Zamaradi Adai Uvumilivu Ulimshinda Akaamua Kumwaga Povu Mtandaoni

Mtangazaji wa Wasafi Tv Zamaradi Mketema amefunguka baada ya bifu lake na mrembo Hamisa Mobetto na kudai uvumilivu ulimshinda ndio maana akamwaga povu lile Instagram.

Siku chache zilizopita Zamaradi na Mobetto waliingia kwenye vita kali ya maneno baada ya kugombana kisa nguo ambayo Zamaradi alivaa kwenye 40 ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Zamaradi amefunguka na kudai kuwa alifunguka na kuongea mambo Yale kwa sababu alishindwa kuvumilia kusemwa vitu vya uongo ili hali ukweli upo.

NI kweli nimeongea na kuweka vitu wazi lakini yule sio mimi ila kuna muda  tu vitu vinakufika kooni na kushindwa kuvivumilia kwa sababu hata uongo unapozungumzwa sana hugeuka na kuonekana kama ndio ukweli na Watanzania ni watu wa kuchukua kitu kama kilivyo na kila mtu hongea lake na sikuongea kama ni povu bali nilitaka kuweka wazi ili watu waelewe nini kinaendelea”.

 

Hamisa na Zamaradi Ndani Ya Bifu Zito

Mtangazaji na mfanyabiashara Zamaradi Mketema ameingia ndani ya bifu zito na Mzazi mwenza wa Diamond Platnumz Hamisa Mobetto wameingia kwenye majibizano makali Kwenye mitandao ya kijamii.

Kisa cha majibizano hayo ni baada ya kuwepo kwa tuhuma za Zamaradi kuiba idea ya mshono wa nguo yake aliyovaa Kwenye 40 ya mtoto wake kutoka kwa Hamisa Mobetto kisha kwenda kushona kwa fundi mwingine bila hata taarifa.

Baada ya tetesi hizo Zamaradi aliandika Kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hakuchukua idea ya mshono kutoka kwa Hamisa  bali yeye ndiye alimpa Hamisa mshono lakini alishindwa kushona kwake kutokana na muda.

Nimeambiwa nilipewa mshono na mtu nikaenda kushona kwingine, na nimeshangazwa na uongo mkubwa wa namna hii, Mimi ndio nimetuma mshono kwake na sio yeye, hakuwa anaufahamu kabla, kutokana na kudai kupishana na muda nikaamua nikashone kwingine na zaidi swala la kushona kokote ni uamuzi wangu since sijachukua mshono wa mtu”.

Baada ya povu hilo la Zamaradi, Hamisa na yeye alimwaga povu zito sana na kuandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram:

https://www.instagram.com/p/BmdYoQZlCv_/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1as2jxfy2tqvq

Zari Aweka Pembeni Tofauti Zake na Hamisa na Kumtumia Dylan Salamu za Birthday

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady ameweka tofauti zake pembeni na Mzazi mwenza mwingine wa Diamond Hamisa, na kumtakia heri mtoto wake Dyalan.

Zari na Hamisa walikuwa kwenye vita kali tangia Zari alipoginfua Diamond kamsaliti na kuzaa na Hamisa wakati wakiwa Kwenye Mahusiano kimapenzi.

Lakini sasa Zari anaonekana kuweka pembeni tofauti hizo hasa linapokuja suala la watoto kwani amemtumia salamu za Birthday Dylan na kukiri yeye ni mtoto na hana makosa.

Kwenye mahojiano hayo na kituo kimoja cha habari nchini Uganda ambapo Zari anategemewa kuwa JAJi katika mashindano ya Miss Uganda, amefunguka na kusema hana kinyongo na Dylan kwani ni mtoto ambaye hana makosa na sio kosa lake yuko pale:

Siku ya Jumatano ilikuwa Birthday ya Dylan mtoto wa Diamond na Hamisa na Zari alimtumia salamu Hizi:

Happy birthday Dylan, Hope you have the best in life and Mummy Z loves and no matter what the public says it was never your fault you were just caught up in it and you happened and i know the internet will torment you and say you were a child who came to break another woman’s family but no matter what you are here and I hope you grow up to be something big”.

Familia Ya Diamond Yadaiwa Kugoma Kwenda Kwenye Birthday Ya Mtoto Wa Hamisa

Familia ya staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz imedaiwa kugoma kabisa kuhudhuria Birthday party ya mtoto wa Diamond aliyezaa na Hamisa Dylan.

Global Publishers wanaripoti kuwa Familia hiyo inadaiwa kususia mwaliko huo ambao ni wa Birthday ya Mtoto wa Mobetto na inadaiwa kuwa bize zaidi na maandalizi ya birthday ya Tiffah itakayofanyika South Africa.

Chanzo makini kilieleza kwamba familia ya Diamond imegomea kwenda kwenye bethidei inayoandaliwa na Mobeto kwa ajili ya Dylan ambaye pia ni mtoto wa mwanamuziki huyo inayotarajiwa kufanyika Agosti 7, mwaka huu.

Unaambiwa familia ya Diamond haitaki kusikia mtu anayeitwa Mobeto maana hawampendi hivyo licha ya kwamba Dylan amezaliwa mwezi mmoja na Tiffah lakini wao wako upande mmoja wa Tiffah“.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Esma Platnumz ambaye ni dada wa Diamond amesema  kuwa hawezi kwenda kwenye birthday ya Dylan kwa sababu hawajawahi kualikwa kwenye sherehe zao hata siku moja, hivyo hawawezi kwenda wala hawatarajii kusogea.

Hivi ushawahi kuona klina Hamisa wanatualika kwenye ishu zao hata kidogo? Hivyo hatuwezi kwenda hata kidogo wala hatutarajii kabisa“.

Kumekuwa na maswali mengi juu ya birthday ya mtoto wa Hamisa na Diamond ambaye pia ana birthday hivi karibuni kwani  inayosikika ni  ya Tiffah na siyo Dylan ambaye pia ni mtoto wa Diamond.

Hamisa na Irene Uwoya Waomba Radhi Kwa Picha Zao Za Utupu

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya na Mjasiriamali Hamisa Mobetto wameomba radhi baada ya kusambaa kwa picha zao za utupu Kwenye mitandao ya kijamii.

Kamati ya maudhui ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) liliwapa onyo wasanii hawa wawili na kuwataka kuomba radhi baada ya kukiuka sheria za maudhui za mtandao.

Irene Uwoya aliomba radhi mbele ya waandishi wa habari baada ya kusambaa kwa video yake iliyomuonyesha akiwa nusu utupu mwezi uliopita na kuzua gumzo zito.

Lakini pia Kupitia ukurasa wake wa Instagram Irene aliandika ujumbe huu kwa nia ya kuomba radhi kwa mashabiki zake:

https://www.instagram.com/p/BlaPZRPn30Q/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=xx260oz7cz56

Lakini pia Hamisa Mobetto naye aliwaomba radhi Watanzania wote Kupitia vyombo vya habari Lakini pia aliandika ujumbe huu Kwenye ukurasa wake wa Instagram:

https://www.instagram.com/p/BlaZbqplAl3/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=9scs819pluxg

Zari Ampa Pole Hamisa Baada Ya Kukanwa na Diamond Hadharani

Zarinah Hassan ‘Zari’ amerudi Kwenye headlines tena baada ya kumuandikia ujumbe adui yake namba moja Hamisa Mobetto baada ya kukanwa na Diamond hadharani.

Sakata hilo lilianza siku ya leo baada ya Diamond kuachia video yake mpya ya wimbo wake wa ‘Baila’ ambapo aliposti Kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika kuwa hajapata mwanamke wa kuwa naye lakini siku akimpata atamsikilizisha Baila:

Kwa machache niliyojifunza Kwenye Mahusiano nilisema siku nikikutana na mwanamke mpya nitakayetaka kuwa naye kabla ya kuianza Safari sitamwambia neno bali nitamuwekea huu wimbo wa Baila”.

Baada ya Diamond kuweka wazi kuwa hayupo kwenye mahusiano moja kwa moja Zari alianza kumnanga Hamisa na kumpa pole baada ya kukataliwa na mwanaume ambaye amekuwa akijitangaza kuwa Kwenye Mahusiano naye.

Kwenye ukurasa wake wa Snapchat Zari aliandika maneno ambayo directly alikuwa anampiga vijembe Hamisa na kumcheka kuwa amekaa Kwenye Mahusiano na mwanaume kwa miaka kumi lakini bado anamkana hadharani kuwa hana uhusiano naye:

Bifu la Zari na Hamisa lilianza baada ya Diamond kuchepuka Kwenye Mahusiano Yake na Zari na kuzaa mtoto na Hamisa Mobetto tangia hapo Zari na Mobetto hawaivi chungu kimoja ni majungu kwenda mbele na kujibizana mitandaoni.

Ray C na Hamisa Mobetto Ndani Ya Bifu Zito na Zari Aingizwa

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amejikuta katikati ya bifu zito na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto.

Sintofahamu hiyo Ilianza siku mbili nyuma baada ya Ray C kuzisema nguo aina ya ‘Fendi’ feki ambazo zimekuwa zikiuzwa sana Hamisa ambaye ni mfanyabiashara ambapo Ray C alitoa kama maneno ya kejeli kuhusu nguo hizo ingawa hakutaja jina.

Basi Hamisa baada ya kuona kama Dongo lile katupiwa yeye basi moja kwa moja akaandika ujumbe ambao uliwakosoa watu ambao hawaonyeshi sapoti kwa biashara za wengine badala yake wanakuwa na wivu.

Baada ya sakata hilo na mashabiki wa Hamisa kumvamia Ray C basi aliweka wazi kuwa hakumtaja Hamisa jina kwa lile Dongo lakini baada ya kuona wanazidi ikabidi amvae Hamisa na kumsema kuhusu Zari na kudai yeye mwenyewe alimuumiza Zari kwa kitendo cha kuzaa na Diamond.

 

Lava Lava- Hamisa Mobetto Ananikubali Sana

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Lava Lava amefunguka na kusema kuwa mzazi mwenza wa Diamond Platnumz Hamisa Mobetto anamkubali sana.

Siku chache zilizopita Hamisa Mobetto aliposti video clip kwenye mtandao wa Instagran iliyomuonyesha akiimba Wimbo Mpya wa Lava Lava unaoitwa ‘Atatulia’.

Kwenye Interview yake na The Playlist ya Times Fm, Lava Lava amesema katika jitihada zake za kutoka kimuziki Hamisa Mobetto amekuwa na mchango pia.

Nashukuru sana nyimbo zangu kina dada huwa wanazipokea kwa mikono miwili, hajalishi wapo kwenye hali gani.

Katika watu waliowahi kunionyesha ile love ambayo sikuwahi kuitegemea wala kuwaza ni huyo Hamisa Mobetto kwa utokaji wangu, alishanifuata akaniambia nakukubali sana, kwa hiyo ni sabaiki yangu namba moja”.

 

Diamond- Mtoto Wa Hamisa ni Mtoto Wangu Kama Walivyo Watoto Wa Zari

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemwaga povu zito kwa mashabiki waliokuwa wanamnanga mtoto mmoja ale aliyezaa na Hamisa wakidai sio mtoto wake.

Siku ya jana Diamond aliachia trailer mpya ya shoo yake ya ‘The real Life of Wasafi’ itakayoonyesha maisha halisi ya familia ya Diamond itakayorushwa Kwenye Wasafi Tv.

Kwenye trailer hiyo kuna kipande kinachomuonyesha Diamond akiwataka anazungumzia watoto wake lakini watoto wanaoonekana ni wawili tu ambao amezaa na Zari huku mtoto wake aliyezaa na Hamisa hakuonekana.

Kuona hivyo mashabiki wa Zari wakaanza kumnanga mtoto wa Hamisa kuwa sio mtoto wa Diamond ndio maaan hajaonekana kwenye trailer ya shoo ile na hapendwi kama watoto wa Zari wanavyopendwa.

Baada ya maneno mengi sana Diamond alishindwa kujizuia na kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa Dylan ni mtoto wake kama walivyo watoto aliozaa na Zari walionekana kwenye trailer ile sababu pekee ambayo ilisababisha mpaka Dyalan hakuonekana ni kwa sababu hakuwa na clip yake:

 

Hamisa Mobetto Atoa Baraka Zote Ndoa Ya Lulu na Majizzo

Msanii wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto ameweka wazi kuwa hana kinyongo na kutoa baraka zote kwa ajili ya ndoa ya Lulu na Majizzo.

Hamisa amewahi kuwa kwenye Mahusiano na Majizzo siku za nyuma na  kuzaaa naye mtoto mmoja ameweka wazi kuwa hivi sasa hana matatizo na Majizzo wala Lulu hivyo kwake ni Poa tu wakifunga ndoa.

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Mobeto alisema kuwa hana kinyongo na Lulu kama ambavyo watu wanasema kwa kuwa mapenzi yake na Majizzo yalishakwisha siku nyingi.

Mimi na huyo anayetaka kumuoa tulishamalizana, hivyo hakuna tena hata chembe ya mapenzi zaidi ya uhusiano wetu wa kulea mtoto.

Kwa maana hiyo sina shida kusikia Lulu anaolewa na siku ya sherehe nikipewa kadi nitakwenda“.

Tangu Lulu atoke jela Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa yeye pamoja na mpenzi wake Majizzo wanategemea kufunga ndoa hivi karibuni na taarifa hiyo ilithibitishwa na Mkuu wa Mkoa Paul Makonda.

Kuna Muda Natamani Kuondoka Tanzania- Hamisa Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi  mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amedai kuwa kuna muda anatamani kuondoka Tanzania.

Hamisa ambaye ameendelea kushika headlines kwani tangu alivyotangaza kuwa ana ujauzito wa Diamond mwaka jana basi hajatoka midomoni kwa watu tena.

Hamisa siku ya jana alizuahgumzo baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anatamani kuondoka Tanzania lakini kila akifika airport anajuuliza Watanzania wataishije bila yeye.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa aliandika:

Sometimes, Natamani Kuondoka Tanzania nafika hadi airport ila najiuliza Watanzania Wenzangu Wataishije Bila Mimi“.

Hamisa amekuwa akiongelewa sana Kwenye mitandao ya kijamii siku hizi tangu arudiane na Diamond na kiukweli imekuwa burudani kwa mashabiki zao hasa ukimuweka Diamond huku Zari pale na Hamisa huku.

Hamisa Mobetto Aanika Mipango Yake Ya Kuzaa Tena

Mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu mipango ya kuongeza mtoto wa tatu.

Hamisa amefunguka kuhusu suala hilo baada ya tetesi kusambaa kuwa hivi sasa ana ujauzito mwingine wa Diamond.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Wasafi Tv hivi karibuni Hamisa amejibu kuwa hivi sasa anaelekeza juhudi zake kwa watoto wake wawili ambao ni wadogo wanaohitaji kulelewa lakini labda hapo baadae ataongeza.

Kwa sababu watoto wangu bado wadogo sana na sina uhakika kama nataka kuongeza familia au la!, may be in the future hatuwezi kujua future inakuwa vipi au Mungu kapanga huku mbeleni lakini ni jambo la kheri sana“.

Tangu Hamisa arudiane na Diamond Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa hivi sasa ana ujauzito mwingine unaosemekana kuwa una miezi mitano ingawa mwenyewe hajathibitisha hilo.

Hamisa tayari ana watoto wawili mtoto wa kwanza na Majizzo na mtoto wa pili na Diamond.

Hamisa Mobetto Atoa Neno Kwa Wote Wanamuonea Wivu

Muigizaji wa Bongo movie Hamisa Mobetto ambaye pia ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, ametoa neno kwa watu wote wanaomuonea wivu.

Hamisa amekuwa Kwenye headlines kwa muda mrefu sana na wiki hizi chache ameonekana kupitia katika kipindi kigumu na Familia ya Diamond kumkana hadharani.

Hamisa aliweka wazi kuimizwa na vitendo vilivyokuwa vinafanywa na Familia ya Diamond ambayo ilionyesha wazi kuwa haimtaki na kumtaka Diamond kurudiana na Zari.

Lakini sasa Hamisa anaonyesha kuwa hatakaa chini na kusema semwa ovyo kwani amewapa ujumbe mzito wale watu wote wanamuonea wivu Kwenye maisha yake na hata maendelea yake:

Kama unakasirika, unahuzunika au unaona wivu pale mtu anapofanikiwa, Tafadhali inamisha kichwa chako chini, funga macho yako na kisha unyanyue mikono kisha sema “Mungu mimi ni mchawi niokoe”.

 

“Hamisa Hata Akitaka Kuzaa Watoto Kumi na Diamond Azae Tu”-Zari

Mfanyabiashara maarufu na mama watoto wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zarinah Hassan amemwaga povu na kusema Hamisa hata akitaka kumzalia watoto kumi Diamond yeye kwake ruksa.

Kauli hiyo ili Jina siku ya jana baada ya Zari kuweka posti yake aliyokuwa anasherehekea kufikisha followers milioni 4 Kwenye mtandao wa Instagram ambapo shabiki alimtahadharisha kuwa kuna tetesi Hamisa ana ujauzito mwingine.

Shabiki huyo aliandika maneno haya:

Zari kuwa makini kuna tetesi huku mtaani kwetu kuwa Hamisa kashanasa mimba nyingine ila lisemwalo lipo kama halipo laja”.

Baada ya kupewa maneno hayo Zari alimjibu hata wangezaa watoto kumi yeye hana habari kwani hayumo.

Zari alijibu kwa kuandika:

Azae hata kumi mimi simo!”.

Huu ni muendelezo tu wa drama iliyoanza mwaka jana baada ya Hamisa kuanika ana ujauzito wa Diamond kwa wakati huo alikuwa mpenzi wa Zari.

Kumekuwa na tetesi tu kuwa Diamond amerudisha majeshi kwa mama watoto wake Zari baada ya kutoonana kwa muda wa Miezi minne.

Mama Mobetto Awatolea Povu Familia Ya Diamond

Mama Mzazi wa mrembo Hamisa Mobetto anayejulikana kama Mama Mobetto amewatolea povu zito wanaomtukana mwanaye Kwenye mitandao ya kijamii.

Hamisa amejikuta Kwenye wakati mgumu kwani  amekuwa akirushiwa  vijembe na Familia ya Diamond ambayo imedai kuwa ni mchafu na hata kusambaa kwa Tetesi kuwa amechezea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa Mama Diamond.

Lakini pia Familia nzima ya Diamond kuanzia mama yake mpaka Dada zake mpaka mameneja wa Diamond wameonekana kumkataa kata kata Hamisa huku wakionyesha wazi kumpenda zaidi Ex wa Diamond Zari.

Hayo yamesababisha Hamisa kurushiwa matusi ya nguoni na mashabiki wote wa Zari lakini hata mashabiki wa Diamond.

Mama Mzazi wa Hamisa ameonekana kuchoshwa na kuimizwa na vitendo anavyofanyiwa mwanaye hivyo ameamua kuingia kwenye mtandao na kuiomva familia ya Diamond iache kumtukana mwanaye na hata mashabiki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mama Mobetto ameandika ujumbe huu:

 

Hamisa Mobetto Akiri Kuwa Katika Kipindi Kigumu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Hamisa Mobetto ameanika undani juu ya mambo anayopitia kwa hivi sasa na kukiri kuwa katika kipindi kigumu.

Hamisa amekuwa Kwenye headlines tangu alipotangaza kuzaa mtoto wa Diamond mwaka jana lakini siku chache hizi mambo yamekuwa mazito kidogo kwa upande wake.

Familia nzima ya Diamond kuanzia mama yake mpaka Dada zake mpaka mameneja wa Diamond wameonekana kumkataa kata kata Hamisa huku wakionyesha wazi kumpenda zaidi Ex wa Diamond Zari.

Hamisa amekuwa akirushiwa vijembe na Familia ya Diamond ambayo imedai kuwa ni mchafu na hata kusambaa kwa Tetesi kuwa amechezea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa Mama Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat Hamisa amefunguka magumu hayo anayopitia kwa hivi sasa ambapo amesema licha ya magumu anayokabiliana nayo kwa sasa bado anaamini Mwenyenzi Mungu atamvusha:

Bado sijafika Mw/Mungu aliponipangia na kama mnavyoona barabara yangu ni mbovu, ina mashimo, mabonde na pia matope mengi kwa hiyo safari yangu inakuwa ngumu kidogo.

Lakini naimani sana na M/Mungu alonileta kwenye dunia hii, naimani ipo siku nitafika na Naimani barabara yangu hii nii mbovu ipo siku ataisawazisha na kuiweka rasmi.

Nina kushukuru sana Mungu, naimani kuna vibaya vingi umeniepusha navyo na pia naimani kuna vikubwa vizuri vyaja. Na naimani hivi vyote visingenipata mimi kama ningekuwa sina u-special wowote ndani yangu”.