Lynn na Tunda Vitani Kisa Penzi La Diamond

Video vixen aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’ Lynn ameingia Kwenye vita kali na video queen mwenzake Tunda Sebastian na inadaiwa kisa ni Diamond.

Global Publishers wanaripoti kuwa warembo hao hivi sasa ni kama Paka na panya kutokana na wote wawili kumpenda Diamond na kuchanganywa kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa chanzo cha GPL, mrembo Lynn ambaye haambiliki kwa Diamond, mara baada ya kusambaa kwa video ya Tunda na Diamond pamoja  ndipo lilipotangazwa bifu jipya mjini kati ya Tunda na Lynn.

Si unajua ni juzi tu Lynn alidaiwa kuzawadiwa mpaka gari na Chibu (Diamond) wakati wa bethidei yake?

Sasa hiyo video ya Tunda imemtibua Lynn na timu yake kwa sababu Lynn humwambii kitu kwa Diamond ‘so’ sasa hivi ni mwendo wa vijembe tu huko social media (mitandao ya kijamii).

Wenyewe wanasema kama mwanamke akitaka kumtibua Lynn, basi ajisogeze kwa Diamond kama alivyofanya Tunda maana ameshasema kuwa yupo tayari kuolewa na jamaa huyo, sasa hataki mtu amtibulie”.

Baada ya Tetesi hizo za bifu gazeti hil lilimsaka Tunda ili kumhoji kuhusu bifu na Lynn ambaye alifunguka:

Jamani kama ujuavyo ile ilikuwa ni sherehe na kila mtu pale alikuwa ameshakunywa (amelewa) na wengi walikuwa wanacheza, nashangaa sana wameniona mimi tu ndiye nilikuwa nacheza na Diamond, kama siyo mambo ya ajabu ni nini?.

Mimi kucheza na Diamond imekuwa ishu kubwa, kitu ambacho kinanishangaza sana. “Ina maana watu waliniona mimi tu? Lakini mimi naona ni kitu cha kawaida kabisa kwangu hivyo watu wasipate tabu sana,” alisema Tunda. Alipoulizwa kuhusu mwanaume wake anasemaje juu ya video hiyo, Tunda alisema kuwa, kwa sasa hana mtu anayemhofia kwani alishaachana na Casto Dickson muda mrefu.”.

Lynn alipotafutwa ili kujibu tuhuma hizi alikataa kuzungumza chochote Lakini tangu sakata hili litokee Diamond ameonekana kwenye party mbili tofauti akiwa na video vixen mwingine maarufu kama Kim Nana.

Diamond Platnumz Atoa Kilio Chake Kwa Raisi Jakaya Kikwete

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz ameandika waraka mzito kuhusu muziki wa Bongo fleva na mchango wa Rais Jakaya Kikwete.

Raisi mstaafu Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mdau mkubwa sana wa Muziki wa Bongo fleva alikuwa anashehwrekea siku yake ya kuzaliwa jana na wasanii mbali mbali walimkumbuka akiwemo Diamond.

Diamond Kupitia ukurasa wake wa Instagram alikumbuka mchango mkubwa wa Raisi Kikwete kwa muziki wa Bongo fleva ambapo ameikosoa serikali ya sasa kwa kutofanya hivyo.

Miezi michache iliyopita serikali ilitangaza kuacha kuwatumia wasanii wa filamu na muziki na Bongo fleva katika kampeni zao za kisiasa hasa katika chaguzi kuu hii ni baada ya skendo zilizotokea baada ya kampeni za mwaka 2015.

Aunty Lulu Amshauri Diamond Afunge Ndoa

Muigizaji wa Bongo movie na Mtangazaji Lulu Semagongo maarufu kama Aunt Lulu ameibuka na kumtaka staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuoa.

Aunt Lulu amedai kwamba kutokana na Diamond ameshakuwa mtu Mzima anaamini kuwa akioa kutamletea heshima sana katika jamii.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la Risasi Jumamosi, Aunt Lulu alidai ameamua kumshauri staa huyo ambaye amekuwa akimpenda siku zote kutokana na kujituma kwake kikazi kwani si kila mwanamke ana nyota nzuri ya kumfanya aende mbali.

Unajua ujana huwa hausubiri, kadiri unavyosherehekea siku yako ya kuzaliwa ndivyo uzee unavyokaribi, sasa kwa Diamond ili azeeke vizuri, angeoa sasa kwani Waswahili wanakwambia kubadilibadili wanawake nako huleta mikosi na kujikuta ukianguka moja kwa moja“.

Aunt Lulu pia ameongeza kuwa akishaoa hata wanawake wanaojigonga kwake watapungua sana kwani ataheshimiwa.

Diamond Amkabidhi Mpiga Picha Wake Gari Jipyaa

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemfanyia bonge la surprise mpiga picha wake anayejulikana kama Lukamba baada ya kumkabudhi gari jipya.

Diamond amempa gari aina ya Toyota Alteza Lukamba siku ya Ijumaa iliyopita alipoenda kutoa msaada Tandale, ambapo Diamond alifunguka:

Lukamba anakaa Bunju, kuna kipindi alikabwa na kuchukuliwa hadi laptop sasa leo nampatia gari,”

Baada ya kukabidhiwa gari hilo, Lukamba alimuandikia Diamond ujumbe huu Kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Hadi Sasa Nimekosa Maneno Ya Kuandika Yatakayoweza Kubeba Hisia Zangu Za Furaha Niliyonayo,Nimekuwa Nikiandika Na Kufuta Kila Neno Ninaloandika Naona Halijitoshelezi Nahisi Halina Uzito Kuelezea Kilichopo Moyoni Mwangu….. Bro @diamondplatnumz umekuwa msaada sana kwa Sisi vijana maskini wenzako, Mungu azidi kukupa moyo wa kidogo unachopata kugawana na wenzako, pia nishkuru uongozi wa @wcb_wasafikwa kudhamini kidogo changu hii imenipa moyo sana wa kuzidi kujituma zaidi na zaidi
God bless you simbaaa ????????????@diamondplatnumz”.

 

Diamond Kutumia Zaidi Ya Milioni 465 Kwa Ajili Ya Misaada Tandale

Siku ya Ijumaa staa wa Bongo fleva Abdul Naseeb maarufu kam Diamond Platnumz anatarajia kutoa missada kwa Wakazi wa Tandale siku ya Kesho.

Katika kusheherekea siku yake ya kuzaliwa Diamond ametangaza kuwa ana mpango wa kutoa msaada mkubwa kwa Wakazi wa  ukifikia jumla ya shilingi 465.

Muimbaji huyo amedai atatoa bima za afya kwa kaya 250, ambapo kila kaya ni tsh milioni 1501200 kwa bima ya NHIF. Kwa maaana hiyo kwa kaya 250 atatumia zaidi tsh milioni 375.

Pia atatoa mitaji ya biashara kwa akina mama ambapo inakaridiwa atatumia zaidi ya tsh milioni 20 kwa akina mama 100. Alisema atagawa tsh laki moja mpaka laki mbili kwa akina mama wa Tandale.

Amesema atatoa pikipiki 20 kwaajili ya vijana ili wajikwamue kiuchumi ambapo inakadiriwa atatumia zaidi ya tsh milioni 50.

Diamond amesema atakarabati shule za Tandale pamoja na kuweka matanki ya maji ambapo ninakadiriwa atatumia zaidi ya tsh milioni 50.Kwa maana hiyo huwenda muimbaji huyo akatumia zaidi ya tsh milioni 465 kwaajili ya kutekeleza ahadi zake hizo.

Diamond amefunguka kuwa ni muhimu kwake kwenda kutoa msaada Tandale kwani ndipo alipotokea katika maisha ya ukata.

Diamond Ahaidi Kutoa Misaada Kwa Kwa Watoto 300 man Wanawake 200 Tandale

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kuweka wazi mipango yake ya kutoa msaada mkubwa Tandale kwa ajili ya kusheherekea Birthday yake.

Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Diamond Platnumz ameahidi kulipia BIMA ya Afya kwa watoto 300, kutoa mitaji kwa akina mama 200, kutoa Boda boda 20 na kukarabati Shule zote za msingi zilizopo ndani ya Kata aliyozaliwa ya Tandale.

Diamond akiongea kwenye sherehe fupi iliyofanyika Live kupitia Wasafi TV, amesema kuwa siku ya Ijumaa Tarehe 5 Oktoba 2018 atatimiza ahadi hiyo ikiwa na pamoja kuchinja ng’ombe na kusherehekea na watu wake wa Tandale.

Jambo la kwanza kabisa ni kuzungumza na vijana wenzangu wa Tandale ili kuwapa maneno ya kuwatia moyo. Lakini pia nitatoa bima za afya kwa watoto wasiopingua 300 na pia nitatoa mitano kwa wanawake 200”.

Diamond ametangaza kusheherekea Birthday kwa muda wa wiki nzima.

Tunda Abambwa na Diamond Baada Ya Kumwaga Casto (+video)

Socialite na video queen maarufu Bongo Tunda Sebastian amerudi Kwenye headlines baada ya kuonekana na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Tunda ameshawahi kusemekana kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond lakini baadae alianzisha Mahusiano na Mtangazaji wa clouds Tv Casto Dickson.

Pamoja na kwamba Casto alichora bonge la Tattoo ya Jina la Tunda Kwenye Mkono wake lakini aliishia  wiki chache zilizopita na siku ya jana ameonekana Kwenye Birthday party Diamond.

Diamond alionekana akicheza na Tunda kwa ukaribu sana kiasi ya kupelekea kuzua tetesi za kuwa Tunda kamtosa Casto na Kurudisha majeshi yake kwa Diamond.

https://www.instagram.com/p/BodZvdkn_6e/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1mcmagtlbnvu

Siku ya jana ilikuwa ni Birthday party ya Diamond na housewarming party ya nyumba yake mpya ambapo alifanya Private party na kualika Mastaa kibao ikiwemo timu nzima ya WCB , Navy Kenzo, Dully Sykes, Billnas, Tunda na wengineo.

Rich Mavoko Afungukia Bifu Lake na WCB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake na Label yake ya zamani ya WCB.

Rich Mavoko ameweka wazi kuwa pamoja na kwamba ameondoka katika Label hiyo lakini hana tatizo lolote na CEO wa Label hiyo Diamond Platnumz.

Kwenye Interview aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Rich amesema kuwa kilichotokea mpaka akaondoka Kwenye Label hiyo sio ugomvi bali muda wa kufanya Biashara ulifikia kikomo hivyo sasa wapo vizuri.

Lakini pia Rich Mavoko amemtaka meneja wa WCB Sallam SK kuwa na busara na heshima ni baada ya Meneja huyo kusema Mavoko hajarudisha hata robo ya pesa waliyowekeza kwake na kumtengeneza kama Brand:

Unajua Kwenye masuala ya kumzungumzia Rich Mavoko unazungumzia Brand ambayo ilikuwepo kwaiyo uliichukua kwa nia ya kufanya nayo biashara sasa umesema hajarudisha sasa na huyo mwenye talent atakuwa amepata?”.

Mavoko aliendelea kutiririka na kumwaga povu zito:

Mimi sitaki kuongelea sana hivi vitu kwa undani kila mtu anatakiwa kuheshimu kitu cha mwenzake ndio tuanze kuongeleana na kuongeleana vitu vibaya ni kutafuta mtu kujitetea”.

Diamond Auanika Mjengo Wake Mpya Wa Mabilioni

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ameanika hadharani kwa mara ya kwanza Mjengo wake unaotajwa kuwa na tahamani ya shilingi Bilioni 2.

Siku ya jana ilikuwa sherehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Diamond

Msanii alikuwa kwenye show yake nchini Zambia hivyo baada ya kurejea ameweza kutumia akaunti yake ya instagram kupitia insta stori kutuonyesha nyumba yake mpya akiwa na wasanii wenzake wa WCB.

Nipo Tayari Kufunga Ndoa na Diamond- Lynn

Video vixen  maarufu kweNey muziki wa Bongo fleva aliyejizolea umaarufu Kupitia video ya Rayvanny, Irene Godfrey maarufu kama  Lynn amesema kuwa yupo tayari kuolewa na Diamond Platnumz na hata mpenzi wake  anajua hilo.

Lynn ambaye katika wiki chache Hizi amekamata sana headlines kutokana na tetesi za kuwa Kwenye Mahusiano na Diamond ameibuka na kudai Yupo Tayari kwa ndoa na Bongo Star huyo.

Kwenye mahojiano na Waandishi kwenye red carpet ya Biko Jibebe Challenge, Lynn amesema kama ikitokea  nafasi hiyo atakuwa tayari.

Yeah! kwa sababu ni mwanaume, siwezi kusema hapana”.

Lakini pia Lynn alionekana kujikanyaga pale alipobanwa sana na maswali ya Mahusiano na Diamond ikiwemo gari ambalo alilopewa kama zawadi siku ya birthday yake ambalo lilisemekana limetoka kwa Diamond.

Hawa Afunguka Baada Ya Diamond Kumpa Milioni 50 Za Matibabu

Msanii wa Bongo fleva Hawa Mayoka aliyewahi kutamba katika ngoma ya Diamond Platnumz ‘Ntarejea’ amefunguka na kumshukuru Msanii huyo kwa msaada wake wa matibabu.

Wiki chache zilizopita Habari zilisambaa kuwa Hawa anaumwa hoi kitandani na kuomba msaada wa matibabu ambapo tatizo ni  ini.

Diamond amethibitisha Kupitia mitandao ya kijamii kuwa yupo katika harakati za kumpeleka Hawa nchini India kwa ajili ya matibabu na kusema anatoa zaidi ya Milioni 50 kwa ajili ya matibabu yake kutoka katika mfuko wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda,  Hawa amesema kitendo cha Diamond kujitolea kumsaidia matibabu ya kumpeleka nchini India kimemliza mno kwa sababu hakujua kama ipo siku angemkumbuka.

Nilivyosikia Diamond ameamua kunisaidia nilijisikia furaha mpaka machozi yakawa yananitoka maana sikuamini, Mungu atamlipa na namuombea azidi kuwa na moyo huohuo.

Nilishakata tamaa kabisa ya kupata matibabu kutokana na uwezo wa kifedha kuwa mdogo kwani madaktari wa hapa walisema natakiwa kutibiwa India, kwa sasa nimepata tumaini jipya baada ya Diamond kujitolea kunipeleka kwenye matibabu India“.

 

Navy Kenzo Wafungukia Tetesi Za Kijamii WCB

Kundi la muziki la Navy Kenzo linaloundwa na wasanii  ambao ni Producer na msanii Nahreel na mpenzi wake Aikah limefungukia tetesi zilizosambaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wamesiniwa na lebo ya WCB.

Navy Kenzo walitengeneza headlines wiki iliyopita baada ya kutotoa ngoma kali waliomshirikisha Diamond lakini baadae kuna tetesi zilisambaa kuwa kundi hilo linasiniwa na linakuwa chini ya WCB.

Tetesi hizo zilishika kasi mara baada ya Harmonize kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anawakaribisha kundi hilo katika Label ya WCB na Nahreel alionekana kukubaliana na Harmonize.

Lakini Navy Kenzo wamekanusha taarifa hizo na kuweka wazi kuwa wenyewe wako chini ya Meneja Salaam SK ambaye pia ni Meneja wa Diamond lakini sio chini ya WCB na kama siku wakijiunga WCB tamko litatoka rasmi kwao.

Navy Kenzo wanafanya vyema sana na wimbo wao mpya wa ‘Katika’ waliomshirikisha Diamond Platnumz ambao mpaka hivi sasa wanashikilia nafasi ya kwanza katika kutrend Kwenye Media mbali mbali.

 

Diamond Alitaka Kunioa Mke Wa Pili, Nilikuwa Tayari- Hamisa

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka na kuweka wazi uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Hamisa amekiri kuwa wakati anaanzisha Mahusiano na Diamond, tayari Diamond alikuwa Kwenye Mahusiano na Zari na walikuwa wamezaa watoto.

Kwenye Interview yake aliyofanya akiwa nchini Kenya, Mobetto amefunguka haya:

Wakati nakutana na Diamond nilijua kuna Zari na nilimuuliza, akasema mimi ni muislam na uwezo wa kuoa hata wanawake wawili,” alisema Mobetto. “Na mimi nipoo tayari hata kama ningekuwa nimeolewa halafu mume wangu anataka kuoa mke wa pili ningemruhusu“.

Hamisa alibeba mimba ya Diamond wakati akiwa Kwenye Mahusiano na Zari jambo lililoleta mtafaruku na kupelekea kuachana kwao mwishowe.

Baada ya Diamond kuachana na Zari alikuwa Kwenye Mahusiano na Mobetto Tena lakini Mahusiano hayo yaliingia doa kwani Hamisa ameishia Kwenye ugomvi mkubwa na Familia na Diamond na kuishia kuachana naye.

Mange Kimambi Amshauri Hamisa Asirudi Kwa Diamond Adai Ana Gundu

Mwanaharakati wa Mambo ya siasa Mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa Mobetto asithubutu kurudi tena  kwa mzazi mwenzake Diamond Platnumz kwa madai kuwa ana gundu.

Hamisa aliweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz waliachana Mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kuwa pamoja kwa miaka kadhaa.

Lakini baada ya kuachana Hamisa aliingia kwenye mgogoro na Familia nzima ya Diamond ambao waliishia kumtangaza kama mchawi mara baada ya kuwaendea kwa mganga.

Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa asirudiane Tena na Diamond kwa madai kuwa familia nzima ya Diamond ilikuwa inampa gundu tu kwani sasahivi tangu ameachana nao amekuwa akipata madili mengi ya ubalozi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BoGFxI6larV/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1o9n4uzj4l67d

Diamond Amkana Irene Adai Yupo Naye Kikazi Tu

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amekana kabisa kuwa Kwenye Mahusiano na video vixen maarufu kama Irene Godfrey maarufu kama Lynn.

Tetesi za wawili hao kuwa Kwenye Mahusiano zilipamba moto wiki iliyopita baada ya picha zilizowaonyesha wako pamoja kusambaa Kwenye mitandao ya kijamii.

Baada ya Tetesi hizo Gazeti la Ijumaa lilimsaka Staa huyo ili kupata ukweli kuhusu taarifa ambapo alimkana binti huyo na kufunguka:

Kwa nini kila mwanamke nahusishwa naye? Tatizo kila mrembo ninayekuwa naye karibu kikazi watu wanasema natembea naye. Hakuna chochote kati yangu na huyo Lynn zaidi ya kufahamiana naye kikazi.

Kuna wakati napata ugumu sana maana kila mwanamke ninahusishwa naye wakati hata sijawahi kumtamkia neno la mapenzi zaidi ya kazi tu.

Unajua kazi yangu ni muziki so (hivyo) kukutana au kuwa karibu na warembo ni sehemu ya kazi yangu, sasa watu wakiniona nao wanajua tayari niko nao kimapenzi

Lakini pia, gazeti la Ijumaa lilimtafuta mwanadada huyo na kumbana ili kupata undani wake na Diamond kama wapo kwenye uhusiano au walikwenda kwa ishu ya kikazi, lakini aliishia kutoa povu kwa mwandishi wetu.

Nini? Bwana? Mi’ sijui, mniache na maisha yangu, tena mniache”.

Diamond Amuunga Mkono Jokate Kupitia ‘Tokomeza Zero’

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz ameingia Mkono jitihada za Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Jokate Mwegelo katika kuboresha elimu.

Wiki iliyopita Jokate alitangaza kufany harambee kwa ajili ya maboresho ya elimu katika Shule ya Minaki siku ya Jumamosi.

Wasanii kadhaa wameunga Mkono jitihada hizo akiwemo Aliyekuwa mpenzi Msanii Diamond Platnumz ambaye Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewataka wananchi mbali mbali kushiriki siku ya kesho.

https://www.instagram.com/p/Bn-5ProhAVW/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=e0qllefy8n56