Harmorapa Kurudi Kijijini Kwao

Mwaka 2017 ulikuwa ni mwaka wake, baada ya kuja mjini na kutafuta kiki ambayo aliipata bila gharama yoyote kutokana na drama nyingi alizokuwa nazo na kumfanya kujulikana karibia kila sehemu alipokuwa anakwenda watu waweze kumnyooshea vidole.

Msanii wa muziki aliyekuja kwa kazi huku baadhi ya wasanii wakimpiga vita sana kutokana na gia yake aliyokuwa ameingilia , Harmorapa  inasemekana kuwa maisha ya mjini yamemshinda na muda wowote atarudi kwao maeneo ya kusini baada ya kutimuliwa na meneja wake kwa kuwa mbabaishaji mjini.

Mara ya mwisho meneja wake aliyejulikana kama Irene Sebuke alisema kuwa walichoshindwana na Harmorapa ni baada ya kurubuniwa na moja ya mapromoter mjini kwa kumpa show za kumzungusha mikioani lakini kitu cha kushangaza meneja huyo akupata hata kiasi kidogo kutoka katika show hizo huku wakimdanganya kuwa walikuwa hawapati show ilhali ni uongo.

Hata hivyo meneja huyo alisema kuwa hrmorapa laiporubuniwa alionekana kumdharau kabisa meneja wake na kumjali sana promoter na kusahau kuwa nani alimleta mjini, hata hivyo harmorapa amekuwa akifichaficha tetesi hizo na kusma kuwa mambo yake na menehja wake yataisha tu huku akionekana mwenye hali mbaya.

Baadhi ya watu wa karibi na Harmorapa wanasema kuwa kwa sasa msanii huyo yuko mbioni kurudi kwao baada ya kuona kuwa meneja wake alishamkacha na maisha ya mjini yameshakuwa sio mazuri kwa uoande wake.

Harmorapa Atimulia na Meneja Wake Kufuatia Tuhuma Za Kumuibia

Msanii wa Bongo fleva Harmorapa ameingia matatani baada ya Meneja wake kumtimua chini ya uongozi wake baada ya kumtuhumu kumdhurumu pesa.

Harmorapa alitawala vichwa vya habari kwa mwaka huu wa 2017 hasa kwa sababu ya vituko vyake na kupenda kiki. Kuanzi bifu lake na harmorapa baada ya kutumia jina lake kupatia umaarufu mpaka kumganda na kumganda mrembo Wema Sepetu na kukiri mapenzi yake kwake.

Lakini kwa hIvi sasa Harmorapa anasemekana kupitia kipindi kigumu kwani aliyekuwa meneja wake mwanamama Irene Sebuka anasemekana kamtema. Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mitandaoni ni kuwa Harmorapa alifuatwa na promoter mmoja na kuzunguka naye mikoani kwenye kufanya show mbali mbali lakini hawakua wakimletea manager wake mrejesho wowote wa mapato waliyopata kwenye show hizo alizokuwa anafanya.

Meneja wa Harmorapa alisema alisikitishwa na usaliti huo uliofanywa na aliyekuwa msanii wake ukitegemea kuwa aliytumia zaidi ya shilingi milioni 70 za kitanzania kumuibua na kumtangaza Harmorapa.

Irene amedai kuwa msanii huyo (Harmorapa) alirubuniwa na promoter huyo hivyo kumuona yeye meneja wake hana maana tena kwake hivyo ameamua kumtimua na kumrudisha kwa huyo huyo promoter aliye kuwa anamuona wa maana.

Harmorapa amekiri kosa na kuthibitisha habari hizo zina ukweli ndani yake lakini amedai kuwa yeye na meneja wake ni watu wanaojuana hivyo ana imani kuwa wanaweza wakakaa chini na kuyamaliza kama watu wazima na watasahemeana na kurudi kufanya kazi.

Harmorapa Kafulia,Meneja Wake Aongea.

Harmorapa ni moja  ya wasanii waliokuja kwa kasi sana katika tasnia ya muziki huku wakiata kiki na kujulikana na mashabiki kwa muda mfupi sana,haha hivyo msanii huyo inasemekana kuwa amefulia na hana soko tena mjini, kitu ambacho mara ya kwanza msanii huyo alipoulizwa akikataa na kusema kuwa sio kweli kuwa amefulia ila kuna vitu bado anafatilia kwa sababu ana mambo mengi.

Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa harmorapa na meneja wake Irene Sebuka wamekuwa katika mgogoro uliomfanaya meneja huyo kumbaga msanii huyo na kuachana nae, hata hivyo chanzo hicho kinasema kuwa kwa kipindi fulani alitokea promota mmoja ambae alisema kuwa anamtaka msanii harmorapa ili wakafanye nae show mikoani lakini kitu cha ajabu ni kwamba walipoanza kufa nya show zao mikoani hakukuwa na mrejesho wowote  wa kumfaidisha meneja huyo kitu ambacho pia kilikwaza meneja huyo.

Akiendelea kumwaga ubuyu huo, alikuwa anatoa habari alisema kuwa promota na Harmorapa walikuwa wakienda mikoani kufanya show walikwa wakisemakuwa show hazikwenda vizuri ilhali meneja huyo akiangalia alishatumia zaidi yamilion 70 kwa ajili ya kumfanya harmorapa kujilikana mara alipokuja katika kiwanda cha muziki.

Akiongea na mwandishi kutoka Global meneja wa Harmorapa anasema kuwa anachojua yeye harmorapa alirubuniwa na promota bila kujali maslahi yake hiyvyo na yeye akaona isiwe tabu akaona bora kuachana nae.

Ninachojua huyo promota alitaka kumsaidia,kumbe alishajua Harmorapa amepata jina kwaiyo alitaka kumtumia.alitaka kumrubuni kwaio na mimi nikamuacha tu kwa sababu najua wapi nilipomtoa.  Aliongea meneja wa Harmorapa.

Hata hivyo Harmorapa alipotafutwa kuulizwa kuhusu jambo ilo alisema kuwa ni kweli amekuwa na matatizo ya hapo na hapo  na meneja wake lakini haimaaishi kuwa hawafanyi kazi pamoja.

kuna vitu vimetokea kweli lakini ninachojua ni kuwa mimi na irene bado tunafanya kazi, Irene bado ni meneja wangu. Amefunguka Harmorapa.

Harmorapa: Naamini Kuna Siku Wema Sepetu Atakuwa Mpenzi Wangu

Mwanamuziki na rapa anayeongoza kwa kupenda kiki ‘Harmorapa’ amerudi tena kwenye vichwa vya habari na kufunguka kuwa ana imani kuwa ipo siku atakuja kumuoa muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu.

Siku za nyuma kidogo Harmorapa hakusita kuweka hisia zake hadharani na kusema kuwa anampenda Wema Sepetu na ndoto yake kubwa maishani ni kumuoa na awe mke wake, kitu ambacho kilimpa sana harmorapa lakini Wema aliibuka na kumkataza Harmotapa kutumia jina lake ndipo pale Harmonize alipogeuza kibao na kuanza kumponda Wema kwa kumuita Bibi.

Siku mbili zilizopita Harmorapa aliibuka tena na kuonyesha hisia zake kuwa hata kama muda umepita Lakini bado hisia zake juu ya Wema ziko pale pale. Harmorapa amedai kuwa naye anaamini ipo Siku atatimiza ndoto yake ya kumuoa Wema kama Dogo Janja alivyobahatika kumuoa Uwoya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Harmorapa alifunguka mazito juu ya kipenzi chake Wema:

Dah Naamini sana katika ndoto, kuwa ipo siku ndoto unayoota kuwa kuja kweli sina la kuongeza zaidu ya kumpa hongera Dogo Janja kwa kutimiza ndoto yake ya kumuoa Irene Uwoya naamini ushupavu wake na kumemfanya kutokuvunjika moyo ndio kumemfanya leo hii akawa mume wa mwanamke wa ndoto zake…Nami sivunji imani naamini ipo Siku Wema Sepetu atakuwa wangu ugumu alioupata Janjaro umenipa matumaini kikubwa ni kutulia na ndoto yangu  na kulenga ipo siku itatimia…one day you will be mine Wema Sepetu”.

Baada ya Dogo Janja kufanikiwa kumuoa Uwoya ameonekana nimfano wa kuigwa kwa vijana mbali mbali huku akiwapa somo la uvumilivu na kuamini kuwa ipo Siku yatatimia, Wema Sepetu hajamjibu bado Harmorapa lakini inajulikana kabisa Wema atakuwa hajafurahishwa na kitendo hicho.

 

Niko Busy Na Biashara- Harmorapa

Msanii wa muziki wa bongo fleva, aliyejulikana na kuwa maarufu kwenye game kutokana na drama zisizoisha , ameibuka na kusema kuwa wale wanaotangaza kuwa amefulia ni uongo ila yuko busy anafanya biashara zake.Harmorapa anasema kuwa ukiachana na maisha ya muziki , kuna kitu kingine anafanya tofauti na icho hivyo kwa muda huu mambo ya biashara yamemfanya kuwa busy ila anakaribia kurudi hivi karibuni na mashabiki wakae mkao wa kula.

Akiongea na eNews ya EATV, Harmorapa amesema kuwa watu inabidi wajue kuwa kuna maisha nje ya muziki,”watu waelewe  kuwa sipo kimya kuwa nimefulia, sasa hivi niko busy na biashara na pia nina safiri sana,ile kuonana tu ni bahati.Project zangu zinaendelea kama kawaida, na wiki ijayo naachia dude jipya, watu wajue mimi nipo ,tatizo wamezoea kuwa harmorapa kafanya hivi mara kafanya vile, kwa sasa niko busy na biashara na muziki wangu bado upo sana.kama kutrend kila siku na-trend, kila siku naingia instagram,nakuta tu mtu amenipost kwaiyo nakuwa najua kumbe bado nipo machoni pa watu.Bado mimi nipo  na muziki upo na vitu vitaendelea”

Kwa muda sasa Harmorapa amekuwa kuwa kimya , tofauti na jinsi alivyokuwa akichukua vichwa vya habari katika vyombo vya habari , na kuna baadhi ya watu wakaanza kusema kuwa inawezekana atakuwa amefulia, hivyo harmorapa kaamua kuwajibu wanaomzushia habari hizo na kwamba hivi karibuni anatoa wimbo mpya hivi wasubiri kitu kipya.

 

 

Alichokiongea Mad Ice Kuhusu Harmorapa

Mwanamuziki wa Ragger na Bongo Fanaefanya kazi zake nchini Tanzania na Uganda pia  Ahmed  Mohamed Kakoyi maarufu kama Mad Ice  amefunguka na kuongelea kipaji cha muziki alichonacho Harmorapa na kazi anayoifanya kwa ujumla,msanii huyo ambae ni raia wa Uganda lakini amekuwa akifanya vizuri nchini Tanzania katika muziki anasema kuwa msanii Harmorapa afai kabisa kuitwa msanii wa Bongo Fleva maana hana kipaji cha Bongo Fleva na wanaompa sifa hizo ni kama wanaua sanaa ya muziki wa bongo.

Alipokuwa akizungumza na kituo cha East Africa Radio katika kipindi cha Planet Bongo, Mad Ice alisema kuwa kipaji chake kinafaa kuwa ni uchekeshaji,”nimesikia ilo jina la Harmorapa nikasikitika sana,kwa sababu kuna vitu tunafanya vinaharibu sanaa yetu wenyewe, kuna baadhi ya wasanii  wanahitaji kupewa fursa, mimi nimemuona kama mchekeshaji tu ,ukiniambia ni comedian nitaheshimu lakini  unaponiambia unamlinganisha na mimi  nitakuona una kitu kinakusumbua kichwani‘ amefunguka Mad Ice

Hata hivyo sio mara ya kwanza kwa wasanii wakongwe kama Mad Ice kutoa kauli kama izo zinazomuhusu Harmorapa, msanii aliyekuja na kuchukua jina katika tasnia ya musiki kwa muda mfupi kutokana na mambo na vituko vyake alivyokuwa akifanya huku wengine wakimshtumu kuwa anatafuta kiki, Harmorapa aliingia katika bifu na baadhi ya wasanii wakubwa kipindi anaanza musiki.Hata hivyo kwa sasa msanii huyo anaonekana kupoa kabisa zile kiki zilizokuwepo mwanzo zimekuwa kimya.Producer maarufu nchini, Master J pia alishawahi kutoa maoni yake juu ya Harmorapa na kauli yake haikupishana na  hii ya Mad Ice kuwa Harmorapa alifaa kuwa msanii wa vichekesho lakini sio Bongo Fleva .

Akiwa kama msanii mkongwe Mad Ice aliyefanikiwa sana kimuziki , alipoanza kufanya kazi chini ya Mikka Mwamba na alifikia hatua ya kutangaza nyimbo zake mpaka katika soko la muziki la Ulaya na kutokana na kujituma kwake na kufanya vizuri katika nyimbo zake mbalimbali msanii huyo alipata bahati ya kualikwa mara nyingi katika matamasha nchini Ulaya ,kitu ambacho kilimfanya muziki wake uendelee kukua.

Harmorapa Amponda Mpenzi Mpya Wa Harmonize Adai ni Bibi

Msanii anayechipukia kwa kasi nchini kwenye miondoko ya hip hop Harmorapa amefunguka mengi juu ya Mpenzi wa wanamuziki mwenzie Harmonize, Anayejulikana kama Sarah pamoja na mpenzi wa zamani wa msanii Diamond “Wema Sepetu” akidai kuwa wote ni mabibi yaani watu wenye umri mkubwa.

Akizungumza kuhusu mpenzi huyo wa Harmonize, alifunguka kwamba:

“Mimi namuona yule mpenzi wa Harmonize ni bibi tu, hajaopoa demu pale bali kaopoa mpenzi ambae ni bibi yaani ni kama mimi nikaishi na bibi angu, yaani ndo Harmonize ni kama  anaishi na bibi mzaa mama yake”.

Harmorapa pia alishawahi kufunguka mengi kuhusu  kumpenda Wema aliposema yupo tayari kumliia fedha yoyote kwa ajili ya kuishi naye lakini Wema alikataa kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya kuona hivyo harmorapa alimgeuka na kumponda na kusema ana umri mkubwa. Harmorapa alimshauri mwanamuziki huyo machachari aachane na Sarah na atafute mwanamke anayeendana na umri wake.

Gigy Money ampa kichapo Harmorapa hadharani

Gigy Money ni malkia wa kiki na Harmorapa ni mfalme wa kiki. Lakini la kushangaza ni kuwa hawa wawili hawali sahani moja.

Gigy anataka Harmorapa awache kiki na kujishugulisha na mambo ya kimuziki ambayo itafanya watu wamtambue kama rapa wa nguvu.

Harmorapa

Mrembo huyo aliambia Harmorapa apige kazi sana watu wamue na apate pesa kwa jasho lake na sio kujishugulisha na mambo yasiyofaa.

Gigy Money alisema haya katika mahojiano hivi karibuni.Tazama mahojiano hayo kwenye video hapo chini:

https://youtu.be/t7MbQG0DqIw

Continue reading “Gigy Money ampa kichapo Harmorapa hadharani”

Harmorapa bado amwongelea Wema Sepetu ata baada ya mrembo huyo kumchapa kiboko

Mwezi moja iliyopita, Harmorapa akiongea na Millard Ayo alidai kuwa anampenda sana Wema Sepetu na ata angependa kufunga naye ndoa.

Wema Sepetu alimjibu rapa huyo kwa kumsomea mwanzo hadi mwisho kwenye ujumbe aliyoandika katika Instagram yake.

Soma pia: Mambo matano ya kuvunja moyo Wema Sepetu aliyomweleza Harmorapa kwenye instagram

Kama ulidhani Harmorapa aliskia kichapo alichopewa na Wema, bado. Rapa huyo anayependa kiki aliongelea ishu ya kudai kuwa anampenda Wema Sepetu alipohojiwa kwenye kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM hivi karibuni.

Tazama mahojiano hayo kwenye video hiyo hapo chini:

“Nundu ya Lulu sio size yangu” Harmorapa akosoa makalio ya Elizabeth Michael ‘Lulu’, Wema Sepetu na Wolper

Harmorapa ametoa hukumu yake kuhusu makalio ya warembo watatu maarufu sana Tanzania; Wema Sepetu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Jacqueline Wolper.

Rapa huyu maarufu kwa kuzua utata aliongelea matako za warembo hao katika wimbo wake mpya ‘Nundu’ ambayo aliwashirikisha Cpwaa na Ronei.

Harmorapa alisema makalio ya Lulu sio size yake, alisema pia hawezi ‘kula’ nundu ya Wolper kwasababu Harmonize ndo anakula.

Tazama video ya wimbo wake Harmorapa hapo chini:

 

Dogo Janja: Harmorapa ni mtu ambaye nimetokea kumkubali mimi

Dogo Janja amesema kuwa anamkubali Harmorapa hata kama watu wengi wameongea matope kumhusu. Rapa huyo chipukizi amewaudhi watu wengi kwa vitendo na muziki wake.

Soma pia: Jacqueline Wolper: Harmorapa anaudhi sana

Akiongea katika kipindi cha eNewz, Dogo Janja alisema kuwa anamkubali Harmorapa kwasababu ameonyesha uthubutu katika muziki licha ya watu kumkatisha tamaa.

Msanii huyo wa Bongo fleva aliongezea kuwa Harmorapa anahitaji vitu vichache tu vya kuongezeka ili muziki wake ukubalike kote.

Harmorapa

“Harmorapa ni mtu ambaye nimetokea kumkubali mimi kama mimi ….Ni mtu ambaye amejaribu kuonesha uthubutu..Step ambayo ameenda ndiyo imenifanya mimi nimkubali zaidi, alianza wimbo wa kwanza watu wakamtisha tamaa, vunja moyo lakini hakuvunjika moyo. ‘Dude’ la pili akajaribu halafu likawa kali mimi nikasema huyu anahitaji vitu vichache tu vya kuongezeka kwa kuwa anaonekana na moyo wa uthubutu na anapenda kujifunza zaidi” alisema Dogo Janja.

 

Harmorapa aendelea na vituko vyake… Sahi ni Kiingereza tu!

Harmorapa ni mchekeshaji kwani mara nyingi ametawala vichwa vya habari kwasababu ya vituko vyake wala si muziki wake.

Rapper huyo anajulikana sana kwa vioja anazopenda kutoa kila mara anapohojiwa kwenye redio ama kwa runinga ama ata atokeapo kwa umma.

Akiongea na mashabiki katika mtandao wa Facebook wa EATV, Harmorapa alikiri kuwa Kiingereza kinampiga chenga.

Hii ni baada ya msanii huyo kuwafanya mashabiki kupasuka kwa kicheko kikubwa  baada ya kujibu swali pasivyo alipoulizwa kwa Kiingereza.

“Wewe ni mwanaume wa aina gani?” Harmorapa aliulizwa kwa Kiingereza.

“Mimi ni strong woman,” Harmorapa alijibu.

Alipoulizwa kama anaelewa Kiingereza vizuri alikiri kuwa anaufahamu lakini kuongea ndo tatizo kwake.

“Lugha ya Kiingereza naifahamu vizuri lakini ile kuongea ongea ndiyo siwezi”

 

Collabo ya kimataifa: Harmorapa aingia studio na Kriticos – staa kutoka Ubelgiji

Nyota ya Harmorapa yazidi kung’aa hata kama watu wengi bado wanamdharau. Msanii huyo alitupiwa chupa wiki chache zilizopita alipokuwa akitumbuiza mashabiki.

Hivi juzi tu Jackline Wolper alidai kuwa Harmorapa anaudhi sana. Mrembo huyo alisema kuwa hapendi vitendo za rapper huyo.

Soma pia: Jacqueline Wolper: Harmorapa anaudhi sana

Harmorapa hata hivyo hana muda na wanaomchukia, staa huyo wa Bongofleva anafanya collabo na mwanamuziki Kriticos kutoka Ubelgiji.

Msanii huyo mwenye asili ya Tanzania na Zambia, amefika nchini kufanya kazi na Harmorapa ambapo leo April 7, 2017 walipata nafasi ya kuzungumza na AyoTV Entertainment

Harmorapa na Kriticos

Harmorapa amewataka mashabiki wake kukaa tayari kupokea ngoma hiyo itakayotengenezwa na mtayarishaji wa muziki P-Funk Majani.

 

 

Jacqueline Wolper: Harmorapa anaudhi sana

Harmorapa amemfika kooni Jacqueline Wolper – mpenzi wa Harmonize. Harmorapa, ambaye anafanana na Harmonize, aliwashangaza wengi alipomtafuta binti mrembo anayefanana na Jacqueline Wolper.

Harmorapa na Wolper bandia

 

Harmonize na Wolper

 

Wolper sasa amesema kuwa kinachomuudhi kwa Harmorapa ni kitendo cha mpenzi wake Harmonize kumuongelea vizuri lakini yeye anapohojiwa na vyombo vya habari anaponda.

“Jamani yaani kama huna moyo unaweza ukapasuka kwa hasira maana Harmorapa anaudhi sana, wenzie wakimuongelea vizuri yeye anawaongelea vibaya unafi kiri mtu ataacha kukuchukia? Abadilike,” alisema Wolper.

 

 

Harmorapa aongelea wanadada watano Tanzania ambao angetaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao…nambari moja ni Wema Sepetu

Harmorapa alikuwa kwenye Millard Ayo juzi ambapo alizungumzia mambo mbali mbali la kwanza ikiwemo wanadada ambao angetaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao mle Tanzania.

Na kama wasanii wengine wote Tanzania, wa kwanza alikuwemo Wema Sepetu ambaye Harmorapa alisifia ubo lake sana na pia macho yake.

Wa pili alikuwemo Lulu and bado akaendelea.

Pata ujumbe wote kwenye hii video:

 

Harmorapa afungua roho na kusema anataka kumoa Wema Sepetu

Wema Sepetu anatajika kwa kupenda kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mstaa; aliwai kuwa na uhusia na Ali Kiba, Diamond and Idris Sultan.

Kwa sasa Wema hana mshikaji yeyote na hii ndio sababu ya Harmorapa kujitokeza na kusema kwamba angependa kumoa Wema.

Harmorapa

Msanii huyu amefungua roho na kusema kama angekubaliwa na Wema basi atatangaza ndoa mara moja.

“Napenda kusema ukweli ulio jificha moyoni mwangu tangu siku nyingi kutokana na jinsi ninavyo sumbuliwa na hisia za kimapenzi kwa mrembo @WEMASEPETU,tangu naanza kumfaham wema sepetu na kumwona kweny tv akigombea umiss tz mwaka 2006 nilitokea kumpenda sana na kupata hisia za kumwoa endapo ntampata basi tu ndo vile nilikua sina uwezo wa kuonana nae wala kukutana nae kwa sababu ya position nilio kua nayo enzi hizo nauza pochi mwenge?nakumbuka kipind kile #WEMASEPETU wamemkata kweny uchaguz wa wabunge wa viti maalum niliumia sana,hadi skupatwa na usingiz nakumbuka niliamka saa 9 za usiku gheto na kuelekea mwenge kulangua mikoba kwa sababu ya kuiuza kipindi npo maeneo ya mwenge rafiki yangu alie kua na smart na alikua akifaham ni kiasigani namkubari #wemasepetunga alinipa taarifa kua #sepetunga anaingia dar kutokea dodoma baada ya jina lake kukatwa Ukwel nilisema lazima nikampokee na dhawadi nimpatie, bas nikaingia zangu kurangua mikoba nilibahatika kupata mkoba mmoja mzuri sana Akili ikanijia kua ule mkoba nmpe dhawad #kiumizaRohoYangu sikuuza nikauhifadh baadae nikafunga gori langu mapema nikaelekea kumpokea #kiumizaRohoYangu baada ya madam kufika niliangaika sana ili nimpatie ile dhawad ya mkoba bahati mbaya niligongwa na bodaboda kweny mguu wa kushoto na skufanyikiwa kumpa ila hadi leo ule mkoba nnao endapo siku nikipata fursa ya kukutana nae ntampatia huo mkoba.

“Ila nachukizwa sana na vijana walio uchezea moyo wa #sepetunga wakina #Mrblue, #diamond,#idrisa na wengineo nawachukia sana kwa kuufanya moyo wa @WEMASEPETU kama danadana na kuwalaum juu.

“Pia nawaonya wale wote mnao mlinganisha #Zarithebosslady na #WEMASEPETU mnakosea sana wema sepetu n mzuri mno kuliko #zarithebosslady sio kwamba #Mamatee n mbaya hapana mamatee ni mzuri ila hajamfikia #wemasepetu.

“Yote ya yote naombeni mumfikishie Taarifa hizi #WEMASEPETU Mwambieni nampenda sana endapo nikampata hato chukua hata wiki kwangu ntamvisha pete na kufunga ndoa nae juu na kumtunza kwa hali yoyote ile,” Harmorapa aliandika.