Diamond aisifu umbo ya Wema Sepetu kwenye wimbo wake mpya

Uhusiano wa kimapenzi kati ya Diamond na Wema Sepetu uliisha miaka kadhaa zilizopita lakini wawili hao bado ni marafiki wa kawaida.

Wiki moja iliyopita Diamond alizua utata baada ya kufunguka kuwa yeye na Wema bado huwa wanaongea na kukutana bila ya vyombo vya habari kupata uhondo wowote.

Soma pia: Diamond: Watu hawajui mimi na Wema Sepetu tunaongea sana lakini sio kwenye media

Diamond alisifu umbo wa Wema Sepetu kwenye wimbo wake mpya ‘Fire’ aliyomshirikisha mrembo kutoka Nigeria – Tiwa Savage.

“Sura Zari nadhani (ayaya) shape Sepetu Wema (ayaya) Ooh, I say, you fire baby oh (Fire fire fire fire) baby…” Diamond aliimba kwa wimbo wake.

Soma mistari ya ‘Fire’ hapo chini:

 

Diamond Platnumz – ‘Fire’ lyrics  Feat : Tiwa Savage

 

[Intro – Tiwa Savage]

It’s Tiwa Savage yeah

 

[Verse 1 – Diamond Platnumz]

Aga, you’re my sexy arose eh

Utamu zaidi ya varila

Yaani cookei wa mose

Kama pochi na ngawila

Sa nipatie dose eh

Kasi itaja nipalila

Usinifanyie ya jose eh

Tange tange kajamila

 

[Hook/Chorus – Diamond Platnumz]

I say, you fire baby

Fire fire fire fire baby

Fire oooh

(Fire fire fire fire) baby

Your love is sweet oh

(Fire fire fire fire) baby

Tamu mpaka mwisho

(Fire fire fire fire) baby

Ah ah, fire ooh

(Fire fire fire fire) baby

Fire baby (Fire fire fire fire) baby

Akicheka sura ya kitoto

(Fire fire fire fire) baby

Akinigusa kabisa ndo moto

(Fire fire fire fire) baby

 

[Verse 2 – Diamond Platnumz]

Wasi wasi ndo akili

Na kwako sina

Nyota njema alfajili

Kesha na uzima

Wanakesha kulitabiri

Pendu kuchina, baby

Tena wengine

Wakubwa mili

Watu wazima

Tanga kunani

Vurugu mechi mkwakwani

Mtoto hatari wakadada

Samba chumbani

Ye ndo messi uwanjani

Msiniibie simba, yanga

Nyuma kama sunami (ayaya)

Jinsi kunatetema (ayaya)

Sura zari nadhani (ayaya)

Shape sepetu wema (ayaya)

 

[Hook/Chorus – Diamond Platnumz]

Ooh, I say, you fire baby oh

(Fire fire fire fire) baby

Fire oooh

(Fire fire fire fire) baby

Akicheka sura ya kitoto

(Fire fire fire fire) baby

Akinigusa kabisa ndo moto

(Fire fire fire fire) baby

 

[Verse 3 – Tiwa Savage]

Let me tell you something ’bout this bobo oh (fire fire)

Love I get for him big pass orobo oh (fire fire)

Come and see the way the love dey make me to jaire (fire fire)

I swear na only him go fit enjoy my figure 8 oh

The way you shut my brain

I cannot explain

Fall for you with no shame

Baby walahi talahi eh (ayaya)

I love you no be lie eh (ayaya)

Your love dey sweet me die (ayaya)

I swear I no go lie

I say

 

[Hook/Chorus – Diamond Platnumz & Tiwa Savage]

I say, you fire baby oh

(Fire fire fire fire) baby

Aga, fire oooh

(Fire fire fire fire) baby

Your love is sweet oh

(Fire fire fire fire) baby

Tamu mpaka mwisho

(Fire fire fire fire) baby

Ah ah, fire ooh

(Fire fire fire fire) baby

Fire baby (Fire fire fire fire) baby

Akicheka sura ya kitoto

(Fire fire fire fire) baby

Akinigusa kabisa ndo moto

(Fire fire fire fire) baby

 

[Verse 4 – Diamond Platnumz & Tiwa Savage]

Tena waambie wasikunyatie darling

(Fire fire)

Hili penzi moto wakilivamia chali

(Fire fire)

Sa nipe kidogo (nitekenye)

Aga polepole (nitekenye)

Ah ah mpaka chini (nitekenye)

Ak inuka kidogo (nitekenye)

If I give it to you (nitekenye)

Will you give me sugar (nitekenye)

Oya give give (nitekenye)

Come and give me sugar (nitekenye)

Mahakama yahairisha kesi ya Wema Sepetu ya kupatwa na bangi

Wema Sepetu na marafiki wake Angelina Msigwa na Matrida wanakabiliwa na mashtaka ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa hizo.

Watatu hao walikua miongoni mwa watu kadhaa walioshikwa na police mapema mwaka huu baada ya Rais Magufuli kutangaza vita dhidi ya mihadarati.

Mara mingi Wema Sepetu amekua akifika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kuskizwa kwa kesi inayomkabili.

Wema Sepetu akiwa Mahakamani Kisutu

Mahakama hio sasa imehairisha kesi ya Wema Sepetu mbaka tarehe 10 Julai. Upande wa mashtaka uliomba shauri hilo liahirishwe hadi Julai 10 kwasababu Hakimu Mkazi Mfawidhi – Thomas Simba ambaye alikua askize kesi ya Wema alienda likizo.

 

Filamu kali inayomshirikisha Wema Sepetu, Gabo Zigamba, Millard Ayo kuonyeshwa dunia kote kwa njia ya kisasa

Filamu ya ‘Kisogo’ itakuwa movie ya kwanza kutoka Bongo ambayo itaweza kufika katika anga za kimataifa kwani imetengenezwa katika teknolojia ya kimataifa.

FC Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ ameeliza kuwa ‘Kisogo’ itatazamwa ata kwenye simu ya mkono kupitia App maalum.

“Nilitumia muda mwingi kufanya utafiti na kugundua kuwa wateja wanahitaji kupata kitu ambacho kinaburudisha, kinaelimisha lakini bila mtu kufika Kariakoo aua katika maduka ya kuuzia filamu, sasa tunakuja Mobile App Uhondo,”alisema Gabo.

Wema Sepetu, Millard Ayo, H. Baba ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao wameshirikishwa kwa movie hio mpya.

Tazama trailer ya ‘Kisogo’ hapo chini:

Diamond: Watu hawajui mimi na Wema Sepetu tunaongea sana lakini sio kwenye media

Diamond and Wema Sepetu walikua wapenzi kabla ya hit maker huyo kumtema Wema na kumoa Zari Hassan, hatua ambayo ilizua utata sana.

Watu wengi waliamini kuwa Diamond alitaka mtoto ndo maana alimwacha Wema Sepetu ambaye mbaka wa leo hajajaliwa kupata mtoto.

Hata kama Diamond alimwacha Wema, wawili hao bado huwa wanaongea na kukutana bila ya vyombo vya habari kupata uhondo wowote.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond alidhibitisha kuwa bado ako na uhusiano mwema na Wema Sepetu ingawa wao hufanya vitu vyao jini ya maji.

Hit maker huyo wa ‘Marry You’ alifunguka na kusema kuwa yale maneno ya kuvutia kwenye manukato yake – ‘The scent you deserve’ ni Wema Sepetu ndo alitoa.

Chibu Perfume

“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana wakati mwingine tunakutana tu sana lakini sio kwenye media. Tushakuwa kila mtu ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake hata ukiangalia katika Perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alilitoa Wema” alisema Diamond.

 

Ujumbe wa Wema Sepetu kwa Rayvanny ambao umewasisimua mtendao wa kijamii

Wasanii na raia wa kawaida wanampigia debe Rayvanny kushinda tuzo la BET – Viewer’s Choice Best New International Act.

Washidi watatuzwa terehe 25 Juni katika ukumbi wa Microsoft, jijini Los Angeles, Marekani. Waliochaguliwa wanapigwa kura na wale ambao watapata kura nyingi ndo watashinda tuzo walizoteuliwa.

Wasanii wa Bongo wamekua wakiwaomba wafwasi wao wampigie kura Rayvanny ili aweze kushinda tuzo hizo la kimataifa.

Ujumbe ya Wema Sepetu kwa Rayvanny akiwaomba watu wampigie kura umesisimua mtendao wa kijamii. Mrembo huyo aliambia Rayvanny tarayi yeye ni mshindi, alisema Rayvanny anastahili kabisa.

“Its Jus a Nomination But To Me You are Already a Winner…. Well Deserved…!!! V-Vanny Boy…!!!! ???????? #IPickRayVanny …. Nd it doesn’t stop here… Keep the Votes Going… ??????” Wema Sepetu aliandika.

 

Wema Sepetu kumsomea kisomo maalum ndani ya Mwezi huu Mtukufu na Shehe Mkuu wa Dar es Salaam

Wema Sepetu ameandamwa na majanga mengi mwaka huu ambazo zimemfanya kutawala vichwa vya habari; kesi yake ya kupatikana na bangi na kashfa yake ya kimapenzi na Freeman Mbowe.

Shehe Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, sasa ameamua kuingilia kati kumsaidia Wema Sepetu kwa kumsomea kisomo maalum ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan.

Akizungunza na Amani, Shehe huyo alisema kuwa amepanga kumfanya kisomo hicho ndani ya mwezi huu endapo Wema na mamake watafika katika ofisi yake jijini Dar kwa maelezo zaidi.

“Unajua Wema amekuwa akikutana na misukosuko mingi, ninachoweza kusema iwe kweli au si kweli Wema anatakiwa kufanyiwa kisomo maalum. Maana kumbukumbu zinaonesha hapitwi na mabaya mara kwa mara, kwa Rehema ya Mwenyezi Mungu amuepushie, kisomo nitakiandaa mimi mwenyewe. “Kuhusu sehemu na siku ya kufanya kisomo hicho bado haijafahamika kwa sababu hadi Wema na mama yake watakapokuja na kupanga nami kama ni nyumbani kwao lakini ni vyema wakaja ofisini kwangu. Ninafikiria kisomo hiki kukifanya ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadan,” alisema Shehe Mkuu.

 

Mchekeshaji Steve Nyerere awekwa motoni kutokana na sakata ya kimapenzi ya Wema Sepetu na Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai na Wema Sepetu wamekua wakitawala vichwa vya habari tangu sauti (voice note) ambazo zinadaiwa kuwa zao kuenea kwenye mitendao ya kijamii.

Voice note hio inaashiria kuwa Freeman na Wema Sepetu wana uhusiano wa kimapenzi lakini wawili hao walikana dhana hii.

Mchekeshaji Steve Nyerere amejipata pabaya kuhusu sakata ya Wema Sepetu na Freeman Mbowe. Mashabiki wa Wema na Freeman wanadai kuwa sauti ya kiume iliyoskika kwenye voice note hio ya utata ni ya Steve Nyerere.

Steve Nyerere na Wema Sepetu

Nyerere ako na kipaji cha kuigiza sauti mbalimbali za viongozi wa kisiasa na watu wengine mashuhuri; na  hii ndo sababu ya watu kumlimbikizia lawama.

“Sio mimi yule na siwezi kufanya kitu kama kile. Ile sauti ukiisikiliza kwa makini utajua sio mimi na siwezi kufanya hivyo,” Steve Nyerere alijitetea kwenye mahojiano na Bongo 5.

 

 

Ukweli wadhihirika kuhusu uhusiano wa Wema Sepetu na Freeman Mbowe

Siku chache zilizopita voice note ambayo inadaiwa kuwa sauti ya Wema Sepetu and mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelao CHADEMA ilisambaa kwenye mtendao wa kijamii.

Wema Sepetu na Freeman Mbowe

 

Mazungumzo kwenye voice note hio unadhihirisha kuwa Freeman Mbowe na Wema Sepetu wako na uhusiano wa kimapenzi.

Mbowe hata hivyo amefunguka na kueleza ukweli wa maneno kufwatia kuibuka kwa voice note hio; mwenyekiti huyo wa CHADEMA alikana kuwa sauti iliyoskika kwenye voice note hio ni yake.

https://www.youtube.com/watch?v=0iZg-JoIRgc

Alisema kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Wema Sepetu. Mbowe alieleza kuwa maadui wake wanamchafulia jina kwasababu Wema Sepetu alijiunga na CHADEMA.

Skiliza maelezo ya Mbowe kwenye video hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=Vfxtv8s08io

 

Harmorapa bado amwongelea Wema Sepetu ata baada ya mrembo huyo kumchapa kiboko

Mwezi moja iliyopita, Harmorapa akiongea na Millard Ayo alidai kuwa anampenda sana Wema Sepetu na ata angependa kufunga naye ndoa.

Wema Sepetu alimjibu rapa huyo kwa kumsomea mwanzo hadi mwisho kwenye ujumbe aliyoandika katika Instagram yake.

Soma pia: Mambo matano ya kuvunja moyo Wema Sepetu aliyomweleza Harmorapa kwenye instagram

Kama ulidhani Harmorapa aliskia kichapo alichopewa na Wema, bado. Rapa huyo anayependa kiki aliongelea ishu ya kudai kuwa anampenda Wema Sepetu alipohojiwa kwenye kipindi cha Ala za Roho ya Clouds FM hivi karibuni.

Tazama mahojiano hayo kwenye video hiyo hapo chini:

“Sasa aliokwambia namtaka Damond ni nani? Wema Sepetu awaonya mashabiki dhidi ya kumhusisha na Diamond Platnumz

Wema Sepetu amesisitiza kuwa uhusiano wake wa kimapenzi na Diamond Platnumz ulikamilika kabisa. Mwigizaji huyo wa filamu ya Bongo amesema anataka mume bora.

Wema na Diamond walikua wapenzi kabla ya mwimbaji huyo kumtema Wema na nafasi yake kuchukuliwa na Zari Hassan.

Mara nyingi watu husema kuwa Wema na Diamond bado wako na uhusiano wa kimapenzi ila wanachezea chini ya maji mapenzi yao isigunduliwe.

Diamond and Wema Sepetu

Wema amesisitiza kuwa yeye na Diamond hawana lolote tena, alisema hayo wakati akimjibu shabiki katika kurasa wake wa Instagram.

“Sasa baby aliokwambia namtaka Damond ni nani? Life has to go on, yule ni baba wa watoto wawili jamani. Its about time u guys accept that me and Naseeb no more. Mnachotakiwa kuniombea ni nipate mwanaume bora na siyo bora mwanaume na mwenye heshima zake,” aliandika Wema Sepetu Instagram.

Upelele wa kesi ya kukutwa na bangi inayomkumba Wema Sepetu umekamilika

Wema Sepetu ako na kesi kujibu mahakamani baada ya kushikwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi.

Mrembo huyo wa filamu za Bongo alishikwa na polisi Januari wakati polisi walianzisha msako kunasa wanaotumia dawa za kulevya.

Wema alizuiliwa katika kitua cha polisi jijini Dar es Salaam kwa siku sita kabla ya kupelekwa mahakamani kushtakiwa kwa kosa la kupatikana na bangi.

Wema aliachiliwa baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakama muda kukamilisha upelelezi wa kesi yake ya kukutwa na bangi.

Wakili wa Serikali Helleni Mushi jana Mai tarehe mbili aliomba kesi hiyo kuhahirishwa tena na kupangwa tarehe ya kuanza kusikilizwa ili watuhumiwa waanze kusomewa maelezo ya awali.

Wema sasa atarudi Mahakamani hivi punde baada ya koti kuweka tarehe ambayo kesi yake itaskizwa. Mrembo huyo alishtakiwa pamoja na wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abas (16).

 

Wanaume tano ambao wameonekana wakiwa katika mapozi ya kimapenzi na Wema Sepetu hivi karibuni (Picha)

Wema Sepetu ameonekana akiwa katika mapozi ya kimapenzi na wanaume watano – wote ambao ni waigizaji wa filamu za Bongo movies.

Mrembo huyo aliweka picha hizo za kitaalamu kwenye mtendao wa Instagram. Tazama hizi picha hapo chini:

1.Wema na Khizzer

 

2.Wema na Luckamo

 

3.Wema na Feisal Mgaza

 

4.Wema na Gambo Zigamba

 

5.Wema na Farid Uwezo

Hii ndio picha ya Wema akiwa kwenye gari na masufuria inayozingua wengi mitandaoni

Na kwa kweli Wema Sepetu anapenda kula?

Kuna mojawapo ya picha ambayo imetokea kwenye mitandao ambayo imezingua wengi na ni kwa sababu ako kwenye gari ambayo imejaa masufuria yaliyojaa kuku.

Na si kuku pekee mbali na pia miguu ya kuku.

Mtazame hapa:

 

Miguu ya Kuku ikikaangwa Na Chumvi inakua mitamu hiyooo ?

A post shared by President / Rais Wa Shilawadu (@soudybrown) on

Hii ndio picha ya Wema Sepetu akivuta sigara ambayo inawazingua wengi mitandaoni

Wema Sepetu anaongelewa sana mitandaoni na ni baada ya picha yake akivuta sigara kuibuka mitandaoni.

Picha hiyo ilitolewa na Soudy Brown na ilifanya mafans wengi wa Wema Sepetu kuhisi vibaya kuona star wao akifanya kitendo hicho cha kuvuta sigara mbele ya watu.

Baadaye lakni ilitokea ya kwamba picha hip ilikuwa moja ya scene ya filamu Wema amehusishwa.

Tazama hii picha hapa:

 

Mi nae mchokoziii ?

A post shared by President / Rais Wa Shilawadu (@soudybrown) on

Wema Sepetu atupiana maneno na mkongwe wa Bongo Movies Jimmy Mafufu

Wema Sepeti aliwakashifu wasanii wa Bongo Movie katika Instagram yake siku tatu zilizopita – alidai wasanii hao ni wanafki  kwasababu waliaacha kuongelea kupotea kwa mwimbaji Roma Mkatoliki badala yake wakapost kuhusu ishu ya kukutana na Mkuu wa Mkoa ili kuongelea ishu za filamu za Wafilipino na Wakorea.

“This Is Scary… Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla… Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino…. Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni…??? Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake…. Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa…??? Oh God help Us Please… Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu… Tumejawa sana Unafki…!!! All in All namuonea sana huruma Nancy…. Our prayers are with u mama… Inshallah mumeo atapatikana… Tuzidi kumuomba Mungu…..??????…. Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani….!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino…?? ??? SMH…” Wema Sepetu aliandika kwa Instagram.

Wema Sepetu

Post yake mrembo huyo ilimkera mkongwe wa Bongo Movies Jimmy Mafufu ambaye alisema Wema ndiye kinara wa wanafki.

“Hata kama hao Team Wema wanitukane vipi, sitaacha kusema ukweli, huyo aliyewaita Bongo movie Wanafiki, yeye ndiye kinara wao asitake kuharibu jina la Bongo Movie na asiwapangie watu cha kuposti kwani nani asiyejua kuwa yeye ni mnafiki? Sitaacha kumwambia ukweli acha watu waendelee kunitusi,” alisizitiza,” Jimmy Mafufu alisema.

Jimmy Mafufu

Wema Sepetu aliendele kumtumpia maneno Mafafu kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya msanii huyo wa Bongo Movies kumwita kinara wa wanafki:

“Nyie wengine ambao mnatokwa mapovu, Ujumbe umefika… Kumbe mnajijua eeh…? Afadhali hata mngekaaga kimya tu…. Maana mnaongea vitu havina hata maana… Alafu I pity all of you…???Sijui niseme Elimu ama ni Exposure tu… Ama ni lack of simple knowledge & common sense… Anyways, ngoja tuone… SMH… Kesho nayo ni siku… Goodnyt world… Oh..! Before I forget, feels good to be 1 against many…. Sad part is eti most of them are grown Men….!!! Y’all shud Man Up first…!!! Ila kama nawaona nyama choma yenu pale leaders if Next atakuwa mimi….????? (nimetania tu)… Usiku mwema jamani…”

 

 

 

Mambo matano ya kuvunja moyo Wema Sepetu aliyomweleza Harmorapa kwenye instagram

Wiki ambazo zimekuwepo, Harmorapa amekuwa akichangamsha mitandao kwa kuonyesha mapenzi yake kwa Wema Sepetu.

Amekuwa akiweka picha ya Wema Sepetu kila siku na kunena ananvyompenda. Kwa video moja alijiami kumuoa Wema Sepetu na kutoa hadi pete.

Soma pia: Harmorapa aongelea wanadada watano Tanzania ambao angetaka kuwa na uhusiano wa kimapenzi nao…nambari moja ni Wema Sepetu

Na si hayo tu, pia aliapa kumlisha na kumvisha.

Leo Wema aliongelea ishu hiyo na hakuwa na mazuri ya kumwambia Harmorapa.

Hivi ndivyo alivyo post kwenye instagramu:

 

Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usinidharaulishe…. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*

A post shared by Wema Sepetu (@wemasepetu) on