Kitendo Cha Diamond Kumuita Mobetto Mchepuko Chamliza Mama Hamisa

Siku chache zilizopita staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz aliwaacha watu midomo wazi baada ya kufanya Interview na Kwenye Interview hiyo kumuita Hamisa Mchepuko.

Kwenye clip hiyo ya Diamond inayodaiwa kuwa ni mahojiano yake aliyoyafanyia nje ya nchi, Diamond alisikika akijilaumu kuwa mwaka 2017 ulikuwa mbaya maishani kutokana na matukio mabaya yaliyomtokea. Alisema, mwaka huo ndiyo ambao aligombana na mpenzi wake wa muda mrefu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ aliyezaa naye watoto wawili, mmoja wa kike.

Alisema hayo yote yalitokea baada ya kuchepuka na Mobeto na kujikuta amempa ujauzito na hata Zari alipojaribu kuhoji baada ya kusikiasikia fununu, alijaribu kumficha ili kulinda uhusiano wake, lakini hata hivyo jipu lilikuja kupasuka baada ya Mobeto kuvujisha picha zao wakiwa kimahaba chumbani, jambo ambalo lilimharibia sana.

Baada ya clip hiyo kusambaa mashabiki wa Hamisa walimjia juu Msanii huyo na kumtuhumu kwa tabia mbaya ya kudhalilisha wanawake hasa ambao amekwisha zaa nao.

Baada ya sakata hilo Global Publishers lilimsaka mama mzazi wa Hamisa Mobetto, Shufaa Lutiginga ambaye alionyesha kutofurahishwa na Kauli hizo za mkwewe  dhidi ya mwanaye Mobetto:

Jamani inauma na kwa kweli nisingependa hayo mambo jamani kuyaongelea mimi… jamani naombeni sana mtafuteni huyo mwenyewe aliyesema au Mobeto tafadhali, niacheni mimi nipumzike”.

Lakini pia Kwenye Interview hiyo  Diamond alisikika akiwaasa vijana wote wenye wapenzi wao ‘serious’ au wenye wake zao, kuwa makini pindi wanapokuwa na michepuko ili kuepuka kupata watoto wa mchepuko kama ilivyomtokea yeye, jambo ambalo limekuwa baya maishani.

Mtoto wa Hamisa Uso Kwa Uso na Familia Ya Diamond (picha)

Mtoto wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto Dylan ameonekana kwa mara ya kwanza aliwa na Familia ya upande wa Diamond baada ya mgogoro wa muda mrefu.

Tangu Hamisa azae na Diamond Kumekuwa na sintofahamu kwani wanafamilia upande wa Diamond hawajawahi kuonekana wakiwa na mtoto wa Hamisa kama ilivyo watoto wengine wa Diamond na Zari.

Mama Diamond ameshawahi kudaiwa kumshushia kipigo kizito Hamisa baada ya kuweka wazi kumchukia baada ya kumuitia Shilawadu ili waweze kumpiga picha.

Lakini wiki chache zilizopita Mama Diamond aliweka wazi kuwa pamoja na  kuwa na  tatizo na Hamisa lakini hana tatizo na mjukuu wake Dylan na amethibitisha hilo kwani siku ya jana picha zilizomuonyesha Diamond, mama Yake na dada yake pamoja na Dylan zilisambaa mtandaoni:

 

 

Diamond Athibitisha Kushusha Mjengo Mwingine Afrika Ya Kusini

Staa wa muziki wa Bongo fleva ambaye anafanya vyema hivi sasa na ngoma  yake ya ‘Jibebe’ (I Like It) ameweka wazi kuwa ana mpango wa kuongeza Mjengo mwingine nchini Afrika ya kusini.

Diamond ambaye tayari anamiliki nyumba moja nchini Sauzi ambayo inatajwa kuwa na thamani Dola za kimarekani 500,000 $ ambazo ni sawa na shilingi 1,143,700,000 za Kitanzania.

Diamond amethibitisha taarifa Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika:

Still in love with my first South Africa house…. adding the new house in here before end of the year”.

Diamond tayari ana mijengo kadhaa nchini lakini pia nyumba yake ya South Africa ndiyo anayoishi mama watoto wake Zarinah Hassan maarufu kama Zari The Bosslady pamoja na watoto wake.

Hakuna Bifu Kati Ya Ali Kiba na Diamond- Sallam Sk

Meneja wa Staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Sallam Sk amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna bifu kati ya Diamond na Ali Kiba.

Sallam amedai kuwa viongozi wa WCB wanakutana mara kwa mara na uongozi wa Alikiba na kuzungumza mambo mbalimbali.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa bifu kati ya Diamond na Ali Kiba ingawa kila mmoja amekuwa akikataa na kusisitiza kuwa hakuna bifu.

Kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Sallam alifunguka mambo mengi huku WCB pamoja na muziki ambapo pia alifunguka kueleza kwamba sio kweli kwamba Diamond ana bifu na Alikiba huku akienda mbali zaidi kwa kudai viongozi wa label hizo mbili hukutana mara kwa mara.

Kati ya Ali na Diamond hakunaga bifu, na haijawi kutokea, na uongozi wa Alikiba na WCB huwa unakutana mara kwa mara kuzungumza,” alisema Sallam. “Bifu ilitengenezwa na sisi baada ya kuona watu wanapenda hivyo vitu tukavitumia kwaajili ya kupromote wimbo wetu”.

 

Diamond Atinga BASATA Kwa Ajili Ya Kesi Ya Mavoko

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi amefika katika ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa ajili ya madai ya aliyekuwa msanii wake Rich Mavoko.

Rich Mavoko alimburuza Diamond na Label nzima ya WCB mbele ya BASATA kwa madai ya mkataba wa kinyonyaji waliompa wakati amesainiwa chini ya Label ya WCB.

Diamond aliongozana na Mameneja wake wawili, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Sallam Sharraf katika ofisi hizo mapema leo ili kuitikia wito.

Kwenye mahojiano na Global Publishers mmoja wa meneja wa Diamond, Sallam, amesema waliitwa na Basata na sasa wapo katika mazungumzo ya kutatua jambo hilo na kufikia mwafaka.

Sallam amesema ni vyema watu wakasubiria yatakayoamuliwa huko, ambapo wanaamini Basata itauambia umma nini kilichoafikiwa badala ya wao  kuwa wasemaji.

 

Zari Aweka Pembeni Tofauti Zake na Hamisa na Kumtumia Dylan Salamu za Birthday

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameweka tofauti zake pembeni na Mzazi mwenza mwingine wa Diamond Hamisa, na kumtakia heri mtoto wake Dyalan.

Zari na Hamisa walikuwa kwenye vita kali tangia Zari alipoginfua Diamond kamsaliti na kuzaa na Hamisa wakati wakiwa Kwenye Mahusiano kimapenzi.

Lakini sasa Zari anaonekana kuweka pembeni tofauti hizo hasa linapokuja suala la watoto kwani amemtumia salamu za Birthday Dylan na kukiri yeye ni mtoto na hana makosa.

Kwenye mahojiano hayo na kituo kimoja cha habari nchini Uganda ambapo Zari anategemewa kuwa JAJi katika mashindano ya Miss Uganda, amefunguka na kusema hana kinyongo na Dylan kwani ni mtoto ambaye hana makosa na sio kosa lake yuko pale:

Siku ya Jumatano ilikuwa Birthday ya Dylan mtoto wa Diamond na Hamisa na Zari alimtumia salamu Hizi:

Happy birthday Dylan, Hope you have the best in life and Mummy Z loves and no matter what the public says it was never your fault you were just caught up in it and you happened and i know the internet will torment you and say you were a child who came to break another woman’s family but no matter what you are here and I hope you grow up to be something big”.

Rich Mavoko Ashinda Kesi Dhidi Ya WCB BASATA

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Rich Mavoko ameripotiwa kushinda kesi dhidi ya Label yake ya zamani WCB na kufanikiwa kuvunja mkataba na kutoka.

Rich Mavoko ambaye alijizolea umaarufu miaka ya nyuma kwa vibao vyake vikali  alisainiwa na kujiunga na WCB siku za nyuma kidogo na kutoa nyimbo kadhaa zilizomrudisha Kwenye chati.

Lakini mapema mwaka huu kulikuwa na tetesi nyingi Baada ya Rich MAvoko kutoonekana Kwenye shughuli mbali mbali za WCB na hata kutoonekana kwenye trailer ya shoo mpya ya Wasafi.

Rich Mavoko pamoja na uongozi wake WCB wamekuwa kimya juu ya Tetesi za Rich Mavoko kuondoka WCB Mpaka sasa ambapo kuna taarifa kuwa Mavoko kajitoa rasmi.

Kituo cha Televisheni cha TV E  wanaripoti kuwa siku ya leo Mavoko amefanikiwa kushinda kesi dhidi ya WCB rasmi na inasemekana amejitoa Kwenye Label hiyo Lakini pia mkataba alikuwa nao umevunjwa.

Mpaka hivi sasa Rich Mavoko hajatoa tamko lolote kuhusu  nini kinachoendelea Mpaka sasa Uongozi wa WCB haujatoa tamko juu ya tuhuma hizo.

Baba Diamond Adaiwa Kukaata Mtoto Wake Wa Nje

Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mzee Abdul Juma ametupiwa tuhuma nzito baada ya kudaiwa kutelekeza mtoto wake wa nje.

Global Publishers wanaripoti kuwa kijana aliyejitambulisha kwa Jina la Emmanuel alidai ni mtoto wa Baba Diamond na ametoka mkoani Kigoma kwa ajili ya kuja kuonana na Baba yake ambaye mama yake amemwambia alimtelekeza.

Gazeti hilo lilimsaka Baba Diamond ili kujua ukweli wa tuhuma hizo ambapo alikiri kumpokea kijana huyo na kusema kwamba siyo mtoto wake kama mwenyewe anavyodai bali ni kijana tu ambaye alikuwa anatafuta njia ya kukutana na Diamond kwa hiyo akaona njia rahisi ya kumfikia ni kujifanya mtoto wake.

Nilikuwa katika pilikapilika zangu, mara nikapigiwa simu nikaambiwa kuwa kuna mgeni wangu nyumbani, nilipouliza ni nani nikaambiwa ni ndugu yake Diamond ambaye ni muimbaji pia katokea Kigoma.

Baada ya kumaliza pilika zangu nilirudi nyumbani na kweli nikamkuta kijana huyo lakini cha kushangaza alikuwa anatetereka sana kujibu maswali kwa sababu hata nilipomuuliza jina la baba yake alitaja lingine kabisa tofauti na langu.

Unajua huyu siyo kijana wa kwanza kuja na kudai kuwa mimi ni baba yao, wanatafutaga njia ya kutaka kuonana na Diamond lakini wanashindwa kutokana na mama yake kule ni mkali hawawezi kuingia, kwa hiyo wanataka waje kwangu kwa sababu wanajua nafika kwa Diamond.

Wanahisi wakidanganya hivyo itakuwa rahisi mimi kuwakutanisha kitu ambacho hakiwezekani, narudia tena mimi sina mtoto wa nje kwa sababu watoto wangu wote nawafahamu”.

 

Masanja Atetea Kitendo Cha Diamond Kuvaa Kikuku na Kudai Mungu Anaruhusu Kwenda na Fasheni

Mchekeshaji maarufu Masanja Mkandamizaji ambaye sasa amegeukia Injili na kujiita Mchungaji amefunguka na kumkingia kifua Diamond Platnumz kwa kitendo chake cha kuvaa kikuku.

Masanja amefunguka Kwenye mahojiano na Masanja Tv, na kudai kuwa kwa imani yake ya Kikristo kuvaa kikuku mguuni kwa mwanaume sio dhambi kwani inahesabiwa kama cheni yoyote unayoweza kuvaa na Mungu hajakateza watu kwenda na fasheni.

Kama mchungaji nasema mwanaume kuvaa kikuu mguuni sio dhambi, lakini nikawaambia kwenye maadili kuvaa kikuku unamaanisha nini? soo shinda ikiwepo kwenye maadili haina maana ni dhambi watu wanadhani kuwa vitu wasivyovipenda wao kuviona, vitu ambavyo sio maadili mazuri wanafikiri kuwa ni dhambi kuna tofauti sana juu ya hivyo vitu. Kwa hiyo narudia tena kusema mwanaume kuvaa kikuku katika Biblia sio dhambi”.

Lakini pia Masanja amesema Cheni ni cheni tu na hakuna mtu wa kumpangia binadamu mwenzie sehemu ya kuvaa na hakuna cheni ya mwanamke zote ni cheni tu.

Kikuku ni cheni tu, hakuna cheni ya kivulana wala cheni ya kike cheni ni cheni na ukiamua kuvaa mkononi au shingoni sio dhambi kufikiria vibaya mtu kuvaa cheni mguuni huo ni uchizi wa hali ya juu. Kwahiyo kama kuna mtu anaona kuvaa micheni miguuni ndio raha muacheni avae”.

Pia Masanja amesema kuwa Mungu hajamuumba binadamu aokoke ili awe nyuma ya fasheni bali alimuumba aendane na fasheni.

“Sina Mpango wa Kwenda SA Kwenye Birthday Ya Tiffah” Povu la Wema Kwa Zari

Muigizaji wa Bongo movie mwanadada Wema Sepetu amemwaga povu zito na kudai hataenda Kwenye Birthday party ya Tiffah nchini South Africa.

Wema amefunguka na kusema kuwa hawezi kwenda Afrika Kusini kwenye party ya mtoto huyo kama walivyoalikwa Diamond Platnumz.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika:

God Bless The Next Big Thing… Like Father Like Daughter. On August 6th, A Star was Born… ??????. Msije mkadhani kwenye Party naenda. Wala siendi. I jus wished the lil angel Dats it…!!! ??? #SinagaHianaMie . Maana hamkawii”.

Povu hilo limekuja siku chache baada ya Zari kumwambia Live kabisa Wema na kundi lake la Bongo movie kuwa hawataki nyumbani kwake maaana watamchafulia Nyumba.

Diamond na Zari wanategemea kumfanyia Tiffah bonge la sherehe huko nchini South Africa.

BASATA Wafungukia Tuhuma Za Kumlipisha Diamond Kibali Cha Kwenda Kwenye Birthday Ya Tiffah

Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limekanusha taarifa za kumlipisha staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kibali cha kwenda South Africa kwa ajili ya birthday ya mtoto wake Tiffah.

Wiki iliyopita BASATA ilitangaza utaratibu mpya kuwa wasanii wote wanatakiwa kuripoti ofisi  za BASATA kabla ya kusafiri kwenda nchi za nje kwa ajili ya kulipia vibali.

BASATA wamekanusha Tetesi zinazoenea Kwenye mitandao ya kijamii na kudai hawajamlipisha Diamond kibali cha kwenda South Africa kwani kibali hicho sio cha Safari binafsi.

Tunapenda kuutarifu umma kuwa taarifa inayosambaa kwamba Msanii Diamond anatakiwa kuchukua kibali BASATA kwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mwanaye si ya kweli.

Vibali vya wasanii kwenda nje havihusiani na safari binafsi. Tunazidi kuwakumbusha wasanii kufuata taratibu zote wanapoenda kufanya maonesho nje ya nchi“.

Diamond ametangaza kufanya bonge la party nchini South Africa kwa ajili ya kusheherekea miaka mitatu ya kuzaliwa ya mwanae Tiffah.

Diamond Ndio Msanii Mwenye Mafanikio Yanayoonekana- Baraka The Prince

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na ngoma yake ya ‘Sina’ Barakah The Prince amefunguka na kumtaja Diamod kama Msanii Mwenye mafanikio ambaye yanaonekana.

Barakah amemtaja Diamond baada ya kuulizwa kuhusu wasanii mwenye mafanikio ambapo amekiri kuwa wasanii kadhaa wenye mafanikio sana lakini Diamond ndiye anayeonekana kufanikiwa zaidi.

Kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Barakah amesema wasanii wenye mafanikio wapo wengi lakini hajui mkwanja wao benki au hawajionyeshi sana lakini Diamond anaonekana wazi kabisa:

Wasanii wengi wana mafanikio wakina Ali Kiba, AY, Joti, Masanja, sitaki kujudge kama Diamond ndio Msanii wa kwanza kwa sababu sijui akaunti yake lakini kwa nje kila mtu anaweza kuwa na mtazamo huo kwa sababu anafanya vitu vinavyoonekana katika jamii”.

Barakah aliendelea kufunguka kuwa:

Lakini hatuwezi kusema nani namba moja kwa sababu hatujui akaunti ya Sugu ipoje? Ommy Dimpoz, Profesa Jay, Juma Nature na wasanii wengineo”.

Msanii Chemical amewahi kumtaja Diamond kama Msanii Mwenye mafanikio na pesa zaidi Kwenye muziki wa Bongo fleva.

Vanessa Mdee na Gabo Waunga Mkono Harakati Za BASATA

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa Vanessa Mdee na Muigizaji bora wa Kiume wa Bongo movie Gabo Zigamba wameonekana kuunga mkono harakati za Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

Wiki iliyopita BASATA ilitangaza sheria mpya kwa wasanii wote Tanzania kuwa wanaenda kujisajili BASATA mara tu wanaenda Safari za nje ya nchi Kwenye shoo mbali mbali.

Vanessa Mdee na Gabo wameonekana kuwa mstari wa mbele kuinga mkono na kutoonekana sheria hiyo kwani wameenda kuomba kibali kw ajili ya kusafiri nje ya nchi kwa kazi zao za sanaa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Onesmo Kayanda amesema Vanessa Mdee ameshapatiwa kibali kaenda Afrika Kusini huku Gabo akipata kibali cha kwenda nchini Ireland.

Wii iliyopita Diamond Platnumz alizuiliwa kusafiri akiwa uwanja wa ndege baada ya kukiuka sheria hiyo na kutaka kusafiri bila kibali.

Familia Ya Diamond Yadaiwa Kugoma Kwenda Kwenye Birthday Ya Mtoto Wa Hamisa

Familia ya staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz imedaiwa kugoma kabisa kuhudhuria Birthday party ya mtoto wa Diamond aliyezaa na Hamisa Dylan.

Global Publishers wanaripoti kuwa Familia hiyo inadaiwa kususia mwaliko huo ambao ni wa Birthday ya Mtoto wa Mobetto na inadaiwa kuwa bize zaidi na maandalizi ya birthday ya Tiffah itakayofanyika South Africa.

Chanzo makini kilieleza kwamba familia ya Diamond imegomea kwenda kwenye bethidei inayoandaliwa na Mobeto kwa ajili ya Dylan ambaye pia ni mtoto wa mwanamuziki huyo inayotarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu.

Unaambiwa familia ya Diamond haitaki kusikia mtu anayeitwa Mobeto maana hawampendi hivyo licha ya kwamba Dylan amezaliwa mwezi mmoja na Tiffah lakini wao wako upande mmoja wa Tiffah“.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Esma Platnumz ambaye ni dada wa Diamond amesema  kuwa hawezi kwenda kwenye birthday ya Dylan kwa sababu hawajawahi kualikwa kwenye sherehe zao hata siku moja, hivyo hawawezi kwenda wala hawatarajii kusogea.

Hivi ushawahi kuona klina Hamisa wanatualika kwenye ishu zao hata kidogo? Hivyo hatuwezi kwenda hata kidogo wala hatutarajii kabisa“.

Kumekuwa na maswali mengi juu ya birthday ya mtoto wa Hamisa na Diamond ambaye pia ana birthday hivi karibuni kwani  inayosikika ni  ya Tiffah na siyo Dylan ambaye pia ni mtoto wa Diamond.

Diamond Ataja Siku Wasafi Fm Itaanza Kurusha Matangazo Yake

Staa wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amefunguka na kutaja tarehe ambayo Wasafi Fm, itaanza kurusha matangazo yake rasmi.

Mwaka jana mwishoni Diamond Platnumz ambaye sio msanii tu bali Mfanyabiashara pia alitangaza kuwa anaingia Kwenye ulimwengu wa Media kwa kufungua radio station na television station ambazo ni Wasafi Tv na Radio.

Diamond Platnumz amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ni lini kituo chake cha radio cha Wasafi FM kitaanza kurusha matangazo kama ilivyo kwa kituo chake cha Runinga cha Wasafi TV.

Kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha Mayotte la 1ère cha kisiwani Mayotte ambapo yupo anafanya shoo Diamond alifunguka:

Nimefungua Tv inaitwa Wasafi TV na inafanya vizuri sana na tupo katika mikakati ya kuhakikisha inapatikana bara zima la Afrika na ulimwenguni kote. Lakini pia mwezi wa kwanza au mwishoni mwa mwaka huu tunafungua pia Wasafi FM itakuwa hewani”.

Wasafi Tv imekuwa hewani kwa kama Miezi miwili hivi na tayari imepata mafanikio makubwa sana ingawa haijaanza hata kurusha vipindi Rasmi na hata matangazo ya wadhamini lakini kwa maangalizo ya awali inaonekana Wasafi Tv inapita katika njia sahihi.

Diamond Akapimwe Akili na Kufanyiwa Maombi-Dudubaya

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva DuduBaya amemwagia povu zito msanii mwenzake Diamond Platnumz baada ya kuvaa kikuku na kumtaka akapimwe akili.

Wiki chache zilizopita Diamond alizua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha yake aliyomuonyesha akiwa amevaa cheni ya mguuni (kikuku) ambayo inavaliwa mara nyingi na wanawake tu.

Dudubaya amefunguka n kumtolea povu zito Diamond ambapo Kwenye Interview yake na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, amedai kitendo alichofanya Diamond ni cha kutia aibu kwa wanabongo fleva wote:

Kwa mdogo wangu Diamond kuvaa kikuku siwezi kujua anatangaza biashara gani hasa labda na yeye anatangaza biashara sawa sawa na wanawake wanaojiuza wanavyojitangaza kwa kuvaa kikuku kwaiyo kwa mimi ni aibu na  kaitia aibu Bongo fleva na hata familia yake na hata mademu zake anaolala nao hawana akili kwa nini wasimshauri asivae kikuku”.

Lakini pia Dudubaya aliendelea kumwaga povu na kumtaka Msanii huyo akapimwe akili:

Mimi naona akapimwe akili yake na pia akae chini na viongozi wa dini ili waweze kumpa ushauri”.