PCK na kumuita Mume wake mtarajiwa lakini pia PCK amekiri kuwa anategemea kumuoa Wema hivi na inasemekana kuwa hivi sasa Wema yupo nchini Burundi kwa ajili ya kutambulishwa kwa ndugu wa PCK.

Kama Utakumbuka kuwa kwenye uzinduzi wa movie mpya ya Wema Sepetu, D.A.D uliofanyika Mlimani City wiki kadhaa zilizopita Harmorapa aliibuka na kumkabisha Wema zawadi ya ua kama ishara ya upendo wake kwake.

Harmorapa Apata Dili Nono la kuwa balozi

Msanii wa bongo fleva Harmorapa amepata dili kubwa katikamoja ya kampuni za usafirishaji nchini inayojulikana kama moovin.

Kampuni hiyoimemtangaza Harmorapa na moja ya watangazaji wa kipindi pendwa katika Clouds Media cha XXL kama mabalozi wao kwa sasa katika maswala na huduma wanazotoa katika jamii.

Akiongea baada ya kutangazwa kuwa balozi wa kampuni hiyo, Harmorapa anasema kuwa anamshukuru mungu na kampuni hiyo kwa kutambua nafasi yake katika kufanikisha huduma zao na anaamini kuwa nafasi hiyo itamfungulia milango mingine mingi.

Hamorapa aliwahi kuwa balozi wa kinywaji cha swala hapo awali ambapo mkataba wao uliisha.

Harmo Rapa Adai Anajutia Kuwa Mtu wa Kiki

Msanii wa Bongo fleva Harmorapa ambaye pia ni maarufu sana Instagram kwa kupenda kutafuta kiki ameibuka na kudai anajutia sana kutafuta kiki kutokana na kinachoendelea hivi sasa.

Harmo Rapa amekuwa Kwenye headlines kwa sababu yeye na Mrembo anayeitwa Khadijah wamekuwa wakijibizana ambapo msichana huyo anadai yeye na Harmorapa ni wapenzi lakini mwenyewe anakataa na kudai msichana huyo anatafuta tu kiki na hawana Mahusiano.

Sakata hilo lilitokea siku ya Ijumaa iliyopita ambapo kwenye studio za EATV katika kipindi cha Friday Night Live, Harmorapa na Khadijah waliingia kwenye ugomvi baada ya Khadijah kudai anaweza kuthibitisha kuwa ana Mahusiano ya Kimapenzi na Harmorapa na kudai ana kovu Kwenye sehemu za siri.

Baada ya kuambiwa hivyo basi Harmorapa aliondoka Kwenye studio hizo kwa hasira na kufanya mahojiano na Kipindi cha Enews cha EATV ambapo amedai kwa sasa anajutia kiki yake na Khadijah.

Harmorapa amekiri kuwa yeye kutangaza kuwa Khadija ni mpenzi wake ilikuwa ni kiki tu lakini hampendi msichana huyo imemkera Khadija kwani amekuja juu na kumtaka Harmorapa amlipe pesa zake alizompa kwa ajili ya kiki hiyo jambo lililomfanya Harmorapa Akiri anaachana na kiki.

Harmorapa Adai Moyo Wake Upo Kwa Wema, Achora Tattoo Ya Jina Lake

Msanii wa hip hop Harmorapa ambaye anajizolea umaarufu kwa vituko vyake amefunguka na kudai anampenda Wema na amechora Tattoo mpya ya Jina lake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Harmorapa amefunguka na kudai mwanamke ambaye anajitangaza kuwa ataolewa na Harmorapa ni muongo kwa sababu hana Mahusiano naye.

Harmorapa amefunguka na kudai hana mpango wa kumuoa mwanamke aliyetoka Mwanza kwa ajili yake aliyejitambulisha kwa jina la Khadijah na kudai anataka kumuoa Wema.

Harmorapa amedai kwamba zile picha zinazosambaa Kwenye mitandao ya kijamii zilikuwa ni clip za Kwenye Movie mpya ambayo amecheza naye lakini sio wapenzi.

Harmorapa amefunguka na kudai hana mpango wa kumuoa mwanamke aliyetoka Mwanza kwa ajili yake aliyejitambulisha kwa jina la Khadijah na kudai anataka kumuoa Wema.

Lakini pia Harmorapa amefungukia mapenzi yake kwa Wema Sepetu na kudai anampenda kupita kiasi na Yupo Tayari kumuoa muda wowote na hata kukiri kuchora Tattoo ya Jina na lake Kwenye shingo.

Siku za nyuma Wema ameshawahi kumtolea povu Harmorapa na kumtaka aache kujitangaza Kwenye vyombo vya habari kuwa anampenda kwani alikuwa anamkera.

Harmorapa Afatwa Dar kwa Ajili ya Kufunga Ndoa na Mwanamke kutoka mwanza

Msichana aliejulikana kwa jina la khadija ambae hivi karibuni picha zake akiwa na Harmoarapa zilisambaa sana katika mitandao ya kijamii kuwa wana mahusiano ya kimapenzi , amefunga safari kutoka  jijini mwanza na kuja dar kwa ajili ya kufunga ndoa na msanii huyo.

Licha ya kuwa Harmorapa amekanusha tetesi za kutembea na mwanadada huyo  ambae amechora mpaka tatoo yenye jina la harmorapa , lakini mwanadada huyo anaonekana kuwa na mapezni ya dhati na kuahidi mpaka kumlipia gharaa zote za harusi .

Khadija anasema kuwa amekuja dar kwa ajili ya kufunga ndoa na harmorapa kwa sababu walikutana  mwanza na walikubaliana kuwa watafunga ndoa hivi karibuni.

nimekuja kufanya maandalizi ya harusi na baby wangu harmorapa,mara ya kwanza harmorapa alikuja kwenye show mwanza, kwa sasa tuna kama miezi miwili tangu tukutane na  ninamlea.

Lkini pia khadija amesema kuwa yuko tayari kugharamia kila kitu kinachohusu harusi kama harmorapa yuko tayari kwa hilo.

Harmorapa Aomba Radhi kwa Mashabiki.

Msanii wa muziki Harmorapa ameomba radhi mashabiki zake baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao ya kiamii ikimuonyesha yeye akiwa na mwanamke anayesemekana kuwa na mpenzi wake wakiwa kitandani.

Harmorapa anasema kuwa amekuwa akipokea simu nyingi sana zikimhoji kuhusu swala la picha hzio huku akisikia taarifa kuwa TCRA wameona picha hzio na wanampnga wa kumchukulia hatua kali.

Ustaarabu haununuliwi wala sifhani kama kuna chuo kinachotoa kozi ya ustaarabu kwa kweli,na kukaa kwangu kimya isiw sababu ya kutembelea nyota yangu.Naheshimu sana idara ya mawasilianoa nchini,napenda hata siku moja nije nishikane mkonona waziri kama msanii mwenye heshima nchini TANZANIA.

Picha zinazosambaa eti mimi na dada mmoja ambae sina uhakika sana kama namjua ila tulikutana katika kazi ya sana huku mwanza  na kuchukua video na kuposti huo ni ushamba.nsema mimi sio type yako na wala sina muda wala mpango wa kufunga ndoa na wewe.

Mpenzi wa Harmorapa Nae Achora Tattoo.

Mwanadada aliejulikana kwa jina la Madam Ziot ambae hivi karibuni picha zake zilisambaa sana katika mitandao ya kijamii akiwa na msanii wa muziki Harmorapa ameamua kuchora tattoo ya mpenzi wake huyo katika maneo ya mkono wake.

Harmorapa amabe hapo awali ilisamba kuwa amepata mwanamke mpya mwenye makazi yake huko Mwanza na kuwa mwanamke huyo amekuwa akimlea na kumpa kila kitu ameamua kuwafunga watu midomo kwa kuchora tatoo yenye jina la Harmorapa.

Haijajulikana kama kweli wawili hao kweli wapo katika mahaba mazito au kuna kiki tu wamekuwa wakitafuta kutokana na matukio ya kiki za Harmoarapa.

 

Harmorapa Amezaliwa kwa Sababu ya Kiki:-Mkali Wenu

Msanii Vichekesho nchini mkali wenu amefunguka na kusema kuwa msanii Harmorapa sio mwanamuziki  bali yupo kwa ajili ya kiki tu na sio kitu kingine.

Mkali wenu anaongezea na kusema kuwa Harmorapa anakuwa hasikiki kwa sababu hana kitu cha kufanya kwa sasa ambacho kinaweza kumpa kiki na ndio maana sasa hivi haonekani katika mitandao.

Harmorapa hakuwa msanii na kujulikana kwa sababu ya muziki,ila harmorapa amejulikana kwa sababu ya kiki, amezaliwa kwa sababu ya kiki tu.harmorapa sio mwanamuziki mzuri yupo kwa sababu ya kiki na kwa sababu hafanyi kiki basi haonekani.

Harmorapa Atoa Sababu za Kutofika Kwenye Harusi ya Kiba

Baada ya ukimya mrefu msanii Harmorapa ameibuka na kueleza sababu ya kilichopelekea kupotea ghafla.

Harmorapa amesema kwa kipindi kirefu alikuwa nje ya Dar es Salaam kwa kuandaa kazi zake mpya ambazo alikuwa akizifanyia nchini Afrika Kusini.

Pia Harmorapa amedai kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii waliohalikwa katika harusi ya msanii Alikiba ila alishindwa kuhudhuria kutokana na safari yake hiyo.

“Uongo dhambi, kualikwa nilialikwa sema nilikuwa sipo Dar es Salaam, kwa hiyo ile kuwa mbali ilisababisha kutohudhuria kwenye harusi, nilikuwa bize nasafiri sana,” Harmorapa ameiambia TV E.

Katika hatua nyingine amedai kuwa nia yake ya kumuoa Wema Sepetu ipo pale pale kwani ni kitu ambacho anaamini kipo ndani ya uwezo wake, huku akieleza kama Dogo Janja ameweza kumuoa Irene Uwoya haoni sababu ya yeye kushindwa.

“Wema na Jokate Wameungana Ili Kumshusha Alikiba”-Harmorapa

Msanii wa Bongo fleva  anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa amewatolea povu tena warembo wengine ambao ni Wema Sepetu na Jokate Mwegelo  na kudai ni wadangaji na wameungana ili kumshusha Alikiba.

Wiki iliyopita baada ya kutoa albamu yake ya ‘A boy from Tandale’ watu wengi walijitokeza na kumpongeza Diamond kwa hatua aliyofikia na warembo kama Wema na Jokate nao walimpongeza kitendo ambacho inaelekea hakikumfurahisha Harmorapa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa aliwatolea povu zito Wema na Jokate kwa kudai kitendo chao cha kumpongeza Diamond ni kwa nia ya kutaka kumshusha Ali Kiba:

Naona hawa wadada na wadangaji wengine wameungana ili kumshusha King Kiba. Nawachana nyie wadangaji mwenye kupewa uwezo kapewa tu nyie bora mkazane na uwezo weny mliopewa wa kudanga. Mnafikiri mkiposti kazi za Diamond ndio mnuumiza moyo KingKiba? Ndio maana mmchezewa mmeachwa Jojo umechezewa na King Kiba umeachwa kaenda kuoa mtoto chokoleti huko Moombasa eti hasira zako umezihamishia huko kwa Chibu, na liwema nalo limechezewa likaachwa nafasi ikachukuliwa na African beauty Zari aliyelishinda kila kitu kuanzia uzuri m, followers mpaka pesa eti likaanza kumtongoza king kiba ili limkomeshe Mondi, KIng nae akapita nalo akalitema likaona lirudi kumwaribia Zari ndoa yake nalenyewe limeungana kumharibia Alikiba”.

 

Harmorapa Amtolea Povu Uchebe na Kudai Ameolewa na Shilole

Rapa wa muziki wa Bongo fleva Harmorapa aliyejipatia umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii kwa vituko vyake amerudi tena Kwenye headlines na safari hii yuko na Shilole pamoja na mumewe Uchebe.

Harmorapa ameibuka na kudai kuwa Mwanamuziki wa Bongo fleva Shilole amemuoa mumewe Uchebe. Huku akidai kuwa kitendo cha Uchebe kuacha kazi yake ya ufundi gereji na kumtegemea mke wake ni sawa na kuoelewa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Harmorapa amerusha dongo hili lililowaelekea Uchebe na Shilole:

Uchebe mtoto wa kiume umeachana Kupiga na spana umekimbilia Kuolewa Kwa nini badgirlshishi akuosheshe vyombo? Uchebe mtoto wa kiume rudi gereji ukapige spana la sivyo utapigwa sana vibao na shishi na kufulishwa mpaka chup*, sura yenyewe imekukunjika kama yangu utafikiri tumetoroka kwenye zui la manyani/ hiyo ndio faida ya wanaume marioo vibenteni demu wanahudumia masponsa mzigo tunakula sisi kimya kimya na chup* tunachafua sisi wahudumiaji alafu  vibenteni kama Uchebe kazi yao kutakatisha chup*”.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa mwaka jana mwishoni, kabla hawajaoana Uchebe alikuwa fundi magari gereji lakini baada ya kufunga ndoa amekuwa akionekana kila mahali na Shilole akimsindikiza kwenye shoo zake zote hali iliyozua maneno maneno.

Albamu Ya Diamond Mbaya Kama Sura Yangu – Harmorapa

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa ameibuka na kuiponda Albamu ya Diamond na kudai ni mbaya kama ilivyo sura yake.

Harmorapa alijipatia umaarufu kwa kupenda kiki katika maswali kadhaa kuliko muziki wake na leo ameibuka na jipya kuhusu Albamu mpya msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Albamu ya Diamond inayoitwa ‘A boy from Tandale’ imetoka rasmi jana usiku ambapo ilifanyiwa uzinduzi rasmi nchini Kenya.

Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram ameinanga Albamu ya Diamond na kudai ameitangaza sana alafu ametoa kitu kibovu:

Bro Chibu naye kelele nyingi za Albamu miezi saba mwisho wa siku anatutolea albamu mbovu kama sura yangu sokwe, cha kukushauri Simba kama mkataba wako wa karanga umeisha kaa dukani kwa dada yako Esma umsaidie kuuza vitenge”.

Lakini Harmorapa amejitamba na kudai kuwa albamu yake ambayo atakuja kuitoa itakayoitwa Uthigawepathi itakuwa kali kuliko hiyo lakini pia amesema albamu ya Ali Kiba itafunika kupita maelezo.

Harmorapa Aachana na Menejiment Yake Mpya Tena.

Msanii wa muziki Harmorapa ambae amekuwa akitengeneza kiki kila siku amekutwa na janga lingine tena la kutemwa na menejimenti yake mpya ambayo amesaini nayo mkataba siku sio nyingi kwa makosa yale yale aliyokuwa ameyafanya mwanzao katikamenejiment yake ya zamani.

Harmorapa ambae miezi kadhaa huko nyuma ilisemekana kufulia kabisa kutokana na kuachwa na menejiment yake baada ya kufanya kazi nje ya menejiment kinyume na makubaliano ya mkataba na kushindwa kumpa meneja wake hata sent tano  alipata bahati ya kuwa na uongozi mpya lakini inasemekana kuwa hata hiyo wameshindwana nayo.

mpaka sasa hakuna aliyeweka wazi juu ya kuachana kwa meneja mpya na msanii Harmorapa lakini tetesi zinasema kuwa msanii huyo ameshindwa kufanya kazi na menejimenti hiyo kwa sababu harmorap aliamua kufanya kazi  nje ya menejiment hiyo bila taarifa wa uongozi wake kitu ambacho ni kinyume na makubaliano

Msanii huyo ambae amezoea kufanya kazi kwa kiki anaonekana kutokutulia na kuwafanya hata wasanii wenzake kumsema vibaya kuwa amekuja katika tasnia ya muziki kwa ajili ya kutafuta jina tu, na watu kama hawa hawakuzi muziki bali wanaua.

Harmorapa- Mimi Nikitua Kenya ni Staa

Mwanamuziki wa Bongo fleva Harmorapa ametamba na kudai kuwa anapoenda nchi za jirani kama vile Kenya anakuwa mtu maarufu sana yaani wanamuona kama staa mkubwa sana.

Harmorapa alipata umaarufu mwaka jana baada ya kuingua kwenye gemu kwa gia za kufanana na msanii wa Bongo fleva kutoka label ya Wasafi Classic Harmonize na hata kuchukua jina lake lakini alizidinkujipatia umaarufu kwa tabia yake ya kupenda kiki kwa kila jambo atakalofanya.

Harmorapa alizidi kujizolea umaarufu baada ya kutangaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa anampenda mrembo Wema Sepetu na kudai kuwa yuko tayari hata kumuoa lakini Wema alimtolea povu zito na kumkataza kumtaja taja na kumuongelea hovyo.

Harmorapa amerudi tena kwenye vichwa vya habari huku safari hii akidai kuwa yeye ni staa mkubwa zaidi nchini Kenya, Harmorapa amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5:

Unajua mimi mbali ya kuwa mwanamuziki lakini pia ni mfanyabiashara kwaiyo nilienda nchini Kenya kwa ishu za biashara zangu sasa si unajua mimi ni maarufu kule yaan nikitua tu watu wakajitokeza ambao ni wadau wakasema kwa nini tusifanye kitu fulani pia nikimaanisha kupiga shoo kwaiyo tukapiga shoo pale Kenya”.

Lakini pia Harmorapa amefunguka kuhusu dili lake na kampuni ya Swala ambayo ilikuwa inahusika na vinywaji jambo ambalo amekiri kuwa lile dili lilizingua na hivyo akaamua kuachana nalo kwa sababu habari zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa analipwa milioni 100 na kampuni hiyo ili kutangaza vinywaji vyao jambo ambalo amesema sio la kweli kwani amedai hajawahi hata kuiona hiyo pesa.

Harmorapa Amuomba Radhi Master J Kwa Upuuzi Aliomuongelea

Mwanaumuziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Harmorapa ameibuka tena na safari hii amedai kuwa anamuomba msamaha producer maarufu Bongo Master J.

Harmorapa amemuomba radhi producer mkongwe bongo baada ya kudai kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia hapo kabla. Master J ni moja kati ya waanzilishi wa mziki wa bongo fleva kwa kuhusika katika kuvumbua vipaji vingi kupitia studio yake ya Mj Records.

Harmorapa alifunguka hayo alipokuwa anahojiwa kwenye kipindi cha Enews ya East Africa TV na kusema katika mwaka huu wa 2017 amemkosea sana Master Jay kufuatia kauli yake aliyoitoa kipindi cha nyuma kupitia katika kipindi hicho ambapo alidai kuwa hamjui wala hamtambui mtayarishaji huyo mkongwe wa Bongo fleva.

Kwa kweli niligundua kuwa nilifanya makosa makubwa sana, unajua kipindi kile nasema vile nilikuwa sijamjua vizuri Master Jay hivyo naomba anisamehe”.

Kipindi cha nyuma Harmorapa aliwahi kumkana mtayarishaji huyo wa muziki na kudai kuwa hamjui wala hatambui kipaji chake Harmorapa alitokwa na povu hilo baada ya kusikia Master J akidai kuwa Harmorapa hana kipaji chochote cha kuimba wala kucheza labada ajaribu fani ya uchekeshaji maneno yaliyomchoma Harmorapa kupita kiasi.

 

Harmorapa Kumuendea Wema Sepetu Kwa Mganga Mara Tatu

Msanii ambae alijitambulisha katika tasnia ya bongo fleva kwa kiki nyingi sana lakini sasa kwa maneno ya chini chini ni kwamba msanii huyo amefulia na inawezekana kabisa akarudi kijijini kwao kutokana na kutemwa na menejementi yake, Harmorapa amefunguka na kusema ukweli kuwa kwa muda amekuwa akimtamani Wema Sepetu na mpaka ameshafikia hatua ya kumuendea kwa waganga wa kienyeji ili aweze kumpata lakini imeshindikana kabisa.

Harmorapa amesema kuwa amekuwa akiangaika sana kwa rafiki zake na Wema ili kumpata Wema lakini ilishindikana hivyo aliamua kwenda kwa sangoma na  kumfanyia dawa msanii huyo lakini cha ajabu ni kwamba mganga alimuagiza kuku mweupe  na akaleta lakini aliporudi mjini kuangalia mafanikio alikuta bado mambo si shwari kabisa.

Nilimuendea Wema kwa mganga mara ya kwanza mganga akaniambia nipeleke kuku mweupe nikapeleka lakini niliporudi Dar mambo hayakuwa sawa kwaiyo nikamuendea tena mabpo aliniagiza nipeleke vitu vingine tofauti mara mbili ambavyo hapa siwezi kuvitaja lakini naona b.ado

Harmorapa anasema kuwa amekuwa akipata wakati mgumu sana kuonana na msichana huyo kwa sababu kuna kipindi ameshaambiwa apeleke  hadi mchanga wa unyayo wa Wema Sepetu na mchanga wa alipotemea mate lakini imekuwa ikishindikana kwa sababu hapati nafasi ya kuwa karibu na Wema Sepetu.

Hata hivyo Harmorapa anasema kuwa kwa sasa ameamua kumuachia mungu swala la mahusiano yake na wema sepetu kwa sababu huko alikojaribu alishaangaika na ameshashindwa, kama bahati yake ipo basi atampta msichana huyo.Harmorapa ameshawahi kusema si zaidi ya mara  kuwa amekuwa akimtaka kimapenzi mwanadada Wema Sepetu .