Diamond Platnumz na Irene Waonekana Pamoja Zanzibar (+picha)

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz amedaiwa kuonekana kwenye visiwa vya Zanzibar akiwa na video queen Irene Hillary.

Diamond ambaye alitangaza kuwa yupo Single wiki iliyopita baada ya kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi na mama  watoto wake Hamisa Mobetto, ameonekana kupata mpenzi mwingine.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Diamond ana Mahusiano ya Kimapenzi na Irene mpaka kuna muda ilisemekana kuwa aliwahi kubeba ujauzito wake.

Diamond ambaye kwa sasa yupo visiwani  Zanzibar kwa ajili ya kazi zake za sanaa anadaiwa kuonekana na Mrembo Irene wakiwa bega kwa bega kuonyesha kuwa wako pamoja.

Picha ambayo inasambaa Kwenye mitandao ya kijamii inawaonyesha wawili hao wakiwa pamoja na crew nzima ya WCB:

 

Zari Ni Hodari Wa Mapenzi- Diamond Platnumz

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amesuka gumzo siku ya jana Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuimba kipande cha wimbo chenye maneno “Zari hodari wa Mapenzi”.

Diamond ambaye alikuwa Kwenye Mahusiano na Zari kwa takribani miaka minne mpaka walivyimwagana mapema mwaka huu aameibuka na kusifia ujuzi wa mapenzi wa mama watoto wake huyo.

Diamond amesema maneno yake Kupitia kipande cha video Kilichomuonyesha akiimba wimbo mpya wa Msanii kutoka WCB Mbosso uitwao ‘Hodari’ ambapo ndani yake amemtaja Zari kama Hodari wa mapenzi.

Miriam Odemba Amtolea Povu Zito Diamond Platnumz

Mlimbwende mkongwe Tanzania Miriam Odemba amemjia juu staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kudai amemfhalilisha mama mtoto wake Hamisa Mobetto.

Miriam Odemba ameibuka na kumpa vipande vyake kuwa, hakustahili kumsema vibaya mzazi mwenzake, Hamisa Mobeto kwa kumrushia tuhuma nzito ambazo zimemfanya

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi akiwa nchini Ufaransa, Odemba alisema kuwa hakuna kitu kibaya kama kumtolea maneno ya kashfa mzazi mwenzio na hata kama kuna sehemu aliteleza, busara inatakiwa kutumika:

Yaani mimi sijapendezwa kabisa na alivyofanya Diamond, kwa maana anapaswa kuheshimu hata kile kiumbe kilichowaunganisha. Kama kuna matatizo ya kifamilia ni vyema kukaa chini na kumalizana, lakini siyo kuyaweka kwenye kadamnasi kama alivyofanya Diamond. Kuna siku watakutana kama wazazi, hivi atajisikiaje? Amekosea sana”.

 

Diamond Adaiwa Kufaidi Penzi La Mrembo Wa Kinyarwanda

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na CEO wa WCB ameingia Tena Kwenye skendo ya Kimapenzi na Mrembo kutoka Rwanda anayejulikana kama Shaddyboo.

Diamond ameshawahi kusemekana kuwa na mahusiano na Mrembo huyo siku za nyuma wakati bado Yupo na Baby mama wake Zari, ambapo ameonekana naye kila akienda nchini Rwanda kwa ajili ya shoo.

Tetesi za wawili hawa kuwa Kwenye Mahusiano zilianza mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Shady Boo kuja Tanzania kwa ajili ya kuwa Host ya Jibebe Challenge ya Diamond Platnumz.

Shadyboo alichochea tetesi za kuwa kwenye mahusiano na Diamond baada ya kuposti video iliyomuonyesha akiwa hotelini ambako inasemekana ni chumba kimoja ambacho alionekana Diamond pia.

Lakini pia Shadyboo aliposti video Kwenye mtandao wa Instagram iliyomuonyesha akikata mauno balaa akicheza wimbo wa Jibebe wa Diamond.

Pamoja na tetesi kusambaa kuwa Diamond anafaidi Penzi la Mrembo huyo, hakuna aliyekiri wala kukataa taarifa hizo.

Diamond Platnumz Atangaza Ujio Wa Kolabo Yake na Lil Wayne

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ametangaza ujio wa Kolabo yake na Staa wa rap kutoka Marekani Lil Wayne.

Siku za nyuma kulikuwa na tetesi kuwa Diamond anakuja kufanya Kolabo na wasanii wakubwa duniani baada ya kwenda kukaa Marekani kwa muda wa mwezi mzima.

Siku za nyuma  meneja wake Sallam Sk wakati anafanyiwa mahojiano na kituo cha habri cha Times Fm alifunguka na kusema kuwa kuna kitu kizuri kinakuja baada ya kuulizwa swali juu ya kolabo ya msanii wake ambaye ni Diamond na msanii wa nje na kusema kuwa kuna kolabo inakuja akiwa amefanya na Lil Wayne

Diamond ametangaza habari njema kuwa kolabo inayokuja na msanii mkubwa ni Rapa Lil Wayne ingawa hajatoa maelezo ya zaidi kuhusu Kolabo hiyo Lakini ametoa kionjo kidogo cha ngoma hiyo.

Diamond licha ya kufanya kolabo kadhaa kutoka nje ya nchini mfano Nigeria na nchini nyinginezo kutoka Afrika lakini pia msanii huyo amewahi kufanya ngoma na wasanii kutoka Marekani wakiwemo Neyo nyimbo inayojulikana kama Marry you, Rick Ross ngoma ya Waka waka na Omario ngoma ya African Beauty lakini pia ngoma ya Halleluyah akifanya na kundi la Morgan.

Uwoya Afungukia Mahusiano Yake na Diamond

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka na kuelezea Mahusiano Yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya kuzua gumzo siku za hivi karibuni.

Uwoya na Diamond walitengeneza headlines mwishoni  wa wiki iliyopita baada ya Diamond kumposti Mrembo huyo Kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kuweka caption yoyote jambo lililozua maswali mengi.

Pamoja na maneno ya hapa na pale ilikuja kujulikana kama Diamond alikuwa amemlipa Uwoya kwa ajili ya ku host Shindano la Jibebe challenge ambalo lilifanyika siku ya Jumapili.

Pamoja na hayo bado Kumekuwa na tetesi kuwa Wawili hao wana mahusiano ya zaidi ya kikazi ilihali Uwoya ni Mke wa Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja.

Kwenye mahojiano na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) Uwoya amesema kuwa alichukulia kitendo Cha Diamond kumposti  kawaida ingawa watu walitafsiri vibaya lakini hana Mahusiano na Msanii huyo zaidi ya urafiki wa kawaida:

Sioni kama ni tatizo kwa sababu aliposti tu picha ambayo mtu mwingine anaweza akaposti. Watanzania wanapenda tu kufikiria vitu, ku-judge wanavyoweza wao, haikuwa tatizo kwangu”.

Siku ya Jumapili Kwenye Biko Jibebe Challenge  Irene Uwoya ndiye alikuwa host wa tukio hilo. Shindano hilo lilianzishwa na Diamond baada ya kutoa wimbo wake unaokwenda kwa jina la Jibebe ambao ameshirikiana na Mbosso na Lava Lava.

Diamond Adaiwa Kumnyapia Nyapia Irene Uwoya

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amerudi tena kwenye headlines akihusishwa na mwanamke mwingine ambapo safari hii Malkia wa Bongo movie Irene Uwoya.

Siku ya jana Diamond aliwashangaza mashabiki zake baada ya kuposti picha ya Irene Uwoya katika ukurasa wake wa Instagram bila kuambatanisha na ujumbe wowote hali iliyopeleka mashabiki hao kukosa majibu.

Baadhi ya watu walimjia juu Diamond kwa kitendo kile na kudai anakuwa anakosea kwa sababu Irene ni mke wa mtu lakini pia anakuwa anamkosea heshima Dogo Janja ambaye ni msanii mwenzake lakini pia ni mume wa halali wa Uwoya.

Lakini pia kuna baadhi ya mashabiki walimvaa Uwoya kwa kitendo chake cha kulike picha ile ya Diamond kumaanisha kuwa anafurahia attention ile anayoipata kutoka kwa Diamond na hata kumwambia anamuonea mume wake Dogo Janja kwa sababu ni mdogo kwake.

Diamond tena alienda kulike na kukomenti makopa kopa kuonyesha amekubali tena picha nyingine iliyopostiwa na Uwoya. Kitendo hiki kimetafsiriwa tofauti tofauti na watu kwani wapo waliosema Diamond anafanya hivyo ili kupata kiki, ingawa hakuna aliyesema kitu chochote yote haya ni mawazo ya mashabiki.

Ikumbukwe siku za nyuma kuliwahi kusemekana kuwa Diamond ameshawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Uwoya.

Aunty Lulu Amdondoshea Mate Diamond

Msanii wa Bongo movie Lulu Semagongo maarufu kama Aunty Lulu amefunguka na kudai anataka sana kuzaa na msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Aunty Lulu amesema kuwa ingawa anajua itakuwa ngumu kwa yeye kuzaa na Diamond kwa sasa kutokana na Msanii huyo kusema amejifunza kutumia kinga ili kuepuka watoto wa nje lakini yuko tayari kutafuta mganga wa kumloga.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Aunty Lulu amesema ni ndoto yake ya muda mrefu kuzaa na Diamond hivyo ili itimie atafanya juu chini mpaka ampate hata kwa kumloga ili akikutana naye asahau hata kutumia kinga aweze kumpa ujauzito.

Diamond amesema kwa sasa yuko makini ili asizae nje ya ndoa lakini kwangu mimi nitamloga mpaka aweze kuzaa nami kwa kuwa ni muda mrefu nina ndoto hiyo na hakuna kitakachonizuia maana namwamini sana mganga wangu“.

Kwenye Interview aliyofanya mwezi uliopita Diamond alidai kuzaa na Hamisa ilikuwa ni kosa hivyo amejifunza kutumia kinga anapokuwa na michepuko.

“Unaonekana Hushindwi Hata Kumuua Mama Yangu” Diamond Amshukia Hamisa Baada Ya Skendo Ya Uchawi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemshirikisha mzazi mwenzake Hamisa Mobetto baada ya skendo za kumloga kwa waganga kupamba moto.

Sakata hilo limetokea baada ya voice note zilizomuhusisha Hamisa na mama yake wakiwa wanazungumza na mganga kusambaa Kwenye mita ya kijamii.

Kwenye voice note hizo Hamisa anasikika akimuomba mganga amfanyie dawa ambayo itamfanya Diamond ampende na amuoe na Mama Diamond na Familia yake imkubali kama zamani.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Diamond amefunguka kuhusu sakata hilo na kumwagia povu zito Hamisa:

Unapotaka kwenda kwa mganga uniroge mimi na mama yangu, unaonekana wewe haushindwi hata kumuua mama yangu, kama unawaza sijui nikupe nyumba. Voice notes zinasambaa sambaa hata mimi nilitumiwa, ninazo unasikia kitu halafu unajua huyu ni yeye, halafu nikamwambia huyu ni wewe.

Watu kuna vitu wanaongea ongea halafu wanajaribu kuvipindisha aonekane Mama yangu na dada yangu wana matatizo, mama yangu na dada yangu hawawezi kuwa na matatizo. Halafu hao watu wako unaowatuma wakatukane nimeshakuona ukiwatuma wakatukane kwa watu wengine kwa sababu pia uliwatuma pia wamtukane na Zamaradi”.

Wiki hii dada wa Diamond Platnumz, Esma aliandika ujumbe mrefu kukanusha taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao kwamba wameandaa voice note kwaajili ya kumchafua Hamisa Mobetto.

Diamond Ataja Kilichomsibu Mpaka Kusuka Rasta

Staa wa muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amefunguka kuhusu staili yake ya kichwani inayoendelea kutengeneza headlines.

Siku ya leo Diamond amezua gumzo baada ya kuanika staili yake baada ya kutupia picha iliyomuonyesha akiwa amesuka Rasta katika staili ya kipekee.

Mara moja Diamond alianza kutrend huku watu wengi wakimponda na kudai amesuka Rasta kama mwanamke huku mashabiki wengine wakimpongeza kwa ubunifu.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Diamond aliulizwa maswali ya Nini hasa kilichomsukuma mpaka kufikia uamuzi wa kusuka nywele kwa staili na akafunguka kuwa ameamua kubadilisha staili ya nywele zake:

Nimeamua kubadilisha muonekano lakini baadae nitabadilisha Tena”.

Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kutengeneza nywele na kuzua gumzo mara kwa mara amekuwa akija staili mpya ambayo inazua gumzo na kutrend sana.

Mange Amkingia Kifua Mobetto Dhidi Ya Familia Ya Diamond Kufuatia Tuhuma Za Uchawi

Mwanaharakati wa mambo ya siasa na mdau wa mitandao ya kijamii Mange Kimambi amemkingia kifua Hamisa Mobetto baada ya familia ya Diamond kumuandama na skendo za ushirikina.

Mama Diamond na Esma Platnumz wamemtuhumu Hamisa kwa uchawi ambapo wamedai kuwa alienda kwa mganga kwa nia ya kumloga Mama Diamond na Esma ili wampende na aolewe na Diamond.

Mange ameibuka na kumtetea Hamisa dhidi ya tuhuma hizo na hata kuwatupia maneno ya shombo familia ya Diamond na Wema Sepetu ambaye pia ameonekana kumsema na kumtupia vijembe Hamisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BnMqWQFFRTt/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1d4duzu19snyf

Familia Ya Diamond Yamtuhumu Mobetto Kwa Uchawi

Familia ya staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz imerudi kwenye headlines kwa bifu lao na mzazi mwenza wa Diamond, Hamisa Mobetto.

Bifu la Hamisa na Familia ya Diamond lilianza baada ya Hamisa kuzaa na Diamond ambapo Hamisa alisambaza picha zake na Diamond na hata kuwaitia Shilawadu Mama Diamond na Esma.

Mama Diamond na dada wa Diamond, Esma wamekuwa wawazi juu ya chuki yao kwa Hamisa lakini siku mbili hizi pande Hizi mbili ziliingia kwenye mzozano mkali kwenye mtandao wa kijamii.

Mama Diamond na Esma wamemtuhumu Hamisa kwa uchawi ambapo wamedai kuwa Hamisa alienda kwa mganga kwa nia ya kumloga Mama Diamond na Esma ili wampende na aolewe na Diamond.

Inasemekana kuwa kuna voice note ambayo Hamisa alirekodiwa na mganga akiwa anaongea na kwa kuwa mganga huyo anafahamiana na Mama Diamond basi akamtumia.

Esma, Mama Diamond na Wema wameonekana kumtupia vijembe Hamisa kwa tuhuma za uchawi:

Hamisa hajakana wala kukubali tuhuma hizo za uchawi lakini kuna baadhi ya mashabiki zake wamekuwa wakidai kuwa skendo hiyo imetengenezwa na Mama Diamond na Esma ambao wamefoji Voice note.

Sallam SK Adokeza Ujio Wa Kolabo Ya Diamond na Rihanna

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Sallam SK amedokeza uwezekano wa Kolabo kati ya Diamond na staa wa RnB kutoka Marekani,  Rihanna.

Kwenye mahojiano na Kituo kimoja cha habari, Sallam SK alijibu maswali katika kipengele cha YES/NO au NDIO/HAPANA kwenye …swali la endapo kuna collaboration kati ya Diamond na Rihanna, Meneja alijibu YES.

Siku za nyuma kumsema wahi kuwa na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kufanya kolabo na Rihanna ingawa uongozi wa Diamond haujaongelea kiundani zaidi kuhusu kolabo hiyo.

Diamond tayari ameshafanya Kolabo na wasanii wakubwa Marekani kama vile Neyo katika wimbo wake wa ‘Marry me’ na Rick Ross wimbo wa ‘Waka waka’.

TID Awashukia Diamond na Wasanii Wengine Wanatumia Jina La Mnyama

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID amewatolea povu Wasanii Wenzake kama Diamond na wasanii wengine wengine ambao wamekuwa Kwenye mgogoro juu la majina ya wanyama na kudai yeye ndiye mwanzilishi.

Siku za nyuma ulishawahi kutokea mgogoro wa majina baina ya wasanii ambapo baada ya Diamond kujiita simba wasanii kadhaa walidai wao ndio walikuwa simba kabla yake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, TID amefungukia wasanii wanaojiita wanyama na kudai wao wamemuiga yeye kwani alipewa jina la Mnyama miaka kumi iliyopita:

Mimi jina la mnyama nimepewa miaka kama kumi iliyopita ndio maaana sasahivi unaona kuna wanyama wengi wanajitokeza tokeza because they like the swagg, they feel the swagg, they feel the talent.

Walikuwa wanataka kuwa mimi huko nyuma na wanataka kuwa kama mimi mpaka leo, so Mnyama is my brand yaani nikitokea watu wanajua Mnyama halafu ndio wengine wanakuja sijui petty anaimals sijui domestic animals”.

 

Waziri Mwakyembe Kulifungia Kazi Bifu La Diamond na Ali Kiba

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kuhaidi kulimaliza bifu linaloendelea kati ya wasanii wawili wakubwa wa Bongo fleva.

Dkt. Mwakyembe ameweka wazi kuwa kama Mlezi wa wasanii Tanzania ameamua kulimaliza kwa kulishughulikia bifu kati ya Diamond na Ali Kiba kwani linaonekana kutoleta picha nzuri  kwenye Muziki wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano na Kampuni ya Global Publishers, Waziri Mwakyembe alisema kuwa, yeye hadhani kama kuna tofauti kubwa kati ya wasanii hao bali anaona kwamba mashabiki ndiyo wanaolikuza bifu hilo kwa sababu wanazozijua wenyewe.

Nahisi mashabiki wa hawa wasanii wawili ndiyo wanaolikuza hili bifu. Lakini pia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vikishaandika ndipo inaonekana kuna shida lakini kumbe siyo hivyo.

Labda niseme tu kwamba, kuna kitu naandaa na hivi karibuni mtawaona pamoja na hiyo itawafanya muamini kuwa hawana bifu kama inavyojaribu kukuzwa”.

Diamond na Kiba kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa kuwa kwenye bifu kubwa ambapo mbali na mara kadhaa kurushiana maneno makali pamoja na kwamba wamekataa kuwa Kwenye bifu.

 

Diamond na Bob Junior Watangaza Kuja Na Kazi Mpya

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB, Diamond Platnumz na msanii mwenzake na producer kutoka Sharobaro Records Bob Junior wametangaza kuja na project mpya.

Diamond na Bob Junior ambao kwa muda mrefu wamekuwa na tofauti wameonekana kuzimaliza tofauti hizo na kuamua kufanya kazi pamoja kama zamani.

Siku ya jana kuna kuna video clip ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Diamond na Bob Junior wakiwa pamoja na kuwataka mashabiki kukaa mkao wa Kula kwani kuna kazi wanafanya pamoja

Wasanii hao wawili walikuwa na tofauti kipindi cha katikati kwani maelewano yao hayakuwa mazuri kutokana na kutofautiana kikazi, lakini hivi sasa wasanii hao wanaonekana kuwa katika nafasi nzuri.