Mama Kanumba Amsifia Wema Sepetu

Mama wa msanii marehemu Steven kanumba amekuwa akitoa maoni mara kwa mara kuhusu tasnia ya sanaa nchini na jinsi ambavyo wasanii na marafiki waliokuwa karibu na mtoto wake wanavyomchukulia kwa sasa tangu alipofariki.

Mama huyo anasema kuwa wasanii wengi waliwahi kusaidiwa ili kunyanyuka na mtoto wake lakini wasanii hao kwa sasa hakuna hata mmoja anaemkumbuka kanumba na mbaya zaidi wanakuwa wakiona hata aibu kusema katika itandao kuwa waliwahi kusaidiwa na kanumba.

Hata hivyo mama huyo anasema kuwa katika wasanii wote amekuwa akimpenda sana Wema sepetu ambae amekuwa hoani aibu kusema kuwa alisaidiwa sana na Kanumba mpaka kuwa msanii.

Katika watu pekee ninaowapenda ni Wema Sepetu kwa sababu amekuwa akikumbuka sana fadhila za mwanangu marehemu Steven kanumba.

Alichosema Mama Kanumba Kuhusu Lulu.

Mama wa marehemu Steven Kanumba amefunguka na kusisitiza kuwa katika maisha yake hajawahi kumchukia msanii Lulu Michael kama ambavyo imekuwa ikisikika masikitonkwa watu na watu wengi kuamini hivyo kwa sababu ya kumuua mtoto wake.

Mama huyo anasema kuwa hajawahi kumchukia Lulu lakini amekuwa na uchungu kila siku kwa sababu kifo chake kimesababishwa na mtu mwingine.

Mama kanumba alipokuwa akiongea na EATV, anasema  “kanumba ni mwanangu na nilikuwa ninampenda sana na ukizngatia nilimlea kwa tabu sana lakini anatokea mtu anamuua, mimi simchukuii lulu mimi ninampenda sana, ninamtakia kila lenye kheri katika maisha yake.

Kama bado kuna kumbukumbu, mama kanumba na lulu walikuwa marafiki sana hasa baada ya kifo cha kanumba lakini baada ya hapo mahusiano yao yalianza kufa na hata kufikia hatua ya kuwa maadui wakubwa.

Mama huyo ukiachana na kulalamika  katika mitandaokuwa lulu amekuwa hamuheshimu wala kumsaidia lakinni alichukizwa sana na hukumu aliyopewa mwanadada huyo ikiwa kama adhabu ya kifo cha msanii huyo ambae alikuwa katika mahusiano  na Kanumba.

Mama Kanumba Afungukia Ndoa Ya Lulu na Majizzo

Mama mzazi wa aliyekuwa Msanii wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amefunguka na kusema yuko tayari kuhudhuria harusi Lulu endapo ataalikwa.

Mama Kanumba ambaye aliweka wazi chuki yake dhidi ya Lulu baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Marehemu Steven Kanumba ambapo alihukumiwa miaka miwili jela.

Mama Kanumba alifurahi baada ya kifungo cha Lulu lakini hivi sasa baada ya Lulu kuachiwa huru Mama Kanumba anafunguka na kusema wazi wazi kuwa hana chuki na Lulu na endapo ataalikwa Kwenye Harusi basi hatasita Kuhudhuria kwani hana kinyongo na Mrembo huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa, Mama Kanumba alifunguka haya:

Hapa duniani sina chuki kabisa na Lulu na mimi akili yangu kwa hivi sasa akili yangu imeegemea upande mmoja tu nao ni kumuomba Mungu tu maana yeye ndio anatoa haki sawa kwa tajiri na hata masikini pia”.

Lulu alivalishwa pete na mpenzi wake ambaye ni CEO wa EFM Majizzo ambapo ndoa yake inatarajiwa kufanyika Miezi ya mbeleni.

Mama Kanumba Kuifufua Kampuni Ya Kanumba Iliyokufa Baada Ya Kifo Chake

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Marehemu Steven Kanumba, Florah Mtegoa ameweka wazi nia yake ya kuirudisha sanaa katika ramani miaka baada ya kifo cha mwanaye kwa kuifufua kampuni yake iliyokufa baada ya kifo chake.

Mama Kanumba amefunguka na kusema baada ya kifo cha mwanaye huyo alidhani huenda mtoto wake mwingine, Seth Bosco angeweza kuvaa viatu vya kaka yake na kuiendeleza sanaa lakini amevishindwa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers,Akipiga stori na Star Showbiz, mama Kanumba alisema kuwa

Baada ya kifo cha mwanangu Kanumba ukweli kila kitu kilivurugika si unajua muanzilishi ni muanzilishi tu nikajua mimi na mwanangu Seth tungeweza kuindeleza lakini baadaye tulishindwa maana Seth alishindwa kuvaa viatu vya marehemu kaka yake kama nilivyotegemea.

Lakini naomba niwaambie kwamba tuko kwenye michakato ya kuifufua kampuni hiyo baada ya kuzisoma chalenji nyingi za tasnia hii ambapo awali sikuwa na uzoefu kama nilionao sasa”.

Baada ya kifo cha Kanumba, Mama Kanumba na yeye alijiingiza kwenye fani hiyo ya kuigiza ingawa amewahi kukiri kuwa mwanaye hakutaka kabisa kumuona akiwa anaigiza lakini anafanya hivyo kwa hivi sasa ili kuingiza kipato.

Mama Kanumba Amuomba Msamaha Muna Baada Ya Kuchekelea Kifo Cha Mwanaye

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amefunguka na kumuangukia Muna kwa magoti baada ya Kauli yake ya kuchekelea Kifo Cha Mtoto wake Patrick.

Jambo hilo lilitokea siku chache baada ya Muna Love kufiwa  na mtoto wake Patrick wiki chache zilizopita ambapo Mama Kanumba aliibuka na kuongea Kauli hii “Muna alinitukana sana, na mungu ametenda”.

Kwenye mahojiano  na Times Fm wiki hii, Mama Kanumba alisema kwamba watu hawakumuelewa alichokimaanisha na watu walikata video fupu tu ya yale yaliyosambazwa.

Muna mwanangu pole sana, ni donda hilo ambalo haliponi ni donda ndugu ila naomba unisamehe.

Sikuwa na  nia mbaya na sikuomba kitokee kilichotokea, watu walininukuu vibaya. Na wewe maneno uliyonisema mwanzoni hukujua kesho mwanangu, wote ni mapenzi ya mungu mimi sina nia mbaya”.

Mama Kanumba ameomba msamaha baada ya watu kumjia juu baada ya kutoa Kauli hiyo.

Steve Nyerere na Mama Kanumba Wafikia Pabaya.

Baada ya mama wa marehemu Steve kanumba kufunguka na kusema kuwa  mtoto wake alikuwa haongei kabisa na steve nyerere na hata yeye mwenyewe hana mahusiano mazuri na Steve nyerere tangu mtoto wake alipofariki mpaka sasa hawaongei na Steve labda kwa kukutana kwa baahati mbaya.

Baada ya Mama Kanumba kusema hayo , Steve Nyerere aliamua kutupa jiwe gizani huku akigoma kuonyesha alikuwa akimenga nani lakini kwa contenbt yake inaonyesha kuwa alikuwa ni kama anamjibu mama kanumba kwa kile alichokiongea .

Katika ukurasa wake wa instagra, steve nyerere aliandika “ukiona mtu mzima anaongea upumbavu tena mbele ya wajukuu , watoto wake na jamii kwa ujumla  bila kuthamini ukubwa wa jina lake  basi ujue huyo anawashwa washwa sana.”

 

Gabo Amefanikiwa Kuziba Pengo La Kanumba- Mama Kanumba

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Flora Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amemtaja msanii ambaye anaamini ameziba pengo la Kanumba Kwenye tasnia ya Bongo movie.

Mama Kanumba ambaye naye aliingia Kwenye Bongo Movie mara baada ya mwanaye kufa amemtaja Gabo Zigamba kama Msanii ambaye ameziba pengo la Kanumba.

Kwenye mahojiano  na Wasafi TV, Mama Kanumba amemtaja Muigizaji wa Kiume Gabo Zigamba kama ndiye msanii pekee mwenye uwezo sawa na Kanumba kwa sasa.

Gabo anajitahidi kwa kweli, nilichogundua kwanza anajua kuuvaa uhusika kwenye filamu zake, akiwa kama mlinzi anakuwa mlinzi kweli, akiwa kichaa anakuwa kichaa kweli. Namwambia asikate tamaa kuna watu watamkatisha tamaa kila atapokaribia kuyafikia mafanikio zaidi.”

Lakini pia Mama Kanumba amelinganisha uwezo wa Kanumba na Gabo:

Ni kweli Gabo ‘anashika kijiti cha Kanumba’ anajitahidi, anauthubutu, anajaribu, anajituma na anaweza”.

Mama Kanumba- Siwezi Kuhudhuria Harusi Ya Lulu na Majizzo

Mama mzazi wa aliyekuwa msanii wa Bongo Movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa ‘Mama Kanumba’ ametoa povu zito hivi karibuni baada ya kuulizwa Kuhusu Ndoa ya Lulu na Majizzo.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi kuwa muigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu na mpenzi wake Majizzo wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.

Mama Kanumba amefunguka kuwa, endapo atapelekewa kadi ya mwualiko wa harusi hiyo hawezi kwenda kwa sababu tangu atoke gerezani hawajawahi kuonana na Lulu wala kusalimiana naye.

Kwenye mahojiano na Ijumaa Wikienda, Mama Kanumba amedai kuwa, hata hiyo habari yenyewe ya Lulu kuolewa na Majizo anaisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba hajui lolote.

Kwanza hiyo habari yenyewe nimeisikia kwenye vyombo vya habari, lakini mimi sijui kabisa kama wanaweza kuniletea hiyo kadi ya mwaliko na hata wakiniletea siendi.

Najua itakuwa ngumu tu katika mazingira tuliyopitia sisi, kwanza mimi sasa hivi muda mwingi ninajikalia nyumbani tu kutoka na maradhi yangu haya presha”.

Mama Kanumba aliweka wazi kutofurahishwa na kitendo cha Lulu kutoka jela mapema baada ya kupata msamaha wa Raisi na kupewa kifungo cha nje mapema mwezi uliopita.

Mama Kanumba Asononeshwa na Kitendo Cha Lulu Kutolewa Jela Mapema

Mama mzazi wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba ameeleza machungu yake baada ya Lulu kuachiwa gerezani jana.

Siku ya jana Jeshi la Magereza lilitangaza rasmi kuwa Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameachiwa rasmi kutoka gerezani baada ya kukaa ndani kwa miezi mitano ambapo alitajwa kwenda kuendelea na kifungo chake nje.

Tangu Lulu afungwe Mama Kanumba aliweka wazi kuwa alifurahia kifungo cha Lulu na hata kudai kuwa kifungocha miaka miwili kilikuwa kidogo kwa mauaji ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na MCL digital, Mama Kanumba amefunguka kuwa tangu amepata taarifa kuwa Lulu ameachiwa amekuwa akikosa usingizi na hata presha kupanda kwani ameumizwa sana na taarifa hizo.

Tangu nilipopata taarifa hizi nimejikuta nakosa usingizi na kuumwa presha hivyo leo imenibidi niende kwenye maombi kwa ajili ya afya yangu.

Lakini siku zote naamini Kuwa maskini hana haki”.

Lakini Mama Kanumba amewashukuru wote walioshiriki katika kumtoa na kuongeza kuwa anaamini hiyo yote ni kwa sababu yeye hana hela.

Mama Kanumba Apata Mualiko Nchini Burundi

Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Bi. Flora Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba Amelamba shavu zito baada ya kupata mualiko wa kuenda nchini Burundi.

Mama Kanumba Amepata mualiko maalumu kutoka kwa wasanii wa filamu wa nchini Burundi kwa ajili ya kuenda kujifunza kazi za sanaa hasa filamu wanazofanya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Mama Kanumba alisema kuwa baada ya kupata mualiko huo kutokana na wasanii hao kuthamini mchango wa marehemu mwanaye, ameona ni vyema kwenda na kitu nchini humo ambapo ataizindua filamu yake inayoitwa Capten Habona.

Yani najisikia ni mtu ambaye ninaheshimika ingawa mtoto wangu hayupo hivyo filamu yangu hiyo nitazindulia huko kwa vile na wao wamenipa heshima kubwa sana kwa kuwa filamu yenyewe ina historia nzuri sana“.

Mama Kanumba aliingia Kwenye sanaa miaka michache iliyopita mara baada ya Steven Kanumba kufariki dunia ambapo alikiri sababu za kimaslahi ndizo zilizomuingiza Kwenye uigizaji japokuwa mwanaye hakupenda aigize.

Mama Kanumba Ateta na Mh Mwakyembe

Mama  mzazi wa marehemu steven kanumba amempongeza mh mwakyembe kwa hatua yake anayotaka kuichukua kuhusu kupitia mikataba ya wasanii ambao walikuwa wakisaini mikataba ambayo inaonekana haiwanufaishi walengwa au ndugu wa  baadhi ya mastaa ambao ni marehemu.

Amesema kuwa hatua hiyo ni nzuri na muhimu kwake kwani amekuwa akiona kazi za mwanae kila siku mitaani lakini yeye hakuna anachonufaika nacho.

Kwangu mimi ni faraja, namshukuru Waziri Mwakyembe kwa kuliona hilo. Kwa mfano mwanangu Steven Kanumba, movie zake naziona lakini mama yake ni masikini wanaofaidi ni wengine, sasa kupitia hilo tamko la serikali nasema asante Mungu,” amesema.

“Mimi ni staa nisiye na hela, kazi za mwanangu naziona tu mtaani lakini mimi ni maskini,” Mama Kanumba ameiambia Clouds TV.

Wiki iyopitia Bungeni wakati wa mjadala wa bajeti ya wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/19, Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe alisema ameunda kamati ya wanasheria ya kuchunguza mikataba ya kibiashara waliyoingia marehemu Steven Kanumba na Mzee Majuto

 

 

Mama Kanumba Amwagia Povu Zito Wema Baada Ya Kugoma Kuigiza Naye

Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu alifunguka hivi karibuni na kuweka wazi kuwa miaka ya nyuma wakati yupo Kwenye Mahusiano na Marehemu Steven Kanumba alimwambia hataki mama yake aigize.

Tangu Kanumba aage dunia miaka michache iliyopita mama yake mzazi na yeye ameingia Kwenye sanaa ya Bongo movie na hivi sasa ameshaigiza Movie kadhaa.

Siku chache zilizopita Wema Sepetu alifanya mahojiano na Global Publishers ambapo aliulizwa kama atakuwa tayari kushirikiana Kwenye filamu na Mama Kanumba ndipo Wema alitoboa kuwa hawezi kwa sababu  Kanumba alikataa mama yake kuigiza.

Baada ya taarifa hizo kusambaa Mama Kanumba ameibuka na kumtolea povu zito Wema na kudai kuwa sababu pekee ambayo ilimfanya mwanaye amkataze kucheza filamu ni kwa sababu alikuwa anamuangalia yeye na kumtunza lakini hivi sasa hana msaada hivyo inatakiwa aigize.

Kanumba alisema hayo kwa kuwa alikuwa ananitunza yaani ananinunulia vyakula na kunilipa mshahara kila mwezi kama mfanyakazi lakini sasa hayupo, je Wema alitaka nishike bakuli nikaombe barabarani au? Maana kulima siwezi hivyo naona tu bora niigize ili niweze kujikimu kimaisha”.

 

Kanumba Alikataa Mama Yake Kuigiza, Siwezi Kuigiza Naye

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuigiza filamu moja na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kwani Mwenyewe hakutaka mama yake ajiingize Kwenye sanaa.

Wema ameanika hayo huku akisisitiza kuwa kipindi wakati Kanumba yuko hai alimweleza Wema ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kamwe hataki mama yake ajiingize kwenye Bongo movie.

Wema alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambao walimuuliza endapo yupo tayari kucheza filamu na Mama Kanumba ambaye hivi sasa amegeukia sanaa hiyo:

Hapana, siwezi kwa sababu Kanumba alikuwa hataki mama yake aigize na hata mimi alishaniambia, sasa nitavunja makubaliano yetu mimi na Kanumba”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Wema alikataa tuhuma alizorushiwa na Mama Kanumba kuwa alipownda nyumbani kwa Wema hakufunguliwa geti badala yake aliishia kuchomeshwa mahindi:

Jamani…kwanza siku hiyo mimi sikuwepo kabisa, niliambiwa tu alikuja na kwa nini nifanye hivyo sasa“.

 

Mama Kanumba Awalalamikia Wasanii Kutofika Katika Kumbukumbu ya Mwanae

Mama wa marehemu Steven Kanumba amewalalamiki wasanii wngi ambao hawakufika katika kumbukumbu ya msanii huyo aliyewahi kuwa nguli na mkombozi wa wasanii wengine katika tasnia ya bongo movie.

Kanumba ambae alikuwa akitimiza miaka 6 tangu kifo chake tarehe 7 April  alifariki baada ya kuwa na ugomvi na mpezni wake lulu michael na kusababisha kifo chake tarehe kama hiyo miaka sita iliyopita.

mama wa marehemu anasema kuwa hashangai sana kuona  wasaini wengi hawajahudhuria katika siku hiyo kwa sababu wasanii hao wameshamaliza msiba lakini yeye bado kwake kidonda ni kibichi na ataendelea kulia tu.

hata hivyo Mama Kanumba anasema kuwa wasanii walipaswa kuwa wengi kutokana na vile kanumba alivyokuwa akiishi na wasanii wenzake wengi walipaswa kumkumbuka.

Idadi ya wasanii waliokuja hapa ni wachache ukilingakisha na namna Kanumba alivyokuwa akiishi nao vizuri,lakini ndio hivyo uwezi kulazimisha watokee,isitoshe labda wao wanaona wamemaliza msiba lakini kwangu  bado upo ila ninachowaombea yasije yakawakuta kama hayandio watajua nin i ninamaanisha.

Mama Kanumba :Kanumba angekuwepo Angemuoa Wema.

Mama wa moja ya wasanii  waliokuwa waigizaji nguli Tanzania , mama Steven Kanumba amefunguka na kukanusha tetesi za kuwa yeye pamoja na Wema amabe aliwahi kuwa katika mahusiano na marehemu mtoto wake kuwa wana ugomvi sio kweli kwa sababu kama yeye Wema ni binti aliyetokea kumpenda sana.

kwakweli wema mimi sina bifu nae na hakuna binti ninaye mpenda kama wema,na ninaomba anielewe hivyo, tukionana tusalimiane na tupendane na hizo habari za kutokunifungulia mlango ni uongo, aache kunifungulia kwani mimi namdai au yeye ananidai.

Mama kanumba pia akanusha tetesi za kwenye mitandao kuwa amekuwa akiombamsaada kwa wema na kwamba amekuwa akienda mpaka nyumbani kwake.

Na wala sijawahi kuomba ela ingawa kuna wengine wanasema kuwa nilitaka kuomba ila sijui na nini, wamuulize hata yeye mwenyewe.sijawahi kwenda kwake eti kulia shida na namshukuru sana kwa sababu ni mtoto mwenye heshima.

Hivi karibuni kulizuka kwa maneno kuwa mama huyo amekwenda kwa wema na akatakaa kumfungulia mlango ,  mama huyo anasema kuwa wema hajawahi kumvunjia heshima hata siku moja na kila siku alikuwa anatamani kanumba angekuwepo basi angemuomba amuoe wema.

Siku zote nimekuwa nikisema kama Mungu angekuwa amemuweka Steven, yule mimi nilikuwa nimempenda na ningempendekeza awe mkwe wangu.

“Lulu Akijishusha Kwangu Akaniomba Msamaha Nitamsamehe”- Mama Kanumba

Mama mzazi wa Marehemu Kanumba ameibuka na kuweka wazi kuwa hana kinyongo na Lulu endapo atakuwa tayari kujishusha na kumuomba msamaha basi atamsamehe.

Lulu alifungwa miezi michache iliyopita baada ya kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia marehemu Steven Kanumba aliyekuwa naye kwenye mahusiano kwa kipindi hiko.

Kipindi chote wakati kesi inasikilizwa ni wazi kabisa Lulu na Mama Kanumba hawakuwa katika nafasi nzuri kwani walionekana wakipishana bila kusalimiana na hata Lulu alipohukumiwa kwenda jela Mama Kanumba alisema amefurahishwa.

Mama Kanumba alijiwa juu na watu hasa mashabiki za Lulu ndipo juzi alipofika kuwa hajawahi kumuombea Lulu mabaya na hana tatizo naye kwani alishamsamehe tangu zamani na hana kinyongo naye.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mama Kanumba amefunguka na kuweka wazi kuwa endapo Lulu Akitoka jela akaenda kumuomba msamaha basi atamsamehe.

Lulu alihukumiwa na Jamhuri ilikuwa nje ya uwezo wangu iwe nilimsamehe au sikumsamehe sikuwa na uwezo wa kufuta kesi. Mimi sina kinyongo na Lulu alikuja mara ya kwanza nikamsamehe na kama akimaliza kifungo akiwa tayari kwa kuwa yeye ni mtoto mimi mtu mzima kwaiyo yeye anapaswa ajishushe kwangu akiwa tayari akinipmba msamaha mimi nitampokea”.