Napitia Changamoto Nyingi Lakini Napambana- Rich Mavoko

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Richard Mavoko ‘Rich Mavoko’ amefunguka na kuweka wazi kuwa amekuwa akipitia Changamoto nyingi kwenye Safari yake ya muziki.

Mavoko amesema katika Safari yake nzima ya muziki tangu ameanza miaka ya nyuma amekuwa mtu wa kukatishwa tamaa katika kila hatua anayofika.

Mavoko aliyejitoa katika kundi la WCB hivi karibuni alisema maisha yake ya muziki yamepitia vikwazo vingi kufika alipo lakini hawezi kukata tamaa na atahakikisha anapigana na kuufikisha muziki wake mbali.

Mimi ni moja ya vijana tuliopitia changamoto nyingi kwenye kazi zetu, lakini napambana kuhakikisha kipaji changu kinazidi kupaa ndani na nje ya nchi“.

Hivi karibuni Mavoko aliwanyooshea kidole WCB kwa kutumia mbinu mbali mbali ili kumzibia riziki katika kufanya muziki Wake .

Rich Mavoko Afungukia Mahusiano Yake na Lulu Diva na Mipango Ya Ndoa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Richard Martin maarufu kwa Jina la usanii kama ‘Rich Mavoko’ amefunguka na kuweka wazi kuhusiana na tetesi za Mahusiano Yake na Lulu Diva.

Kunekuwa na tetesi za muda mrefu kuwa Rich Mavoko na Msanii mwenzake Lulu Diva wapo Kwenye Mahusiano ingawa wamekuwa wakikataa mara kwa mara lakini bado tetesi hizo zimekuwa zikiwaandama.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Rich Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa hana uhusiano na Lulu Diva zaidi ya kikazi na kirafiki:

Hivi unajua sijawahi kusema au kukiri sehemu nina uhusiano na Lulu Diva! Nafikiri hayo ni mambo ya kazi na yameshapita”.

Lakini pia Mavoko amefungukia mipango ya kufunga ndoa hapo baadae na tofauti na wasanii wengi yeye anaamini kufunga ndoa hakuwezi kuharibu Taratibu za mtu kimuziki:

Sijaoa bado ila nina watoto wawili, lakini kuoa ni jambo la kheri sana wanaosema wakioa watashuka kimuziki kwa hiyo wataoa lini sasa, uzeeni? Kwangu mimi muda ukifika nitafanya hivyo“.

 

 

Mavoko- Sina Tatizo na WCB, Niko Tayari Kupiga Nao Kazi

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Richard Martini maarufu kama Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo kabisa na uongozi wake wa zamani WCB.

Miezi michache iliyopita Rich Mavoko alitangaza Rasmi kujiengua Kwenye Label ya WCB alipokuwepo kwa miaka kadhaa kutokana na matatizo ya Kimkataba.

Leo hii Rich Mavoko yupo chini ya uongozi mpya ambao hajauweka wazi Lakini pia ameachia nyimbo zake kadhaa kama Ndegele, Hongera, Naogopa na Navumilia.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kuondoka WCB lakini hana tatizo nao:

Unajua watu wengi wanashindwa kuelewa, sikuondoka WCB kwa ugomvi kule hata kidogo ni mambo tu ya kawaida ya kimuziki lakini sina tatizo na yeyote yule”.

Lakini pia Mavoko ameweka wazi kuwa kama itatokea WCB watakuwa tayari kufanya naye kazi hivi sasa basi yeye hana tatizo:

Sina tatizo kabisa, tutakaa chini na kuzungumza si ni biashara tu?”.

 

Rich Mavoko Atangaza Kuwa na Lebel Yake, Ataja Wasanii Anaotamani Kufanya nao Kazi

Msanii Rich Mavoko amefunguka na kusema kuwa kwa sasa ameanza kujisimamai mwenyewe baada ya kutoka katika kusimamiwa na msanii Diamond Platinumz katika label ya Wasafi na kuachana nayo kwa migogoro hivyo ameamua kufanya kazi mwenyewe.

Akiongea na clouds Media, Rich Mavoko anasema kuwa pamoja na kufanya hivyo alkini pia amekuwa na lebel yake ambayo inasimamiwa na mama yake mzazi na dada yake Dokii na ameanza kutafuta wasanii ambao anaweza kuwasimamia katika uongozi wake.

kwa sasa nimesimama mimi kama mimi sina menejiment yoyote, billionaireskids ni lebel yangu ambayo inasimamiwa na mama yangu na dada yangu dokii ambae yuko kama mshauri wangu.

Hata hivyo Rich amewataja wasanii ambao anatamani kufanya nao kazi katika uongozi wake kuwa ni Foby na  Sheby na sasa wapo katika mazungumzo.

Foby na Sheby ni wasanii ninaotamani sana kufanya nao kazi kwa sasa na kama tutakubaliana basi  watakuwa wasanii wa kwanza katika lebel ya bilionaireskids.

Rich Mavoko Afungukia Bifu Lake na WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake na Label yake ya zamani ya WCB.

Rich Mavoko ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba ameondoka katika Label hiyo lakini hana tatizo lolote na CEO wa Label hiyo Diamond Platnumz.

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Rich amesema kuwa kilichotokea mpaka akaondoka Kwenye Label hiyo sio ugomvi bali muda wa kufanya Biashara ulifikia kikomo hivyo sasa wapo vizuri.

Lakini pia Rich Mavoko amemtaka meneja wa WCB Sallam SK kuwa na busara na heshima ni baada ya Meneja huyo kusema Mavoko hajarudisha hata robo ya pesa waliyowekeza kwake na kumtengeneza kama Brand:

Unajua Kwenye masuala ya kumzungumzia Rich Mavoko unazungumzia Brand ambayo ilikuwepo kwaiyo uliichukua kwa nia ya kufanya nayo biashara sasa umesema hajarudisha sasa na huyo mwenye talent atakuwa amepata?”.

Mavoko aliendelea kutiririka na kumwaga povu zito:

Mimi sitaki kuongelea sana hivi vitu kwa undani kila mtu anatakiwa kuheshimu kitu cha mwenzake ndio tuanze kuongeleana na kuongeleana vitu vibaya ni kutafuta mtu kujitetea”.

Rich Mavoko Atoboa Ya Kuandika Nyimbo za Wasanii wa WCB, Akiwemo Queen Darlen

Msanii aliewahi kufanya kazi WCb amefunguka na kusema kuwa kwa muda ambao amekuwa akifanya kazi ndani ya lebo hiyo amekuwa akiandika nyimbo za wasanii wenzake wengi huku nyingine zikiwa tayari zimeshatoka.

rich ambae alitoka WCB hivi karibuni kwa mbinde hasa baada ya kesi yake kufka mpaka katika abarza la sanaa na kusemekana kuwa alikuwa akinyonywa sana na mabosi wake anasema kuwa moja ya nyimbo hizo ni ile ya queen Darleen ya  Touch.

Rich anasema kuwa zipo nyingi zikiwemo zilizotoka na ambazo hazijatoka lakini alikuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu mpaka sasa anaondoka.

 

 

Sina Mpango wa Kusainiwa na Ali Kiba:-Rich Mavoko.

Msanii wa Bongo Fleva mwenye ‘hit song’ ya Ndegele, Rich Mavoko amesema hana mpango wowote wa yeye kusainiwa kwenye ‘label ya King’s Music’, iliyopo chini ya Alikiba kwa kile alichodai anatamani kufanya kazi bila ya kusimamiwa na mtu.

Rich Mavoko amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye PLANET BONGO ya East Africa Radio, baada ya kuenea taarifa mitandaoni kuwa kwa sasa anaelekea kuchukua mkataba King’s Music’ na kuwa msanii wa sita ndani ya kundi hilo ikiwa ni muda mchache tokea alipoachana na uongozi wake uliopita.

“Niweke wazi tu, kiukweli mimi sihitaji kwa sasa kusainiwa katika uongozi wowote ule, ninafanya kazi zangu mwenyewe chini ya ‘Bilionea kid’ ambayo ninaisimamia mimi“, amesema Rich Mavoko.

Mbali na hilo, Rich Mavoko amesema kwa sasa hana mpango wa kuachia albamu kwa kuwa amejipanga kuachia ngoma mfululizo ili kusudi aweze kutengeneza nyingine ambazo zinakuwa zenye nguvu na ushawishi wa kuwepo kwenye albamu.

“Sasa hivi nitaachia kazi nyingi, kama video zikifika 10 ndio nitatangaza rasmi kuhusu kutoa albamu, nasio hizi nyimbo hizi ambazo natoa kwasababu nyimbo hizi ninazozitoa sasa nimezitengeneza miaka 2 au 3 nyuma. Kwa hiyo inabidi zitoke halafu nitengeneza material mapya hivyo mashabiki watanisamehe kidogo”, amesisitiza Rich Mavoko.

Gigy Money Adai Akipewa Nafasi Atawamaliza Ali Kiba na Hemed PHD

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kudai kuwa endapo akiambiwa awagonge wanaume wowote ambao amewahi kuwa nao Kwenye Mahusiano basi atakuwa Ali Kiba na Hemed PHD na Rich Mavoko.

Gigy Money ambaye alianza kuongia Kwenye ulimwengu wa kisanaa kama Video vixen Mpaka sasa Msanii wa Bongo fleva amekiri Kuwahi kuwa Kwenye Mahusiano na wasanii wengi.

Gigy amekiri hapo nyuma kutokana na kufanya kazi za video na wasanii wengi basi pia ameshawahi kuwa nao Kwenye Mahusiano wengi sana na baadhi yao ni Rich Mavoko, Ali Kiba, Hemed PHD na wengineo.

Kwenye Interview moja aliyofanya hivi karibuni Gigy Money aliulizwa ni Ex gani wake staa ambaye leo hii akipewa ruhusa ya kumgonga na gari na kummaliza atamchagua nani?

Ikitokea nimepewa pesa niwagonge wapenzi wangu wa zamani, nitaomba nipewe fuso kabisa tena nitawasaga haswa nikianza na Hemed PHD, Ali Kiba na Rich Mavoko maana waliniumiza sana”.

 

Rich Mavoko na Diamond Wakutana BASATA Uso kwa Uso

Msanii wa Bongo Fleva, Rich Mavoko na lebo ya WCB wamekutana tena Baraza la Sanaa Taifa (BASATA).
Team ya WCB ilikuwa ikiongozwa na Diamond Platnumz pamoja na Sallam SK.
Pande hizo mbili ziliitwa na BASATA kwa lengo la majadiliano mara ya baada ya upande wa Rich Mavoko kulalamikia kile walichodai ni mkataba wa unyonyaji kutokea WCB.
Hata hivyo hadi pande zote mbili zinaondoka eneo la BASATA hazijaweka wazi ni kipi hasa kinaeendelea, hivyo wenye kauli ya kueleza yalipofikia mazungumzo hayo ni Baraza hilo lenyewe.
Mavoko alijiunga na WCB mwaka 2016 akisaini chini ya lebo hiyo na kuanza kufanya kazi akiwa chini ya lebo hiyo ambayo boss wake ni Diamond Platinumz.
Baada ya kujiunga na lebo hiyo Mavoko alianza malalamiko mapema mwaka huu kuwa anataka kujitoa katika lebo hiyo ya WCB wasafi kwa madai kwamba ananyonywa kimaslahi.
Mbali na kunyonywa kimaslahi lakini pia ilidaiwa kuwa kuna vitu ndani ya makataba huo msanii huyo hakutimiziwa na boss wake kama mkataba ulikuwa unaelekeza.
Malalamiko ya Mavoko yalionekana kuwagusa wengi na ikachangia Mavoko kukaa kimya kwa muda ingawa siku za hivi karibuni aliachia ngama yake mpya inayokwenda kwa jina la Ndegele.
Katika moja ya mahojiano aliyofanya meneja wa Diamond Salam Sk katika moja ya Redio hapa nchini alipoulizwa kuhusiana na madai haya ya mavoko alisema “Mavoko bado ni msanii wa WCB na hayo malalamiko anayotoa sisi hatujui yanahusiana na nini kwani huduma zote wanazopatiwa wasanii wa WCB anazipata”
Meneja huyo aliongeza “Kabla ya mavokonkusaini mkataba alipewa akakae nao aupitie hadi ajirizishe na Mavoko alifanya hivyo na kukaa nao ndani ya wiki mbili ndio akaurizia mwisho wa siku akaja kusaini sasa anacholalamika ni nini? sisi hatujui kwani makataba huo una kurasa 10 kwahiyo hatujui ni kitu gani anataka haswa”
Baada ya Mavoko kupeleka malalamiko hayo Basata,Basata nao waliamua kuwaita Maboss wa WCB walipofika wakaongea nao na ndio wakakubaliana wakutane siku ya leo August 23 katika ofisi hizo hapa Jijini Dar Es Salaam.

WCB Watoa Tamko La Rich Mavoko Kwenda Kujisajili BASATA Kwa Mara Ya Pili

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameamua kujitoa rasmi katika Label yake iliyokuwa ikimsimamia ya WCB kwa ajili ya mgogoro wa mkataba aliopewa.

Baada ya kutoka WCB, Mavoko alionekana akienda kushtaki katika Baraza la Sanaa Tanzania ambapo pia alidaiwa kwenda BASATA kwa ajili ya kujisajili upya pamoja na kwamba alishasajiliwa chini ya WCB.

WCB wameibuka na kudai taarifa za Msanii huyo kwenda kujisajili BASATA sio sawa kwani tayari ameshasajiliwa chini ya Label hiyo mapema mwaka huu.

Kwenye mahojiano na GPL, Meneja kutokea WCB, Sallam SK amesema hayo alipokuwa akieleza ushirikiano uliyipo kati ya WCB na Baraza hilo kwa sasa.

Suala la kusema hatushirikiani na BASATA hilo litakuwa si la kweli na sisi tunashirikiana nao sana kuna vitu vinatokea bahati mbaya. Lakini ukiangalia wasanii wetu wote wamesajiliwa BASATA na hamna yeyote ambaye hajawahi kujisajili. Hata juzi kati hapa ilisemekana kuwa Rich Mavoko ndio alienda BASATA akajisajili, hapana!, kashasajili kupitia WCB, actually mwezi wa saba mwaka huu”.

 

WCB Wadai Mamilioni Waliyowekeza Kwa Mavoko Hayajarudi Hata Robo

Msemaji wa Label ya WCB ambaye pia ni mmoja wa meneja wa Diamond Platnumz, Sallam Sk amemfungukia sakata hilo na kudai pesa ambazo Label hiyo zimewekeza kwa Rich Mavoko hazijrudi.

Wiki iliyopita msanii Rich Mavoko ambaye alikuwa chini ya Label hiyo kwa muda kidogo alitinga BASATA na kwenda kuwashitaki kwa mkataba wao wa kinyonyaji.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Sallam Sk ameweka wazi kuwa mpaka hivi sasa Rich Mavoko yupo chini ya WCB kimkataba zaidi.

Lakini pia ameweka wazi Kuwa mpaka sasa pesa ambayo wamewekeza kwa muimbaji huyo katika project zilizotoka haijarudi hata robo.

Mpaka sasa sielewi malalamiko ya Mavoko ni yapi kwa sababu ukisema sisi tunamnyonya mtu hicho kitu hakiwezekani alafu isitoshe Pesa ambayo tumewekeza kwa Rich Mavoko haijarudi hata robo”.

 

Diamond Atinga BASATA Kwa Ajili Ya Kesi Ya Mavoko

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi amefika katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya madai ya aliyekuwa msanii wake Rich Mavoko.

Rich Mavoko alimburuza Diamond na Label nzima ya WCB mbele ya BASATA kwa madai ya mkataba wa kinyonyaji waliompa wakati amesainiwa chini ya Label ya WCB.

Diamond aliongozana na Mameneja wake wawili, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Sallam Sharraf katika ofisi hizo mapema leo ili kuitikia wito.

Kwenye mahojiano na Global Publishers mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam, amesema waliitwa na Basata na sasa wapo katika mazungumzo ya kutatua jambo hilo na kufikia mwafaka.

Sallam amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji.

 

Lemutuz Amtaka Rich Mavoko Ajirudi na Kuwaomba Msamaha WCB

Mdau wa mambo ya sanaa na mwanasiasa William Malecela maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kama Lemutuz amemfungukia Rich Mavoko na kumtaka amalize mgogoro wake na iliyokuwa Label yake WCB.

Wiki iliyopita Rich Mavoko aliwaburuza WCB, Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kwa madai ya mikataba mibovu ambayo amedai imemnyonya na kutompa maslahi ya kufaa.

Baada ya sakata hilo Lemutuz amepima uzito suala hilo na kumshauri Rich Mavoko arudi WCB awaombe msamaha ili asiondoke kwa shari kwani hajui kesho yake ikoje.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lemutuz ameandika:

https://www.instagram.com/p/BmYiv0XgHtg/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=748bchr3azkz

Kitu cha Kwanza Alichoongea Rich Mavoko Baada ya Kushinda Kesi.

Baada ya kushinda kesi dhidi ya uongozi aliokuwa nao kwanza wa WCB ambapo kesi hiyo ilienda kusikilizwa katika ofizi za BASATA  nakuoneka kuwa Rich mavoko alisainishwa mkataba ulikuwa ukimkandamiza yeye pamoja na muziki wke kwa mara ya kwanza msnii huyo ametoa ujumbe mzito alkini wa kuishukuru BASATA kwa kumsaidia kutoka huko.

Katika ukurasa wake wa instagram, Rich mavoko aliandika “Nimejifunza vingi lakini kikubwa ni umhimu wa kukaa karibu na walezi wetu maana changamoto ni nyingi, na kuna mengi lakini yote mnaweza kuyajua kama tukiwa karibu na nyie, leo mmenipa maana ya neno mama ni mama hata kama akiwa kilema, hata iweje nyie ndio walezi wa sanaa yetu.”

Tangu kumekuwa na tetesi za Rich Mavoko kutoka katika lebel hiyo hakuwahi kuzungumza kitu chochote mpaka hapo alipomaliza kesi  hiyo na kuanza kuonekana kwa habari hiyo katika vyombo vya habari.

Rich Mavoko ni Moja ya Wasanii Waliosaini Mikataba ya Kinyonyaji:-BASATA

Katibu mtendaji wa Baraza la sanaa la taifa ,ameongea na waandishi wa habari na kuzungumzia swala la kushindwa kwa kesi ya Rich mavoko ambapo amethibitisha kuwa Rich Mavoko alikuwa amesainishwa mkataba wa kinyonyaji hivyo wao kama baraza kazi yao kubwa ni kwasaidia wasanii kama hao na kwa Rich mavoko ameshasaidiwa.

sio kwamba kila msanii anaekuja hapa anakuja kwa sababu anamatatizo na baraza hapana, rich mavoko alikuja baraza kuangalia maswala yake ya mktaba, kama vile ambavyo baraza lilitangaza kwamba  baraza linapokea wasanii wote wenye shida  na mikataba yao.

kwaio rich mavoko amelata mkataba wake ambao tumesema tutaupeleka kwenye ile kamati inayshughulikia mambo hayo ya mikataba ya wasanii ambayo ni ya kinyonyaji na rich mavoko ni mmoja wao.

Lakini pia mh mungerza amesema kuwa Rich mavoko hakuwahi kusajiriwa BASATA kwa kiindi chote alichokuwa akifanya kazi hivyo wamesajiri na kwa sasa anatambulika rasmi na baraza hilo.lakini pia ametoa wito kwa wasanii kutosaini mikataba bila kuielewa au kuwa na sheria ya kuwalinda.

lakini pia leo hiii amekuja na amesajiriwa na baraza , kumbe siku zote hizo alikuwa anafanya kazi lakini alikuwa hatambuliki na BASATA, kwaio amekuja na tumempa kibali cha kufanya kazi.Kwaio naomba wasanii wasiingie katika mikataba wasioielewa.

Rich Mavoko Afunguka Baada Ya Kuwaburuza WCB BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko amefunguka kwa mara ya kwanza na kuongelea sakata lake na uongozi wake wa zamani WCB.

Siku ya jana taarifa zilisambaa kuwa Rich Mavoko amepeleka kesi yake mbele ya Baraza la Sanaa (BASATA) baada ya Tetesi za wiki kadhaa kuwa ameamua kujitoa WCB.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rich Mavoko amesema kuwa anashukuru kukutana na BASATA na kupata elimu ya kutosha huku akiwamwagia sifa kuwa hao ndio maana halisi ya walezi wa sanaa yetu nchini Tanzania.

https://www.instagram.com/p/BmRCQzVAj05/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=133n0dixilgpb

Siku ya jana Rich Mavoko alikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza ambapo amepeleka mkataba wake na WCB ambapo ameomba uangaliwe upya na kudai ni wa unyonyaji.

Wasanii kadhaa na wafanyakazi wanaojitoa WCB wamekuwa wakilalamikia suala la mikataba mibovu kutoka katika kampuni hiyo na wengine kudai walikuwa hawalipwi.

Mpaka sasa uongozi wa WCB hawajajibu tuhuma hizo na madai hayo ya Rich Mavoko.